BABA katika jina la YESU,
ninawaombea wasikilizaji, ninawaombea watoto wako mahali popote ninawafungua kwa
jina la YESU. MUNGU mkuu mwenye uweza na
mamlaka hakuna MUNGU kama wewe, ninawatuma
malaika wako pande zote, kila mahali kila nyumba, kwa kila kiumbe kinachosikia ujumbe huu kwa jina la YESU
ukaende kufanya mabadiliko kwa kila
mmoja katika jina la YESU wakapate kujua wewe ni MUNGU, wakazidi
kusimama imara, hata waliodondoka, waliokata
tamaa, MUNGU wakakurejee au waliopotezwa katika jina la YESU, BABA
ninakushukuru, Amen.
BWANA YESU asifiwe watoto wa
MUNGU, katika kipindi cha leo nitaenda kufundisha kuhusu kujengwa katika
misingi ya mitume na manabii wa MUNGU na kujengwa juu ya misingi ya mitume na
manabii wa uongo. Nitasoma katika kitabu
cha Waefeso kile cha pili mstari wa ishirini
mpaka ule wa ishirini na mbili (Waefeso 2:20-22).
Neno la MUNGU linasema hivi; mmejengwa
juu ya msingi wa mitume na manabii naye Kristo YESU mwenyewe ni jiwe kuu la
pembeni. Katika yeye jengo lote linaunganishwa vyema na kukua hata liwe hekalu
takatifu katika BWANA. Katika yeye ninyi nanyi mmejengwa pamoja kua maskani ya
MUNGU katika Roho.
Bwana YESU asifiwe! katika somo
hili la leo, Bwana YESU asifiwe ninakwenda kufundisha na kuvunja misingi
mibovu. Misingi mibovu ni mafundisho ya shetani, haleluya….na misingi mizuri ya
MUNGU ikapate kuingia ndani ya watoto wa MUNGU na MUNGU akapate kutukuzwa na kufurahi, haleluya.. Kwa
nini biblia inasema tumejengwa katika misingi ya mitume na manabii? Ndivyo
ilivyo lakini misingi ya mitume na manabii tuliyojengwa nayo ni ile ya kweli, lakini
sasa hivi mambo yamebadilika watu wamejengwa pia katika misingi ya manabii na mitume wa uongo,
vilevile nataka kukufundisha kwamba shetani alikopi kila kitu akabadilisha,
utajiuliza kwa nini YESU alikuja au wakati anahubiri akawa anapingwa, yeye alileta msingi wa kweli.
Lakini msingi wa uongo ulikua
umeshaa tawala na YESU amekuja kutafuta kilichopotea, Bwana YESU asifiwe na
kulijenga kanisa lake. Kama analijenga kanisa
lake nataka uelewe vile vile na
shetani analijenga la kwake lakini YESU anavyolijenga kanisa lake ni katika
mafundisho ya neno la MUNGU la kweli sawa sawa na biblia ilivyo ambalo ndio
msingi wa mitume na manabii wa kweli walioandika, wako kina Musa, wako kina Eliya, Bwana YESU asifiwe
wako kina Marko,wako kina Petro.
Bwana YESU
asifiwe, walisema kweli ile ambayo ndio tunaifuata sasa hivi, kina Yeremia, lakini
vile vile nataka nikujulishe mtoto wa
MUNGU, shetani na yeye ana Eliya wake wa kuzimu, ana Yusuph wake, ana Musa
wake, ana Mathayo wake! Bwana YESU asifiwe, amekopi vile vile, na vimeletwa
katika dunia hii sasa hivi watu wengi wamepotea, wanaona wapo katika msingi wa
mitume na manabii wa kweli wa MUNGU lakini asilimia kubwa kwa kujua au
kutokujua wako katika misingi ya mitume na manabii wa uongo, lakini nitakavyo
kufundisha utakwenda kuelewa je wewe umejengwa katika msingi wa manabii na
mitume wa kweli au umejengwa katika msingi wa mitume na manabiii wa uongo.
Bwana
YESU asifiwe cha kwanza
ukitaka kujua wewe upo katika
msingi wa MUNGU wa kweli, tazama YESU
alileta huduma tano akasema Mtume na Nabii
ndio kiongozi yeye hana askofu? Bwana YESU asifiwe, alileta Mtume na
alileta Nabii,
alileta Mwinjilisti, alileta Mwalimu, alileta Mchungaji, Bwana YESU
asifiwe.
Lakini sasa na shetani na yeye ana vya kwake hivyo hivyo Bwana YESU
asifiwe, na
mwanadamu unapokua unaongozwa au kusikiliza tayari na wewe unakua
umejengwa katika msingi wa mitume na manabii wa uongo au wa kweli
kivipi kupitia
mafundisho ya uongo.
Ukisoma biblia, hii biblia
takatifu imeandikwa na mitume na manabii wa kweli haleluya; tukaachiwa
mafundisho ambayo YESU na yeye ni mmoja wapo wa mtume na nabii haleluya.
Bwana YESU asifiwe, hapo utakuta kuna
ubatizo wa maji mengi yanayotembea,
unapoupata ule tayari na wewe unakua umejengwa katika msingi wa mitume na manabii wa kweli
ambao ni manabii na mitume wa MUNGU, lakini wewe ukiwa umebatizwa kinyume na
ubatizo aliobatizwa YESU, haijalishi unasema kwa jina la Baba, Mwana na Roho
Mtakatifu, wewe unakua kwenye ulimwengu wa roho na mwili tayari wewe umejengwa
katika msingi wa manabii na mitume wa uongo kwa sababu huo ubatizo ni wa uongo
sio wa kweli. Au unabatizwa kwa jina la mchungaji, kubatizwa kwa jina la mitume,
hakuna ni YESU peke yake ukiwa hivyo
tayari wewe umejengwa katika msingi wa mitume na manabii wa uongo kwa hiyo
huendi, nataka leo hiyo misingi ikavunjike na wewe umfuate YESU mahali ambapo
unaona kuna YESU wa kweli alijenga misingi ya mitume na manabii wa kweli ndipo
umfuate kinyume cha hapo umepotea.
YESU anarudi kuangalia kazi
yake aliyoanzisha, je unafikiri atachukua msingi wa mitume na manbii wa uongo? unafikiri
atachukua? Atachukua msingi alio uleta yeye kupitia manabii wake na mitume wake
haleluya; maana MUNGU yeye niwa haki anaangalia neno lake, Bwana YESU asifiwe
ukisoma Biblia YESU alileta wokovu lakini cha ajabu utakuta makanisa baadhi
yanasema hakuna habari ya kuokoka, ninawaeleza huo ni msingi wa mitume na
manabii wa uongo ambao hautaki wokovu, YESU alileta wokovu na bila kuwa na
wokovu wewe hukamiliki kuwa mkristo, hakuna cha kukata shauri hakuna, ni unatakiwa umekua mkristo umeokoka, wakatuletea
kukata shauri, kataa, tafuta kwenye biblia hakuna jambo la kukata shauri ,ivi
wewe unakata shauri? shauri ni nini? unatakiwa uokoke. YESU akija ataangalia
msingi wake wa wokovu, je umeokoka? Lakini wengine wanakwua wamepotea wanasema
mimi mlokole, mimi nakwambia YESU hajaleta msingi wa ulokole, hata kwenye
biblia hakuna neno ulokole! Yeye alileta wokovu Bwana YESU asifiwe, kwa
kingereza inaitwa salvation, sasa wewe umepokea ulokole au umepokea salvation?
YESU
ameleta wokovu, msingi wake, mnatakiwa
muupokee, lakini vile vile unaweza kuta watu wameokoka, nataka niwaeleze
kwa
sababu mambo yamebadilishwa badilishwa sehemu nyingi hata katika
mataifa niliyotembelea. Bwana YESU asifiwe! injili imebadilishwa na
wana wa MUNGU hawaelewi wanampenda sana MUNGU lakini wengi wamejengwa
katika
msingi wa manabii na mitume wa uongo!
Asikuambie mtu kwamba yeye ametumwa na MUNGU
halafu hataki kubatizwa ubatizo wa maji yanayotembea mtoni; huo sio
msingi YESU aliouleta alisema
mimi ndiye njia ya uzima na kweli nifuateni mimi nilivyofanya, aliingia
mtoni
Bwana YESU asifiwe akiwa mtu mzima sasa leo hii imebadilishwa uwe mtoto
mdogo ndio
unabatizwa tayari huo ni msingi wa mitume na manabii wa uongo, unajua
mambo ya
kiroho yamefichika sana lakini jinsi MUNGU anavyonipa neema
nakunfunulia nitakua nikiendelea kuwaelezea na
zaidi endelea kusoma katika website,
katika blog; www.prophethebron.org utakuta mafundisho nikiendelea
kuelezea na
vitabu vingi mtajua ukweli, hata kama wewe umejengwa katika msingi wa
manabii na
mitume wa uongo utapona uchukue hatua, unaweza ukawa wokovu wako
umejengwa
katika misingi ya mitume na manabii wa
uongo.
Bwana YESU asifiwe, unabatizwa
kwa jina la mchungaji wewe umejengwa katika msingi wa mtume na manabii wa uongo,
umebatizwa kwenye kisima, hakuna huo ubatizo. Bwana YESU asifiwe, tafuta kwenye
biblia ukisoma biblia inasema katika kitabu cha Ufunuo 22:18-19, ole wake
aongezaye maneno ya kitabu cha unabii sehemu yake itaondolewa, ninakueleza ndivyo
ilivyo na mafundisho yote ya uongo siyo msingi wa MUNGU. Bwana YESU asifiwe…Haleluya…MUNGU
anawapenda sana ni wakati wa kuambiwa ukweli,YESU anarudi atakuja kuchukua
alichokipanda yeye na kukivuna yeye, kama kimepandwa na shetani au mpinga kristo utabaki huko
huko, ukisoma biblia hii inasema msiabudu sanamu, ni ajabu wakristo wanaabudu
sanamu huo ni msingi wa mitume na
manabii wa shetani, hayupo YESU hapo!
Jambo lingine endelea kusoma
kitabu hiki Bwana YESU asifiwe, kuna watu wanafanya kazi ya MUNGU wanasubiri
mshahara, na mwisho wa mwezi wanaenda kuchukua mshahara tena wanasubiri waongezewe.
Bwana YESU asifiwe, na wanalipwa makato kama kawaida NCCF, PPF…Bwana YESU
asifiwe, vitu ambavyo wanapewa watu wa kaisari; kwa MUNGU watumishi wake
wanabarikiwa ila wale ambao wako upande ambao siyo wa MUNGU, wale wanaitwa
watumishi wa mishahara ,na kama unaitwa mtumishi wa mishahara?
Wewe umejengwa katika msingi wa
mitume na manbii wa uongo; ukibisha turudi katika neno hakuna mtumishi
anatakiwa kupewa mshahara MUNGU kwa mtumishi anambariki soma neno hata kama
unachukia; chukia lakini ukweli utabaki hapa hapa, tena mshukuru na mpone,
maana yake shetani anakunyanyulia bango hata kama unampenda MUNGU, anasema huyu
ni mtumishi wa mshahara….huyu ni mtumishi wa mshahara, je MUNGU una watumishi
wa mshahara? neno lako linasema utawabariki kwa hiyo nataka muelewe watoto wa MUNGU watumishi wa MUNGU hawana mshahara
wanabarikiwa basi!
Sasa
siku hizi wamenyanyuka wakutafuta
pesa au wa misingi ya shetani; wakujiita, misingi ya mitume na manabii
wa
uongo. MUNGU yeye anamuita mtumishi wake, anapomuita anampa chanel na
direction
ya kazi yake haleluyaa..habahatishi lakini misingi ya mitume na manabii
wa uongo,
mtu atakwambia nimeongea na MUNGU, sawa! Ameongea na mungu shetani pia
ni aina
ya mungu, ataanzisha huduma zitaitwa kwa jina la YESU, zina upako wake,
zina uponyaji wake, lakini ukija
ukiangalia misingi ya mitume na manabii huku, nimekupa bure toa bure,
wewe
utasikia leta pesa yako ndio MUNGU atakufungua, ninakwambia huo ni
msingi wa
mitume na manbii wa uongo hauwapeleki mbinguni mtaangamia rejeeni kwa
MUNGU acheni
hayo mambo, na wako watu wengi hata wokovu wao haukui, hata hawabadiliki
kwa sababu umejengwa chini ya misingi ya mabii na mitume wa uongo,
japo wewe
muumini haujui, hayo ninakufunulia ukapate kuelewa…haleluya...
Watu wengi wanaomba sana
wanasoma biblia, umejengwa kwenye msingi wa uongo wewe, unakuja
unasema….nasimama na kitabu fulani neno litakua hili, haliwi! kwa nini? jiulize
kwanza msingi wako wewe asili yake
jichunguze, umejengwa katika misingi ya
mitume na manabii wa kweli au wa
uongo, kivipi utajuaje? Angalia mafundisho ya uongo au mafundisho ya kweli. Bwana
YESU asifiwe, au kanisani kwenu mnatoa huduma kwa kuchaji pesa Bwana YESU asifiwe, maana na shetani ana
miujiza yake…haleluya…
Katika misingi ya mitume na
manabii wa uongo kazi zao za injili ni
lazima wachangishe pesa, YESU alivokuja alivyoingia hekaluni alikuta wanafanya
biashara, alifukuza maana siyo mahali pake kwahiyo makanisa ukikutaa mahali wanachangisha pesa wa elfu laki moja
simama hapa huo ni msingi wa mitume na
manabii wa uongo na ukikaa hapo na baraka zako zimejengwa katika hao,
mfilisi,masikini na Mbinguni huendi. Ninachokwambia ndicho hicho lakini katika
msingi wa mitume na manabii wa MUNGU, aliojenga kwa ajili ya kanisa lake
linalopeleka watu Mbinguni linakujenga wewe, katika nyumba yake hakuna harambee
nawaeleza mkichukia mchukie!
Tusome kwenye biblia hakuna
mahali imeruhusiwa kufanyika kanisani. Kama kazi ni ya kwake mtumishi arudi kwa
MUNGU amuulize yeye, kama amejengwa kwa misingi ya mitume na manabii wa kweli
wa MUNGU, amrudie yeye ataona njia zinafunguka,lakini waliojengwa katika
misingi ya mitume na manabii wa uongo
watarudi hapo hapo,na wengine hata walianza na MUNGU
lakini wamepotea kwa sababu ya
kufuata hayo mambo ya elimu za uongo za wanadamu.
Mtu atakwambia ni Doctor pamoja na degree yake lakini ukiangalia
anafanya vitu kinyume na MUNGU. MUNGU haangalii hicho kazi hiyo inafanywa na
Roho Mtakatifu, inawezekana hata upo darasa la tatu MUNGU akakutumia, unajua kusoma biblia tu
basi…haleluya...Roho mtakatifu mwalimu wa kweli anaingia ndani. Bwana YESU
asifiwe.
Hayo ni mambo umekua ukisikia. Sasa hivi huduma watu ni wachawi, watu
ni washirikina, Mchungaji ni mshirikina, mara anatoa watu kafara, nini hiyo
nachowaambia ni misingi ya mitume na manabii wa uongo,mara mwingine atakwambia
anadondosha watu angani nakwambia hivi, msingi wa mitume na manabii wa
MUNGU wa kweli wanaonyesha watu
kinachofufuliwa kama wanabisha wapelekee hapo maiti watakimbia! Lakini wanataka watengeneze njia njia
za kudondosha dondosha watu kataeni hii misingi na hata kama mnashiriki
unajenga ufalme wa misingi ya mashetani
pasipo wewe kujua lakini wewe ukifikiri
kwamba unamjengea MUNGU.
Hatakama unaimba hapo unapoabudu
ujue kwamba kwenye ulimwengu wa roho inabadilishwa wewe hapo unamwimbia mungu
wa manabii wa uongo ambaye ni lusifa, joka kuu na serikali yake wanatukuzwa na
mpinga kristo, ni ajabu sana Bwana YESU anarudi alipokuwa akiniambia mambo haya
nilikua naogopa sana maana nilikua mtoto mdogo sana kama miaka minne hivi kiroho,
Bwana YESU asifiwe, nakutuma kwa mataifa yote misingi imeharibika imebaki
asilimia mbili( 2%) , hata sasa nimeanza kwenda na bado nitazunguka dunia
nzima, na yeye ndiye atanipeleka kwa jina la YESU njia zake MUNGU ni MUNGU na
zitafanyika tu.
Nahakikisha misingi hii
iwaachilie wana wa MUNGU, watasikia sauti ya MUNGU watabadilika siyo kwamba
watakuja wote, wa shetani wapo. Bwana YESU asifiwe, kwa nini neno la MUNGU
linasema acheni magugu na ngano yakue pamoja, mengine yatabadilika yatakua
ngano ila yakikataa yabaki kua magugu, yawezekana wewe ni ngano lakini ukikaa
na magugu ukikataa kubadilika nawe utakua hivyo hivyo, inamaana kwamba ukikaa na msingi mbovu nawe unakuharibu Bwana
YESU asifiwe…haleluya..msiogope watoto wa MUNGU, YESU anarudi, ili wewe
utengenezwe wewe akukute na akuchukue kubali kujengwa katika kweli ya neno lake…haleluya…
Cha kwanza hakikisha umetimiza
ahadi zote; umeokoka,umebatizwa, hutendi
dhambi, unaisha maisha ya kitakatifu, YESU hayo ndiyo aliyoyaleta, wanadamu
mwogopeni MUNGU, msimuone MUNGU ni rafiki au jirani. MUNGU hafananishwi na kitu,
msimuone MUNGU niwakuchezewa. BwanaYESU asifiwe, ametulia, wakati wake unakuja,
watu watalia na kusaga meno, huu ni wakati wa neema ninawaeleza watoto wa
MUNGU, mahali popote ulipo mrejee Bwana YESU, uliyejengwa katika msingi wa
uongo hutaki kuokoka acha, na ndio maana kuna watu hawataki kuokoka kabisa hata ukiokoka wanakwambia
umechanganyikiwa, yeye amejengwa katika msingi wa mitume na manabii wa uongo
ambao ile roho imekaa ndani yao kwa hiyo anashangaa wokovu ni nini lakini
unakuta anang’ang’ania YESU, wewe siyo rafiki wa YESU umegombana na YESU, kubali
leo upatane na YESU, hii dunia itapita mambo yatapita haleluya..hao marafiki
wataishia kaburini.
Bwana YESU asifiwe, utakapoingia
kaburini ule mwili wako ndio utapambana na yeye, huko hakuna wa kukusaidia,
hakuna wa kuongea na wewe, wakati wako ni sasa Bwana YESU asifiwe…haleluya..nitatoa
labda mfano mwingine ili muelewe, Bwana YESU asifiwe, kuna neno linaitwa
kafiri! Bwana YESU asifiwe, maana ya kafiri ni mtu yeyote ambaye haendi sawa
sawa na neno la MUNGU lilivyo, kwa hiyo unaweza kukuta mtu anasema kafiri, lakini
yeye mwenyewe ajichunguze kwanza ndani yake je anafuata sheria za MUNGU? ameokoka?
anasema kweli? anahubiri kweli? au ananyang’anya watu pesa? Sasa akiwa kinyume
hivyo yeye ankua ni kafiri. Bwana YESU asifiwe, je unafikiri YESU atakuja
kuchukua kafiri?
YESU anakuja kuchukua mtu ambaye siyo kafiri, Bwana YESU
asifiwe, nataka nielezee maana hii ya kafiri ni mtu yeyote ambaye hafuati
sheria za mwenyezi MUNGU,ni mtu ambaye yeyote hamfurahishi MUNGU, siyo umchekee
kutoa meno bali kubali sheria zake na amri zake, sasa hapa duniani tayari
umekua kafiri au umekua siyo kafiri ni wewe mwenyewe uamue, unataka kuwa kafiri
au kwenye maisha ya kafiri au unakuja kwa YESU? Mimi nakwambia njoo kwa YESU, usiwe
kafiri Bwana YESU asifiwe, lakini
makafiri nataka uelewe hapo,wapo makafiri wakubwa wa kiroho ambao ni watumishi,
na wako makafiri wadogo, hao makafiri wakubwa ndio hao watumishi ambao
wanatumia uongo,na kutumia neno la MUNGU
katika uchawi, utawajuaje hao makafiri? Kwa matendo yao, neno la MUNGU linasema
hivi….kwa mtumishi wangu niliyekujenga katika msingi wa mitume na manabii wa
kweli, nimekutuma wewe usifikiri utapata pesa wapi, mimi nitakuongoza utapata
pesa njia zitafunguka haleluya..lakini wanao ongozwa na kafiri hao manabii na mitume
wa uongo katika ulimwengu wa roho katika ufalme wa shetani, watakaa kwenye TV, na
kuomba pesa na M-PESA kumwaibisha mwenyezi MUNGU, MUNGU wetu siyo masikini, MUNGU
wetu ana kila kitu, kazi zaoni kunyang’anya watu, watu mpaka wamechoka,
hawataki habari za MUNGU zimewakwaza mimi nawaambia hivi. Zilizo wa kwaza siyo
za MUNGU, siyo za YESU habari za YESU wa kweli na MUNGU wa kweli kama umekutana
naye zina neema, zinafurahisha, zinakuponya wewe funguka sasa mrejee MUNGU wa
kweli…haleluya..usiogope anakupenda, wako malaika wanakuangalia ni wakati wa
kuharibu ufalme wa ma shetani, lakini hautaitwa wa shetani maana kuna makanisa
ndiyo ya shetani, lakini shetani ana mbinu nyingi amekopi biblia!
YESU alianzisha kanisa akasema
na ubatizo wa maji mengi, naye akaanzisha wa maji kidogo, haupo mbinguni huo, unasema
unakwenda mbinguni, mbingu ipi utakwenda? wanakwambia hivi ukisoma katika msingi wa mitume na
manabii wa kweli, MUNGU wetu si MUNGU wa wafu, huu mwingine wanatengeneza
kwamba ukifa tutakuombea, ninakwambia toka mwaka 1949, hakuna rais aliyeingia
au mfalme mbinguni paradise. Kama ni watu wanaombewa ni hao, MUNGU anaangalia
haki haangalii cheo chako Bwana YESU asifiwe, anakuangalia kama alivyokuleta
umekaa katika line yake? kama hujakaa katika line come now! this is your time. Bwana
YESU asifiwe, hakuna mambo ya kuogopa,unayeogopa mimi nakuombea usiogope, walipokushika na kukushindilia
MUNGU anakwenda kukunyanyua, misingi iliyokujenga naenda kuivunja, ikuachilie
maisha yako, ikuachilie ukaokoke, ikuachilie ukapate kutawala na kumiliki,ukatembee
kama mwana wa MUNGU kifua mbele.
Sasa hivi watu wengi wameokoka
yaani ndiyo wana shida,wana shida, shida si ya kwao wamejengwa katika misingi
ya manabii wengi wa uongo, ni viliyo, hakuna watu wanalia shida kama wakristo, mimi
nakwambia asilimia kubwa omba omba, lile jina unapolipata la huyu YESU anasema mtakua nuru kwa nini
hamuwi nuru? Umasikini ndio umejaa, shida zimejaa,wakristo wachawi, haiwezekani
Bwana YESU asifiwe, yeye MUNGU awafungue
macho,YESU anarudi, ulikuja mwenyewe mwanadamu sijui utarudije. Amenituma kwako
nikueleze, mimi amenituma habari njema ndio hizi nakwambia, habari mbaya sasa hivi
ni nyingi zinasambazwa, injili za uongo za uongo za uongo maana shetani
anatajirishwa na watu wake nataka uelewe! Bwana YESU asifiwe, ni wakati wa
kumsimamisha
Bwana YESU..haleluya..hili jina la YESU linatumika vibaya kwa
sababu wanadamu wanajua ya kwamba jina
hili linapendwa na shetani naye amelichukua analitumia vile vile kwa watumishi
wake, nataka nikwambie kuna watumishi wanaenda kuzimu kabisa, anapewa uchungaji
na shetani, uinjilisti, unabii anasema naye na ndio maana utashangaa kuna mtu
anasema unabii alafu inakua ni muongo, sasa huyo mungu ni muongo, ndio msingi
wa manabii wa uongo.
Bwana YESU asifiwe, kama
nilivyokwisha kuwaambia Tanzania ndio taifa linaenda kunyanyuka na
limeshaanyanyuka dunia nzima itakuja kusarenda hapa, MUNGU ameniambia na ndivyo
ilivyo, msingi wa nabii na mitume wa kweli na neno lake linatimia,walio wa kwanza
watakua wa mwisho, na wa mwisho watakua wa kwanza, nchi iko mikononi mwake
nilikwisha kusema hakuna uchawi hapa nchi itabadilika hata wanao iba iba pesa
miaka minne watu walioona napiga kelele mmeyaona sasa na bado YESU yupo kazini
anawatu wengi atawatumia hao hao, Bwana YESU asifiwe msiogope, imefika mahali
nchi hii haiendi vizuri, wachawi tu laity ungekua na macho, wengi ni wachawi
wanakaa makanisani lakini wanaenda kuzimu wanapanda na kushuka wanapanda na
kushuka kuharibu hata uchumi kuharibu viongozi,
kuharibu bunge wasielewane, kuna wakati utashangaa hata wabunge wanatukana
tukana tu, Bunge haliombewi; tuliombee. Bwana YESU asifiwe ni wanadamu pale ni
vita bana pale wakikaa vizuri nchi itaenda vizuri!
Wasameheane hata yaliyotokea
Bwana YESU asifiwe, mipango yote ya wachawi haitafanikiwa ni mpango wa Bwana
YESU dini nyingine wanamwita nabii Issa, kila mahali inajulikana anayekuja
nabii wa mwisho kuchukua kanisa kuchukua watoto wa MUNGU ni nabii Issa, wewe
umemkubali Bwana YESU? mkubali sasa kama hujajengwa chini ya msingi wake leo na
sasahivi ndio nafasi yako wa kweli
usikubali kujengwa katika msingi wa YESU wa uongo, hakuna wokovu ni michango,
Bwana YESU asifiwe, hata ukitaka kubatizwa unatoa ada, unajua hata serikali ni
nzuri sana haichaji kanisa kodi, inahofu na MUNGU, Bwana YESU asifiwe ,lakini
huku wako baadhi yao wanafanya mambo yao kwa kuharibu jina la Bwana YESU, simama
umtetee Bwana YESU, msingi wa mitume na manabii wa kweli, ukisoma Biblia
anasema hivi, MUNGU anasema hivi, usilipe riba,usichaji riba, lakini leo hii
unakuta makanisa ya mitume na manabii yana benki yanachaji riba, nataka uelewe
hao wamejengwa juu ya misingi ya mitume na manabii wa uongo na waumini ni huko
huko wanakwenda kwa muongo, baba yao atakua ni muongo, maana MUNGU analiangalia
neno lake.
Kuna mbinu nyingi sana anaweza akakwambia kwamba ameongea na MUNGU
amefika mpaka anapelekwa kuzimu anaongea na shetani, si baba yake hawezi muita
shetani nataka uelewe…haleluya...Bwana YESU asifiwe, mnasikia watoto wa MUNGU? lakini
jeuri yao imekwisha, njia zao zimekwisha kufungwa…haleluya...YESU atanyanyuliwa
na ni wakati wake wa YESU wa kweli sasa kusimama ndio…vita vitaendelea lakini
YESU atashinda tu! Na nakwambia wewe ambaye unashindwa kila siku nitakuombea
utashinda utasonga mbele..haleluya…zaidi karibu katika kanisa la YESU NI BWANA
NA MOKOZI WA MATAIFA YOTE nitakuombea na mambo mengine utaendelea kufunguliwa.
Bwana YESU asifiwe, ingia
katika website yangu www.prophethebro.org ingia katika link ya blog na youtube
Bwana YESU asifiwe, karibu sana na utafunguliwa kuna vitabu, Bwana YESU asifiwe
nataka mumuelewe MUNGU, mimi nilikua si mtu wa kuhubiri, nilivyokutana na YESU
kwanza nilikua namshangaa akili yangu mimi nilikua nimejengwa katika msingi wa
mitume na manabii wa uongo kwa hiyo sura ya YESU nikajua ni yule mwingereza
Brian, hizi picha mnasema ni YESU. YESU anakuja anaongea na mimi ninamkemea, ninamkemea,
ninamkemea, nilikuja kutubu baadaye baada ya kunielewesha, wala hafanani wala
hakuna sura ya Bwana YESU hapa yeye ni MUNGU hata jicho lake huwezi kuchora, Bwana
YESU asifiwe,uku wake na uweza wake niwa ajabu, hapa duniani mnaona ona kuna
vitu, hakuna vitu!
Mbinguni nimefika yako makao
yanakusubiri wewe, kuzimu pia nimekwenda nikaoneshwa na YESU palivyo, siyo huyu
YESU mnayeoneshwa picha za Brian hapa, hizi anaact huyo siyo YESU. Nimefika
mbinguni nimepaona ,nimepelekwa kuzimu nimepaona na kuzimu inavyokushangilia
inakusubiri wewe, Bwana YESU asifiwe, nimewakuta wachungaji, maaskofu, mitume, manabii
wengi wako huko ambao duniani walikua wanajulikana ni watumishi haswa kumbe ni
mapepo tu! Na hata waliopo hapa duniani mnaona wanaendesha kazi zao kichawi chawi,
wako kule kuzimu kwa hiyo wanakua connected na shetani kuintroduce kazi zao
huku na branch zao zinasambaa, wewe unapokaa tuu pale nafsi yako imeshavunwa
YESU hakupati, nataka sasa ukapate kusimama.
Misingi ya mitume na manabii
unakuta eti mchungaji anjiita MUNGU, soma biblia ni nani anayefananishwa na
MUNGU? hakuna ! mrejee Bwana YESU …haleluya...mtatolewa na ishara za uongo na
shetani anaweza hivyo hivyo, kumbukeni kipindi cha Musa, farao naye
akatengenezewa nyoka, zaidi njoo kwenye neno la MUNGU hatua kwa hatua, muulize
wewe unasema ni mkristo je mbona hujabatizwa kama YESU? Tuchambue ubatizo gani
uliwekwa na YESU? wa misingi ya uongo siko huko! Toka rejea uokoke ukabatizwe
upya usimame imara, usiimbe hapa wewe ni mkristo unaenda mbinguni kila siku
jumapili, kumbe unaenda kukonektiwa kupigiliwa misumari kila wiki unaenda kuwa msingi mbovu kataa! Bwana YESU
asifiwe.Ukisoma katika misingi ya mitume na manabii wa MUNGU, tumepewa roho
mtakatifu atuombee, tafuta hakuna mahali ipo Petro anatakiwa atuombee! Hakuna
mahali iko Musa, hakuna mahali iko jina la Frank hakuna la mtu yoyote nakazalika,mtume
yeyote hapa, hakuna! tunaye ruhusiwa kumuomba yuko Roho mtakatifu, ni mambo
yameharibika watoto wa MUNGU na leo watu wamejengwa katika misingi hiyo, hiyo
misingi ya mitume na manabii ya uongo, nawe umekua ni muongo, mkristo muongo
mbele za MUNGU wala MUNGU hakutambui, iko neema MUNGU amenituma kwako wewe
rejea, haleluya Bwana YESU asifiwe.
Nilikua mahali fulani, nikashangaa
sana,ukisoma misingi ya mitume na manbii waliojengwa na MUNGU, nimekupa bure
toa bure, mtumishi kwenda kumuona anakwambia dollar mia kumsalimia, hao
niwaongo, kusikilizwa pesa waongo, unapewa na risiti hao ni waizi! Na wewe
ukristo wako hujajengwa na MUNGU, umejengwa na shetani, lakini hujui ni shetani
wanasema shinwa shindwa shetani, shindwa shetani,hakuna ufalme ambao unaweza
ukaharibu ufalme mwingine, kataa ondoka huko, Bwana YESU asifiwe, mrejee Bwana
YESU wengi wamepotezwa, wengi wanalia,wengi wamekata tamaa, Bwana YESU asifiwe.
Nimekuta kuna mafuta ya upako, unajua MUNGU wa mbinguni siyo mlanguzi, unakuta
mafuta yanauzwa elfu tano au elfu sita dukani mchungaji mwingine anauza laki
mbili! Je wananchi au wanadamu wana moyo wa ukarimu zaidi kuliko MUNGU? sasa
huku kutafuta vitu wizi! Lakini ni maagano ya kishetani, MUNGU awafungue macho
wewe unayesikiliza, Bwana YESU asifiwe, utaenda kwenye semina, kwenye maombi
sana lakini unakutana na mapepo, nakueleza kama ulikua hujui, sasa ukaelewe
Bwana YESU asifiwe. Lakini nakutia moyo neema yake ipo bado, anarudi YESU
angalia usikutwe umejengwa kwenye misingi ya mitume na manabii wa uongo.
Kanisa mtu Baba yake na watoto
wake ndio wanalichukua hayaa! Umeangalia vitu kama hivyo,watu wanafanya
makanisa ni sehemu ya kupata pesa si mahali pa kumwabudu mwenyezi MUNGU, ni
mahali pa kwenda kukaa na amani, we umeenda kutafuta amani kabla hujaondoka
simama mchango wa kwaya kama kwaya ni ya MUNGU hiyo sadaka unayotoa wakati wa
sadaka si inafanya kazi hiyo? haya kikapu cha Mama mchungaji ni msingi wa
uongo!Bwana YESU asifiwe, sijui mchungaji anasimama unamsainia hela nisainie kwenye shati! ni misingi ya manabii
wa uongo, au unakuta kanisani,wanakujua
kiasi chako unaitwa Gold wewe saizi ya Gold , Almasi lulu, wanaangalia
pesa yako huyo ni msingi wa manbii wa
mitune wa uongo wa shetani hata unaitwa
umedanganywa unaliwa pesa wala MUNGU hajapokea zimepotea na unazidi kuvuna umasikini
unajenga ufalme shetani na unaingia katika hukumu hiyo, uliwekwa hapa duniani
ukafanye kazi ya MUNGU, ukaende kufanya kazi ya MUNGU na kuombea hata kumsifu
ili siku moja kule mbinguni ukavalishwe
taji, tazama siku ile ya mwisho,utavalishwa taji na shetani kama ulikua hujui elewa
sasa, amenituma kwako elewa kwa mataifa
yote.
Bwana YESU asifiwe...msiogope, Bwana YESU asifiwe, MUNGU anawapenda watu
wake wote, wala yeye habagui, tatizo ni ukafiri umeingia, ukafiri sasa wewe
unasema unamfuata MUNGU, jichunguze matendo yako kama hauko sawa na MUNGU, neno
linaitwa kafiri halikuachi na mimi sitaki muwe kafiri, Bwana YESU asifiwe, kile
kilichokua kafiri nataka kibadilike kimrejee Bwana MUNGU.
Bwana YESU asifiwe ili siku moja
urudi na wewe Mbinguni, lakini na hapa duniani umfurahie MUNGU. Bwana YESU
asifiwe haleluya..Bwana YESU asifiwe, msiogope watoto wa MUNGU, MUNGU
anawapenda sana, alipokuwa akinieleza mambo haya mpaka natoa machozi Bwana YESU
alikua akinieleza Mbinguni yupo na Petro aliyekua mwanafunzi wake hata wao kina Yeremia walioandika biblia wako
mbinguni na kina Daudi na kina Yohana na muda wa kurudi YESU
umeshafika,wameshamaliza maandalizi yote
mpaka ya hukumu, na mimi sasa ninakufunulia siri hii nabii wake MUNGU, rejea
kwake hukumu isikukute tazama utasema
nasubiri lini utabadilika mpaka kesho au lini
usimwambie MUNGU ukampangia time,time yako na sasa hujui yajayo kesho. MUNGU
hana mpango na watu ambao hawamtaki sasa hivi,wanasema wakati mwingine tutakua
tuna time na MUNGU inamaana unavyosema hivyo inamaana una time na shetani, sasa
sema time ya shetani sitaki bye bye.
Bwana YESU asifiwe, yawezekana
hata hujaokoka lakini wewe ni mkristo kumbe uko katika msingi mbovu ondoka sasa
simama imara biblia inasema tokeni mkatengwe nao ukakae mahali ambapo kuna neno
la kweli lisiloghoshiwa, utaambiwa neno lisiloghoshiwa lakini watu wanabatizwa
kwa kisima na neno lisiloghoshiwa hapo
utasikia watu wanaandika majina wanapewa
risiti hii imekua biashara. MUNGU haangalii pesa zako, Bwana YESU asifiwe, siku
moja nilikua naongea na mtu mmoja hii
misingi ya aibu, moja mtumishi mmoja wa mahali fulani ana kanisa sasa viatu
vyake vimetoboka akaingia madhabahuni siku ya ibada akaanza kunena rikoboshondo
rakashika akaanza kulia anajifanya anaomba MUNGU, ananena… baba wasamehe kanisa hili…wamemuacha mchungaji
wao mpaka viatu vimetoboka... wasamehe baba usiwapige, kanisa zima likaanza
kulia saa hiyo hiyo wakaenda knunua viatu… wakamletea mchungaji madhabahuni
akavalishwa, eti wanaomba rehema!huyu ni muongoo…MUNGU watumishi wake
hawajiabishi yeye hana shida. YESU anarudi na katika ulimwengu wa roho wachawi
wanajua, kuzimu wanajua na wako wanadamu ambao ni watumishi wa shetani na wao
wanajua….anarudi yuko njia, dalili zimeshatimia, mambo yao hayaendi. YESU
anakwenda kunyanyuliwa, toka kwenye mgome ya mashetani.
Sema BWANA YESU, NINAOMBA
UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE NILIZOZIFANYA KWA KUJUA AU KUTOKUJUA. UKANIVUNJIE
MISINGI YOTE MIBOVU NDANI YANGU ILIYOJENGWA NA MITUME NA MANABII WA UONGO.
IKABAKI MISINGI YA MITUME NA MANABII WA KWELI ULIYOIJENGA WEWE BWANA YESU, UNIONGOZE
NA JINA LANGU ULIANDIKE KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA. AMEN
NABII
HEBRON.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni