JE UNAO UHAKIKA UTANYAKULIWA NA YESU KWENDA MBINGUNI AU UTAACHWA HAPA DUNIANI?
BWANA YESU ASIFIWE, watu wote wa mataifa yote, MUNGU anawapenda watu wake ila shetani hawapendi watu wa MUNGU sababu anajua watarithi mbinguni ambapo ndipo ni pazuri na yeye atabakia katika shimo la moto. Utasoma katika kitabu cha Yohana 14: 6-7; 6YESU akamwambia, mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi. 7 Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na BABA; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. Katika somo hili nataka watu waelewe vizuri ili wapone roho zao na siku moja wafike mbinguni na jambo hili linafurahiwa na MUNGU na serikali yake. Hapa utaona YESU anasema yeye ndiye njia ya uzima wa milele na mtu yeyote hatafika mbinguni pasipo kumjua YESU, lakini hapa watu wengi wametekwa na shetani sababu ya mafundisho ya uongo, neno ni lile lile tu ila tafsiri zimeletwa za uongo na watu wakaufwata uongo wengine wakijua na wengine pasipo kujua ila utakapo uelewa ukweli hapo utakuwa umemjua YESU pia umemjua MUNGU.
Mimi Hebron hapo mwanzo nilikuwa ni mkristo ambaye niliporithi udini ambao niliukuta kwa wazazi wangu na niliamini kabisa nitaenda mbinguni lakini kumbe ilikuwa nisingeenda mbinguni kwa sababu nyingi ambazo niliziamini na zilinifunga nisimjue YESU wala MUNGU wa kweli. Hapo utaona YESU anasema katika mstari wa 6-7, ina maana ili umjue YESU ni lazima umwamini na ukisha mwamini upokee alichokileta yaani wokovu na ukishapokea wokovu wa kweli sasa hata hapo utamjua MUNGU, lakini ikiwa wanajiita wewe ni mkristo lakini haujaokoka nakutangazia sasa bado haujamjua YESU wala MUNGU na zaidi huu ni mtego uliowekwa na shetani kuwapiga watu upofu waone wapo na YESU lakini wapo na mpinga kristo au yesu wa uongo. YESU huyo ambaye alisema mwenyewe alipokuwepo hapa duniani kuna wengi watapotezwa na kudanganywa kwa kupitia jina hilo.
Tazama sasa haujadanganyika na kama umedanganyika basi uelewe unamwamini mpinga kristo na haumjui MUNGU wa kweli bali unaijua miungu ila wewe haujijui wala haupendi ila unatekwa na shetani kwa kufwata elimu ya uongo. Tunajua kuwa shetani ndiye baba wa uongo na unapouamini uongo tayari yeye anakuwa ndiye baba yako uliyemwona na ukiwa unaufwata ukweli kama neno lilivyo basi umemwona MUNGU na yeye anakujua na siku moja utafika alipo yeye mbinguni na ikiwa umepokea uongo yaani mafundisho ya uongo basi uelewe hiyo ndiyo njia yako ya kwenda jehanamu sasa uanze leo njia ipi utaifuata, ifuate ya kweli mkatae shetani.
YESU anasema ukiniamini usiniamini kuwa ni mwana wa MUNGU kama vile mashetani yanayoamini, unatakiwa uamini na uokoke na ubatizwe kwa maji mengi, imani bila matendo imekufa, huko ndiko kufa kiroho watu wengi wamemwamini YESU kama vile mashetani yanavyoamini. Mashetani hayaokoki, na wewe mkristo, unajiita mkristo lakini hauokoki? Basi uelewe umekufa kiroho na haumjui YESU wa kweli na MUNGU wa kweli. Sasa ni wakati wa mataifa yote kumjua YESU wa kweli na MUNGU awe BABA yenu, msifikirie mnamfurahisha MUNGU mnapojiita ni wakristo lakini hamuokoki, nawaeleza mnamfurahisha shetani sababu anakuwa amekuteka wewe na wewe ndiye mtumwa wake katika ufalme wa giza.
Zaidi ukisoma katika kitabu cha Yakobo 2: 14-20, 26 utaona Ibrahim alihesabiwa haki kwa matendo yake na wewe unajiita ni mkristo halafu hauokoki, je MUNGU atakuhesabia haki gani mbele zake? Imani pasipo matendo imekufa na hata sasa ndivyo ilivyo katika ulimwengu wote shetani amefanya kazi yake ya kuua roho za watu kwa kuwazuia watu wasiokoke na wajiite wao ni wakristo na watu wanaridhika. Amenituma YESU niwaeleze ukweli, watu wa namna hiyo hawapo upande wake wapo upande wa mpinga kristo. Ni mamilioni ya wakristo nilionyeshwa wakijiita ni wakristo na wakakataa kuokoka na wakazikwa na makanisa yao ambayo yaliwazuia wasiokoke sasa wapo kuzimu kwa sababu waliifuata na kuitii injili ya uongo.
Lengo la YESU ni watu wamwamini na kuokoka, ikiwa unamwamini YESU tu wewe hauna tofauti na mashetani kwa jinsi wanavyoamini kuwa ni mwana wa MUNGU. Nawasihi muokoke YESU anarudi kwa mara ya pili atamnyakua yule ambaye amemwamini akaokoka na kubatizwa katika maji mengi ya mto, siyo ya kisima, ya tenki wala ya kubatizwa kwa jina la mchungaji au kubatizwa kwa kikombe, katika batizo hizi YESU alivyoonyesha njia katika mto Yordani ndivyo tufwate hivyo hivyo na kama umebadilishwa basi uelewe umepoteza njia na kujizuia kwenda mbinguni sababu hizi batizo za tofauti na kwenye biblia ni chapa za shetani na kila mwenye chapa za shetani haendi mbinguni hiyo basi ni lazima uokoke upya na ubatizwe upya utolewe satanic nembo au alama upokee alama za mbinguni takatifu.
NOTE:
Na jambo lingine ambalo shetani aliona ni jinsi gani atawawekea alama za shetani hata wale walioamua kuokoka akaungana na wanadamu ambao ndiyo watumishi baadhi yao wamefundishwa na shetani jinsi ya kubadili neno la MUNGU, wakaanzisha baadhi yao mtu ameokoka halafu amebatizwa kwenye kisima au kwa jina la mchungaji, na hao wanakuwa wametiwa alama za shetani na mauti na kufungiwa kuwa na uzima wa milele wa mbinguni bali watakuwa na mauti milele. Na wengine wanasema YESU alibatizwa katika maji tele, ndiyo ni kweli maji yalikuwa tele yamejaa mtoni na sisi tufwate hivyo hivyo sababu wangekuja kubadilisha watu wangebatizwa mtoni hata pasingekuwa na maji ay wangebatizwa kwa kuwaeleza watu katika mto usio na maji na kuwamwagia vumbi. Ukisoma katika Yohana 22: 18-19, ipo laana ya kuzuiwa kwenda mbinguni unapobadilisha neno. Hapo ndipo mlipofungiwa na shetani watu waliookoka wakabatizwa tofauti na mtoni zaidi usome kitabu cha UBATIZO WA KWELI KWA ULIMWENGU WOTE cha Nabii Hebron utaelewa zaidi, nimeelezea utapata majibu zaidi, hii yote nakupenda wewe uliyewekewa alama ya shetani katika roho itoke na upokee ya YESU wa kweli ili akija unyakuliwe.
Zaidi siri ambayo ipo ndani ya watumishi wanaobatiza huu ubatizo wao wanaelewa kabisa wanafanya agano na shetani kukuzuia usiende mbinguni na shetani anawasaidia kiuchumi katika mambo yao ya kimwili, lakini hapa duniani watu wanawaona ni watumishi wa MUNGU ila katika ulimwengu wa roho MUNGU anawaona ni watumishi wa shetani na hata baadhi ya wenye macho ya rohoni wanaonyeshwa na ROHO MTAKATIFU pia. Na madhabahu ya jinsi hiyo siyo ya MUNGU wa kweli imebadilika ni ya miungu na ndiyo sababu unafuata mambo ya miungu badala ya kufuata biblia na kuwafanya mamilioni ya watu wapotee pasipokupenda wala kujua. Ninakusihi uokoke ili ukristo wako ukamilike na umjue YESU na MUNGU pia.
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozifanya kwa kujua na kutokujua, niliamini miungu, nilikuwa mgumu kuokoka, sasa nakukubali wewe uwe BWANA na mwokozi wa maisha yangu. Uliandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Uniongoze na roho wako mtakatifu na umtoe roho mchafu katika imani yangu akaniteka nikakukataa. Nakupenda YESU. Amen.
Sasa umeokoka, zaidi fuatilia katika website
ingia katika link ya blog na YouTube utajifunza mengi, roho wa MUNGU akuongoze. Nitaendelea katika somo lijalo kuelezea zaidi somo hili ni refu bado. Natumaini sasa umepata picha katika maisha yako ya kuwa yngenyakuliwa na YESU kwenda mbinguni au ungeachwa. Watumie na wengine ujumbe huu ili wengine wafunguke wasije wakaachwa na YESU au hata wakifa wasije wakaachwa kwenda paradise wakaenda jehanamu.
Mathayo 24: 34-35, Mathayo 23: 23-28, 13, 14.
NABII HEBRON.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni