Wafilipi 2:10-11
  • MBINGUNI NA JEHANAMU: "ELFU KWA MOJA"

    Na mchungaji Park Yong Gyu www.DivineRevelations.info/SWAHILI Mnamo mwaka wa 1987, mchungaji Park
    alifariki
    kutokana na ugonjwa wa shinikizo la
    damu. Lakini kwa neema ya Mungu,
    maisha yake
    yaliongezwa kwa miaka mingine ishirini. Lakini kwa miaka minne ya kwanza kati
    ya hii miaka
    ishirini hakuweza kuongea kutokana na
    hali yake. Alikuwa na miaka takribani
    hamsini
    alipofufuliwa. Katika kifo chake Bwana alimuonyesha Mbinguni na Jehanamu. Nataka ufahamu kwamba, ukiwa
    mwenye kiburi na majivuno utajiletea laana. Nilikuwa na kanisa kubwa mno
    lenye washirika elfu tano lakini
    Mungu alinichapa kichapo kutokana na
    kiburi changu.Sasa namuogopa Mungu. Nilikuwa na mali ya takribani dola million
    mia moja hamsini. Nilikuwa na magari
    matano ya kifahari .Lakini baada ya mkasa wa kufa
    na kufufuliwa kwangu nilipeana vyote.
    Tafadhali
    kumbuka kwamba wokovu hauwezi
    kupatikana kupitia kwa mali uliyonayo ila
    ni kwa imani pekee. Na sasa nawasihi mashemasi
    wote, wazee wa kanisa na viongozi
    wengine wa makanisa
    kuwatumikia wachungaji wao kwa mioyo
    yao yote. Mnamo Desemba kumi na tisa mwaka
    wa 1987, baada ya kumaliza kula
    chakula cha mchana
    nilipokuwa napumzika, nilianza kuhisi
    uchungu mkubwa mno, ulikuwa uchungu
    nisioweza kuustahimili nami nilihisi kana kwamba
    nitakufa. Kisha nikapoteza fahamu.
    Niliamka miezi
    minne baadaye nikiwa katika hali mbaya
    sana tena mahututi, kisha Daktari
    akaniambia kwamba nitakufa. Sehemu zote za mwili wangu zilikunjana
    vibaya kutokana na kupooza kwanga. Hata jamii yangu
    haikuwaruhusu washirika wa
    kanisa langu kunitembela kutokana na
    jinsi mwili na hali yangu ilivyokuwa mbaya. Mwishowe nikafariki. Nilipofariki, niliwaona watu wawili
    wakiingia chumbani mwangu. Lakini watu hawa waliingia
    chumbani mwangu kupitia
    ukuta. Nikapiga ukulele nikauliza, "kina
    nani nyinyi? Nyumba yangu itaporomoka mkiingia jinsi
    mlivyofanya." Mmoja wao akasema, "sisi
    tu malaika tulioshuka kutoka mbinguni, tumetoka
    katika ufalme wa Mungu". Mwangaza
    mkali ulimulika kutoka kwa Malaika wale. Page 2 2 Malaika aliyekuwa mkono wangu wa
    kulia akajitambulisha hivi, "mimi
    humtekelezea Yesu kazi za ujumbe katika ufalme wake. Yesu
    aliniita akaniamauru nishuke duniani
    nije nikuchukue Mbinguni. Wewe umefariki lakini kwa
    vile jamii yako inalia kwa huzuni sana,
    Yesu anataka kukuongezea muda kidogo wa ziada wa
    kuishi duniani. Lakini kwa sasa anataka
    kukuonyesha Mbinguni na Jehanamu. Yeye
    atakuonyesha nawe utawashuhudia
    watu wa ulimwengu. Na idadi ya wale wangetokomea Jehanamu
    itapunguka, nayo idadi ya wale watakao
    enda Mbinguni itaongezeka kupitia kwa
    ushuhuda wako. Huu ndio utakuwa
    ujumbe wako. "Mungu ametuagiza tukuambie
    usichelewe kwani ukichelewa basi
    hautaweza kuzuru Mbinguni na Jehanamu". Kisha malaika aliyekuwa mkono wangu
    kulia akasema, "tangu pale ulipozaliwa
    hadi wakati ulipoaga dunia, nimekuwa nawe". Mimi
    sikuelewa alichomaanisha malaika huyo lakini sasa
    nimefahamu alikuwa malaika wangu mlinzi. Basi nikasema,
    "siwezi kwenda! Nami sitaenda! Mimi ni mchungaji! Siwezi
    kukutana na Bwana katika hali hii niliyonayo.Nataka tukutane naye
    nikiwa mtu mwenye afya. Mimi pengine nitapokea makemeo
    mengi kuliko pongezi kutoka kwa Bwana. Mimi ni mtu mwenye
    kiburi na majivuno na sasa nimelaaniwa tena ni mgonjwa.
    Nitawezaje kuingia mbinguni? naogopa
    sana.Tafadhali rudini mbinguni mumsihi Bwana
    aniponye .Kisha mtarudi mnichukue
    mbinguni kupitia kwa ndoto.Tafadhali nawasihi mniombee
    msamaha kwa Bwana kwa niaba yangu". Lakini malaika hawakuwa wakiisikia hoja
    yangu. Wakanivua nguo zangu kisha
    wakasema zilikuwa chafu mno na hazifai kuvaliwa
    mbinguni. Nao wakanivisha vazi jeupe. Wakanishika mikono yangu nasi
    tukapaa moja kwa moja hadi mbinguni. Tulipaa mawinguni na
    nilipotazama chini nikaona dunia ilikuwa ndogo.
    Wakaniacha niende karibu na njia ya dhahabu isiyokuwa na mwisho.
    Nikaona mwangaza mkali mno. Nikauliza, "mwangaza huu
    watoka wapi?" nao wakanijibu kwamba watoka mbinguni. Nikawaza, "Lo ni pakubwa mahali hapa!"
    Nikaona kikundi cha watu waliovalia mavazi meupe
    wakipaa mbele yetu. "Kina nani wale?" nikauliza. Malaika
    akajibu. "Hao ni wale waliomtumuikia
    Yesu kwa kutii na kufuata kuongozwa na Roho mtakatifu.
    Miili yao imekufa duniani. Sasa nafsi zao
    zinaelekea mbinguni". Huyo malaika mwingine
    akaendelea. "Kuna malango kumi na
    mbili mbinguni. Wakati nafsi iliyookoka inapowasili
    mbinguni, ni sharti iingie kupitia moja
    wapo ya malango Page 3 3 haya." Tulikuwa tumesimama katika
    lango la kusini lakini lilikuwa
    limefungwa. Tulipokuwa tunangoja nikamuuliza malaika. "Mbona
    lango halifunguki?" naye akanijibu "ni
    kwasababu hauuimbi wimbo wa kuabudu wa
    mbinguni." Nikamuuliza malaika,
    "nilikuwa na kiburi tena mwenye majivuno na ndio sababu ya
    mimi kulaaniwa na ugonjwa, ikiwa mimi
    sio mkakamavu wa kuziimba nyimbo za kuabudu za
    duniani, nitawezaje kuziimba nyimbo za
    kuabudu za hapa mbinguni nami sijawahi kuzisikia?" Naye malaika akanijibu, "ulivyosema ni
    kweli lakini sharti ujitayarishe kuabudu.
    Wewe ni mtu mwenye majivuno lakini jitayarishe
    kuimba." Nao malaika wakaanza kuimba
    na walipokuwa wakiimba nami pia nikaanza kuimba
    nao. Kuimba kule kukawa kawaida
    kwangu, basi tukaingia ndani. Eneo la mbinguni lilikuwa zuri ajabu
    hata siwezi kueleza kwa maneno ya
    humu duniani. Nami nikasema " Bwana! Asante Sana! Japo
    nilikuwa mwenye kiburi na majivuno na
    aliyelaaniwa kwa ugonjwa, umenileta mbinguni
    kunionyesha sehemu zake." Kisha nikasikia sauti ya Mungu,
    "mchungaji wangu mpendwa PARK
    Yong GYU", nakukaribisha. Umefanya safari ndefu sana kuja hapa." Sauti yake ilijawa na upendo tena
    ilikuwa nyororo sana. Nami nakamjibu huku nikilia kwa
    machozi, "Bwana…" wale malaika mara
    moja wakasema, "umekuwa mchungaji kwa miaka ishirini,
    kwani hauyajui maandiko", mbinguni
    hakuna machozi. Tafadhali usilie hapa"
    sikuweza hata kulia. (Ufunuo 21:4) Bwana akaniuliza maswali matano: 1. Uliutimia wakati wako kiasi gani
    kuisoma bibilia? 2. Ulitoa sadaka kiasi gani? 3. Mara ngapi umeeneza injili kwa watu? 4. Je? Ulitoa zaka ipasavyo? 5. Uliutumia mda wako kiasi gani katika
    maombi? Nikashindwa kulijibu swali la tano. Naye
    Bwana akanikemea kwa ajili ya swali
    hilo la tano. "Baada ya kuwa mchungaji wa kanisa
    kubwa ukawa mvivu wa maombi. Kuwa
    na shughuli nyingi sio udhuru kwangu!" ilinibidi
    nitubu kuhusu hili jambo baadaye.
    "Malaika hao watakuonyesha sehemu nyingi hapa
    mbinguni na pia jehanamu. Tazama jinsi
    utakavyo. Nawe utaondoka baada ya kuzishuhudia
    sehemu tofaui za mbinguni na pia
    jehanamu." Lakini Bwana hakuniruhusu niutazame uso wake. Page 4 4 Malaiaka wakanipeleka sehemu tatu
    tofauti za mbinguni. Sehemu ya kwanza, niliwaona watoto
    wadogo wakiishi pamoja. Sehemu ya pili paliishi watu
    wazima. Sehemu ya tatu palikuwa na nafsi ambazo ziliingia
    mbinguni chupuchupu. Hata kama waliwahi
    kuingia mbinguni, wao waliingia kwa njia ya aibu. Watu wengi waliniuliza umri wa wale
    watoto. Walikuwa kana kwamba waliokuwa shule ya chekechea.
    Kila mtoto alikuwa na malaika wake
    mtoto wa kuandamana naye. Mbinguni nafsi nyingi zitakuwa na
    makao yao binafsi. (Yohana 14:2) Lakini kuna wale amabao hawakuwa na
    makao. Hii nitafafanua baadaye. Tena
    wale watoto hawakuwa na makao yao. Nami
    nikauliza, " hawa watoto pia ni nafsi
    ,mbona hawana makao?" Malaika akanijibu, "hata jinsi duniani
    watu huhitaji vifaa vya kujengea
    nyumba , hali ni hiyo hiyo hapa mbinguni. Wakati mtu
    anapoihudumia kanisa na watu wengine
    kwa utiifu katika Bwana, haya matendo mema ndio huwa
    vifaa vya kumjengea mtu nyumba hapa
    mbinguni". Wakati vifaa hivi vinapotolewa basi
    malaika waliopewa jukumu la
    kumjengea mtu nyumba huanza kazi ya ujenzi hapa mbinguni.
    Kwa vile hawa watoto walikuwa chini ya
    umri wa kuwajibika, basi hawangeweza
    kujilimbikizia au kupata vifaa vya
    kujijengea nyumba hapa mbinguni. Kwa ufupi, hawakuwa na
    muda wala nafasi ya kujikusanyia vifaa
    vya kujengea nyumba na ndio maana hawana makao." Nami nikanedelea kuuliza maswali,
    "nitafanyaje nikiwa duniani ili nipate
    vifaa vingi vya kuijengea nyumba yangu hapa
    mbinguni?" nao wakanijibu, "kuna vitu
    saba impasavyo mtu kuvifanya ili kupata na kujilimbikzia vifaa
    vya kujengea nyumba." 1. Kwanza ni malimbikizi yao ya sifa na
    kumuabudu Mungu. 2. Pili ni wakati wautumiao kuisoma
    bibilia. 3. Tatu ni wakati wautumiao kuomba. 4. Nne ni wakati wautumiao kueneza
    injili. 5. Tano ni sadaka wazitoazo kwa
    Bwana. 6. Sita ni utiifu katika kutoa zaka. 7. Saba na ya mwisho ni ule wakati mtu
    autumiao kuitumikia kanisa kwa njia
    yoyote ile. Haya ndiyo matendo ya utiifu
    yamwezeshayo mtu kukusanya vifaa vya
    kujengea nyumba zao huko mbinguni. Page 5 5 Palikuwa na watu wengi amabao
    hawakuwa na nyumba huko mbinguni
    .Wengi wa wale ambao hawakuwa na makao huko
    mbinguni ni wachungaji, ,mashemasi na
    hata wazee wa kanisa. Nami nikauliza kwa udadisi,
    "Basi hawa watoto wanaishi wapi?" Malaika akanijibu, "wao huishi hapa". Nilipotazama hapa na pale, niliona wamekusanyika pote kwenye bustani la
    maua. Bustani hilo la maua lilikuwa zuri ajabu
    na lilikuwa na harufu nzuri sana
    isiyopatikana humu duniani. Eneo lile lilikuwa nzuri kushinda jinsi ninavyoweza kueleza kwa maneno
    yangu binafsi. Mahali pa pili palikuwa na watu wazima waliokuwa waaminifu. Kuna tofauti kati
    ya wokovu na kutuzwa. Mahali hapo
    palikuwa na nyumba nyingi sana. Nazo nyumba hizo
    zilijengwa kwa vito vizuri sana pamoja
    na mawe ya thamani ambayo ni adimu mno. Baadhi
    ya makao yale yalikuwa marefu sana
    kama zile nyumba ndefu za gorofa humu duniani.
    Wale watu amabo walimtumikia Bwana
    kwa uaminifu wakiwa humu duniani walikuwa na
    nyumba zilizojengwa kwa vito vizuri
    pamoja na mawe ya thamani ambayo ni nadra sana. Katika mahali hapa, watu walionekana
    kana kwamba wana umri wa miaka ishirini hadi thelathini. Hapakuwa
    na wake au waume kulingana na jinsia. Hapakuwa na watu wagonjwa,
    wazee au viwete. Niliwahi kumjua mzee mmoja aitwaye
    Oh Im Myung. Alifariki akiwa na miaka sitini na tano. Alikuwa mtu mfupi
    mno, urefu wake ulikuwa kama wa watoto wa darasa la pili hivi.
    Aliteseka sana kutokana na ugonjwa wa nyongea lakini yeye alibobea sana
    katika mambo ya bibilia.Alikuwa
    ameaandika mafafanuzi mengi sana ya bibilia .Nilikutana naye
    mbinguni naye alikuwa buheri wa afya .
    Mbinguni ni mahali pazuri sana. Nina matarajio
    mengi sana. Tafadhali aminini yale
    ninayowaambia wapendwa wenzangu. Mahali pa tatu palikuwa na wale ambao
    waliokolewa kwa njia ya aibu.
    (Wakorintho 3:15). Kijiji hiki kilikuwa kikubwa sana, na kilikuwa ni
    kikubwa zaidi ya mahali pale pa pili
    ambapo nyumba zilijengwa kwa vito vya thamani na
    mawe ya thamani yaliyo nadra. Page 6 6 Nilifika mahali hapa kwa kasi sana
    nikiwa nimeabiri gari la farasi wa
    dhahabu.Palikuwa mbali sana na sehemu nzuri za mbinguni
    ambazo niliziona hapo awali. Nikawauliza wale malaika, "naona
    jangwa kubwa mno na viwanja, mbona
    sioni nyumba?" malaika akanijibu, "kile unachotazama ni
    makao". Niliona nyumba kubwa sana tena pana
    ambazo zilinikumbusha nyumba za kuku au mabohari. Makayo
    haya hayakuwa mazuri bali yalikuwa chakavu. Kijiji hiki na
    nyumba zile zilikuwa za zile nafsi ambazo ziliokolewa kwa aibu.
    Palikuwa na nyumba kubwa tena nyingi sana ambazo
    ziliikuwa chakavu. Mji huu ni mkubwa mara kadhaa zaidi ya pahali
    ambapo nafsi zilizotuzwa zinapokaa. Malaika akasema, " je ? Waona nyumba
    mbili kubwa zilizoko kushoto na kulia
    kwako?" nami nikamjibu "naam nimeziona". Malaika akasema kwamba alitaka
    kunionyesha nyumba hizo mbili
    haswa.Akasema "nyumba iliyopo mkono wa kulia ni ya wale
    waliokuwa wachungaji duniani. Nayo
    iliyoko mkono wa kushoto ni za wazee wa kanisa. Tulipofika mbele ya nyumba zile nikaona
    zilikuwa kubwa ajabu. Nami nikabaki
    kinywa wazi!. Tulipofungua mlango na kuingia
    matarajio yangu yalikuwa ni kama
    tunaingia nyumba ya kuku. Badala ya kuona maelfu ya kuku mahali
    pale, niliona nafsi . Malaika akanishauri
    nitazame kwa makini kwani nitaweza kuwatambua
    wachungaji maarufu katika historia.
    Ilikuwa ukweli. Niliwatambua wachungaji wengi katika
    historia. Niliwahi kumuona mchungaji
    mmoja haswa,nami nikamuuliza malaika,
    "namjua mchungaji huyo amabaye ni
    mkorea, najua jinsi alivyo kuwa maarufu na ile kazi
    amemfanyia Bwana . Mbona yuko hapa?
    Sielewi!" Nikauliza kwa udadisi, "hii ilifanyikaje?
    Mbona hakuwa na vifaa vya kumjengea nyumba?" Malaika akanijibu,
    "wakati alipokuwa akifanya kazi yake ya uchungaji, alipenda
    kusifiwa sana na watu. Alipenda kuheshimiwa sana. Pia alipenda
    kutumikiwa. Hakuwa na kujitolea wala utumishi kwa upande wake." Huyu
    mchungaji aliheshimika sana Korea tena alikuwa bingwa mkubwa katika
    historia ya kanisa la Korea. Lakini hakutunukiwa chochote! Page 7 7 Enyi wachungaji mlio huko nje, tafadhali
    sikieni. Inawapasa kuwaongoza watu
    zaidi ya ile ibada ya jumapili kanisani. Sharti
    uwatembelee majumbani mwao. Sharti
    uwatunze masikini, viwete na wazee. Wachungaji waliotumikia bila ya
    kujitolea maisha yao, ambao walipenda
    kutukuzwa hawana zawadi yoyote mbinguni. Baada ya Mimi kuvishuhudia vitu hivi
    mbinguni na kurudi hapa ulimwenguni,
    nilipena vyote nilivyokuwa navyo vikiwemo magari
    yangu ya kifahari. Maisha yetu ni ya
    muda mfupi tu. Kataika bibilia maisha ya mwanadamu ni
    takribani miaka sabini hadi themanini.
    Lakini ni Mungu pekee ajuaye atakapofariki mtu.
    Yeyote aweza kufa kabla ya miaka
    sabini au themanini. Niliamua kupena vyote
    nilivykuwa navyo hata nguo zangu. Wale niliowaona wamepokea wokovu
    kwa aibu walikuwa wachungaji,wazee
    wa kanisa,mashemasi na hata waumini wa
    kawaida.Palikuwa na umati wa wazee
    wa kanisa na mashemasi katika nyumba hizi chakavu.
    Lakini hata hivyo, ni bora kuliko
    jehanamu. Licha ya hayo, mtu gani angependa kuingia
    mbinguni kwa njia hii?. Mimi sitaishia
    mahali pale pa aibu. Hata nguo zao zilikuwa chakavu. Ni masharti yapi yampasayo mkristu
    kufuata ili apate makao yanayopendeza
    mbinguni? Kwanza ni sharti tueneze injili kwa watu
    wengi kabisa iwezekanavyo. Nasi
    tutaieneza injili vipi? Malaika akaniambia, "hebu dhania
    kwamba pana mtu asiyekuwa muumini
    au asiyeokoka ambaye hamjui Bwana. Wakati
    uamuapo kumuenezea injili mtu huyo,
    basi vifaa vya kukujengea nyumba mbinguni
    vitatolewa. Unapozizdi kuuombea
    wokovu wao, basi vifaa zaidi hutolewa kwa ajili yako. Lazima
    uendelee kuwatazama na kuwaanagali,
    kuwatembelea na kuwaeleza kuhusu injili. Hii
    itakuongezea vifaa zaidi kwa ujenzi wa nyumba yako. Ikiwa mtu atasema hawezi fika kanisani
    kwa sababu hana nguo nzuri basi lazima umpatie. Ikiwa
    mtu atasema hana miwani ya kusomea, basi wewe mpe. Ni
    sharti umpe mtu Yule chochote uwezacho ili yeye aweze
    kuongozwa kwa Bwana. Wale waishio kwenye nyumba zilizo
    nzuri zaidi ni wale ambao wameeneza
    injili kwa wingi. Kisha malaika akanisindikiza mahali
    ambapo watakatifu waliishi katika
    makao mazuri. Hapa ndipo walioeneza injili kwa wingi
    waliishi. Ilikuwa ni kama sehemu ya hali
    ya juu huko mbinguni. Page 8 8 Katika historia ya ukristo kuna watu
    wanne ambao wana moja wapo za
    nyumba kubwa sana tena za kupendeza sana. Malaika
    akanionyesha nyumba ya mwinjilisti wa
    kimarekani D.L Moody, mchungaji wa uingereza John
    Wesley, mwinjilisti wa kiitaliano na
    mwinjilisti wa kikorea mchungaji Choi Guu Nung.
    Hawa wane wana mmoja wapo za
    nyumba kubwa sana mbinguni. Wanne hawa waliyatumia
    maisha yao yote kuieneza injili kwa watu
    hata mpaka wakati wa kufa kwao. Katika Waumini wa kikorea, palikuwa na
    muumini wa kawaida alieykuwa na
    jumba kubwa. Huyu muumini alijenga makanisa mengi.
    Alikuwa amepeana magunia elfu tatu ya
    mchele kwa masikini. Kwa kisiri aliwasiadia maelfu
    ya wachungaji na viongozi wa kanisa
    katika hali ya kifedha. Yeye pia aliwasaidia wanafunzi
    waliokuwa wakisomea thiologia na
    waliokuwa katika vyuo vya masomo ya bibilia. Alimchukua
    mchungaji wa miaka sitini na tano
    nyumbani mwake naye akamtunza vyema. Mchungaji huyu alikuwa amefukuzwa
    kutoka kanisa lake. Nikasikia malaika akisema, "kuna vifaa
    vimewasili!". Nikamhoji malaika aliyekuwa kulia kwangu kuhusu vifaa
    hivi vilivyowasili, naye akaniambia. vifaa hivi ni vya shemasi wa
    kike kutoka kanisa dogo. Kwa kweli yeye hupokea vifaa kila siku.
    Ingawa yeye ni masikini, yeye huja mapema kwa ibada ya asubuhi kila siku.
    Yeye huawaombea washirika themanini na saba kila siku. Amalizapo
    kusali yeye huisafisha kanisa. Nikasikia malaika mwingine akisema
    kwa sauti, "utoaji maalum umeasili, bintiye shemasi wa kike
    ametoa pesa kidogo amabzo ndizo zote alizokuwa nazo na kumpa mama
    yake. Lakini shemasi yule hakuzitumia
    kwa ajili yake binafsi bali alimnunulia mchungaji mayai
    matano na jozi mbili za soksi". Ingawa
    itaonekana ni sadaka kidodgo yeye alipeana vytoe
    alivyokuwa navyo siku hiyo. Hivi vikawa vifaa maalum vya kuijengea
    nyumba yake mbinguni. Pili, wale ambao pia wana nyumba
    kubwa ni wale waliojenga makanisa au majumba mengine kwa ajili
    ya ufalme wa Mungu wakitumia rasilmali zao. Mbinguni pia nilikutana na mzee aitwaye
    Choi, kati ya wazee wa kikorea na mashemasi walioko
    mbinguni, yeye alikuwa na nyumba nzuri zaidi. Nyumba yake
    ilikuwa ndefu kuliko jumba ndefu zaidi
    nchini Korea. Choi alijenga makanisa mengi nchini Korea
    kwa kutumia mali yake. Page 9 9 Nikamuuliza malaika, "na nyumba yangu
    je?, bado iko katika hali ya kujengwa?"
    Naye malaika akanijibu, "ndio". Nikamsishi niione
    nyumba yangu lakini wakaniambia
    haikuruhusiwa. Nilizizdi kumsishi na baada ya kusisitiza kwangu
    , wale malaika wakanijibu kwmaba
    Bwana sasa ataruhusu. Tukaingia kwenye gari livutwalo na
    farasi na tukasafiri mbali sana mpaka
    mahali pengine. Nilijawa na matarajio. Nikauliza, "
    nyumba yangu I wapi?" malaika
    akanijibu, "iko pale". Lakini ikaonekana ni kana kwamba mahali pale
    palikuwa ni msingi tu tayari kwa
    kujengwa. Nami nikauliza kwa sauti, "mbona
    mkanifanyia hivi? Hii itawezekanaje?
    Itakuaje nyumba yangu I katika eneo linalokuwa?" Nikiwa
    mnusurika wa vita vya kikorea , niliuza
    nyumba yangu ya kipekee ili nijenge kanisa. Hili kanisa
    mwishowe lilikuwa hadi likawa na
    washirika elfu tano. Niliandiaka vitabu vingi kwa muelekezoa
    wa Roho mtakatifu. Kitabu kimoja
    kikauza sana. Kupitia kwa mapato ya kitabu hicho
    nikajenga shule ya kikristo. Shule hiyo
    ikawawazaa wachungaji mia mbili arubaini. Katika
    hatamu yangu kama kiongozi, nilipeana
    udhamani kwa zaidi ya watoto mia nne waliokuwa
    masikini. Nimewajengea nyumba
    wajane ili waishi mle. Hii yote iligharimu pesa nyingi sana. Saa
    mbona mambo yakawa hivi ? kwa nini
    nyumba yangu imo eneo ambalo bado linakua?
    nimeghadhibika sana". Malaika akajibu kwa ukali, "wewe haufai
    kamwe kuishi kwenye nyumba nzuri
    mbinguni kwani umeheshimiwa na watu idadi isiyoweza
    hesabika". "Kila wakatai ulipojenga au
    kufanya jambo nzuri, ulisifiwa na watu. Hata vyombo
    vya habari huko duniani vilikusifu. Kwa
    ajili ya hii matendo yako yote yalikuwa ni bure".
    (Mathayo 6:1) Nikaitazama nyumba yangu katika eneo
    lile ambalo ndilo mwanzo linajengwa.
    Lilikuwa liko kati ya nyumba zingine tatu. Lilikuwa na
    gorofa tatu pekee. Nyumba yangu
    Ilikuwa na vyumba vingi vidogo katika orofa mbili za kwanza.
    Nikamuuliza malaika. "mbona nina vyumba vidogo hivyo?" naye
    malaika akanijibu" vyumba hivyo ni vya wana na mabinti wako." "Nina
    watoto wane pekee" nami nikamjibu. Malaika akanifafanulia "la sio
    za watoto wa kidunia bali ni za wale amabao uliwainjilisha na
    wakaokoka". Nikapendezwa sana nikauliza "li wapi chumba changu
    kikuu cha kulala?." Malaika akasema ki juu ya paa. Hii ikanitatiza
    sana. Chumba changu hakikuwa kimemaliza kujengwa. Kwa
    sauti ya kukasirika nikasema, "ni ndogo sana! Mbona ni vigumu
    kuimaliza?". Malaika akajibu, "wewe
    bado hujafa, hatuwezi kuimaliza nyumba yako au vyumba
    vyake kwasasbabu hatujui kama vifaa
    zaidi vitatolewa. Umeelewa?" Page 10 10 Tulipoingia chumbani mwangu, nikaona
    vyeti vikining'inia ukutani , basi nikaenda
    kuvisoma. Cheti cha kwanza kilieleza nilipokuwa
    na miaka kumi na minane nikiishi
    kwenye nyumba ya watoto mayatima. Siku ya krismasi,
    nilikuwa narudi kutoka ibada ya asubuhi kanisani nikamuona mzee
    Fulani akitetemeka pale barabarani. Nikalitoa koti langu
    nikampa. Tendo hilo likanipa tuzo mbinguni. Cheti cha pili kilieleza tukio
    lilo hilo lakini ilikuwa kwa ajili ya mkate niliomnunulia mzee huyo
    kutumia pesa zangu kidogo nilizokuwa nazo. Zile pesa sio muhimu.
    Kitendo lazima kaindamane na imani au kujitolea kwa kweli. Kiasi
    cha pesa au zile dola hazikuwa muhimu. Tuliondoka mahali pale tukarudi.
    Tulipokuwa njiani mmoja wa wale malaika akaniuliza , " je
    umesononeka? Nitakuambia jinsi ya kujengewa nyumba ya
    kupendeza". "Bwana alisema urudipo duniani, lazima uwaambie watu
    kuhusu mbinguni na jehanamu jinsi ulivyzishuhudia. Pili
    Bwana anataka ujenge mahali pa kuwakusanya wachungaji
    wazee wa kike na mashemasi ambao hawana makao au
    pa kwenda.Ikiwa utafanya hivi kwa uaminifu basi utakuwa
    na nyumba nzuri. JEHANAMU Wale Malaika wawili wakanipeleka
    jehanamu. Wakasema, "sasa utazuru
    jehanamu. Wewe haufahamu ukubwa wa jehanamu."
    Nilizizdi kusema kwa sauti "nipakubwa
    sana! Niapakubwa sana!" . Hapa ndipo mahali nafsi
    zizlizolaaaniwa milele huwekwa. Ilihisika
    kana kwamba jehanamu ni kubwa sana mara elfu
    kuliko dunia. Nusu ya jehanamu ilikuwa
    nyekundu na nusu ingine ilikuwa nyeusi tititi. Nikawauliza
    malaika "mbona sehemu hii ni
    nyekundu?" nao wakanijibu. "Kwani hufahamu, ni madini
    ya kiberiti yanayoungua. Nusu ya pili ni
    giza. Watu wafanyao dhambi na kuishia hapa
    watateswa toka pande zote". Kuna makanisa mengi sana
    duniani na nyingi yazo zimejawa na watu wengi amabao wengi
    wao sio wakristu wa kweli. Wao ni wale wajao
    kanisani tu. Kanisa za kweli zitaamini kwa ukweli kwamba
    kuna mbingu na pia jehanamu. Maisha ya wakristu wengi yana
    machafuko mengi kwani hawaamini kwa
    dhati kuwa kuna mbinguni na jehanamu. Page 11 11 Nafsi moja iingiapo mbinguni, nafsi elfu
    moja zilizolaaniwa huingia jehanamu.
    Uwiano wa wale waingiao mbingunia na wale waingia
    jehanamu ni moj kwa elfu. (Mathayo
    7:14) Mimi ni mchungaji wa kiprisbiteriani
    aliye fahamika sana. Nimehitimu kutoka
    chuo kikubwa cha masomo ya kibilia nchini Korea.
    Sikuamini hivi visa kuhusu jehanamu na
    mbinguni. Lakini sasa mimi ni Yule aandikaye
    mashuhudio yangu ili kuwashuhudia
    wengine. Ingawa waweza amini wewe ni mkrsito,
    ikiwa unayaishi maisha kulingana na
    matakwa ya mapepo basi utaishia jehanamu. Mahali pa kwanza nilipopaona ni mahali
    pa madini ya kiberiti yanayoungua.wewe
    huwezi hata kudariria jinsi mioto ya jehanamu ilivyo.
    Hakuna awezaye kuusthimili moto huo. Watu waliojehanamu hutamka mambo
    matatu. Kwanza pana joto jingi na
    wanahisi kufa (luka 16:24) Pili, wana kiu kingi na wanahisi kufa.
    Tatu utasikia wengi wakiitisha maji
    (zecheria 9:11) Na mateso haya ni ya milelel!. Watu
    wengi husema tuko uhuru katika Kristo nao huishi maisha yao
    watakavyo. Nikamuuliza malaika, "wale waliomo humu wamefanya nini?"
    wakanijibu . "kikundi cha kwanza ni wasio waumini, wale ambao
    hawajaziinjilisha jamii zao lazima watubu". Malaika akaendelea,
    "kundi la tatu ni la wale waliomwamini Yesu lakini hawakutubu
    dhambi zao". Ni lazima tutubu dhambi zetu na kumkiri Yesu ni
    Bwana. Tusitende dhambi. Kunyamaza tu sio kutubu. Kwa mioyo
    iliyopondeka yatupasa kutubu. Page 12 12 WAKRISTU JEHANAMU Kisha nikawaona wachungaji wengi,
    wazee wa kanisa na mashemasi wakiwa
    jehanamu. Nikawauliza malaika. "Nawafahamu
    watu hawa, walimtumikia Bwana kwa
    uaminifu wakiwa duniani. Walifariki wakati mwingine
    iliopita na sote tulidhani wako mbinguni
    na Mungu, lakini sasa nawaona wote jehanamu tena
    wanalia kwamba moto ni mkali sana,
    mbona wako hapa?" palikuwa na wachungaji wengi, wazee
    wa kanisa,mashemasi na waumini wa
    kawaida wengi . Malaika akajibu, "mchungaji Park Yong
    GYUU mtu anaweza onekana kuwa
    mfuasi wa kweli wa Yesu kutoka nje lakini Mungu ndiye
    aijuaye roho ya mtu na yale yaliyomo
    ndani mwake". Hawakuichukua jumapili kuwa siku
    takatifu. Walipenda shughuli za kutafuta
    pesa jumapili. (Jer 17:27) Mashemasi wengi na wazee wa kanisa
    waliyashutumu mahubiri ya wachungaji wao .(zaburi105:15) (hesabu
    12:8-9) Hawakutoa zaka ipasavyo. (Malachi 3:9)
    hawakuomba. Hawakueneza injili kwa watu kamwe .
    (Ezekiel 33:6). Wengi wa wazee hawa na mashemasi
    waliwasumbua wachungaji wao na kuyapinga mamlaka yao. Waliyatatiza majukumu na shughuli za
    wachungaji . Wakiwa vitandani mwao
    karibu kufa. Walidhani kuwa walikuwa wamefanya
    kazi nzuri hapa duniani, kwa hiyo
    hawakutubu dhambi zao. Hii ndio sababu walitupwa kwenye
    mioto ya jehanamu. Kisha nikaona mfalme na mwana wa
    mfalme waliowatesa wakristo nchini Korea.
    Mfalme huyu na huyo mwana wa mfalme
    waliwakata vichwa wengi wa waumini wa kwanza
    nchini korea. Waliwekwa katikati mwa
    jehanamu ambapo moto ulikuwa mkali zaidi kuliko sehemu zingine zote. Niliwaona Hitler,Stalin, Mae Zedong na
    mhubiri mashuhuri kutoka Korea
    kaskazini aitwaye mchungaji Kang, shujaa Fulani wa
    kijapanisi na wengine wengi. Kisha tukawasili mahali penye giza
    totoro hadi hungeweza kuona mahali
    ukanyagapo. Nikapiga kelele, "malaika! kuna giza jingi sana,
    mimi nitaonaje chochote?" malaika
    akanipapasa begani mwnagu akasema "ngojea kidogo tu". Page 13 13 Baada ya muda kidogo, niliweza kuiona
    idadi ya watu wasiohesabika waliokuwa
    uchi. Wote walijawa na wadudu waliowatambaa
    miili yao . Hakuna sehemu ya miili yao
    iliyosazwa kwani yote ilifunikwa kabisa na wadudu wale. Wale watu wakiwa uchi walijaribu
    kuwafukuza wadudu wale huku
    wakisaga meno. Nikauliza , "ni nini walichokifanya watu hawa
    walipoishi duniani?". Hawa ni wale walioshutumiana na
    kusengenyana, hawakujali yale waliyoambiana. (Mathayo 5:22)
    niliwaona mapepo wakizidunga na kuzitoboa tumbo za watu wale
    wakitumia mundu. Singeweza kuzistahimili kelele zao. Nikawauliza
    malaika, "ni nini walichofanya watu hawa walipokuwa duiniani?" "watu hawa walikuwa na kazi, majumba
    na hata jamii, lakini hawakumtolea Bwana Mungu.
    Hawakuwasaidia masikini, makanisa yao au kazi za Mungu, walikuwa
    wabanifu tena walafi. Hata walipokutana na masikini waliwapuuza
    na hawakuwajali. Walijali tu masilahi
    yao na ya jamii zao. Walivaa vizuri na kula vizuri na
    walikua na maisha ya starehe. Hii ndio
    sababu tumbo zao zinatobolewa kwani tumbo zao zilijaa
    tama". ( methali 28:27) Lilikuwa ni jambo la kuogofya sana.
    Baada ya kushuhudia jambo hilo,
    niliporudi duniani, nilipeana pesa na mali yangu yote kwa
    watu wengine. Wokovu hauwezi
    patikana kwa pesa au mali. Ni kwa imani pekee. Jehanamu
    hakustahimiliki na ni pahali duni. Ni
    mahali pa mateso. Niliona pia watu amabao vichwa vyao
    vilikatwa kwa msumeno mkali sana.
    Nikamuuliza malaika, "ni nini walichokifanya watu
    hawa? Ili wastahili mateso namna hii?" Naye akanijibu, " Mungu aliwapa akili ili
    wawaze mambo yaliyo mema tena yenya manufaa. Lakini hawa
    watu walikuwa na mafikira potovu tena machafu. Walifikiri
    kuhusu mambo ya tama na anasa". (Mathayo 5:28) Kish nikawaona watu wanadungwa na
    kukatwa vipande vipande. Ilitisha sana. Nikauliza "vipi kuhusu watu
    hawa? walifanya nini?, Hata wateswe
    nama namna hii?." Malaika akaibu "hawa walikuwa
    mashemasi na wazee wa kanisa ambao hawakuzitumikia kanisa zao.
    Hawakutaka wala kupenda kuzitumikia
    kanisa zao wala kuzifanyia kazi. Wao walipenda tu
    kupokea na kupokea vitu kutoka kwa
    washirika wa kanisa". (Zecheria 11:17, hosea 6:5) Page 14 14 Nliwaona wazee wa kanisa ,mashemasi
    na waumini wa kawaida wakiteswa na mapepo. Mapepo yalitengeneza
    shimo katika ndimi zao na kuingiza kamba kupitia matundu yale kwenye
    ndimi zao. Kisha mapepo yakawaburura kwa kamba ile. Nikauliza
    tena. "walifanya nini duniani?" malaika akajibu, "wao walifanya dhambi
    nne tofauti. Kwanza waliwashutumu wachungaji wao.
    Waliongea mabaya kuwahusu. Waliwasengenya na kuwakejeli
    wachungaji wao." ()akobo3:6)( mathayo 12:37) Nawasihi nyote mliofanya matendo
    kama haya tubuni! Tubuni! Malaika akaendelea , "pili
    waliwasumbua wakristo wengine hadi
    hata wale waliokuwa waaminifu wakaathirika na kuacha kuja
    kanisani na hata wengine waliacha
    kuamini. Walifanya kila wawezavyo kuwafanya wakrsisto
    waaminifu wasitende kazi ya Bwana.
    Waovu hawa walisababisha waumni wengi wajikwae .
    mwisho kuna wake na waume
    waliokunywa pombe na kuwatusi watu wa jamii zao. Niliona
    mapepo wakitoboa tumbo za waume na
    wake wale kutumia msumari mkubwa. Niakuliza , "
    walifanya nini hawa? Malaika akanijibu . " hawa ni waume na
    wake walioishi pamoja pasina kuoana pia wana hatia ya uavyaji
    mimba kwani waliwahi kushika mimba pia na hawajatubu.". Nikaoana kundi la watu. Mapepo
    waliikata midomo yao kama vile mtu akatavyo nyama au mboga kwa
    vipande vidogo. Niakuliza, "mbona watu hawa
    wanateswa hivi? Malaika akajibu, " hawa ni wana na mabinti , na
    mabinti na wana katika sheria
    waliojibizana na wazazia wao. Kile iliwapasa kufanya ni
    kuomba msamaha badala ya kufanya
    mambo kuwa mabaya zaidi. Wengi wao walitumia
    lugha ya matusi, waliwashambulia
    wazazi wao mananeo makali.waliasi. hii ndio sababu midomo
    yao inakatwa viapande vidogo." Wandugu, sote tutakufa siku moja, lakini
    hatujui itakuwa lini. Tafadhali
    sameheaneni kila wakati na ipasavyo ikibidi. Tubu na
    utubu tena na fanya hivi hata siku nzima
    ikikubidi. Wandugu wapendwa nilizipuuza
    shuhuda kama hizi . nilikuwa mchungaji
    wa kiprisbiteriani wa kihifadhina aliyepuuza mambo kama
    haya. Lakini sasa lazima niwashuhudie
    yale niliyo yaona. Page 15 15 Tafadhali usisite kuishi maisha
    matakatifu. Tafadhali epuka hukumu hii
    iliyojaa mateso mengi. Usiishi kwa ajili ya mwili wako bali
    jiwasilishe kwa ufalme wa Mungu. Tafadhali waombee wasiomjua Yesu.
    Waenezee watu injili na uzae matunda ya kiroho .Tafadhali omba
    asubihi sana na ifanye jumapili kuwa takatifu. Toa zaka ipasavyo.
    Jilimbikizie tuzo mbinguni na sio humu ulimwenguni. Naomba na
    kukubariki kwa jina takatifu la Yesu. Kutoka kwa mchungaji Park Yong Gyu.

    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate