UNABII KWA TANZANIA NA KWA DUNIA YOTE KWA UFUPI MWAKA 2017
BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE. Nawatakia heri ya mwaka mpya watu wote wa ulimwengu kwa rangi zote alizowaumbia wanadamu. Katika mwaka huu wa 2017 yapo mambo mabaya yatakayotokea katika nchi mbali mbali ikiwemo; matetemeko, njaa na maafa, na viongozi katika baadhi ya nchi mbali mbali walio katika madaraka hawatashinda uchaguzi na wengine wataachia madaraka kabla ya muda wao kwa sababu ya mambo fulani yatakayotokea. Yapo mengi ambayo tayari MUNGU ameshanieleza ila nitaelezea machache na myaonapo yasiwatishe kwa sababu ni lazima yatokee tu.
TANZANIA
Nchi ya Tanzania itaendelea kuinuliwa sana, wala maneno yote mabaya juu ya serikali hii, hakuna litakalofanikiwa. Nchi hii ipo mkononi mwa MUNGU na ni MUNGU mwenyewe anaitengeneza nchi hii, hivyo waliozoea kuichezea hii nchi na kuiba wataendelea kulia machozi tu. Soma unabii wa Nabii Hebron katika blog yake “unabii wa Tanzania 2015”, utayaona yametokea na haya yatakuwa tu.Nchi hii ni mali yake MUNGU na siyo ya shetani au ya miungu au wachawi. Wanaomtakia mabaya Rais huyu watapigwa na MUNGU, yeye ni mtumishi wa MUNGU na yeye ndiye kamweka na wala hajawekwa pepo, mchawi wala mtu. Nilielezea katika unabii wa 2015 kwamba rais ajaye atakuwa ni mtu asiyetazamiwa na ndivyo ilivyokuwa. MUNGU ataendelea kumwinua nakuwa tofauti kila wakati sawa sawa na jinsi yeye atakavyoendelea kumtii MUNGU. Nchi itaendelea kuwa salama kabisa. Yapo mambo mabaya ambayo watu walitamkiwa na watumishi, hayo mabaya siyo ya MUNGU, watavuka mwezi wa tatu na wawe na amani kabisa na mtaona wakiishi, waendelee kusema ukweli daima.MAMBO YATAKAYOWATOKEA WATUMISHI WANAOTUMIA NGUVU ZA GIZA NA WALIOMUASI MUNGU KWA DUNIA YOTE.Huu mwaka 2017, hii ni kwa ulimwengu wote, watumishi hao watapatwa na vifo vya ajabu na wapo wenye magonjwa ya aibu yataonekana wazi wazi na sura zao zitabadilika. Zipo huduma zitakufa kabisa na uovu wao utafichuliwa kwa njia anayoijua MUNGU mwenyewe, wengine watakuwa vichaa na hapa Tanzania itatokea sana, myaonapo msijiumize akili zenu, mjue ni MUNGU atakuwa anaifanya kazi yake ya kuwashughulikia waasi na wakala (agents) wa shetani, walijificha miaka mingi kwa kivuli cha kutumia jina la YESU kuiendeleza kazi ya shetani na kuangamiza roho za watoto wa MUNGU ili kuzipeleka jehanamu na wengine kufanywa misukule na makafara.KWA UPANDE WA BIASHARA ZINAZOFANYWA NA MAKANISA AU HUDUMA ZA KIROHO WATALIPA KODI KWA KAISARI.Tarehe 23.11.2016, nilikuwa barabarani katika gari MUNGU akanieleza haya; kuwa “ataamuru serikali itoze kodi kanisa kwa sababu kanisa kwa sehemu kubwa limekuwa likiibia nchi mapato ya kodi na serikali ikijua inanifanyia mimi MUNGU na kumbe siyo mimi, nimeruhusu na itafanyika”, akaniambia “mimi ni MUNGU na watumishi wangu sikuwatuma wafanye biashara bali watoe huduma. Kutoa huduma ni bure, sasa kanisa limejiingiza kwenye biashara na wanaibia nchi kodi kwa miaka mingi”. Akaniambia “ya MUNGU mpe MUNGU na ya Kaisari mpe Kaisari”. Niliogopa kwa sababu ilikuwa ni sauti ya ukali akisema na mimi. Akaniambia “wewe ni mmoja katika watumishi wanaye iombea nchi hii ikiwemo na uchumi ili kodi zilipwe, sasa hawa wanaofanya biashara kwa kutumia jina langu kwa nini hawalipi kodi?” Nilikosa jibu.Akaniambia “na ndiyo sababu nilipokuita nilikueleza acha kazi fanya kazi hii ya kanisa kuponya roho, hauwezi kuwa na mabwana wawili; utampenda huyu na utamchukia huyu na ndivyo ilivyo, mimi MUNGU siyo wa miradi”. Akanieleza kwa ufupi “zipo shule, vyuo, mahoteli, majumba, redio, TV, maduka yanaitwa ni yangu yaani ni ya kanisa”, akasema “yeye siyo mfanya biashara, hayo ni ya Kaisari na wanatumia jina la YESU kuziibia nchi mbali mbali mapato ya kodi”.Soma Luka 12:16-17, YESU mwenyewe alipokuwa kwa Kaisari alidaiwa kodi na alilipa, sasa iweje leo kanisa linafanya biashara tena ya Kaisari na halilipi kodi linamsingizia MUNGU! Akaniambia, “yapo mapato mengi sana ya nchi yameshikiliwa na biashara zinazoitwa kwa jina la kanisa hayalipi kodi matokeo yake yanasababisha uchumi kutokuinuka kwa sababu ya hiyo miradi, kama kanisa lisingefanya, wananchi wangefanya na wangelipa kodi”. Sasa hiyo kodi haipo inaibiwa na wananchi kodi zao zinaibiwa kwa njia hii, hivyo ni lazima kodi ilipwe. Hii ndio sababu kanisa linapata faida. Kama shule za kanisa zingekuwa ni huduma basi zingesomesha watu bure, hapo isingefaa kulipa kodi, cha kushangaza ukikosa pesa hauingii chuoni, au shuleni. Cha kujiuliza kodi ya mwananchi iko wapi na inaenda wapi? Mapato ya nchi yapo wapi?Imeandikwa ya Kaisari mpe Kaisari sasa kwa nini Kaisari asilipwe haki yake? Matokeo yake wananchi tu ndio waaminifu kwa Kaisari, hii siyo haki mbele za MUNGU, huu ni wizi wa kuibia nchi mapato yake. Hata wakiacha watafanya wengine ila sababu wanapata faida hawataacha. Watu wote wa dunia nzima msidanganyike MUNGU siyo mwizi MUNGU ni wa haki anatenda haki na yeye siyo mfanya biashara.Akaniambia nchi hii inaibiwa mapato mengi na wafanya biashara wakitumia jina langu YESU mfano mtu ameagiza magari 20 kwa jina la kanisa kwa $40,000 kila moja na inasamehewa kodi kwa kujua ni huduma ya kiroho, yakifika nchini kila gari anauziwa mtu mfano $60,000 halafu anayelinunua huku nchini anaandikiwa mkataba wa $5,000 au TSh. 10,000,000 na kiasi hiki ndicho kinalipiwa ushuru. Je huu sio wizi mkubwa? Je kama unayo akili timamau na unampenda MUNGU hauoni huu ni ujangili mkubwa sana wa kuibia nchi mapato na ushuru.MUNGU akaniambia hivi ndivyo kodi inavyoibiwa na baadhi ya watu wakitumia jina langu na kumbe siyo mimi MUNGU na mengineyo mengi alinieleza ili nimwelewe zaidi. Sasa nchi mbali mbali zinahangaika kufuatilia kodi sehemu mbali mbali zimesahau kuwa zipo pesa zao katika makanisa au sehemu za ibada za biashara. “Kupitia jina langu mimi MUNGU, watu wanajifichia uovu na kufanya wizi na baadhi yao wanatumia nguvu za giza, uchawi lakini wanajiita wachungaji, mitume, manabii, wainjilisti, walimu, maskofu na mengineyo kumbe ni watoza ushuru. Wanatoza wananchi ushuru wa serikali halafu wanaweka katika mifuko yao. Kama Mathayo alivyokuwa anakusanya, yeye alipeleka kwa Kaisari, ila hawa wanamwibia hata Kaisari wanaiweka mifukoni mwao, ndivyo pesa ya mapato ya nchi mbali mbali yanavyoibiwa.Ameniambia MUNGU aliyeumba mbingu na dunia hayo siyo mambo yake, hata huduma zenye mabenki, redio, TV hawafanyi bure wanadai pesa, sasa ipo wapi VAT ya hizo nchi? Hivyo itakapotokea watu wasishangae, ameruhusu mwenyezi MUNGU na haitabadilika. Kodi italipwa tu hata mtu akichukia kwa sababu ya ujumbe huu mimi ni lazima niseme atakavyo MUNGU na siyo mtu atakavyo. Makanisa yanayofanya kutoa huduma bure ndiyo hayatatozwa kodi. Akaniambia ukiangalia katika dunia hii watu wanaambiwa watoe pesa kiasi fulani ili waombewe, hao ni wezi na wanyang’anyi. Mimi MUNGU namponya mtu bure sawa sawa na NENO langu.Yapo mengi nitaendelea kuyatoa jinsi atakavyoniruhusu nitoe kwa ulimwengu wote. Mengine ni yake kwa utukufu wake. MUNGU anawapenda watu wote, mrejeeni mwenyezi MUNGU na kuishi maisha matakatifu, mwanae wa pekee karibia anarudi sasa wewe utakuwa wapi? Wakati wa neema ni sasa. Sema, BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, uandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele, sikutaki shetani na mambo yako, Potea katika jina la YESU.MUNGU ibariki Tanzania na dunia yote.Brought to you By Prophet HEBRON on 02.01.2017
UNABII WA KWELI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni