Wafilipi 2:10-11
  • UJUMBE KUTOKA KWA BWANA KWA WACHUNGAJI,MAKASISI NA WAKRISTU:

    Umeandikwa na Dkt. Augostino
    Maquengo Ulipokewa na Dkt. Augostino
    Maquengo mnamo tarehe 16/5/11: www.DivineRevelations.info/SWAHILI Bwana alinitembelea asubuhi mara tu
    nilipofika ofisini. Niliuhisi uwepo Wake
    kisha mkono
    ukanijia juu ya mabega yangu.Nami
    nilihisi moto juu yangu na nikaisikia
    sauti ya Bwana ikiniongelesha akisema: " yaandike chini
    na uwaambie." Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenyezi
    Mungu kwa wachungaji, wainjilisti,
    makasisi na
    watumishi wengine: " ghadhabu yangu
    itawamaliza" Nanyi hamtanyakuliwa,
    kwani mmeziacha njia zangu na kuwafanya kondoo wangu
    mali yenu binafsi na chanzo cha utajiri
    wenu ,Kwa hiyo
    Bwana hatawanyakua wachungaji
    hawa,wanjilisti na watumishi wangu
    waliopenda ufanisi badala ya ujumbe wa kutubu,kubadilika, kuja
    kwangu ambako kuko karibu na mada ya
    kunyakuliwa. Kanisa wanalolisema kuwa langu,
    limekuwa ukumbi wa kujitumbuiza
    likiongozwa na
    wachungaji,makasisi na mashemasi wa
    kanisa. Wala na kunywa na
    kusherehekea nyumbani mwangu na mbele yangu pasina
    kuogopa,kutetemeka au kuniheshimu.
    Oh, Utukufu Wangu
    umeondoka mahekaluni mwao na
    uwepo Wangu uliondoka kitambo kutoka
    makanisani mwao. Wao hawatanyakuliwa wasiponililia
    mimi Mungu wao kwa uchungu katika
    toba. Watumishi wangu wamepotoshwa na
    ulimwengu nao sasa wanafanya
    mipango ya kuingiza njia za
    kiulimwengu makanisani. Wao
    husherehekea siku ya wapendanao
    kanisani na pia husherehekea siku ya kimataifa ya waongo kanisani
    ,nao husema katika siku ya kuomboleza
    ,leo ni siku ya
    majonzi nasi basi tuvalie mavazi meusi.
    Wote wamepotoshwa. Wachungaji,wainjilisti na makasisi
    wametabiri nyakati za utele,nyakati za
    kukombolewa na
    kufanikiwa ilhali panakuja humu
    ulimwenguni misiba na mateso
    makubwa, na kuharibiwa kwa ulimwengu. Watumishi wangu
    hawanisikii kamwe. Wamejipotosha na ulimwengu na hata
    wameziacha njia zangu. Wao hawanitafuti katika maombi
    ,kufunga na kulitafkari neno langu. Wao
    hufunga na kuomba ili
    kuniomba vipawa vya kuponya,miujiza
    na kutabiri kwa manufaa yao wenyewe.
    Na hata wao husema: Nitatayarisha ujumbe wa
    kuhubiri. Nitatayarisha mkutano. Mimi
    nina shughuli nyingi ya
    kuwapa ushauri nasaha waumini.lazima
    niwatunze waumini, nao hawana wakati
    kwa ajili yangu Mimi, ambaye ndiye mmiliki wa kondoo
    hawa. Hawa wachungaji
    hawatanyakuliwa asema Bwana
    wa majeshi. Ikiwa hamniogopi mimi, basi
    zirarueni nguo zenu,nyoyo zenu na hata
    akili zenu kwa machozi na kutubu. Nataka toba la
    kitaifa la kanisa ,maombolezo na kilio.
    Mjivishe mavazi ya vumbi na mlie kwa toba la sivyo nyinyi
    hamtakuja kwangu mbinguni. Page 2 2 Kondoo wangu wanakula chakula kilicho
    oza,kilichorogwa kutokana na jumbe za
    watumishi Wangu na hawa wachungaji. Wanaekeza kwa ajili ya siku za usoni
    kwa miradi ya ujenzi kanisani nao
    hawafahamu kwamba hii miradi yote itakatizwa na maangamizo
    na majangwa ya ghafla. Baada ya
    kuliokoa kanisa langu kutoka humu ulimwenguni,hii miradi yote
    ya ujenzi itageuzwa kuwa bure. Ni
    viwekezo ambavyo havita zaa chochote. Badala yake yafaa muwekeze katika
    kuhubiri neno la uhai lisilo bandia.
    Hubirini badala yake Kufanikiwa kwa nafsi na roho kupitia
    kwa toba na uzima wa milele. Bwana
    asema hivi, nalipenda sana kanisa langu,ambalo hunitafuta
    kila siku na huliogopa jina langu
    takatifu!! Wakati umekwisha. Wakati umefika
    tamati. Saa yaja sasa hivi,
    nitakapolinyakua kanisa langu. Mara tu baada ya tukio hili, Majanga,
    misiba, na mateso ya kutisha ambayo
    haijawahi kuwa humu duniani itaangamiza maisha
    mengi. Wakati adui yangu atachukua
    hatamu, hapatkuwa na toba tena,wala wakati wa kunitafuta
    ,kwani Mimi sitayajibu maombi yoyote,
    neema itakuwa imeondolewa na Roho wangu Mtakatifu
    hatakuwa ulimwenguni. Adui atachukua
    hatamu nanyi mtasaga meno yenu na kupiga mayowe
    mioyoni mwenu kwa mateso na
    kuvunjika. Zivunjeni nyoyo zenu sasa na mzifanye zimwage
    damu ya toba,zipasuenii nyoyo zenu
    kwa toba katika sekunde za mwisho za wakati uliosalia,
    la sivyo ghadhabu ya kutisha iwapate. Lakini watu hawa wana roho ya kuasi,
    nao wameasi na kwenda zao. Hakuna
    asemaye moyoni mwake, wacheni sasa tumuogope
    Bwana Mungu wetu apeanaye mvua ya
    sasa na hata ya awali katika wakati wake.Ametuhifadhi kwa
    ajili ya wakati teule wa mavuno. Uovu
    wenu umeyageuza mambo haya, na dhambi zenu zimezuia
    mambo mazuri kuja kwenu. Kwani miongoni mwa watu wangu
    panapatikana watu waovu,
    wananyemelea kama afanyavyo yule amtegae nyoka,wameweka mitego
    na wamewanasa watu. Kama vile
    kizimba kilivyojaa ndege basi ndivyo nyumba zao zimejaa
    udanganyifu, kwa hivyo wao wamekuwa
    wakubwa na tajiri sana. Wao wamekuwa wanono, wanang'ara,
    naam, wamezidi matendo ya waovu,
    wao hawahukumu vyema mambo ya wakiwa lakini bado
    wanafanikiwa; na haki za wanyonge
    hawazihukumu au kuzitilia maanani. (Jeremiah 5:24-28) Nyinyi hamtanyakuliwa asema Bwana,
    isopkuwa mbadilishe mienendo yenu na
    kutubu. Mimi sitawanyakua wale waliooana na
    televisheni, sinema na burudani ambazo
    zimechukua muda wenu mwingi nanyi hamna wakati
    kwangu miye Mungu na neno langu. Mimi sitawanyakua wakristu waendao
    kanisani jumapili pekee ili kutuliza
    ghadhabu yangu juu ya maisha yao ,nao wanadhani kwamba
    Mimi Mungu sioni wala kuyafahamu yale
    wafanyao. Jumapili, wao huenda tu kanisani
    kujionyesha nguo zao nzuri na kupiga
    gumzo na marafiki wao. Nyumba yangu imekua mtandao wa
    kijamii . Mimi Yesu Kristo, Bwana wenu
    sitawanyakua wale wanaoutumia muda
    wao mwingi kuitazama televisheni au katika kuvisoma vitabu
    vya riwaya na mambo mengine.Kwa
    sababu wamezigeuza riwaya hizi pamoja na mafunzo ya
    kisayansi kuwa washauri wao, badala ya
    kuwa na Roho Mtakatifu kama rafiki wao wa kweli tena
    bora. Muumini yeyote aliyesahau kumtafuta
    Roho Wangu Mtakatifu na amezifanya
    televisheni na itikadi zingine za kipepo kuwa marafiki wake
    wa dhati badala ya neno Langu ata
    achwa nyuma kukumbana na mpinga Kristu na alama
    ya mnyama muovu. Page 3 3 Mapepo yamefaulu kujiipenyeza ndani
    na katikati ya kanisa na kanisa leo
    limegeuzwa kuwa na tabia na itikadi za kipepo,
    badala ya kuwa na neno Langu na tabia
    zangu Mimi Bwana Yesu. Kanisa kama hili lita achwa nyuma. Wale waishio maisha yao wakiitangaza
    miili yao kwa kuvaa miundo ya nguo iliyo
    chafu na isiyokuwa ya heshima, wakiiweka wazi
    na kuionyesha matiti yao na kuifunua
    miili yao;huu bila shaka ni mfumo wa kidunia. Wakrsitu
    hawa wananiambia Mimi Mungu wao,
    Mungu , tayari nimekupa moyo wangu na hiyo
    imetosha. Kuhusu sehemu yangu ya nje,
    niache niitunze kwa kuvaa nipendavyo. Wacha ijulikane kweli kwamba tayari ni
    mekwisha waacha muishi na kuufurahia
    ulimwengu. Kwani hamfahamu kuwa Mimi ni Mungu
    aliye na wivu? Mimi nina wivi kwa ajili
    yenu lakini nyinyi mnanishiriki na ulimwengu, kamwe
    sitokubali hivyo. Muumini yeyote ambaye amenigeuza
    kitu cha kuchezea asemaye moyoni
    mwake; Mungu sio mbaya hadi hawezi elewa kwamba
    tunaishi katika karne ya ishirini na moja
    na kwamba sisi huishi jinsi tuishivyo. Wakati wa Nuhu uovu ulikuwa mchache
    kuliko sasa, wakati wa luti hapakuwa na
    uovu kama leo, kwa hiyo tubuni la sivyo hamtakuwa na
    udhuru. Mimi sitawachukua wale
    wanunuao,kuuza na kucheza michezo
    siku yangu takatifu ya kuabudu ya jumapili au jumamosi. Siku yoyote ile viongozi wenu
    wameweka kwa ajili ya kuniabudu Mimi
    ni sharti iwe Yangu pekee, Mimi ndiye Bwana. Siku hii lazima itakaswe kwangu pekee.
    Watu hawaniheshimu Mimi Bwana na
    Mungu wao. Wao huniambia na kubishana na
    watumishi wangu wa kweli wakisema hii
    ni sheria nasi tu katika wakati wa neema.Kwani Bwana wenu
    hawezi kuheshimiwa na kuogopwa? Kwani neema yamaanisha kumkosea
    heshima Mungu wenu? Nyinyi
    hubishana nami hata maombini namna vile mtabishana
    muunapo ujumbe huu. Mimi sitawachukua waongo,wenye
    kiburi, waumini wabatili ambao marafiki
    wao wakuu ni watu wa kawaida nao hujipotosha wenyewe
    na ulimwengu. Mimi Bwana na Mungu
    wenu nimewaamuru katika neno langu jitengeni kutoka
    miongoni mwao nanyi msijihusishe na
    kongwa zisizo sawa. Mimi sitawachukua wale waongezao
    maneno yao ndani ya ukweli , wale
    wawasengenyao watumishi wangu na wachungaji ambao
    hunitumikia kwa kweli na kulibeba neno
    langu. Ole wake Yule aongezae na kuondoa kutoka kwa
    neno langu la unabii ! Huu ndio msimamo wangu, kubalini au
    kataeni asema Bwana. Mimi Yesu mesia, Mungu wenu na
    hapana mwingine. Jitayarishe ,jitayarishe Mimi naja upesi!

    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate