Wafilipi 2:10-11
 • ZIJUE SIRI KUBWA ZA SHETANI
  KITABU: JINSI NABII HEBRON ALIVYOITIKISA KUZIMU  (MAFUNDISHO YA NABII HEBRON)
  Zijue siri za shetani (Part I)

  TOLEO LA 16
  ISBN 978 9987 9717-7-0
  UTANGULIZI
  Nawasalimu watu wote wa mataifa yote kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI ambaye ndiye mwana wa pekee na sasa yupo mbinguni kwa BABA yake anasubiri tena kuja katika unyakuo akiwa angani awanyakue wale wote ambao wamemkubali, wakaokoka, wakabatizwa ubatizo wa maji mengi yanayotembea na watakaokuwa wanaishi maisha matakatifu peke yake.
  Jina langu mimi naitwa Hebron Wilson Kisamo, kabla ya kuwa mtumishi wa MUNGU, mimi kazi yangu ni Professional Driver Guide kazi ambayo niliifanya katika nchi ya Tanzaniakatika mbuga za wanyama katika miji na milima mikubwa yote ya Tanzaniapamoja na Zanzibar. Ilipofika August 2009 nilikuwa nyumbani mchana nilikuwa ninaomba ni siku ya jumapili mchana, ghafla akaja Malaika Mkuu wa MUNGU anayeitwa Mikaeli nikiwa katika maombi, akaniambia Hebronusiogope, katika maombi uliyoyafanya leo na rekodi ya makanisa yote, wewe umefanya kazi kubwa hata kuliko watumishi wote kwa kile ulichokifanya katika ulimwengu wa roho katika ulimwengu wote, niliogopa hiki ni nini? Akanieleza mengine ambayo hayo ni yangu peke yake kisha akaniambia tumekuja watatu nipo na YESU na pia Malaika Gabriel, akanishika mkono, akaja YESU sasa akanikumbatia, na wakati huo kwa ule ukuu wa YESU nilikuwa ninaogopa, na yeye akanieleza yale aliyoniambia ambayo ni yangu, akaondoka, akaja Malaika Gabriel. Yeye akasema na mimi kwa muda mrefu, akaniambia Hebron wewe ni mtumishi wa MUNGU na utakuwa na huduma yako peke yako ambayo utasimamia wewe peke yako na itafika wakati huduma utaianza ukiwa unafanya kazi na itakuwa ni mahali fulani hapa hapa Arusha. Akaniambia MUNGU akubariki sana, haya narudi mbinguni. Niliendelea na kazi zangu lakini maneno hayakutoka katika ufahamu wangu na kila nilipokuwa nataka kuwaeleza watumishi mdomo wangu ulikuwa bubu.
  Ilipofika 2010 March, hali ikajirudia YESU akaanza kusema na mimi hata nikiwa na wageni katika gari, na hata nikiwa peke yangu iwe natembea kwa miguu au ninaendesha gari na mara nyingine hata nikiwa Game Drive porini, lakini hakuna mtu yeyote aliyejua, akanieleza mengi sana hata katika habari za wanyama aliowaumba MUNGU ambao wanyama wote hao ni wa BABA yake. Nilikuwa naagalia simba, nyumbu, punda milia na wanyama wengine tukiangalia na YESU na yeye pia anawapenda wanyama na uumbaji wa MUNGU na anachukia sana uumbaji alioumba MUNGU unapoharibiwa na akaniambia Ole wao wanaoharibu uumbaji wa MUNGU yaani kazi ya mikono ya MUNGU. Na wakati mwingine nilikula na yeye chakula nilichokuwa ninakula mimi na akinipa mifano ya maisha aliyoishi hapa ulimwenguni akiwa na wanafunzi wake. Akaniambia nimekula na wewe chakula hiki unachokula kama vile nilivyokula na wanafunzi wangu kipindi kile, wewe ni rafiki yangu na ni mwanangu.
  Ilipofika 14.6.2010 siku hii akanitamkia rasmi wewe ni mtumishi wa MUNGU na umeandaliwa kwa ajili ya kanisa la mwisho ili kuwapeleka watu mbinguni. Ndani yako nitaishi mimi, ataishi MUNGU, ataishi ROHO MTAKATIFU. Nitakufundisha kuongoza wewe nipe mwili wako tu. Nikamuambia sawa BABA nipo tayari, kanisa uliite YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, usiogope lolote, adui yako ni adui wa MUNGU. Anayepigana na wewe ajijue anapigana na MUNGU na hakuna chochote kitakacho kudhuru au kukuweza siku zote za maisha yako kuanzia siku hiyo. Akaniambia Hebron utachukiwa sana kwa sababu umenikubali mimi na kwenda na mimi, ila wewe furahi na upige makofi. Na wivu utainuka kutoka kwa watumishi wengi zaidi sababu ya huduma niliyokupa, ila uonavyo hayo uelewe ni shetani yupo ndani yao.
  98% wamenisaliti imebakia 2% katika ulimwengu wote ndio watumishi wa kweli na hawa 2% wamekandamizwa na shetani kupitia hawa hawa watumishi, wamekuwa freemason, wachawi, wanyang’anyi, wanatoa makafara, wameifanya nyumba ya MUNGU kuwa ni sehemu ya biashara, michango, kubadilisha neno la MUNGU na kuwalisha watoto wa MUNGU maneno ya uongo, mfano ubatizo wa kikombe, kuabudu sanamu, kuwazinisha na waumini na matendo mengi ya ufisadi. Akaniambia sasa hivi mimi siyo BABA yao wao wanaye babayao ambaye ndie shetani, midomoni mwao wanalitaja jina langu ila ndani ya mioyo yao ni wanafiki, wauwaji wa roho za watoto wa MUNGU. Ila kwa wewe nalijenga kanisa ambalo malango ya kuzimu halitaliweza, kamavile nilivyolijenga kwa Petro. Petro wa leo ndio wewe.
  Sikumuelewa YESU ila siku zilivyoendelea aliendelea kunifundisha nikamuelewa na mpaka nikaanza kuifanya kazi yake. Ila hapa nitaelezea nilivyoenda kuzimu kuipiga, nilienda na wazee 24 na Malaika Mikael, baadaye nikawa naenda na YESU akanionyesha mahali pa kupiga na kulipua kuzimu na mpaka nilivyomkamata Joka Kuu 5.11.2012 baadaye nikawa naenda peke yangu kama ilivyo sasa, nikifanya kazi ya kuubomoa ufalme wa shetani na hata ilipofika 2.6.2014 nilimkamata mwanadamu ambaye alikuwa yupo katika nafasi ya tatu katika ufalme wa shetani 1) Joka Kuu, 2) Lusifa, 3) Maxwell; na sasa yupo katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, sasa anaitwa Isaya, yeye alikuwa ndie mtunza siri, zote za shetani na alikuwa anayo mafaili yote ya ulimwengu huu na siri zote za shetani. Ila sasa mafaili hayapo tena kuzimu yapo yamehifadhiwa na serikali ya mbinguni. Hivyo nitawaelezea siri za kuzimu ili mfunguke, sababu shetani ni mpumbavu sana na nia yake ni kutaka hata wewe uangamie ili uchomwe pamoja naye kuzimu
  Na sasa ndipo ule unabii wa kanisa la mwisho unatimia na milango ya kuzimu haitaliweza zaidi soma katika blogwww.prophethebron.blogspot.com na website www.prophethebron.org na YouTube yangu utayakuta mambo mengi na utakuwa huru. Ni maneno ya habari njema ili ulimwengu upone na watu wamrejee YESU sababu kweli yupo ila 98% ni yesu wa maboksi (wa uongo ndiye aliyemiliki 98%).
  SHUKURANI
  Nawashukuru watoto wangu wa kiroho wote niliowazaa kiroho pamoja na watumishi wangu walio katika kanisa langu, wameniombea, na wengine wote wenye mapenzi mema na mimi na kwa YESU WA NAZARETI.
  Asante.
  MTUME NA NABII HEBRON WILSON KISAMO
  KIONGOZI NA MWANZILISHI WA HUDUMA
  KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRY.
  P.O.BOX 74
  ARUSHA, TANZANIA.
  EAST AFRICA.
  EMAIL: maombi@prophethebron.org
  WEBSITE: www.prophethebron.org
  BLOG: www.prophethebron.blogspot.com
  NAMBA ZA SIMU: +255 759 610 820
                                     +255 764 042 149
                                     +255 763 567 402
                                      +255 759 253 593  YALIYOMO
  1.    Utangulizi.
  2.     Shukurani.
  3.    Kuzimu ilivyo.
  4.    Benki ya Kuzimu.
  5.    Mavazi ya Kuzimu.
  6.    Nchi 15 za Kuzimu.
  7.    Mto wa Maji ya Kuzimu.
  8.    Silaha tisa kubwa za shetani.
  9.    Nini maana ya Christmas Tree?
  10.                       Nini maana ya Father Christmas?
  11.                       Siri za Kuzimu.
  12.                       Mawigi (weave) ni nywele za siri za Majini.
  13.                       Nguo zote za mitumba zina Mizimu.
  14.                       Adamu wa pili ni nani?
  15.                       Madawa ya Nywele yaliyotokea Kuzimu.
  16.                       Sifa za Nabii wa Mwisho.
  17.                       Brian Deacon siyo YESU.
  18.                       Sala Ya Toba.
  JINSI KUZIMU ILIVYO
  Kuzimu ni nini?
  Kuzimu ni mahali ambapo ni makao ya shetani na Joka kuu pamoja na malaika zake na mapepo na majini. Kuzimu ipo chini ya ardhi ya 900. Kuzimu kuna miji kama hapa ulimwenguni palivyo ila tofauti yake kuzimu pamejengwa kwa mpangilio, kuna magorofa ambayo hapa duniani hamna, kuna viwanda vya magari, nguo, vyakula, silaha na vinginevyo vingi. Katika dunia hii siyo kila mahali kwa chini ni kuzimu, mfano hapa Tanzania katika ardhi yake hata utoboe mpaka mwisho hautafika kuzimu, sababu kuzimu haipo full kama vile huku duniani palivyo, ila nitaelezea kwa ramani ya kuzimu ilivyo kwa chini ukitoboa ardhi utatokea au wanatokea katika ardhi ya China, Russian Federation, Australian Federation, United Kingdom, Lagos, U.S.A, Madagascar, Sudan, Syria, Ethiopia, Angola, Egypt na Libya. Katika utawala wa Joka Kuu alikuwa anao wakuu watatu; wa kwanza Joka Kuu huyu ndiye mungu wao na ndie kiongozi wa miungu yote ya uongo. Pili Lusifa, yeye ndiye mwana wake wa pekee, na tatu ni Maxwell yeye alikuwa ndiye roho mtakatifu wa kuzimu ambaye ndiye roho mchafu wa shetani. Ila sasa nimemtoa kuzimu anaitwa Isaya, ameokoka.
  Joka kuu yeye alikuwa anao mji wake unaoitwa Freeman Village ila kwa sasa nimeshaulipua kwa kutimiza kazi ya BABA yangu wa mbinguni alionituma. Yeye aliishi umbali wa ardhi ya milioni mia tatu (300,000,000) kutoka katika ardhi ya dunia.
  Lusifa yeye anaishi umbali wa ardhi 299,500,000 kutoka katika ardhi ya dunia.
  Maxwell (ambaye ndiye Isaya) yeye aliishi ardhi ya 299,000,000.
  Hao wengine wote huko kuzimu wapo mbali katika ardhi ya 100,000. Ukiangalia hapa utaona jinsi Joka Kuu alivyoitengeneza Serikali yake na kujitenga nao mbali, hao wengine wote.
  Ofisi ya kuzimu head office ambayo sasa imeshachomwa haipo ilikuwa inaitwa (JLM)- Joka Kuu, Lusifa, Maxwell Office, hapo ndipo palipokuwa na mafaili ya serikali ya shetani ili kuwaangamiza watu.
  NOTE:
  Katika ofisi hii wachawi wote ndipo walikuwa wanaenda kuchukua nguvu na hata watumishi wanaotumia nguvu za giza na freemason, sasa ulimwengu utapumua sababu ya YESU WA NAZARETI kuubomoa ngome zao na wataaibika huo ndio ukweli, hapo ndipo wanapochukulia pesa na pesa za kuzimu wanatumia dola kabisa.
  Kuzimu ni pabaya ajabu chakula chao ni nyama za watu ambao wamekufa huku ulimwenguni na sahani zao ni mafuvu ya vichwa vya watu.
  Katika hii ofisi kubwa ilikuwa inavitengo vya kila aina mfano cha makanisa na kiongozi wake ni jini linaitwa Amakuta, wanabadilisha biblia halafu wanawaletea wanadamu elimu tofauti iingizwe kanisani na inapoingizwa tu tayari hilo kanisa linakuwa ni la kuzimu na YESU haonekani hapo. Mfano kanisa lenye ubatizo wa kikombe tayari muelewe limekuwa la kuzimu haijalishi jina la YESU linatajwa. Jiulize ubatizo wa kikombe upo katika biblia unayoisoma? Jibu, haupo au ubarikio wa watu wazima, au kuabudu sanamu, au watumishi kuvaa kofia kanisani, hawa wote asili yao ni biblia ya kuzimu na wanadamu wengi wanapokea mapokeo bila kujua wanamtumikia shetani na mbinguni hawataenda bali ni kuzimu. Hiyo tayari ni njia ya kuzimu.
  Kanisa linaloruhusu ndoa za jinsia moja hilo usidanganyike silo la mbinguni, lipo kuwapeleka watu kuzimu katika kanisa nililoliona pamoja na biblia yao, YESU alisema watakuja makristo wengi na watatumia jina lake kuwateka wengi na ndivyo ilivyo. Ashukuriwe YESU aliyenionyesha hayo na niwaeleze siri hizi mpate kupona, ni mambo yaliyofichika yasingejulikana ni mpaka YESU kwa neema yake. Na zaidi wewe mkristo kama unaabudu katika kanisa linalofanya hayo niliyoyaandika chukua biblia yako mfuate pastor muulize mbona ubatizo huu haupo katika biblia akueleze, hana jibu. Ila wewe uelewe ameingiziwa biblia ya shetani na ndio sababu anabatiza ubatizo wa shetani, funguka uelewe hapo hapapeleki mtu mbinguni bali ni mahali pa kuwapotezea watu muda wasimjue YESU wa kweli na akija asiwapate. Amenituma niwaeleze ukweli, watu wote wa mataifa yote, hata unaposoma kitabu hiki maneno haya usione ni ya Hebron, hapana, ndivyo ninavyoelezwa na YESU mwenyewe na wewe uyapokee ili upone, na shetani hapendi mjue siri hii kabisa ila endelea kusoma, yapo mambo mengi katika kurasa zifuatazo.  BENKI YA KUZIMU (JLM BANK)
  Benki hii kirefu chake ni Joka Kuu, Lusifa, Maxwell benki. Ndiyo benki ambayo ilikuwa inawapa watu pesa huku ulimwenguni pamoja na freemason ila nimeichoma na mtaona baadhi ya nchi zilizokuwa zikipata pesa kutoka kwenye benki hii, mtaona uchumi ukishuka, au mabenki yakififia na pia matajiri waliokuwa katika mtandao wa freemason wataporomoka. Ni wakati sasa ya watu wanaomtegemea MUNGU kutajirika na kumiliki. MUNGU anachukia sana na kazi hii ataifanya yeye mtakapoyaona hayo msishangae. Benki hii ina wanachama wengi sana waliopo duniani, wakiwemo manabii, wachungaji, wainjilisti, mitume, waalimu, wachezaji mpira maarufu, wasanii maarufu, idadi kubwa wanachukua pesa huko na ni watenda kazi wa shetani  (Black Money). Wana pesa ambazo ukiwakagua kimahesabu utaona ni pesa zisizojulikana zimetoka wapi asili yake.
  Kama nilivyowaelezea tokea YESU aniite nikamtumikie lengo ni kuwakomboa watu wa mataifa yote wamrudie yeye na kuwatoa katika mateso ya shetani na kuubomoa ufalme wake kama ilivyo sasa na mpaka ule mwisho wake. Hapa ulimwenguni siyo jambo geni mnasikia watu wamekuwa freemason iwe katika kila sekta ili wapewe pesa na shetani, ni wengi mmesikia kuwa kuna watu wanapesa nyingi hata ukifikiria asili ya pesa zake hautajua alipatia wapi na ndio matajiri wengi katika ulimwengu wote hao walikuwa wanachukua pesa katika benki ya shetani ilivyokuwaga kuzimu ila sasa benki hiyo imechomwa na YESU WA NAZARETI haipo tena na wala watu waliokuwa wanategemea pesa za freemason mtaona wakiporomoka, filisika katika dunia yote, myaonapo hayo ujue ujumbe aliyokuletea Nabii Hebron wa Tanzania umetimia, hawatapata pesa tena sababu benki ya kuzimu nimeichoma moto pamoja na wafanyakazi wake wote huko kuzimu.
  Benki hiyo ya kuzimu ilikuwa inaitwa (JLM BANK) kirefu chake ni majina matatu ya shareholders (Joka kuu, Lusifa, Maxwell Bank) benki hii ilikuwa inatengeneza pesa aina ya dola tu na cha ajabu hata huku duniani zikiwekwa katika machine ya kukagua pesa zinaonekana ni original kamahizi hizi zinazotumika duniani. Pesa hizi ndio walizokuwa wakipewa watumishi waliojiingiza katika mtandao wa freemason, wasanii, viongozi mbali mbali, wafanya biashara na baadhi ya vyama vya siasa katika nchi mbali mbali (pesa chafu). Nitaelezea katika kanisa ili watu wapone wasidanganyike sababu kupitia hizi pesa, kupitia watumishi wanaompenda shetani walijiingiza na kuliingiza kanisa kiasi cha 98% ikatekwa na shetani na YESU akabakia na 2% ya watu, 98% ikawa ni idadi ya joka kuu. Ndugu msomaji pesa hizi zilikuwa zinaletwa kimwili kutoka kuzimu kupitia malango ya nchi ambazo nimezitaja katika makala ya Nabii Hebron isemayo Je unajua kuzimu ipo wapi katika ramani ya dunia? Na cha ajabu hata hizo serikali za nchi hazihusiki na kupokea hizo pesa wala kujua. Ilikuwa ni jambo la siri, na cha ajabu mtaona baadhi ya makanisa yanaibuka na utajiri ambao unaleta maswali ghafla ghafla, waliokuwa wanapewa pesa ili waje waieneze injili ya shetani kwa spidi ili YESU akose watu, na utaona ukichunguza sababu wengi mnayajua haya  ila leo ni siku ya kuhakikishiwa jibu lako ulilosubiri muda mrefu hadi leo YESU WA NAZARETI anakufichulia. Na kupitia pesa hizo za shetani hapa ulimwenguni yamejengwa makanisa mengi sana kupitia pesa za shetani na watu wakaona ni pesa kutoka kwa MUNGU kumbe ni shetani. Nanukuu maneno ya YESU alivyonieleza hata kabla ya kuiivunja hii benki, akaniambia Hebron mtumishi wangu wanadamu wanafikiri mimi nipo katika hayo magorofa, vinanda, mimi sipo hapo kabisa na sitendi mimi, hayo ni majengo ya shetani, mimi nilibakia nikishangaa ila sasa namuelewa, kumbe pesa ni za shetani. Je nikuulize swali, je shetani akijenga nyumba yake YESU ataweza kuja kukaa katika hekalu la shetani? Jibu, haji, hii ni sababu ya pesa za freemason na unapoabudu katika kanisa la jinsi hilona wewe muumini tayari umetekwa na shetani, leo ufunguke utoke huko.
  Kanisa lenye benki- benki hiyo asili ya mwanzilishi wa huduma hiyo uelewe ukweli, huyo amepewa mtaji na shetani na kazi anayoifanya ni kueneza ufalme wa shetani, na kupitia benki hizo kila anayeweka pesa hapo ananyang’anywa nyota, uthamani wa pesa zake zinapelekwa kwa joka kuu na matokeo yake matatizo na kufilisika hakukuachii na mwisho wa kifo chako unabakia kuzimu, sababu pale tu unapopeleka pesa yako katika benki za kanisa nafsi yako inatekwa unakuwa umeshakufa kiroho ila mwili unabakia gogo. Siri anakuwa anajua kiongozi mkuu wa huduma hiyo hayo ni maagano ya kutoka kwa shetani afanye biashara. Wakati YESU WA NAZARETI alisema usisumbukie chochote, fanya kazi yangu, sasa pima maneno hayo.
  Yatakayotokea na yameshaanza kuanzia sasa, mtaona muelekeo unapotoa na kufilisika na mengineyo atafanya MUNGU peke yake sababu ya hasira aliyotesewa watoto wake na baadhi ya wachawi na watumishi kuwateka watoto wa MUNGU, ndivyo ilivyo na hakutabadilika.
  Pesa hizi za kuzimu zinatumika katika nchi mbali mbali kuvuruga amani iliyoletwa na MUNGU, kazi kubwa ni VITA.
  NOTE:
  Hivi umeshajiulizaga huko wanakotoaga misaada ya kuwaletea pesa makanisani na miradi je wao hawana shida na hizo pesa? Hivyo ndivyo ilivyotumika kuliingiza kanisa kwenye freemason na kupitia watumishi ambao wanatekwa na shetani. Na kuanzia kutumia jina la YESU kuzini roho za wana wa MUNGU pasipo kujua na kupenda.
  MAVAZI YA KUZIMU
  A)    WANAWAKE
  Ø  Mavazi haya ya kuzimu ambayo wanawake wanayovaa hapa ulimwenguni pasipokujua na wengine wakijua kabisa ni ya shetani ambayo yanabuniwa na Yezebeli ili kila anayevaa tayari amemfungia mwanamke baraka zake na pia kuyateka maisha yake na kumfungia asiende mbinguni, sababu katika mwili wake yeye anakuwa ni kahaba kiroho mpaka kimwili haijalishi kimwili yeye hatendi mambo ya ukahaba, ila kutokana na hilo vazi alilolivaa basi tayari anakuwa amevaa ukahaba na mapepo huishi juu yake bila kikwazo chochote.
  Ø  Mavazi haya asili yake ni kuzimu na mengine yamebadilishwa kwa kuandikwa kinyume mfano MAX wa kuzimu ikaandikwa WAX, huyu MAX yeye ndiye aliyekuwa namba tatu katika ufalme wa shetani na unapovaa kitu kilichoandikwa kwa jina lake tayari na wewe unamsujudu mzimu wa MAX na kuporwa baraka za maisha yako. Sasa wakawapiga watu upofu wakavipa vitu majina WAX- (MAX), pia NIDA nayo asili yake ni kuzimu.
  Ø  Yapo mavazi ya mwanamke ya kuonyesha tumbo wazi.
  Ø  Nguo za kuonyesha matiti na kuonyesha mgongo.
  Ø  Chupi za bikini.
  Ø  Chupi za kike zenye zip na zenye mifuko ya kuwekea pesa.
  Ø  Chupi zilizochorwa moyo au zimeandikwa katika nguo za ndani za kike mfano; girlfriend, boyfriend, na maneno mengi tu ya ajabu, karibu, furahi, nakupenda mpenzi.
  Ø  Nguo za transparent.
  Ø  Stocking zote unapovaa unakuwa unavaa miguu ya majini.
  Ø  Vimini, katika ulimwengu wa roho wewe ni kahaba maarufu.
  Ø  Nguo zote zenye magamba au picha mfano wa nyoka, mamba, na nyingine zenye madoa doakama ya chui.
  Ø  Viatu vyote virefu- unapovivaa tayari unakuwa unaitwa twiga wa kuzimu na madhara yake maisha yako yanaibiwa ni kwa kupitia mlango huo.
  Ø  Pochi za mikononi pamoja na mabegi yote yenye scales au magamba au viatu mfano kamamagamba, ukiona tu utajua unapovitumia unakuwa umebeba nyoka na roho za shetani zinakumiliki. Inakuwa ni pamoja na mikanda yeyote yenye mfano wa picha za magamba.
  Ø  Nguo zenye mipasuko mbele, mfano katika skirt unapoivaa ina maana umewafungulia mapepo wa uzinzi waingie katika mwili wako na kwa njia hiyo ni lazima wataingia tu sababu wanao mlango.
  Ø  Eyeliner-  unapopaka katika jicho lako unakuwa unajiwekea alama na wewe ni mfuasi wa shetani, pia napenda uelewe kuwa na shetani na yeye huwa anajipaka eyeliner (wanja) katika jicho lake la kulia ila yeye hulizungushia mchoro wa duara, na unapojipaka wanja basi unakuwa wewe ni mali yake yamkini hata haujui na unampenda MUNGU.
  Ø  Kukata nyusi- unapokata hizo nywele unakuwa unayakata maisha yako na ndio sababu maisha ni magumu kwa wanawake wengi hiyo ni sababu moja wapo.
  Ø  Kuvaa shanga za kiunoni- kila unapovaa shanga katika kiuno chako unakuwa umejifungia majini, hata ukijifungia cheni ya gold au silver, uelewe tayari unayo majini katika mwili wako na madhara yake wanandoa wanakuwa wazinzi, faraka, ndoto za zinaa, mikosi na balaa, vitu hivyo havifai katika jina la YESU. Unapovivaa unakuwa unaliharibu hekalu la MUNGU kwa kufunga ndoa na mapepo katika kiuno chako, au kwa lugha nyingine hizo shanga ni pete za majini na unapovaa unajifungisha ndoa na wao katika ulimwengu wa roho.
  Ø  Nguo za kubana na kuonyesha maumbile yako yalivyo, jinsi ulivyoumbwa mfano hili siyo jambo jipya. Embu tembea katika maeneo mbali mbali utaona wanawake wamevaa suruali zinazoonyesha figure zao, sasa ujiulize wanamuonyesha nani? Jibu, wanawaletea wanaume maroho ya ushawishi ya uzinzi hivyo wanapovaa mavazi hayo tayari wao ni makahaba. Mavazi haya yameletwa ulimwenguni ili uzinzi ustawi na kuwateka wanaume katika majaribu, ili amri za MUNGU zivunjwe na kila anayevaa hivyo uelewe kwanza ni machukizo mbele za MUNGU na pia unatumikishwa katika upande wa shetani eidha kwa kujua au kutokujua. Sasa ufunguke, uyasitiri maungo yako au mwili, ili upone roho yako.
  Ø  Kuvaa mavazi ya kiume.
  Ø  Kuvaa hereni kubwa kuliko sikio- unakuwa unavaa hereni ya mama wa makahaba. Hereni salama ni ile ambayo ni ndogo ambayo inakuwa sawa na kasehemu cha kuwekea tundu la sikio, hizo kubwa kama bangili hizo ni za mama wa makahaba.
  Ø  Kila rangi unayoipaka katika kucha yako uelewe ni dhambi na unayafunika maisha yako usije ukafanikiwa, na pia yanaibiwa na yanapelekwa kuzimu unapewa wewe ya mapepo ambayo ni shida tupu, hata kupaka hyena kujichora mwili, matatoo yote ni dhambi. Unapojichora tattoo, unajiwekea alama wewe ni freemason, ni wa kuzimu siku zote.
  Ø  Kila product yenye neno ultra, iwe katika kitu chochote, kinatoka kuzimu kuja kuiba vitu vya wanadamu na kuwaharibu.
  Ø  Unapoweka rollers kichwani, unakuwa umejiwekea funza wa kuzimu katika akili zako. Na akili zako na ufahamu kuibiwa na hao funza wa kuzimu na matokeo yake mtu unakuwa haujielewi elewi na akili zinadumaa.
  Ø  Kutairiwa wanawake hiyo ni dhambi MUNGU hajamruhusu mwanamke atairiwe. Mwanamke anapotairiwa kile kiungo kilichokatwa kinapelekwa kuzimu na kumuibia mwanamke uthamani wa uke wake na uzao wake na kuharibu ndoa na kufanya mwanamke achanike wakati wa kuzaa na kijiwekea alama wewe ni wa mapepo.
  Ø  Pedicure- unaposugua miguu salooni unakuwa unayaondoa maisha yako na unamkufuru MUNGU yeye aliyekuumba na kukuwekea utayari wako katika miguu.
  B)    WANAUME
  Ø  Mavazi ya wanaume ambayo asili yake ni kutoka kuzimu katika viwanda vya kuzimu yapo mengi sana ila nitaelezea kwa kiasi fulani ili mpate picha na mpone.
  Ø  Mavazi yote yenye nembo za ajabu, mfano T-shirt inapicha ya mti wa bangi au sigara.
  Ø  Nguo yenye picha ufunguo- ina maana ule ufunguo umeivaa hiyo nguo ufunguo huo umekufungia usiende mbinguni na ufanikiwe kumkufuru mwenyezi MUNGU, na hata katika cheni, ukikuta kamaufunguo uelewe ni hatari tupu, hata cheni yenye msalaba ina maana uelewe unapovaa unakuwa wewe umelaaniwa na maisha yako yanasulubiwa katika ulimwengu wa roho. Pia uelewe hakuna msalaba mtakatifu kabisa hata ule aliouliwa nao YESU siyo msalaba mtakatifu ni msalaba wa laana na ndio sababu damu yake ilipomwagika pale msalabani ikatuondolea laana, sasa shetani akabuni njia nyingine na kuwapiga upofu watu waone msalaba ni kitu kizuri na kumbe siyo. Unajihukumu mwenyewe, hata kuzikwa na msalaba ni makosa.
  Nikuulize swali unapozikwa je unaenda kuhukumiwa na wewe? Au je msalaba ni alama ya mkristo? Jibu siyo. Watumishi wanawapotosha watu kwa kumuamini shetani na kumfanya YESU akose watu wa kwenda mbinguni. Jiulize swali kina Ibrahim, Isaka na Yakobo katika makaburi yaoipo misalaba? Jibu hakuna. Na kamasisi tu uzao wa Ibrahim, kwa nini tusiige mfano wa Baba yetu Ibrahim? Na zaidi je YESU yeye alizikwa na msalaba? Jibu hapana, je YESU si ndiye kweli na alionyesha njia ili tuifuate. Sasa swali, kama alionyesha njia, tuanze katika maisha yake je uliletwa msalaba? Jibu hapana. Sasa hii misalaba madhara yake unapokufa ukawekewa katika kaburi inakufanya wewe uliyekufa usulubishwe katika ulimwengu wa roho, na wote waliozikwa na misalaba wanateseka katika ulimwengu wa roho na shetani anamnyanyulia MUNGU  si unaona msalaba wanataka wenyewe niwasulubishe na MUNGU ni MUNGU wa haki analiangalia neno lake, kataa kuzikwa na msalaba iga YESU alivyozikwa, iga mazishi ya Ibrahim, Isaka na Yakobo, pamoja na mitume na manabii wa MUNGU wa kweli waliopita ambao kwa heshima MUNGU amewaita wazee 24. Kataa huo uchafu watu wanapotezwa, amenituma YESU niwaeleze ukweli utakaye sikia utapona, utakaye kaza shingo damu yake haitamlilia MUNGU katika mikono yake.
  Ø  Boxer- hizi ni chupi za nyani wa kuzimu unapozivaa  unaibiwa na mapepo uthamani wa nguvu zako za kiume na pia unaolewa na majini katika ulimwengu wa roho unakuwa wewe ni shoga. Na mlango ni hii boxer.
  Ø  Nguo zote zenye zipu kifuani tu, unapokuwa na nguo ya aina hiyo kila unapofungua zip unakuwa unayachana maisha yako katika moyo wako na unapofungua zipu hiyo unakuwa unayafungua usifanikiwe.
  Ø  Kila kitu chenye neno ultra kinatoka kuzimu.
  Ø  Mikanda yenye bastola au bunduki- unakuwa umevaa jini bedui katika maisha yako na makata hivyo wanayaharibu. Mikanda yote yenye sura za watu katika bacol au nembo yeyote ile uelewe umeivaa kuzimu na kuzimu inajiunganisha na wewe kupitia katika kitovu chako kwa njia ya bacol ya mkanda.
  Ø  Kusuka rasta- unakuwa umevaa pepo kichaa na mara nyingi huja kutokea katika mwili mtu anakuwa kichaa, na pia unakuwa na mambo ya freemason pasipokujua na wengine wanajua.
  Ø  Kuvaa suruali mlegezo- hiyo ni dalili wewe ni shoga katika ulimwengu wa roho na unapovaa hivyo unayaita majini yaliyokuoa katika ulimwengu wa roho yeye yazini na wewe.
  Ø  Kofia zote ambazo vijana wanasema ni za kileo zote zinatoka kuzimu na kijana anapovaa akili yake huibiwa ndoto zake zote hubakia boksi, na ndio sababu idadi kubwa ya wanaovaa hizo kofia fuatilia utakuta ni wavuta bangi, walaji wa cocaine, wahuni, wameharibika ni sababu ya hizo kofia zenye majina ya ajabu na ya wanamziki na watu ambao tayari ni wanachama wa freemason..
  Ø  Nguo za kubana kupitiliza mfano T-shirt, suruali, inakubana unayaonyesha maungo yako jinsi yalivyo.
  Ø  Kusuka nywele- unaposuka tayari uelewe wewe tayari  ni mke wa jini fulani kuzimu, na unaye mume unayemtumikia katika ulimwengu wa roho japo wanadamu hapa duniani wanakuwa ni wanaume tu ila ni boksi.
  Ø  Mashati yenye mipasuko katika sehemu za mifuko, mashati haya watu hawapendi kuyachomekea sababu yana mipasuko, sina haja ya kuelezea sana, yapokama Kaunda suti. Nguo yeyote ya mwanaume yenye mipasuko sehemu za kiunoni hizo zote ni za kuzimu, unapoivaa uchumi wako unapasuka na maisha yako yanakuwa ni ya shida shida tu.
  Ø  Nguo zenye sura ya nyoka, mamba, chui, madoa doa, viatu venye magamba au ukiviona vina sura ya magamba haijalishi ya aina gani havifai, ni viatu vya kuzimu.
  Ø  Viatu vilivyochorwa tick (Ö) au X ina maana hiyo tick unakubali jina lako liandikwe katika ufalme wa shetani na X ina maana maisha yako yanatiwa X yote.
  Ø  Kila kitu chenye jina MAX uelewe asili yake ni kuzimu na kina madhara.  
  Ø  Viatu vyenye majina ya ajabu na vingi havielezeki hata sitaweza kuviacha kuandika even kwa 30 days, omba ROHO MTAKATIFU akufunulie wakati unahitaji viatu omba atakuongoza na roho ikigoma tu wacha, hiyo ni dalili.
  Ø  Kofia zote za duara zisizo na chepeo halafu zina kamba au kinaninginia unapozivaa, unakuwa umeweka kwato ya jini katika maisha yako na nyingine ni kofia za duara ile zimetobolewa mashimo mengi zote hizo ni makwato ya majini na shetani amewaletea wanadamu ili wawe wajinga na wasimjue MUNGU wa kweli siku zote za maisha yao, sasa uamuzi unao wewe utavaa makwato ya majini au utayatupa.
  Ø  Mwanaume anapovaa bangili (ringi) hapo unakuwa umejiingiza na kufunga ndoa na shetani, ila utakapoivua tu tayari umevunja ndoa na shetani, ringi hizi watu wengi wanafungulia vinywaji au kutumia kama silaha wakati wa kupigana na zaidi mwanaume hautakiwi kuvaa bangili katika mkono kabisa, unapovaa unafunga ndoa na shetani, na pia hata wengine wanafunga nyuzi katika mikono, hapo tayari umefunga ndoa na shetani na wewe ni mtu wa shetani, sasa amua, ila wengi wanajua kabisa ni masharti waliyopewa kuzimu inawezekana ni raia, mfalme, au mtu wa karibu, utashangaa siku zote ipo katika mkono, watu wanafikiri ni urembo, hapana hilo ni agano la shetani.
  Ø  Kutoboa masikio au sikio- iwe ni mtu yeyote yule wapo hata wachungaji wanatoboa masikio na kuvaa hereni- hao wote katika ulimwengu wa roho ni mashoga wala YESU hana ushirikiano nao. YESU hana mashoga. Jiulize hawa wanatokea wapi? Ni mashoga wanaoeneza injili ya yesu wa uongo na kuwapeleka watu kuzimu.
  Ø  Shetani aliwateka wengi hata waliookoka katika maeneo mbali mbali ila YESU amenituma niwaeleze ukweli sababu anaona mnavyoteseka na hampati majibu na akaniambia Hebron haya mateso yasingewapata wanadamu ila yamewapata sababu niliowaita wamemgeukia shetani na ndio anakuwa baba yao hivyo wanafanya kazi ya baba yao ambao ni lusifa hata wanangu wanateseka na kuangamia ila nimefurahi sasa sababu upo wewe Hebron, nimekupata wewe uliyenikubali kunitumikia na kuyatenda yale ambayo mimi na BABA yangu mbinguni na ROHO MTAKATIFU ndio tunayoyataka, na pia Hebron nataka uelewe kabla ya wewe kuumbwa MUNGU alishakuandaa na akajua ikifika muda wake atakusimamisha na anajua utaifanya kazi yake sababu anajua yeye aliyokuumba hivyo usiogope lolote. MUNGU alikuficha siku zote kama vile alivofichwa Musa akatunzwa na Farao hakuuwawa, hivyo ndivyo ilivyo kwako na utaifanya kazi yangu vizuri sana na kuzimu haitakuweza milele. Sasa nimefurahi sababu kila akusikilizaye na kubadilika na kutii unayowaeleza atapona sababu ndani yako MUNGU ameweka majibu ya viumbe vyote na kila kitu. Maneno haya kila nikumbukapo nasikia machozi yananitoka kwa ajili ya watumishi walivyomsaliti YESU hata na kugeuka freemason, wachawi, waongo, wanyang’anyi ila usiogope ninajua kinachokuja na watu mtamfurahia YESU WA NAZARETI.
  Ø  Haya magauni ya harusi ya kuzimu- kila gauni la harusi lenye kuburuza mkia- ina maana ule mkia unaoburuzwa ni mkia wa lusifa. Lusifa anao mkia ila nilimkata mkia wake. Unapofunga ndoa na gauni la jinsi hiyo ndoa yako unampa lusifa. Na unapovaa gauni la harusi unaonyesha mabega na manyonyo unakuwa unavaa gauni la pepo kuzimu la kufungia harusi zao na wewe unajiunganisha hivyo hivyo na mama wa makahaba. Ukiangalia leo hii watu ndio wanasema ndio fashion. Hii siyo fashion mimi nasema yote ili nisije nikaulizwa na YESU siku ile ya mwisho sikuwaeleza ukweli ili mpone na usijisumbue hata kama jina lake YESU linatajwa haiunganishi hiyo ndoa sababu la hilo vazi mimi pia nilikuwa sijui, ila sasa uelewe ili upone. Wanawake mkatae sasa msiwekewe tena mikia ya shetani ukauburuza.
  Ø  Kujipaka rangi ya kucha. Kila rangi inayo maana yake, rangi zote ulimwengu maana za kucha asili yake ni kuzimu. Ukipaka hizo rangi unaharibu maisha yako pasipo wewe kujua na hizo rangi zimechanganywa na rangi za ngozi za watu waliokufa baada ya kuchunwa ngozi zao na mashetani wakala nyama zao. Sasa unapozipaka unakaribisha majini katika maisha yako na uthamani wa mikono unaibiwa, hata pesa hazikai wala kazi zako hazibarikiwi sababu MUNGU hana mahali pa kupitishia baraka katika mikono yako sababu shetani ameshaweka vitu vyake katika mikono yako.
  Ø  Kucha za bandia- hizo ni kucha za majini walizozikata  kuzimu kama vile na wewe unavyokataga zako, unapozivaa kucha za bandia unakuwa unawapa majini  uthamani wa kucha zako ambapo katika kucha zako zipo Baraka wanaziiba zako unabakia na zao na unakuwa tayari umeingia urafiki na majini pasipo kujua japo wengine wanajua na wanayapenda majini.
  Ø  Nguo zote ambazo za wanawake zinakuwa na mipasuko zote hizo asili yake unakuwa unajitengenezea mkia wa lusifa na lusifa kuitumia njia hiyo kukupata.
  Ø  Nguo ambazo ni short ni fupi zinazoonyesha mapaja na hupendwa sana kuvaliwa na masecretary katika ofisi mbali mbali, sasa hilo vazi kila unapolivaa ina maana unamkubali shetani kabisa ila sasa uelewe haifai.
  Ø  Kuvaa pini katika ulimi, unapotoboa ulimi tayari unampa mama wa makahaba ulimi wako na vitu vyako kisha unabakia na ulimi wake na anakamata fahamu zako na kisha kwa kutumia ulimi huo uliovalisha pini anautumia kunyonya viungo vya siri vya kiume na mwanaume atakayefanyiwa hivyo anakuwa viungo vyake vimemezwa na Yezebeli katika ulimwengu wa roho kupitia mwili wa mwanadamu. Kazi kubwa ni kumeza viungo vya kiume kwa njia ya kuvinyonya na pia hata ukinyonywa ulimi au kiungo chochote na mtu aliyetoboa ulimi, uelewe anatumika kumeza vitu vya watu na ndani yake yupo Yezebeli na ndiyo sababu ametoboa ulimi. Ilikumjua mtu mwenye Yezebeli au Yezebeli anaishi ndani yake angalia ulimi ametoboa na katika ulimwengu wa roho na yeye anakuwa ni mtoto wa Yezebeli na Yezebeli anauhalali sababu anayo alama yake katika ulimi.
  Ø  Alama nyingine ya Yezebeli ni inayokufanya kuunganika katika kitovu cha mtu na Yezebeli utaona mtu anatoboa kitovu au anatoboa pembeni ya kitovu, hii ina maana  amejiunganisha kupitia kitovu, huyo mwanadamu atakuwa anatabia za kipepo, hata kutembea uchi, mlevi, hafai kuolewa au kuwa mke bora, sababu atakuwa ni kahaba.
  Ø  Na wengine wanatoboa (wanawake) wanakitoboa KISIMI wanakivalisha pini, yaani ukiona hivyo uelewe kile kiungo cha kike alicho nacho huyo binti siyo cha bindadamu ni cha pepo, kama alivyo mama wa makahaba na yeye amejitoboa na anavaa pin kubwa ya dhahabu ambayo ina urefu wa 30 cm na unene wa 2 cm. Mmh, haya mambo yanatisha kiasi hata mimi nimeandika huku nilikataa nisione alivyo ila YESU amenitia nguvu ili niwaeleze mjiepushe msifikiri ni vizuri hayo sasa yaelewe, okoka uvitupe hivyo vitu.
  Ø  Na alama nyingine ya mtu mwenye Yezebeli anavaa pini katika macho, bangili miguuni hasa bangili moja katika mguu mmoja na kujichora katika mapaja au kuchora moyo na alama ya mshale au kuandika majina ya watu katika mapaja au tumboni, mgongoni au popote katika mwili.
  Ø  MALAPA MEKUNDU
  Malapa yote yenye rangi ya nyekundu siyo salama sababu unapoyavaa unaibiwa maisha yako na shetani. Na katika haya malapa shetani aliweka pepo kivutio na ndio sababu utaona idadi kubwa ya watu wana malapa mekundu, haya yapo hapa ulimwenguni kwa ajili ya kuharibu maisha ya mwanadamu. Unapoyavaa maisha yako yanakuwa ni magumu sababu yale yako uliyopewa na MUNGU yanaibiwa utayari wako katika miguu na kukufanya wewe kubakia na maisha hatari ndio sababu ya hiyo red.
  Ø  PIPI KIFUA, PIPI KIJITI
  Kila unapokula pipi kifua uelewe unakuwa unakula makamasi ya majini na unakula TB, unakula ukimwi na magonjwa ya kifua pamoja na pumu.
  Pipi kijiti- kila unapokula pipi kijiti ina maana ile pipi ndio dunia na kile kijiti kilichoichoma hiyo pipi ni wewe unaichoma dunia katika maisha yako usifanikiwe, na maana nyingine ni wewe unajiharibu maisha yako.
  Ø  VIFAA VYA UJENZI (Baadhi)
  Ø  Mabati- yapo mabati yanayotoka katika nchi za America na South Africa ni tofauti na mabati yaliyozoeleka miaka mingi katika nchi mbali mbali. Unapoyatumia katika nyumba yako tayari paa lako umelifunika na shetani na ni vigumu YESU hata Malaika kuja katika nyumba za watoto wa MUNGU sababu ni haya mabati, tayari kuna kitu cha shetani.
  Ø  Vipo vitasa vya milango vyenye rangi yeyote ya brown, unapotumia vile vitasa katika nyumba yako vinatumika sasa ndio mlango wa majini kuja kwako na kuingia bila tatizo na kuiba vitu vya watu kwa njia ya kipepo, na hata ukifunga na ufunguo wana kuja na kuvifungua na kuingia kimwili kabisa katika nyumba
  Ø  Rangi- zipo rangi zinaanza na herufi S na nyingine herufi C unapopaka ragi hizi katika nyumba yako unakuwa umepaka makamasi ya majini katika nyumba yako, makufuru, balaa mikosi na kukufanya Baraka za MUNGU zisije katika nyumba yako na hata Malaika kuja kwako, hii ni sababu ni uchafu na watu hawajui, asili yake ni kuzimu, hazikomboleki wala hazitakasiki. YESU anawasaidia watu wote ili wapone. Unapoipaka katika nyumba, unapaka chuma ulete na ni mlango wa majini kuja kwako sababu upo na vitu vyao
  Vipo vingi ila endelea kusoma vitabu vya Nabii Hebron na kuingia katika blog yawww.prophethebron.blogspot.comutajifunza mengi. Yote aliyowatendea wanadamu huyu mjinga shetani. YESU akanipeleka ninayajua na ninapowaeleza ukweli huu mnapona roho zenu na maisha yenu yatakuwa mazuri sawa sawa na MUNGU alivyopanga. Ila shetani alibuni viwanda ili aharibu maisha ya watu, YESU WA NAZARETI anawapenda sana mrejeeni yeye, wakati wake umefika wa kurudi, usidanganyike tena, katika makanisa mkifundishwa kinyume na biblia hao ni maajenti wa shetani ili kufaulisha kazi zake za kuua roho za wana wa MUNGU.
  NCHI 15 ZA KUZIMU.
  Nchi hizi ni tofauti na nchi zilizopo hapa ulimwenguni ila katika nchi hizi ambazo viongozi mkuu ni Rais ambaye anaitwa Kaini, huyu ndiye mtoto wa Adamu wa kwanza ambaye ndiye aliye muua Abel (Soma Kitabu cha Mwanzo 4: 6-14) baada ya kifo chake Kaini kufa kimwili, shetani alimpa cheo cha Urais katika hizi nchi 15 na katika hizi nchi 15 wapo Marais na hufanya uchaguzi kila tarehe 25.12 kila mwaka hufanya uchaguzi wa Urais na katika hawa Marais ambao wengine wapo hapa ulimwenguni ni watu maarufu na matajiri, wengine ni waimbaji wa mziki matajiri sana, kumbe ni Marais kuzimu ikiwemo pamoja na baadhi ya makochi maarufu wa timu za mpira katika vilabu maarufu huku ulimwenguni. Mnawaona ni watu wa kawaida kumbe ni Marais katika nchi za shetani huko kuzimu. Lengo za hizi nchi za kuzimu zimechukua utajiri wa nchi za huku ulimwenguni wakapeleka huko na ndio sababu utaona nchi huku ulimwenguni lazima maana na hata baraka zilizopo hazitoshi kumbe hizi nchi 15 za shetani ndizo zilizoiba Baraka za nchi hizo, na katika nchi hizi ili hawa freemason na manabii wa uongo waende kwa Joka Kuu lazima wafike katika nchi hizo, hapo ni mahali pa kupumzikia na wapewe visa ya kwenda au kibali, na pia kulikuwepo na ndege kubwa sana moja ambayo ilitumika kama ya usafiri, ndege hiyo ikaitwa AIR-UWMK- Air Umoja wa Mataifa Kuzimu. Ila sasa nimesha ilipua pamoja na nchi zote sasa hivi hamna mahali pa kwenda ni vita katika ulimwengu wa roho. Haya yote nakufunulia watu wote wa mataifa ili muelewe jinsi shetani alivyo mbaya na manabii wa uongo, muelewe kazi walizokuwa wanazifanya ili kuangamiza roho za wana wa MUNGU. Sasa mtapona, mliokata tamaa na mlio uliwa kiroho, utafufuka. Amenituma YESU niuharibu ufalme wa shetani na ndivyo ilivyo, waliokuwa wanategemea nguvu za gizahawatafanikiwa tena, kila Rais aliyepata cheo hicho kwa shetani lazima alienda katika hizo nchi za kuzimu apewe amri ya kuua watu na kutoa makafara na kupewa pesa za kampeni. Kwa sasa hizi nchi nimezilipua na Malaika Mikaeli hazipo tena.
  MTO WA MAJI YA KUZIMU?
  Nampenda YESU WA NAZARETI sana ambaye ananifunulia haya ili niwaeleze mpone na kumvua shetani mavazi yake abakie uchi kama ilivyo sasa mmemjua mambo yake na alivyowafunga na ni adui ya wanadamu ila amenituma YESU kazi yangu niuharibu kabisa ufalme wake na ufalme wa YESU WA NAZARETI usimame katika ulimwengu wote.
  Yeremia 1: 9-10.
  Nilipoenda kuzimu nikiwa na Malaika Mkuu anayeitwa Mikaeli pamoja na Malaika wengine wapiganaji na YESU akiwepo na serikali yake akinionyesha shetani jinsi alivyowaunganisha wanadamu na kuzimu na kuwaunganisha na vitu vyake pasipo kujua na akijua kuwa kwa kutumia njia hiyo YESU WA NAZARETI hata wapata hawa wanadamu tena. Sasa kama ni mtu mwenye akili ni YESU WA NAZARETI, hakuna kama yeye na yeye ndiye anipaye akili za kuupindua ufalme wa shetani na mengineyo yote.
  Nitaelezea kuhusu mto uliopo kuzimu, ni mto mkubwa sana kama vile mto mississipi uliopo Marekani. Mto huo wa kuzimu unaitwa Timberland river, nilishtuka sana kusikia jina hilo la Timberland, akanionyesha ulivyo na kazi zake. Mto huu ndio mto ambao kila mtu anayebatizwa kwa ubatizo wa maji ya kikombe, au ya kisima, au kubatizwa kwa jina la mchungaji hao watu wanakuwa katika huo mto wa shetani na YESU hawapati na katika mto huo ni mto ambao manabii wa uongo huenda kuchukua maji ya kuzimu halafu wanawaambia watu huku duniani ni maji ya baraka, kumbe ni kinyume, ni maji ya mauti na ukimwagiwa lazima uanguke chini unapoanguka chini basi unaunganishwa na kuzimu kupitia ardhi unakuwa tayari wewe ni wa shetani. Na pia kila walipokuwa wanaishiwa nguvu waliokuwa wanaenda katika huo mto wanaoga na kupata nguvu. Ila sasa nimeuharibu hakuna tena huo mto na utaona wakiaibika, wale wote waliomsaliti YESU WA NAZARETI wakamkimbilia shetani, kiburi chao tayari kimeisha. Na pia katika ulimwengu kila unapovaa kitu kimeandikwa Timberland unakuwa wewe mwanadamu tayari ni wa shetani japo wewe hauelewi kimwili, iwe ni chochote cha jina hilo, asili yake ni mto uliopo kuzimu, freemason na manabii wa uongo wanaelewa ninachokisema na wanatamani kufa sababu siri zao YESU anaziweka peupe.
  Shetani kavuliwa nguo sasa yupo uchi. Na mimi Hebron siri hizi nazitoa kamavile aniagizavyo BWANA WA MABWANA, MFALME WA WAFALME, ambaye vitu vyote ni yeye kaviumba. Usikie, uamue, upone na umrejee YESU. 98% shetani aliteka kwa njia mbali mbali, ikiwemo na mto wa kuzimu unaitwa Timberland River.
                                SILAHA 9 KUBWA ZA SHETANI.
  Majini haya yapo tisa na chakula chao yanakula chuma, haya majini yapokama roboti, kila jini ana nyota zake. Golo 1 ana nyota 10, Golo wa 2 ana nyota 8, Golo wa 3 ana nyota 6, Golo wa 4 ana nyota 4, Golo wa 5 ana nyota 2, Golo wa 6 ana nyota 1, Golo wa 7 ana nyota 50, Golo wa 8 ana nyota 40, Golo wa 9 ana nyota 100.
  Hizi ndizo silaha za mwisho za shetani anazotegemea na kwa sasa serikali ya mbinguni ipo kazini inazibomoa nikiwemo na mimi ambaye niliyetumwa kuangamiza ufalme wa shetani.
  Msaidizi wa majeshi ya kuzimu baada ya Max, kumtoa katika kazi ya Joka Kuu yeye ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi mkuu. Nilipomteka na kutolewa katika serikali ya jeshi hilo la shetani, alibakia msaidizi wake ambaye ni jini linaloitwa Samora, ila Samora lenyewe nimelifunga pingu lipo katika gereza ambalo limejengwa  na Malaika ili kuwafunga hawa mashetani na kuwatesa mpaka ile siku ya Jehanamu ifike uchomwe moto pamoja na baba yao Joka Kuu.
  NINI MAANA YA CHRISTMAS TREE?
  BWANA YESU ASIFIWE, nawasalimu watu wote wa mataifa yote kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI, ambaye kupitia yeye ndio tunapata siku ya Krismasi ambayo watu husherekea kukumbuka kuzaliwa kwake mwana huyu wa MUNGU  aliye hai na aliye maarufu kupitia manabii wote waliopita na maarufu kupita viumbe vyote na ndiye MWANA WA PEKEE wa MUNGU.
  Leo nitaelezea maana ya mti wa Krismasi, unayo maana gani na pia nitaelezea kuhusu mti unaoitwa (Christmas Tree) hauna uhusiano na siku aliyozaliwa YESU kabisa bali mti huu unao uhusiano na miungu iliyoitwa Tammuz. Kama nilivyoelezea katika makala ya Nabii Hebron uisome kuhusu Father Christmas (neno) huyo ni mzimu wa mtu aliyeitwa Santa Claus ila usome utaelewa vizuri na wewe utaachana na kuweka midoli katika siku ya Christmas, badala ya kuiita hiyo siku ni ya YESU peke yake, mbinu za shetani kuivuruga hii siku ya Christmas na kuwapiga wanadamu upofu wajijue kama wanamsherekea YESU siku hiyo. Shetani aliwateka wakristo wa enzi hizo ambao ni wana dini wakaamua katika siku hiyo maarufu ambayo ni kukumbuka kuzaliwa kwa YESU WA NAZARETI, na kumtukuza MUNGU aliye hai, shetani akawashika wanadamu fahamu zao katika siku hiyo wakaweka mti na mti ukaitwa mti wa Christmas. Na siri ya mti huu, zamani wapagani waliamini miungu wa mimea na ndio waliamini ndiye mungu wao, sasa wakamuingiza huyo mungu wao wakampamba katika tarehe hiyo ya Christmas ili kuiteka hiyo siku asiabudiwe MUNGU wa kweli na kila anayeweka mti huo wa Krismasi hadi leo ajielewe  anaupanda ufalme wa Babeli katika moyo wake na anatekwa katika ulimwengu wa roho  anakuwa anampamba mungu Tammuzi au mungu mimea pasipokujua.
  Asili ya mti uitwe jina la Christmas tree ilianza Europe, France na Germany, katika biblia hakuna neno mti wa Krismasi, na cha ajabu katika ulimwengu wote watu wanapigwa upofu waliookoka, wapagani, watu wa dini hawaijui siri hii na hata wakiijua hawasemi ukweli wazi wazi ili watu wapone roho zao. Amenituma niwaeleze ukweli peupe peupe. Anayetaka apone atapona, anayekaza shingo majibu atayapata. Huu mti unaoitwa Christmas tree nataka muelewe kwanza haina ushirikaa kabisa na siku hiyo ya kuzaliwa BWANA YESU WA NAZARETI, ila lengo la mti huo ni miungu inayoitwa Tammuz (miungu ya mimea ambayo watu waliamini ile rangi ya kijani ina nguvu katika mimea enzi hizo) hivyo pasipo kumjua MUNGU wa kweli wakaona eti aliyemzaa YESU ndie miungu ya mimea, wakati ukifikiria wewe peke yako utaona mti hauwezi kumzaa mtu, hata kumuuumba, bali mti unatawaliwa na wanadamu kama viumbe vingine. Na pia Christmas tree siyo ishara ya kuzaliwa kwa YESU bali ni ishara ya Ashera au mhimili wa miungu ya Tammuz, na shetani alitumia mbinu kubwa mpaka akauteka ulimwengu na hadi leo watu badala ya kumpokea YESU na kufurahia katika mioyo yao wanatekwa na shetani katika ulimwengu wa roho  kila aliye na huo mti iwe nyumbani, kanisani, ofisini, hotelini anakuwa amaemuabudu mungu Tammuz, na siku hiyo unakuwa umejiimarisha kwa mungu Tammuz pasipo kujua. Ila wachawi wanajua na viongozi wa freemason, wanajua na watumishi wa uongo wanajua kabisa, wanafurahia mpigwe upofu mfe roho.
  Natumaini mpaka hapo at least umepata picha kiasi Fulani ila zaidi endelea kusoma makala ya Nabii Hebron utajifunza mambo mengi sanaaliyonifundisha YESU na niwafundishe ili mpone. Madhara ya kuita mti au kitu chochote kiitwe ni Krismasi hiyo ni dhambi, na ni kumnyang’anya YESU happy birthday yake na kuipa miungukama vile huu mti badala ya kuitwa mti tu ukaongezwa Christmas hapa ni kumkufuru MUNGU. Kama ulikuwa haujui tubu, usiweke miungu tena nyumbani kwako, hata katika kanisa, na kila mahali wanapoweka mti katika kanisa panakuwa ni mahali pa miungu siku hiyo na MUNGU wa kweli hashiriki katika kambi ya miungu. Je upo tayari kuweka miungu ya Tammuz kwa kuweka mti wa Krismasi? Na kumkana MUNGU aliye BABA yake YESU WA NAZARETI? Ambaye siku yake ya kukumbuka kuzaliwa imeingiliwa na kubadilishwa jina lake pasipo watu kujua. Yeye ni mfalme asiyefananishwa na kiumbe chochote wala kwa jina lolote lile, na ndiyo maana katika ulimwengu huu hakuna mtu anayestahili kuitwa YESU. Sasa muulize swali yeye anayejiita ni YESU, je alizaliwa na Maria? Na je alikufa na kufufuka? Na je yeye ndie atakayekuja kutunyakua katika unyakuo? Na je muulize mbona upo hapa ulimwenguni haujapaaga tokea enzi hizo? Na mbona haupo na wale wanafunzi wako hapa uliwenguni, tuonyeshe Petro na wenzake 11, jibu hana. Huyo ni feki ndani yake ni miungu inayojifananisha na YESU ili awadanganye watu kuwa yeye ndie na kumbe ni uongo.
  Nataka muelewe injili ya kweli na siyo ya uongo na ukweli unachanganya, yaani nuru na giza, kitu chochote cha MUNGU halifai kufananishwa au kuitwa kwa jina lake, unapofananisha au ukaita ujue tayari umemkufuru MUNGU. Hata leo wakristo wengi wanamkufuru MUNGU pasipo kujua sababu ya mapokeo ya miungu mfano halisi ni tendo la kuweka mti wa Krismasi kanisani, nyumbani pako, wewe badala ya kumpamba YESU katika roho, sifa na kusujudu, unampamba mti halafu unaviita ndiyo siku kuu ya kuzaliwa YESU WA NAZARETI hapo umepotea kinachotokea katika ulimwengu wa roho unapandiwa roho za huo mti katika moyo wako na mambo ya miungu na ule mwisho unabakia kwenda jehanamu sababu utakuwa umevunja moja ya amri kumi, usivisujudie vitu, mheshimu MUNGU aliye muumba wako, usimfananishe na chochote kile, sasa huu mti haujafananishwa na YESU? Je haujavunja amri ya MUNGU? Tubu leo na uitupilie mbali wala usiweke kanisani wala popote kama kweli wewe hautaki kumkufuru MUNGU.
  Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote naomba unisamehe niliabudu miungu ya mimea bila kujua au kwa kujua narudi kwako MUNGU WA KWELI nisamehe nioshe kwa damu ya mwanao YESU WA NAZARETI, najitenga na miungu yote, sishiriki tena kuita mti uitwe jina lla Christmas wala kuinunua, najitenga na mapokeo ya miti hiyo na maroho yote. Nisaidie nikuabudu wewe katika roho siku ya Christmas na siku zote nikusifu wewe peke yako. Amen.
  NINI MAANA YA FATHER CHRISTMAS?
  Ndugu msomaji, napenda kuwafundisha watu wote wa ulimwengu huu kuhusu neno FATHER CHRISTMAS ni nini na chanzo chake, maana watu wengi hata mimi nyumbani kwangu wakati wa Krismasi nilinunuaga huyo mdoli anayeitwa Father Christmas pasipo kujua maana yake mpaka YESU WA NAZARETI aliponifunulia siri hii.
  Akaniambia Hebron nikuulize swali?  Nikasema ndiyo BABA, akaniuliza hivi Krismasi ni sikukuu ya nini? Nikamjibu, ni siku ya kukumbuka kuzaliwa kwako, akasema sawa kabisa. Sasa kwa nini badala ya wanadamu kumkaribisha YESU yaani mimi katika nyumba zao na makanisayao, wanampamba huyo anayeitwa Father Christmas. Nikashtuka. Akaniambia, je? Hebron, mimi ndiye huyo mdoli anayevalishwa nguo nyekundu na madevu? Nikajibu, siyo.
  Akaniambia shetani amewateka wanadamu na wanafanya wasilolijua. Huyo Father Christmas asili yake na mpaka kufikia kuitwa hivyo na wanadamu waliomuasi MUNGU aliye hai. Akaniambia, asili yake ni mzimu, tena ni mwanadamu ambaye tayari ameshakufa miaka mingi iliyopita. Naye aliitwa Nicholas, huyu ni mturiki, aliachiwa mali nyingi na wazazi wake akiwa mdogo, ila alikuwa anawasaidia watu hata kuwalipia mahari wale waliokwama na hakupenda ajulikane ila yale aliyoyafanya watu waliyasema. Na baadaye akawa askofu na alijiita Saint Nicholas. Na hata alipokufa mifupa yake ikachukuliwa kwendaItaly katika bandari Bari, na watu wanabaharia pia huiabudu hiyo mifupa yake eti bahari itapoa na yeye ndiye anayeipooza bahari itulie mwaka mzima.
  Akaniambia, wanadamu wakajipangia katika nchi za Ulaya wakamtungia jina wamuite Father Christmas. Sasa ndugu msomaji, nimeeleza kwa kifupi tu ili upate picha. Kumbe siku ya Krismasi ni siku ya BWANA YESU TU (Happy Birthday yake) sasa jiulize, kwa nini siku hiyo ambayo ni ya mfalme YESU WA NAZARETI ambaye ndiye mtoto wa MUNGU wa pekee, je? Ni halali siku hii kuiita na kumpa huyu Nicholas ndiye aitwe baba wa Krismasi? Jibu, siyo sawa. Ni dhambi na kumkufuru MUNGU aliyemuumba mtoto wake na akaifanya ni siku yake ya pekee na ndiyo maana siku ya Krismasi ni sherehe ya kukumbuka kuzaliwa kwake mkombozi wa ulimwengu huu.
  Ila shetani ameingiza mchomeko wake hapo wakampa jina Nicholas eti ndiye Father Christmas. Embu fuguka ufahamu wako, je ni sahihi siku ya YESU kuzaliwa apewe mwanadamu yeyote aliye hai au aliye kufa? Sasa basi, kila anayeweka huyu mdoli au cartoon ya Father Christmas ajue kuwa anamuadhimisha Nicholas ambaye amekufa na hajafufuka. Na kamaanaadhimishwa mtu aliyekufa inamaana hiyo ni mitambiko au ibada ya wafu. Watu wengi wameshiriki bila kujua na zaidi cha ajabu siku ya Krismasi utakuta huyo mdoli ya Father Christmas imepambwa makanisani, haifai kabisa.
  Na mfano uliotumika kumpata Father Christmas ni sawa sawa tuu na wale viongozi  maarufu waliokufa halafu baadaye wanadamu waamue kumpa jina la Father Christmas, au kina Petro, Musa, Eliya, hawa walitenda mema zaidi kuliko watumishi wote waliopita lakini bado hawakuchukua utukufu wa MUNGU wajiite Father Christmas. Na sasa ulimwengu muwe macho msije mkashangaa wanadamu wakatafuta tena mtu yeyote wamuite Father Easter, huku ni kumuasi MUNGU na mnashiriki matendo  ya shetani.
  Mpaka hapo umeelewa na kama makanisani na katika nyumba zenu mmeweka hiyo midoli ya Father Christmas, mjijue ni mzimu wa Nicholas ndio mnaouadhimisha na siyo YESU WA NAZARETI, hivyo na sikukuu hiyo imeharibika kwako na haujashiriki Krismasi safi ya YESU WA NAZARETI bali umeshiriki mzimu. Umeshajiuliza, imeandikwa katika biblia msiabudu sanamu, sasa hata kibinadamu nyie wakristo mkiangalia hauabudu sanamu? Na je dhambi haijakuotea? Fungukeni ufahamu shetani alibuni njia nyingi sana ili kuhakikisha tuu mmemkosea MUNGU aliye hai na mbakie mali yake. Na akajichomeka katika siku ya Krismasi na kuiharibu kwa kuwakamata fahamu wanadamu wamtafute mtu na wampe jina yeye ndiye Father Christmas.
  Sasa nikuulize swali, yaani hata BABA yake YESU WA NAZARETI aliyemleta hapa duniani, amenyimwa utukufu huo na badala yake ni kumpa mzimu utukufu na midoli. Wanadamu, hizi elimu za uongo muwe makini sana, mtaangamia pasipo kujua, usishiriki kabisa kuweka hiyo midoli ya Father Christmas ni kumkufuru MUNGU.
  MUNGU siyo mdoli, siyo sanamu, wala YESU siyo sanamu. Sanamu haina uhai, haiongei, haina akili. Sasa watu wametekwa na kuabudu sanamu ya Nicholas ambaye huyu ni mwanadamukama wewe tuu, wala haikupaswa aitwe yeye ndiye BABA WA KRISMASI. Na kama siyo sahihi elewa umetenda dhambi umeabudu sanamu. Tazama sasa katika siku hiyo ya Krismasi kila mahali utaona midoli ya Father Christmas, mahotelini, makanisani baadhi na hata  kwenye nyumba za watu wanazoishi.
  NOTE:
  Ukimweka ndani huyo mdoli ujue umeweka sanamu ya Saint Nicholas na yeye siyo YESU. Na ni machukizo matupu mbele za MUNGU, msifanye hivyo. Ukisoma mueleze na mwenzako ili Krismasi yako isiwe na laana, ukawa umemwadhimisha mzimu.Kama ilivyo miaka yote watu hawajui na wanamuabudu sanamu siku hiyo na kuiweka itawale katika nyumba zenu.
  Sasa umeujua ukweli na upone. Ili YESU WA NAZARETI peke yake na MUNGU aliyemleta aje hapa ulimwenguni ndiyo wainuliwe tuu na utukufu wa siku hiyo arudishiwe yeye peke yake maana ndiye anayestahili na siyo kumpa mwanadamu. Jina la Father Christmas life kabisa katika ulimwengu wote na hiyo roho iangamie kwa damu ya YESU WA NAZARETI na malaika wa mbinguni waiteketeze kabisa, abaki MUNGU wetu tuu arudishiwe utukufu katika kiti chake cha enzi.
  SIRI ZA KUZIMU
  BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE, YESU ambaye aliyenichagua na kunituma kwenu nyie mataifa yote ambao mnategemea kwenda mbinguni siku moja ila kati yenu mlio idadi kubwa mmefungwa msiende mbinguni kwa sababu mbali mbali, ila amenituma, atakayesikia atapona, atakaye kaza shingo yake atayapata majibu kwenda kwa farao. Wiki mbili zilizopita nilikuwa naongea na MUNGU ambaye vitu vyote hivi ni yeye kaviumba, akaniambia Hebron mimi ndiye nilikuandaa kwa kazi yangu na nilijua ukifika wakati wake utaifanya na nitakutuma kwa mataifa yote ili kupitia wewe watu wanijue mimi MUNGU wa kweli sababu niliwatuma 98% wanafanya kazi ya shetani na kuwatesa wanadamu ambao wananipenda ila wao wananwapeleka katika njia ya jehanamu. Akaniambia mengi ila machache nitayasema, haya mengine ni yangu.
  Kazi hii unayoifanya ni mimi MUNGU ndiye ninayoifanya peke yangu kupitia mwili wako sababu wewe ni mwanangu mpendwa wangu, na rafiki yangu kama ilivyokuwa kwa Musa, Eliya, Ibrahim na mwanangu wa pekee na wengine waliopita ndivyo na kwako ilivyo. Ghafla akaniambia hivi Hebronunajua ni lini mwanangu atakuja kulinyakua kanisa? Nikashtuka, akaniambia andaa kanisa muda wa mwanangu kurejea umefika ila ni siri yangu mimi MUNGU ndiye ninayeijua siku hiyo, akaondoka, kurudi katika kiti chake cha enzi. Nawasihii mrejeeni YESU muokoke na kubatizwa ubatizo wa maji mengi na kuishi maisha matakatifu ili katika unyakuo unyakuliwe na wewe.
  Hapa sasa ninaelezea baadhi ya siri za shetani zilizopo kuzimu ambazo amezibuni ili kuhakikisha amekupa wewe na haya yote nilikwenda kuzimu nilikuwa na Mikaeli malaika mkuu na kuvunja viwanda vya shetani vya nguo vilivyopo kuzimu ambavyo wanatengeneza nguo zao na kuzileta ulimwenguni ili unapozivaa unakuwa umetekwa na unamtukuza shetani, joka kuu na mama wa makahaba (Yezebeli) na jini Abubakar . nitaelezea katika mambo mawili:-
  a.       Mavazi ya Kuzimu.
  b.      Magari ya kuzimu na mengineyo kidogo, yapo mengi sana.
  A.    MAVAZI YA KUZIMU (YAJUE)
  Mavazi haya yamebuniwa kwa jinsia mbili; moja ya wanawake na ya pili ni ya wanaume. Mavazi haya yapo kwa lengo maalum ili kumwangamiza mwanadamu. Nitaelezea vazi linaloitwa BIKINI (nguo za ndani za kike). Nguo hii unapoivaa hapa ulimwenguni unakuwa umeolewa na majini katika ulimwengu wa roho, unakuwa unamtukuza mama wa makahaba, majini mahaba yanakuwa ni rafiki yako, unakuwa ni shoga katika ulimwengu wa roho. Unakuwa unaoana na jini la kike japo ni mwanadamu, unapoivaa hiyo BIKINImapepo yanatumia ndio mlango wa kukuibia Baraka zako ulizoumbwa nazo na MUNGU, wanaiba uthamani wa ndoa na kukufunga binti usiolewe au kukufunga hata kizazi, kukufarakanisha usimpende YESU WA NAZARETI na usidumu katika wokovu wa kweli. Na pia nguo hii ndiyo chupi ya mama wa makahaba anayoivaaga. Amelibuni yeye na unapovaa ujielewe umemvaa mama wa makahaba, funguka usivae tena, choma kwa usalama wako ili uwe upande wa MUNGU. Nguo hii wanawake wengi zaidi wanazivaa lakini hawajui wengi wao, ila wale washirikina au freemason wanajua, ni lazima avae ili kumtukuza mama wa makahaba. Zaidi okoka na uendelee kufuatilia makala ya Nabii Hebron pamoja na YouTube na katika vitabu nilivyoandika.
  Viatu vyote vyenye sura kama magamba ya nyoka au scales za mamba, kitu chochote chenye scales, iwe ni pochi, mikanda, hata saa, kanga, gauni au nguo ina magamba ya chatu kwa sura, mtu akivaa utaona ni nguo ila kavaa chatu, na perfume zenye sura yeyote unayoona inatisha au macho unayaona hilo silo jicho la kawaida ni jicho la mama wa makahaba, na matokeo unakuwa mzinzi na hauachi uzinzi sababu hiyo, bikini ina maroho ya mama wa makahaba, na unayeivaa katika ulimwengu wa roho unakuwa ni makahaba.
  Na upande wa mwanaume amebuni nguo za ndani (chupi) ambazo ni tofauti na chupi, yupo jini anayeitwa Abubakar, huyu ndiye anayebuni mtindo ya sharobaro ili aweze kuwateka wanaume na yeye akabuni vazi la mnyama ambaye yupo kuzimu, mnyama huyu ni nyani. Kuzimu wapo wanyama ambao wanabuniwa na joka kuu, nitaelezea kwa upande wa nyani. Nyani wa kuzimu anaitwa BOXER, huku ulimwenguni nyani (baboon). Sasa nyani wa kuzimu huwa anavaa maroho ya uzinzi, uhuni, ukorofi, ukatili, ushoga, tabia chafu chafu. Katika kiwanda cha kuzimu wakatengeneza nguo za ndani tofauti na chupi (za kawaida), nguo hizo hapa ulimwenguni zinaitwa Boxer wanaume wanazivaa sana, inawezekana pia labda umeivaa muda au unazo nyingi. Sasa nguo hizo siyo salama, unapoivaa unakuwa umevaa nyani wa kuzimu anayeitwa Boxer na ndio sababu hata hapa ulimwenguni inaitwa Boxer, sasa uelewe asili ya boxer ni chupi (nguo ya ndani ya nyani wa kuzimu) na unapoivaa unakuwa umemtukuza jini Abubakar, na yule nyama maroho yake yanakufuata huku ulimwenguni. Madhara yake unapoivaa tu katika ulimwengu wa roho unaolewa na majini, unaitwa shoga, hapa ulimwenguni unakuwa mzinzi wa kupindukia kama alivyo nyani, ukimuona katika mbuga za wanyama pozi anafanya uzinzi na ushoga hasa akiona watu wanamuangalia, kwa wanaowajua nyani fananisha tabia zake na mtu anayevaa boxer. Hupenda wanawake wanayovaa hizo BIKINI na mengineyo, ulevi, bangi, madawa ya kulevya, na miziki ya kidunia. Na anayevaa siku zote roho mchafu lazima aishi ndani yake.
  Vazi hili huwafanya vijana wanapotembea suruali huvalia kwenye mapaja na nguo za ndani kuonekana na watu, hii ina maana anajionyesha sasa yeye ni shoga katika ulimwengu wa roho na kimwili baada ya muda itatimia anakuwa shoga kabisa, ushoga ni maroho ya zinaa ya shetani ili akupate wewe. Zinaleta faraka katika ndoa, kuua nguvu za kiume ili usikutane na mwanadamu kimwili wabakie mapepo waliokuoa wewe. Ili upone na uende mbinguni okoka, usivae mavazi haya kamaunataka kwenda mbinguni na mapepo yakukome na uweze kukaa na YESU vizuri. Hizi ni siri ambazo watu hawajui, wanampenda YESU lakini utashangaa unaanguka katika dhambi, ni sababu unavaa vazi la kuzimu ambalo ni chupi ya nyani wa kuzimu anayeitwa BOXER, jitenge naye, fanya maamuzi.
  Nyingine ni nguo za harusi za kuonyesha mabega wazi, mgongo, unapovaa vazi hilo katika ndoa yako uelewe ndoa yako umempa mama wa makahaba, hivyo mtavuna ukahaba siku zote. Utafunguliwa na utapona roho yako, sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozitenda najivua mavazi yote ya mama wa makahaba kiroho na kimwili, najivua mavazi ya nyani wa kuzimu (Boxer) na sivai tena, nazichoma kwa jina la YESU WA NAZARETI. BWANA YESU uniandike katika kitabu chako cha uzima wa milele, uniokoe, uniongoze siku zote nisitekwe na shetani na mavazi yake na chochote. Amen.
  MAWIGI (WEAVE) NI NYWELE ZA SIRI ZA MAJINI!
  BWANA YESU ASIFIWE watu wote wa mataifa yote na ambao mmeumbwa kwa mapenzi ya MUNGU na siyo shetani ila shetani hawapendi wanadamu kabisa na anataka waangamie na kuja kuchomwa nae mto kwa kumfanya mwanadamu amkosee MUNGU eidha kwa kujua mwanadamu mwenyewe au mwanadamu asijijue kuwa amemkosea MUNGU. Katika makala hii nitaelezea machache ya yale ambay niliyaona kuzimu kwa macho yangu bila kuhadithiwa na mtu yeyote na zaidi ilikuwa ni mpango wa MUNGU mimi Hebron niende nikaone kila kitu ambacho shetani na serikali yake wanachokifanya na kwa ajili ya kuwateka wanadamu wamkosee MUNGU na wasifanikiwe sawa sawa na mpango wa MUNGU, na pia sikuonyeshwa haya nije nikae kimya nilionyeshwa ili niwaeleze watu ili wapone na atakaye kaza shingo asije akamlaumu MUNGU Ufunuo Wa Yohana 3:6 (yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo ayaambia makanisa, kanisa ni wewe mtu ambaye siku ya unyakuo YESU atakunyakuwa kama ukiwa umeokoka, batizwa ubatizo wa maji mengi na kuishi maisha matakatifu, ikiwa kinyume hautanyakuliwa.
  Nilipofika kuzimu nilipelekwa sehemu za viwanda na viwanda vingi ambayo nilikuta kuzimu huku duniani vipo na viwanda hivyo vimeletwa ulimwenguni ili kuwadhoofisha wanadamu na kuwaharibu maisha yao, japo sasa nitaelezea kuhusu mawigi (weave) asili ya hizi nywele ya wigi, hizi nywele zinatoka kuzimu, kuna majini ambayo ni makubwa kuliko majini yote yanaitwa (GOLO) na yana manywele mengi sana, upana au unene wake ni kama mita nne kwa unene. Haya majini ndiyo yakisha nyolewa hizo nywele zao za siri ndizo zinazoletwa huku duniani kisha watu wanazivaa kichwani. Niliogopa sanana kushikwa na mshtuko na kuna salooni maarufu kuzimu ya kuwanyolea nywele za siri hawa majini hiyo salooni inaitwa YML saloon kirefu chake ni Yezebel, Makata, Lusifa. Katika hii salooni ndipo hawa majini wanaendaga kunyoa nywele zao kama vile hapa ulimwenguni watu wanapoenda salooni kunyoa nywele zao, ila tofauti hawatumii mashine ya kunyolea kama hizi ambazo watu hunyolea huku duniani wa hutumia mapanga makali sana na shoka kali kunyolea nywele zao za siri sababu ni nyingi kama kakichaka, na wakishazinyoa hizo nywele hukusanywa na hiyo salooni ya (YML) kisha zinaletwa huku duniani zinauziwa watu na wanazivaa katika vichwa, nilizidi kushtuka ila MUNGU akanitia nguvu sababu ni jambo la kutisha niliporudisha picha duniani, mamilioni ya watu wanavaa kitu wasichokijua asili yake ni nini? Na lango lake ni nini? Ndugu wasomaji ingekuwa labda ni wewe sijui ungejisikiaje japo nitaeleza kwa ufupi. Sasa unapoona haya mawigi (weave) kwanza uelewe siyo salama kwa mwanadamu, pili hizo ni nywele zilizotokea katika viungo vya siri vya majini ya kike na kiume, hivyo unapovaa ujue katika kichwa chako umevaa nywele za sehemu za siri za majini katika kichwa chako, na hata kama unafanya biashara ya kuvaa mawigi uelewe unafanya biashara ya kuuza nywele za siri za majini na hata kama unazo uelewe unazo nywele za majini katika miji yako.
  MADAHARA YA KUVAA WIGI (WEAVE).
  1.      Kwanza kabisa uelewe katika kichwa chako unakuwa umevaa nywele za siri za majini na pia umevaa pepo.
  2.      Madhara yake unakuwa umeuzuia utukufu wa MUNGU ushuke katika kichwa chako sababu tayari upo utukufu wa shetani katika kichwa chako yamkini unavaa pasipo kujua au kwa kujua.
  3.      Akili yako na maono yako yanaibiwa na shetani na kisha shetani anakuwekea ya kwake pasipo wewe kujua.
  4.      Mawigi yanakufanya usiweze kusimama katika wokovu.
  5.      Mawigi haya yanaletwa ulimwenguni ili kuwazuia wanawake wasiende mbinguni sababu shetani anajua kabisa katika mioyo ya wanawake wengi wanampenda YESUkama vile kipindi ambacho YESU alikuwepo ilionekana wanawake ndio waliokuwa wengi na hata sasa ukiangalia idadi kubwa ya wanawake ndio wengi waliookoka kuliko wanaume. Sasa alichokifanya shetani akabuni njia hii wanadamu wavae nywele za siri za majini kwa kuwapiga upofu wasielewe (huku ndiko kutekwa na shetani). Ila YESU atakaporudi kulinyakua kanisa wale waliookoka wakiwa wamevaa mawigi, wasiweze kunyakuliwa sababu katika vichwa vyao vitakuwa vimefunikwa na nguvu za giza ambazo ndizo nywele za majini yanayoitwa (GOLO). Ashukuriwe YESU aliyenipeleka na kunionyesha haya ili niwaeleze watu mpate kupona na niliporudi katika mwili akasema na mimi Hebron nimekufunulia haya uyaone na uyajue ili  uniandalie kanisa ambalo nitalinyakua katika unyakuo wangu, tazama wanadamu wananipenda ila mwovu amewatengenezea njia ili wasifike mbinguni, uwafundishe, uwaeleze ili wapone, na hata katika unyakuo niweze kuwanyakua.
  6.      Ndani yako mizimu inaishi.
  7.      Mapepo yanakuwa na uhalali wa kuishi ndani yako na wachawi hukuloga kwa urahisi na kukuibia vitu vyako.
  8.      Unakuwa unayo alama ya mama wa makahaba (Yezebel) sababu unavaa vitu vyake.
  NOTE: vitu vyote venye asili ya kuzimu ni vitu vya shetani hivyo havikomboleki wala havitakasiki, wala havibarikiki kwa jina la YESU WA NAZARETI sababu hauwezi ukazibariki kazi za shetani kwa jina la YESU, bali kazi za shetani huharibiwa kwa jina la YESU WA NAZARETI.
  9.      Humfanya mwanamke kuwa na tabia za uzinzi, asiweze kutulia katika ndoa na huwaletea ndoto za uzinzi, na kuwaibia wanawake baraka zao walizoumbwa nazo na mwenyezi MUNGU.
  10.  Kila anayevaa nywele hizi katika ulimwengu wa roho yeye ni mke wa jini pasipo kujijua na wengine hujijua, haijalishi umeokoka au haujaokoka, ukweli ndio huo.
  11.  Katika ulimwengu wa roho jina lako unaitwa kahaba, na mfano rahisi tu angalia watu wenye tabia za ukahaba katika ulimwengu wote leo hii kwa upande wa watu weusi. Hata katika street wale wanaofanya uzinzi kujiuza mwili tazama katika kichwa utaona mawigi.
  12.  Mwanawake anapokufa akazikwa na wigi tayari anajifungia asinyakuliwe katika unyakuo sababu anacho cha kuzimu na MUNGU anaangalia haki amenituma niseme ukweli ili watu wapone, sababu shetani alishaona kuwa watu waliookoka hatawapata sasa akabuni njia hii ya mawigi, nikuulize swali labda umeokoka unampenda YESU na unaishi maisha matakatifu lakini katika kichwa chako umevaa mapepo je utukufu wa MUNGU utashuka katika maisha yako? Jibu hakuna na je MUNGU atakubarikije wakati unavaa kofia ya shetani?
  13.  Na majini haya ambayo yanayotoa nywele za siri ambazo ndizo wigi, majini haya nguo za ndani wale wa kiume wanavaa boxer na majini ya kike yanavaa BIKINI. Ukubwa wa size ya kiuno ni kama mita 4 kiuno.
  14.  Ufahamu unashikiliwa na shetani na anayeongoza maisha yako na hapo ndipo unapotea na kuacha njia za MUNGU pasipo kupenda hii ni sababu moja wapo ni hizi zinazovaliwa zinatoka katika viungo vya siri ya majini.
  NOTE:
  Yapo madhara mengi ila zaidi pata dvd na cd kutoka kwa kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE na usome makala ya Nabii Hebron Kisamo na katika YouTube sikiliza utayapata maelekezo zaidi na utapona roho yako ukiamua na kwa njia hii shetani anaitumia kuliteka kanisa 98%. Rudisha picha angalia makanisa utaona ni mawigi yamejaa, na watu wakifikiri ndio kujiremba kumbe ni kujipa cheo cha mama wa makahaba pasipokujua au kupenda. Nimewajulisha na mataifa yote sababu YESU aliyenituma ni wa mataifa yote na siyo nchi moja au kabila moja leo amenituma nikuletee habari hii na yeye anakuangalia wewe unayeupata ujumbe huu anasema na wewe. Amua na uchukie kabisa na uzivue katika kichwa chako ili akurejeshee akili zako na afunge milango ya kuzimu katika kichwa chako, na uokoke, sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, nimeamua kutovaa tena nywele za majini, nazitoa na nitazichoma, unikomboe YESU, unifunike sasa kwa uweza wako. Nilikuzuia muda mrefu, ila karibu ndani yangu uniandike na katika kitabu chako cha uzima wa milele, uniongozee wewe nisipotee tena kuvaa vitu vya kuzimu. Amen.
  NGUO ZOTE ZA MITUMBA ZINA MIZIMU!
  BWANA YESU ASIFIWE, YESU WA NAZARETI, ambaye ndiye mtoto wa pekee wa MUNGU na ndiye ambaye kupitia jina lake tunapona na unampiga shetani. Nawaelezea kuhusu nguo za mitumba au mavazi ya mitumba, hasara zake, sababu hata mimi sikuelewa hayo ni mpaka pale YESU aliponifundisha mwenyewe sababu hata mimi Hebron nilikuwa nazo nyingi sana ila aliponijulisha mara moja nilizichoma siku bakiza hata moja. YESU akanieleza Hebronningemtuma nani? Sasa uyajue haya na watu wapone, ila nimekujulisha wewe uliyenikubali ili niuokoe ulimwengu kupitia mwili wako, akaniambia Hebron nilikueleza nitautumia mwili wako kuukomboa ulimwengu huu lakini huu mwili wako ni mtakatifu sababu mimi ninaishi ndani yako ila usiogope sababu ya haya ninayokueleza. Hizi nguo za mtumba unapozivaa huwa unanajisika ndani yako, niliogopa sana, ni sababu ya nguo hizo, zina mizimu na mapepo na ni mali zao.
   MTUMBA NI NINI?
  Mtumba ni kitu chochote ambacho kimeshamilikiwa na mtu wa kwanza kikiwa kipya na yeye, na linapotumika na mtu mwingine yeye anakuwa anatumia mabaki ya mtu mwingine.
  MADHARA YA KUVAA MITUMBA.
  Unapokuwa unavaa nguo ya mtumba au viatu au mkanda au nguo yeyote ile, ile nguo inakuwa inayo mizimu ya hao watu ambao ndio waliokuwa wamezivaa kwanza. Na unapovaa mtumba uelewe kuwa kama yule mwenye nguo alikuwa na mikosi na wewe utaipata tu sababu umeivaa nguo yake ndio sababu inaitwa mtumba, kama alikuwa anayo madhaifu ya aina yeyote ile na wewe utayarithi, iwe ni magonjwa, tabia za ajabu, uzinzi, ulevi, hasira, uwizi, uongo, ni mchawi, ni freemason, unapovaa na wewe hiyo mizimu inakufuata ulipo sababu ya hiyo nguo yao ambayo wewe umeivaa.
  Najua mitumba imetoka katika mataifa mbali mbali na nchi nyingi raia wake wanavaa nguo za mitumba, ila hawaelewi madhara yake ni nini kiroho. Mimi aniponifunulia haya YESU WA NAZARETI ni sababu ananipenda, na mimi nawafunulia ulimwengu wote ni sababu YESU wa mataifa yote anawapenda na anataka mpone ili awabariki na awaokoe na shetani asipate kitu cha kukushtaki na shetani asipate chochote cha kukuibia.
  Nataka uelewe jambo hili, je utakuwa unajua nguo za mitumba unazovaa ni za mtu aliyekufaga au yupo hai? Jibu haujui. Na je unajua kuwa katika kila nguo ya mtu kuna vitu vyake vinakaa hapo? Tazama vazi la Eliya lilikuwa lina vitu vya Eliya na alivyolipokea Elisha nay eye akavipokea, hivi ndivyo ilivyo nguo zote za mitumba inavyo vitu vya watu na unapovaa ile mizimu ya kwao inakufuata na kuharibu maisha yako katika roho na kumfanya mtu kuwa na tabia za ajabu ajabu ni sababu ya nguo za mtumba, na cha ajabu hata kanisa linapigwa upofu halikuelewa madhara ya mitumba na kulifanya kanisa ndio msambazaji maarufu wa mitumba ili kuwaletea watu maangamizi.
  Ile mizimu ya yule ambaye umevaa nguo yake inakuwa inakuja kukumiliki wewe katika maisha yako kiroho na kimwili na ndio sababu utakuta watu wanampenda MUNGU lakini hawaokoki hii ni sababu mizimu wa mtumba unakushikilia na kukutumikisha pasipo wewe kujua. Nguo hizi hazikomboleki.
  Kama mwenye nguo hiyo amekufa na yupo kuzimu na wewe unayavaa mtumba  huo utavutwa kuzimu usiende mbinguni, hii ni sababu unalo vazi lake yeye aliyekuwa mmiliki wa vazi la kwanza.
  Kama mwenye nguo wa kwanza yeye ni freemason na wewe unayo vazi lake, kule kuzimu mizimu inakuona wewe ni mtu wao na itakufuatilia inahakikisha tu na wewe unamfuata mwenye nguo hiyo.
  Unapovaa mtumba uelewe mlango wa shetani kukupata upo wazi kabisa na mapepo kukuvamia, hata kama unalalia mashuka, blanketi za mitumba kila unapolala na wewe unachukuliwa nafsi yako unapelekwa kutumikishwa kama msukule na siku zote maisha yako ni shida na mahangaiko tu.
  Kila ukivaa mtumba uelewe umevaa mizimu, sasa watu wengi hawapendi mizimu wanaipiga ila wameivaa, hapo umejisumbua, jibu ni kuacha kuvaa mitumba upone, ili Baraka zako zikae katika hekalu la MUNGU ambalo ndio mwili.
  Nguo za kurithishwa za watu waliokufa hizo pia ni mtumba, zinazo madahara makubwa sana. Unayavaa madhaifu ya aliyokufa na hata kujiunganisha na kifo alichokufa, kama amekufa cha HIV na wewe itakufuata au ajali au ugonjwa fulani na wewe linakufuata, au kama marehemu alikuwa na matatizo na wewe unayarithi. Jambo hili ni hatari kweli. Je ni salama kwa picha hii uliyoipata? Mimi Nabii Hebron ninajua shetani hanipendi kabisa na ukweli hata mimi simpendi. Zaidi ya 100% na kupitia blog hii na mafunuo ninayowaeleza watu wote wa mataifa yote, sasa hivi shetani anatoa machozi hapa ninapoandika ujumbe huu ninamuona analia machozi ila sina huruma kwa shetani, analia anasema Hebron usitume somo hilo sababu sitawapata watu niwachezee maisha yao na kuishi katika miili yao.
  Nitaelezea kuhusu nguo za ndani za mtumba. Kila unapovaa nguo ya mtumba ya ndani, kile kiungo chako cha siri linakuwa ni cha mizimu na mizimu wanakuoa au kukufanya mume wao na kukuwekea tabia za uzinzi, utajitahidi uache lakini unashindwa ni sababu ya hiyo nguo ya ndani ya mtumba, na ndoa zinaharibikia, na pia mapepo hupitia katika njia hiyo kuharibu uzazi, au kumfanya mwanamke atoke damu kupitiliza siku. Mizimu ndio inayofanya hayo, inakunywa damu yako ni chakula chao ila wewe binadamu haujui.
  NOTE:
  Kuvaliana nguo pia ni hatari kiafya na kiroho. Kiafya kama mtu anayomagonjwa ya mwili na wewe utayapata na kiroho mtu anapovaa nguo yako anavaa na matatizo yako, balaa, mikosi, magonjwa ya kurithi, kama ni masikini na wewe unauvaa, mlevi na wewe unauvaa, muongo na wewe unauvaa uongo. Kwa njia hii wengi zaidi shetani amewateka, ashukuriwe YESU pamoja na serikali yake ya mbinguni akiwamo Eliya, Musa, Ibrahim wa mbinguni wanaonifundisha na wote 24, MUNGU awabariki sana.
  Unapovaa mtumba kama aliyevaa mara ya kwanza katika ukoo wao hawafanikiwi na wewe inakufuata hivyo hivyo.
  Unapovaa mtumba ROHO MTAKATIFU haishi ndani yako sababu unakuwa umelifunika hekalu lako.
  Unapovaa mtumba ile mizimu inakuja kukuibia vitu vyako mfano Baraka zako ulizokuwaga nazo umepewa na MUNGU, na kukutesa.
  Na unakuwa hata kama umeokooka shetani alikukosa au amekutafuta katika ulimwengu wa roho hakuoni. Ila endapo ukiwa umevaa mtumba tu tayari anakuona ulipo sababu ile nguo uliyovaa inakuwa na mizimu, na mizimu inayo uhusiano mkubwa na shetani.
  Viatu vya mtumba, viatu hivi unapoivaa kama nilivyoelezea kuwa siku zote katika kitu cha kuvaliwa na mtu wa kwanza ni chake tu, hivyo hivyo mizimu inabakia katika viatu hivyo unavyovivaa tu, hivyo mizimu inaiba utayari wa maisha yako, utayari wa kuokoka, kwenda mbinguni, utayari wa mafanikio yako katika maisha yako na ndio sababu hata kimwili fuatilia utaona watu wengi sana wanaovaa mitumba wachunguze au kama ni wewe jichunguze. Matatizo hayaishi na unafanikiwa kwa shida au hata haufanikiwi, hii ni sababu siku zote aliyekufa ambaye ndiye mzimu hupendi ufanikiwe huku ulimwenguni ni hivyo atahakikisha tu na wewe usifanikiwe. Inawezekana aliyekufa yeye hajaolewa au hakuoa na yeye atahakikisha na wewe hufanikiwi katika eneo hilo au yeye hajasoma na wewe hautasoma, au yeye hakuwa tajiri atahakikisha na wewe unakuwa maskini tum au yeye alikuwa ni mchawi, freemason, tapeli atahakikisha na wewe yanatokea kwako.
  Jambo lingine mitumba kamanilivyoelezea madhara yake kiroho katika mitumba ni mkusanyiko wa nguo za watu wengi idadi hakuna ajuaye. Sasa inamaana pia inakuja na maroho ya mizimu ya mataifa mbali mbali na madhaifu mbali mbali na unapoivaa na wewe unakuwa unayakaribisha katika mwili wako.
  Unakuwa kama mtu asiye na msimamo kiroho na kimwili na hatima yako labda neema ya MUNGU ikushukie vinginevyo siku unakata roho wanakuchukua wanakupeleka kuzimu sababu wanao uhalali na wewe.
  NOTE:
  Ili maisha yako yasiwe na balaa epuka mitumba, na usivae hata kurithishwa nguo za watu waliokufa tayari hiyo inakuwa ni mtumba. Watu wengine wanasema itakuwaje nitavaa nini. Yakupasa kumshukuru YESU ambaye amenifunulia mimi Nabii Hebron wa kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, ili ugonjwa huu sugu uliyofichika sasa unafichuliwa ili watu wapone roho zenu.
  Roho za mfilisi zimeambatana na biashara ya mtumba, omba MUNGU akupe biashara ya nguo mpya. Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote. Uniokoe, uniandike katika kitabu chako cha uzima wa milele.  Na univue mavazi ya mitumba na mizimu iachie maisha yangu ili unimiliki wewe. Nifungulie milango ya nguo mpya na mimi nivae mpya. Amen.
  ADAMU WA PILI NI NANI?
  BWANA YESU ASIFIWE watu wote wa mataifa yote, wakristo, wapagani na wengineo wote mlioumbwa kamawanadamu, nawasalimu kwa jina la mwana wa MUNGU wa pekee ambaye ndiye YESU WA NAZARETI aliyekuja mbinguni akafanyika kuwa yeye ndiye Adamu wa pili. Nitaelezea kwanza kwa nini yesu anaitwa ndiye Adamu wa pili? Hii ni sanamu MUNGU alikwisha muumba mwanadamu wa kwanza na akampa jina Adamu huyu ndiye Adamu wa kwanza na ambaye kupitia yeye tunaitwa wanadamu kwa heshima ya jina lake na kama ndiye mtu wa kwanza kuumbwa na mwenyezi MUNGU, baada ya Adamu wa kwanza kuanguka katika bustani ya Edeni akiwamo na bustani ya Edeni akiwemo na mke wake Eva soma katika kitabu cha Mwanzo 3 yote. Hivyo basi haikuwezekana tena binadamu ajikomboe tena kutoka katika mikono ya shetani. Ikabidi sasa MUNGU amlete mtu wa mbinguni mwenye nafsi yake akiwa na sura ya mbinguni ili aje aukomboe ulimwengu akazaliwa kwa kupitia Mama Maria ndiye aliyeibeba hii mimba kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU bila ya kubeba uja uzito wa mwanadamu, ndiyo sababu YESU anaitwa Adamu wa pili sababu yeye alitoka mbinguni na ndio sababu Mama Maria hata ukisoma biblia utaona mchumba wake Yusuph akimkuta tayari ana mimba japo ni bikira ila akaeleweshwa na MUNGU kupitia ndoto akaelewa.
  YAFUATAYO NI MANENO KUTOKA KATIKA BIBLIA YANAYOHAKIKISHA YESU NDIYE ADAMU WA PILI NA SIYO BINADAMU MWINGINE.
  a)      Daniel 7: 13-14: nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa usiku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo haitapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
  Sasa hapa unaona unabii ambao ulioandikwa kuhusu mwanadamu atokaye mbinguni na akaja ambaye yeye ndiye aliyepewa mamlaka yote ya kutawala mataifa yote ni kwa lugha zote na mamlaka yake ni ya milele. Sasa huyu ndiye Adamu wa pili, sasa cha ajabu wametokea waongo wanaomkufuru MUNGU kwa kuchukua utukufu wa YESU na kujiita Adamu wa pili, sasa jamani hauoni huu ni ushetani wa kumchokoza YESU wa kulipindua neno lake? Je anayejiita Adamu wa pili yeye ndiye anayetawala mataifa yote zaidi kushinda YESU? Jibu, siyo. Swali lingine je biblia imetuagiza tutumie jina lipi? Jibu ni YESU WA NAZARETI. Sasa mpaka hapo uelewe ni dhambi na ni ushetani kuingilia cheo cha YESU au kujiita wewe ni YESU.
  b)      1 Wakorintho 15: 45- 49- ndivyo ilivyoandikwa, mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyohai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho. Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili hutoka mbinguni. Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa binguni. Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.
  Hapa ni mistari ambayo inakuhakikishia kuwa YESU ndiye Adamu wa pili. Adamu wa pili ametoka mbinguni ambaye ndiye YESU alitoka mbinguni akazaliwa kwa sura ya mwana wa Adamu, ndiye sababu anaitwa Adamu wa pili na ilitabiriwa akatokea na akaja hapa ulimwenguni akaifanya kazi yake akaimaliza akarudi mbinguni. Sasa hivi tunasubiri aje katika unyakuo kulinyakua kanisa.
  Mpaka hapa umeshapata picha ya ukweli kuwa YESU ndiye Adamu wa pili sababu nimekula sifa za kweli za Adamu wa kweli ambaye ndiye YESU WA NAZARETI na hata katika ulimwengu wote hakuna jina lenye nguvu na mamlaka kama la YESU WA NAZARETI.
  Swali je binadamu akijiita yeye ni Adamu wa pili je hauoni huyu anavuruga mpango wa MUNGU ili kuwapoteza watu waende Jehanamukama wenyewe watakavyo kwenda na wengine tayari wamesha kwenda kusubiri hukumu ya moto? Kila bara watumishi wa ajabu ajabu wametokea ili kuwapoteza hata wale wateule.
  Kila mtu unayoisoma biblia na unayo akili timamu kama haujatekwa na shetani au fikra zako kufungwa lazima utakubaliana na mimi Nabii Hebron kuhusu kuwa hakuna Adamu wa pili tena zaidi ya YESU. Kama atatokea ajiite hivyo au alishatokea muelewe huyo ni muongo na ni adui wa MUNGU na pia amechukua utukufu wa MUNGU na kumpinga YESU yeye hajui lolote, au kwa maana nyingine, niulize swali sababu umeshajua Adamu wa kwanza alitokana na mavumbi na Adamu wa pili 1 Korintho 15: 47 alitoka mbinguni, sasa hivi inaingia katika akili yako mtu amezaliwa hapa duniani, ametenda dhambi, wala hajatabiriwa kuwa yeye kwa jina lake ataumiliki ulimwengu kama YESU? Sasa hauoni wanaojiita hivyo ni waongo? Na unapokuwa chini yao ina maana unatawaliwa na wao na siyo YESU wala MUNGU sababu MUNGU hajapanga hivyo ila shetani ili awateke watu fahamu na awamiliki anawatumia wale watumishi ambao yamkini YESU aliwaita hapo mwanzoni na wengine wamejiita wakamsaliti yeye sasa shetani anawatumia hao hao ili kuwapoteza wanadamu kama ilivyo sasa. Hii ni dalili tosha uelewe watumishi walivyomsaliti YESU mpaka shetani akateka kama 98% ya watu wote wa ulimwengu huu.
  Jambo lingine niwaulize swali je YESU hakuimaliza kazi yake hapa ulimwenguni? Jibu, alimaliza. Sasa wengine wanakuja kuwadanganya watoto wa MUNGU eti YESU hakuifanya kazi yote aliyotumwa? Je inakuingia katika akili yako? Wanaosema YESU hakumaliza kazi yake aliyotumwa na MUNGU hao ni waongo na ndani yao ni Lusifa anaongea siyo roho wa MUNGU.
  Yohana 1:1, 14, Mathayo 11:9-14 SOMA.
  NOTE:
  Mimi kama mimi Nabii Hebron, nawasihi watu wote huu ni wakati mbaya na wa hatari sana YESU ambaye ndiye Adamu wa pili, muda wowote atarudi kulinyakua kanisa lake ila siku na muda hiyo sijui. Utaulizwa wewe je uliliteteaje jina lake pale lilipochafuliwa? Au kama unampenda kweli YESU kwa nini usiwaeleze watu ukweli wasidanganyike pale ambapo hata wanadamu wanajifananisha na yeye wakati tunajua hakuna zaidi ya YESU aliyetoka mbinguni akawa binadamu? Akaishi na wanadamu kisha akapaa na atakuja kulinyakua kanisa lake!
  Na siku moja nilikuwa naongea na YESU 2013 akaniambia Hebron, hivi mwanadamu ni nani mpaka ajifananishe na MUNGU? Kama YESU mwenyewe anachukia pia Malaika je ni nani ajiite yeye ni MUNGU wa majeshi? Sasa kama yeye ni MUNGU wa majeshi na anaonekana kwa macho ya wanadamu basi kila mtu angekufa sababu imeandikwa hauwezi ukamuona MUNGU halafu ukaishi. Sasa kama tunaishi au unaishi na umemuona mtu anajiita yeye ni MUNGU wa majeshi basi hiyo ni picha halisi yeye ni adui wa MUNGU kama vile shetani alivyotaka kuuchukua utukufu wa MUNGU akatupwa kuzimu na ndivyo njia ni moja na hata atakayemuamini mtu wa jinsi hiyo na yeye atafuata njia hiyo hiyo. Tazama hata shetani alipofukuzwa mbinguni alifukuzwa na wafuasi wake ambao ndio malaika waliomuasi MUNGU. Najua hata sasa watu wanatengenezewa njia ya kumuasi MUNGU ili wachomwe moto na wao hawajui wanatekwa fahamu na akili zao.
  Sasa mfunguke fahamu na akili watu wote wa mataifa yote msiamini kabisa mtu yeyote awe ni Nabii, Mtume, Mchungaji, Mwinjilisti au kiumbe chochote kile. Kitakachojiita chenyewe ndio Adamu wa pili, anayo mapepo siyo ROHO MTAKATIFU 100% wala hapeleki mtu kwa YESU bali ni kwa shetani. Adamu wa pili ni YESU WA NAZARETI ndiye tuliyopewa zawadi na MUNGU ili kupitia yeye ndio njia atufikishe mbinguni na atulinde! Sasa iweje wengine katika nchi mbali mbali wajiite wao ni Adamu wa pili? Je inakuingia katika akili yako? Nawasihii kama unapenda usiende Jehanamu epuka na watu wote wanaojiita wao ni YESU au MUNGU wa majeshi au ROHO MTAKATIFU. Hao ni wapinga Kristo.
  Jambo lingine Adamu wa pili anaishi milele na ndiye atakayekuja kuuhukumu ulimwengu na ndiye atakayekuja kulinyakua kanisa ambaye ndiye YESU WA NAZARETI. Sasa swali je hawa wanaojiita Adamu wa pili ndio watakao uhukumu ulimwengu?? Jibu siyo na je wanaishi mbinguni kama YESU au wapo hapa hapa tu kama wewe? Na pia niulize swali, je YESU anafananishwa na mtu yeyote? Jibu hakuna. Watoto wa MUNGU ulimwengu umemgeukia shetani, sasaa mnaomjua YESU wa kweli mpinge kwa nguvu watu wanaobadilisha biblia na pia akatokea mtu mwingine ajiite yeye ndiyo Adamu wa kwanza, nawatangazia hao ni mapepo kutoka kuzimu kwenye asili ya baba yao wa uongo. Akitokea mtu anajiita yeye ndiye Adamu wa kwanza elewa yeye ni muongo na ni adui wa MUNGU. Akitokea ajiite yeye ni Adamu wa pili mjue yeye ni adui wa YESU 100%.
  Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu, unitoe katika mikono ya watumishi wa jinsi hii ili nisiangamie. Uniandike jina langu upya katika kitabu chako cha uzima wa milele, najitenga nao kiroho na kimwili najikabidhi kwako wewe uliye Adamu wa pili kutoka mbinguni ambaye ndiye YESU WA NAZARETI. Uniongoze, unilinde, mi simtaki shetani tena, nimetambua kwamba nilikuwa katika upande wa adui yako. Amen.
  MADAWA YA NYWELE YALIYOTOKA KUZIMU.
  Kama nilivyokwisha elezea katika makala na vipindi mbali mbali ya redio na television, nasema tena wazi wazi shetani ni mpumbavu na hawapendi wanadamu wamtafute MUNGU na zaidi lengo lake nikuyaharibu maisha ya watu peke yake yamkini unajua au haujui. Katika nchi ya kuzimu vipo viwanda vya mafuta ya nywele za wanadamu ambavyo hata mimi Hebron pasipokujuaga hapa ulimwenguni niliyapaka lakini namshukuru ROHO MTAKATIFU sanapale nilipoitwa na YESU nilipokea neema ya kubadilika na nilijikuta ghafla siyapendi mafuta ya nywele nikawa napaka mafuta ya kawaida.
  Nakumbuka siku moja hata mke wangu aliniambia daddy mbona unajipaka body lotion mpaka kichwani kwani nywele si paka mafuta yake yapo na hayajaisha nikashangaa najipaka tu wala siyapaki, kumbe ROHO MTAKATIFU aliye ndani alikuwa ananiongoza, ila siku aliponipeleka YESU kuzimu na kunipa maelekezo ya kufanya nikapitishwa katika viwanda vya vipodozi, madawa ya nywele, nikaona yanavyotengenezwa na vitu vinavyowekwa huko na kasha viletwe huku duniani ili kuwaangamiza wanadamu. Mafuta haya ambayo hata mimi niliyatumiaga pasipo kujua nikakuta kule kuzimu yanachanganywa na mafuta ya mwili ya watu waliokufa na vitu vya ajabu ajabu, ila nitaelezea kwa ufupi.
  a.       Mafuta yote ya curl yanatoka kuzimu na nimeyaona.
  b.      Mafuta ya kuzifanya nywele ziwe nyeusi (mfano nywele za watu ni nyeupe halafu anapaka dawa zinakuwa ni nyeusi) anapopaka katika kichwa chake anayaweka mapepo na pia anauzuia utukufu wa MUNGU usishuke katika kichwa chake, na pia maisha yake yatakuwa nyeusi au yana giza siku zote, na akili zake na nyota imeibiwa na mapepo.
  c.       Mafuta ya kubadilisha nywele rangi mfano zinakuwa njano, blue, nyeupe, au brown na rangi nyinginezo zote zimetoka kuzimu na madhara yake soma katika kifungu (b) yanafanana.
  d.      Kwa jinsi nilivyoangalia na niliporudi ulimwenguni niliona mafuta ya nywele 95% yote ni ya kuzimu ikiwemo na vipodozi, madawa yote ya kujichubua.
  e.       Mafuta ya kujifanyia scrub- mafuta ya aina yeyote ya scrub yanatoka kuzimu, unapofanyiwa na mafuta hayo, kwanza yanaondoka na uthamani wa ngozi yako na maisha yako, na kama unafanyiwa katika uso au kichwani unanyang’anywa macho ya rohoni, akili zako, sura yako, kibali chako ulichopewa na MUNGU na kuwekewa ya kipepo.
  f.       Shampoo zote siyo salama, asili yake ni kuzimu. Shampoo ile nzito nzito iwe ya aina yeyote ila kule kuzimu ni makohozi ya majini yote vinavyotemewa yanahifadhiwa kisha wanayaleta kwa wanadamu wajipake, na madhara yake ni mikosi, kujipaka nuksi balaa. Na shampoo nyingine ni ile ambayo ni shampoo nyepesi, hiyo shampoo nyepesi kule kuzimu ni mbegu za kiume na kike za majini, unapoitumia huku ulimwenguni wewe binadamu unafanyika kuwa nyumba ya kuzaa majini pasipokujua, na inasababisha vijana na mabinti unakuta yeye haoi au kuolewa kumbe sababu moja wapo ni kuwa yeye ni chombo cha kuzalia majini hivyo akija mwanadamu ili watafute mtoto unakuta uzazi yaani yai lina majini vitoto, na kufanya mtu hazai kabisa katika maisha yake, na pia majini hukamata akili za wanadamu pale wanapopata mlango kisha wanawawekea kupenda vitu vyao na ukipata pesa utashangaa unaenda kuvinunua vitu vyao na kuvitumia na kwa njia hiyo, biashara ya kuzimu inayofanywa na majini ikashamiri duniani na viwanda kukua kumbe ni vya shetani vimeletwa ili kuharibu maisha ya wanadamu na ndiyo sababu watu wengi ni vigumu kumpenda MUNGU au kumfuata MUNGU ni sababu ya product za shetani wanazozitumia, watu wasingeijua siri hii naelewa hata shetani pamoja na wale wafuasi wake ambao ni wanadamu ambao wanashirikiana na shetani hawafurahi kabisa sababu wanajua malengo yao yamefika mwisho na watu wa MUNGU hawatawapata tena na katika mitego hiyo YESU kaifichua siri. Sasa uamuzi ni wako wewe, pia sabuni asilimia kubwa ni makohozi ya majini, ila watu hawajui wanadanganyika na harufu za manukato yanayowekwa, ndio sababu watu nuksi na mikosi haziishi, faraka katika ndoa, magonjwa ya ngozi, sura kuharibika na mengineyo mengi ni sababu ya sabuni za kuzimu.
  -        Mfano shetani akabuni njia ya kuwakamata au kuiba uthamani wa mikono yao na pesa zao, kila unapotumia hand wash kuoshea mikono hapo unaibiwa kila kitu, unabakia kulalamika pesa hazikai na hazifanyi kazi.
  -        Kupiga deki na shampoo- unakuwa unaipaka makufuru nyumba yako au makohozi, mfano unamfahamu kono kono huyu ni kiumbe ambaye yeye hutumika na shetani kusambaza makufuru kwa ile njia ya kumwaga ule ute ambao ukiuangalia hauna tofauti na makohozi, konokono akipita kwako uelewe ameacha makufuru, sasa cha ajabu watu wengine wanakula kono kono waelewe walikula makufuru au wanakula makufuru.
  NOTE:
  BWANA YESU namba unisamehe dhambi zangu, uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima simtaki kabisa shetani navikataa vipodozi vyake na mafuta yake sipaki tena unirejeshee vitu vyangu ili niwe nina vyote ulivyonipa na niishi katika utukufu siku zote za maisha yangu. Naomba ROHO MTAKATIFU anionyeshe mafuta yote ya kuzimu na vipodozi vyote nisitumie tena na nivichome, visikae tena katika nyumba yangu balaa ikanifuata sababu ni mlango. Nirejeshee uzuri wangu na sura yangu nipendeze zaidi.
  Ili kuyajua mafuta yanaytokea kuzimu- yanaharufu kali na ukiona tu katika perfume ukasikia harufu ya ubani au harufu ya mchele mchele, iwe ni katika sabuni au perfume na mafuta yenye picha ya mwanamke ya curl, haya nimekufunulia uelewe yanatoka huko. ROHO MTAKATIFU akufunulieni zaidi awape macho myajue sababu ni aina nyingi hata nikiandika 100 days bila kupumzika sitayamaliza, ina maana maduka ya vipodozi 95% ni vitu vya kuzimu, hii ni katika ulimwengu wote. Hapo ndipo penye mtego kubwa wa shetani. Ila mshukuru MUNGU ambaye amekufunulia haya ili watu wapone. Sababu na MUNGU hapendi kabisa watoto wake wapake mafuta ya nyama za watu au vitu vya majini mfano makohozi, mikojo, jasho, huduma za shetani sasa mwisho, katika jina la YESU.
  SIFA ZA NABII WA MWISHO.
  BWANA YESU ASIFIWE, yeye ambaye ndiye Nabii wa mwisho ambaye alitumwa na MUNGU hapa ulimwenguni, kukomboa ulimwengu, nitaelezea kwa ufupi kuhusu Nabii wa mwisho, katika vipengele viwili.Kwanza katika kifungu cha kwanza katika biblia kuhusu Nabii wa mwisho. Alikuwa ni YESU WA NAZARETI peke yake, na katika kipindi kile na katika kipindi hiki cha mwisho MUNGU ameteuwa mtu ambaye ndio Nabii wake wa mwisho lakini katika sehemu hii watu wengi wanapotoshwa na bado wanazidi kupotoshwa na watumishi ambao wanajiita wao ni Nabii wa mwisho na kumbe ni waongo watupu. Wanamsingizia MUNGU kuwa wao ndio Nabii wa mwisho, hii imetokea katika ulimwengu wote, ni wengi wanaojiita hivyo.
  Sasa unatakiwa ujiulize je MUNGU alisema atakuwa na manabii wengi wa mwisho? Jibu, siyo, huu ni uongo na sababu ni baada ya watumishi kumsaliti YESU ikaingia roho nyingine ya kuasi hivyo kujiita yeye ni Nabii wa MUNGU wa mwisho hivyo usishangae, ujue analo pepo, ila nitakufundisha ili upate kupona na umuelewe kimwili yule ambaye ndiye Nabii wa mwisho wa MUNGU, ina maana akiwa yeye ndio Nabii wa kweli wa MUNGU wa mwisho, kwanza MUNGU hatamnyanyua Nabii yeyote yule mwingine sababu MUNGU yeye siyo kigeugeu.
  SIFA ZA NABII WA KWELI WA MWISHO ALIYETEULIWA NA MUNGU MWENYEWE…
  a.       Nabii huyu hatakufa kimwili wala kiroho atafanya kazi ya YESU aliyotumwa mpaka siku ile ya unyakuo amkabidho YESU watu na ripoti ya kazi aliyoifanya.
  b.      Hujua majibu ya viumbe vyote na nchi zote na hakuna jambo lolote ambalo litamshinda yeye sababu  ndani yake yeye ni MUNGU anaishi.
  c.       Haabudiwi kama MUNGU au YESU.
  d.      Habatizi watu kwa majina yake, wala haibadilishi biblia akaongeza maneno yake.
  e.       Siyo mzinzi, muuza madawa, mchawi, freemason, siyo mfanya biashara ya aina yeyote.
  f.       Anaongozwa na MUNGU peke yake wala siyo kutumia akili zake.
  g.      Unabii anaoutoa unatimia kila anaposema, hanyang’anyi watu malizao wala pesa zao, na hafanyi kazi ya MUNGU kwa kutafuta pesa kama ilivyo leo hii,wamekuwa ni wezi wanalichafua jina la YESU na MWENYEZI MUNGU.
  h.      Endapo Nabii atasema yeye ndio Nabii wa mwisho halafu akafa kimwili sasa upate picha huyo ni muongo kabisa na kama angekuwa yeye ni wa mwisho nikuulize swali je mbona hatujanyakuliwa? Na bado tupo hapa ulimwenguni? Au je sasa tupo tayari katika kipindi cha dhiki kuu? Jibu, bado. Hapo uelewe Nabii wa jinsi hiyo popote katika ulimwengu wote watoto wa MUNGU uelewe huyo anajiita jina hilo na kumkufuru MUNGU na pia kwa picha hiyo hata branch yake itakuwa inao msingi wa uongo na ni mahali pa kuulia roho za wana wa MUNGU.
  i.        Siku zote Nabii wa mwisho hawezi kuimaliza kazi aliyotumwa na MUNGU ni mpaka katika siku ya unyakuo, atakapokuja YESU kulinyakua kanisa na yeye ndiye atakayekuwa wa kwanza kushikwa mikono na YESU na kukumbatiwa kwa ajili ya pongezi ya kazi aliyoifanya wala siyo kinyume. Hivyo inapotokea au itatokea hapa mataifa yote mfunguke ufahamu. Shetani amewapa manabii wengi vyeo vya uongo ili kuwapotosha watu ili wawaamini wao ili watu watekwe. Ila umshukuru MUNGU sababu umeelewa sasa ukweli na ujitenge nao na uyachunguze matendo yao, hapa nimeelezea kidogo kwa upande wa kimwili ila kwa upande wa kiroho wewe omba utaijua kweli aliye Nabii wa mwisho na wa kweli.
  j.        Kila jambo linatokea liwe zuri au baya iwe ni katika kanisa lake, nchi yake, ni lazima MUNGU amjulishe yeye kwanza na haiwezi ikatokea pasipo yeye kujua, na inapotokea na kuleta madhara kwa watu wake sasa uelewe kabisa huyo siyo, sababu biblia inasema MUNGU hatafanya jambo lolote bila kumjulisha Nabii wake. Sasa iwaje asijue? Jibu unalo.
  NOTE:
  YESU anachukia sana watu wanaomchafulia MUNGU majina yake ambayo hajawapa, hawajui, ila yeye atapambana nao, neno la MUNGU halirudi bure, maneno haya siyo yangu mimi Hebron, ni maneno yaliyotoka katika serikali ya mbinguni kwa ajili ya mataifa yote.
  BRIAN DEACON SIYO YESU!
  Katika ulimwengu huu kwa kweli watu wengi wamepotea roho zao na mioyo yao kwa kutokujua na wengine wakijua kabisa, ila ipo neema ya YESU WA NAZARETI aliyenituma kwa mataifa yote alinionyesha kweli yake ya njia ambayo amenionyesha ili niwaongoze watu kwenda mbinguni kama vile alivyomuagiza Musa kule jangwani awaongoze wana wa Israeli waende katika nchi ya ahadi, na sasa ni kipindi cha mwisho, nchi ya ahadi sasa ni mbinguni, njia hii inaongozwa kiroho katika kweli yake tu na siyo kwa copy.
  Wakristo wengi wamedanganyika kuwa Brian yeye ndiye YESU na katika fahamu zao iyo sura ya Brian hata wakiomba inawatokea wanasema wamemuona YESU na kumbe siyo kweli. Brian aliyetunga sinema pamoja na wenzake nia yao ni kufundisha na siyo wao wachukue sehemu ya YESU, natumaini hata wao wanamkiri YESUkama BWANA NA MWOKOZI WAO. Sasa cha ajabu hii ni katika makanisa baadhi hata wanathubutu kusema uongo eti hii ni picha ya YESU. Nawaeleza wacheni uongo mmewapoteza watu kwa uongo wakaacha kusoma neno na kumtafakari YESU katika roho badala yake mioyo ya wakristo ndani yao na katika fahamu zao wamemjaza binadamu aliye act katika sinema. Hivyo madhara yake watoto wa MUNGU kwa kupitia njia hii imani zao zinaibiwa na shetani na wala hawapati YESU wa kweli. Zaidi hivi kama kweli hawa ni watumishi walioitwa na YESU waifanye kazi yake je niwaulize swali, je mlimuona ndio anafanana na Brian? Au Brian ndiye kivuli cha YESU?
  Hii inaonyesha wazi wazi kuwa hao siyo watumishi wanaomjua YESU wa kweli ndio sababu wanamsingizia Brian ndiye YESU na kuwafundisha watoto wa MUNGU wakaanza kumuabudu Brian wakati hata yeye hapendi aitwe YESU au afanywe ndiye YESU au achukue utukufu wa YESU. KAZI YA Brian na wenzake ni nzuri waliyoifanya ili kuwaelimisha watu, ila watumishi vipofu wanaiharibu kwa kumfanya Brian eti ndiye YESU. Hivi nikuulize swali ndugu msomaji, je Brian alizaliwa na Maria miaka 2000 iliyopita ? jibu, hapana. Je Brian alikufa na kufufuka na akapaa mbinguni? Jibu, yupo Uingereza ni mwanadamu tu kama wewe.
  Huku Afrika watu wengi wanamuita Brian ndio YESU na wengine mpaka wanalalia picha ya Brian wakisema wamelala na YESU. Mmh… fungukeni mtubu, tayari ni dhambi kumuabudu binadamu na hata makanisa mengi yanadanganya watu eti yeye ndiye YESU. Hii ni sababu hawa pastors hawajaitwa na yeye YESU na ndio sababu hawamjui. Hii ni hatari sana, roho za watu zinapotezwa na shetani, ametumia mtego huu ili kuwateka watu waone Brian ndiye YESU na ukiona ndiye ujielewe umepotea sababu huu ndio ukweli. Kupitia picha ya video ni ya mafundisho tu wala yule siyo YESU WA NAZARETI, leo funguka ili YESU aingie katika moyo wako, utoe picha za video zilizo act katika ufahamu wako. Hakuna picha wala sura ya YESU katika ulimwengu wote, huo ndio ukweli na ukweli uwaweke huru.
  NOTE:
  Ndugu wasomaji na wanadamu mlioumbwa na mwenyezi MUNGU haya ni machache tu nilivyokuletea wewe upate picha uelewe ni jinsi gani YESU WA NAZARETI na serikali yake akiwemo na Nabii Hebron walivyopindua ufalme huu ili MUNGU atukuzwe. Ninachopenda kuwaeleza sasa hivi muwe makini makanisa yalikufa yakawa ni mfu ndio sababu shetani akapata mwanya wa kuwateka wanadamu, shetani akaanzisha makanisa yake katika ulimwengu wote na ikabakia asilimia 2% ndio yake, injili ya uongo ikastawi, watumishi wengine hata wakajiita nao ndio MUNGU na watu wakawaamini pasipo kujua kumbe wameuliwa roho zao na wengine wakajiita MUNGU wa majeshi. Yaani hawa wanadamu, hivi kweli unavyosoma kitabu hiki inaingia katika akili yako eti mtumishi ajiite yeye ni MUNGU wa majeshi? Ina maana anachukua nafasi ya MUNGU anaupindua kama vile shetani alivyotaka awe MUNGU wa majeshi, matokeo yake ametupwa kuzimu na hao wanaojiita hivyo iwe yupo hai au walishakufa nakueleza ukweli wa MUNGU hao ni wana wa shetani na mbinguni hawaendi bali wataenda alipo baba yao, haijalishi aliitwa na MUNGU hapo mwanzo, hata shetani aliitwa na MUNGU hapo mwanzo amtumikie mbinguni ila alipomsaliti tu alitupwa, hivyo ndivyo ilivyo, hata hawa watumishi walioitwa wakafanya kazi ya MUNGU vizuri halafu wakamsaliti njia yao ni moja na shetani.
  Ninawasihi kila mtu awe mtetezi wa kuliteka jina la MUNGU pale unapoona mtu anatumia jina la YESU kuficha uovu wake, zifichueni, hata serikali ziwakatae hao ni mashetani ipo siku wataziangamiza nchi zenu zikaingia katika maafa sababu mahali walipo na shetani huweka vitu vyake, ukiwaona au kuwajua wanauza madawa ya kulevya, halafu wanajiita ni Askofu, mchungaji, mwinjilisti, mwalimu, mtume, nabii, nawaeleza hao ni WEZI, wanamchafua YESU, na ndani yao shetani anaishi.
  Mchunguze kila mtumishi kiroho, kimwili, kimatendo jinsi alivyo. Ukikuta dosari, wewe akili kichwani especially uzinzi, kuchangisha pesa katika nyumba ya sala, kufanya biashara, kuchaji riba kama ni benki, kubatizwa tofauti na YESU WA NAZARETI, usikubali katika jina la YESU WA NAZARETI, sababu unakuwa unauliwa roho yako, zaidi soma katika website yangu www.prophethebron.org vingine katika YouTube yangu na blog utafunguliwa, soma utaijua ukweli na hautakuwa na giza tena.
  SALA YA TOBA
  Nakusihi uokoke, sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote uniokoe, uniandike katika kitabu chako cha uzima wa milele, shetani sikutaki tena na kazi zako, YESU uniongoze pamoja na ROHO wako MTAKATIFU nisitekwe na shetani au kudanganyika. Na pia niwezeshe nielewe neno lako na endapo nitahubiriwa na mtumishi yeyote ambaye amekusaliti wewe, nisimuelewe kabisa wala kumsikiliza kwa jina la YESU.
  Karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, upokee uzima na ufufuliwe maisha yako na ubatizwe ubatizo wa maji mengi ili uwe mkristo wa kweli. Amen.

  Hakuna maoni:

  Visits

  Translate