naBill Wiese Imenakiliwa kutoka katika CD ya audio,
Sio kutoka katika kitabu chake. Kwa
simulizi iliyokamilika, tafadhali nunua
kitabu chake! Hii
imetoka katika mkutano wa Kansas City,
KS ulioitwa "Kansas City kwa ajili ya America". Uzoefu huu wa kuzimu
ulitokea Novemba 23,
1998. www.DivineRevelations.info/ SWAHILI (Utangulizi na mtangazaji) Miezi michache iliyopita, Mike Bickle,
ambaye ninafanya kazi nae katika
Nyumba ya Kimataifa ya Maombi (International House of Prayer), alinisihi nifundishe juu ya somo la Kuzimu.
Wakati najifunza somo hilo, nilipewa
kanda na rafiki aitwaye Steve Carpenter,
kwenye kanda hiyo kulikuwa na ujumbe
ambao utaenda kusikia kutoka
kwa Bill Wiese na mke wake Annette. Ujumbe wake ulibadili Dunia yangu. Na
moja kwa moja ilibadili namna
ambavyo familia yangu, marafiki zangu,
na hata watu nisiowajua. Iliwabadili
moja kwa moja. Siongezi
chumvi,kwa hiyo usifikirie naongea kwa kuzidisha maneno hapa, Ilibadili jinsi
navyotazama kweye miaka
michache niliyobakiza hapa duniani. Ni
maombi yangu kwamba Mungu atafanya
hivyo hata kwako leo. Siongezi
chumvi umuhimu wa ujumbe huu. Bill ni Mkristo. Aliyatoa maisha yake kwa Kristo
alipokuwa na umri wa miaka
16. Amemjua Bwana kwa miaka 32.
Alihamia California mwaka 1976 na
alitumia miaka 10 akiwa chini ya
huduma ya Mchungaji Chuck Smith pale Costa Mesa , California. Bill ni muonaji,
kama alivyo mke wake. Kwa
miaka 15 iliyopita , Bill amekuwa katika
mikutano na katika uongozi kwa misimu
tofauti ya Eagles Nest, chini ya
uchungaji wa Dk Gary Greenwald , pale Orange County, California. Mchungaji
huko Eagles Nest aitwaye
Mchungaji Raul alikuja kwa Bill na
alisema miezi kadhaa iliyopita , "Bill,
Mungu atakwenda kufanya kazi ya
uamsho atakwenda kuanzia Cansas City kwa America. Atakupeleka pale na
inabidi uende". Bill na Annette
hawakuwahi kwenda Kansas City katika
maisha yao yote. Siku iliyofuata, mimi
nilimpigia Bill na nikasema," Je,
unaweza kufikiria kuja Mji wa Kansas? Nimeona video yako na nadhani
unatakiwa kuja . " Naamini wako hapa
kwa ajili ya amri ya Mungu. Utaenda kusikia maono ya Kuzimu,
lakini muhimu zaidi, utakwenda kusikia
maono ya uhusiano wa karibu na Yesu Kristo na upendo alionao kwa
dunia nzima. Bill alikuwa kuzimu.
Hakuwa akiangalia kwa kawaida, kama watu wengi wamekuwa katika maono
halali, lakini alipata uzoefu wa mateso
ya kuzimu kwa muda wa nusu saa na hakuwa na matumaini kabisa ya kutoka
milele. Bill na mke wake wamejitoa kwa
Yesu Kristo kikamilifu, na kwa kazi ya Mungu, na kwa uongozi wa Roho
Mtakatifu. Utakwenda kumsikiliza pia.
Tafadhali nawakaribisha Bill na Annette Wiese. Page 2 2 (Bill Wiese anaongea) Ni heshima kuwa hapa. Safari hii yote
imekuwa baraka sana kwetu. Kama Hal
alivyosema, Tuko katika biashara isiyotambulika sana. Hatufanyi hivi kwa
ajili ya kuishi. Hatufanyi hivi kwa fedha.
Sisi tunachojua ni kwamba Mungu ametuambia kwenda na
kuwaambia dunia kuhusu upendo wake
kwa watu na mahali pale Yeye hataki yoyote wa viumbe wake kwenda. Hiyo
ndiyo sababu tuko hapa. Hivyo, kwa ajili
ya muda, nitakwenda kufupisha ushuhuda huu na kusimulia moja kwa
moja. Lakini kwanza nataka kusema mambo
kadhaa, maswali ambayo yanaweza
kuwa katika akili yako. Swali la kwanza kwangu kama ingekuwa
najisikiliza, ingekuwa, "Umejuaje
haikuwa ndoto tu uliyoisikia? Ndoto
mbaya?" mambo kazaa ya kuzingatia, kwanza
kabla ya yote, Niliuacha mwili wangu.
Nikauona mwili wangu wakati narudi, umelazwa juu ya sakafu. Hivyo nilijua
kwa uhakika nilikuwa nje ya mwili (out of
body experience). Baadhi ya wakristo wamesema, "Oh Mkristo hawezi
kuuacha mwili wake." Lakini hiyo si kweli,
Katika 2 Wakorintho 12:2, wakati Paulo alipokuwa juu katika
mbingu ya tatu, Alisema, "kama katika mwili, au nje ya mwili sijui." Hivyo kama hujui hii inamaanisha kuwa
inawezekana. Na pia alisema katika
mstari wa kwanza kwamba ilikuwa ni maono, hivyo naamini hii inakuja chini
ya uainishaji wa maono. Katika Ayubu 7:14 inasema, "unitishapo kwa ndoto na kunishangaza mimi kwa
maono." Hivyo hii ni dhahiri hiki ndicho Bwana alifanya, alinishangaza
kwa njia ya maono. Pia niliporudi kutoka
katika uzoefu huu, ilinichukua mwaka mzima kutulia, na kuwa kama
mtu wa kawaida tena. Nilikuwa
nimezimia moyo na kuchanganyikiwa kutokana na hofu kwamba ilibadili
mtizamo wangu wa jinsi ya kushuhudia
na kiasi gani kutambua kile nini Mungu alituokoa nacho. Nitamuomba mke wangu aje kwa dakika
chache ili aweze kushiriki tu kilichotokea
wakati yeye aliponikuta katika sebule, kwa sababu mimi sikumbuki kwa
sehemu hiyo. Hivyo nataka yeye aseme
maneno machache. Asante. (Mke wa Bill anaongea) Ilikuwa yapata saa 09:23 alfajiri
nilipoamka. Nimekumbuka hilo kwa
sababu nilitazama saa yetu ya digital, na niliona Bill hakuwa karibu na mimi,
nikasikia kelele zinatokea sebuleni.
Nilianza kutembea/kushuka koridoni. Nilimuona mume wangu kwa namna
ambayo sikuwahi kumwona kabla. Kama
kuna mtu anamjua Bill, yeye ni mtu wa misimamo kwa asili, mtaratibu sana,
na mtu mtaalamu. Yeye si mtu wa
kupata msisimko tu au kupata hisia za haraka juu ya kitu chochote, isipokuwa
Mungu anapokuwa kazini. Lakini,
hatahivyo, nilimuona pale akiwa ameshikwa na butwaa/mshangao, akiwa
ameshika kichwa chake, akiwa ameweka
kichwa chake katika mikono yake akipiga kelele na mayowe. Alikuwa
katika hali ya kujilaza chali sakafuni
amejikunja. Sikujua nini cha kufanya. Nilidhani alipatwa na ugonjwa
wa moyo. Nilianza kuomba na alilia na
akasema, "Omba kwa Bwana ili aliondoe hili nje ya akili yangu! Bwana
amenipeleka Kuzimu. Najisikia kama
mwili wangu umekufa, siwezi kulibeba hili." Kwa hiyo nikaendelea
kuomba juu yake, na katika muda wa
dakika kumi hadi ishirini alianza kutulia. Alikuwa katika hali ya
mshangao, kama mtu ambaye alikwenda
Vietnam na akatokea tena kwa mara ya pili, au mtu aliyeponea ajali ya gari ya
kutisha. Haikuwa tu mtu ambaye alikuwa
anaota ndoto mbaya na akaamka. Hivyo ndivyo nilitaka kushuhudia. (Bill Wiese anaongea) Nimebarikiwa kuwa na mwanamke
mzuri. Kweli namshukuru Mungu.
Nimekuwa katika ndoa kwa miaka
minne, na nimemjua kwa miaka sita ya maisha
yangu, ninaweza kusema, asifiwe
Mungu. Nilitaka kujua zaidi niliporudi kutoka
katika uzoefu huu, kama kuna yoyote
katika Biblia ambaye amewahi kupata uzoefu huu. Kwa hiyo nikaanza kufanya
utafiti. Huwa namsikiliza Chuck Missler
sana. Yeye ni mwalimu wa Page 3 3 Biblia katika mataifa mengi, msomi halisi
na yeye alisema kuwa Yona alipatwa na
uzoefu wa Kuzimu. Katika Yona 2:2 inasema, "katika Kuzimu alipiga kelele." Na Katika Yona 2:6 inasema, " Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na mapingo yake
yalinifunga hata milele; Lakini
umeipandisha nafsi yangu kutoka
shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu, Basi angalau kulikuwa na mtu katika Biblia mwenye
uzoefu na kuzimu, Yona. Nilitaka kujua, kwa sababu nilikulia katika siku
za mwanzo za kanisa la Calvary, uzoefu
wowote wa kiroho ambao uliupata ni lazima uendane na Neno la Mungu.
Hivyo nilijua kuwa kama uzoefu huo ni
kweli, basi utakuwa tayari upo katika maandiko. Kwa hiyo nikaanza
kufanya utafiti na nimeona zaidi ya
maandiko 400 ambayo yanaonyesha kila kitu nilichokiona, nilichosikia, nilichohisi,
na kila kitu kinachohusiana na Kuzimu.
Tayari kimeandikwa, hivyo chochote nawaambia tayari kiko pale.
Nitafanya kukuhakiki baadhi ya
maandiko. Siwezi kunukuu yote 400,
lakini nitafanya kwa baadhi. Pia walipatikana
watu 14 wengine ambao tayari walikuwa
na uzoefu wa baadhi ya sehemu ya Kuzimu. Wengi wao walikuwa karibu
na kifo, watu katika hospitali waliokufa
wakarudia tena uhai wao. Hivyo kwa haraka tu: Mimi na mke
wangu tulikuwa katika mkutano wa
Jumapili usiku wa maombi ambao sisi mara nyingi hudhuria na wachungaji
wetu. Na baadae tukaenda nyumbani
kama kawaida ili kulala. Ilipofika saa 09:00 asubuhi nilichukuliwa. Sikujua
jinsi nilivyoondoka pale mpaka wakati
niliporudi. Kisha Bwana alianza kunielezea. Hata hivyo nilitupwa tu katika chumba
cha gereza, kama gereza lolote
unaloweza kufikiria, lenye kuta mbaya
na mihimili ya mlango. Sikujua bado
ambapo nilikuwa. Nilichojua ni kwamba
kulikuwa na joto sana, joto sana. Sikuamini, kwamba nilikuwa bado hai.
Nilihisi kama ningekufa na kujitenga na
moto huu, lakini bado nilikuwa hai. Kulikuwa na mwanga mdogo katika
chumba kwa muda kidogo, na nikaamini
kuwa uwepo wa Bwana ulikuwa pale kwa ajili yangu ili niweze kuona
tukio zima kwa uzuri, lakini baada ya
dakika moja giza liliingia tena Katika Isaya 24:22 inasema: " Nao watakusanywa pamoja kama vile
wakusanywavyo wafungwa katika shimo
nao watafungwa katika gereza…. Mithali 7:27 " Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka
vyumba vya mauti" Kwa chemba ina maana ya vyumba". Kwa hiyo sehemu ya
kuzimu ina selo, vyumba, mashimo ya
moto, na maeneo makubwa ya moto, hivyo nilikuwa katika selo ya
kuzimu. Katika Yona 2:6, "Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele…; " Na Ayubu 17:16 "Litashuka kwenye makomeo ya kuzimu,… " Kwa hiyo tena, kila kitu nilichokiona
kilikuwa katika Neno. Mawe
yanaongelewa katika Isaya 14:19. Nikajikuta katika selo, na viumbe hawa 4
walikuwa katika selo na mimi. Sikujua
walikuwa mapepo wakati huo, kwa sababu nilikwenda huko kama mtu
ambaye hajaokoka. Mungu aliliondoa
hili katika akili yangu kwamba mimi ni Mkristo niliyeokoka. Sikuelewa
kwa nini, lakini alinifafanulia kwangu juu
ya hili hapo nilipokuwa nikirudi. Viumbe hawa, sikuweza
kutambua kwamba walikuwa mapepo,
lakini walikuwa wakubwa. Walikuwa kama futi 12 au 13 kwa urefu, mmoja
utamuona katika video. Mmoja wa watu ambao walitoa ushuhuda wao, aliona pepo sawa na yule niliyemuona.
Hivyo utaona mmoja anavyofanana.
Kuna picha nzuri kwa kweli katika video ambapo kijana mmoja alivutwa
hadi katika misingi ya Kuzimu. Ni
ushuhuda wa Kenneth Hagin.. Kivyovyote walikuwa wanatisha. Huyu
mmoja alikuwa na magamba juu ya
mwili wake wote, taya kubwa na meno makubwa, na makucha
yamejitokeza, pamoja na macho
yalioingia ndani. Yaani walikuwa
wakubwa. Na huyu pepo mwingine hakuwa
anaonekana kama huyu kabisa, lakini
alikuwa na mapezi makali pote na
mkono mmoja mrefu na miguu isiyo na uwiano.
Kila kitu kilikuwa kimekaa vibaya na
vilicheza pasipo uwiano, hakuna Page 4 4 ulinganifu, hakuna ulinganifu, mkono
mmoja mrefu na mmoja mfupi yaani ni
viumbe visivyo na muonekano mzuri, vinatisha, vya kuogofya. Basi, walikuwa wanamtukana Mungu.
Muda wote walikuwa wanamlaani
Mungu. Mimi nikajiuliza, "Kwa nini wanamlaani Mungu? Kwa nini
wanamchukia Mungu hivyo?" Kisha
wakanigeukia mimi, na mimi nikahisi
vivyo hivyo wanavyojisikia kwa Mungu na
mimi wananichukia na tena Nilifikiri: Kwa
nini wanachukia?Na sijafanya lolote kwao" Lakini wananichukia mimi
na chuki ambayo sijawahi kuiona katika
dunia; kwa namna zaidi ya mwanadamu anaweza kunichukia.
Kabisa walinichukia mimi, na mimi
nilifahamu walikuwa wameletwa ili wanitese. Kulikuwa na mambo ambayo
nitakwenda kusema, ambayo sijui ni
jinsi gani niliyajua. Kule kuzimu fahamu
zako ni halisi zaidi, unafahamu zaidi ya miili
yetu. Niliweza kufahamu umbali,
Nilifahamu muda, na kadhalika, nilifahamu mengi zaidi kuliko
unapokuwa hapa. Nilijua mapepo hayo
yaliwekwa pale kwa ajili yangu, ili
yanitese milele mahali hapo. Nilikuwa nimelala juu ya sakafu katika
selo hii na sikuwa na nguvu kabisa katika mwili wangu.
Nikajiuliza, "Kwa nini siwezi hata kujisogeza, nina tatizo gani?"
Nilikuwa nafahamu kuwa sina nguvu, na sikuwa na msaada
wowote. Pepo moja likanibana na kunichukua na kunirusha kwenye
ukuta kama kioo. Alinichukua kama uavyochukua kioo.
Hivyo ndivyo jinsi nilivyokuwa mwepesi, au jinsi nguvu
zake zilivyokuwa. Na Alinirusha katika ukuta, na kila mfupa
katika mwili wangu ulivunjika. Na nilihisi maumivu! Nikawa
nimejilaza sakafuni nikipiga kelele za kutaka msaada, lakini
viumbe hawa hawana huruma yoyote wakati wote, hawana
huruma kabisa. Mmoja alininyanyua, na mwingine
mmoja, mwenye makucha makali mithili
ya wembe, aliukata mwili wangu. Akaurarua kabisa, na hakuwa anajali
kabisa kwa habari ya mwili huu wa ajabu
ambao Mungu aliuumba. Alikuwa na chuki ambayo ilikuwa ni kali sana
dhidi yangu. Nikajiuliza, "Kwa nini niko
hai, kwa nini ningali hai katika hili? Sielewi kwa nini sijafa." Mwili wangu
ukawa umetundikwa katika riboni/cheni.
Na hapakuwa na damu, ila ni mwili tu umetundikwa, kwa sababu
maisha yako katika damu, na hakuna
maisha Kuzimu. Na hakuna maji katika Kuzimu. Katika Isaya 14:9-10 inasema Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili
yako, Ili kukulaki utakapokuja;
Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa
dunia; Huwainua wafalme wote wa
mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi. Hao wote watajibu na
kukuambia, Je! Wewe nawe umekuwa
dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi! Zaburi 88:4 Nimehesabiwa pamoja nao washukao
shimoni; Nimekuwa kama mtu asiye na
msaada. Page 5 5 Na tunafahamu ya kuwa shetani anazo
nguvu, katika maandiko ambapo
palikuwa na mtu mwenye pepo akiishi katika eneo la makaburi, biblia inasema: Marko 5:1-4 Wakafika ng'ambo ya bahari mpaka nchi
ya Wagerasi.Na alipokwisha kushuka
chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka
makaburini, mwenye pepo mchafu;
makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote
aliyeweza kumfunga tena, hata kwa
minyororo; kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa
pingu na minyororo, akaikata ile
minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa
na nguvu za kumshinda. Hawakuweza kumfunga, alivunja
minyororo vipande vipande. Na huyo
alikuwa tu mtu mwenye nguvu ya
mapepo. Nilielewa mapepo haya yalikuwa na
nguvu mara 1000 zaidi ya mtu. Hivyo
hata kama nilikuwa na nguvu yangu ya asili, sikuweza kupigana nao
kuwashinda. Hivyo nilikuwa pale
nikitegemea huruma yao, ambapo
hawakuwa na huruma yoyote. Mapepo huongoza
maisha yako kuzimu. Harufu ya mapepo haya na harufu ya
Kuzimu ilikuwa mbaya inatisha, Siwezi
hata kukuelezea wewe. Kulikuwa na harufu ya mwili unaoungua, na ya salfa.
Harufu ya mapepo haya ilikuwa kama
mfereji wa maji machafu ulio wazi, yaliyooza, nyama iliyooza, mayai
yaliyoharibika, maziwa yaliyochacha na
kila kitu ambacho unaweza kufikiria. Zidisha, mara 1000, na uiweke juu ya
pua yako. Na uvute hewa ndani. Ilikuwa
na sumu sana,ambayo inaweza kuua, kama ungekuwa hapa katika mwili
huu, unaweza ukafa. Na mimi nilijiuliza,
"Kwa nini naweza kuishi katika harufu hii, na ni mbaya sana ya
kutisha?" Lakini tena huwezi hata kufa,
unatakiwa kuivumilia. Makufuru, ambayo walikuwa
wakimkufuru Mungu yameelezwa katika Ezekieli 22:26 " nami nimetiwa unajisi kati yao. " Kufuru, lugha ya matusi na kukashifu. Mateso waliyokuwa wakinifanyia
yametajwa katika Kumbukumbu la
Torati 32:22-24. Maana, moto umewashwa kwa hasira
yangu, Unateketea hata chini ya kuzimu,
Unakula dunia pamoja na mazao yake, Unaunguza misingi ya
milima. Nitaweka madhara juu yao
chunguchungu; Nitawapiga kwa mishale yangu hata
ikaishe;Watakonda kwa njaa, wataliwa
na makaa ya moto, Na uharibifu mkali; Nitawapelekea meno ya wanyama
wakali, Pamoja na sumu ya wadudu
watambaao mavumbini. Hivyo kuna meno ya mnyama juu yako. 2 Samueli 22:6 inasema: Kamba za kuzimu zilinizunguka; Mitego
ya mauti ikanikabili. Na katika Mika 3:2 kuna mstari wa mzuri ambapo wafilisti, waliowachukia
waisraeli walisema: Ninyi mnaoyachukia mema, na
kuyapenda mabaya; ninyi mnaowachuna
watu ngozi yao, na nyama mifupani mwao. Page 6 6 Hivyo ndivyo walivyowafanyia watu wa
Israeli. Hiyo ilikuwa katika uhalisia, je ni
wapi walipata wazo hilo? Hilo wazo la kufanya hivyo lilitoka kuzimu.
Hivyo ndivyo mapepo hufanya, na
rehema je? Kuna rehema Mbinguni tu. Rehema inatoka kwa Mungu, na shetani
hana maarifa yeyote kuhusu wema
wowote ule, yuko kinyume kabisa kuhusu hilo. Zaburi 36:5 " Ee Bwana, fadhili zako zafika hata
mbinguni, Uaminifu wako hata
mawinguni.." Na Zaburi 74:20 inasema: Ulitafakari agano; Maana mahali penye
giza katika nchi Pamejaa makao ya
ukatili. Ni mahali pa kutisha penye ukatili,
huzuni ambao unatakiwa uvumilie.
Unatakiwa kuvumilia mambo haya yote. Mungu amemfanya mwanadamu kwa
kiwango cha juu cha uumbaji, na
mapepo haya ni uumbaji wa kiwango
cha chini. Sisi kama binadamu tunafanya
kazi kwa bidii ili kuendelea mbele na
maisha, tunajifanyia ubora sisi wenyewe, tunajifunza. Lakini kule
kuzimu, maisha yako yanaongozwa na
mapepo. Viumbe hawa wana IQ sifuri, viumbe hawa ni wajinga kabisa. Kile
wanacho kijua ni chuki kwa Mungu,
chuki kwako wewe na mateso. Na wanaongoza maisha yako, na huwezi
kufanya lolote kuhusu hilo. Kuna maandiko kuhusu udhalilishaji
unaotakiwa kukabiliana nao. "Jambo hili
linakwenda kuongoza maisha yangu, siwezi kuliacha!" Katika Isaya 5:
14-15 Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa
yake, kumefunua kinywa chake bila
kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia
afurahiye miongoni mwao, hushuka na
kuingia humo. Na mtu mnyonge ainamishwa, na mtu mkubwa
amedhilika, na macho yao walioinuka
hunyenyekezwa, Isaya 57:9-16 Ulimwendea mfalme na mafuta ya
marhamu, ukaongeza manukato yako,
ukawatuma wajumbe wako waende mbali, ukajidhili sana hata
kuzimu. Ulikuwa umechoka kwa ajili ya
urefu wa njia yako; lakini hukusema, Hapana matumaini; ulipata
kuhuishwa nguvu zako; kwa sababu hiyo
hukuugua. Tena ni nani uliyemwogopa na kumhofu, hata
ukasema uongo, wala hukunikumbuka
mimi, wala kuweka hayo moyoni? Je! Mimi sikunyamaza tangu
zamani, hata huniogopi?Mimi
nitatangaza haki yako, na matendo yako hayatakufaa. Utakapolia,
na wakuponye hao uliowakusanya; lakini
upepo utawachukua; uvuvio tu utawachukulia
mbali; lakini yeye anayenitumaini
ataimiliki nchi, na kuurithi mlima wangu mtakatifu. Naye atasema,
Tutieni, tutieni, Itengenezeni njia,
Kiondoeni kila kikwazacho Katika njia ya watu wangu. Maana yeye
aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele;
ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi
mahali palipoinuka, palipo patakatifu;
tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili
kuzifufua roho za wanyenyekevu, na
kuifufua mioyo yao waliotubu. Kwa kuwa sitashindana na
watu siku zote, wala sitakuwa na hasira
siku zote; maana roho ingezimia mbele zangu, na hizo nafsi
nilizozifanya. Ezekieli 32:24 Elamu yuko huko, na watu wake wote
jamii, pande zote za kaburi lake; wote
pia wameuawa, wameanguka kwa upanga, walioshuka
hali hawana tohara hata pande za chini
ya nchi; ambao Page 7 7 waliwatia watu hofu katika nchi ya walio
hai, nao wamechukua aibu yao, pamoja
nao washukao shimoni. Inaendelea na kuendelea. Hiyo ilikuwa
ni kitu kibaya kuona maisha yako
yanaongozwa na viumbe hawa, ambao hawana hata huruma kwa lolote lile! (Giza na vilio kuzimu) Nilikuwa nimelala katika selo na mara
pakawa giza, kiini, kiini cha weusi wa
giza. Namaanisha giza ambalo sijawahi kuliona kabla. Na nilikuwa chini
kabisa katika mapango, ni chini sana
kama katika migodi ya chuma kule Arizona. Kulikuwa na giza ambalo
huwezi hata kufikiria. Niliweza kutambaa
kuelekea nje, kwa namna fulani niliweza kutambaa na waliniacha
kidogo. Nilikumbuka ambapo mlango
ulikuwa hivyo nikatambaa kuelekea kwenye mlango na nikatoka nje ya selo.
Nikaangalia mwelekeo mmoja, na
tazama ni peusi pote, na nilichosikia ilikuwa ni mayowe, mabilioni ya watu
walipiga mayowe mahali hapo. Nilijua
kulikuwa na mabilioni, na kulikuwa na sauti kubwa. Kama umewahi kusikia
mtu akipiga kelele, huwa inachukiza.
Naam kama wewe ukisikia mabilioni ya watu wakipiga mayowe,
huwezi kufikiria ni jinsi gani inaathiri akili
yako. Hauwezi kuvumilia. Unajaribu kushikilia masikio yako kwa
sababu sauti ni kubwa lakini inapenya.
Huwezi ukakimbia mayowe haya. Na hofu inayokujia inakuwa ya ajabu.
Kila kitu kinaongozwa na hofu. Hakuna
uwepo wa Mungu katika sehemu hii, hivyo inakupasa kuishinda hofu na
mateso na giza wewe mwenyewe.
Huwezi kuona chochote. Huwezi hata kuona ni kitu gani kinakuja dhidi yako.
Maandiko yanasema sana kuhusu giza
hili Zaburi 88: 6 Mimi umenilaza katika shimo la chini,
Katika mahali penye giza vilindini. Ufunuo16:10 Na huyo wa tano akakimimina kitasa
chake juu ya kiti cha enzi cha yule
mnyama; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao kwa
sababu ya maumivu, Yuda 1:13 Ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika,
yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni
nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao
waliowekewa milele. Na kulikuwa na giza ambalo unaweza
ukalihisi, kama ilivyoonyeshwa Kutoka 10:21 Bwana akamwambia Musa, Nyosha
mkono wako kuelekea mbinguni, kuwe
giza juu ya nchi ya Misri, watu wapapase-papase gizani. Unaweza ukalihisi giza hili. (Hofu kuzimu) Hofu niliyopata niseme tu, ilikuwa kubwa
sana. Inakukamata. Kama umewahi
kuona muvi(tamthilia) za kutisha,ambapo hofu inakukamata
mpaka kwenye koo, sasa unaweza
ukachukulia hiyo na ukazidisha mara
1000 hivi, na ukawa nayo hiyo wakati wote, na
ninafahamu kitu kuhusu hofu.
Nilipokuwa mdogo nilikuwa nikiogelea. Nilipokuwa mdogo sana tulikuwa katika
ufukwe wa Coco Frolida tukiogelea na
kulikuwa na kundi la papa walikuwa wakinizunguka. Na papa wa
karibu futi 9 alikuja na kuupiga ubao
wangu wa kuogelea kwa katikakati. Page 8 8 Alinichuchuka kwa mguu wangu na
kunivuta chini. Hivyo mguu wangu
ulikuwa kwenye mdomo wa huyu papa mkubwa. Nilikuwa bado sijawa mkristo,
nilikuwa hata sijaokolewa. Na mara
gafla aliniacha ili niondoke. Nafahamu Mungu alifungua kinywa cha
Yule papa. Lakini kwa muda mfupi huo
hofu inayokuijia ni kubwa sana ya kushangaza. Kama yeyote amewahi
kuona mataya ya papa, hofu ile ni kubwa
sana huwezi kufananisha mpaka ikutokee. Hofu ilikuwa ni ya kutisha.
Aliyekuwa pembeni yangu alikuwa futi
chache mbali kidogo, papa huyu alimtafuna mguu wake! na wakamvuta
pembeni ya ufukwe, na damu kila
mahali. Alikuwa akilia na mguu ukiwa umeliwa tayari. Kwa hiyo naifahamu
hofu lakini ile hofu haikuwa kitu
ukilinganisha na hofu niliyopitia Kuzimu, Hakuna jinsi ya kufananisha. Nafikiri
hofu niliyoipata juu ya papa ni moja ya
hofu kubwa ambayo tunaweza kupitia hapa duniani. Kwa hiyo haya ni mambo machache
tunayotakiwa kuyashinda kule
kuzimu.Isaya 24:17-18 inasema: Hofu, na shimo, na mtego, vi juu yako,
Ee mwenye kukaa duniani. Itakuwa kila
akimbiaye sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na kila
apandaye na kutoka shimoni atanaswa
na mtego; kwa maana madirisha yaliyo juu yamewekwa wazi,
na misingi ya dunia inatikisika. Ted Koppel, alipokuwa akifundisha
alifundisha akiwa na mada ya "Night
Line" mwaka mmoja na nusu uliopita, aliwatembelea wafungwa baadhi nchini
na akakaa nao usiku mzima mahali pale.
hakuweza kuamini jinsi kulivyokuwa na kelele, hakuweza kulala,
kila mmoja alipiga kelele za juu sana
kwa nguvu zake zote. Alisema alishagazwa jinsi watu walivyopiga
kelele na kuunguruma usiku kucha.
Hivyo hata katika magereza yetu ya duniani, watu hupiga kelele, je ni kiasi
gani kule kuzimu. Katika Ayubu 18:14 inazungumzia maovu ya mwanadamu, kwa mtu atakayemkataa
Bwana... Atang'olewa katika hema yake
aliyokuwa akiitumaini; Naye atapelekwa
kwake mfalme wa utisho. Shetani hakika ni mfalme wa Hofu. (Kuachwa Kuzimu) Sasa nilikuwa nje ya selo na niliangalia
upande huu Niliona miali ya moto, kama
maili 10 hivi kutokea nilipokuwa. Nilifahamu kuwa ilikuwa maili 10. Na
shimo la moto kama maili 3 kwa upana,
lilikuwa na moto uliokuwa ukiwaka mpaka angani ulioweza
kunifanya kuona ardhi ya kuzimu kidogo. Giza lilikuwa ni nene; liliweza kula
mwanga wote. Lakini angalau kulikuwa
na mwanga wa kuweza kuona anga. Palikuwa ni kahawia na ukiwa.
Namaaanisha hakuna hata kijani
kimojawapo, hakuna hata maisha ya
aina yeyote, ni jiwe/mwamba, kuchafu na anga
nyeusi na moshi katika anga. Miali
ilikuwa ni mirefu hivyo niliweza kuiona. Kuna andiko katika Mambo ya nyakati 29:23 Ya kuwa nchi yake nzima ni kibiriti, na
chumvi, na kuteketea, haipandwi, wala
haizai, wala nyasi hazimei humo, kama mapinduko ya
Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu,
aliyoipindua Bwana kwa ghadhabu yake na hasira zake; Hakuna maisha hata hivyo kuzimu.
Inatisha kama nini kuwepo kwenye
ulimwengu ambao hauna maisha. Hapa tunafurahia miti na hewa safi, lakini
mahali pale kila kitu kimekufa. Page 9 9 (Moto) Moto ulikuwa ni mkubwa sana, huwezi
hata kuelezea. Mambo ya nyakati 32:24 inasema; Watakonda kwa njaa, wataliwa na
makaa ya moto, Na uharibifu mkali;
Nitawapelekea meno ya wanyama wakali, Pamoja na sumu ya
wadudu watambaao mavumbini. Yuda1:7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji
iliyokuwa kando-kando, waliofuata
uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya
mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa
dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele. Zaburi 11:6 Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na
kiberiti na upepo wa hari, Na viwe fungu
la kikombe chao. Hicho ndicho kilichokuwa kikiendelea
Kuzimu, pana joto kali. Hivi vitu vyote
vilitosha kabisa kukuua, lakini hufi! Unatakiwa kuendelea kuvumilia haya
mateso. Nilihitaji amani ya moyo,
kuondokana na vilio hivi na kutoka mahali pale. Ni kama ambavyo unataka
kwenda nyumbani usiku baada ya siku
ngumu, unahitaji amani ya moyo. Lakini pale unavumilia mateso yote na
vilio. na hauwezi kamwe kutoka mahali
pale. Isaya 57:21 inasema: " Hapana amani kwa wabaya; asema
Mungu wangu." Pia kuzimu unakuwa uchi. Ni kitu kingine
ambacho inakupasa uvumilie. Aibu! Ezekiel 32:24 inaongelea kuhusu aibu ndani ya kuzimu. Elamu yuko huko, na watu wake wote
jamii, pande zote za kaburi lake; wote
pia wameuawa, wameanguka kwa upanga, walioshuka hali hawana tohara
hata pande za chini ya nchi; ambao
waliwatia watu hofu katika nchi ya walio hai, nao wamechukua aibu yao,
pamoja nao washukao shimoni. Na katika Ayubu 26:6 Kaburi li wazi mbele yake, Uharibifu nao hauna
kifuniko. Hii inamaanisha Mungu anaweza kuona
Kuzimu, Hivyo inaonekana kwake. (Ukame) Hakuna maji kuzimu, kabisa, hakuna.
Hakuna unyevunyevu katika anga na
maji ya aina yeyote. Kuna ukame sana Unakuwa unahitaji maji ya kunywa hata
tone la maji tu, moja tu. Kama vile
ambavyo maadiko yanasema katika Luka 16:23-24, Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake,
alipokuwa katika mateso, akamwona
Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema,
Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume
Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe
ulimi wangu; kwa sababu ninateswa
katika moto huu. Page 10 10 Ibrahimu akasema, "Mwanangu
kumbuka", na kisha aliendelea
kuzungumzia ndugu zake. Alimtaka tu
achovye ncha ya kidole chake katika maji, apate
tone moja tu. Hiyo ingekuwa ni kitu cha
thamani, tone moja, lakini haiwezekani, kupata hata tone. Ni
vigumu kupata picha ni jinsi gani mdomo
wako unakuwa mkavu. Kama unaweza kufikiria kufanya mbio za
marathoni za kufa na kupona na ukawa
na pamba katika mdomo wako na unaendelea kuwa huko kwenye bonde la
uvuli wa mauti kwa muda wote, iendelee
hivyo, kukame, kabisa, unahitaji tone la maji. Kitu kingine andiko hili limebainisha
kwangu tunajua kuna shimo kubwa sana
limewatenganisha kati yao, kuzimu; kati ya peponi na Kuzimu. Na mtu huyu
aliyekuwa tajiri akamwona Abrahamu
kwa mbali. Kwa asili, anawezaje kumtambua Lazaro na Ibrahim? Awali ya
yote kamwe hakuwahi kukutana na
Ibrahimu na kisha kuona mtu kwa mbali namna ile, usingeweza kujua ni
nani hao. Lakini kuna mambo fulani tu
unajikuta unayajua kuzimu. Unaelewa, kama nilivyosema, kuhusu
kina, umbali wake na kadhalika. Kisha pepo mojawapo likanikamata, na
kunirudisha tena selo na nikarudia yale
mateso tena, ambayo sipendi kuyaongelea, kwa sababu sipendi
kuendelea kukumbushia mateso yale.
Walianza kuniponda fuvu langu. Pepo moja likanikamata nakujaribu kupasua
kichwa changu. Nalikuwa nalia mayowe
na kuomba rehema, lakini hakuna rehema! Kwa wakati huu sasa kila pepo
lilishika mkono na mguu wangu na
walikuwa karibu kuniachanisha. Nilifikiri kichwani "siwezi kuvumilia hili,
siwezi kuvumilia hili!" (Jirani na shimo) Na mara gafla, kitu kikanishika na
kunivuta nje ya selo. Najua alikuwa ni
Bwana, lakini wakati huo sikuwa nimejua. Nilikuwa mahali pale kama mtu
asieokoka, kwa hiyo sikujua vitu hivi.
Nilikwenda pale kama sikuwahi kumpokea Bwana. Niliwekwa jirani
kidogo na moto niliouona. Nilikuwa
nimesimama peke yangu pembeni mwa shimo lile. Nilikuwa chini ya pango, kama
pango kubwa, lenye tanuru iliyokwenda
juu. Ndani ya moto ule niliweza kuona ndani miili na watu ndani
ya moto wakilia mayowe, walilia rehema,
huku wakiungua! Na nilifahamu sikutaka kwenda mahali pale.
Maumivu niliyoyapata tayari yalikuwa ni
makubwa lakini moto uliokuwa ukitokea mle kwenye miali ile ya moto
nilitambua ilikuwa ni hari zaidi sana.
Watu hawa waliomba kutoka nje. Kulikuwa na viumbe hawa wakubwa
wamejipanga wamezunguka pembezoni
mwa shimo hilo, na watu walipokuwa wakijaribu kutoka nje,
walirudishwa tena kwenye moto
wasiweze tena kutoka. Nikafikiri, "Oh, hii sehemu ni mbaya, mbaya sana na
inatisha sana." Haya yote yanafanyika kwa wakati
mmoja. Una kiu, una njaa, umechoka.
Pia kuzimu hupati muda wa kulala. Unahitaji usingizi kama unavyohitaji
sasa. Mwili wako unakuwa unahitaji
kulala. Ufunuo 14:11 inasema, Na moshi wa maumivu yao hupanda juu
hata milele na milele, wala hawana raha
mchana wala usiku,… Hata huwezi kulala. Unaweza kufikiri ni
jinsi gani kulivyo, yaani hakuna kulala. Kuhusu maji, Zakaria 9:11, ... Nimewatoa wafungwa wako katika
shimo lile lisislo na maji. Page 11 11 Hakuna maji kabisa kuzimu. Nilitambua kuwa mahali ilipo kuzimu ni
katikati ndani ya duni. Hapo ndipo
mahali ilipo, ndani katikati ya dunia. Nilitambua hivyo nilipokuwa kama maili
3700 ndani chini ya dunia.Tunafahamu
kwamba kipenyo cha dunia ni maili 8000. Na nusu ya kipenyo hicho ni
kama Maili 4000. Nilikuwa kama maili
3700. Katika waefeso 4:9 inasema kwamba Yesu alishuka mpaka
chini pande za dunia/nchi. Hesabu 16:32 inasema, Na nchi ikafunua kinywa chake na
kuwameza,na watu wa nyumba zaona
wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote. Hapo ndipo Kuzimu ilipo sasa. Baadae
Kuzimu na mauti vitatupwa katika moto
wa Jehanamu na kutupwa katika giza kuu. Hiyo ni baada ya hukumu,
Lakini kwa sasa iko duniani. (Pepo) Nilikuwa pembezoni mwa shimo la
kuzimu na nikaona mapepo yote haya
yamejipanga katika kuta, yana ukubwa tofauti tofauti na maumbo ya kila
namna, mabaya, viumbe vibaya kiasi
unachoweza kufikiri. Walikuwa wamejikunja, wameharibika, wakubwa
na wadogo. Kulikuwa na ng"e wakubwa,
wakubwa hivi. (uefu futi5) Panya, nyoka na minyoo, kwa sababu biblia
inaongelea kuhusu minyoo yenye
inayoambaa (Isaya 14:11). Kuna kila aina ya viumbe wabaya kila eneo na
inaonekana kana kwamba imefungwa
kwa minyororo kwenye
kuta.Nikashangaa "Kwa nini vitu hivi vimefungwa kwenye
kuta". Sikuelewa, lakini kulikuwa na
andiko katika Yuda 1:6 linasema, "Na malaika wasioilinda enzi yao
wenyewe, lakini wakayaacha makao yao
yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza
kwa hukumu ya siku ile kuu;" Na hivyo ninahisi hiki ndicho nilikiona,
sijui, lakini hicho ndicho kilichonitokea.
Nilifurahi kwa sababu sikutaka wanisogelee. Walionyesha kunichukia
sana! Hiko kilikuwa kitu kingine
ambacho sikukielewa, hawakuwa tu ni viumbe, walikuwa na chuki kubwa kwa
wanadamu. Hivyo nilifurahia kuona
wamefungwa kwenye kuta. Nilianza kupaa shimo hili kwenye tanuru
hili, na kuachana na miali. Mara kukawa
na giza, lakini niliweza kuona mapepo yote haya pembeni ya tanuru
na walikuwa na nguvu kubwa sana.
Nikafikiri,"Nani anayeweza kupigana nao viumbe hawa. Hakuna anayeweza
kupigana nao viumbe hawa." Lakini
bado,Hofu ile ilikuwa ni kubwa sana, sikuweza kabisa kusimama juu ya hofu
hii. (Hakuna Matumaini) Kitu kibaya Kuzimu, kitu kibaya, kitu
kibaya kuliko mateso yote, niliweza
kutambua, kwamba kuna maisha yanaendelea hapa duniani. Na ya kuwa
watu hapa juu, watu wengi, hawana
hata habari kuwa ulimwengu huu uko hapa chini na ni halisi! Hawajui kabisa
kuwa ni ulimwengu mwingine na halisi
huko hapa chini na kuna mabilioni ya watu wanaumia na kuomba nafasi
nyingine ya pili, kama wangekuwa na
nafasi ya kutoka tu mahali pale. Lakini hawawezi kupata nafasi nyingine tena,
na wanakuwa vichaa kabisa kuona kuwa
hawawezi kuwa na fursa ya kuwa na Yesu, kwamba wameishia mahali
pale maisha yao yote. Hiki ndicho kitu
kibaya kuliko vyote, kwamba hakukuwa na matumaini ya kutoka nje.
Nilifahamu hivyo. Nilitambua umilele.
Niliweza kuelewa umilele. Hapa duniani, hatuwezi kuwazia, Hatuwezi
kuujua. lakini pale niliuelewa. Nilijua
nitakuwa huko milele na milele, wala sikuwa na matumaini ya kutoka nje.
Niliwaza kuhusu mke wangu. Sikuweza
kwenda kwa mke wangu! Nimekuwa nikimwambia kama tukitenganishwa na
kitu chochote kwa namna yeyote labda
tetemeko au kitu cha kutisha, Page 12 12 nilisema "Nitarudi. Nitakutafuta.
Nitakurudia kama tumeachanishwa."
Lakini hapa sikuweza kumrudia.
Sikuweza kumuona tena. Hakuwa hata na wazo
lolote ni wapi nilikuwa na sikuweza
kamwe kuongea naye tena milele. Hilo wazo tu lilinisumbua sana! Kutokuwa na
uwezo wa kuongea naye, kuwa naye, na
kwa yeye kutojua ambapo mimi nipo, na sikuwa na matumaini kwa milele
kutoka nje! Unakuwa unaelewa, kuwa
huwezi kutoka hapo, milele! Angalia duniani kuna matumaini siku
zote. Hata watu katika kambi za mateso
huwa na matumaini ya kutoka nje, au kufa angalau, ili waondokane na
taabu. Lakini hatujawahi kabisa kukosa
matumaini kama ilivyo kuzimu. Katika Isaya 38:18 inasema, "Wale washukao shimoni hawawezi
kuitarajia kweli yako." Hakuna matumaini, na kweli ni Yesu (Yesu akatokea) Wakati huu, nilikwenda juu ya tanuru
hili, na nikiwa na hofu kubwa, sina
matumaini nimepotea, na nikiwa naogopa mapepo haya. Kwa ghafla, kwa
ghafla tu, Yesu akajitokeza! "Usifiwe
wewe Bwana", Yesu alijitokeza. Mwanga huu mkali ulimulika mahali
pale. Mimi niliona tu umbo lake, umbo la
mwanadamu. Sikuweza kuona uso wake, mwanga ulikuwa mkali sana.
Niliangalia katika mwanga huu na kuona
umbo lake tu. Na mimi nikapiga magoti yangu nikaanguka. Sikuweza
kufanya jambo lolote tofauti na
kuabudu. Nilijisikia furaha. Sekunde
moja iliyopita nilikuwa nimepotea milele, na
sasa ghafla natoka nje ya eneo hili, kwa
sababu nilikuwa tayari nimemjua Yesu. Watu wale hawawezi kutoka nje,
lakini mimi naweza kwa sababu nilikuwa
tayari nimeokolewa. Nilijua na kuelewa kwamba kulikuwa hakuna njia a
kutoka nje ya eneo hili, ni kwa Yesu
pekee. Yeye ni njia pekee ya kukufanya usiende mahali hapa. Ufunuo 1:6 inasema Yohana, alipokwenda mbinguni, alimuona Yesu,
na sura yake ilikuwa kama jua liking'aa
kwa nguvu zake. Naye alipomuona kwake,
akaanguka mbele ya miguu yake kama
mtu aliyekufa. Hivyo ndivyo nami nilifanya. Nilianguka mbele ya miguu
yake kama mtu aliyekufa. Sasa unaweza
kufikiria nilikuwa na maswali milioni ya kumuuliza, lakini wakati uko
pale, kile unachoweza kufanya ni
kumwabudu na kumtukuza jina lake Takatifu, na kumshukuru kwa kile
alichotuokoa. Nilipotulia sasa, angalau kiasi ambacho
naweza kuanza kutengeneza mawazo,
Niliwaza kumwaambia Bwana, Hata sikumbuki kama nilimuuliza kwa sauti
kubwa, niliwaza tu na akanijibu. Mimi
nikasema, "Bwana kwa nini umenileta mahali hapa? Kwa nini
umenileta mahali hapa?" Akaniambia "Kwa sababu watu hawaamini
kwamba eneo hili ni halisi." Alisema "Hata baadhi ya watu wangu mwenyewe
hawaamini eneo hili ni halisi." Nilishitushwa kwa usemi huo. Nilidhani
kila Mkristo anaamini Kuzimu. Lakini si
kila mtu anaamini katika uhalisi wa moto wa Kuzimu. Nilisema Bwana
"kwa nini umenichukua mimi?" Lakini
hakujibu swali hilo. Mimi sijui ni kwa nini yeye alinichukua
mimi kwenda huko. Uwezekano wa mimi
kwenda mahali hapo ulikuwa ni mdogo. Mke wangu na mimi huwa
tunachukia sinema za maovu.
Tunachukia lolote baya. Sipendelei hata
maisha ya majira ya kiangazi, sana napendelea
kiasi kidogo cha joto. Ni machafu.
Hakuna mpangilio. Ni kero muda wote na machafuko na machukizo. Na mimi
upendelea kila kitu chenye utaratibu na
ubora. Hakunijibu swali hilo. Akaniambia, "Nenda ukawaambie kwamba ninachukia mahali hapa,
kwamba si mapenzi yangu kwa
yeyote mmoja wa viumbe wangu kwenda
mahali hapa, hata mmoja! Sikuumba
hili kwa ajili ya mtu. Hii ilifanyika kwa ajili ya shetani na malaika zake.
Unatakiwa kwenda na kuwaambia!
Nimekupa kinywa, wewe nenda na uwaambie. " Nikajifikiria, "Bwana, hawatakwenda
kuniamini. Watanifikiria mimi ni kichaa
au nilikuwa na ndoto mbaya." Namaanisha je wewe usinge fikiria hivi?
Kama Nilipofikiria hivi, Bwana akanijibu
akasema, "Siyo kazi yako Page 13 13 kuwashawishi. Ni kazi ya Roho
Mtakatifu! Wewe nenda na
uwaambie!" Na niliitika ndani, "Ndiyo Bwana!" Ni sahihi kabisa, nitakwenda na
kuwaambia." Hutakiwi kuwa na wasiwasi
na hofu juu ya mtu anafikiria nini juu yako, wewe unachotakiwa tu ni kwenda
na kufanya hivyo na kumuachia Mungu
afanye yaliyobakia. Amina? Nami nikasema," Bwana, kwa nini
wananichukia sana? "" Kwa nini viumbe
hawa wananichukia? "Akasema," Kwa sababu umefanywa kwa mfano
wangu na wananichukia mimi.
"Unajua shetani hawezi kufanya kitu chochote dhidi ya Mungu. Hawezi kumdhuru
Mungu, kwa kusema, lakini anaweza
kuumiza viumbe vyake. Ndiyo maana shetani anachukia watu, na
anawadanganya na kuwapeleka kuzimu.
Naye anaweka magonjwa juu yao, kitu chochote anaweza kufanya ili mradi
auumize viumbe wa Mungu. (Amani ya Mungu) Na kisha Mungu akanijaza Mawazo
yake. Aliniruhusu niguse kiasi cha moyo
wake, ni kiasi gani anampenda mwanadamu. Ajabu, sikuweza hata
kulichukulia hili. Ilikuwa ni zaidi hakuna
mfano wake. Upendo alionao kwa mtu, huwezi ukauchukulia katika mwili
huu. Unajua ni kiasi gani tunawapenda
wake zetu na watoto wetu? Naam upendo tulionao hatuwezi hata
kuulinganisha na upendo wa Mungu
kwetu sisi. Upendo wake ni mkubwa
zaidi kuliko upendo wetu na uwezo wetu wa
kupenda. Ni sawa tu kama inavyosemwa
katika Waefeso 3:19, "... ili kujua upendo wa Kristo ambao hupita maarifa
..." Inakwenda mbali kupita maarifa, huwezi hata ukapata ufahamu wake. Sikuamini kuona ni kiasi gani alimpenda
mwanadamu, kwamba anakufa kwa ajili
ya mtu mmoja tu ili asiende mahali hapo. Na anakuwa na uchungu
mwingi kuona mmoja wa viumbe vyake
anakwenda mahali hapo. Inamuumiza Bwana, Analia kuona mtu
mmoja anakwenda. Na nilijihisi vibaya
kwa Bwana. Nilihisi moyo wake, basi akaniacha
niguse kidogo moyo wake. Alijisikia
huzuni kwa viumbe wake kwenda mahali pale. Nikawaza "Imenipasa kutoka nje
na kushuhudia na kuchukua kila pumzi
ya mwisho kuwaambia dunia habari za Yesu, Jinsi alivyo mzuri." Naama ka
kuwa, tuna injili. Ni habari njema. Ni
habari njema, na dunia haijui. Imewapasa kuambiwa! Unajua, inabidi
tushiriki maarifa haya. Watu wanakosa
elimu katika eneo hili. Mungu anataka sisi tushiriki pamoja nao jinsi
yeye alivyo mzuri, na jinsi Yeye
anachukia mahali hapo. Akaniambia pia, "Waambie ninakuja hivi karibuni, karibu sana." Akasema tena, "Waambie ninakuja hivi karibuni, karibuni sana." Sasa nafkiri, kwa nini sikumwambia, "Ni nini
umaaanisha Bwana?'hivi karibuni' ikoje kwako?" Hivyo ndivyo jinsi tunafikiri.
Lakini sikuweza kuuliza vitu hivyo wakati
huo. Unataka tu uendelee kumwabudu sana. Amani ya Mungu
inayokuja juu yako kuwa karibu naye
haielezeki. Nimekuwa katika huduma za upako, lakini hakuna cha
kulinganisha na upendo na amani ya
Mungu unayojisikia kuwa karibu naye. Na kisha nikatazama juu na nikaona
mapepo hayo juu ya ukuta, walionekana
wakiwa na uso wa ukali, walikuwa wanaonekana kama mchwa kwenye
ukuta! Walionekana kama mchwa! Bado
walikuwa ni wakubwa, lakini kwa uwezo wa Mungu uliokaribu nawe,
nguvu zote za uumbaji wa Mungu,
walikuwa wanaonekana kama mchwa kwenye ukuta. Sikuweza kwenda juu
yake. Nikafikiri, "Bwana ni kama mchwa
tu hawa!" Naye akasema, "Wewe unachotakiwa tu ni kuwafunga na
kuwatoa nje kwa jina langu." Nikafikiri "Kijana, nguvu alizotoa kwa
kanisa." Hivi vitu ambayo vilikuwa na ukali,
tusingeweza kushindana navyo bila
Yesu, hakuna. Wanahasira, lakini unapokuwa pamoja naye, ni bure tu !
Ujasiri ukaja ndani yangu, nilipoona
viumbe hawa nilihisi kama niseme, "Nyie viumbe mliokuwa mnanitesa,
mkataka kunigawana? Haya njooni!
Haya njooni sasa!" Labda inawezekana nafsi yangu ilijiinua au kitu kingine,
unajua, Niliwaza, "Yesu wafate." (Kuondoka Kuzimu) Tulipoondoka, tukapanda juu ya uso wa
dunia. Tulikwenda juu, kwa sababu
tulikuwa bado katika shimo. Punde sikuweza kuiona tena, lakini ilikuwa ni
kama upepo wa kisulisuli, kimbunga
kikubwa nasi tuko ndani yake. Ilibidi Page 14 14 kuendelea kwenda juu, ili tutoke nje
yake ilivyoonekana. Tulipofika juu yake,
nikaangalia chini duniani na tulikuwa juu namna hii. Mviringo wa
dunia ulionekana kama hapo. Nifuraha
kuangalia tena katika nchi! Najua Mungu aliruhusu hilo kwa ajili yangu.
Tungeweza kuondoka kwenye handaki
kwa namna yoyote ambayo Angetaka. Alijua ndani ya moyo wangu,
kwamba nilipokuwa mtoto siku zote
nilitamani kuona dunia inaonekana vipi kutokea angani. Labda ni
kwasababu niliangalia sana, Safari ya
nyota au kitu, unajua? Nilijiwadhia
itakuwa vizuri kweli kuona dunia, na kuona
ikielea angani bila kushikiliwa na
chochote. Kama Biblia inavyosema.
Inasema katika Ayubu 26: 7, Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi
isiyo na kitu, Yeye lipo duniani juu ya
chochote. Kama ukiangalia, unafikiri, "Ni nini
kinashikilia hii dunia juu? Nini kinafanya
izunguke kwa ukamilifu?" Mungu anadhibiti hilo. Uwezo wa Mungu
ulionifunika, ulikuwa ni wa kutisha. Ana
uwezo sana. Kila kitu kimoja kimoja viko chini ya udhibiti wake. Si tu nywele
juu ya kichwa chako zishukazo mpaka
chini kwamba hawezi kuzijua kwa idadi. Sio tu ndege aliyeanguka sakafuni
kwamba hawezi kujua. Nilikuwa
nimejazwa na mawazo haya. Mungu ana nguvu sana. Ilinishangaza sana. Kuna
maandiko katika Isaya 40:22 yanayosema Bwana anaketi katika
muhimili wa nchi/dunia. Pale nilikuwa juu ya
mhimili wa dunia. Hata nikawaza pia,
"Bwana, kwa nini kabla ya Christopher Columbus wasingesoma maandiko na
kujua kuwa nchi/dunia ilikuwa ni
mviringo." Unajua? Watu walishangaa, walidhani ilikuwa ni tambarare? Hata hivyo, tuliporudi chini tulipita
katikati ya ngao; Nilijua tulikuwa tukipita
katikati ya ngao za joto lililokuwa lililozunguka duniani. Nilijua tu hivyo.
Hata niliwaza mawazo ya kijinga, hapa
niko na Mungu, na "sijui atakwendaje kupita katikati ya ngao ile
ya moto?" Unajua jinsi ambavyo angani
wanavyotakiwa kupenya ngao hiyo kwa pembe/makadirio sahihi.
Tulikwenda kwa njia hiyo na hakuna
tatizo lolote gani lillilotokea. Hakuna cha kushangaa! Nina hakika Bwana
alitazama kwa macho yake na kusema
ninaweza tu kupita, Kuna maandiko Zaburi 47: 9 inasema kwamba, ... Kwa ngao za dunia ni zake Mungu ... Mungu yuko katika udhibiti wa kila kitu,
kila kitu. Sikutaka aondoke. Nilitaka
kuwa katika uwepo wake. Tulikuwa tunashuka kutokea juu kwa kasi
California. Tulikuwa tunashuka kwa
haraka, haraka sana, tukaingia mpaka nyumbani kwetu. Na niliangalia
nikaweza kuona kutokea kwenye paa la
nyumba yetu. Na niliweza kujiona mwenyewe nimelala juu ya sakafu. Hili
kweli lilinishangaza sana, kwa sababu
niliona mwili wangu umelala hapo, nikawaza, "Huyo hawezi kuwa mimi,
mimi niko hapa, huyu ni mimi!" Unajua,
wewe hujawahi kuona wawili ambao ni wewe mwenyewe. Hapa nilikuwa
nimelala pale nikawaza, "Huyo si mimi
halisi." Na kwamba andiko Paulo analolisemea, kwamba tuko ndani ya
hema (2 Wakorintho 5:1), likanijia kwa
nguvu. Nikawaza "hiyo ni hema, si kitu. Huyo ni wa muda. Huyu ni mimi
halisi." Hiyo ndiyo umilele inavyokuwa.
Kwamba haya ndiyo maisha tunayojisumbua nayo, nikakumbuka pia
sisi ni mvuke, maisha haya ni kama
mvuke kama katika Yakobo 4:14 inazungumzia juu ya ufupi wa maisha
haya. Ni muda mfupi. Miaka mia moja
kama ukiwa hai, si kitu! inapotea kama mvuke. Na nikawaza, "Imetupasa
kuishi kwa ajili ya Mungu."
Tunachofanya sasa, hapa, kinaandaa
umilele. Imetupasa kushuhudia. Imetupasa
kutoka nje na kuokoa waliopotea.
Hatuwezi kuwa tunajisumbua na vitu
hivi vidogo kila siku vimetufunga na
tunahangaika navyo. Tunahitaji kweli
kutoka nje na kuhubiri injili na habari njema, kwa sababu hii ni zaidi ya haraka
sana. Nikaona mwili wangu umelala hapo na
nilifikiri ilikuwa tu kama vile umetoka nje
ya gari yako na ukangalia nyuma tena kwenye gari yako. Huyo si
wewe, ni gari yako. Ni vile imekuzunguka
tu. Hivyo ndivyo jinsi ilionekana kwangu. mwili huo
umenizunguka tu hapa duniani, lakini
huyu ndiye mimi halisi. Na nikafikiri, Page 15 15 "Bwana usiondoke, usiondoke". Nataka
kuendelea kuwa na wewe kwa muda.
Lakini aliondoka. Nikaurudia mwili wangu, na kitu kikanivuta kwenye mwili
wangu, kama vile nimerudishwa kwenye
pua yangu au kinywa changu. Wakati huo, alipoondoka, hofu yote,
mateso, na adhabu zote zilinirudia
kwenye mawazo yangu! Kwa sababu inasemwa katika Biblia (1 Yohana 4:18), "Upendo wa kweli hufukuza mbali hofu." Hivyo nilikuwa karibu na upendo kamili muda wote huo, sasa
akaniacha, na alipoondoka, kwa ghafla
hofu yote na machungu ya kuzimu yaliingia mawazoni mwangu. Sikuweza
kuvumilia, sikuweza kuvumilia! Nikapiga
mayowe. Nilikuwa katika maumivu/uchungu makali/mkali.
Sikuweza kuishi nayo. Nilijua kuwa mwili
huu haukuwa na uwezo wa kujisimamia kwa aina hiyo ya hofu.
Huwezi ukajizuia juu ya shinikizo hiyo.
Mwili wako hauna nguvu za kutosha kujizuia. Hivyo wakati huo sasa niliomba
na niliweza wa kuomba, "Ondoa katika
akili yangu!" Kwa asili, ni lazima upitie kila aina ya
ushauri nasaha ili kutoka nje ya aina hii
ya kiwewe, lakini Mungu aliondoa hili nje, papo hapo aliondoa kiwewe,
majeraha. Aliniachia kumbukumbu,
lakini aliniondolea kiwewe na hofu. Nilimshukuru. Hata hivyo, baada ya hayo, mambo
mengi yaliyotokea, Ningependa
tungekuwa na muda wa kugusia yote
ambayo Mungu alithibitisha yangetokea kwangu. Kama kuna mtu hapa usiku wa leo,
ambaye hamjui Bwana; unatakiwa
ujiulize swali. Unatakiwa kusema, "Je, nawaamini watu hawa, kile walichokiona
ni halisi, watu wote hawa na mimi
mwenyewe?" Lakini cha muhimu zaidi, nini Neno la Mungu linasema
kuhusu Kuzimu. Je, unataka kuchukua
nafasi hiyo na kusema, "Hapana mimi siamini hii kama ni kweli,. "Basi tupa
Neno la Mungu lote, na sisi sote
tunaojaribu kukuambia. Je, uko tayari kuchukua nafasi hiyo milele yako yote?
hiyo naona ni ujinga kwangu. Huwezi
ukamruhusu shetani akudanganye. kile kiumbe kikubwa pale mwishoni
kikicheka. (inavyoonekana katika video) hivyo ndivyo jinsi shetani atakuwa ukifika kuzimu. Atakucheka, kwa sababu
ulikuwa na nafasi ya kupokea Bwana na
umeikosa. Lakini utakapokuwa pale, hakuna kurudi nyuma. hakuna
kabisa kurudi nyuma. Utakuwa huko
pale umepotea milele. Unaweza kuwa unajisemea wewe
mwenyewe. "Mimi mzuri. Mimi ni mtu
mzuri sana. Sistahili mahali pale." Na pengine ni mzuri, ukilinganishwa na
watu wengi. Lakini sivyo ambavyo
unahitaji kujilinganisha mwenyewe. Tunahitaji kujilinganisha wenyewe na
kiwango cha Mungu. Kiwango cha chake
kiko juu sana kuliko chetu. Anasema katika Neno kwamba kama
ukisema uongo mara moja, mara moja
tu katika maisha yako yote, inakufanya mwongo. Kama ukiiba kitu
kimoja tu katika maisha yako, kwa
mfano kibanio cha karatasi, dakika kadhaa za bosi wako, au kitu chochote,
mara moja tu. Inakufanya uwe mwizi.
Kama ukiwa na hasira bila sababu, kama haukumsamehe mtu aliyekufanyia
kitu kibaya juu yako, kama ukimtamani
mwanamke, chochote ya mambo hayo mojawapo, kama wewe ulifanya
hayo mara moja tu, Hii inakufanya uwe
mwenye dhambi, na hivyo hauwezi kuingia mbinguni. Hivyo unaweza kuona
kila mmoja wetu amepungukiwa. Sote
tumepungukiwa na hatuwezi kufika pale kwa matendo yetu wenyewe. Tito 3:5 inasema, Wala si kwa matendo ya haki ambayo
tumefanya, bali kwa rehema yake
alituokoa ... Amina, inategemea na jinsi
unavyolinganisha. Ni kama mwanamke
ambaye ameona kundi la kondoo katika mlima, na wote walikuwa weupe sana na
wazuri upande wa mlima. Akasema,
"Angalia hao kondoo weupe, angalia jinsi walivyowazuri, weupe."
Kisha alikwenda kitandani na ghafla
usiku barafu ikaanguka. Alitazama asubuhi yake na kuona kondoo wote
wakiwa katika hali ya kufa, wachafu na
wakijivu kulinganisha na barafu Page 16 16 nyeupe. Hivyo tunapaswa kujilinganisha
sisi wenyewe na Mungu. Viwango vyake
viko juu zaidi ya vyetu. Hivyo tunamuhitaji Mkombozi. Hatuwezi kufika
pale sisi wenyewe. Mungu alifanya hii
kuwa zawadi ya bure. Alisema katika Yohana 14:6, "mimi ni njia, kweli na uzima. hakuna awezaye kuja kwa
baba , isipokuwa kupitia mimi." Yeye ni njia pekee ya kutoka hapo. Kwa hivyo kama kuna yeyote Yule
asiyemjua Bwana, yeyote Yule mahali
hapa ambaye hakuwahi kumsihi Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha
yake. Haukuwahi kufikia maamuzi haya
ambapo inakubidi upaze sauti yako kwa mdomo wako na kumsihi aje
maishani mwako, Unaweza kusimama?
Kama kuna yeyote mahali hapa
unaweza ukasimama, Kwa ajili ya Yesu?
Usimruhusu shetani, kile kiumbe
kikucheke. Simama hivi sasa, ukiwa
bado unanafasi, kwa sababu haujui ni muda
gani tulionao. Haujui labda kesho
unaweza kuaga dunia, na kuishia mahali pale. Ngoja nikueleze, mahali pale, moto tu
wenyewe ni ngumu kuweza kuvumilia.
wale watu tuliowaona wakiruka kutokea katika minara wa new York.
Wanashikana mikono yao na kuruka.
Inatisha kiasi gani. Unajua kama umewahi kuwa juu na ukaangalia chini,
kuruka ni kitu kisichofikirika. Lakini kule
ni lazima ukabiliane na moto. Na hiyi ni kwa muda wa sekunde
tano,unakuwa umeungua tayari, na
moto wa pale ni kama digrii elfu mbili. Wanasayansi wanasema katikati ya
dunia ni kama digrii kumi nna mbili elfu.
Kwa hiyo inakupaswa kuvimilia moto ule kwa umilele. Kama uko tayari
kupitia hayo, huo utakuwa ni ujinga
sana. Sasa ni wakati muafaka…. (mtangazaji anaongea) Biblilia iko wazi sana, isi wote ni wenye
dhambi,na yeyote atakayeliita jina la
Bwana ataokolewa. Yesus anasema kama ukinikiri mimi mbele za watu , naye
mbele zao atakiri jina lako mbele ya
baba yake na malaika watakatifu. na kama ukinikataa mimi mbele ya watu,
nitakukana mbele ya baba yangu.
Nataka nikuambia jambo la kufanya kama haujawahi mbele za watu kumkiri
Yesu Kristo kuwa ni Bwana na mwokozi
wa maisha yako,au kama hauna uhakika kuwa mbinguni ni mahali ppako
pa milele, kumbuka Yesu alisulubiwa
uchi msalabani, sokoni,alisulubiwa pale kwa ajili yako, Alivumilia aibu yako. Kama ukiomba ombi hili kutokea moyoni,
Mungu ataokoa nafsi yako, na atakupa
nafasi kwa wakati ujao kulithibitisha hili mbele za watu. Omba
nasi, hasa wale walio kwenye
kongamano hili na wanajua imewapasa
hivi. "Mungu naamini katika wewe. Wewe
ni muumbaji wangu. mimi ni mwenye
dhambi. Nimetenda dhambi katika maeneo mengi, kwa kukusudia, na
kwakutokusudia. Nimepungukiwa na
utukufu wako.Nimekosa chapa yako Ninanuka uovu. Yesu naamini katika
wewe. Wewe ni mtoto pekee wa
Mungu. wewe ni kondoo wa Mungu, uichukuae dhambi ya ulimwengu,
uliyechukua dhambi zangu. Naamini
ulukufa msalabani.Ukamwaga damu yako isiyo na hatia kwa ajili ya nafsi
yangu. Naamini ulizikwa na siku ya
tatu ulifufuka. Uko hai millele na milele. Nitakuita wewe Bwana.
Nakuita wewe mwokozi wangu.
Nakupa wewe maisha yangu.
Nitakupenda, nitakutumikia siku zote za maisha
yangu. Nitakuwa wako, chema,
kibaya, uovu, mipango, ndoto zangu
nakupa kila kitu. Mapenzi yako yafanyike
kwangu. Naamini nimeokolewa. Si
kwa matendo mema, lakini kwa
imani, kwa kukuamini. Kwa jina la Yesu
ninaomba. Amen." >>>>> MUITO MKUU KABISA<<<<< Jibu hilo ni sahihi kabisa. Biblia inasema
mbingu inazizima kwa furaha kwa
mwenye dhambi mmoja anayetubu. Na sisi tunajua mfano wa yale
yanayoendelea mbinguni wakati mbingu
inaposhuhudia nini umefanya leo.
Nataka niwatangazie baadhi yenu, kisha
nitahairisha mazungumzo haya. Nataka
kutoa wito wa mabadiliko kwa wale baadhi yetu walioshuhudia haya. Tuna
neema ya kipekee kusikia yale ambayo
kaka yetu Bill aliyapitia. Nakwenda Page 17 17 kutoa changamoto kwako na
Ninakuonya, usikubali hili isipokuwa uwe
tayari kwa ajili ya maisha ya Roho maishani mwako. Sijaribu kukutania,
nasema tu usifanye hili kuwa ni ukiri
wako labda uwe umeamua kweli kweli. hivi ndivyo ilivyo. Kuna sehemu mbili.
Moja, sitaendelea tena kuogopa uso wa
mwanadamu. Kizuizi kimojawapo kikubwa kwetu sisi ni kutofanya kama
vile unajua kuwa kuna Mbingu na kuna
Kuzimu. Sitaendelea kuogopa uso wa mwanadamu. Mbili, Nitaongea na
kila mmoja ninayemjua, Kuhusu Yesu,
mbinguni na kuzimu, kwa maisha yangu yote. Hiyo ni dhamira/ahadi
kubwa. Kila mtu ninayemjua mimi
ambaye anahubiri/anawafikia watu kwa
ajili ya Kristo anakuwa amefanya maamuzi
haya. Kwa nini sasa ufanye uhusiano na
mtu yeyote tu, kama si huu wa kushiriki pamoja nao habari njema
yenye utukufu iokoayo roho zao na moto
wa Kuzimu. Ni kosa katika Roho kumjua mtu, kuzungumza nao, na
kufurahi pamoja nao, kufurahia uwepo
wao, na kamwe huwaambii kuhusu hili, ya kuwa bila Kristo, watakwenda kuzimu.
Kila uhusiano unapaswa kuwa ni mlango
wa kuwasiliana kuhusu kweli ambayo umeshuhudia leo. Hiyo inaleta
mantiki. Kama wewe hauko tayari
kufanya hivyo, nitakuelewa. Lakini kama uko tayari kufanya maazimio hayo
mawili, kama unakubaliana, sema haya
kwa Mungu, "Mungu nakumini

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni