BWANA YESU ASIFIWE, watu wa mataifa yote, nawaandikia ulimwengu wote kuielewa habari hii ya yesu asiyejulikana ili watu wasiomwelewa wamjue na wamkatae na wamrejee YESU anayejulikana na ambaye ndiye Mwana wa pekee wa MUNGU aliye hai ambaye yuko mbinguni. Wakati wake YESU wa kurejea kulichukua kanisa umefika, ni wakati wowote, hii ni siri ya MUNGU peke yake ambaye anaijua siku hiyo. Habari hii mimi Hebron nilielezwa na MUNGU peke yake nami nawaeleza mataifa yote kwa sababu yeye ni MUNGU wa watu wote na mataifa yote zaidi yake hakuna mwingine. Ukisoma kitabu cha Matendo ya Mitume 19: 14-16
“14 walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu waliyofanya hivyo. 15 Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, YESU namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? 16 Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.”
Nitaelezea kuhusu huyu yesu asiyejulikana yukoje. Nitaelezea katika neno la MUNGU na siyo katika sura. Jina la YESU ni jina mashuhuri kuliko majina yote ya viumbe vyote duniani na mbinguni na popote pale. Huyu YESU alipokuwepo hapa ulimwenguni alisema watakuja watu watakaotumia jina lake na hata kuwapoteza wengi hata wateule na yawezekana wewe ni mteule lakini pasipokujua au kujua tayari na wewe upo katika ufalme wake, shetani amekuteka na amekuwa ndiyo kiongozi wako na tegemeo lako.
Nitaelezea kwa ufupi jinsi ya kumjua huyu yesu asiyejulikana na anafanya kazi kubwa ya kuuangamiza ulimwengu au kuwavuna wanadamu wawe mazao ya shetani au kwa lugha nyingine ni mpinga kristo.
Kila mtu anajua kuwa Yohana mbatizaji ndiye aliyetumwa amtengenezee njia huyu YESU, soma katika Matendo ya Mitume 19:4, Yohana akambatiza YESU kama alivyotumwa na MUNGU mbinguni yeye aliyetuonyesha njia ya kweli kiroho na kimwili na akasema tuifuate njia yake kama alivyoonyesha, na katika kitabu cha Ufunuo 22: 18-19, akasema, mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki mtu huyo ataondolewa sehemu yake ya uzima, na je ikiondolewa kinachobakia basi ni sehemu ya mauti, hukumu au jehanamu ya milele.
Alivyosema watatumia jina langu YESU alijua na aliona mbele na ndivyo ilivyo na imekuwa na mnayaona kwa sababu kila alilolisema YESU neno lake lazima litimie yeye ni MUNGU.
NOTE:
Huyu yesu asiyejulikana na kama hajulikani ina maana yeye hajazaliwa na Maria hapa duniani wala hakufa na kufufuka wala hakuonekana akitenda miujiza yeyote wala kuhubiri hapa duniani.
Huyu yesu asiyejulikana hutumia biblia kulichanganya neno la MUNGU wa kweli na mafundisho ya uongo ambayo hayapo katika biblia. Kama angetumia kitabu kingine tofauti na biblia watu wangekataa, hivyo alibuni njia hiyo na akafanikiwa kuwateka wengi zaidi na watu waka amini wapo sehemu sahihi kabisa wakijua wataenda mbinguni na kumbe katika ule mwisho wataenda jehanamu iwapo hawatabadilika leo na kumrejea yeye YESU wa kweli ili watengwe na huyo yesu asiyejulikana.
YESU anayejulikana yeye alisema tubatizwe kama yeye katika maji mengi yanayotembea. Sasa huyu yesu asiyejulikana yeye ana viapo vyake na unapovipokea tu na wewe unakuwa mfuasi wa yesu asiyejulikana bila kujua wala kupenda japo wapo wengine wanaopenda.
Ubatizo wowote ambao ni tofauti na YESU alivyobatizwa unakufanya kuwa mfuasi wa yesu asiyejulikana kwa sababu ni viapo visivyo kuwepo katika kitabu kitakatifu cha neno la MUNGU.
Ubatizo wa maji ya kikombe, je ubatizo huu utasema ni wa YESU anayejulikana? Jibu siyo. Unapompokea tu na wewe unafanyika kuwa mfuasi wa yesu asiyejulikana. Kama unabisha tafuta ni wapi YESU alibatizwa kwa maji ya kikombe? Na zaidi neno kubatiza maana yake ni kuzamishwa, je huoni kufanya tofauti ni uongo mtupu.
Umemwagiwa maji matone wakati miguu, mikono, mgongo, haujaingia katika maji! Hivyo usipinge, acha kutetea uongo, unapoutetea na wewe unapokea dhambi ya kuiharibu injili ya kweli na kuimarisha uongo, huyo ni yesu asiyejulikana, hivyo hata ibada zako, maombi yako, sadaka zako, uelewe unampatia yesu asiyejulikana.
Hivi nikuulize wewe unamjua yesu aliyebatizwa katika maji ya kisima? Sema ukweli, jibu lake ni haumjui!
Hivi unamjua yesu aliyebatizwa kwa jina la mchungaji? Huyo hajulikani, huyo ni pepo.
Hivi unamjua yesu anayetoza watu pesa za maombezi? Mimi Hebron simjui wala siyo YESU aliyezaliwa na mama Maria wala siyo YESU ambaye ndiye mwana wa pekee wa MUNGU, na wewe mkatae huyo yesu asiyejulikana na mambo yake. Namfahamu YESU aliyesema“nimekupa bure, toa bure” huyo ndiye YESU anayejulikana. Ukikutana na maombezi ya pesa uelewe unakutana na yesu asiyejulikana au yesu wa wanyang’anyi au wezi.
Yesu asiyejulikana yeye hufufua misukule kwa mazingaombwe bali YESU anayejulikana yeye alifufua kina Lazaro na wengineo waliojulikana na jamii na watu wakawaona kwa macho ya nyama na wakafufuka. Hao wanaofufua misukule ni wachawi, wapeleke hospitali maiti zimejaa mortuary hawatafufua, watakimbia. Hao wanafanya miujiza ya kichawi.
Ili uwe na YESU anayejulikana ni lazima uokoke, ila huyu yesu asiyejulikana utajiita ni mkristo na wala hautaki wokovu. YESU anayejulikana yeye alileta wokovu ili kila atakayempokea awe mfuasi wake na asiyempokea hatakuwa mfuasi wake. Sasa huyu yesu wa uongo yeye anaaminiwa na watu wengi zaidi katika ulimwengu wote na mataifa wamepigwa upofu wanaona wapo sawa sawa wanampendeza MUNGU wa mbinguni kumbe wanamchukiza MUNGU wa mbinguni kabisa na kumkana kwa hayo matendo.
YESU anayejulikana katika kitabu kitakatifu cha BABA yake (Biblia) amesema usitoze riba, ila huyu yesu asiyejulikana yeye huweka benki na kutoza riba. Hapa sasa mnaelewa tofauti ya YESU anayejulikana na asiyejulikana na yapo mengi utazidi kufunuliwa ili hili giza liondoke katika maisha yako na kwa wengineo.
Imeandikwa nyumba ya BABA yangu ni nyumba ya sala, YESU anayejulikana alipoingia katika nyumba ya ibada akayakuta yameletwa mambo ya yesu asiyejulikana, aliyatupia nje. Sasa yamerudishwa na kutawala, mfano harambee, michango, mwenye pesa anatoa ndiyo anaombewa, kulazimishwa kuahidi utatoa pesa ngapi na mengineyo. Mimi Nabii Hebron nawaeleza huyo ni yesu asiyejulikana, mimi simfahamu na simtaki kabisa, na wewe mkatae, ni mnyang’anyi 100%.
Huyu yesu anayewapenda matajiri tu, huyo ni yesu asiyejulikana hata hao wanaoona wanakutana na YESU kupitia huyo mtumishi nawaeleza wamekutana na myang’anyi, ni pesa zao ndizo zinazotakiwa tuu na si chochote.
YESU anayejulikana yeye alianzisha huduma tano (5) zilizoongozwa na Mtume na Nabii, wala hakusema huduma ya uaskofu ndiyo iongoze kanisa na hii ya uaskofu ni huduma ya sita na huduma hii ya uaskofu kibiblia ni kazi ya uangalizi wa kanisa kama kufanya usafi, kupanga viti na mengineyo.
YESU anayejulikana amesema utoapo sadaka yako iwe ni siri yako tu. Isijulikane na mtu. Ila yesu asiyejulikana yeye sadaka utaandika jina, utapewa risiti na hata utapewa cheti cha hongera umetoa vizuri, zaidi huyu yesu asiyejulikana husoma majina ya watu waliotoa sadaka kupitia mtumishi wake katika kanisa lake, kinyume cha MUNGU alivyoagiza katika neno lake au sheria.
Yesu asiyejulikana ili kumwelewa kwa wepesi yeye huchanganya uongo na neno la MUNGU yaani giza na nuru, na tunajua kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya giza na nuru.
Yesu asiyejulikana na yeye vile vile ana manabii wake, mitume, wachungaji, wainjilisti, waalimu na zaidi wale watumishi ambao hapo awali walikuwa wameitwa na MUNGU kisha wakamuasi MUNGU wao hujiunga na huyu yesu asiyejulikana na kuendeleza yale ya uongo wakijificha kwa kutumia jina la YESU.
Watumishi wa yesu asiyejulikana hutumia uchawi, mizimu, kwenda kuzimu, hutoa makafara na hata makanisa yao katika ulimwengu wa roho hufanyika kuwa sehemu ya kuwatoa waumini kafara na sadaka kwa shetani hiyo huwa ni siri ya kuhani na maagano yake na shetani.
Je, umeshajiuliza ni kwa nini wakristo wengi zaidi wanateseka, wanalogwa na shetani na wachawi? Jibu ni kwamba ndani yao hayupo YESU anayejulikana na huyo hawezi kuwapiga wachawi, kwa sababu ufalme ulio pamoja hauwezi ukaufitini ufalme mwenzake.
YESU anayejulikana yeye alivyokuwa mtoto alibarikiwa tu na alipokuwa mtu mzima alibatizwa, huyu ndiye mfano wa kuifuata. Ila yesu asiyejulikana yeye hufanya kinyume; mtoto mdogo humbatiza (tena uongo), hazami kwenye maji na akiwa mtu mzima ndiyo hubariki sasa angalia huu upinzani unavyopewa kipaumbele na yale ya YESU anayejulikana hayatakiwi.
Nawasihi mataifa yote mrejeeni YESU anayejulikana, wakati ni sasa, ukifa pasipo kupata huyo YESU wa kweli hakika utakwenda kwa huyo huyo asiyejulikana ambaye anayo mbingu yake isiyojulikana (amabyo ni Jehanamu) na usifanye kazi ya yesu asiyejulikana utaangamia, unapata dhambi unafanya kazi ya shetani pasipokujua.
Kwa YESU anayejulikana yeye mkitaka kumwomba MUNGU mnapitia kwake (YESU anayejulikana) tu na siyo kwa watoto wa MUNGU waliopita. Ila kwa yesu asiyejulikana, unapitia kwa watakatifu waliopita ambao ni watu kama wewe tu, na kukupeleka jehanamu. Hapo unakua unaabudu mizimu na majini ya miungu.
Sema, BWANA YESU unayejulikana naomba unisamehe dhambi zangu zote. Namkataa shetani na kazi zake na sikutaki tena wewe yesu usiyejulikana, toka ndani yangu. Kuanzia sasa wewe YESU unayejulikana ingia ndani yangu wewe ndiye mwana wa pekee wa MUNGU aliye hai. Amen.
Ubarikiwe! Watumie na wengine.
NABII HEBRON.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni