Wafilipi 2:10-11
 • JINSI MKRISTO ANAVYOLAANIWA NA MUNGU NA ANAVYOLAANIWA NA SHETANI


  JE UNAJUA NI JINSI GANI MKRISTO ANAVYOLAANIWA NA MUNGU NA ANAVYOLAANIWA NA SHETANI?

  BWANA YESU ASIFIWE, nafikiri watu wengi watashangaa kusikia kuwa mkristo anaweza akalaaniwa na MUNGU na shetani akamlaani mkristo tena ni katika tendo moja unakuwa umelaaniwa na shetani na pia na MUNGU na yeye anakuwa amekulaani hapo hapo pasipo kujua mtu na wengine wakijua. Yapo mambo mengi yanayosababisha kulaaniwa na MUNGU na pia shetani kupata nafasi ya kukulaani maana biblia inasema katika Mithali 26: 2(b) laana isiyo na sababu haimpati mtu ila ikiwa ipo sababu ni lazima itakupata tu na hata sasa wakristo wengi katika ulimwengu huu wamelaaniwa na shetani na pia na MUNGU kwa sababu lipo jambo ambalo linatoa sababu ya wao kulaaniwa na ni wengi hawajui ila utakapoelewa na kutubu na kubadilika hiyo laana itaondolewa.

  Laana ambayo nazizungumzia sasa ni laana ya kwenda tofauti na neno la MUNGU na sheria za MUNGU. Jambo kubwa hapa ni ubatizo wa watoto wadogo, ukisoma katika kitabu cha Luka 2: 29-34, utaona YESU alivyokuwa mtoto mdogo yeye alibarikiwa sababu ndivyo MUNGU alivyopanga yeye sasa cha ajabu badala ya MUNGU nafasi yake ya kubariki watoto wadogo amepewa shetani katika ulimwengu wa roho ila hapa duniani watu wamepigwa upofu waone wamebatizwa kumbe ni kinyume na mpango wa MUNGU ndiyo sababu watu hawainuki na kubarikiwa sababu zinakuwepo ahadi za shetani na inapokuwa hivyo uelewe hata mtoto huyo na yeye anafanyika kulaaniwa na MUNGU sababu ni kinyume cha MUNGU alivyopanga hivyo inakuwa MUNGU analaani hicho kitendo.

  Shetani na yeye anakuwa tayari alishamteka mtoto tokea akiwa mdogo na hii kufanya mkristo awe amelaaniwa na MUNGU na shetani  pia sababu MUNGU analiangalia neno lake na alisema lisibadilishwe wala kuongezwa sasa utabisha hapo hakuna sababu ya hizo laana kukupata? Jamani nawajulisha watu wote wa mataifa yote MUNGU anawapenda sana ila shetani hawapendi kabisa. YESU karibu anarudi kulinyakua kanisa na kanisa ni mtu, mtu mwenye laana haendi mbinguni, watakaoenda mbinguni ni lazima wasiwe na laana. Shetani alibuni njia hii ya ubatizo wa watoto wadogo ili wakristo mjipe moyo muone upo na YESU kumbe upo na yesu wa uongo. Sasa ni wakati wa kuamka na kukataa haya mafundisho ya uongo yamewafanya maelfu kulaaniwa na MUNGU na shetani pasipokujua sababu ya mpinga kristo.

  Uokoke ukabatizwe upya kwa maji mengi yanayotembea na siyo ya kisima, tank, drum au kwa jina la mchungaji batizo hizo zote hata kama umeokoka bado. Ukisoma neno la MUNGU na shetani anaijua biblia vizuri na mistari yake mfano Ufufuo wa Yohana 22:18-20 imeeleza ukiongeza au kupunguza neno la MUNGU mbinguni hautaingia sasa hapo ndipo aliwatekea wakristo na kuwapiga upofu haraka haraka alijua unyakuo umekaribia na hawataenda mbinguni japo watu wanapenda kwenda mbinguni. Amenituma YESU wa Nazareti niwaeleze ulimwengu wote, yeye ndiye kanieleza haya yote siyo yangu mimi Hebron, mimi ni chombo tu kukuletea ujumbe na kukusihi utubu sababu huu ndiyo wakati wa neema bado giza halijaja, zaidi usome makala hizi utafunguliwa zaidi yapo mambo mengi sana yamewafanya wakristo wajilaani wenyewe na kufanya MUNGU akose furaha na wakristo wanaoenda kinyume na neno lake na kama kawaida kwa MUNGU ukitubu na kuacha atakusamehe na hata sasa mnatakiwa mbatizwe upya ili laana zote zitoke ya kulaaniwa na MUNGU na ya kulaaniwa na shetani pia.

  Siku zote ukiomba lolote kwa MUNGU wakati yeye kasha kulaani je wewe hauoni unajisumbua tu sababu yeye anaangalia neno lake iondoe hiyo laana kwanza na hata hao wanaoisimamia na wao wanayolaana kubwa zaidi ya kuwatengenezea watu mateso japo wapo wanaojua na wasiojua na zaidi hata huo utumishi MUNGU haujui na haupendi na haujatokea kwake wa kuwatengenezea au kuwafungia watu laana na waitii pasipokujua au kujua. Hivyo ndivyo wakristo walivyojitengenezea njia za kumwezesha MUNGU awalaani na shetani awalaani. Sasa uchukue uamuzi uokoke na utubu na uende ukabatizwe katika maji ya mto utolewe hiyo laana ili ukubalike na MUNGU na shetani akukimbie, laana hiyo iwaondokee katika maji mengi tu yanayotembea na siyo ya kisima, bahari, ziwa au kwa jina la pastor au swimming pool hizo batizo zinakuongezea laana zaidi na kujitenga na MUNGU pasipo wewe kujua . Amen.

  NABII HEBRON.

  Hakuna maoni:

  Visits

  Translate