Wafilipi 2:10-11
 • JINSI YA KUTOFAUTISHA ROHO WA MUNGU NA ROHO WA SHETANI

   JE UNAONGOZWA NA ROHO MSAIDIZI WA MUNGU?  JE UNAONGOZWA NA ROHO MSAIDIZI WA SHETANI ?  JE UNAJUA YUPO ROHO MSAIDIZI WA SHETANI? YUKOJE?  

  BWANA YESU ASIFIWE, watu wote wa mataifa yote ambao mmeumbwa na MUNGU na ambaye ndiye BABA yake YESU, na kwa dini nyingine wanamwita yeye ni Nabii Issa, kipindi hiki amekaribia kurudi kwa ajili ya unyakuo. Ukisoma katika kitabu cha Yohana 14:16-17 16 Nami nitamwomba BABA, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa Kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui. Bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu,  naye atakuwa ndani yenu.”
  Utaona hapa YESU kabla ya kupaa aliwaahidi mitume wake atawatumia roho msaidizi kutoka mbinguni na yeye atawaongoza awapeleke mahali alipo yeye mbinguni sababu hakuna mwanadamu atakayeweza kujiongoza yeye peke yake afike mbinguni, njia aliyetutumia YESU ni kupitia roho mtakatifu ambaye ndiye msaidizi wa YESU, na roho huyu yeye huyasimamia yale tu ambayo YESU aliyaelekeza na katika neno la MUNGU lifuatwe kama lilivyo bila kuchanganywa na uongo.
  ROHO MSAIDIZI WA SHETANI NI NANI?

  Roho msaidizi wa shetani ni roho ambaye katika biblia ya shetani na yeye alicopy hivyo hivyo ila dunia imefungwa macho na kupigwa upofu ila wapo baadhi ya watumishi ambao wanaenda kuonana na shetani uso kwa uso kama baba yao na huku duniani  wakijifanya ni watumishi wanaomtumikia MUNGU kumbe ni watumishi wa shetani kabisa na wanamipango ya kuangamiza nafsi za watu ziende jehanamu. Kama nilivyoelekeza katika mafundisho yangu Nabii Hebron nilisema yupo yesu wa uongo na huyu ni shina la shetani na yeye yupo kuzimu ila ile siku ya mwisho na yeye atatoka kimwili kuwapokea wafuasi wake ambao ni wakristo vile vile ambao hawakumfwata YESU wa kweli wa mbinguni sababu na YESU wa kweli na yeye atakubalika na ile siku ya mwisho atawachukua wale walio wakristo wa kweli sasa umeshaelezwa kuwa kama wewe ni mkristo wa uongo siku ile ya mwisho utapokelewa na mkristo wa uongo na kama wewe ni mkristo wa kweli utapokelewa na YESU wa kweli.
  Huyu roho msaidizi wa shetani alitumwa duniani kuwasaidia watumishi ambao ni wapinga kristo na ambao wamemsaliti YESU ambao wapo kwa ajili ya kuwapoteza wanadamu wasiende mbinguni. Roho huyu msaidizi ndiye ndiye anayewaongoza na ndipo utashangaa mbona mtumishi anamtaja roho mtakatifu kanisani lakini hawaruhusu kuokoka au wanamtaja YESU lakini hawabatizwi kama YESU au mtumishi anawaombea watu kwa kuwachangisha watu pesa tofauti na neno la MUNGU lisemavyo “umepewa bure, toa bure” unapoona ni tofauti basi sasa uelewe anaongozwa na roho msaidizi wa shetani na ndiyo sababu biblia haifuatwi na umeshajiuliza ni kwa nini biblia inabebwa kanisani lakini inafuatwa kwa kuchanganywa na uongo? Ni sababu huyu roho msaidizi wa shetani yeye siyo mtakatifu ni muongo hiyo ndiyo dalili ya kujua ni roho msaidizi wa shetani.
  Jambo hili ni moja ya mambo ambaye alinifundisha YESU aliponipeleka mbinguni tokea 2010 ili nijue ni jinsi gani shetani alivyoiteka ulimwengu na kufanya YESU akose watu wengi wa kwenda mbinguni na shetani akawa ndiyo mwenye watu wengi 98% na YESU akawa na 2% ya watu watakaoenda mbinguni. Hii idadi inatisha natumaini mnazidi kuelewa na kuweza kumrejea YESU wa kweli na kumkataa na kumkana yesu wa uongo hadharani pamoja na roho wake msaidizi aliyemtuma hapa ulimwenguni kote akaweka mizizi yake, sasa ni wakati wake kuporomoka na ni serikali ya mbinguni itafanya hiyo kazi na wataendelea mpaka atakapokuja YESU kulinyakua kanisa takatifu yaani mkristo wa kweli. Kama ilivyo kazi za roho mtakatifu zilivyo na yeye roho msaidizi wa shetani hufanya hivyo hivyo mfano kazi ya roho mtakatifu ni kusimamia kweli ya neno la MUNGU lifuatwe, roho huyu wa shetani. Roho huyu wa shetani hulipindua pindua mfano; tazama ubatizo aliobatizwa YESU katika  mto je ndiyo batizo wakristo wanazofuata? Hapo uelewe roho msaidizi wa shetani ndiye anayewaongoza na siku ile ya mwisho atawakabidhi hao watu kwa shetani na watu hawajui jambo hili. Ameintuma YESU, amenituma MUNGU, amenituma ROHO MTAKATIFU wa kweli, ninaeleza ukweli utakayesikia na kugeuka utapona ila utakaye ng’ang’ana huyo roho msaidizi wa shetani atakupeleka jehanamu; yeye kazi yake ni kuwapeleka watu jehanamu ndiyo kazi aliyetumwa na shetani, ni jinsi gani utamjua au kumtambua kuwa ni roho msaidizi wa shetani ndani ya kanisa au ndani ya mtumishi yeyote yule.
  Jambo la kwanza kabisa nataka uelewe haitwi kwa jina lake kuwa ni roho msaidizi wa shetani yeye anatajwa kama roho mtakatifu ila utamjua kwa matendo anayoyaongoza huyo anayeitwa roho mtakatifu. Utayaona ni kinyume na neno la MUNGU mfano wa kufuata matendo baadhi yanayofanywa makanisani katika sehemu baadhi.
  1.     Kubatizwa kwa maji ya kikombe, kubatizwa katika kisima, kubatizwa kwa jina la mchungaji, kubatizwa ubatizo tofauti na  wa mtoni, maji tele yanayotembea (hapa ni roho msaidizi wa shetani anayetia nguvu na watu humfuata. Batizo hizo siyo za haki mbele za MUNGU na siku ile ya mwisho shetani atamwambia MUNGU wewe ni wa haki je kwa nini wamepokea kinyume na neno lako? Sijui utamjibuje MUNGU.  2.     Unapopewa huduma ya maombezi halafu ukachajiwa pesa hapo uelewe siyo roho mtakatifu anayewaongoza kabisa kabisa, bali ni roho msaidizi wa shetani anayempa nguvu hizo na pia nataka uelewe roho huyu msaidizi na yeye ananena vile vile na hapo watu wengi wamepigwa upofu wanaona ni MUNGU.  3.     Kuwa mkristo halafu hataki kuokoka bali kung’ang’ania kujiita mkristo na hautaki wokovu, watu wa namna hiyo wanashikiliwa na roho msaidizi wa shetani na ndiye anayewaongoza na kuwapa mioyo migumu hata madhabahu za jinsi hiyo nataka uelewe zinaongozwa na  roho msaidizi wa shetani ili awaongoze kwenda jehanamu sababu hata wewe soma katiba ya MUNGU yaani neno lake hayo hayapo yamekatazwa ila katika katiba ya shetani yapo. Yametolewa katika ulimwengu wa roho yafuatwe na yamefuatwa sana na jinsi unavyoyafuata ndivyo unavyojiunganisha zaidi na safari ya kwenda jehanamu.  Upokee wokovu sasa uikamate barabara ya kwenda mbinguni, ila nataka uelewe pia roho huyu msaidizi wa shetani na yeye yupo katika makanisa ya dini ya wokovu baadhi yake na kwa watumishi wengi zaidi na kama yupo ndani ya kuhani basi kanisa lote litaongozwa na roho huyu msaidizi wa shetani pasipo watu kujua na kulipeleka kanisa jehanamu na ndivyo ilivyo sasa kwa kupitia njia hii wakristo wengi wanafikiri wapo salama kumbe tayari wameishika njia ya jehanamu pasipo kupenda na wengine kujua.  4.     Roho mtakatifu aliyeletwa na YESU alituambia atatuombea yeye na kutuongoza tufike yeye alipo, wala hatukuelezwa tuwataje malaika ndiyo watuombee. Tuliambiwa katika kuomba ni watatu tu wapaswao kusujudiwa nao ni MUNGU BABA, MUNGU MWANA na ROHO MTAKATIFU na zaidi yeye atatuombea. Sasa cha ajabu utashangaa anatajwa MUNGU, YESU, ROHO MTAKATIFU hapo hapo utashangaa imani za watu zimepelekwa kumwomba Maria atuombee, Petro atuombee au Musa au jina la mtume yeyote. Sasa nikuulize ni wapi pameandikwa tuwafuate hao tuwaombe? Jibu hakuna na zaidi unapofanya hivyo unakuwa umemfanya Maria, Petro na wengineo ndiyo miungu yako hivyo ndiyo roho huyu msaidizi wa shetani alivyowateka watu wengi imani zao na wakifikiri wanaenda mbinguni, sasa muelewe ukweli ndio huo, unaongozwa na roho msaidizi wa shetani na ndiyo sababu unayafuata hayo. Na haikutosha MUNGU amekataa katika neno lake watu wasiabudu sanamu na bado watu wanaabudu na zaidi anatajwa YESU hapo mahali huyo siyo YESU wa kweli ni wa uongo na YESU wa mbinguni hawatambui watu hao kabisa sababu wapo katika njia nyingine ya msaidizi wa shetani  5.     Maombi ya kutengenezewa kamba zenye misalaba halafu unafanya kama ndiyo formula unataja jina la mtakatifu yeyote kwa kuhesabu mafundo na kutaja mambo yako, hiyo pia hayupo roho wa kweli huyo ni roho msaidizi wa shetani ndiye aliyeleta hiyo njia kimwili ya kushika hiyo kamba na kuwekea msalaba. Sasa badala ya roho mtakatifu wa kweli yeye akuombee hata pasipo wewe kujua nini anakuombea akaja roho msaidizi wa shetani akaleta sheria yake ambayo biblia haijaruhusu tuombe kwa kuhesabu vitu hapa mpaka pale na kuyataja majina ya mitume wake; hili ni kosa ni dhambi na msitegemee kumwona roho mtakatifu akiwaongoza kwenda mbinguni bali ni njia ya kwenda jehanamu, haya ni mapokeo ya wamisionari waliotumwa na shetani yamesambaa na watu wameyashika, ili upone yakatae sasa, ndipo utakuwa salama na YESU atakufurahia.  6.     Watumishi wote wanaojiita wao ni YESU au wao ndiyo MUNGU wa majeshi hao wote wamepewa hayo mafunuo na roho msaidizi wa shetani. Kila mtu anajua hakuna mtu anayeitwa MUNGU au YESU au ROHO MTAKATIFU, Je hauoni huku ni kumkufuru Mwenyezi MUNGU?  7.     Kufanya harambee makanisani, hapo siyo sokoni hayo ni makelele mbele za MUNGU bali ni roho wa shetani hapo ndipo furaha yake na ni lazima aongoze ifanyike hivyo ili aujenge ufalme wa shetani au mpinga kristo, aliitwa na shetani. Nyumba za ibada zilizojengwa kwa jinsi hiyo ni mali za shetani wala msitegemee MUNGU aingie katika jengo hilo sababu kama uhalali napo.  8.     Kukopa benki ili kumjengea MUNGU kanisa- roho wa shetani.  9.     Kanisa kuwa na benki, hayo ni mambo ya kaisari, MUNGU yeye hachaji riba, bali roho msaidizi wa shetani ni lazima afanye hivyo yeye hana baraka.  10.                       Watumishi wa freemason wote wanaongozwa na roho msaidizi wa shetani.  11.                       Ibada za wafu- zimeongozwa na roho msaidizi wa shetani, twajua katika neno la MUNGU, yeye siyo MUNGU wa wafu.  12.                       Watumishi wote wanaoomba pesa za tv, radio na michango mbali mbali kwa ajili ya kazi ya kanisa, neno linasema msijisumbue watumishi wangu nitafanya nini sasa hao wanaongozwa na roho msaidizi wa shetani ni lazima wafanye hivyo sababu baba yao ni masikini na wanapofanya hivyo unafikiri wanajenga ufalme wa YESU wa kweli bali ni kujenga ufalme wa shetani ndiyo sababu utashangaa hawana aibu kabisa kuomba pesa, ni sababu yule roho msaidizi wa shetani ndiye anayewatia nguvu hiyo na wale watumishi wa MUNGU wenye roho mtakatifu wa kweli wao hutiwa nguvu na roho mtakatifu na kumtegemea MUNGU na yeye hufanya.

  IPO SIKU YA PENTEKOSTE YA MSAIDIZI WA SHETANI.
  Kama ilivyo ipo siku ya pentekoste ya roho mtakatifu wa kweli na katika siku hiyo hiyo na yeye hujiadhimisha katika makanisa yake na kwa watumishi wake, japo utaelezwa pokeeni roho mtakatifu katika kinywa bali katika ulimwengu wa roho ni kumpokea roho msaidizi wa shetani. Nikuulize swali je iweje roho mtakatifu aongoze wakristo wasiokoke?  Utaona ni roho wa shetani, au iweje wachungaji ni mashoga na wanamtaja roho mtakatifu je jiulize ni roho mtakatifu anayewatia nguvu ya kuwa mashoga? Jibu siyo roho mtakatifu huyo ndiye yule roho msaidizi wa shetani aliyetumwa kuongoza kanisa la mpinga kristo wenye ufahamu na wafahamu zaidi.
  Wapo watu siku ya pentekoste wanapigwa makofi na wachungaji, kuingiliwa kimwili, kutemewa mate, kupigwa busu  eti ndio njia ya kumpokea roho mtakatifu, hapo mmepokea roho msaidizi wa shetani.
  Ukiona unachajiwa pesa ndio uonane na Nabii au mtumishi yeyote, ninakusihi usiende, unaenda kuonana na shetani uso kwa uso aliyopo ndani yake.
  Ukikutana na mtumishi ukamweleza matatizo yako ya ndoa halafu akakuambia akusaidie kwa kukutana na wewe kimwili huyo ni pepo, kimbia kabisa. Huyo anaongozwa na roho msaidizi wa shetani kuendeleza uovu wa shetani.
  Kapu la mama mchungaji- hili ni pepo.  Kulazimishwa kutoa sadaka na kupangiwa kiasi- pepo hilo.
  Kwa leo watu wote wa mataifa yote mjifunze haya na mliokuwa mmepotea njia sasa tubuni maana hata sasa ninavyoandika ujumbe huu nasikia sauti ya MUNGU ikiniambia katika ulimwengu wote hakuna aliyemfunulia siri hii ailete duniani hivyo muishike sana na mumkatae roho msaidizi wa shetani mumfuate roho mtakatifu wa kweli wengi mmelia mmemtolea MUNGU na mmefilisika angalia neno lake katika Malaki 3 sasa kwa nini iwe ni uongo. Jibu roho wa kweli hakuhusika na sadaka zako bali ni roho msaidizi wa shetani yeye ni muongo. Tubu BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozifanya kwa kujua au kutokujua. Naomba uiandike jina langu katika kitabu chako, ulitoe katika kitabu cha yesu wa uongo kupitia roho wake msaidizi wa shetani, nami namkana kabisa. Sirudi tena kwenye madhabahu zake ili asinipate tena. Niongoze YESU mahali ulipo wewe wa kweli na roho wako mtakatifu wa kweli. Amen.
  Mbarikiwe! Zaidi karibu katika kanisa langu lililopo popote. YESU anarudi nyakati hizi ni za hatari amenieleza yeye mwenyewe, uyasikie na uyatumie, watumie na wengine blog hii.


  Hakuna maoni:

  Visits

  Translate