Wafilipi 2:10-11
  • MUDA KWA HARAKA SANA UNAKWISHA! USHUHUDA WA VICTORIA NEHALE – NCHINI NAMIBIA

    UTANGULIZI Nimezaliwa na kuishi Namibia maisha
    yangu yote. Niliokoka tarehe
    06/02/2005. Bwana Yesu amenifunulia mambo mengi ya
    ulimwengu wa roho pamoja na
    kunipeleka mara kadhaa kuzimu. Bwana aliniambia niwaelezee watu
    niliyoyaona; na akanionya nisiongeze
    wala kupunguza chochote kwa yale aliyonionyesha au
    kuniambia. Kufikia kuandika kitabu hiki,
    mwisho wa 2006, nilikuwa nimetembelewa na Bwana
    Yesu mara 33. Kwa kila utembezi huo
    Bwana alinisisitizia: MUDA UMEISHA. SAFARI YA KWANZA KWENDA
    KUZIMU Mwisho wa juma la 23/07/2005,
    nilichukua teksi kutoka mji wa
    Ondangwa (Nchini Namibia) ninakoishi na kufanya kazi, kuelekea
    kijijini kwetu kuwaona wazazi wangu.
    Nilipokwa njiani nilihisi kuwa kitu cha ajabu kilikuwa kinaenda
    kutokea jioni hiyo. Nilifika nyumbani
    mwendo wa saa kumi na mbili jioni na ndio wakati watu
    walikuwa wakiandaa chakula cha jioni.
    Nilikuwa jikoni na ndugu zangu nimelala juu ya shuka
    kukuu chini, na wapwa zangu walikuwa
    wakiimba nyimbo za kanisani. Ghafla nikahisi nguvu kuu za Mungu juu
    yangu zilizoufanya mwili wangu kuzimia.
    Nilimwona mtu mwenye kanzu nyeupe na kamba yenye
    rangi sawa, akinisogelea nilipokuwa
    nimelala. Kulikuwa na mwanga wa ajabu unamzunguka
    kana kwamba unatoka kwake. Alikuwa
    amevaa viatu vya hudhurungi. Alifanana na watu wa
    mashariki ya kati hata ngozi ikawa
    inampenda. Mwili wake ulikuwa umejaa utukufu nilishindwa
    kumwangalia kwenye macho.
    Alipoongea sauti yake ilikuwa ya upole, huruma, upendo, na yenye
    mamlaka. Mawimbi ya upendo yalikuwa
    yakinijia kutoka kwake. Akainyosha mikono yake kuelekea
    kwangu na kuniinua. Ghafla nikajikuta
    nipo katika mwili mzuri uliobadilishwa. Nilionekana kama vile
    nilivyo kuwa kijana wa miaka kumi na
    nane. nilikuwa nimevalia kanzu nyeupe iliyofungwa
    kamba nyeupe. Ijapokuwa kanzu yangu
    ilikuwa nyeupe lakini malighafi yake ilikuwa tofauti na kanzu
    yake. Vazi lake lilikuwa la kitani safi na
    mwanga na mng'ao wake ni vigumu kuelezea. Alisema kwa upendo na sauti ya upole, ''Victoria fuatana nami,
    nitakuonyesha mambo ya kuogopesha na kukupeleka sehemu
    ambayo hujawahi kuona maisha
    yako yote". Akanishika mkono wa kuume na
    tukaanza kuenda. Nilihisi kama vile
    tunatembea hewani na tunapanda wakati wote. Baada ya muda
    njiani nikawa nimechoka sana.
    Nikamwambia nisingeweza kuendelea na safari na
    nikaomba kurudi nyumbani. Aliniangalia kwa upole na kusema
    "Haujachoka uko safi, ukichoka nitakubeba. Lakini sasa uko safi. Amani na iwe nawe, tuondoke". Sehemu tuliyofika ilikuwa kame na
    mbaya kuliko jangwa lolote baya
    lililojulikana na binadamu, bila dalili yoyote ya uhai au maisha.
    Hapakuwa na mti wowote, nyasi au
    kiumbe chenye uhai hakikuonekana. Ilikuwa ni sehemu
    mbaya sana. Tulikuja kwenye lango na yule mtu
    akanigeukia akisema, "Victoria tutapitia langoni na vitu utakavyofundishwa vitakuogopesha
    na kukufadhaisha. Lakini uwe na
    uhakika kokote nitakako kupeleka utalindwa vizuri. Fungua
    macho yako uangalie kila kitu
    nitakacho kuonyesha". Nilitishika na kuanza kulia. Nilipinga na
    kutaka anirudishe. Nikamwambia kuwa sikutaka kuingia
    mahali pale kwakuwa nilikuwa naona
    yanayotendeka ndani akaniambia, "Amani na iwe nawe; niko pamoja nawe ni lazima tuingie ndani,
    kwa maana MUDA UMEISHA". Kuzimu kulivyo Tukapita lango lile mpaka ndani na kwa
    niliyoyaona nashindwa kusimulia mahali
    pale palivyo. Nina uhakika hakuna mahali pengine
    duniani pa kutisha kama pale. Mahali
    pale palikuwa pakubwa sana na nilihisi kuwa palikuwa
    panaongezeka wakati wote. Giza la
    mahali pale lilikuwa kubwa sana na moto uliokuwa unawaka
    haupimiki. Moto wenyewe au miali yake
    ilikuwa Page 3 Page 3 of 8 haionekani ila ukali wake ulikuwa juu
    sana. Nzi wa kila namna na rangi
    walikuwa kila mahali. Palikuwepo pia na minyoo wafupi,
    wanene na weusi wakijaribu kupanda
    juu ya kila kitu. Minyoo wakanza kupanda juu yetu huku inzi
    wakiruka kila mahali. Harufu ya mahali
    pale ilikuwa mbaya mno, ilikuwa kama nyama iliyooza ila ni
    zaidi ya mara mia ya harufu yoyote ile
    niliyo wahikuihisi. Kulikuwa kumejaa sautu za vilio na
    kusaga meno, pia nilisikia vicheko viovu
    vya pepo wabaya. Cha kuhuzunisha ni kuwa mahali pale
    palikuwa pamejaa watu wasiohesabika.
    Watu walikuwa kwa namna ya mifupa. Nilijua mifupa
    hiyo ilikuwa ni watu kwani niliweza kwa
    uhakika kuwajua ndugu zangu kutoka kijijini kwetu.
    Mifupa hiyo ya rangi ya kijivu ilikuwa
    imekauka sana. Walikuwa na meno makali kama ya wanyama,
    midomo mikubwa na ndimi ndefu na
    nyekundu. Mikono na miguu ilikuwa na vidole virefu vyenye
    kucha za kutisha. Wengine walikuwa na
    mikia na pembe. Pepo wachafu walikuwa
    wakichangamana na watu. Mapepo hao
    walikuwa kama kenge wakitembea kwa miguu minne.
    Waliifurahia hali ile na wakawa
    wakiwatesa na kuwakejeli wanadamu, huku wao wakirukaruka na
    kushangilia wakati wote. Wanadamu
    kwa upande wao walionekana wa kusikitisha na kuvunjika
    moyo, walionekana kukata tamaa na bila
    matumaini yoyote. Kelele za wanadamu zilikuwa
    kwasababu ya maumivu. Walikuwa
    wakilia, kupaza sauti na kusaga meno. Hali yao haikuwa ya
    kusikitisha tu, bali pia ya uchungu na
    masitikiko.Watu wa mahali pale walikuwa wengi lakini
    niliona wazi kuwa wengi walikuwa
    wanawake. Makundi ya watu kuzimu Waligawanywa kwa makundi tofauti
    lakini haikuwezekana kuwahesabu kwa
    makundi yao kwani walikuwa wengi sana. Niliyekuwa naye
    akanipeleka kwa kikundi kimoja cha
    mashariki na kuniambia, "Hili ni kundi la walioshindwa KUSAMEHE. Niliwaeleza mara nyingi na
    kwa njia tofauti jinsi ya kuwasamehe wenzao lakini wao
    wakakataa. Niliwasamehe dhambi zao
    zote lakini wao wakakataa kuwasamehe wengine. Muda
    wao duniani ulipoisha wakajipata mahali
    hapa. Watakuwa mahali milele yote,
    wanavuna matunda ya matendo yao
    milele na milele. Ila ni uchungu kwangu kuwaona hapa katika
    hali hii – kwa kuwa nawapenda". Nikaongozwa kwa kundi la pili na
    nikaambiwa na yule mwenye kunipeleka,
    kuwa walikuwa wenye MADENI na makundi yao yalikuwa matatu: 1. Wa kwanza ni wale waliodaiwa na
    wenzao na walikuwa na uwezo wa
    kulipa lakini wakawa wakihairisha siku baada ya siku.
    Wangeahidi kulipa wakati ujao, mwezi
    ujao, mwaka ujao mpaka muda wao duniani ukaisha na
    wakajipata mahali hapa. Watakaa
    mahali hapa milele na milele wanavuna matunda ya kazi
    yao. 2. Wa pili ni wale waliodaiwa madeni
    waliyoweza kulipa na walikuwa tayari
    kulipa lakini waliogopa madhara yake. Waliona kuwa
    wakiongea ukweli watakataliwa,
    watapelekwa jela au walichokifanya kingejulikana dunia
    yote na wangedhalilishwa. Yule mtu
    akaniambia, "Hakuna hata mmoja aliyeniuliza njia ya
    kulipa. Wangefanya hivyo
    ningewaonyesha njia rahisi. Walitumia hekima na sababu zao
    ambazo hazikuwasaidia hata kidogo". 3. Waliokuwa na madeni wasiyoweza
    kulipa ila hawakuniambia kwamba wana
    madeni wasiyoweza kulipa. Wangefanya hivyo
    ningewalipia madeni yao. Pia walijaribu
    kutumia hekima na sababu zao, ambazo
    hazikuwasaidia hata kidogo. Sasa
    wamejikuta sehemu hii wasiyoweza kutoka. Wanakula matunda
    ya matendo yao. Moyo waniuma kwa
    ajili ya hawa wote kwasababu nawapenda sana. Katika kundi la kwanza niliwaona ndugu
    zangu wawili wa kike wa karibu, vilevile
    na ndugu yangu mmoja wa miaka kumi na miwili. Nilijua
    miaka yake kwani huo ndio uliokuwa
    umri wake alipofariki. Katika kundi la pili niliwaona
    baadhi ya ndugu zangu na hata
    mchungaji niliyekuwa namfahamu vizuri. Jakes mpenzi wangu
    aliyejinyonga baada ya mimi kuokoka
    alikuwa kwenye kundi la pili. Niliwaona baadhi ya
    majirani zangu katika makundi yote. Niliwajua watu tuliokuwa
    tukifahaminiana na wao pia wakanijua.
    Watu wa ukoo wetu waliponiona walianza kunitukana kwa
    lugha chafu. Mmoja wao akaniambia
    kuwa sikustahili Page 4 Page 4 of 8 kumfuata yule niliye kuwa naye.
    Wakanikumbusha hali niliyokuwa kabla
    ya wokovu. Waliyoyasema yalikuwa kweli kwani ni
    mambo niliyoyafanya. Jakes mpenzi
    wangu akasema kuwa nilikuwa wake na nilistahili kuwa
    alipokuwa maana dhambi zetu zilikuwa
    sawa. Mwanzoni Mchungaji alifurahia kuniona nikienda
    alikokuwa, lakini alipoona
    niliyeandamana naye akaungana na wenzie kunitukana.
    Aliyekuwa nami akaniambia niyapuuzie
    maneno hayo kwani hawakujua walichokuwa wakifanya. Nikaogopa na kushikwa na huzuni sana,
    nilikuwa nikitetemeka nikashindwa
    kusimama. Nikalia bila kujizuia ndipo niliyekuwa naye
    akanikumbatia na kusema, "Amani na iwe nawe Victoria". Palepale nguvu zikanirudia na nikapata
    faraja na amani kuwa naye. Wakati wa
    kuondoka ukawa umefika naye akasema, "Victoria nimekuonyesha haya ili uchague ni
    kundi lipi ungependa kuwa, kwa kuwa uamuzi ni wako.
    Lazima uwaambie watu kila kitu
    ulichoona bila kupunguza au kuongeza kitu chochote." Kurudi kutoka kuzimu Nakumbuka tulipotoka mahali pale pa
    mateso tukiwa pamoja, ila sijui
    nilipomuacha kwasababu niliposhtuka na kufungua macho
    nilijikuta mwilini kama kawaida. Nilikuwa
    nimelazwa hospitali ya Oshakati. Kulikuwa na mpira wa
    kuingizia maji mwilini, mamangu na
    ndugu zangu walikuwa chumbani humo. Machozi yalikuwa
    hayajamkauka mamangu. Nilipomuuliza
    Nesi kilichokuwa kikiendelea akaniambia, "Umerudishwa,
    pengine una makosa na unahitaji
    kutubu." Japo Nesi aliongea kwa furaha bado
    niliona anaogopa kunisogelea.
    Nikamuulizia daktari aliyekuwa akinishughulikia. Daktari alipofka hakuweza kuelezea
    ugonjwa niliokuwa nao. Alidhania kuwa
    malaria lakini matokeo hayakuonyesha hivyo. Joto la
    mwili na shinikizo la damu vyote vilikuwa
    chini sana lakini hakujua sababu yake. Hakujua la
    kufanya kwani hangeweza kunilaza
    Hospitalini kwani sikuwa mgonjwa. Maji waliyoniingizia kwa mpira
    yalikuwa hayaingii vizuri lakini mara tu
    nilipofungua macho yakaanza kuingia bila tatizo.
    Daktari akaagizia niongezewe maji
    mengine. Niliendelea kuhofu na kulia kwa ajili ya
    mahali pale pa mateso. Matukio ya
    mahali pale yaliendelea kupita machoni kwangu saa
    zote. Sikuweza kulala mwili mzima
    ulikuwa unaumwa, viungo vyote vilikuwa kama
    vimetenganishwa na kuunganishwa
    tena. Tumbo lilinisumbua na kichwa kikaniuma juma zima. Niliamua kutomwelezea mtu yeyote
    niliyoyaona. Ni nani atakayeniamini?
    Watu wangenichukuliaje? Nikajiwazia. Baada
    ya siku tatu nikamwambia mama mmoja
    aniombee na nikaishia kumwelezea yote yaliyotokea.
    Nikajihuzunikia sana kwa kuisimulia
    hadithi hiyo maana sasa haingeweza kufichika. Mwishowe
    nilielewa kuwa Mungu ni Mungu. Akitaka
    kitu kisimuliwe sina uwezo wa kukizuia eti kwasababu
    ya ya mawazo na hofu yangu. Maelezo juu ya safari Agosti 19, niliamka nikihisi nguvu za
    Mungu. Nilikuwa dhaifu nikitetemeka na
    nikajisikia kama nguvu za umeme zinapita mwilini. Jioni
    nikaona miale ya mwanga mkuu na
    katikati yake nikamwona mtu yule aliyenipeleka
    sehemu ya mateso. Wakati huu akaketi
    kwenye kiti karibu na kitanda changu. Kiti chenyewe
    hakikuwepo lakini alipotaka kukaa
    kilionekana. Kilikuwa kiti cha mapambo mazuri huku kikiwa
    kimeundwa na dhahabu tupu. Baada ya kunisalimia akaniambia kuwa
    anaelewa kuwa nina maswali mengi na
    ndio maana alikuwa amejitokeza ili ajieleze yeye na
    mambo mengine yaliyokuwa yametokea.
    Akaanza kusema, "Mimi ni Yesu, mwokozi wako, kama una mashaka yoyote angalia mikono
    yangu. Mahali tulikokwenda ni kuzimu". Nikaona mahali alipogongwa misumari. Rafiki ningependa nikwambie kuwa
    kuzimu sio mawazo ya mtu bali ni mahali
    pabaya pa mateso kulikotengenezewa shetani na mapepo
    yake. Wanadamu wanastahili kwenda
    mbinguni pamoja Page 5 Page 5 of 8 na Yesu lakini lazima tumchague yeye
    kabla hatujachelewa. Leo ukisikia sauti
    yake usiufanye moyo wako kuwa mgumu. Mkubali Yesu
    kama mwokozi wako, na kama
    umempokea basi mwishie yeye. Sikujua sababu ya kuambiwa nichague
    kati ya makundi mawili huko kuzimu na
    ilhali mimi nimeokoka. Nimemwamini yeye na bado
    ananiambia nichague kwenda kuzimu au
    la. Sikumuelewa. Nikamwomba Mungu
    anifunulie maana ya usemi huu na kile
    angetaka nifanye. Akaniambia kuwa nilikuwa mtu wa HASIRAna pia SIKUWASAMEHEdadangu na binamu yangu mmoja. Nikaomba msamaha kwa
    dhambi hiyo halafu nikamwomba dada
    msamaha kwa kuweka hasira na chuki dhidi yake.
    Ikabakia kwenda kumwomba binamu
    msamaha. Bwana akanikumbusha kuwa niliwahi
    kupata ajira ya ualimu nikitumia cheti
    bandia cha diploma. Akasema kuwa kitendo hicho ni DENI pamoja na WIZI. Nilitaka kutenda lililo haki na nikamwomba anipe njia nzuri ya kufuata
    kwani hilo lilitosha kunipeleka gerezani.
    Akaniambia nikatubu kwenye idara ya elimu.
    Nilikuwa tayari kwa lolote, hata kwenda
    gerezani ikiwa haiwezi kuepukika. Mungu akatenda maajabu na
    wakuu wakaniambia nichague kama
    nataka kulipa au la. Hawakutaka kunipeleka mahakamani
    kwasababu kukiri kwangu
    kuliwashangaza. Hakika Mungu ni wa ajabu na analiheshimu neno lake. Ukiwa na jambo kama hili nakusihi
    kufanya kilicho cha haki bila kujali
    matokeo. Unaweza ukafungwa jela hapa dunuiani lakini
    hiyo ni ya muda. Hakuna uchungu au
    fedheha inayoweza kufananishwa na kutengwa na Mungu
    milele na milele. Kuzimu sio mahali
    pazuri; ni afadhali umwache Mungu akuhukumu sasa kabla
    haujachelewa. Tusiogope hukumu ya
    Mungu katika siku hizi za neema, NI VYEMA TUMWACHE YEYE ADHIHIRISHE CHOCHOTE
    KILICHO KIBAYA MAISHANI MWETU KAMA BADO TUNA WAKATI
    WA KUJIREKEBISHA kwani hakuna msamaha upande ule mwingine wa kaburi. SAFARI YA PILI KUZIMU Tarehe 18/10/2005, niliamka saa kumi
    na moja unusu alfajiri, sikuweza kwenda
    kazini. Nilikuwa najisikia dhaifu sana na nikawa
    nimenyong'onyea; nisingeweza
    kujisogeza au kugeuka kitandani pangu, uwepo wa Mungu ulikuwa
    mkubwa chumbani. Nilikuwa
    nikitetemeka na kuhisi kama nguvu za umeme zinapita mwilini
    mwangu. Bwana akaja kunichukua kabla
    ya saa mbili. Alinisalimu na kuniambia kuwa
    inatupasa kwenda tena kwani MUDA UMEISHA. Nikasimama na tukaanza kutembea. Jinsi tulivyokuwa
    tukitembea siku hii ilikuwa tofauti na
    siku zingine. Japo miguu yetu ilikuwa ikitembea, ilikuwa ni
    kama tunaogelea zaidi kuliko kutembea. Tukiwa safarani, Yesu akaniambia,
    "Dhambi zote ni mbaya na hakuna dhambi kubwa wala ndogo. Dhambi zote huleta mauti,
    haijalishi ukubwa wala udogo". Akaniambia kuwa tunaelekea tena kuzimu na kisha
    akaniuliza kama nilikuwa na hofu.
    Nikamwambia kuwa nilikuwa naogopa. Akasema, "Roho ya hofu haitoki kwa Baba yangu, inatoka kwa
    shetani. Hofu itakusababisha ufanye vitu vitakavyo
    kupeleka kuzimu. Bila imani ni vigumu
    kumpendeza Mungu na hofu ni kinyume cha imani. Nidhahiri
    hofu haimpendezi Mungu kwasababu
    huharibu imani ya mtu ya mtu ". Kwa muda wote tukiwa njiani tulikuwa
    tukitembea upande upande lakini baada
    ya kufika lango la kuzimu akanishika mkono wangu kwa
    muda wote tuliokuwa kuzimu. Nilikuwa
    na furaha kwasababu alinishika mkono na kwa
    kunishika aliondoa hofu yote ndani
    yangu. Sehemu hiyo ilikuwa bado inafanana na ya kwanza;
    hapakuwa na tofauti na sehemu ya
    kwanza. Kulikuwa na vijidudu virukavyo, minyoo, joto
    lililokithiri, harufu mbaya, mifupa, kelele.
    Kila kitu kilikuwa kama nilivyoona mara ya kwanza. Mtumishi aishia motoni Tuliingia lango kama lilelile tena
    akanipeleka kwenye moja ya makundi
    ya watu. Kulikuwa na watu wengi niliokuwa nawafahamu
    walipokuwa hai duniani. Watu walikuwa
    katika hali mbaya sana; walionekana wamefedheheka na
    uchungu mzito lakini kibaya zaidi
    walionyesha sura zisizo na matumaini. Page 6 Page 6 of 8 Bwana akamwashiria mwanamke mmoja
    mwenye umri wa kati. Nilimjua kabla ya
    kifo chake kilichotokea kwa ajali ya gari mwanzoni
    mwa 2005. Nilishtushwa kumuona
    kuzimu kwani sote tulimjua kama mcha Mungu. Bwana
    akaniambia kuwa mwanamke alimpenda
    Mungu na Mungu pia alimpenda mwanamke huyo.
    Alinitumikia alipokuwa duniani,
    Aliwaongoza wengi kwa Bwana na alimjua Bwana vizuri. Alikuwa
    mwema kwa maskini na wahitaji; alitoa
    kwa ajili yao na aliwasaidia katika njia mbali mbali.
    Alikuwa mtumishi mzuri wa Bwana
    katika njia nyingi. Maneno haya ya Bwana yalinishtua
    sana na zaidi nilipomuuliza kwanini
    akamwacha mtu aliyemtumikia vizuri aishie kuzimu.
    Bwana akajibu kuwa ijapokuwa alijua
    sana maandiko alikubali uongo wa shetani kuwa kuna dhambi
    ndogo na kubwa. Alifikiri dhambi ndogo
    haitamwangamiza kuzimu maana yeye ni mkristo. Bwana
    akaendelea kusema, "Nilienda mara nyingi na kumwambia aache alichokuwa
    akikifanya lakini mara nyingi
    aliendelea kufikiria kuwa dhambi hiyo ni ndogo sana na mwisho
    akachukulia kuwa maonyo niliyompa
    yalitokana na dhamiri dhaifu aliyokuwa nayo. Kuna wakati
    aliacha dhambi hiyo lakini baada ya
    muda akairudia huku akajishawishi kuwa maonyo hayo ni
    sauti ya kwake mwenyewe maana
    dhambi hiyo ni ndogo na haiwezi kumhuzunisha Roho
    Mtakatifu". Nikamuuliza tena Bwana anieleze
    dhambi aliyoifanya mwanamke huyo,
    naye akanijibu kwamba, "Mwanamke huyu alikuwa na rafiki yake Nesi katika hospitali ya
    Oshakati. Wakati wowote alipokuwa mgonjwa hakuwa akilipia
    kadi ya hospitali kama inavyotakiwa
    bali alikuwa anampigia rafiki yake simu na
    wanafanya mpango wa yeye kupata
    dawa kutoka kwenye zahanati. Rafiki yake alikubali
    kumfanyia hivi wakati wote". Hukumu yake ni kuwa:  alikubali uongo wa shetani juu ya
    dhambi ndogo na kubwa na hivyo
    kuikataa kweli yangu.  alimsababisha mwenzie kutenda
    dhambi ya kuiba kwa niaba yake.  lililo baya zaidi, alimhuzunisha Roho
    Mtakatifu. Hii ndio lilimpeleka kuzimu. "Haijalishi kama utaleta mamilioni ya
    nafsi kwa wokovu bado unaweza kuishia
    kwenda kuzimu kwa kumhuzunisha Roho Mtakatifu. Ni
    lazima uangalie wokovu wa wenzio
    lakini uwe mwangalifu usisahau roho yako. Uwe makini na kila
    jambo unaloambiwa na Roho Mtakatifu".
    Baada ya Bwana kuyasema hayo akaniambia
    turudi. Unayachukuliaje maneno haya? Wakristo wengi waliosikia simulizi hii
    hupata maswali mengi. Wanajiuliza, "Je kuhesabiwa haki, huruma na neema
    za Mungu hazina nafasi yoyote?". "Na je unaweza kuupoteza wokovu
    baada ya kuupokea?". "Mbona neno hili lina ukali sana? Mungu
    anaweza kuwa katili hivyo?". Kama nilivyosema mbeleni mimi
    sifundishi theolojia. Ninasema tu
    mambo ambayo Bwna alinionyesha na kunifundisha.
    Nakuomba uangalie Biblia yako vizuri
    kwa majibu. Hebu angalia vifungu vifuatavyo halafu ujiamulie. Bali nautesa mwili wangu na
    kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri
    wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa. (1Wakorintho 9:27 ) Tuseme nini basi? Tudumu katika
    dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?
    Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? ( Warumi 6:1-2 ) Basi dhambi isitawale ndani ya mioyo
    yenu ipatikanayona mauti, hata mkazitii
    tamaa zake – (Warumi 6:12 ) Maana, kama tukifanya dhambi kusudi
    baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli,
    haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi. Bali kuna
    kuitazamia hukumu kwenye kutisha, na
    ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.
    (Waebrania 10:26, 27 ) Je naweza kuishia kwenda kuzimu
    baada ya kumtumikia Bwana na
    kuwaongoza wengi kwa Kristo? Jiamulie mwenyewe. Page 7 Page 7 of 8 Kutotii Jumatatu tarehe 06/03/2006, niliamka
    saa kumi na moja na nusu alfajiri.
    Nilipoanza kuomba nikaona kuna nguvu za Mungu za ajabu
    juu yangu. Mwili wangu ulikuwa dhaifu
    na nilikuwa natetemeka. Nguvu kama za umeme
    zilikuwa zinapita mwilini mwangu. Mchana nilipokuwa nimelala nikaona
    mwanga mkubwa wa ajabu ukikijaza
    chumba chote. Nikaona vitu vidogo vyeupe vyenye
    umbo la mviringo vikiniangukia kama
    mvua na kuingia mwilini. Kisha nikaona wingu la kitu
    kama ukungu likishuka, kukijaza chumba
    chote na pia kuanza kuingia mwilini mwangu. Nikamwona
    Yesu akinijia akiwa katikati ya wingu lile
    la ukungu na akaketia kiti chake kandokando ya
    kitanda changu. Sijui kiti hicho hutoka
    wapi ila huwa kinatokea akiwa tayari kukaa. Kiti chenyewe
    kimeundwa na dhahabu tupu, kuna
    nyota ya shaba kwenye kila mguu wa kiti hicho. Mahali pa
    kujiegemezea pamewekwa pia nyota
    kubwa ya shaba na kila mguu wa kiti hicho kuna magurudumu ya
    mviringo. Yesu akaninyoshea mkono kunisalimia.
    Akaniambia niinuke kwa kuwa MUDA UMEISHA. Akanivuta kwa mkono na nikakaa juu ya
    kitanda. Akaniambia, "Victoria tuombe". Akaomba kwa lugha ambayo sikuelewa. Nilichoelewa
    pekee ni neno 'Amina'. Akaniuliza
    nilichokuwa naona. Watu walikuwa wakiingia kazini.
    Nikaona vile vitu vidogo vya mviringo
    vikiwaangukia kundi la wale waliotangulia kufika mahali pao pa
    kazi. Waliofika baadaye walipata mvua
    ya vitu vile imekatika. Jambo hili pia nikaliona
    kanisani, waliotangulia waliangukiwa na
    vitu hivi vyeupe lakini waliofika baadaye hawakuvipata. Yesu akaniuliza kama naelewa maana
    ya maono hayo nami nikamjibu kuwa,
    "Sielewi". Basi akanieleza, "Maono hayo yana maana kuwa kila
    mahali unapostahili kufika kwa wakati
    fulani, na unaujua wakati huo, kuna Malaika
    wanawagawanya baraka, kwa muda ule.
    Anayewahi anapata baraka zile anayechelewa anazikosa – kwa kuwa
    Malaika hugawa baraka kwa muda tu.
    Vitoria nataka nikuonye kwa kuwa unachelewa kwenda
    kazini na unachelewa zaidi kwenda
    kanisani. Elewa kuwa siku ulizochelewa bila sababu
    umekosa baraka zako za siku hizo
    milele. Baraka hizo haziwezi kukurudia. Victoria ni lazima
    uache jambo hilo na usirudie pengine
    uwe na sababu nzuri". Aliponiambia hivyo nilitamani kumkimbia
    au kumpa sababu nzuri kwa kosa hili.
    Nikamwambia nilikuwa na tatizo la kulala sana lakini
    akaniangalia moja kwa moja usoni na
    kusema kuwa nilikuwa na tatizo la kurudi tena
    kitandani baada ya kuamka, nilikuwa
    naangukia majaribu ya kutaka kulala dakika zingine chache. Yerusalem Mpya Baadaye akaniambia, "Amka twende MUDA UMEISHA na kuna vitu lazima
    kuvifanya". Akanipeleka mahali sijawahi kufika,
    barabara yenyewe ilikuwa mpya
    kwangu. Tukafika kwenye bustani yenye maua mazuri na miti
    mizuri ya kijani kibichi; hakuna kitu
    duniani cha kulinganisha na uzuri huu. Tukakalia kiti cha dhahabu
    kilichokuwa kwenye bustani hiyo nzuri. Tulipokuwa tumekaa, Yesu aliniashiria
    mbele kwa kidole chake na kusema,
    "Victoria angalia, je wauona mji ule?". Nilipoangalia nikaona mji mkubwa uliokuwa na
    mwanga mkubwa. Mji huo ulikuwa mzuri kupita maelezo. Lango
    lake lilikuwa la dhahabu huku liking'aa
    ajabu, na mtu mwenye umri mkubwa alikuwa amekaa
    pale. Mtu huyo alikuwa na ndevu na
    nywele nyeupe. Nilikuwa nimemwona hapo mbeleni na
    nilipomuuliza Bwana, akaniambia kuwa
    ni Abrahamu, baba wa Imani. Niliona barabara nyingi ndani ya mji ule
    zilizojengwa kwa dhahabu. Kulikuwa na
    majumba ya ghorofa yalokuwa yaking'aa kama
    dhahabu. Mng'ao wa jiji lile kwa kweli
    hauelezeki. Yesu akanigeukia na kuniuliza,
    "Unafikiria nini juu ya mji ule?" Nilijibu kuwa ni mji mzuri na nataka
    niende huko. Yesu akasema,
    "Nitakupeleka huko ukiendelea kuwa mtiifu, maana ndiko iliko nyumba
    yako. Ishi kwa uaminifu ukishindwa,
    nyumba yako Page 8 Page 8 of 8 itakaliwa na kunguru na bundi. Itakuwa
    uwanja wa pepo wabaya. Hata hivyo
    usihofu, kwasababu niko pamoja nawe, wewe kuwa mtiifu tu.
    Asiyetii nyumba yake itakuwa makazi ya
    bundi na uwanja wa mapepo wabaya". Yesu Kristo kweli yupo na anatupenda
    kwa upendo usioelezeka. Hitaji kubwa la
    moyo wake ni wanadamu tuchaguwe uzima ili tukae
    nae milele. Moyo wake unaugua kwa ajili ya
    watu wanao kufa na kuishia kuzimu kwasababu ya kuuacha wokovu aliowapa na kuchagua mauti. Haijalishi umeokoka au haujaokoka
    neno moja tu ukumbuke ni kuwa: MUDA KWA HARAKA SANA UNAKWISHA.

    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate