Wafilipi 2:10-11
  • YOUTUBE VIDEO: MAKAFARA

    BABA katika jina la YESU  ninakushukuru kwa muda na wakati huu kwa ajili ya ujumbe na somo kwa mataifa yote. Ninakushukuru, ninakutukuza MUNGU. Amen.
    Katika somo la leo nitakwenda kufundisha kuhusu “Makafara” yanayofanyika na wakristo makanisani. Makafara haya yanakuwa yanawasaidia kufanya kazi za kanisa au huduma zao zinaendelea lakini watu wanafikiri ni kazi ya MUNGU. Pia nitaelezea makafara ambayo wanadamu wanayatumia ili wafanikiwe lakini nitakwenda kuyaharibu dunia nzima katika jina la YESU. Kwa sababu kuna watu pia wanakuwa wanateseka hawafanikiwi kwa sababu kuna watu wanawatolea makafara kwa mashetani, labda damu za wanyama, kuuwa watu, damu za wadudu na kuzinenea mambo mabaya ambayo ardhi iliyapokea kwa hiyo hawafanikiwi.
    Nitasoma katika kitabu cha Kutoka 22:20 “20Mtu atakayemchinjia sadaka mungu yeyote,  isipokuwa ni yeye BWANA peke yake  na aangamizwe kabisa.” Na ukisoma katika kitabu cha Mambo ya Walawi 19:26, 28 “26Msile kitu chochote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi.”28 “Msichanje chale yoyote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu, mimi ndimi BWANA.”
    BWANA YESU ASIFIWE! Katika muda huu nitakwenda kufundisha, kuna mambo ambayo yanawatesa dunia nzima, mambo ya makafara. Hapo zamani MUNGU alikuwa akichukua sadaka za wanyama, baadae baada ya kumtoa mwana wake wa pekee; damu yake kumwagika hayo mambo akayaacha na akakataza, Shetani ndiyo ameyachukua, damu ya YESU inatunenea mambo mazuri; inatunenea amani, inatunenea furaha kwa wale ambao wamempokea BWANA YESU. Lakini Shetani na yeye akaweka namna yake ya kuwafanikisha watu wake kwa kupitia nyama na damu  za wanyama au hata watu labda hata wewe. Kule kuzimu ili mwanadamu labda abarikiwe anaambiwa labda atoe watu au aangushe magari, aangushe meli, aangushe ndege ili damu inapomwagika ndipo wanapata cheo au umaarufu na njia nyinginezo nyingi za kufanya damu zimwagike pasipo amri ya MUNGU hizo damu anakunywa Shetani.
    BWANA YESU ASIFIWE! Nitazungumza katika pande mbili ila nitaanza upande wa kanisa. Makanisa mengi yanafanya makafara na yanajiita makanisa ya YESU lakini siyo nguvu ya YESU inayofanya kazi. Nafikiri wengi mmeshasikia wanazika watu kanisani, wanazika na vichwa vya watu, hayo ni makafara. Wanaweka watu ndipo shetani anawaletea watu kuja katika jengo hilo na wanakaa wanaendelea kupata pesa wale watu wanachukuliwa nyota zao ,vitu vyao na wanafikiri wanakwenda mbinguni kumbe wametekwa na shetani. Jambo lingine nitaeleza kwa ufupi makafara ambayo shetani anayatoa, ni ubatizo wa kikombe, ubatizo wa maji mengi, ubatizo kwa jina la mchungaji. Mchungaji anapofanya hivyo au hiyo huduma shetani anaiba nguvu ya  kuongezeka kwa kusanyiko kubwa kwa sababu hilo ni agano la shetani, hapo ndipo unakuta wanadamu wanatekwa na shetani pasipo wao kujua kupitia hayo makafara. Ni watu wangapi wamefanyiwa makafara leo hii?
    BWANA YESU ASIFIWE! Makafara mengine ni michango makanisani, hayo ni makafara, lakini wanadamu hawaelewi, nataka niwaeleze nyie wenyewe ni mashahidi. Utakuta labda mfanya biashara ni mchawi au ni freemason lakini anakuja kujenga makanisa na wachungaji wanamkumbatia, wanapokea misaada, nataka niwaeleze kwamba, anapotoa tu zile pesa zake nyie kanisa pia mmefanywa kafara na waumini hivyo hivyo. Haya ni mambo ambayo yalikuwa yamefichika sana lakini ni wakati wake wa kuwaeleza watoto wa MUNGU sasa wapone. Yapo makafara ya mapete ya vyeo vya kitumishi, unaona wanavaa yale mapete makubwa hayo ni makafara. Haleluya. Ninachotaka kukuambia pete ya unabii au uaalimu ikiwa mtu ana pete ya cheo fulani hilo ni kafara either anajua au hajui ina nguvu inayofanya hiyo kazi. 

    Unaweza kuta labda ni mwanasiasa kwenye kampeni amevaa lipete likubwa sana yale ni makafara watu wana wafuata wengi sana. Anakuwa ameshafanya kafara kubwa shetani anafurahi kwa hiyo anawavutia  watu, kwa sababu ni maagizo anayopewa.Pia yapo makafara ya kuua watoto wa MUNGU, lakini hao hawajui hiyo ni siri wanajua watumishi wenyewe. Mtu yeyote  ulimwengu mzima  ambaye amebatiwa kwa jina la Mchungaji ajue kwamba Mchungaji amemtoa kafara kwa Shetani na hiyo ministry inaongozwa na nguvu ya kafara kwa sababu wanapoenda kuzimu wanapewa katiba ya kufuata. Ukifuata katiba ya MUNGU haijaeleza watu wabatizwe kwa jina la Mchungaji. Kafara lingine ni kubatiza watu kwenye kisima. Hilo ni kafara la kuwazika, ndiyo maana kisima kipo square hilo ni kaburi tayari, MUNGU hakuagiza watu wabatizwe kwenye kisima bali katika mto. Haleluya.
    BWANA YESU ASIFIWE! Kafara lingine ni kuwanyima watu kuokoka na watu wamekubali hawataki kuokoka, leo sema silitaki hili kafara nalikataa nina kutaka BWANA YESU. Umeshawahi jiuliza nini kinakuzuia wewe usiokoke? Umeshajiuliza kwanini unampinga YESU? Iko nguvu ya shetani ya makafara iliyokushikilia ni wakati wa wewe kuokoka. Wako wengine, watumishi wana makafara kazi yao ni kuzini tu. Utashangaa mtumishi anazini sana ,unasema ameanguka siyo kuangauka ni kafara anafanya amri ili abarikiwe. Kuna makafara mengine utasikia mtu anajiita YESU, mwanadamu anajiita YESU lile ni kafara aliloambiwa ili kazi iende ya kanisa la kishetani.
    BWANA YESU ASIFIWE! Nafikiri mnanielewa, kafara lingine kila mtu unapoona amejichanja labda ni kwa mganga  hilo ni kafara .Mtaona waimbaji muziki, au wachezaji mpira, au watu maarufu wamejichora matatoo sana huku mwilini yale ni makafara ya shetani lazima achore ili afanikiwe. Lakini watu wanafikiri ni urembo wanajua wanafanya nini. Wapo wanaiga ni wachache lakini asilimia kubwa wanajua kabisa wanachokifanya na shetani. Ili kutoka huko ni ukabatizwe upya na kuoshwa na damu ya YESU ili hayo makafara yatoke. Watu wengi wanasema hawajatoa makafara lakini ngoja nikuulize swali; unapoenda kwa mganga unapeleka kuku, mbuzi  ile ni kafara unaenda kufanya. 

    Sasa zile damu unapozimwaga zinaendelea kunena mambo mabaya sana juu yako na zimetesa watu wengi sana na kuna watu wanakaa na kutajirika kwa sababu wanafanyia watu makafara hawafanikiwi, ninasema katika jina la YESU ninaangusha makafara yote ni wakati wa damu ya YESU kunena mema kwa watu wote. Makafara yamezungumza sana juu ya maisha ya watu na yakaharibika hata waende jehanamu. Kuna watu wamepata uwaziri, uraisi, ubunge dunia nzima kwa njia ya makafara kupewa na shetani, yawezekana na wewe pia ndugu mtazamaji, msikilizaji pia umeyafanya,tubu uokoke ili ukapate kupona maana mwisho mtu yeyote anayefanya makafara ataangamia tu. Vivyo na watoto wa MUNGU makanisani wanafanyiwa makafara kama nilivyo kwisha kufundisha  lakini  wao hawaelewi ni mambo amabayo yamejificha sana lakini nimekufunulia.
    Mafundisho ya uongo ni makafara pia.Haleluya. Mapokeo ya uongo yote ni makafara yanasababisha watu wasisonge mbele, nataka damu ya YESU ikanene mema katika maisha yako na ukombolewe na utakaswe, na hata sasa naona  kuna watu wanateseka kwa sababu wamefanyiwa makafara, hawapati watoto maisha yameharibika, watu wamewaendea kwa waganga na kuwafanyia mafundo mbalimbali naamuru yakatike kwa jina la YESU na hawa watu wanaotoa makafara ni waaminifu sana kwa shetani, unakuta mtu labda ni msanii lakini unasikia labda kwenye kituo fulani kapeleka msaada anaonyesha kwenye TV.
    Wengi ni wachawi ni makafara wanafanya kwa sababu ni amri. Kazi hizi zinasimamiwa na waganga wakienyeji, washirikina na watumishi wa kipepo ndiyo wanasimamia kupokea hizi sadaka huku duniani  na kuzipeleka kwa shetani na wao kuhakikisha watu wanaendelea kufanya mabaya. Unaweza kukuta “hudi “au” ubani” unachomwa hayo ni makafara ukiwa dukani au kwenye nyumba ya biashara ile ni makafara shetani anakaribishwa .
    BWANA YESU ASIFIWE! Maisha ya watu yamefungwa kupitia makafara. Nina amuru wote waliokufanyia makafara  nina vunja hiyo nguvu kwa jina la YESU na bomoa .Ninaamuru dunia nzima makafara yote yateketee angani, kuzimu kila mahali na wanaokwenda wasifanikiwe tena.
    Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote niliposhiriki kwenye makafara na kutenda dhambi ,naomba uniokoe uandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele .Shetani sikutaki, makafara yako yote nayachoma moto katika jina la YESU.Amen.
    BABA ninavunja makafara yote, ninachoma kwenye makaburi, ninachoma kwenye milima, ninachoma kwenye maofisi, ninachoma kwenye madhabahu zote, ninachoma kwa mataifa yote. Ninapiga kuzimu, ninapiga nguvu ya makafara ninachoma hiyo nguvu ya makafara zisifanye kazi tena. Nimeamuru katika jina la YESU. Nimepiga muhuri duniani na mbinguni. Damu ya YESU inene katika dunia nzima pande nne za dunia. Amen.

    NABII HEBRON.

     

    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate