Wafilipi 2:10-11
  • MASAA NANE(8) MBINGUNI

    naRicardo Cid www.DivineRevelations.info/SWAHILI Bwana akasema, "Ninatuma ujumbe huu kwa watu wangu katika dunia,kwa
    sababu mimi niko hai katika
    ulimwengu wa roho." Ufunuo 4:1 Baada ya hayo naliona, na tazama,
    mlango ukafunguka mbinguni, na
    sauti ile ya kwanza
    niliyoisikia kama sauti ya baragumu
    ikinena nami, ikisema, Panda hata
    huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo
    hayana budi kuwako baada ya hayo. Ufunuo 5:11-12 Kisha nikatazama, nikasikia sauti ya
    malaika wengi sana, idadi
    isiyohesabika, maelfu na
    maelfu. Walikuwa wamekaa
    kuzunguka kiti cha enzi, wale viumbe
    hai wanne na wale wazee; wakasema kwa sauti kuu:
    "Mwanakondoo aliyechinjwa
    anastahili kupokea uwezo, utajiri,
    hekima, nguvu, utukufu na sifa." Tafadhali, kanisa sikilizeni nini
    kilichotokea katika maisha yangu. Katika
    ndoto, Bwana alianza
    kushughulika nami. Nakumbuka katika
    ndoto hiyo, Nilitembea nje ya nyumba
    yangu. Nilitembea katika mitaa kwa jirani zangu na mara nilihisi
    kwamba mtu akiniinua mikono yangu juu
    angani nami nilikuwa
    nikitembea mbio juu ya mawingu na
    nikimtukuza Mungu. Mwangaza mkubwa
    alikuja juu yangu na sauti ilisema nje ya mwangaza huo, "Ricardo, Ricardo, acha kazi yako
    kwa sababu nataka kufanya kitu
    kwa maisha yako na kwa kanisa
    langu juu ya dunia." Baada ya kusikia maneno haya, mimi
    nilitetemeka na nikaamka kutoka katika
    ndoto yangu. Nikainuka na mimi
    nikaanza kulia kwa Mungu na
    kuuliza, "ni kitu gani, hiki Bwana?" Sauti hiyo ilikuja kwangu kwa nguvu
    sana. Ilitokea kwangu kwa siku nyingi.
    Kisha nikaendelea kulala
    tena na nikaota ndoto hiyohiyo moja na
    Bwana alirudia mara kwa mara ujumbe
    huo kwangu. Baada ya mara kwa mara kurudia, niliamka na
    kupiga mayowe kwa sababu sauti ya
    Mungu iliongezeka kwa kiasi
    kila wakati. Niliamka nikiwa natetemeka,
    nilipiga kelele na wazazi wangu
    waliniuliza, "Je, kuna tatizo gani?" Niliwaambia kuhusu ndoto na
    mama yangu aliniombea na aliniambia,
    "Kama Bwana anazungumza na wewe, basi Yeye
    atakupa ufahamu. "Tuliendelea kuomba
    usiku kutwa mpaka wakati wa mimi kwenda kazini asubuhi. Mama
    yangu aliniambia nijiandae kwenda
    kazini. Tulimuomba Bwana Page 2 2 ishara ili tujue kama yeye ndiye
    alizungumza na mimi. Nilioga,
    nikajiandaa, na nikaenda kazini. Nilikuwa nafanya kazi katika "maabara
    ya Chile". Mimi kwa kweli napenda kazi yangu.
    Nilikuwa nikipitiwa katika kituo cha basi
    na kwenda kazini. Mara niliposhuka, mtu mmoja aliniambia
    kwa haraka, "Unafanya nini hapa?
    Hautakiwi kuwa mahali hapa tena. "Katika matukio kadhaa,
    wengine waliniambia kitu hiko. Jambo la
    kushangaza ni kwamba wao hawakuwa wamezaliwa mara ya
    pili. Hii ni ishara ambayo Mungu alinipa.
    Baada ya ishara hii, niliamua kwenda kwa bosi wangu ili
    niache kazi. Nikamwambia, "Mimi
    menipasa kuondoka katika kampuni kwa sababu Mungu ameniagiza
    kujiondoa." Bwana anapotupa amri, ni
    LAZIMA kutii. Bosi wangu alikuwa na wasiwasi kwa ajili
    yangu na aliuliza, "Je,utakwenda
    kufanya nini? Wapi utapata kazi nyingine nzuri kama hii? "Nilimwambia
    imenipasa kumtii Mungu. Basi,
    walinifanyia mahafali makubwa ya kuniaga ya watu elfu mbili kwa ajili
    yangu. Baada ya hapo, nilikusanya vitu
    vyangu vyote na kurudi nyumbani. Nilifika nikiwa nalia, mama
    yangu alikuwa tayari ananisubiri kwa
    mbele ya nyumba. Nilimwambia kuwa niliamua kuacha kazi
    yangu kwa sababu Bwana alithibitisha
    ndoto zangu kupitia watu hao. Yeye akajibu, "Kama Bwana
    amekuambia, basi namuomba afanye
    katika maisha yako vile apendavyo." Tuliingia ndani na tukaongea mpaka
    usiku. Basi, niliimuambia ninahitaji
    kwenda kitandani kwa sababu Mungu
    atazungumza na mimi usiku wa leo
    katika ndoto. Nilidhani angeongea nami katika ndoto,
    lakini haikutokea kama nilivyowaza. Lakini alisema nami kwa njia ya tofauti.
    Nilipokwenda katika chumba cha kulala
    na nilipotoa nguo zangu, chumba kikaanza
    kutikisika. Na nilianza kupiga kelele, "Ni tetemeko linaikumba Santiago, Chile."
    Nilijaribu kuondoka katika chumba
    changu, lakini mtu asiyeonekana alinizuia kupita
    mlangoni. Nilikuwa na uwezo wa kumuona mama yangu na familia yangu
    katika chumba hicho na nilipiga kelele kwa msaada lakini hakuna mtu
    aliyeweza kunisikia. Sasa najua, kiumbe
    huyu asiyeonekana alikuwa ni malaika wa
    Bwana. Nilirudi nyuma na kujilaza juu ya kitanda changu na nikalmlilia Mungu,
    nikaomba aniambie nini kinaendelea. Sauti ikasema nami. Roho mtakatifu
    akaanza kusema nami katika sauti nzuri sana, akisema, "Ricardo, Kwa kuwa umeacha kazi kwa sasa, nitahitaji
    wewe uende kanisani na uwe unaomba kwa muda wa saa saba
    kila siku kwa maisha yako, na kwa
    kanisa langu duniani." Baada ya Bwana kuacha kuongea nami, chumba
    kikaacha kutikisika. Nikaainua mkono
    wangu na kuona ya kuwa ninaweza kuondoka chumbani tena.
    Kishanikamkimbilia mama yangu na
    kumueleza " Nimesikia sauti ya Roho mtakatifu" na nikatoka nikaanza
    kuongea kwa sauti nje ya nyumba. Watu
    hawaamini kuwa Mungu bado anaongea na watu hata leo
    lakini nakueleza ni kweli, Anaongea na
    watu! Kama Bwana aliweza kuongea na Abrahamu,
    anaweza kuongea nasi pia na kanisa
    lake leo. Nikaenda kanisani na kuongea na Askofu na tukakubaliana
    kufungua kanisa kila siku asubuhi saa 2
    ili niweze kutii agizo la Mungu alilonipa. Kila asubuhi nilikwenda
    kanisani na nikaomba saa moja, mawili
    na kwa mara ya tatu sikuwa na chochote cha kuombea na
    nikawa nikimuuliza Mungu, " Bwana ni
    kitu gani kingine niombee?Nimebakiwa na masaa manne
    yaliyobakia!" Kisha, nikasikia tetemeko linatokea
    nyuma ya mlango wa kanisa. Nikahisi
    kanisa linayumba kushoto na kuliakama mtu aliyelewa. Lilipokuwa
    likiyumba, nikasikia sauti ikiongea nami
    lakini wakati huu haikuwa sauti kama ile ya
    kwanzaniliyokuwa kwenye maono. Suti
    ile ya kwanza ilikuwa ya mamlaka, lakini wakati huu aliongea nami kwa
    sauti ya huzuni. Akasema, "Ricardo, Ricardo omba kwa ajili ya kanisa langu! Kanisa langu si kama
    lilivyokuwa kabisa, Kanisa langu
    duniani limebadilika. Kanisa Page 3 3 langu limepoteza imani yake. Kanisa
    langu haliamini kuhusu mimi na wala
    kuamini kama mimi ni hai hata leo . Liambie kanisa langu
    kwamba nipo ni hai!! Omba kwa ajili
    ya kanisa, kwa sababu kanisa langu haliombi wala kufunga
    tena!" Mtikisiko uliacha baada ya yeye kumaliza.Nikaanza tena kuomba na kutembea juu na chini kwa
    muda wa masaa manne yaliyobakia
    nikiwasihi watu wa Mungu wawe na uhamsho. Siku ya Alhamisi ya wiki ya pili ya
    maombi, niliamka na maumivu makubwa
    katika mifupa yangu na viungo vyangu na sikutaka kuinuka.
    Mama yangu alikuwa akiniamsha
    kwenda kanisani kuomba, lakini nililalamika kuwa mwili wangu na mifupa
    yangu ilikuwa ina maumivu. Basi
    akanishauri kuwa niombee pale nyumbani. Hata hivyo
    nilimkumbusha kuwa Mungu
    ameniambia niombee kanisani. Hivyo akanisaidia kunivalisha na kunipeleka
    kanisani. Asubuhi ile kulikuwa na watu
    wengi waliokuwa wakiomba pale kanisani, nami
    nikawaomba waniombee kwa ajili ya
    mwili wangu kwa sababu ya maumivu katika mwili wangu.
    Niliwaeleza kuwa nilikuwa mdhaifu sana
    kuweza kufanya maombi. Hivyo walinipaka mafuta na kuniombea
    mwili wangu na nikapata nguvu za ajabu
    kutoka kwa Mungu!!Haleluya! Nikaanza kuomba
    nikitembea mbele na kurudi nyuma,
    nikiomba rehema za Mungu kwa taifa la Chile na kwa familia na watu
    walioathiriwa na madawa na kwa kanisa. Nilimaliza maombi na kisha nikarudi
    tena baadae kwa ajili ya ibada ya usiku.
    Baada ya Baraka za askofu,niliinua mikono yangu na nikahisi
    mtu fulani alipita na kuugusa mgongo
    wangu. Lilipotokea jambo hili nilipoteza nguvu zangu zote
    na nikaanguka sakafuni.Askofu
    aliniuridha nini kilikuwa ni tatizo na mimi, na nikajibu hata sifahamu,
    nikamueleza kuwa sina nguvu na siwezi
    kuzumgumza vizuri. Kisha kanisa likanizunguka na kuanza
    kuniombea kwa lugha huku wengine
    wakiomba kwa sauti. Baadhi ya watu walianza kuona malaika akija na
    kuniuliza niuache mwili wangu. Askofu
    akakemmea, "Hautauacha mwili wako!" Aliposema
    hivyo, Malaika waliacha kuniita ili
    niuache mwili wangu. Unaona, Mtu yeyote mwenye mamlaka
    katika Yesu ataheshimiwa na malaika
    wa Bwana. Askofu akaniomba pia, "Kwa muda gani
    malaika anahitaji akuchukue kutoka
    katika mwili wako?" Nikamuuliza malaika, "unanichukua kwa
    saa moja?mawili?Matatu?"Malaika
    akajibu, " hapana, utaondoka kwa muda wa masaa 8
    kwenda kumuona Yesu katika mbingu ya
    tatu kwa sababu anataka kuongea nawe."Kisha malaika
    akanieleza, "Mimi siye ambaye
    nitakuongoza wewe kwenda mbinguni, kwa sababu mimi ni malaika wako
    ambaye nimekulinda wewe kila siku
    tokea kuzaliwa katika dunia hii. Malaika wawili watakuja kutokea
    mbinguni ili kukuchukua wewe mpaka
    mbingu ya tatu usiku wa manane." Nikamueleza hili askofu na na
    akaazimia kunichukua mimi kwa gari ya
    ndugu mmoja katika kristo kwa nyumba ya mchungaji katika
    ghorofa ya pili. Nilipofika tu chumbani,
    tuliweza kusikia mbwa wakibweka na watu wakilia. Baada ya maono yangu nilielezwa kuwa
    wanaume wawili waliovalia mavazi
    mazuri meupe yanayong'aa walionekana mtaani na
    wakaja hadi ghorofa ya kwanza ya
    nyumba na wakapanda hadi ghorofa ya pili nilipokuwepo. Malaika
    hawa ni wazuri. walikuwa na nywele
    nyeupe zinazong'aa, nyeupe zaidi ya barafu/theluji, na macho yao
    yalipendeza kama lulu.Ngozi yao ilikuwa
    nyororo kama ya mtoto lakini bado walikuwa wakionekana kuwa
    na misuli kama wanyayuaji wa vitu vizito
    (bodybuilders). Malaika hawa walikuwa na nguvu!! Kisha
    nikamueleza Askofu, malaika hawa
    wako mahali hapa walotumwa kunichukua twende
    mbinguni.Malaika mmoja akaanza
    kunisihi niuache mwili wangu. Lilipokuwa likitokea hili, mifupa yangu
    ilianza kuniuma tena. kwa hiyo ndugu
    wangu katika Kristo pembeni mwangu walianza kunichua na
    kunieleza kuwa walihisi baridi
    ikiongezeka katika mwili wangu.Kwa hiyo walichukua hita ili
    kuupa joto mwili wangu, nilianza
    kuogopa na kuanza kwenda huku Page 4 4 na huku. Nilianza kuhisi kifo
    kinanichukua na nikasema kwa sauti wa
    ndugu zangu hawa katika Kristo, " Msinizike, nitarudi tena!" Niliuacha mwili wangu na nikarukia
    kitandani. Niliwaona ndugu hawa
    wakiushikamwili wangu na kusema, "Ameondoka, "Ameuacha mwili
    wake!" Lakini nilikuwa pembeni yao
    nikiwaeleza "niko hapa!" Lakini hawakuweza kuniona kwa
    sababu ulikuwa ni mwili usioharibika wa
    kiroho. Ndugu hawa walianza kuufunika mwili wangu katika
    blanketi. Malaika mmoja aliniambia, "Ni wakati wa
    kuondoka sasa kwa kuwa Bwana
    anakusubiri!" Kila mmoja aliushika mkono wangu na
    kuninyanyua kwenda mbinguni na
    tulipita katika anga kwa mwendo wa mwanga. Nitakueleza wewe hivi,
    hata kama hauamini mojawapo ya
    mambo haya, Yesu Kristo yupo na anaishi milele!! Baadae ,Bwana aliponieleza niurudie
    mwili wangu , nikimueleza,, " Ni nani
    katika dunia ataniamini, niache tu niishi na wewe!! hakuna
    atakaye amini huu ufunuo, hakuna
    atakayeamini kwa sababu hawana imani! Tatikzo la kukosekana kwa imani
    ni kubwa sana, ni nani ataamini huu
    ufunuo?" Bwana akajibu, " Kuna mtu fulani ataamini maono
    haya, ni wale walio wa kanisa langu
    la kweli wataamini." Nilipokuwa nimeuachaa mwili wangu
    usiku ule nilikuwa nikipaa kwa spidi ya
    ajabu nikiwa naenda kwa Bwana. Niliweza kuangalia chini na
    kuona sayari dunia. Kisha nikapita
    karibu kabisa na mwezi, Mwezi huu mzuri uliiangaza anga usiku
    katika dunia. Kisha, niliweza kuona jua
    na ukubwa wake kwa macho yangu; Niliweza kuona miali ya
    moto ilivyokuwa ikilipuka na kutoa joto
    mpaka kwenye dunia. Kisha tuliendelea na kuona nyota nyingi
    tulizozipita. Mungu aliruhusu mimi nione
    jua, mwezi na nyota kwa kusudi: Kusudi hilo ni kuuambia
    nyinyi nyote kwamba Mungu wetu ni
    muumbaji mkuu wa Ulimwengu!!! Si mdogo kwa namna
    yeyote ile! Tuliendelea kusafiri kwa mwendo huu
    mkali hadi tulipofika mahali ambapo
    hakukuwa na nyota tena. hakukuwa na uumbaji wowote, ilikuwa ni
    Giza tu.Niliweza kuangalia chini na
    kuona nyote zote zikiwa chini. Nilianza kuogopa na nikawauliza
    malaika, "Mnanipeleka wapi?
    Nirudisheni kwenye kitanda changu duniani" walinishika na kunibana
    zaidi na kuniwekea miguu yao kwa
    miguu yangu na kunishika. Nilianza kulegea kwa sababu ya hofu
    niliyokuwanayo. Malaika wakaniambia "
    Nyamaza Kimya! Tunakupeleka kwenye mbingu ya tatu
    ambapo Yesu anakusubiri ili aongee
    nawe!" Malaika walisimama na wakati huu niliangalia pande zote na
    sikuona chochote cha uumbaji,
    sifahamu nilikuwa wapi, nafikiri ilikuwa ni mbingu ya pili. Kisha nikiwa katika hali ya kujiachia
    malaika wakiwa wamenishika na mara
    nikajisikia na kusikia kelele za kutisha juu yangu. Malaika
    wakanibana na kusema, " Ricardo,
    usiogope, Yesu yuko pamoja nasi!" walipokuwa wakiongea,walisema, " Inua
    kichwa chako na uangalie juu yako!"
    Nilishangazwa sana na kile nilichokiona kwa sababu kulikuwa
    na viumbe vilivyokuwa katika mwendo
    juu yetu. Malaika mmoja akasema, " Angalia, tutakuonyesha
    wewe kile ambacho unakiona juu yetu!
    Malaika mmoja akanyoosha mkono wake akapunga huku na huku ili
    kutoa mwanga uangaze sehemu yote ile
    ya anga ili kuona kitu kilichokuwepo mahali pale. Anga
    lilipokuwa na muangaza hakukuwa na
    kitu chochote ila mapepo na mashetani yalikuwa yamezunguka anga
    lote lile. BWANA AWAKEMEE WOTE
    KWA JINA LA YESU!!Biblia ni kweli!! Kila kitu
    kinachoendelea katika ulimwengu huu
    ndo kile ambacho unakiona katika Ufunuo. Yesu anakuja hivi
    karibuni!! Nawezaje kukushawishi, ni hivi KARIBUNI!!Nikamuuliza malaika, "Mahali hapa ni wapi?Mmoja
    akajibu, " Hapa ni mahali pa ulimwengu
    wa Giza ambapo Shetani na malaika zake ( mapepo)
    wanaishi," Akaanza kusema, " Ndio
    maana kuna uharibifu mwingi duniani! Mapepo haya yanakuja duniani
    kutokea mahali hapa na kusababisha
    uharibifu na uovu wa kila Page 5 5 aina na uovu katika makabila ya
    wanadamu!" Dunia imejaa mapepo!"
    Kuna mapepo milioni na milioni , idadi haihesabiki. Kisha malaika, alianza kunipeleka niangalie kwa ukaribu na kunionyesha sura za viumbe hivi na nyingi ya hivi viumbe vimekwisha onekana kwenye Runinga. Viumbe hivi ni VIBAYA!! Niliona viumbe vilivyofanana na viumb vya kwenye michezo ya runinga ya Thundercats na Power Rangers na
    katuni ya caricatures ambavyo ni halisi kabisa kwa maisha ya duniani. Wabunifu wote wa muvi na michezo hii wameweka mkataba na shetani kutoa vitu hivi kwenye runinga na sinema!! Michoro
    yote ile inatokea katika ulimwengu war oho ambao niliuona. Unafikiri kwa nini
    watoto wa siku hizi wamekuwa
    wakaidi?? ni kwa sababu mapepo haya yanawanigia watoto hawa
    wanapokuwa wakiangalia maonyesho
    haya ambayo yanawaoyesha wao (mapepo). Ndiyo
    maana imetupasa kuwafundisha watoto
    kuchagua nini cha kuangalia kwenye TV. Malaika
    aliniambia hiki ni halisi na kweli. Mapepo
    haya yote yapo na watu wanafanya makubaliano na shetani ili
    kuleta mapepo haya duniani. Haya
    mapepo yanaanza kunitukana mimi, na kanisa, na Baba, na Bwana
    Yesu na Dunia kwa sababu
    hawamuheshimu Mungu au uumbaji wake wowote. Kisha nikaona kiumbe halisi kabisa
    kiitwacho Hugo, huyu ni katuni maarufu
    sana nchini Chile. Ilikuwa inaogopesha kuangalia. Alikuja karibu
    yangu na kunieleza, "Tutaenda duniani
    na kuwaua watoto wote!" Kwa nini unafikiri watoto wanaua watoto
    wenzao? Ni kwa sababu baadhi yao
    husema kuna kitu kilikuja kutoka katika runinga na kuniambia
    nifanye hivi au vile. Mapepo haya
    hupanda chuki duniani, Bwana akomboe na kusafisha Chile!! Mmoja wa
    malaika akaniambia "Endelea
    kuangalia!" Na mapepo yakasema, "Tumejaribu kuharibu kanisa,
    lakini hatuwezi kwa sababu
    tunapomuuua mmoja, basi wanainuka maelfu kuchukua nafasi ya
    kifo chake!" Tokea kuanza kwa kanisa,
    Shetani amejaribu kuliharibu, kanisa ambalo huubiri injili ya
    kweli na kufanya kazi ya Mungu, lakini
    hawezi kwa sababu Yesu anatulinda! Utukufu kwa Mungu!
    Kisha mapepo yakasema, "Ngoja
    tufanya jambo jipya, ngoja tuingie makanisani, kwa sababu pale
    kuna wengi ambao ni wetu! Tutaenda
    kuwatumia watu hawa kusambaza umbea na kuleta
    migawanyiko katikati ya ndugu ndani ya
    kanisa." Shetani anazunguka kila mahali akitafuta kuharibu wale
    wanaopenda haki ya Mungu. Kama
    andiko linavyosema: 1Petro 5:8 Muwe macho; kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi,
    huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mawindo. Sikutaka kuendelea kuona tena, lakini
    malaika akaniambia niendelee
    kuangalia matukio yanayotokea. Niliona mapepo yakiruka kila kona pindi
    nyota moja ing'aayo ilipokuwa inakuja.
    nyota hii ilipokuwa inatokeza na kusogea, ilikuwa inaleta
    sifa nyingi na ibada kwa Bwana. Hii
    haikuwa nyota kama nyota, kumbe ilikuwa ni mamilioni ya
    malaikawakiwa juu ya farasi weupe
    wakimtukuza Mungu wa Majeshi!! Walikuwa wakiimba
    "Mtakatifu,Mtakatifu, Mtakatifu, ni yeye
    aishie enzi na enzi! Bwana ndiye Alpha
    na Omega, Mwanzo na Mwisho na kila
    chenye pumzi na kimsifu Bwana!" Kisha
    nikaaona vita kubwa na Page 6 6 sikuona mapepo tena. "Usiogope kabisa
    kwa sababu kuna malaika wengi zaidi
    upande wetu zaidi ya upande wa adui!" Malaika walifa ya njia mpaka mbingu ya
    tatu. Walijigawa katika makundi mawili,
    moja kulia na jingine kushoto.Ilikuwa ni njia iliyowazi mpaka
    mbingu ya Tatu! Njia hii ilinyooka mpaka
    mbinguni na uliweza kuona Mji mtakatifu wa Mungu. (Kuna
    picha ya satellite duniani ambayo
    imechukua picha kutokea katika mji huu.
    Mji huu Mtakatifu upo! Hii imetokea kwenye
    radio na TV.) Nilweza kuona njia ya
    utukufu na malaika wa ajabu.
    Waliisafisha njia yote kuwafukuza mapepo na
    hawakuacha kumsifu Mungu na kubariki
    Jina lake! Malaika wakaniweka mbele yao na kuniambia, "
    Imekupasa kusubiri hapa!" Kwa mbali, niliangalia na kutokea katika
    mji huu niliona mtu fulani akiwa na
    mazazi mazuri meupe amepanda farasi mweupe. Mtu huyu
    alipokuwa akizidi kunisogelea, malaika
    waliendelea kusifu jina la Mungu na kumtukuza. Mtu huyu alikuja
    mpaka umbali wa mita 4 tokea nilipo.
    Kiumbe huyu alikuwa mzuri, alikuwa ni mzuri zaidi ya wale
    malaika wengine. Nilitegemea
    angeongea nami, lakini alichokifanya ilikuwa ni kuniangalia na
    kusema kwa sauti, "Mimi ni malaika
    mkuu Mikaeli ambaye ninajukumu la kukulinda wewe pamoja
    na kanisa la Duniani!" Nilimuona malaika
    mkuu Mikaeli uso kwa uso na alikuwa ni kiumbe cha
    thamani sana! Aligeukia upande wake
    na kuonyesha njia ya mimi kuingia mji Mtakatifu. Alisema, "Ingia!
    Bwana Yesu anakusubiri!" Nilikuwa
    nikitembea katika njia ile nikifuata mji ule na nilipokuwa
    nikitembea, Malaika walikuwa wakiimba
    na kumsifu Bwana. Nililia na kulia nilipokuwa nikiuangalia mji ule. Mji ulikuwa umeumbwa kwa dhahabu
    halisi angavu na mlango wa kuingilia
    ulikuwa umeundwa kwa lulu. Sakafu ilikuwa ni ya muonekano wa
    kioo angavu(crystal). Sijawahi kuona
    kitu kama hiki duniani na hakuna mwanadamu awezaye
    kukiunda. Msanifu wa majengo ya
    mbinguni ni Bwana wetu na Mungu wa Ulimwengu wote.Nilikuwa nje ya mji
    na milango yote ilikuwa imefunguliwa.
    Na milango hiyo ikiwa bado hii wazi, niliweza kuona ndani na
    katika kuta kulikuwa na madini ya Rubi
    na safira na lulu ambayo yaling'aa. Na ndani ya mji ule
    kulikuwa na sauti milioni na milioni ya
    sauti zikimsifu Mungu! Nilitetemeka kutokea nje ya mji
    niliposikia hivi. nilisikia sauti moja
    ambayo ilitikisa mbingu na nyuma ya sauti hii ilikuwa ni mamilioni na
    mamilioni ya sifa kwa Mungu yakisifu
    "Mtakatifu, MtakatifuMtakatifu ndiye mwanakondoo
    wa Mungu na Baba ambaye utukufu una
    yeye na heshima milele na milele AMEN!" Sauti kubwa
    ikasikika ikisema "IWENI WATAKATIFU KWA SABABU MIMI NI MTAKATIFU! NI WATAKATIFU
    TU NDIO WATAKAOINGIA KATIKA MJI
    HUU!KWA SABABU PASIPO UTAKATIFU HAKUNA
    ATAKAYEMWONA BWANA." Bila utakatifu hakuna atakayemuona Bwana. Sauti ikasikika ikisema, "Ingia" na
    nikaingia ndani ya mji ule. Na nikaona
    Kiti cha ajabu cha enzi kimezungukwa na moto. Na moto
    unatoka katika kiti kile cha enzi,
    Nikatulia kimya na nikamuona Yesu , Mfalme wa wafalme na Bwana wa
    mabwana! Nilijihisi mdhaifu mbele zake
    na nikaanguka chini nikaishiwa na nguvu.Mkono wake
    ukatoka kwenye miali ile ya moto na
    kunishika na akasema, "Simama kwa miguu yako!" Nilipata nguvu na nikasimama. Nilianza kugusa
    miguu yake na mikono yake na mwili. Nilipoona uso wake,
    muonekano wake ni tofauti sana na
    wachoraji wa dunia wanavyochora katika michoro yao! Watu
    wengi wanaunda miungu ya mbaona
    wengine taswira mbalimbali! Lakini nataka nikuambie hivi
    ndugu yangu, Yesu Yule hafanani na
    taswira hizo. Ni Mungu mwenye misuli na nguvu! Si Mungu wa
    ukawaida, Ni Mungu mwenye nguvu
    zote!! Anasema, "Mimi si Mungu niliyeumba na mbao, au
    chaki,Ni Mungu ninayeishi!" Anaendelea, "Liambie kanisa langu duniani mimi ni halisi!! Ni kweli
    ninaishi na nipo! Waambie watu
    wangu kuwa Mbinguni ni Halisi na ninawasubiri!" Aliniambia,"Njoo, tembea pamoja nami na
    nitakuonyesha jambo moja kubwa. Page 7 7 Tuliangalia chini na niliweza kuona
    dunia na vitu vyote vilivyofanywa
    kwenye dunia. Yesu akasema, "Ninaweza kuona kila kitu ambacho
    kanisa langu linafanya!" Anajua kila kitu tunachokifanya na mimi niliweza kuona wengi wenu
    kutokea mbinguni. Yesu akaniambia,
    "Angalia katika kanisa langu!" Niliweza kuona ndugu kwa ndugu, na
    makanisa kwa makanisa. Yesu
    akaniambia, "Kanisa langu limepoteza imani yake,hawataki
    kuniamini, uovu umeongezeka
    duniani na watu hawataki kuamini kuwa nipo. Waambie watu wangu
    ninakwenda kufanya kitu kikubwa
    duniani! Kanisa langu linarudi nyuma badala ya kukua." Bwana alianza kulia kwa ajili ya kanisa lake na
    akasema, " Hili kanisa si kanisa langu! Nikamuambia Bwana, "Bwana usiseme hivyo! Wewe unajua
    kuwa tu kanisa lako." Bwana Yesu akajibu, "Hapana kanisa langu linatembea kwa nguvu za
    miujiza,ishara na maajabu! Kanisa langu limepungua! Hatahivyo,
    waambie, nitakuja kuwafufua tena!" Aliniambia niendelee kutembea pamoja
    nae na tulikwenda mahali fulani penye
    mlango na mlango ulikuwa umetengenezwa kwa dhahabu
    halisi.Nilianza kukimbia huku na huku
    kwenye mtaa uliofanywa kwa dhahabu na nikawa ninachukua
    vumbi la dhahabu na kujipaka kwenye
    mwili wangu. Na Yesu aliniambia nirudi na akaniambia kuna
    mitaa ya dhahabu mbinguni. " Hii yote ni urithi kwa watu wangu," Bwana akasema. " Lakini kwenye kanisa langu kuna wezi
    wengi ambao wananiibia fungu la kumi na sadaka! Waambie watu
    wangu hakuna mwizi atakayeingia
    kwenye ufalme wa Mungu!" Inabidi turekebishe maisha yetu kwa ajili
    ya Bwana.Kisha tuliona meza ndefu
    sana kwa ajili ya watu mamilioni ikiwa na chakula cha kutosha
    na vinywaji. Kulikuwa na mataji mengi
    na glasi kwa ajili ya watu kunywea. Bwana akasema, "Yote haya yameandaliwa kwa ajili ya
    watu wangu!" Meza hii iliandaliwa kwa ajili ya harusi ya Mwana
    kondoo. Kuna dada mmoja katika Kristo ambaye
    pia alipelekwa mbinguni na kasha aliona
    malaika wakienda na kurudi wakiwa wanatayarisha chakula
    cha Harusi hii! Nikamuambia Bwana, "
    Kwa nini dada huyu aliona malaika wakitayarisha vitu hivi,
    lakini mimi sioni matayarisho yoyote
    yanayofanyika? Bwana akajibu, "Ni kwa sababu matayarisho yote yamekamilika!" Kuna mataji kwa wote wanaofanya kazi na ni watii kwa Bwana. Kisha nikamuuliza, "
    Bwana utakuja lini basi,kama maandalizi
    yote yamekamilika?Itachukua muda gani
    mpaka utakaporudi? Nionyeshe muda,
    Ni muda gani umebaki katika saa ya mbinguni?" Watu wengine
    wamekuwa na maono ya muda,
    wakionyesha kuwa itakuwa ni usiku muda ambao Bwana Yesu atarudi.
    Niliuliza, " Ni lini saa itagota katika mshale wa saa sita usiku?Je ni dakika moja imebakia?
    dakika tano?" Bwana Yesu akausoma uso wangu kwa muda kidogo, kasha akajibu,
    "Ricardo,mbinguni hakuna muda tena!" Kisha nikaitikia, "Vizuri bwana , kama hakuna muda tena, kwa nini
    bado haujarudi?" Yesu akanyanyua mkono wake na kuchukua kidole gumba chake na vidole vyake
    vingine na kunionyesha alama
    inayoonyesha kitu fulani kidogo sana na akasema,"Muda wote uliobakia ni Neema ya Mungu kwa
    wale waliorudi nyuma warejee tena na kutubu na kuifanya kazi ya
    kwanza." Na Bwana wa Majeshi hajarudi kwa sababu ametupa sisi sote muda kidogo sana wa kutubu na Muda
    huo unaitwa, " Muda wa neema/rehema
    ya Baba" Yesu anarudi muda wowote, ni lazima tuanze
    kumtafuta kwa moyo wetu wote na
    tufunge na kuomba na tuzifanye kazi za kwanza. Nimemaliza kila kitu. Yesu
    alirudia, " Tuko kwenye muda wa Neema ya Mungu!" Kisha malaika alitokea upande wetu wa
    kuume akisema kwa sauti, "Muda
    umewadia!! muda umekwisha. Maandalizi yote
    yamekamilika! Yesu anampokea bibi
    harusi wake( kanisa)!" Bwana Yesu anarudi na kila ishara iliyoko kwenye
    maandiko inatimia! Sinema zinaonyesha
    kitu fulani cha kutisha kinakuja. Wanasayansi wanatambua
    kitu fulani kikubwa kitatokea, hawajui ni
    kitu gani hicho!Hatahivyo, Sisi kanisa tunatambua
    kwamba Yesu anarudi hivi karibuni!
    Malaika walipomaliza kusema, kasha mamilioni ya malaika
    walianza kuruka na kushangilia kwamba
    bibi harusi(kanisa) linarudi mbinguni. Nikaendelea
    kumuuliza, " Kitu gani kinaendelea?"
    Lakini hakuna aliyeonekana Page 8 8 kujali, wote walikuwa wakishangilia kwa
    habari njema. Nilijumuika na malaika na
    kuanza kulisifu jina la Yesu pia! Wakati huo nilipoinua
    mikono yangu nilihisi mtu fulani
    ameninyanyua kuondoka mbinguni na kunirudisha chini kwa spidi ya ajabu. Hivi sasa, malaika wanashangilia
    kwamba Bwana Harusi anarudi. Nilirudi
    duniani na niliachwa pale madhabahuni kanisani ambapo
    nitakuwa ninaomba kila siku. Muda ni mfupi sana!! Kama hutaki kuniamini mimi, basi usiamini. Lakini
    anakuja na itakuwa ni ujio wa milele.
    Watu wa Mungu hawaamini katika unyakuo. Tafadhali
    amka, Kwa jina la Mungu amka katika
    ukweli!! (Ricardo analia) . Bwana Yesu alikuwa karibu yangu, na
    aliniambia, "Ricardo, hivi ndivyo ambavyo unyakuo utakuwa kama utatokea hivi sasa!" niliweza kuona dunia yote na Roho mtakatifu
    mzuri ambaye anatupa amani na furaha ya kuishi katika dunia.Kisha
    nikaona kama mvuke ukiingia kanisani
    na ukanizunguka na nikamuuliza Bwana, "Hii ni nini?"
    Akasema, "Hiki ndicho nakiita Unyakuo."Kisha nikaona watu wakivunja milango ya kanisa, wakitaka
    kuja ndani, na kupayuka, "Watoto
    wangu wako wapi? Wote wametwaliwa!" Watoto wote katika
    ulimwengu wametwaliwa kwa sababu
    Mungu hata waacha nyuma. Mtu wa kwanza kuingia katika kanisa
    alikuwa ni Mwalimu wa kwaya,
    akapayuka, " Kanisa liko wapi! nimeachwa nyuma! Nimebaki!
    Nimebakia!" Baada ya mwalimu wa
    kwaya, niliona wachungaji wengine, waumini wa wakiume na wa
    kike,na waangalizi wa kanisa wote
    wanalia, "Nimeachwa nyuma!" Wazazi wengi na wanandoa
    wengi waliwatafuta wale wawapendao
    na watu wale walioko kanisani wakawajibu, "Muwapendao
    hawako mahali hapa! Bwana
    amewachukua," Watu hawa walianza kulia, "Yaani kumbe ni kweli,
    Yesu amekja na kuchukua bibi harusi!". Watu walikuwa wakilia na kuomboleza
    wakitamani kama tu wangemuamini
    Yesu Kristo. Kila mtu asiyemuamini Yesu kama Masihi
    amepotea! Nikaona watu wengi na
    wachungaji wakilia na watu walianza kuwadai wachungaji, "Kwa nini wewe hukuhubiri ukweli, kwa nini
    hukufundisha utakatifu na kunionya mimi kuhusu yote haya?
    Ni kwa sababu yako nimeachwa
    nyuma! "Wengi wataachwa nyuma kwa sababu hawaishi maisha
    matakatifu. Tunahitaji kuhubiri utakatifu
    wa kweli na kuwafundisha watu toba ya kweli! Niliona jinsi watu
    walivyopiga wachungaji na
    kuwakatakata na kuondoa nywele zao. Wachungaji walilia na kuomba
    watu wasiwadhuru. Watu hawakuacha
    kwa sababu walikuwa sasa na mapepo. Kuna makanisa kabisa ambayo
    yataachwa nyuma. Nilimuona kaka
    mmoja alikuwa anajaribu kuyakwarua macho yake mwenyewe
    kwa sababu ya huzuni kuu. Na watu
    walipigiza vichwa vyao sakafuni na kwenye kuta kwa sababu
    hawakutambua kuwa Yesu alikuwa
    ndiye jibu pekee. Kwa sababu watu walitaka kuendelea katika dhambi
    na uovu na kuishi maisha vile
    walivyotaka. Watu walijikata wenyewe na kupigiza vichwa vyao
    mpaka kiasi cha kuona fuvu zao
    zikiweka ufa na walianguka chini. Damu ilitiririka bure ndani ya kanisa kwa
    watu ambao walikuwa wakijijeruhi
    wenyewe. Kisha nikaona kijana akipiga kelele kwa Mungu,
    "Tafadhali Bwana, nichukue!" Alikuwa
    amechelewa mno. Yesu alikuwa tayari amekwishakuja na
    kulipokea kanisa lake. Hapo nilianguka
    chini kwa sababu niliona mambo mengi zaidi ya kutisha. Yesu akaniambia, "Katika dhiki kuu, kutakuwa na matatizo makubwa
    haijawahi kutokea kabla." Kisha nikauliza, "Kwa nini watu
    wanaruka nyuma baada ya kuumizana
    vibaya wao wenyewe?" Bwana Yesu akajibu, "Kwa sababu kwa wakati huu, watu watatamani kifo,
    lakini hawatakipata. Kifo kitakuwa kimetoweka katika uso wa
    dunia. Nilimwuliza Bwana, "Kwa nini wachungaji wote hawa na watu wameachwa nyuma?" Na Bwana
    akasema, "Kwa sababu ninajua mioyo
    yao. "Mungu anatujua sisi .. Anajua yote ya mioyo yetu. Nilianguka
    chini, karibu kuzimia. Yesu alisema, "nimetaka kukuonyesha Page 9 9 hili ili kwamba uonye kanisa langu na
    kuwapa matumaini. Waambie
    kwamba kama watu watatubu sasa, mimi nitawasamehe wakati
    bado kuna muda. Nitafanya jambo
    kubwa katika dunia. " Tafadhali,fungua macho yako. Kanisa la
    kiinjili nchini Chile linaongezeka. "Waambie watu wangu kama wataomba msamaha,
    nitawasamehe." kisha nikaona maono mengine na nikaona moto umefunika mbingu nzima. Yesu akasema, "Je, umeweza kuona? Huo moto uliona
    juu ya nchi/dunia, ni moto juu ya nchi ya Chile. Kwa sababu Chile
    itakuwa kwa ajili ya Kristo! Mungu
    ataibadili Chile! " kisha nikaona moto unataka kuja juu ya Chile
    na Yesu akasema," Macho ya Baba yangu yako juu ya Chile. "Mara moto utakapokaa juu ya Chile,
    nchi nyingine zitaona na kujua kuwa
    Mungu yuko mahali hapo. Kanisa lote duniani litafurahi kwa
    sababu Uwepo wa Mungu unatembea
    Chile. Bwana alinichukua katika maono mpaka mahali paitwapo
    "Paseo Humada " Akanionyesha watu waliokuwa vilema
    na walio na matatizo. Kisha nikaona
    waamini wa kweli wakiomba juu ya viwete wasio na miguu
    na wakitiisha viungo kukua. Viungo vilitii
    na kukua mbele ya macho yao. Watu wasio na mikono
    waliiota mikono kwa upya mara moja.
    Wakati huu, Bwana ataonesha miujiza ya uumbaji. Katika
    makanisa watu ataponywa. Katika siku
    hii, wafu watafufuliwa na Mungu akutumia wewe ndani ya Chile
    kufanya miujiza hiyo kama mitume wa
    zamani walivyofanya katika Biblia. Huo ni ufunuo mzima ambao Mungu
    alinipa (Ricardo Cid). Yeye anakuja hivi
    karibuni. Maranatha! Amina! Ndugu aliyefasiri ufunuo wa Ricardo
    Cid wa Masaa 8 Mbinguni ni Peter
    Kahale ni kijana aliyeokoka na anampenda Yesu na mwenye shauku
    ya kuhubiri injili ya Yesu Kristo. Simu ya Mkononi:
    +255-755-255043,
    +255-653-610460. Barua Pepe:
    kahalepeter@gmail.com

    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate