Wafilipi 2:10-11
  • BAADHI YA MITEGO ANAZOZITUMIA SHETANI KUWATEGA WAKRISTO NA KUWA MAWINDO YAKE.

    BWANA YESU ASIFIWE!

    Karibu tena katika somo la Nabii Hebron ambapo katika somo hili litawafungua mataifa yote na watu wengi zaidi waliowindwa na shetani au tayari wameshategwa na shetani kuwa ni mawindo ya shetani pasipokujua au kupenda; japo wapo baadhi yao wanajitambua kabisa wao ni mateka wa shetani. Ukisoma katika kitabu cha Zaburi 91:3
    3Maana yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji na katika tauni iharibuyo”

    Mitego ya shetani ipo mingi lakini nitaelezea michache, natumaini wengi mtapona na kutoka katika hiyo mitego ya shetani kwa sababu MUNGU amesema atakuokoa na mitego hiyo. Uamuzi ni wako wewe kutoka katika mitego either imeshakutega au inakufuatilia ikutege na ikikutega mwishowe unamezwa na shetani. Mfano kila mwindaji anapowinda ni lazima anakuwa na lengo la kufanya kuwa chakula na hivyo hivyo chakula cha shetani ni nyama za watu na damu. Sasa ili akupate ni lazima akuwinde na akutege katika mitego soma Zaburi 35: 7 na akishakutega anakuwa amekupata na baadaye atakula nyama yako; unakuwa ni chakula.
    Mtego mkubwa ni kutenda dhambi ila nitaelezea mitego ambaye YESU alinifundisha na uyajue; yale aliyonifundisha aliponitokea 2010 nikiwa Serengeti National Park nchini Tanzania aliniambia “uwaeleze mataifa yote wanirejee mimi, uwafundishe neno la kweli na siyo uongo. Wakristo wengi shetani ameshawatega tayari na shetani anawasubiria ule mwisho awafanye chakula chake.” 
    Mitego nitaielezea michache;

    1.     Kubatizwa kwa ubatizo wa maji ya kikombe, hapo tayari umenaswa na mtego wa shetani katika ulimwengu wa roho na upo chini ya himaya yake na anao uhalali na wewe kabisa.

    2.     Kubatizwa kwenye kisima, kubatizwa kwa jina la mchungaji na batizo nyingine zote ambazo ni tofauti na wa kwenye biblia. Unapozipokea pasipo wewe kujua tayari umeshategwa na shetani na kwa njia hiyo tayari na wewe upo katika mtego na ndiyo sababu ukisoma kitabu cha Ufunuo 22:18-19 MUNGU alikataa neno lake lisiongezwe wala kubadilishwa. Inapokuwa hivyo tayari mnategwa na shetani na baadaye unakuwa chakula cha shetani na yeye atakumeza.

    3.     Upo utumishi ambao unaendeleza kazi ambazo sizo za YESU na watu wengi hawaelewi wanafungwa fahamu zao na serikali ya kuzimu na kupumbazwa wanaona wanaenda mbinguni kumbe wanaelekea Jehanamu. Wakati ni sasa, hiyo mitego itoke kwako uje kwa YESU WA KWELI.

    4.     Zipo nyumba za ibada ambazo zinatumia jina la YESU lakini kinachofanyika ni tofauti na neno lilivyo; inachanganywa uongo na ukweli. Hapo tayari panakuwa ni nyumba ya kuwatega watoto wa MUNGU wawe mateka ya shetani. Mfano; kufanyika michango, harambee ndani ya kanisa, kubariki watoto wakubwa, kubatiza watoto wadogo, kuandikiwa risiti ya malipo ya sadaka, kanisa kukopa benki, kuchajiwa pesa za maombezi kama hospitali za kibinadamu, kanisa kuongozwa na mashoga, kuongozwa na watumishi freemason na mengineyo mengi zaidi. Endelea kusikiliza na YouTube ya Nabii Hebron yapo masomo mengi yatakusaidia usitegwe na shetani tena, na unapoujua ukweli kwa usalama wako wa kiroho usiingie tena mahali hapo omba MUNGU akuongoze palipo salama usije ukawa chakula cha shetani.

    5.     Madhabahu inayoabudu sanamu, kufanya ibada za wafu hayo yote ndiyo mitego ambayo shetani ameingiza hapa ulimwenguni ili aweze kuwatega na watu wengi  wameshategwa. Mimi nakueleza ukweli wala siweki neno langu. Ukweli ndiyo huo wewe umeshaelewa, uamuzi ni wako, ila karibu upande wa YESU WA KWELI yeye hatakufanya chakula chake, yeye hali watu bali yeye ndiye chakula cha watu wamfuatao kupitia neno lake la kweli. Kula neno la kweli usile neno la uongo; hilo ni mtego linakutega.


    6.     Mafundisho ya mpinga kristo yote ni mitego ya shetani. Unapojiita ni mkristo lakini wewe umebatizwa kwa ubatizo wa maji ya kikombe, nakueleza ubadilike kama unataka kwenda mbinguni uondolewe huo mtego wa shetani ukabatizwe upya katika maji yanayotembea mtoni na siyo ya kisima. Wengi wanategwa na shetani, hata mimi nilitegwa kwa kupitia ubatizo wa maji ya kikombe ila YESU ameniondolea huo mtego na yeye amenipata, sipo katika ngome ya shetani kwenye ulimwengu wa roho na hata wa kimwili. Najua inashtua lakini wacha ukweli niuseme na MUNGU afurahi na shetani anune kabisa, kwa sababu kupitia ujumbe huu mtapona maelfu. Uwatumie na wengine popote, hakuna cha kubisha, uamue kuwa mkristo wa kweli, usiwe wa uongo. Japo wengi mnapenda kuwa wakristo wa kweli ila shetani akaleta mapokeo yake ya uongo yakasambazwa dunaini zaidi, wakayaammini, yakachanganywa na uongo, hapo unatekwa. Soma Wagalatia 1:6.

    SALA YA TOBA

    BWANA YESU naomba unisamehe, uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa kweli, uliondoe katika kitabu cha mauti ambacho nilitegwa na shetani ili anifanye mawindo na chakula chake. Mimi sitaki. Asante YESU nishike mkono, usiniache. Amen.
    Ubarikiwe!
                           
    NABII HEBRON.

    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate