Wafilipi 2:10-11
 • JE UTATOFAUTISHAJE UTENDAJI KAZI WA NGUVU ZA MUNGU KATIKA KANISA NA NGUVU ZA SHETANI KATIKA UTENDAJI KAZI WAKE MAKANISANI?  BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE, YESU wa watu wote na ndiyo sababu anaitwa YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE. Ikiwamo na wewe na wengine, YESU anakupenda sana, haya ni maneno aliyonieleza mimi Hebron kwa mdomo wake YESU niwaeleze mataifa yote anawapenda sasa na nyie mpendeni ili awe mwokozi  kweli uokoke sasa.


  Nitaelezea jinsi nguvu za MUNGU zinavyotenda kazi  kwa mtumishi na pia nitaelezea kuhusu nguvu za giza vile vile huwa zinatenda kazi makanisani katika sehemu baadhi, ila watu wanafikiria ni nguvu za MUNGU au YESU sababu tu kanisa linaitwa kwa jina la YESU la hapana, mimi pia nilipokaa na YESU aliponifunulia siri hii niliogopa sana nikajikuta hata  mimi  nilikuwa namtafutaga YESU sehemu mbali mbali katika makanisa baadhi na kwa watumishi baadhi yao, ila sikumpata YESU wa kweli bali nilimpata yesu wa uongo na sasa simtaki hata kumuona tena wala kumsikia sababu yeye ndiye anajaa 98% katika ulimwengu wote ila sasa yule YESU wa kweli sasa atajulikana na waliopotezwa sasa mtaponywa na yeye. Ukisoma katika kitabu cha ( 1Yohana 4:1-2) YESU anasema wapenzi msiamini kila roho bali zijaribuni kama zimetokea kwangu, na mtazijua kwa kuliangalia neno je lipo kweli sawa na ilivyoandikwa ( Yohana 17: 17) neno lake ni kweli na silo la uongo, ila hapa watu wameshindwa kutofautisha katika roho  wa MUNGU ni yupi na wa shetani ni yupi, miujiza ya MUNGU ni ipi na ya shetani ni ipi? Mshukuru YESU sababu unapona sasa katika jina la YESU.


  a.) JINSI NGUVU ZA MUNGU ZINAVYOFANYA KAZI KATIKA KANISA.


  Nguvu za MUNGU ikiwamo na miujiza yake, siku zote hutolewa bure sababu neno lake ni kweli. Anawaponya watu bure bila malipo yoyote yale wala MUNGU hakudai pesa au chochote ndio akuponye wala haangalii wewe ni tajiri au maskini. Miujiza yake inapitia kwa watumishi wake ambao hawachaji mtu pesa na siyo wachawi au waliomsaliti YESU.


  b.) JINSI NGUVU ZA SHETANI ZINAVYOTENDA KAZI KATIKA KANISA.


  Nguvu hizi makanisani haziitwi nguvu za shetani sababu watu wakijua watakimbia katika kanisa hilo au kwa huyo mtumishi, ila linatajwa jina la YESU hivyo hivyo. Sasa usishangae kwa nini linatajwa, kumbuka YESU alisema watakuja na watatumia jina langu hivyo hivyo na watawapoteza wengi kama ilivyo sasa, mtawajuaje ni kwa matendo yao katika kila jambo  yapo mengi ila nitakuelezea katika utendaji na nguvu za shetani  makanisani na miujiza yake .

  Kwanza kabisa uelewe kuna neno la MUNGU  na ahadi zake ni kweli na siyo uwongo alisema mtaponywa bure bila pesa. Sasa unapoelezwa ili uponywe leta pesa kiasi fulani na mtumishi uelewe ndani yake yeye anatumika na shetani na mizimu 100% hata kama ananena au anasoma biblia hata kama anayo master ya bible, na hata akibatiza ubatizo tofauti na wa Yohana, bado pia hapo ni roho ya shetani na hata hao watu wanakuwa wamewekwa katika mikono ya roho wa shetani katika ulimwengu wa roho na waumini wakijua wapo kwa roho mtakatifu kumbe wapo kwa roho mchafu yaani roho wa shetani. Hii ni siri iliyofichika sana ila YESU amenituma niwajulishe wewe utakayesikiliza utapona roho yako sasa.

  c.)   Ukiona maombi ya kusali uchi, maombi ya kufanyiwa watu wanachukuliwa nguo zao za ndani na watumishi eti wakaziombee hao ni wachawi na roho waliyonayo ni ya shetani. Pia nguvu za MUNGU hashiriki hata siku moja katika kanisa linaloabudu sanamu, au ubatizo tofauti hivyo basi uelewe umedanganyika kama upo katika eneo hilo sababu yale aliyoyakataa MUNGU wao wanayatenda sasa jiulize mwenyewe je MUNGU ni kigeugeu aende katika sanamu? Hapo ni roho wa shetani (au mpinga kristo) na mtu  ukisali hapo na wewe unaunganishwa katika madhabahu hiyo ya jehanamu.


  d.) Mtumishi huduma yeyote au kanisa linalochangisha watu pesa, kuwachaji watu pesa za aina yeyote kwa ajili ya kuindeleza huduma hizo hazina ROHO MTAKATIFU bali ni roho wa shetani, tazama neno linasemaje? na neno ni kweli sasa hauoni huu ni uwongo? Na kama ni uwongo je uwongo unatokea mbinguni? Jibu hapana. Iwe ni muujiza, mapepo yanalia, utabiri wowote ule na mafanikio hayo uelewe yanatokea kwa roho wa shetani ili awateke watu. Utajuaje? ni kwa matendo yao hata kama anafufua watu misukule ni roho mchafu atendaye kazi na hayo ni masharti yake lazima malipo na michango.

  e.)  Tunajua  YESU ndiye mtenda miujiza  mkubwa, sasa cha ajabu wapo watu wanawazuia watu wasipokee miujiza ya YESU au kusema wanakimbilia mujiza, katika jambo hili nataka muelewe ipo miujiza ya shetani na ipo ya MUNGU vile vile na inafanyika katika makanisa baadhi kupitia watumishi wa shetani wanafanya ya shetani, na wa MUNGU wanafanya ya MUNGU kama nilivyoelezea hapo juu sasa utaijuaje utaipima katika neno, na tabia za mtumishi wa kanisa hilo  kwa kumuomba ROHO MTAKATIFU atakuelezea  kama unaye kweli. Kanisa lisilotenda miujiza hilo limekufa kiroho na YESU mtenda miujiza hayupo sasa kama hayupo unafanya nini hapo? Na watu wengi wanafungiwa makanisani wanaelezwa wanafuata miujiza jiulize kwa nini hautendeki hapo unaposali ipo shida gani? Je YESU anawachukia jibu hapana, ipo shida.


  Na uelewe pia miujiza  ya shetani ndiyo imetawala katika mabara yote kwa kiwango kikubwa sana na watu huifuata pasipokujua bado wanakuta  wanaenda kwa shetani tena. Hivyo omba kabla ya kwenda mahali na utaongozwa na MUNGU ili shetani asikupate.
  Zaidi ingia katika websitewww.prophethebron.orgingia katika link ya youtube na mengineyo utafunguka zaidi. Na uwatumie wengine address hii utabarikiwa na YESU.

  Sema, BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele uniongoze wewe nisitekwe tena  katika miujiza ya shetani nikawa tena mtu wa shetani.
  Amen.

  NABII HEBRON

  Hakuna maoni:

  Visits

  Translate