YALIYOMO
·
KANISA NI NINI
· HEKALU LA BWANA
· WATUMISHI WAMEMSALITI YESU
· WATUMISHI WANAFUNDISHA MAFUNDISHO YASIYO YA YESU
· SABABU YA KANISA KUTOKUJIBIWA NA MUNGU
· WATUMISHI KUNYANG'ANYA MALI ZA WATU, PESA NA KUMFANYA YESU AITWE MNYANG’ANYI
· WATUMISHI 98% WAMETEKWA NA SHETANI ULIMWENGUNI MWOTE
· NAMNA YA KUPONA USITEKWE
TOLEO
LA KWANZA
APRIL
2012
ISBN
978-9987-9553-1-2
UTANGULIZI
Ndugu nakusalimu kwa
jina la YESU KRISTO, ambaye ndiye BWANA na mwokozi wa mataifa yote, pia ndiye
mfalme wa wafalme na bwana wa mabwana na hapana mfalme mwengine zaidi yake.
mimi jina langu naitwa Hebron Wilson Kisamo, YESU amenichagua nimtumikie yeye
kwa jinsi anavyotaka yeye ili kukomboa ulimwengu huu ambao umepotea na shetani
ameumiliki kwa asilimia 98% sawa sawa na YESU alivyoniambia mwenyewe. Amenituma
ulimwenguni kote ikiwa ina maana nchi
zote, mabara yote.
Ujumbe huu aliniagiza rasmi na kunipa mamlaka yake tarehe
14.6.2010. Na akanipa jina la kanisa lake niliite YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA
MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRY. Akaniambia mwanangu nitautumia huu mwili
wako kuukomboa ulimwengu wote, utachukiwa sana,
utafanyiwa na kuitwa majina mabaya lakini usiogope tena ufurahi zaidi, kwani
mimi YESU walinifanyia mabaya zaidi na ya uongo yakitokea kwa baba yao wa uongo ambaye ni
lusifa, nilifurahi daima. Hakuna jambo lolote litakalofanikiwajuu yako au
silaha yoyote juu yako nipo na wewe milele. Nitakutumia kwa namna ya tofauti na
kwa kiwango kikubwa sana
ambacho hakijaonekana tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu. Adui yako ni
adui yangu, akasema YESU kwa sauti ya uchungu sana, watumishi wamenisaliti maagizo
niliyowapa hawayafanyi na wamegeuza neno langu kuwa maandiko badala ya neno,
maandiko yanatoka kwa shetani maana lusifa anaijua bibilia yote na maandiko
hayana uthibitisho wa nguvu zake YESU. Neno linatoka kwa YESU na
linaudhihirisho wa nguvu za MUNGU. Na pia wana wa Adamu wanateseka wanalia na
kuomba hawapati majibu, na zaidi wanazidi kupotoshwa na viongozi wa kanisa,
maagizo niliyoyaacha nilivyokuwa ulimwenguni kabla ya kurudi kwa BABA yangu ili
kuniandalia maandalizi ya ujio wangu ili nipate kuwaponya wengi waende
mbinguni, imekuwa kinyume idadi kubwa ni ya watu wa shetani. Waliokuwa
watumishi wangu wamenisaliti 98% sipo nao. Wameamua kwenda kuzimu, na shetani
anawatumia na jinsi anavyowatumia, ni kubadili au kwenda kinyume na agizo la
MUNGU, mfano watumishi kwa sasa wamefanya kanisa ni mahali pa biashara,
kunyanganya watu vitu vyao na wakijua wananitolea mimi, na kufanya mimi YESU
ndiye mnyanganyi, kwa midomo yao hunitaja kama wananipenda ila mioyoni mwao
hawapo na mimi, wamekuwa watumishi wa pesa na siyo mimi, wamekuwa wakitenda
miujiza lakini siyo yangu ni miujiza ya shetani, na hao ni kati ya wale ambao
siku ya mwisho nitawakataa na kuwaambia sikujui. Kanisa limeniacha kunitegemea
mimi, imebaki 2% tu ulimwengu mwote. Sasa mimi YESU ninalikomboa kanisa
mwenyewe na ndipo unabii na utukufu wa kanisa la mwisho utakuwa mkubwa kuliko
wa kanisa la kwanza unatimia sasa.
SHUKURANI
- Namshukuru mke wangu sana kwa kunitia moyo na kuniombea, nawashukuru watumishi wote wanaoniombea na kutumiwa na MUNGU kutumika pamoja na YESU aliyeniita, mkono wa MUNGU uwe juu yao siku zote za maisha yao.
Asante.
MTUME
NA NABII- HEBRON
WILSON KISAMO
KIONGOZI
NA MWANZILISHI WA HUDUMA
P.O.BOX 13657
ARUSHA, TANZANIA
EAST AFRICA
KANISA NI NINI?
Kanisa ni YESU, na
wewe unafanyika kuitwa kanisa la YESU baada ya YESU mwenyewe kuingia ndani
yako. Kanisa ni nyumba ya MUNGU kwa ajili ya sala, kanisa ni mahali pa kuongea
na YESU, na YESU ndiye njia ya uzima na kweli na hakuna mtu yeyote atakaye
kwenda mbinguni bila kupitia njia ya YESU. YESU ambaye ndiye mfalme wa wafalme na
bwana wa mabwana, ndiye mwanzo wa kanisa la kweli. YESU ni mtakatifu na
hakufanya dhambi, alikuja ulimwenguni ili aukomboe ulimwengu na alifundisha
yote aliyoagizwa na MUNGU BABA na akatulipia deni zetu zote pale msalabani kwa
mateso magumu mpaka kupigwa viboko ili sisi tupone. Ukisoma katika kitabu cha
injili ya Mathayo 21: 12- 17 YESU aliingia hekaluni ambapo ni nyumba ya sala
akawakuta watu wakifanya biashara, kubadilishana vitu, pesa na mengineyo, kwa
hasira aliwafukuza na kutupa kila kitu hata mifugo, akawaambia imeandikwa
nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala, bali ninyi mmeifanya nyumba ya wanyanganyi
akawafukuza na YESU akaingia hekaluni na watu waliokuwa na vifungo vya shetani,
wakamfuata YESU hekaluni na YESU akawafungua na kuwaponya. Ndugu msomaji,
naomba uelewe na usidanganyike tena, kanisa sasa hivi limeyapuuzia mafundisho
yake YESU aliyoaagiza na zaidi usipo yafuata maagizo ya YESU hayo ni kumdharau YESU,
wanadamu hofu ya MUNGU haipo na wanamzoea MUNGU kama
watu wanavyozoeana. , YESU alivyoyakataa mambo hayo inamaana ni ya shetani
yangekuwa ni ya MUNGU angeyaruhusu yafanyike kanisani. YESU alikuja kukomboa
kanisa yani hekalu la MUNGU maana shetani alishaingia ndani yake na katika
injili hii ya Mathayo 21:12-17 tunaona jinsi YESU KRISTO alivyoyatoa mambo ya
shetani kwenye hekalu na alipo yatoa ndipo YESU akaweza kuingia hekaluni na
ndipo watu waliokuwa wanatafuta majibu walimwona na wakajibiwa au kuponywa.
Ndugu msomaji, leo hii mambo aliyoyakataa YESU yasifanyike kanisani
yamerudishwa yote na mengine ni zaidi na zaidi yameongezeka na mambo hayo
yanamfanya YESU asiwepo makanisani na ndiyo maana wakristo yaani mfuasi/wafuasi
wa Kristo mnakata tama na ukristo maana hamna majibu au uponyaji na haya
yanafanywa na watumishi ambao mioyo yao ni migumu haitaki kumtii YESU.Na YESU
hakai mahali au katika kanisa ambalo haliyafuati mambo ambayo muasisi wa kanisa
yani YESU aliweka muongozo aliopewa na MUNGU na kanisa kuyapuuzia, hiyo ni njia
moja wapo inayomhuzunisha YESU, kanisa la YESU linafuata maagizo aliyoyaagiza
yeye na ndugu msomaji mshukuru YESU kwa ajili ya mafunuo ili ulimwengu upone.
Siku hizi kuna makanisa aina mbili japo yote yanaitwa makanisa, na shetani
amewakamata na kuwapiga upofu ili watu wajijue wapo salama lakini leo hii YESU
anakufungua umjue YESU wa kweli maana pametokea wakristo wa uongo na ndiyo
wengi sana, japo hao wanaohusika wanajijua wanafanya nini ili kuharibu kazi ya
YESU. Sasa mwisho wa hao wanaoiharibu kazi ya MUNGU kwa kutumiwa na shetani
mwisho wao umefika na sasa wanakwenda kuaibika katika jina la YESU, haya ndiyo
aliyoniambia Bwana wetu YESU KRISTO.
KANISA LA YESU WA KWELI
Kanisa la YESU wa
kweli analiongoza mwenyewe na halipingi au kubadilisha neno kwenda kinyume.
Kanisa la kweli lina majibu yako, na Baraka zako za rohoni na mwilini unazipata,
Live Live. Kanisa la YESU wa kweli watumishi wake siyo walevi, siyo wachawi,
siyo wanyang’anyi, hawavuti sigara, hawana mambo ya kidunia, hawaombei watu
maombi mabaya, hawatumii jina la YESU kujitafutia mali, hawafundishi mafundisho
ya uongo kwa faida zao, siyo wabinafsi, ,tabia zao zimefanana na za YESU na
mtumishi anayetumiwa na YESUndani yake ni YESU anakaa na kama YESU anakaa ndani
yake nilazima YESU ayafanye yale YESU anayoyataka maana mtumishi wa YESU
anaongozwa na YESU tu. Kanisa la YESU wa kweli lina macho yaliyohai kama YESU
alivyo mwenyewe, Kanisa lake lina nguvu zake tena hata milango ya kuzimu
haliwezi. Kanisa la YESU linaongozwa kwa ushirikiano wa MUNGU BABA, MWANA NA
ROHO MTAKATIFU. Na kazi zao pia ni kuhakikisha yale yote yanayotakiwa yatendeke
na MUNGU, yatimie na siyo yasitimie au kuyabadili, maana unabii uliyoandikwa
katika kitabu cha injili kutoka kwa MUNGU ni muongozo wa kumfuata yeye kwa hiyo
ili kupona lazima kufuata anayoyataka. Soma ufunuo wa yohana 22;18-20.
MTUMISHI WA YESU WA KWELI
Mtumishi wa YESU ni
lazima aweameokoka, na pia lazima apitie ubatizo kama wa YESU wa maji mengi
kama alivyobatizwa yeye, Je? Jiulize ubatizo huu mwingine umetoka wapi?
Kuanzia Yohana alitumwa abatize kwa maji mengi katika kijito cha utakaso
na YESU alibatizwa hivyo hivyo, sasa ili ukamilike ni lazima ubatizwe kama YESU
ndiyo utakamilika uwe mkamilifu. Mtumishi wa YESU hachangishi pesa kanisani,
hakunyang’anyi mali zako, mfano nyumba, gari na vinginevyo kwa kutumia jina la
YESU. Mtumishi wa YESU hatoi vyeti vya hongera kwa kutoa fungu la kumi kwa
uaminifu.. YESU alishayakataa hayo mambo maana hayatoki kwa MUNGU na ndiyo
sababu ukuu wa MUNGU hauonekani. Watumishi wanaomtumikia YESU wa kweli
hawafanyi biashara haramu, mfano madawa ya kulevya. Watumishi wa kweli
hawalitumii kanisa kufanya biashara. YESU alishayakataa na neno linasema kweli
na zaidi wapo watumishi wa kweli ambao wamenajisika kutoka kwa baba zao wa
kiroho na kujikuta wamejiingiza kwenye uchafu na ili wawe safi ni lazima
waoshwe na Damu ya YESU upya, tena aamue mwenyewe kutoka rohoni aombe rehema,
na MUNGU atamsamehe maana MUNGU wetu ni wa rehema.
WATUMISHI WA UONGO
Watumishi wa uongo
kwanza kabisa hutumia jina la YESU kukupofusha japo wanaongozwa na kiongozi wa
uongo yaani shetani. Kazi yao kubwa ni kusema uongo, kubadilisha neno kuwa
kinyume na maagizo aliyoyaacha YESU mfalme wa wafalme ili aweze kulihudumia
kanisa lake, na shetani hutumia njia hiyo moja wapo japo zipo nyingi
nitakueleza baadhi.
Kwanza kabisa
shetani amewawekea roho yakupenda pesa, na jinsi wanavyowakamata waumini ambao
ni kondoo wa YESU, hutumia njia ya sadaka na kufanya michango michango
wanamwaibisha YESU, kama YESU ameishiwa, YESU sio masikini. Japo neno linasema
katika kitabu (Mathayo 6:2-4) utoapo sadaka yako hata mkono wako wa kulia au
kushoto usijue, hapa neno la MUNGU lina maana kwamba sadaka ni siri yako wewe
na MUNGU tu, sadaka ni ibada yako kamili kati yako wewe na MUNGU na hapaswi mtu
yeyote kujua au kuona sadaka yako inapokuwa imeonekana au kujulikana na mtu
yeyote tayari thawabu yako imebaki kwa watu uliyowaonyesha hivyo, utapata
thawabu kutoka kwa watu na siyo kwa MUNGU. Sasa shetani amelikamata kanisa 98%
ulimwengu wote ili wewe usibarikiwe maana haufuati atakavyo MUNGU. Wanawaambia
watu waandike sadaka majina yao wakati neno la MUNGU limekataa, sasa huo ni
mpango wa YESU au wa shetani? Jibu ni shetani. Shetani amewaongezea tamaa
nyingi na zimewashika kwenye pesa na wameongeza majina mengi ya sadaka. Sadaka
ya kweli ni fungu la kumi na sadaka ya shukurani au hiari yako kwa MUNGU. Leo
hii kuna majina ya sadaka hata hayaelezeki, mfano sadaka ya injili, ujenzi,
nabii, ulinzi, afya, ukombozi na nyinginezo nyingi mpaka ni aibu kuzisema jinsi
muenendo aliouacha YESU umeachwa. YESU ameniambia sizo za kweli. Pesa zote za
kanisa ni kwa ajili ya kazi yake umekuwa ukitoa mpaka unafilisika maana yake
haukumtolea yeye, maana ungemtolea yeye angekubariki sawa sawa na ahadi za
MUNGU (Malaki 3:10-12). Zaidi mwana wa MUNGU nimekuwa nikiletewa kesi na
manunguniko ya wana wa MUNGU kuhusu kilio kikubwa walichonacho inawezekana pia
na wewe ni mmoja wao au unayoshida hiyo hiyo. Tena watumishi wanafundisha toa
mpaka roho ikuume MUNGU ndiyo anapendezwa na sadaka kama hiyo! Huo ni uongo
wala usidanganyike tena wewe ni wa thamani sana mbele za MUNGU na YESU, kupitia
kusoma kitabu hiki unafunguliwa katika jina la YESU. Sadaka yako unatakiwa utoe
kwa upendo kutoka moyoni na ni siri yako. Usifanye kama Kaini, soma Mwanzo
4:2-16, Abeli alimtolea MUNGU sadaka kwa moyo mweupe na msafi MUNGU aliipokea
na Kaini alimtolea MUNGU kwa moyo wa kuuma na uchungu! Sadaka ya uchungu MUNGU
haipokei maana inakuwa kama amekunyanganya na yeye siyo MUNGU wa kunyanganya.
Madhara yake haubarikiwi maana hajapokea na kama hajapokea yupo aliyepokea yaani
shetani, na shetani akishapokea anakupatia Baraka zake; nuksi, balaa, mikosi,
umaskini na kufilisika na mwishowe unakosa mwelekeo unakuwa kama Kaini, mpaka
leo anazurura tu, sababu ya kuwa na uchungu wa kumtolea MUNGU. Hii roho
haikuanza leo, tokea enzi za kina Kaini na Abeli na sasa huu ujanja shetani
ameurudisha tena katika kanisa ili watu waagamie kama Kaini. Mwana wa MUNGU
kataa usidanganyike tena, mtolee MUNGU kwa moyo mweupe.
YESU anasema yeye
hakopi bali yeye ndiye anakopesha, leo hii huu usemi aliousema yeye kanisa
lisikope, leo kanisa ndilo linakopa na likikopa tayari YESU hayupo hapo ni
mpinzani wa YESU. Shetani ili kuwa na majengo mengi amelikamata kwa namna hiyo
na likikopa tayari YESU hashuki hapo tena, ibada inakuwa ya kutiana moyo na
siyo YESU na ndipo watu wanaangamia na roho za wana wa MUNGU kuteseka maana
hapo panakuwa siyo madhabahu yake tena, wao wanaona wanafanya kazi ya YESU
kumbe siyo, haya yote ameniambia YESU niwaeleze ulimwengu mzima wapate kuijua
kweli yake na ole wao walioibadili injili Wagalatia 1: 6- 10. Akaniambia japo
utapingwa na hao wanaoibadilisha injili ya YESU wewe niangalie mimi tu, maana
nimekuita na kukuchagua unitumikie kwa namna ya KIMUNGU na siyo ya kibinadamu.
Mfano ni kama nilivyomtumia Paulo, ila nitakutumia zaidi, wewe siyo mtume wa
kibinadamu ni mtume niliyekuteua mimi, nitakutumia hivyo hivyo ulivyo
nimependezwa na wewe mimi YESU.
YESU anahuzunika
sana juu ya kanisa kumwaibisha na zaidi anasema kanisa linaitwa kwa jina lake,
eti mimi YESU kila mwezi nirejeshe marejesho yaani mimi YESU nadaiwa na bank?
Mimi YESU sipo katika kanisa hilo japo wanalitaja jina langu. Na kondoo wake
wanashurutishwa kulipa deni la riba, mimi YESU nimesema kwenye neno langu
ukimkopesha mtu usitake riba kwake, je mimi kanisa langu lilipe riba na mimi
mmiliki wa kanisa sitaki? Hapo sipo nawao mwisho wao umefika na hukumu
inawasubiri.
Watumishi wa uongo
pia wamekuwa wakifanya miujiza kwa kupitia nguvu za giza japo wanalitaja jina
la YESU lakini miujiza wanayoifanya haidumu, mtu anafunguliwa lakini akiondoka
hapo yanamrudia. Mfano unakuta watu wakienda kwenye kanisa au mikutano ya
injili huwa wanatupiwa mapepo kutoka kuzimu yanawaangusha watu na watu wanasema
nguvu za MUNGU zimemshukia na kumbe siyo. Na ujanja mwingine kwa sababu huyo
mtumishi anaongozwa na lusifa wanachokifanya watu wenye mapepo wanajiunganisha
na kuzimu mapepo yanapiga kelele halafu baada ya muda wananyamaza, mnaona
amefunguliwa kumbe hakuna kitu yanapiga kimya. Hii yote ni kuwapofusha muzubae
na mnyang’anywe pesa zenu, na huyo. Au hao walioanguka hali yao huzidi kuwa
mbaya siku kwa siku.
Ukombozi wowote au
maombi unayofanyiwa halafu unaambiwa leta pesa kiasi Fulani MUNGU anataka hiyo
pesa au mifugo au chochote, hapo umedanganywa. Neno la MUNGU linasema “Mmepewa
bure toa bure,” hayo unayoambiwa siyo ya YESU ni ya shetani (Mathayo 10: 8).
Watumishi wa uongo
hufanya kazi ya MUNGU kama mradi wao na kuwafanya waumini (ATM MACHINE) YESU
hakufanya hivyo au director wa kanisa, haya yametokea wapi? Jibu kwa shetani.
Kanisa lenye matabaka ya watu mfano matajiri wanajitenga na maskini hivyo hivyo
mahali hapo upendo wa kikweli wa YESU haupo ni upendo wa kinafiki, mfano kama
hauna pesa au kauwezo kidogo mtumishi hakupendi au kukuombea na kukujali
anawajali wenye pesa tu ,na wewe usiyekuwa nacho hana mda na wewe. Mahali hapo
ujue YESU ameondoka siku nyingi, maana sisi watu wote ni wa YESU na safari yetu
ya mbinguni ni moja na anayetuongoza ni jemedari mkuu YESU hana ubaguzi anao
upendo. Mtumishi wa namna hiyo tayari shetani amemkamatia kwenye pesa.
Tunajua kuwa sasa
sadaka ni siri yako na MUNGU, sasa kwa nini unaambiwa uandike jina lako tena
hata namba za simu? Kwani MUNGU aliye sirini hakuoni? Haya mafundisho
yametokea wapi ? Jibu siyo ya MUNGU, sasa amua mwenyewe na ujue jinsi ya kumtolea
MUNGU sadaka na zizungumze na MUNGU na siyo na watumishi. Shetani ametumia huo
ujanja badala sadaka MUNGU anenenayo na uinuliwe, sasa sadaka yako inanena na
mtumishi au watunza pesa. Madhara ya sadaka yako kujulikana na watu badala ya
MUNGU hupati Baraka zake unapata Baraka za watu na kama hawakupendi, wana wivu
juu yako hayo maroho yanaingia kwenya kazi zako na biashara zako. Ila MUNGU
ndiye mwema tuu juu yako anakuwazia mema na amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu,
amebarikiwa amtegemeaye MUNGU. Siri ya sadaka yako mwandamu akijua umelaaniwa,
siri ya sadaka yako ikijulikana na MUNGU tu umebarikiwa. Kuanzia sasa ndugu
msomaji na mpenzi wa YESU anayekupenda ufunguke ufahamu wako ili uanze
kubarikiwa zaidi na uinuliwe. Sadaka ni haki yako na MUNGU, wala mtumishi
yeyote hanaruhusa kujua unatoa kiasi gani ni YESU peke yake tu. Na watumishi
wengine watakuambia haumtii kwa nini hauandiki jina kwenye bahasha, usifanye
hayo ni mambo yake na siyo ya YESU.
Pia uwe makini na
umwombe YESU akuongoze mahali pa kutoa sadaka zako maana haijatosha kujua namna
ya kutoa tuu pia ujue pa kutoa, kama mtumishi huyo ni wa kuzimu au nabii wa
uongo sadaka zako kiasi Fulani kinaenda kwa mungu wake ambaye ni lusifa, na
nyingine inabakia kwake na kwa njia hiyo unazidi kuangamia badala ya
kubarikiwa, unaanza kufilisika maana roho ya mfilisi inatoka kwa shetani na
ndiye mungu wa watumishi wa uongo, au kwa lugha yakueleweka sadaka yako inakuwa
imeungana na wewe kwa hiyo ikienda mbinguni na wewe umeenda, ikipelekwa kuzimu
na wewe umepelekwa. Haya yote kanifunulia YESU niueleze ulimwengu tena kwa
ujasiri kabisa aliyenipa yeye maana shetani amechanganyikiwa na sasa hana kitu
na ulimwengu unafunguliwa wote, na mimi siogopi natembea na YESU, yaliyofanyika
gizani nayataja kwenye mwanga ili kila mtu ajue maana YESU ametaka hivyo na
ndivyo ilivyo na haitabadilika milele.
Watumishi wa uongo
hawajachaguliwa na YESU wamejuchagua au kujiita wenyewe, na wengine wameitwa na
shetani kabisa, maana kwanza hawa watumishi wanaenda kwa waganga wa kienyeji na
wengine watoa makafara, wanalala makaburini, wanawanga usiku na mchana. Shetani
anawatumia watumishi wa namna hii ili kuliangamiza kanisa na kulifanya kanisa
liwe la masharti au sheria. Shetani huwa hawapi nguvu zake bure lazima wafanye
agano nao, kwa mfano kutoa kafara au unakuta kanisa linguine watu
wanavuja damu hazikatiki, au mabinti au vijana hawaolewi wala kuoa, au kanisa
linakua na wajane na ndoa zimevurugika kupita kiasi. Au mchungaji anabatiza kwa
jina lake na siyo la YESU, na niwengi sana wamebatizwa na pia baada ya muda
anakubatiza tena, anakuunganisha na lusifa, kwa hiyo wewe unakuwa siyo wa YESU
wewe ni wa huyo mtumishi. Na madhara yake huyo mtumishi wa kipepo chochote
atakachosema juu yako libaya lazima likupate. Maana wewe siwakwake japo umeokoka.
Ubatizo ni kiapo kati yako wewe na YESU na ndiyo maana anasema (Mathayo
28:18-20) Enendeni mkawabatize kwa jina langu nakuwafanya kuwa wanafunzi
wangu; Hicho ni kiapo, ukiwa wa YESU hakuna mwenye uhalali juu yako, ni
YESU peke yake tuu. Na kama ulibatizwa hivyo unaitajika kubatizwa upya na
kuvunjiwa hayo maagano ili uwe wa YESU.
Jambo lingine
manabii wa uongo wanafundisha na kusema na kutoa baaadhi ya mistari ya maandiko
eti ili likamilike juu yako lazima ulitolee sadaka, huo ni uwizi mbele za MUNGU
na kwa kupitia injili ya YESU, hiyo ni namna ya watumishi wametekwa na shetani
na kulinajisi kanisa la YESU hadi kuwa kanisa jina tu. Na mahali alipo Roho wa
MUNGU yani Roho Mtakatifu akiwa ndani ya mtumishi huyu roho hawezi kumruhusu
huyo mtumishi kuruhusu uchafu ndani ya kanisa, maana Roho Mtakatifu hawezi
kuyakubali mambo yasiyo ya MUNGU, hivyo Roho Mtakatifu huondoka. Wengi
wameanza Rohoni kazi ya YESU na sasa wanamalizia mwilini. Ukikuta maombi
yanafanyika mahali /kanisa fulani au kwa mtumishi kwa pesa sio ya YESU.
YESU humbariki mtu bure bali Baraka za shetani lazima uzilipie hakupi bure,
mfano ukienda kwa mganga lazima atataka kitu kwako na kukuambia mungu wake
anataka hivyo vitu ndio akujibu, maana shetani hatoagi kitu bure isipokuwa YESU
tu na ndio maana YESU anasema “mmepewa
bure na mtoe bure”. Sasa hivyo unavyo fanya kwa pesa ni vya shetani, ni
ujanja shetani anaoutumia katika kanisa na wewe unaona ni YESU. YESU anakuponya
bure,kuokoa bure na kukubariki bure. Hii pia ni njia nyingine ambayo shetani
ameliteka kanisa na watumishi baadhi wamepofuka, wanafanya vitu ambavyo YESU
alivyovikataa na kufanya kinyume na maagizo aliyoacha YESU! Funguka, omba toba
wewe unayefanya hivyo, ujue hapo haufanyi kazi ya YESU, japo unalitumia jina
lake, unafanya kazi ya shetani.
Sadaka au pesa
zozote unazoambiwa uahidi kutoa kuhusu kazi ya MUNGU, huo siyo mpango wa MUNGU,
MUNGU siyo omba omba ni kumuaibisha MUNGU. Kama hiyo kazi ya injili unayoifanya
ni ya YESU wewe mtumishi piga magoti muulize na umuombe yeye atafanya, wacha
kutumia akili zako, watu wamechoshwa na michango ya kanisani mpaka hawatamani
siku ya saba ifike (Jumapili). Badala ya injili ya YESU watuwaseme na YESU,
mnawakaba kondoo vikao vya pesa tuu, Je, Nakuuliza wewe unayefanya hivyo ndiyo
YESU kakupa kazi hiyo? Na zaidi ya haya watumishi walioiacha injili ya YESU
huwatafuta waumini wenye pesa halafu huwaita (partners wake) kila mwezi
anawapangia kiasi cha kutoa ili kumsaidia aishi vizuri na kufanya kazi ya
MUNGU. Na wewe ukiambiwa umechaguliwa kuwa partner, unafurahi sana, yaani ni
bora Yule ambaye hajachaguliwa huyo atabarikiwa sana. YESU hana ubaguzi na YESU
watu wote ni wanafunzi wake. Hapo ni mtumishi ametekwa na shetani kwa tamaa ya
pesa. YESU amewaita watumishi kuokoa na kuponya Roho zilizopotea na zinazoteswa
na shetani, na akasema msijisumbukie mtakula nini, mtaishije, yeye
mwenyewe atawashughulikia, kwani mana na ndege si bora kuliko nyie? MUNGU
huwalisha na kuwatunza na wanapendeza. Partner ni mtu yeyote mfuasi wa YESU awe
anahela au hana, anavyokwenda kanisani anamfuata YESU na siyo mtumishi, wewe
unayemfuata mtumishi badala ya YESU umelaaniwa, anza kumfuata YESU tu.
Nakupa mfano halisi
ulionitokea, mimi siku mmoja nilikuwa mahali Fulani na watumishi, mmoja wao
akaniambia wewe wacha kupoteza muda tafuta pesa sikumuelewa, nikaona ni jambo
jema ananiambia, akaanza kuniambia bwana wewe sasa hivi hapo kanisani kwako
tafuta wamama sitini (60) wa nguvu uwafanye partners wako na kila mwezi, kila
mmoja akupe shilingi laki moja, mara sitni (100,000*60= 6,000,000) Je, hapo
haujauchinja? Kila mwezi unaingiza (6 milioni) zako mfukoni. Kwa kweli
niliishiwa nguvu, nilipofika nyumbani BWANA akaniambia nilitaka uyasikie na
ujue na uwaelewe hawa watumishi, hii ni namna moja wapo ya kunisaliti maana
mimi sijaruhusu hayo huu ni unyanganyi: Tena hawa partners mpaka wanakopa pesa
ili wapeleke pesa kwa mtumishi, YESU akaniambia jiulize mtu akinitolea mimi
anaishiwa hadi kukopa? Nikamjibu hapana, akaniambia hizo pesa sio zangu ni za
mambo yao na sababu watu wanawaamini kupitia jina langu na wanalitumia vibaya.
Nilishangaa sana na kuogopa. Nakusihi usifanye hivyo na kama ni mtumishi wacha,
utubu, urejee upya kwa YESU huo ni unyanganyaji. YESU hataki na hasira ya MUNGU
itakua juu yako, wacha unyang'anyaji.
Namna nyingine
unakuta eti mtumishi anavaa suti anasimama mbele yenu anajifanyia mnada na kuwa
laghai kutoa kiasi fulani cha pesa unaandika kwenye suti au gauni alilovaa
unaandika kiasi na unapiga saini yako kwenye suti au nguo aliyoivaa, tena watu wanapanga
foleni na kupigania mstari. Hiyo ni namna shetani anachukua uchumi wako na wewe
mwenyewe umekubali kwa saini yako mwenyewe. Hapo uchumi wako na Baraka zako
zinapelekwa kwa lusifa na lusifa anawapatia wale wanao muabudu yeye (Freemason)
na wewe ndiyo shida zinazidi. Kama ulishafanya hivyo, mwambie mtuimishi
anayetumika na YESU wa kweli akufungue na utakua huru kweli kweli, milele na
daima.
Ukikuta mtumishi
anafukia majina yenu au lako au picha yako au pesa yako au chochote chako hii
ina maana anakuzika na hiyo siyo madhabahu ya YESU hapo ni full kwa shetani.
Kimbia kwa usalama wako utaponywa kiroho na kimwili haya yote ni YESU ndiye
anayayenifunulia ili wewe upate kupona maana anakuona unavyoteseka, hii yote ni
sababu watumishi wamemsaliti, hawasemi kweli ni uongo na kufanya yasiyo ya
YESU.
Jinsi nyingine ya
kumjua mtumishi ambaye analitaja jina la YESU na YESU hayupo ndani yake
haijalishi anafanya miujiza, hiyo ni ya shetani haitoki kwake YESU. Mtumishi
anayekuwa na daftari la mahudhurio ya utoaji sadaka au siku ya ibada anasoma
listi ya majina ya watu waliotoa fungu la kumi hadharani, hapo unauwawa kiroho
na MUNGU hajaruhusu bali shetani karuhusu, sasa mtumishi anatakiwa afanye ya
MUNGU au shetani? Akifanya yashetani ina maana shetani ndiye amemtawala,
akifanya mapenzi ya MUNGU huyo ametawaliwa na MUNGU. Mtumishi anayewanyang’anya
watu na kufunga huduma zao, huyo siyo mtumishi wa YESU maana YESU hanyang’anyi
mtu nyota yake, wala Baraka za maisha yake. Mtumishi yeyote anayetoa vyeti vya
hongera kwa ajili ya kutoa sadaka huyo amepotea au ametekwa.
Watumishi wa uongo
ndani yao shetani amewawekea roho za majini ya utambuzi, majini ya maandiko,
jini muhubiri, akisimama kuhubiri utasema kweli umemuona MUNGU kumbe umemuona
shetani ndani yake. Wanachokifanya ili msiwatabue unapokuwa kanisani hapo
kwanza wanakuua macho yako ya Rohoni ili uwe kipofu usiyaone anayoyafanya kwa
kutumia nguvu za giza na wakishindwa au akishindwa ataanza kukuchukia sana, au
anakuita majina ya mapepo aliyo nayo ya utambuzi au agenti, japo kuna agenti wa
kweli. Ikishindikana anakufukuza kimwili lakini wakati huo umechafuliwa hata
watu wanakuogopa na wanafanya hivyo ili ukimbiwe na watu maana wakiwa karibu na
wewe utawaambia na wao watafunguka na ukweli ujulikane na watu watamkimbia.
Pia ndugu msomaji
ukimkuta mtumishi anasema mfano, mungu wake amekuonekania, naomba uwe makini
sana maana MUNGU tunayemjua ni MUNGU wa Ibrahim, Isaka na Yakobo. Shetani
amekuwa akilikamata kanisa au waumini kwa kujipatanisha na mungu wa mtumishi
Fulani kwa kutaja jina lake, kama huyo mtumishi anaongozwa na shetani inamaana
mungu wake ni shetani na wewe unaunganishwa, maana pia tunajua ipo miungu
mingi, yote ni ya uongo kasoro MUNGU wa Ibrahim, Isaka na Yakobo na huyu ndiye
MUNGU aliyeumba vitu vyote ikiwa pamoja na wewe sasa kwa nini usimuabudu yeye,
tena amefanana na wewe, amekuumba kwa mfano wake, cha ajabu haumtaki
unahangaika na miungu mengine. Unapokuwa unaiabudu miungu ya uongo ina maana
umefanana nayo, na ndiyo maana MUNGU alikuumba wewe kwa mfano wa sura yake ili
umuabudu yeye. Je, wewe unamuabudu MUNGU yupi? Muabudu MUNGU wa kweli na ili
umfikie ni lazima uokoke na YESU ndiye kiunganishi cha kweli, wengine wote ni
waongo.
Ndugu msomaji wa
kitabu hiki, MUNGU akubariki sana kwa kujua ukweli ambao shetani ameliteka
kanisa na pia ni jinsi ya YESU kuwafichua hadharani mambo yao wanayo yafanya
kanisani kwa kutumia jina la YESU na kusababisha watu wazidi kuteseka kanisani,
sababu kubwa ni baadhi yao ulimwenguni mwote siyo waaminifu katika kufanya kazi
ya YESU badala yake ni roho ya shetani inafanya kazi ndani yao wengine wakiwa
wanajua wao ni maajenti wa shetani na wengine hawajielewi, wametekwa,
wanatumikishwa wakijua wanafanya kazi ya YESU kumbe siyo. Ujumbe huu uwaeleze
na wenzako, ndugu, jamaa, marafiki ili wasije wakatekwa na wao na kila mtu
amtegemee YESU tu, maana nyakati hizi ni za hatari YESU yu karibu kuja na
shetani anafanya bidii zaidi ili apate idadi kubwa ya watu wachomwe naye
jehanamu kwenye shimo la moto. Ndugu msomaji YESU akufungue ufahamu wako na
akili yako na macho ya rohoni ili uweze kuona na usikamatwe na adui. Na zaidi
usiogope maana YESU ameniambia tayari ameshaanza mapinduzi kwenye ulimwengu
waroho na mwisho wao hao wataabishaji umefika na malango yao ya kuzimu YESU
ameyafunga na baba yao lusifa hana nguvu tena. Hakuna amani kwa wabaya asema
Bwana Wa Majeshi.!
Kwa wewe ambaye haujaokoka soma sala hii:-
BWANA YESU, nipo mbele zako mbele ya agano la Damu ya
YESU, naomba unisamehe dhambi zangu zote, uliandike jina langu kwenye kitabu
chako cha uzima wa milele, namkataa shetani na kazi zake zote, kuanzia leo mimi
ni mali yako YESU, nishike mkono uniongoze milele, Amen. !!
Mpaka hapo utakuwa
umeokoka na mara umalizapo sala hii ,malaika Mkuu Mikael akushukilie hapo
ulipo, akulinde milele na shetani asikupate tena katika jina la YESU KRISTO WA
NAZARETI. Hongera umeokoka sasa, MUNGU akuongoze kanisa lolote ambalo yeye yupo
hapo.
Kwa kumalizia,
lengo kubwa kuhusu ujumbe huu pia ni kukujulisha haya yanayofanywa kanisani,
ndiyo maana majibu kutoka kwa MUNGU hayapatikani na ndiyo maana kanisa
linateseka yani watu wanateseka, siyo YESU anawatesa ni shetani anawatesa na
matokeo yake watu wanaona MUNGU hajibu, wanaenda kwa waganga na ndiyo maana
watu wamemuacha YESU. Wamekua washirikina na huko ndiko wanapoenda kuangamia
milele maana shetani ndiyo anawatumikisha haswa na mwisho wake wanafia dhambini
na kuangamia milele. Kazi na maagizo aliyonipa YESU, niwatoe huko walipotekwa
wana wa MUNGU haijalishi umeshikiliwa wapi utafunguliwa hapo hapo (live!live!).
Na madhabahu zote za shetani hazina mamlaka tena katika jina la YESU KRISTO na
wafuasi wake wanajijua wenyewe. Malaika Mikael na kikosi chako kila siku
teketeza na kuangamiza jeshi la shetani ,na wana wa MUNGU sasa wapumue
wamfurahie YESU nawaone Baraka zao na YESU awakumbatie milele daima, na kila
asomaye, Bwana YESU nakuomba umponye na awe na wewe siku zote, Amen.
MASOMO YA ZIADA:-
Mathayo 10:8
Mathayo 6:1- 4
Mathayo 7: 15- 19
Mathayo 6: 25- 26
Mathayo 15: 8- 14
1 Wakorintho 3: 16-
17
Warumi 10: 9-11
Wagalatia 1: 6- 8
Wagalatia 1: 11- 12
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni