Enyi mataifa yote nawaandikia waraka huu kama vile mimi
Nabii Hebron nilivyofunuliwa na YESU WA NAZARETI mambo haya ambayo yanaupata ulimwengu kwa kiasi kikubwa cha hatari hata
pasipo wakristo kujielewa wapo katika MUNGU au shetani wakiwa wamefungwa fahamu
zao hata wasijitambue na hata ule mwisho waje wakahukumiwe pamoja na lucifa japo
wakristo hawapendi.
Ninapowaeleza kuwa wakristo wanaenda kwa waganga wa kienyeji
wakifikiri wanaenda katika nyumba za ibada kuombewa na watumishi wa MUNGU kwa
idadi kubwa kumbe sivyo kabisa. Wanajikuta wanaenda kwa waganga wa kienyeji hao
hao ambao wanajiita manabii, mitume, wachungaji, wainjilisti, waalimu na
wengineo wenye huduma sita na kuendelea. Nitaelezea kwa ufupi na hakika utaenielewa
na ukielewa hautaenda tena kwa waganga wa kienyeji bali utawafuata watumishi wa
kweli wa MUNGU ili uonane na MUNGU.
a.
Kila mtumishi anayejiita kwa cheo chake na yeye
yupo katika mtandao wa freemason au illuminati halafu anaongoza kanisa na
waumini na matawi yake, hawa ni wachawi na wewe mkristo unayoenda akuhudumie,
akuombee pamoja na mengineyo, uelewe haujaenda kanisani bali umeenda kwa mganga
wa kienyeji.
b.
Watumishi wanaowatoa watu vitu kama mawe,
nywele, chupa, na vinginevyo hao ni waganga wa kienyeji (ni watu ambao ni
waganga wa kienyeji wakajiita ni watumishi ili wawateke watu na mali zao kwa
kutumia kivuli cha jina la utumishi kumbe yeye ni mganga.
c.
Watumishi wanaozini na waumini hao ni waganga wa
kienyeji, siyo watumishi wenye roho ya MUNGU, ndani yao ipo roho ya uganga ya
kipepo. Tazama hata watu wengi waliokwenda kwa waganga wa kienyeji wengi wao
wanazinigi na mteja wake akiwaeleza miungu imesema waingiliane kimwili na hata sasa mnayajua haya siyo mambo
mageni.
d.
Watumishi wanaonyang’anya watu mali zao, vitu
vyao, wake, na kutoa huduma za kiroho kwa kuchaji watu pesa, kuwaeleza watu
wasaini katika magari yao na nguo zao ndio watoe pesa wabarikiwe, hao ni
waganga wa kienyeji 100%
e.
Mafundisho tofauti na biblia ya Mwenyezi MUNGU
inapokuwa tofauti uelewe unaenda kwa mganga wa kienyeji sababu wao ndio wapogo
kinyume na MUNGU, na mtumishi anapokuwa kinyume na MUNGU na yeye asimcheke
mganga wa kienyeji au kumchukia sababu hao ni moja na tena ni rahisi sana
mganga wa kienyeji ambaye hajiiti mtumishi kuokoka na kwenda mbinguni kuliko
anayejiita mtumishi lakini yupo kwa kivuli cha mganga wa kienyeji. (Utawajuaje?
chunguza matendo yao).
NOTE:
Yapo mambo mengi ila haya yatakupa picha angalau uelewe
umeendaga kwa mtumishi wa MUNGU au kwa mganga, picha umeipata. Na madhara yake
ni watu wamechoka na ukristo wakaona YESU hayupo katika makanisa, ni sababu
watumishi wengi zaidi tayari wapo katika upande wa shetani wanaganga na
makanisa yao katika ulimwengu wa roho yanaonekana ni nyumba ya shetani. Sasa swali,
je? YESU anafanya kazi na watumishi waganga wa kienyeji? Jibu, hapana. Ila mapepo
ya michango, harambee ndio yamejaa makanisani kuwafilisi wanadamu, sasa mpone
roho zenu.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe. Nilifikiri naendaga kwa
mtumishi wako kumbe nilienda kwa mganga wa kienyeji pasipo kujua. Nanikaandikiwa
jina langu katika vitabu vyao vya shetani badala ya mbinguni. Nisaidie YESU,
uniokoe, nichomoe na vitu vyangu sasa hivi. Niongoze ulipo wewe. YESU WA
NAZARETI WA KWELI. Amen.
NABII HEBRON.
Posted 19th March 2015 by Prophet Hebron
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni