Wafilipi 2:10-11
  • JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI - Kitabu cha Nabii Hebron


    YALIYOMO

    ·        KANISA NI NINI

    ·        HEKALU LA BWANA

    ·        WATUMISHI WAMEMSALITI YESU

    ·        WATUMISHI WANAFUNDISHA MAFUNDISHO YASIYO YA YESU

    ·        SABABU YA KANISA KUTOKUJIBIWA NA MUNGU

    ·  WATUMISHI KUNYANG'ANYA MALI ZA WATU, PESA NA KUMFANYA YESU AITWE MNYANG’ANYI

    ·        WATUMISHI 98% WAMETEKWA NA SHETANI ULIMWENGUNI  MWOTE

    ·        NAMNA YA KUPONA USITEKWE




    TOLEO LA KWANZA
    APRIL 2012
    ISBN 978-9987-9553-1-2




    UTANGULIZI

    Ndugu nakusalimu kwa jina la YESU KRISTO, ambaye ndiye BWANA na mwokozi wa mataifa yote, pia ndiye mfalme wa wafalme na bwana wa mabwana na hapana mfalme mwengine zaidi yake. mimi jina langu naitwa Hebron Wilson Kisamo, YESU amenichagua nimtumikie yeye kwa jinsi anavyotaka yeye ili kukomboa ulimwengu huu ambao umepotea na shetani ameumiliki kwa asilimia 98% sawa sawa na YESU alivyoniambia mwenyewe. Amenituma ulimwenguni  kote ikiwa ina maana nchi zote, mabara yote.

    Ujumbe huu aliniagiza rasmi na kunipa mamlaka yake tarehe 14.6.2010. Na akanipa jina la kanisa lake niliite YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRY. Akaniambia mwanangu nitautumia huu mwili wako kuukomboa ulimwengu wote, utachukiwa sana, utafanyiwa na kuitwa majina mabaya lakini usiogope tena ufurahi zaidi, kwani mimi YESU walinifanyia mabaya zaidi na ya uongo yakitokea kwa baba yao wa uongo ambaye ni lusifa, nilifurahi daima. Hakuna jambo lolote litakalofanikiwajuu yako au silaha yoyote juu yako nipo na wewe milele. Nitakutumia kwa namna ya tofauti na kwa kiwango kikubwa sana ambacho hakijaonekana tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu. Adui yako ni adui yangu, akasema YESU kwa sauti ya uchungu sana, watumishi wamenisaliti maagizo niliyowapa hawayafanyi na wamegeuza neno langu kuwa maandiko badala ya neno, maandiko yanatoka kwa shetani maana lusifa anaijua bibilia yote na maandiko hayana uthibitisho wa nguvu zake YESU. Neno linatoka kwa YESU na linaudhihirisho wa nguvu za MUNGU. Na pia wana wa Adamu wanateseka wanalia na kuomba hawapati majibu, na zaidi wanazidi kupotoshwa na viongozi wa kanisa, maagizo niliyoyaacha nilivyokuwa ulimwenguni kabla ya kurudi kwa BABA yangu ili kuniandalia maandalizi ya ujio wangu ili nipate kuwaponya wengi waende mbinguni, imekuwa kinyume idadi kubwa ni ya watu wa shetani. Waliokuwa watumishi wangu wamenisaliti 98% sipo nao. Wameamua kwenda kuzimu, na shetani anawatumia na jinsi anavyowatumia, ni kubadili au kwenda kinyume na agizo la MUNGU, mfano watumishi kwa sasa wamefanya kanisa ni mahali pa biashara, kunyanganya watu vitu vyao na wakijua wananitolea mimi, na kufanya mimi YESU ndiye mnyanganyi, kwa midomo yao hunitaja kama wananipenda ila mioyoni mwao hawapo na mimi, wamekuwa watumishi wa pesa na siyo mimi, wamekuwa wakitenda miujiza lakini siyo yangu ni miujiza ya shetani, na hao ni kati ya wale ambao siku ya mwisho nitawakataa na kuwaambia sikujui. Kanisa limeniacha kunitegemea mimi, imebaki 2% tu ulimwengu mwote. Sasa mimi YESU ninalikomboa kanisa mwenyewe na ndipo unabii na utukufu wa kanisa la mwisho utakuwa mkubwa kuliko wa kanisa la kwanza unatimia sasa.





    SHUKURANI

    Namshukuru mke wangu sana kwa kunitia moyo na kuniombea, nawashukuru watumishi wote wanaoniombea na kutumiwa na MUNGU kutumika pamoja na YESU aliyeniita, mkono wa MUNGU uwe juu yao siku zote za maisha yao.
    Asante.
    MTUME NA NABII- HEBRON WILSON KISAMO
    KIONGOZI NA MWANZILISHI WA HUDUMA
    P.O.BOX 13657
    ARUSHA, TANZANIA
    EAST AFRICA








    KANISA NI NINI?

    Kanisa ni YESU, na wewe unafanyika kuitwa kanisa la YESU baada ya YESU mwenyewe kuingia ndani yako. Kanisa ni nyumba ya MUNGU kwa ajili ya sala, kanisa ni mahali pa kuongea na YESU, na YESU ndiye njia ya uzima na kweli na hakuna mtu yeyote atakaye kwenda mbinguni bila kupitia njia ya YESU. YESU ambaye ndiye mfalme wa wafalme na bwana wa mabwana, ndiye mwanzo wa kanisa la kweli. YESU ni mtakatifu na hakufanya dhambi, alikuja ulimwenguni ili aukomboe ulimwengu na alifundisha yote aliyoagizwa na MUNGU BABA na akatulipia deni zetu zote pale msalabani kwa mateso magumu mpaka kupigwa viboko ili sisi tupone. Ukisoma katika kitabu cha injili ya Mathayo 21: 12- 17 YESU aliingia hekaluni ambapo ni nyumba ya sala akawakuta watu wakifanya biashara, kubadilishana vitu, pesa na mengineyo, kwa hasira aliwafukuza na kutupa kila kitu hata mifugo, akawaambia imeandikwa nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala, bali ninyi mmeifanya nyumba ya wanyanganyi akawafukuza na YESU akaingia hekaluni na watu waliokuwa na vifungo vya shetani, wakamfuata YESU hekaluni na YESU akawafungua na kuwaponya. Ndugu msomaji, naomba uelewe na usidanganyike tena, kanisa sasa hivi limeyapuuzia mafundisho yake YESU aliyoaagiza na zaidi usipo yafuata maagizo ya YESU hayo ni kumdharau YESU, wanadamu hofu ya MUNGU haipo na wanamzoea MUNGU kama watu wanavyozoeana. , YESU alivyoyakataa mambo hayo inamaana ni ya shetani yangekuwa ni ya MUNGU angeyaruhusu yafanyike kanisani. YESU alikuja kukomboa kanisa yani hekalu la MUNGU maana shetani alishaingia ndani yake na katika injili hii ya Mathayo 21:12-17 tunaona jinsi YESU KRISTO alivyoyatoa mambo ya shetani kwenye hekalu na alipo yatoa ndipo YESU akaweza kuingia hekaluni na ndipo watu waliokuwa wanatafuta majibu walimwona na wakajibiwa au kuponywa. Ndugu msomaji, leo hii mambo aliyoyakataa YESU yasifanyike kanisani yamerudishwa yote na mengine ni zaidi na zaidi yameongezeka na mambo hayo yanamfanya YESU asiwepo makanisani na ndiyo maana wakristo yaani mfuasi/wafuasi wa Kristo mnakata tama na ukristo maana hamna majibu au uponyaji na haya yanafanywa na watumishi ambao mioyo yao ni migumu haitaki kumtii YESU.Na YESU hakai mahali au katika kanisa ambalo haliyafuati mambo ambayo muasisi wa kanisa yani YESU aliweka muongozo aliopewa na MUNGU na kanisa kuyapuuzia, hiyo ni njia moja wapo inayomhuzunisha YESU, kanisa la YESU linafuata maagizo aliyoyaagiza yeye na ndugu msomaji mshukuru YESU kwa ajili ya mafunuo ili ulimwengu upone. Siku hizi kuna makanisa aina mbili japo yote yanaitwa makanisa, na shetani amewakamata na kuwapiga upofu ili watu wajijue wapo salama lakini leo hii YESU anakufungua umjue YESU wa kweli maana pametokea wakristo wa uongo na ndiyo wengi sana, japo hao wanaohusika wanajijua wanafanya nini ili kuharibu kazi ya YESU. Sasa mwisho wa hao wanaoiharibu kazi ya MUNGU kwa kutumiwa na shetani mwisho wao umefika na sasa wanakwenda kuaibika katika jina la YESU, haya ndiyo aliyoniambia Bwana wetu YESU KRISTO.



    KANISA  LA YESU WA KWELI
    Kanisa la YESU wa kweli analiongoza mwenyewe na halipingi au kubadilisha neno kwenda kinyume. Kanisa la kweli lina majibu yako, na Baraka zako za rohoni na mwilini unazipata, Live Live. Kanisa la YESU wa kweli watumishi wake siyo walevi, siyo wachawi, siyo wanyang’anyi, hawavuti sigara, hawana mambo ya kidunia, hawaombei watu maombi mabaya, hawatumii jina la YESU kujitafutia mali, hawafundishi mafundisho ya uongo kwa faida zao, siyo wabinafsi, ,tabia zao zimefanana na za YESU na mtumishi anayetumiwa na YESUndani yake ni YESU anakaa na kama YESU anakaa ndani yake nilazima YESU ayafanye yale YESU anayoyataka maana mtumishi wa YESU anaongozwa na YESU tu. Kanisa la YESU wa kweli lina macho yaliyohai kama YESU alivyo mwenyewe, Kanisa lake lina nguvu zake tena hata milango ya kuzimu haliwezi. Kanisa la YESU linaongozwa kwa ushirikiano wa MUNGU BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU. Na kazi zao pia ni kuhakikisha yale yote yanayotakiwa yatendeke na MUNGU, yatimie na siyo yasitimie au kuyabadili, maana unabii uliyoandikwa katika kitabu cha injili kutoka kwa MUNGU ni muongozo wa kumfuata yeye kwa hiyo ili kupona lazima kufuata anayoyataka. Soma ufunuo wa yohana 22;18-20.

    MTUMISHI WA YESU WA KWELI
    Mtumishi wa YESU ni lazima aweameokoka, na pia lazima apitie ubatizo kama wa YESU wa maji mengi kama alivyobatizwa yeye, Je? Jiulize ubatizo huu mwingine umetoka wapi? Kuanzia  Yohana alitumwa abatize kwa maji mengi katika kijito cha utakaso na YESU alibatizwa hivyo hivyo, sasa ili ukamilike ni lazima ubatizwe kama YESU ndiyo utakamilika uwe mkamilifu. Mtumishi wa YESU hachangishi pesa kanisani, hakunyang’anyi mali zako, mfano nyumba, gari na vinginevyo kwa kutumia jina la YESU. Mtumishi wa YESU hatoi vyeti vya hongera kwa kutoa fungu la kumi kwa uaminifu.. YESU alishayakataa hayo mambo maana hayatoki kwa MUNGU na ndiyo sababu ukuu wa MUNGU hauonekani. Watumishi wanaomtumikia YESU wa kweli hawafanyi biashara haramu, mfano madawa ya kulevya. Watumishi wa kweli hawalitumii kanisa kufanya biashara. YESU alishayakataa na neno linasema kweli na zaidi wapo watumishi wa kweli ambao wamenajisika kutoka kwa baba zao wa kiroho na kujikuta wamejiingiza kwenye uchafu na ili wawe safi ni lazima waoshwe na Damu ya YESU upya, tena aamue mwenyewe kutoka rohoni aombe rehema, na MUNGU atamsamehe maana MUNGU wetu ni wa rehema.

    WATUMISHI WA UONGO
    Watumishi wa uongo kwanza kabisa hutumia jina la YESU kukupofusha japo wanaongozwa na kiongozi wa uongo yaani shetani. Kazi yao kubwa ni kusema uongo, kubadilisha neno kuwa kinyume na maagizo aliyoyaacha YESU mfalme wa wafalme ili aweze kulihudumia kanisa lake, na shetani hutumia njia hiyo moja wapo japo zipo nyingi nitakueleza baadhi.

    Kwanza kabisa shetani amewawekea roho yakupenda pesa, na jinsi wanavyowakamata waumini ambao ni kondoo wa YESU, hutumia njia ya sadaka na kufanya michango michango wanamwaibisha YESU, kama YESU ameishiwa, YESU sio masikini. Japo neno linasema katika kitabu (Mathayo 6:2-4) utoapo sadaka yako hata mkono wako wa kulia au kushoto usijue, hapa neno la MUNGU lina maana kwamba sadaka ni siri yako wewe na MUNGU tu, sadaka ni ibada yako kamili kati yako wewe na MUNGU na hapaswi mtu yeyote kujua au kuona sadaka yako inapokuwa imeonekana au kujulikana na mtu yeyote tayari thawabu yako imebaki kwa watu uliyowaonyesha hivyo, utapata thawabu kutoka kwa watu na siyo kwa MUNGU. Sasa shetani amelikamata kanisa 98% ulimwengu wote ili wewe usibarikiwe maana haufuati atakavyo MUNGU. Wanawaambia watu waandike sadaka majina yao wakati neno la MUNGU limekataa, sasa huo ni mpango wa YESU au wa shetani? Jibu ni shetani. Shetani amewaongezea tamaa nyingi na zimewashika kwenye pesa na wameongeza majina mengi ya sadaka. Sadaka ya kweli ni fungu la kumi na sadaka ya shukurani au hiari yako kwa MUNGU. Leo hii kuna majina ya sadaka hata hayaelezeki, mfano sadaka ya injili, ujenzi, nabii, ulinzi, afya, ukombozi na nyinginezo nyingi mpaka ni aibu kuzisema jinsi muenendo aliouacha YESU umeachwa. YESU ameniambia sizo za kweli. Pesa zote za kanisa ni kwa ajili ya kazi yake umekuwa ukitoa mpaka unafilisika maana yake haukumtolea yeye, maana ungemtolea yeye angekubariki sawa sawa na ahadi za MUNGU (Malaki 3:10-12). Zaidi mwana wa MUNGU nimekuwa nikiletewa kesi na manunguniko ya wana wa MUNGU kuhusu kilio kikubwa walichonacho inawezekana pia na wewe ni mmoja wao au unayoshida hiyo hiyo. Tena watumishi wanafundisha toa mpaka roho ikuume MUNGU ndiyo anapendezwa na sadaka kama hiyo! Huo ni uongo wala usidanganyike tena wewe ni wa thamani sana mbele za MUNGU na YESU, kupitia kusoma kitabu hiki unafunguliwa katika jina la YESU. Sadaka yako unatakiwa utoe kwa upendo kutoka moyoni na ni siri yako. Usifanye kama Kaini, soma Mwanzo 4:2-16, Abeli alimtolea MUNGU sadaka kwa moyo mweupe na msafi MUNGU aliipokea na Kaini alimtolea MUNGU kwa moyo wa kuuma na uchungu! Sadaka ya uchungu MUNGU haipokei maana inakuwa kama amekunyanganya na yeye siyo MUNGU wa kunyanganya. Madhara yake haubarikiwi maana hajapokea na kama hajapokea yupo aliyepokea yaani shetani, na shetani akishapokea anakupatia Baraka zake; nuksi, balaa, mikosi, umaskini na kufilisika na mwishowe unakosa mwelekeo unakuwa kama Kaini, mpaka leo anazurura tu, sababu ya kuwa na uchungu wa kumtolea MUNGU. Hii roho haikuanza leo, tokea enzi za kina Kaini na Abeli na sasa huu ujanja shetani ameurudisha tena katika kanisa ili watu waagamie kama Kaini. Mwana wa MUNGU kataa usidanganyike tena, mtolee MUNGU kwa moyo mweupe.

    YESU anasema yeye hakopi bali yeye ndiye anakopesha, leo hii huu usemi aliousema yeye kanisa lisikope, leo kanisa ndilo linakopa na likikopa tayari YESU hayupo hapo ni mpinzani wa YESU. Shetani ili kuwa na majengo mengi amelikamata kwa namna hiyo na likikopa tayari YESU hashuki hapo tena, ibada inakuwa ya kutiana moyo na siyo YESU na ndipo watu wanaangamia na roho za wana wa MUNGU kuteseka maana hapo panakuwa siyo madhabahu yake tena, wao wanaona wanafanya kazi ya YESU kumbe siyo, haya yote ameniambia YESU niwaeleze ulimwengu mzima wapate kuijua kweli yake na ole wao walioibadili injili Wagalatia 1: 6- 10. Akaniambia japo utapingwa na hao wanaoibadilisha injili ya YESU wewe niangalie mimi tu, maana nimekuita na kukuchagua unitumikie kwa namna ya KIMUNGU na siyo ya kibinadamu. Mfano ni kama nilivyomtumia Paulo, ila nitakutumia zaidi, wewe siyo mtume wa kibinadamu ni mtume niliyekuteua mimi, nitakutumia hivyo hivyo ulivyo nimependezwa na wewe mimi YESU.

    YESU anahuzunika sana juu ya kanisa kumwaibisha na zaidi anasema kanisa linaitwa kwa jina lake, eti mimi YESU kila mwezi nirejeshe marejesho yaani mimi YESU nadaiwa na bank? Mimi YESU sipo katika kanisa hilo japo wanalitaja jina langu. Na kondoo wake wanashurutishwa kulipa deni la riba, mimi YESU nimesema kwenye neno langu ukimkopesha mtu usitake riba kwake, je mimi kanisa langu lilipe riba na mimi mmiliki wa kanisa sitaki? Hapo sipo nawao mwisho wao umefika na hukumu inawasubiri.

    Watumishi wa uongo pia wamekuwa wakifanya miujiza kwa kupitia nguvu za giza japo wanalitaja jina la YESU lakini miujiza wanayoifanya haidumu, mtu anafunguliwa lakini akiondoka hapo yanamrudia. Mfano unakuta watu wakienda kwenye kanisa au mikutano ya injili huwa wanatupiwa mapepo kutoka kuzimu yanawaangusha watu na watu wanasema nguvu za MUNGU zimemshukia na kumbe siyo. Na ujanja mwingine kwa sababu huyo mtumishi anaongozwa na lusifa wanachokifanya watu wenye mapepo wanajiunganisha na kuzimu mapepo yanapiga kelele halafu baada ya muda wananyamaza, mnaona amefunguliwa kumbe hakuna kitu yanapiga kimya. Hii yote ni kuwapofusha muzubae na mnyang’anywe pesa zenu, na huyo. Au hao walioanguka hali yao huzidi kuwa mbaya siku kwa siku.

    Ukombozi wowote au maombi unayofanyiwa halafu unaambiwa leta pesa kiasi Fulani MUNGU anataka hiyo pesa au mifugo au chochote, hapo umedanganywa. Neno la MUNGU linasema “Mmepewa bure toa bure,” hayo unayoambiwa siyo ya YESU ni ya shetani (Mathayo 10: 8).

    Watumishi wa uongo hufanya kazi ya MUNGU kama mradi wao na kuwafanya waumini (ATM MACHINE) YESU hakufanya hivyo au director wa kanisa, haya yametokea wapi? Jibu kwa shetani. Kanisa lenye matabaka ya watu mfano matajiri wanajitenga na maskini hivyo hivyo mahali hapo upendo wa kikweli wa YESU haupo ni upendo wa kinafiki, mfano kama hauna pesa au kauwezo kidogo mtumishi hakupendi au kukuombea na kukujali anawajali wenye pesa tu ,na wewe usiyekuwa nacho hana mda na wewe. Mahali hapo ujue YESU ameondoka siku nyingi, maana sisi watu wote ni wa YESU na safari yetu ya mbinguni ni moja na anayetuongoza ni jemedari mkuu YESU hana ubaguzi anao upendo. Mtumishi wa namna hiyo tayari shetani amemkamatia kwenye pesa.

    Tunajua kuwa sasa sadaka ni siri yako na MUNGU, sasa kwa nini unaambiwa uandike jina lako tena hata namba za simu? Kwani MUNGU aliye sirini hakuoni? Haya  mafundisho yametokea wapi ? Jibu siyo ya MUNGU, sasa amua mwenyewe na ujue jinsi ya kumtolea MUNGU sadaka na zizungumze na MUNGU na siyo na watumishi. Shetani ametumia huo ujanja badala sadaka MUNGU anenenayo na uinuliwe, sasa sadaka yako inanena na mtumishi au watunza pesa. Madhara ya sadaka yako kujulikana na watu badala ya MUNGU hupati Baraka zake unapata Baraka za watu na kama hawakupendi, wana wivu juu yako hayo maroho yanaingia kwenya kazi zako na biashara zako. Ila MUNGU ndiye mwema tuu juu yako anakuwazia mema na amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu, amebarikiwa amtegemeaye MUNGU. Siri ya sadaka yako mwandamu akijua umelaaniwa, siri ya sadaka yako ikijulikana na MUNGU tu umebarikiwa. Kuanzia sasa ndugu msomaji na mpenzi wa YESU anayekupenda ufunguke ufahamu wako ili uanze kubarikiwa zaidi na uinuliwe. Sadaka ni haki yako na MUNGU, wala mtumishi yeyote hanaruhusa kujua unatoa kiasi gani ni YESU peke yake tu. Na watumishi wengine watakuambia haumtii kwa nini hauandiki jina kwenye bahasha, usifanye hayo ni mambo yake na siyo ya YESU.

    Pia uwe makini na umwombe YESU akuongoze mahali pa kutoa sadaka zako maana haijatosha kujua namna ya kutoa tuu pia ujue pa kutoa, kama mtumishi huyo ni wa kuzimu au nabii wa uongo sadaka zako kiasi Fulani kinaenda kwa mungu wake ambaye ni lusifa, na nyingine inabakia kwake na kwa njia hiyo unazidi kuangamia badala ya kubarikiwa, unaanza kufilisika maana roho ya mfilisi inatoka kwa shetani na ndiye mungu wa watumishi wa uongo, au kwa lugha yakueleweka sadaka yako inakuwa imeungana na wewe kwa hiyo ikienda mbinguni na wewe umeenda, ikipelekwa kuzimu na wewe umepelekwa. Haya yote kanifunulia YESU niueleze ulimwengu tena kwa ujasiri kabisa aliyenipa yeye maana shetani amechanganyikiwa na sasa hana kitu na ulimwengu unafunguliwa wote, na mimi siogopi natembea na YESU, yaliyofanyika gizani nayataja kwenye mwanga ili kila mtu ajue maana YESU ametaka hivyo na ndivyo ilivyo na haitabadilika milele.

    Watumishi wa uongo hawajachaguliwa na YESU wamejuchagua au kujiita wenyewe, na wengine wameitwa na shetani kabisa, maana kwanza hawa watumishi wanaenda kwa waganga wa kienyeji na wengine watoa makafara, wanalala makaburini, wanawanga usiku na mchana. Shetani anawatumia watumishi wa namna hii ili kuliangamiza kanisa na kulifanya kanisa liwe la masharti au sheria. Shetani huwa hawapi nguvu zake bure lazima wafanye agano nao, kwa mfano kutoa kafara au unakuta kanisa linguine watu  wanavuja damu hazikatiki, au mabinti au vijana hawaolewi wala kuoa, au kanisa linakua na wajane na ndoa zimevurugika kupita kiasi. Au mchungaji anabatiza kwa jina lake na siyo la YESU, na niwengi sana wamebatizwa na pia baada ya muda anakubatiza tena, anakuunganisha na lusifa, kwa hiyo wewe unakuwa siyo wa YESU wewe ni wa huyo mtumishi. Na madhara yake huyo mtumishi wa kipepo chochote atakachosema juu yako libaya lazima likupate. Maana wewe siwakwake japo umeokoka. Ubatizo ni kiapo kati yako wewe na YESU na ndiyo maana anasema (Mathayo 28:18-20) Enendeni mkawabatize kwa jina langu nakuwafanya kuwa wanafunzi wangu;  Hicho ni kiapo, ukiwa wa YESU hakuna mwenye uhalali juu yako, ni YESU peke yake tuu. Na kama ulibatizwa hivyo unaitajika kubatizwa upya na kuvunjiwa hayo maagano ili uwe wa YESU.

    Jambo lingine manabii wa uongo wanafundisha na kusema na kutoa baaadhi ya mistari ya maandiko eti ili likamilike juu yako lazima ulitolee sadaka, huo ni uwizi mbele za MUNGU na kwa kupitia injili ya YESU, hiyo ni namna ya watumishi wametekwa na shetani na kulinajisi kanisa la YESU hadi kuwa kanisa jina tu. Na mahali alipo Roho wa MUNGU yani Roho Mtakatifu akiwa ndani ya mtumishi huyu roho hawezi kumruhusu huyo mtumishi kuruhusu uchafu ndani ya kanisa, maana Roho Mtakatifu hawezi kuyakubali mambo yasiyo ya MUNGU, hivyo Roho Mtakatifu  huondoka. Wengi wameanza Rohoni kazi ya YESU na sasa wanamalizia mwilini. Ukikuta maombi yanafanyika mahali /kanisa  fulani au kwa mtumishi kwa pesa sio ya YESU. YESU humbariki mtu bure bali Baraka za shetani lazima uzilipie hakupi bure, mfano ukienda kwa mganga lazima atataka kitu kwako na kukuambia mungu wake anataka hivyo vitu ndio akujibu, maana shetani hatoagi kitu bure isipokuwa YESU tu na ndio maana YESU anasema “mmepewa bure na mtoe bure”. Sasa hivyo unavyo fanya kwa pesa ni vya shetani, ni ujanja shetani anaoutumia katika kanisa na wewe unaona ni YESU. YESU anakuponya bure,kuokoa bure na kukubariki bure. Hii pia ni njia nyingine ambayo shetani ameliteka kanisa na watumishi baadhi wamepofuka, wanafanya vitu ambavyo YESU alivyovikataa na kufanya kinyume na maagizo aliyoacha YESU! Funguka, omba toba wewe unayefanya hivyo, ujue hapo haufanyi kazi ya YESU, japo unalitumia jina lake, unafanya kazi ya shetani.

    Sadaka au pesa zozote unazoambiwa uahidi kutoa kuhusu kazi ya MUNGU, huo siyo mpango wa MUNGU, MUNGU siyo omba omba ni kumuaibisha MUNGU. Kama hiyo kazi ya injili unayoifanya ni ya YESU wewe mtumishi piga magoti muulize na umuombe yeye atafanya, wacha kutumia akili zako, watu wamechoshwa na michango ya kanisani mpaka hawatamani siku ya saba ifike (Jumapili). Badala ya injili ya YESU watuwaseme na YESU, mnawakaba kondoo vikao vya pesa tuu, Je, Nakuuliza wewe unayefanya hivyo ndiyo YESU kakupa kazi hiyo? Na zaidi ya haya watumishi walioiacha injili ya YESU huwatafuta waumini wenye pesa halafu huwaita (partners wake) kila mwezi anawapangia kiasi cha kutoa ili kumsaidia aishi vizuri na kufanya kazi ya MUNGU. Na wewe ukiambiwa umechaguliwa kuwa partner, unafurahi sana, yaani ni bora Yule ambaye hajachaguliwa huyo atabarikiwa sana. YESU hana ubaguzi na YESU watu wote ni wanafunzi wake. Hapo ni mtumishi ametekwa na shetani kwa tamaa ya pesa. YESU amewaita watumishi kuokoa na kuponya Roho zilizopotea na zinazoteswa na shetani, na akasema msijisumbukie  mtakula nini, mtaishije, yeye mwenyewe atawashughulikia, kwani mana na ndege si bora kuliko nyie? MUNGU huwalisha na kuwatunza na wanapendeza. Partner ni mtu yeyote mfuasi wa YESU awe anahela au hana, anavyokwenda kanisani anamfuata YESU na siyo mtumishi, wewe unayemfuata mtumishi badala ya YESU umelaaniwa, anza kumfuata YESU tu.

    Nakupa mfano halisi ulionitokea, mimi siku mmoja nilikuwa mahali Fulani na watumishi, mmoja wao akaniambia wewe wacha kupoteza muda tafuta pesa sikumuelewa, nikaona ni jambo jema ananiambia, akaanza kuniambia bwana wewe sasa hivi hapo kanisani kwako tafuta wamama sitini (60) wa nguvu uwafanye partners wako na kila mwezi, kila mmoja akupe shilingi laki moja, mara sitni (100,000*60= 6,000,000) Je, hapo haujauchinja? Kila mwezi unaingiza (6 milioni) zako mfukoni. Kwa kweli niliishiwa nguvu, nilipofika nyumbani BWANA akaniambia nilitaka uyasikie na ujue na uwaelewe hawa watumishi, hii ni namna moja wapo ya kunisaliti maana mimi sijaruhusu hayo huu ni unyanganyi: Tena hawa partners mpaka wanakopa pesa ili wapeleke pesa kwa mtumishi, YESU akaniambia jiulize mtu akinitolea mimi anaishiwa hadi kukopa? Nikamjibu hapana, akaniambia hizo pesa sio zangu ni za mambo yao na sababu watu wanawaamini kupitia jina langu na wanalitumia vibaya. Nilishangaa sana na kuogopa. Nakusihi usifanye hivyo na kama ni mtumishi wacha, utubu, urejee upya kwa YESU huo ni unyanganyaji. YESU hataki na hasira ya MUNGU itakua juu yako, wacha unyang'anyaji.

    Namna nyingine unakuta eti mtumishi anavaa suti anasimama mbele yenu anajifanyia mnada na kuwa laghai kutoa kiasi fulani cha pesa unaandika kwenye suti au gauni alilovaa unaandika kiasi na unapiga saini yako kwenye suti au nguo aliyoivaa, tena watu wanapanga foleni na kupigania mstari. Hiyo ni namna shetani anachukua uchumi wako na wewe mwenyewe umekubali kwa saini yako mwenyewe. Hapo uchumi wako na Baraka zako zinapelekwa kwa lusifa na lusifa anawapatia wale wanao muabudu yeye (Freemason) na wewe ndiyo shida zinazidi. Kama ulishafanya hivyo, mwambie mtuimishi anayetumika na YESU wa kweli akufungue na utakua huru kweli kweli, milele na daima.

    Ukikuta mtumishi anafukia majina yenu au lako au picha yako au pesa yako au chochote chako hii ina maana anakuzika na hiyo siyo madhabahu ya YESU hapo ni full kwa shetani. Kimbia kwa usalama wako utaponywa kiroho na kimwili haya yote ni YESU ndiye anayayenifunulia ili wewe upate kupona maana anakuona unavyoteseka, hii yote ni sababu watumishi wamemsaliti, hawasemi kweli ni uongo na kufanya yasiyo ya YESU.

    Jinsi nyingine ya kumjua mtumishi ambaye analitaja jina la YESU na YESU hayupo ndani yake haijalishi anafanya miujiza, hiyo ni ya shetani haitoki kwake YESU. Mtumishi anayekuwa na daftari la mahudhurio ya utoaji sadaka au siku ya ibada anasoma listi ya majina ya watu waliotoa fungu la kumi hadharani, hapo unauwawa kiroho na MUNGU hajaruhusu bali shetani karuhusu, sasa mtumishi anatakiwa afanye ya MUNGU au shetani? Akifanya yashetani ina maana shetani ndiye amemtawala, akifanya mapenzi ya MUNGU huyo ametawaliwa na MUNGU. Mtumishi anayewanyang’anya watu na kufunga huduma zao, huyo siyo mtumishi wa YESU maana YESU hanyang’anyi mtu nyota yake, wala Baraka za maisha yake. Mtumishi yeyote anayetoa vyeti vya hongera kwa ajili ya kutoa sadaka huyo amepotea au ametekwa.

    Watumishi wa uongo ndani yao shetani amewawekea roho za majini ya utambuzi, majini ya maandiko, jini muhubiri, akisimama kuhubiri utasema kweli umemuona MUNGU kumbe umemuona shetani ndani yake. Wanachokifanya ili msiwatabue unapokuwa kanisani hapo kwanza wanakuua macho yako ya Rohoni ili uwe kipofu usiyaone anayoyafanya kwa kutumia nguvu za giza na wakishindwa au akishindwa ataanza kukuchukia sana, au anakuita majina ya mapepo aliyo nayo ya utambuzi au agenti, japo kuna agenti wa kweli. Ikishindikana anakufukuza kimwili lakini wakati huo umechafuliwa hata watu wanakuogopa na wanafanya hivyo ili ukimbiwe na watu maana wakiwa karibu na wewe utawaambia na wao watafunguka na ukweli ujulikane na watu watamkimbia.

    Pia ndugu msomaji ukimkuta mtumishi anasema mfano, mungu wake amekuonekania, naomba uwe makini sana maana MUNGU tunayemjua ni MUNGU wa Ibrahim, Isaka na Yakobo. Shetani amekuwa akilikamata kanisa au waumini kwa kujipatanisha na mungu wa mtumishi Fulani kwa kutaja jina lake, kama huyo mtumishi anaongozwa na shetani inamaana mungu wake ni shetani na wewe unaunganishwa, maana pia tunajua ipo miungu mingi, yote ni ya uongo kasoro MUNGU wa Ibrahim, Isaka na Yakobo na huyu ndiye MUNGU aliyeumba vitu vyote ikiwa pamoja na wewe sasa kwa nini usimuabudu yeye, tena amefanana na wewe, amekuumba kwa mfano wake, cha ajabu haumtaki unahangaika na miungu mengine. Unapokuwa unaiabudu miungu ya uongo ina maana umefanana nayo, na ndiyo maana MUNGU alikuumba wewe kwa mfano wa sura yake ili umuabudu yeye. Je, wewe unamuabudu MUNGU yupi? Muabudu MUNGU wa kweli na ili umfikie ni lazima uokoke na YESU ndiye kiunganishi cha kweli, wengine wote ni waongo.

    Ndugu msomaji wa kitabu hiki, MUNGU akubariki sana kwa kujua ukweli ambao shetani ameliteka kanisa na pia ni jinsi ya YESU kuwafichua hadharani mambo yao wanayo yafanya kanisani kwa kutumia jina la YESU na kusababisha watu wazidi kuteseka kanisani, sababu kubwa ni baadhi yao ulimwenguni mwote siyo waaminifu katika kufanya kazi ya YESU badala yake ni roho ya shetani inafanya kazi ndani yao wengine wakiwa wanajua wao ni maajenti wa shetani na wengine hawajielewi, wametekwa, wanatumikishwa wakijua wanafanya kazi ya YESU kumbe siyo. Ujumbe huu uwaeleze na wenzako, ndugu, jamaa, marafiki ili wasije wakatekwa na wao na kila mtu amtegemee YESU tu, maana nyakati hizi ni za hatari YESU yu karibu kuja na shetani anafanya bidii zaidi ili apate idadi kubwa ya watu wachomwe naye jehanamu kwenye shimo la moto. Ndugu msomaji YESU akufungue ufahamu wako na akili yako na macho ya rohoni ili uweze kuona na usikamatwe na adui. Na zaidi usiogope maana YESU ameniambia tayari ameshaanza mapinduzi kwenye ulimwengu waroho na mwisho wao hao wataabishaji umefika na malango yao ya kuzimu YESU ameyafunga na baba yao lusifa hana nguvu tena. Hakuna amani kwa wabaya asema Bwana Wa Majeshi.!

    Kwa wewe ambaye haujaokoka soma sala hii:-
    BWANA YESU, nipo mbele zako mbele ya agano la Damu ya YESU, naomba unisamehe dhambi zangu zote, uliandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele, namkataa shetani na kazi zake zote, kuanzia leo mimi ni mali yako YESU, nishike mkono uniongoze milele, Amen. !!

    Mpaka hapo utakuwa umeokoka na mara umalizapo sala hii ,malaika Mkuu Mikael akushukilie hapo ulipo, akulinde milele na shetani asikupate tena katika jina la YESU KRISTO WA NAZARETI. Hongera umeokoka sasa, MUNGU akuongoze kanisa lolote ambalo yeye yupo hapo.

    Kwa kumalizia, lengo kubwa kuhusu ujumbe huu pia ni kukujulisha haya yanayofanywa kanisani, ndiyo maana majibu kutoka kwa MUNGU hayapatikani na ndiyo maana kanisa linateseka yani watu wanateseka, siyo YESU anawatesa ni shetani anawatesa na matokeo yake watu wanaona MUNGU hajibu, wanaenda kwa waganga na ndiyo maana watu wamemuacha YESU. Wamekua washirikina na huko ndiko wanapoenda kuangamia milele maana shetani ndiyo anawatumikisha haswa na mwisho wake wanafia dhambini na kuangamia milele. Kazi na maagizo aliyonipa YESU, niwatoe huko walipotekwa wana wa MUNGU haijalishi umeshikiliwa wapi utafunguliwa hapo hapo (live!live!). Na madhabahu zote za shetani hazina mamlaka tena katika jina la YESU KRISTO na wafuasi wake wanajijua wenyewe. Malaika Mikael na kikosi chako kila siku teketeza na kuangamiza jeshi la shetani ,na wana wa MUNGU sasa wapumue wamfurahie YESU nawaone Baraka zao na YESU awakumbatie milele daima, na kila asomaye, Bwana YESU nakuomba umponye na awe na wewe siku zote, Amen.


    MASOMO YA ZIADA:-
    Mathayo 10:8
    Mathayo 6:1- 4
    Mathayo 7: 15- 19
    Mathayo 6: 25- 26
    Mathayo 15: 8- 14
    1 Wakorintho 3: 16- 17
    Warumi 10: 9-11
    Wagalatia 1: 6- 8
    Wagalatia 1: 11- 12

    YESU akuponye roho yako na maisha yako na majeraha yote uliyojeruhiwa na shetani. YESU AKUBARIKI SANA, UTUKUFU WAKE NA MKONO WAKE UWE JUU YAKO.

    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate