Wafilipi 2:10-11
  • KUZIMU NI HALISI. 'NILIKWENDA HUKO'.

    na Jennifer Perez
    Ushuhuda wa msichana mwenye umri
    wa miaka 15 ambaye alilelewa katika
    Familia ya Kikristo.
    lakini baadaye alirudi nyuma katika
    safari yake ya wokovu, alijikuta akitumia madawa ya
    kulevya kupindukia, akafa, na kupelekwa
    Kuzimu. Kwa neema tu, alipewa nafasi
    ya pili na
    mpango/ ujumbe wa haraka wa kuja
    tena na kuonya waliovuguvugu na waliopotea, www.DivineRevelations.info/
    SWAHILI Mungu akubariki kaka na dada,
    ningependa ufungue Biblia
    yako na urejee Yoeli 2:28 "Na baada ya hayo, nitamimina
    Roho yangu juu ya watu wote wana
    wenu na binti zenu.
    watatabiri, wazee wenu wataota ndoto,
    na vijana wenu
    wataona maono. " Jina langu ni Jennifer Perez na mimi
    nina umri wa miaka 15. Ni
    vigumu kwa kijana kama mimi kuja
    kwenu na kutambua/kukiri
    makosa yangu mwenyewe. Lakini kwa
    msaada wa Roho Mtakatifu, Yeye atanisaidia, na kunipa
    mimi nguvu ninazohitaji. Awali ya yote
    nataka kusema
    kwamba hii ni kwa Heshima na Utukufu
    wa Bwana wangu Yesu Kristo. Sitaki
    kusema fundisho/msingi au kuweka fundisho/
    msingi mpya, ninakwenda tu kuwaambia
    kile nilichokiona,
    nikasikia, na kukihisi.
    Ningependa kukuambia kidogo kuhusu
    familia yangu. Wazazi wangu ni Wakristo, na wao daima
    wamekuwa wakinifundisha mimi mifano
    mizuri, na njia ya Bwana. Nilikuwa
    Mkristo miaka 3
    iliyopita, nilipokiri Yesu na kumkubali
    awe Bwana na Mwokozi wangu kupitia kwa ndugu/kaka Nicky Cruze . Nilitembea katika njia ya Bwana
    kwa miaka 2. Lakini nilipoanza High
    School, nilianza kuasi na kuacha njia
    ya Bwana. Nilikuwa muasi kwa wazazi
    wangu na nikajitumbukiza kwenye
    madawa ya kulevya. Rafiki zangu walinifundisha kufanya mambo hayo.
    Mimi nilifikiri bado nilikuwa Mkristo, na
    kwamba naweza kuwaleta
    marafiki zangu kuwa Wakristo. Lakini
    badala yake, walinivuta nyuma katika
    ulimwengu. Ndivyo nikazidi kuwa muasi hata kwa
    wazazi wangu, na wao walidhani ilikuwa
    tu kitu cha
    kwawaida vijana hupitia. Lakini kwa
    kweli, ilikuwa ni madawa ya kulevya
    yaliyofanya mimi kufanya hivyo. Roho za uovu ziliingia
    ndani yangu, ilikuwa ndio wakati mimi
    nilikuwa muasi
    kwao. Walikuwa wakali juu yangu,
    hawakuniruhusu kwenda nje mahali
    popote, hata kutumia muda wa usiku nikiwa katika nyumba ya
    rafiki. siku zote nilifanya vitu kwa ujanja
    au nyuma ya
    migongo yao. Nilitoroka shule, ilikuwa ni
    vigumu hata kwenda shule, ilimradi tu
    kuendeleza tabia yangu. Nilikuwa katika hatua
    mbaya ya kupata ulevi wa madawa
    (addiction ), lakini Bwana
    aliniondoa nje ya yote hayo.
    Kama nilivyosema, mimi nilikuwa
    Mkristo. Ushahidi wangu ulianzia mei 2, 1997. Mimi
    nilikuwa na rafiki, na tulikuwa marafiki
    tu, hakuna kitu zaidi ya hapo, naye alijua
    hivyo pia.
    Mimi nilifikiri nilikuwa nimemjua, lakini
    kumbe sikuwa nimejua kwa halisi alikuwa nani. Huo usiku, alinipigia na kuniuliza kama
    tunaweza kutoka pamoja.Wazazi wangu
    hawakuwa nyumbani. Walikuwa kwenye mkutano
    wa maombi , kama kila Ijumaa.
    Niliwaambia wazazi wang u kuwa nilitaka kukaa nyumbani kwa
    sababu nilijihisi mgonjwa. Page 2 Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
    aliojaliwa na Mungu Mimi nilikuwa ninawadaganya, kwa
    sababu nilikuwa na mipango ya kwenda
    nje usiku na rafiki yangu huyo tofauti, lakini wazazi wangu
    hawakuniachia kwenda kwa rafiki yangu.
    Hivyo waliniamuru kukaa nyumbani,
    walipokwenda kwenye mkutano wa
    Maombi, rafiki yangu alinipi gia. Akaniambia, "Kwa nini usitoke, kila
    mtu wakati huu anatoka?" nilijifikiria
    mwenyewe. "Sitaki kuwa mtukutu kwa wazazi wangu,
    lakini labda nikitoka kwa ujanja, wazazi
    wangu wasingekuja kujua kamwe ", na ndivyo
    nilivyofanya usiku wazazi wangu
    waliporudi nyumbani, na kulala usingizi. Nilikuwa tayari
    kuchoropoka hivyo nilimpigia rafiki
    yangu na kumwambia anisubirie katika kona ya mtaa wangu.
    Nilimwambia asipitie nyumbani kwa
    sababu sauti inaweza kuwaamsha wazazi wangu, na
    kuharibu kila kitu. Hivyo nikaweka mito chini ya blanketi na
    kuruka kupitia dirishani. Ninaishi katika
    nyumba yenye ghorofa mbili na madirisha yote
    mawili ya nyumba yangu yana nati
    inazozishikilia lakini kwa sababu wazazi wangu walikuwa
    wakiniamini, dirisha langu halikuwa na
    nati zinazoshikilia, na kwa kuwa ninaishi katika nyumba
    yenye ghorofa mbili, hivyo nikachukua
    uaminifu wao kama kigezo cha mimi kuruka kutoka juu
    na nikatua chini. Bwana alikuwa na
    mpango na kila kitu kwa sababu ningeweza hata
    kuvunjika mguu wangu, na hiyo
    ingeharibu kila kitu ambacho alipanga kwa ajili yangu. Nikatembea
    kuelekea mtaani, na rafiki yangu
    alikuwepo tayari akinisubiri. Nilipoingia kwenye gari niliona vijana
    watatu na msichana mmoja. Nikajiwazia
    mwenyewe sitaenda kufanya chochote, nitakunywa
    sana na kutumia madawa ya kulevya, na
    kufurahi sana ila sitaweza kufanya zaidi ya hapo, lakini
    nilihofia wanaweza kuchukulia hali
    yangu hiyo kama nafasi yao kunifanyia chochote.
    Nikaingia katika gari, kisha tukaondoka.
    Kabla, wakati nilipokuwa nazungumza na rafiki yangu
    katika simu, alisema kwamba tutakuwa tukizungukazunguka mji tu. Mimi
    nikasema "sawa hiyo inaonekana kuwa
    safi", ndio maana nilikwenda. Sikudhania kuwa
    angenichukua mpaka kweye moteli.
    Lakini ndipo waliponipeleka, tulipofika walitushusha katika chumba
    chenye huduma ya kufulia ambacho ni
    cha moteli hiyo, wakatuambia tuwasubiri pale;
    wakasema wanakwenda kumchukua
    rafiki mwingine, nikasema sawa, lakini nilihisi walikwenda kupanga
    chumba.Waliporudi kutuchukua
    ,walitupeleka katika hicho chumba. Wakasema, "msijali,
    wekeni imani yenu kwetu Sisi hatuta
    kwenda kufanya chochote!, Tunakwenda kumsubiri rafiki
    yetu mwingine aje, na kisha tutaondoka
    wote kwa pamoja "Kwa hiyo mimi nikaweka imani
    yangu kwa rafiki zangu, mimi nilidhani
    kamwe wasingeweza kunidhuru, lakini kwa kweli
    sikuwa nimefahamu marafiki zangu
    walikuwa ni watu wa namna gani. Mara ya kwanza,
    tulikuwa tukizungumza tu, hivyo
    nikasema, "wakati sisi tunawasubiri, kwa nini tusipate kitu cha
    kunywa? "Hivyo mimi na rafiki yangu
    tukaondoka mle chumbani, na kutembelea kwenye
    mgahawa mdogo mbele ya moteli.
    Tukanunua sprite tatu na kisha tukarudi chumbani. Wakaanza
    kumimina Sprite katika vikombe.
    Hawakuleta mfuko au kitu chochote kwamba kinachoonekana
    kinatuhuma, kwamba kingenifanya
    niwaze kuwa wanataka kuweka kitu chenye madhara
    katika kinywaji changu au kunifanyia
    chochote. ilionekana hakuna hatia yeyote
    Nilikwenda chooni kurekebisha nywele
    zangu na kufanya mambo ya kisichana, na nilipotoka
    kikombe changu kilikuwa tayari
    kimekwisha hudumiwa Page 3 Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
    aliojaliwa na Mungu nikaweka jojo (gum) yenye ladha ya
    strawberry kinywani mwangu, na kuanza
    kunywa kile nilichofikiri kuwa sprite yangu. Baada ya hili, sijui nini kilitokea. Lakini
    nilipopata kuona, nilihisi roho yangu
    ikitoka nje ya mwili wangu. Nilikuwa tayari katika
    hospitali; nikaona madaktari na wauguzi
    wote wamenizunguka karibu yangu. Wakati
    nilipokuwa nje ya mwili wangu, niliona
    mwili wangu juu ya kitanda. Wewe unajua jinsi
    unavyoonekana ukijiangalia katika kioo,
    unaweza kuona taswira. Lakini ile haikuwa taswira bali, niliona
    mwili wangu pale juu ya kitanda. Nilipogeuka nyuma, kulikuwa na watu 2
    wamevaa nguo nyekundu, "wakija
    tulipo" wakanishika mimi, mmoja katika kila mkono.
    Walinipeleka hadi mahali, na wakati
    nilipoangalia ni wapi ilikuwa ni mbinguni! Kitu cha kwanza
    kuona tazama ilikuwa ni ukuta mkubwa
    sana. Ulikuwa ni mweupe na umepanda juu hata usiweze
    kuona na mwisho wake, katikati ya ukuta
    ulikuwepo mlango, mlango mrefu, lakini ulikuwa
    umefungwa. Katika Agano la Kale, Musa
    anaongea kwa habari ya hema na anaeleza sifa zake.
    Nami nilikumbuka hili, na nikaona kuta
    zake zinafanana na jengo hilo. Pembeni mwa mlango,
    kulikuwa na kiti kikubwa, na kulikuwa na
    kiti kidogo katika mkono wa kuume. Navyo
    vilionekana vimeundwa kwa dhahabu ,
    na upande wangu mimi wa kuume ulikuwa ni mlango mkubwa
    mweusi, palionekana ni giza kuzunguka
    eneo lile lote lakini nilifahamu kwa sababu ya kitasa.
    Ulikuwa ni mlango mbaya. Upande
    wangu wa kushoto ilikuwa ni paradiso, kulikuwa na miti,
    maporomoko ya maji safi ,ilikuwa ni
    sehehmu nzuri sana yenye amani ila hapakuwa na mtu. Nikaangalia nikamuona Baba mbele
    yangu, sikuwa nimeona sura yake, kwa
    sababu ya utukufu wake, ulikuwa mkubwa, unaangaza
    sana, uliangaza mbingu yote.Utukufu
    wake unafanya kila kitu kuangaza. Hakukuwa na jua, mwezi,
    nyota, yeye ndiye alikuwa mwanga.
    Niliweza kuona mwili wake, mwili wake ulikuwa pamoja
    na wa mwana, walikuwa kila mmoja
    ndani ya mwenzie, walikuwa pamoja, unaweza
    kuona muachano wa miili yao, lakini
    walikuwa pamoja kila mmoja ndani ya mwenzie, walikuwa
    pamoja. Pembeni mwao kulikuwa na
    malaika wawili Gabrieli na Mikaeli. Sababu ya mimi
    kujua majina yao ni kwa sababu
    yaliandikwa kwenye paji la nyuso zao kwa Dhahabu. Nilipokuwa
    mbele ya Baba, nilijiona mchafu!
    nilianguka kwa magoti nikaanza kulia. Nilikuwa
    najionea aibu, Ijapokuwa nilikuwa
    naweza kuona nyuso zao, sikutaka kuwaangalia, kwa sababu
    nilijionea aibu mwenyewe kwa jinsi
    nilivyokuwa mchafu. Nilipokuwa mbele ya Bwana
    alinionyesha mkanda/picha nzima ya
    maisha yangu kuanzia mwanzo mpaka sasa. Akaniambia kitu
    cha msingi ni vile ambavyo nilifanya
    baada ya kuokoka. Nilikuwa nawaambia marafiki zangu
    kuwa mimi ni mkristo, lakini kiukweli
    sikuwa naonyesha matunda yangu. Akaniambia kuwa
    ilinipasa niende kuzimu. Malaika Gabriel
    akaja na akanishika katika mkono wangu. Akanipeleka katika
    mlango ule mweusi mbaya ambao
    nilikuwa sitaki hata kuuangalia. Nilijitahidi kujizuia, lakini
    nilikuwa katika roho, na tukapita
    mlangoni, nilipokuwa upande mwingine wa mlango, ilikuwa ni
    giza kila upande. Sikuweza hata kujiona
    mwenyewe. Kisha tukaanza kuanguka Haraka sana
    kama wimbi la ufukweni (roller
    coaster).Nilipokuwa nikidondoka chini palikuwa panazidi
    kuwa na joto zaidi. Nikafunga macho
    yangu; Sikutaka kuona mahali tulipokuwa. Page 4 Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
    aliojaliwa na Mungu Tulipoacha kudondoka, nilifungua
    macho yangu, na nilikuwa nimesimama
    kwenye barabara kubwa. Sikuwa nimefahamu inaelekea
    wapi, lakini kitu cha kwanza ambacho
    nilihisi ilikuwa na kiu. Nilikuwa na kiu sana! Nikawa
    naendelea kumsisitiza malaika "ninakiu,
    ninakiu" Lakini ilikuwa ni kama hakuwa ananisikia.
    Nikaanza kulia, na machozi yangu
    yalipodondoka chini kwenye mashavu yangu, yalipotea
    kabisa kama mvuke. Kulikuwa na harufu
    ya Sulphur, kama tairi ikichomwa. Nilijitahidi kuziba pua ,
    lakini hiyo ndiyo iliongeza harufu. Hisia
    zangu zote tano zilifanya kazi kwa nguvu sana.
    Nilipokuwa najitahidi kujifunika
    mwenyewe, ndivyo nilivyozidi kunusa harufu ya sulfur zaidi.
    Pia, vinyweleo vyangu katika mikono
    vilipotea. Nilihisi joto lote, kulikuwa na joto sana. Nilipoanza kutazama mahali pale,
    Niliona watu wakiteswa vibaya sana na
    mapepo. Kulikuwa na msichana pale anaumia sana, pepo
    lilikuwa likimtesa. Hili pepo lilikuwa
    likimkata kichwa chake kwa mkuki mrefu, na likimchomachoma
    kila sehemu. Halikujali. Kwenye macho,
    kwenye mwili, kwenye mikono, halikujali. kisha
    linarudisha kichwa chake tena na
    kumchoma kila sehemu. Alikuwa akilia kwa sauti ya kilio kikuu
    cha huzuni. Kisha tena nikaona pepo jingine, hili
    pepo lilikuwa likimtesa kijana wa kiume
    mdogo mwenye umri kati ya miaka 21-23. Huyu kijana
    alikuwa na mnyororo kwenye shingo
    yake, na alikuwa amesimama mbele ya shimo lenye moto.
    Hili pepo lilimchoma kwa mkuki mrefu
    kila sehemu ya mwili wake, kwenye macho, kila sehemu.
    Kisha pepo linamvuta kwa nywele zake
    kijana na kwa mnyororo wake na kumtupia shimoni,
    kisha linamchukua tena na kuanza
    kumtesa na kumtesa. Hii iliendelea hivi wakati wote, na kila
    alipokuwa akiingia ndani ya shimo hilo,
    nilikuwa sisikii kilio chake, Lakini pepo lilipokuwa
    likimtoa mle shimoni ndipo nilisikia kilio
    kikuu sana cha uchungu. Nilijitahidi kuziba masikio
    yangu kwa sababu sauti ilikuwa
    inaogopesha sana, lakini nilikuwa namsikia. Masikio yangu
    yalikuwa na nguvu ya kusikia zaidi. Niliangalia pepo jingine, hili pepo
    lilikuwa ni baya, na mengine yale mawili
    yalikuwa mabaya lakini hili lilikuwa baya zaidi ya yale
    mengine. Mfano wake lilikuwa na sura
    na tabia ya wanyama mbalimbali; siwezi hata
    kusimulia kwa maneno. Lilikuwa
    likizunguka na kuwatishia watu, na watu walikuwa wakiogopa
    sana. Kisha nikaona pepo jingine, lakini
    hili pepo lilikuwa lina sura nzuri kama ya malaika wa
    Mungu, lakini sivyo.Tofauti niliyoiona
    kati ya malaika wa Mungu na mapepo ni kuwa mapepo
    hayakuwa na majina yaliyoandikwa
    katika paji ya nyuso zao kwa dhahabu, lakini malaika wa Mungu
    walikuwa na majina katika nyuso. Kisha nikamuangalia malaika Gabrieli,
    na alikuwa akiangalia juu. Nadhani
    alikuwa hapendi kuona wengine wanavyoteswa. Nikafikiri
    moyoni mwangu, "kwa nini bado yuko
    mahali hapa? Je , sitakiwi kuwepo mahali hapa na
    kusubiri zamu yangu ya kuteswa?
    Nilikuwa na kiu. Nikalia kwa malaika, "Nina kiu, nina kiu," Nafikiri
    alinisikia kwa sababu alitazama chini na
    kuniangalia akasema, "Bwana anakwenda kukupa
    nafasi moja nyingine." Mara aliposema hivyo, kiu yangu yote
    ikaondoka, uchungu wangu, maumivu
    yangu, yote yakaondoka . Nikajihisi nina amani.
    Kisha akauchukua mkono wangu,
    tulikuwa karibu na kuondoka, Kisha nikasikia sauti yangu
    ikiitwa , "Jennifer, Nisaidie mimi,
    nisaidie !" Niliangalia Page 5 Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
    aliojaliwa na Mungu chini. Nilihitaji kujua alikuwa ni nani,
    Lakini nilipojaribu moto uliwaziba sura
    zao sikuweza kuwajua. Ilikuwa ni sauti ya msichana.
    Niliweza kuona mikono yake ikiwa
    imetokeza, alitaka nimsaidie. Nilikuwa natamani kumsaidia
    kweli, Nilipojaribu, nilishindwa , kwa
    sababu mikono yangu haikuweza kumshika, Nilitaka
    kumsaidia kabisa lakini unaweza kuona
    hakuwa na matumaini tena. Sikuweza kumsaidia. Na kisha nikaangalia kote nikaona rafiki
    zangu, watu ninao wafahamu, na watu
    wengine. Walionekana kama ninawafahamu lakini
    sikuweza kuwatambua walikuwa ni
    akina nani. Sikufahamu maisha yao, lakini
    nilipowaona marafiki zangu wa shuleni
    pale, iliniumiza sana!. Nikajiwazia mimi mwenyewe, "Labda
    kwa sababu ya ushuhuda mbovu
    niliowaonyesha, wa kusema kuwa nilikuwa mkristo lakini
    nikarudi nyuma, ndicho kilichowafanya
    nao wasipende kumjua Mungu, na wakaamua
    kumuacha. Labda ilikuwa ni mimi
    niliyewaleta pale".Hivyo ndivyo nilifikiri. Niliona katika kuzimu
    hakuna muda, hakuna wakati uliopita,
    wakati wa sasa, wakati ujao, kila kitu ni vile vile, na
    imewapasa kwenda pale. Lakini kama
    nilivyosema mwanzoni sipendi kuweka msingi
    wowote, Lakini hicho ndicho
    nilichokiona. Watu niliowaona pale bado wanaishi hivi leo. Malaika akanichukua tena na kunipeleka
    katika uwepo wa Mungu. Nilipokuwa
    nimesimama mbele zake, nilipiga magoti kisha
    nikaanza kulia na kulia. Nilikuwa bado
    siwezi kumtazama kwenye uso wake, kwa sababu nilikuwa
    ni mwenye kujionea haya. Lakini Yesu
    pamoja na sauti yake hiyo nzuri akasema, "Nakupenda"
    Upendo wake ni kama wa haki,
    Nawapenda wanaonisikia mimi. Lakini akaniambia
    amenisamehe makosa yangu yote
    nilipokuwa nimemuasi. Alinisamehe. Mungu akaniangalia kisha akanionyesha
    mambo mengi yajayo. Akanionyesha
    Ulimwengu yaani dunia. Kuzunguka Dunia niliona kitu
    kama kilaini, kama tabaka la ozone,
    lilikuwa limezunguka ulimwengu mzima, lilikuwa ni laini sana,
    nilitamani hata kushika. Niliposhika
    nilijua alikuwa ni Roho Mtakatifu, kwa sababu ilinibatiza
    na kuanza kuongea kwa lugha nyingine. Wakati huo, Nilitazama juu na kuona
    roho chafu nyingi zikitoka nje yangu.
    Nilipokuwa nikijiachia na kutumia madawa, ambayo
    yaliingia mpaka kwenye fikra zangu na
    kuruhusu mlango, wa roho hizi chafu kuja na
    kukaa ndani yangu. Roho hizi chafu
    zilinitesa. Kiasi kwamba nilivyokuwa nikifanya haikuwa ni mimi
    halisi, ilikuwa ni zile roho chafu ndani
    yangu. Neno la Mungu linasema kwamba nyumba yako
    inapokuwa imesafishwa roho chafu
    zitajaribu kuja tena kwa kuleta wengine 7. Nyumba yangu
    ilisafishwa mara nilipokuwa nimeokoka.
    Na niliziona hizi roho chafu nilipokuwa nikibatizwa
    na Roho mtakatifu, walikuwa wako 7, na
    hizo 7 zilikuwa na wengine 7, na sikuweza hata
    kuzihesabu zote! Lakini Bwana
    alinisafisha na roho zote chafu. Pia alinionyesha kwa habari ya mambo
    yajayo, akanionyesha Dunia na mambo
    ambayo yatakuja kutokea, matukio yakakayokuja kutukia.
    Maono niliyopewa ni kuanzia sasa
    mpaka wakati wa unyakuo. Hakunionyesha unyakuo, lakini
    alinionyesha mambo yatakayotokea
    kabla ya unyakuo. Kila siku ilisogea kidigokidogo, na
    ninakuambia kuwa unyakuo umekaribia!
    Unatakiwa Page 6 Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
    aliojaliwa na Mungu kujichunguza mwenyewe, maisha yako,
    na kujiuliza " Je niko tayari kwenda na
    Bwana?" Bwana alinionyesha hili, lakini aliniambia
    nisimueleze mtu yeyote, lakini kusubiri
    na kuona kuwa mwisho umekaribia, sipendi nimjaribu
    Mungu, ndio maana sitapenda
    kuwaambia kile nilicho kiona. Lakini nawaeleza na
    kuwatahadharisha kuwa unyakuo
    umekaribia. Ninasoma katika Joel 2:28, ni moja kati ya unabii wa mwisho; kila kitu kingine
    kimekwisha timia. Unabii huu ndio wenyewe tu
    ambao haujatimia na ninakueleza wewe
    kuwa unabii huu unaendelea kutimia, Vijana wengi hivi
    sasa wanatokeza na kuhubiri neno la
    Mungu. Shetani anataka kufanya jeshi la vijana lakini
    Bwana atakuwa na nguvu zaidi yake. Na
    kama kweli ukimkubali na ukipenda kumtumikia,
    Bwana atakupa uwezo wa kumshinda
    shetani, ili ukahubiri neno la Mungu Ulimwengu wote, Kama
    jinsi alivyoamuru katika Biblia. Aliniambia mimi kuwa nina mpango, na
    mpango huu ni kuwaeleza vijana wote
    kuhusu maono yangu. Hata kama sitataka kufanya hivi,
    ni amri ambayo Mungu alinipa, na
    nitaimaliza. Niliporudia mwili wangu, niliamka na
    kujikuta nikiwa hospitali.Niliangalia huku
    na huko na kuona sindano katika mikono yangu,vitu
    vikiangalia moyo wangu, mashine. Mara
    wazazi wangu wakaingia ndani nikaanza kulia.
    Walionekana ni wenye ghadhabu, lakini
    Bwana akaniambia niwaeleze kila kitu na hicho ndicho
    nilichofanya. Niliwaeleza kila kitu. Nesi alipoingia ndani ya chumba,
    wakanieleza kuwa walikuwa wanahofia
    sana kwa habari yangu. walisema nilikuwa naondoka na
    kurudi. Nilikuwa sijitambui halafu mara
    najitambua tena. Hii ilitokea mara tatu. Wanasema kuna
    wakati fulani katika matukio hayo
    matatu sikutaka kurudi kabisa, wakawa na hofu sana kwa
    habari yangu. Wanasema moshi ulikuwa
    ukitoka katika kinywa changu na kutoa maneno
    yasoyoweza kueleweka. Pia usiku ule, mama yangu alikuwa na
    ndoto mbaya. Kimbwa kidogo ambacho
    nilikuwa nikilala nacho kilikwenda kwenye chumba cha
    wazazi wangu na kukwarua mikono ya
    mama yangu na kujaribu kumuamsha. Alipoamka,
    alikwenda kwenye chumba changu na
    kuona mito ikiwa imewekwa vizuri na kufunikwa. Akafikiri
    nilikuwepo akarudi tena kwenye chumba
    chake. Kisha akaangalia dirishani akaona taa za polisi
    nje ya dirisha zikimulika. Alipochungulia
    dirishani, akaona polisi wakija kwenye Nyumba
    yetu, hivyo akamuamsha baba yangu.
    Polisi akawaambia wapige simu kituo cha polisi ili kupata
    taarifa zaidi kuhusu mimi. Wazazi wangu
    ndipo walipofahamu kuwa nimedhurika zaidi
    na sumu na kwamba niko hospitalini.
    Wakati huo Bwana akaongea na baba yangu na
    kumwambia asiogope, Nilitumia muda
    wa siku tatu nikiwa hospitali. Wiki moja baadae tuliongea na
    maaskari, na wakatusimulia kwa habari
    ya usiku ule. Wakasema Yule msichana niliyekuwa nae ,
    hakutakiwa kutoka nje pia, na baba yake
    aliogopa sana. akawa akimtafuta, akizunguka , lakini
    hakuweza kumuona. Hivyo akaenda
    katika kituo cha polisi, na akatangaza aina ya gari ambayo rafiki
    yangu alikuwa akiendesha kwa wote
    wanaofanya patrol. Afisa fulani aliyekuwa hayuko kwenye
    zamu, alikuwa akipita mtaani
    kuzungukia wauzaji wa magari, alikuwa akitafuta gari ya
    kununua iliyotumika. Akawa ameona
    gari ya rafiki yangu akawa amewaita polisi. Polisi
    walipokwenda kuchunguza, gari ya rafiki
    yangu ilikuwa Page 7 Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
    aliojaliwa na Mungu imeegesha mahali pengine, hivyo
    hawakujua mahali gani alikuwepo binti
    huyo.Tulikuwa kwenye ghorofa ya pili katika chumba
    kilicho kwenye kona. Polisi walitaka
    kuanza kukagua katika chumba kile, na washuke chini
    wakimuuliza kila mmoja ni nani mwenye
    gari ile iliyopaki pale nje. Walikuwa hawamtafuti Yule
    msichana; walikuwa wakimtafuta mmiliki
    wa gari ile. Walipogonga mlangoni petu, walifungua
    mlango na kuniona mimi niko chini.Lakini wakaondoka. Niliowaita rafiki zangu
    walidhani kuwa Polisi wameondoka tu ,
    kumbe waliondoka kuchukua gari ya wagonjwa Ambulance.
    Mara tu polisi wengine wakaingia ili
    kuona nini kinaen delea.Walipofungua mlango, muda ule
    sasa, rafiki yangu yule niliyekuwa
    nikimuongelea, Yule niliyemuamini alikuwa katika pointi ya
    kunibaka. Lakini Bwana akatumia polisi
    ili kuzuia kitendo kile, na hawakunifanya
    chochote. Hicho ndicho nacho mshukuru
    Bwana, kwa kuwa alikuwa mwenye Rehema kwangu. Na maombi ya wazazi wangu, naongea
    na nyie wazazi. Msiache kamwe kuomba
    kwa ajili ya watoto wenu. kama hawatembei katika
    njia ya Bwana, endeleeni kuwaombea,
    msikate tamaa. Wazazi wangu hawakukata tamaa, na
    angalia mahali nilipo hivi sasa,
    ninahubiri neno la Mungu; nikiwaambia vijana waje kumtumikia
    Mungu, kwa sababu wanamuhitaji. Ningependa kutoa ujumbe kwa vijana
    wote, ningependa wewe uwaze kwa
    habari yako, na ujichunguze mwenyewe. Fikiria, kwa nini
    ujali kile mtu yeyote anasema kwa ajili
    yako wewe. Nimekuwa nikifikiri kile Watu wamekuwa
    wakisema kwa habari yangu mimi lakini
    sasa nimegundua hata hawanijali.
    Hawatakuwa pale Bwana atakapokuwa
    mbele yangu. Nakumbuka nilipokuwa mbele ya Bwana, marafiki
    zangu hawakuwepo pale
    kunisaidia,familia yangu haikuwepo pale kunisaidia,mchungaji
    wangu hakuwepo pale kunisaidia,kanisa
    halikuwepo pale kunisaidia. Nilikuwepo pale peke yangu,
    na nilihitajika kujitetea
    mwenyewe.Mbele zake huwezi kuona uongo, kwa sababu ni mtakatifu
    sana. Na nilipokuwa pale, sikujisikia
    kuwa mimi ni wa pale, kwa sababu nilikuwa katika dhambi
    na mbinguni ni patakatifu. Ninakueleza wewe hivi leo kama
    haujampokea Bwana Yesu, basi mpokee
    hivi leo.Huu ni uamuzi wa Busara sana katika maisha
    yako yote. Sikuelezi haya yote ili
    kuwaogopesha ili muingie mbinguni, lakini ili muweze
    kuona rehema, upendo alionao kwetu
    sisi. Yeye Baba, alimtuma mwanae wa pekee afe kwa
    ajili yetu. Hivyo kila tone la damu
    alilomwaga linasafisha dhambi zetu zote. Kama unataka
    kumpokea Bwana, ni uamuzi muhimu
    sana katika maisha yako. Njoo kwa Bwana, Usijali nini kile mtu
    mwingine anasema kwa habari yako. Kama unataka kumtumikia Bwana ,basi
    fanya kwa moyo wako wote , usiiseme tu
    kwa mdomo wako,sema kwa moyo wako na fikra
    zako.Usihofu kwa habari ya maisha ya
    baadae,usihofu kwa ajili ya leo, huwezi jua ni lini utakwenda
    kufa. Nina umri wa miaka 15 tu na katika
    fikra zangu sikuwa nimewaza kuwa nitakufa katika
    umri wa miaka 15, sikuwahi kuwaza hivi. Unatakiwa kufikiri pia kuhusu hilo.
    Maisha yangu si yangu,maisha yako si
    yako,tumekopa maisha yetu, maisha yetu ni ya Mungu.
    Huwa tunapuuzia sana kuhusu hili na
    hatujali, tunarudi katika ulimwengu, na kufanya mambo ya
    ulimwengu. Ulimwengu una mambo
    mengi ya kukupa, Page 8 Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
    aliojaliwa na Mungu lakini kumbuka Mungu anamambo
    mengi pia ya kukupa. Ulimwengu una
    kuzimu na mauti, lakini Mungu anao uzima wa milele.
    Maisha ya milele ni milele. Hivi sasa kama unataka kumkubali
    Bwana, Ninataka uinamishe kichwa
    chako na kufunga macho yako, nifuatishe maneno haya "Bwana Mungu, katika jina la Yesu,
    nakuja kwako leo, O Bwana Mungu wangu kwa wakati huu
    nakukubali Wewe kama Mwokozi
    wangu, nataka uje katika maisha yangu. Kama dada
    alivyosema kuhusu ushahidi wake
    kwamba Kuzimu ni halisi, yeye alikuwa huko. Bwana Mungu, sitaki
    kwenda huko, sitaki hata kufikiri kwa
    habari ya kwenda huko. Bwana Mungu ninaomba
    unisamehe dhambi zangu zote
    nilizozifanya. Nisamehe kwa kila kitu ambacho nimekuwa
    nikifanya. Kila dhambi ndogo ya siri,
    Bwana Mungu wangu, mimi nazitangaza mbele yako, hivyo
    tafadhali nisamehe kwa kila kitu. Bwana
    Mungu naamini kwamba Wewe alikufa msalabani na
    kwamba ulifufuka kutoka katika wafu.
    Naamini kwamba utakuja moyoni mwangu na kutawala
    moyo wangu, na kuwa moyoni wangu.
    Nitasoma neno lako, na nitakuwa zaidi katika Neno.
    Nitakwenda Kanisani, Bwana Mungu
    wangu kwa sababu mimi najua Wewe unapatikana pale
    Kanisani. wewe umesema kwamba watu
    wawili au watatu wakikusanyika pamoja, Wewe
    hukokatikati yao. Bwana, Mungu wangu
    nataka kuwepo ambapo Wewe upo. Naomba haya yote katika
    jina la Yesu, Amina " Kama umeomba sala hii, ningependa
    kukukaribisha katika ufalme wa
    Mbinguni. Sasa una ndugu kaka na dada zako ulimwengu mzima.
    Hii ndio uamuzi wa muhimu sana katika
    maisha yako kati ya maamuzi ambayo ulishawahi kufanya
    , hivyo usipuuzie. Usirudi tena kwenye
    ulimwengu. Ulimwengu unakuongoza kwenye mauti,
    lakini Mungu anatuongoza kwenye
    uzima wa milele.Kila muda imekupasa uishi kana
    kwamba ni siku ya mwisho, na siku yako
    ya mwisho. Kama ushuhuda huu umegusa moyo
    wako, mpe pia rafiki yako ili kwamba
    amkubali Mungu katika moyo wake. Usiruhusu muda huu
    ukupite, huu unaweza kuwa ndio wakati
    wako wa mwisho. Kuzimu ni halisi, nilikwenda
    huko! na Jennifer Perez Ndugu aliyefasiri ufunuo huu ni Peter
    Kahale ni kijana aliyeokoka na
    anampenda Yesu na mwenye shauku ya kuhubiri injili ya
    Yesu Kristo. Simu ya Mkononi: +255-769-610460,
    +255-653-610460. Barua Pepe: kahalepeter@gmail.com

    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate