Wafilipi 2:10-11
  • JIANDAE KUKUTANA NA MUNGU WAKO! FALME ZA MBINGUNI NA KUZIMU,NA KURUDI KWA KRISTO NA Angelica Zambrano USHUHUDA WA TATU

    Huu ni ufunuo wa 3 wa Mbinguni na
    Kuzimu ambao Bwana alimpa
    Angelica Zambrano. Alionyeshwa
    uzuri wa Mbinguni na pia watu wengi
    ambao wamelizia maisha yao katika
    mateso ya milele ya Kuzimu kwa sababu ya dhambi mbalimbali.
    Alipewa maonyo muhimu kwa habari
    ya kanisa na aliambiwa kuwa
    asilimia chache tu ya Wakristo wako
    tayari kwa ajili ya KURUDI KWA
    BWANA. Mwinjilisti Angelica Zambrano anaishi
    Ecuador Amerika ya Kusini. Ilikuwa
    yapata saa 6:30 usiku wakati
    uzoefu wa karibu na kufa na ufunuo wa
    mbinguni na kuzimu ulipoanza (angalia
    video yote mwishoni mwa makala hii kwa maelezo zaidi).
    Watumishi na ndugu wote walikuwepo
    katika maombi wakati wa uzoefu huu.
    Jambo la kwanza ambalo lilitokea ni
    kwamba malaika alimchukua kutoka
    nyumbani kwake na kumtazamisha katika muonekano wa kimbingu. HALI YA KANISA – NI WACHACHE
    TU WAKO TAYARI Katika muonekano wa kutokea mbinguni
    malaika alisema " Angalia unaona dunia.
    Angalia katika makanisa
    yote na makusanyiko ya dunia. Kanisa
    hili lina waumini 20,000. Kuna jingine
    lina waumini 10,000. Kanisa hili jingine lina waumini 1000. "Aliendelea
    kunionyesha makusanyiko mengine
    mengi na kisha alisema" Lakini
    kuna watu wachache sana katika
    makanisa haya ambao ni Kanisa la kweli
    . " Malaika alisema, "Ni lazima mimi
    niwaambie kile Baba anataka mimi
    nikuambie ". Malaika Mkuu Michael
    ndiye aliyekuwa akizungumza na mimi.
    Alisema, " Angalia katika dunia.
    Makanisa yamejazwa na dhambi, kuna dhambi nyingi sana katika
    makanisa haya. Wengi wa watu hawa
    wamekufa kiroho " . Kupitia malaika, Bwana alinionyesha
    kwamba 80% ya Kanisa la Kiinjili la
    Kikristo duniani (Evangelical
    Christian Church) wataachwa nyuma .
    Wataachwa nyuma kwa sababu wao ni
    baridi . Kwa sababu hawatafuti uwepo wa Mungu. Kwa sababu ya
    dhambi zao. Kwa sababu wamekata
    tamaa. Ni 20% tu watanyakuliwa (
    kunyakuliwa ) kuwa pamoja na Yesu , hii
    ni kwa Wakristo wa kweli pekee. Hii ni
    kwa sababu neno lake linasema ` Wengi wamealikwa, lakini wachache wameteuliwa'(Mathayo
    22:14). Sisi wote tumeitwa/tumealikwa lakini sio tu
    kualikwa pekee, ni lazima kuchaguliwa/
    kuteuliwa. Napenda kueleza kile kinachofanyika
    ndani ya makanisa mengi. Kuna udini
    mwingi sana. Hakuna uaminifu katika neno la Mungu. Ndani ya kanisa,
    kaka na dada wanamsifu Bwana kwa
    furaha. Wanafurahia, wanacheza na kunena kwa lugha. Lakini mara
    wanaporudi tu nyumbani wanakuwa
    tofauti kabisa. Wanatenda kama shetani Page 2 mwenyewe. Hiki ndicho kinafanyika.
    Watu wanakwenda nyumbani na
    kuongea mambo ambayo huumiza moyo wa Mungu. Nyumbani hawaombi ,wala
    kusoma neno la Mungu au kutafuta
    uwepo wake. Mungu hapendi mtu yeyote kati yetu aachwe nyuma.
    Inaniumiza kwamba 80% ya waumini wa
    makanisa hawako tayari kwa ajili ya kurudi kwa Bwana . Kwa sababu
    makanisa machache tu ndiyo huonyesha
    upendo wa kweli wa Yesu. Kulikuwa na malaika pande zote, kisha
    Yesu akasema nami, wakati malaika
    wamekaa kimya. Bwana akaniambia "Binti moyo wangu unaumia kuona jinsi watu wengi
    wamekata tamaa. Kuona jinsi watu
    wengi walivyorudi nyuma. Waambie watu
    wangu warudi katika njia zao za
    zamani, ule upendo wa kwanza " Kanisa, ni lazima kuwatia moyo waumini.
    Kuwaambia wamtafute Mungu, wakatae
    unafiki. Sikiliza kile ambacho Bwana aliniambia. Bwana
    akaniambia "Je, unajua amri ipi kanisa langu wamesahau? Wengine wanadhani ni Upendo. Wengine
    wanafikiri ni imani. Amri
    iliyosahauliwa ndani ya kanisa langu
    ni Utakatifu. Neno langu kusema '
    Kuweni watakatifu , kwa kuwa mimi
    ni mtakatifu."(1Pet1:16). Hiki ndicho, Bwana alisema, Imetupasa kuwa
    watakatifu ndani na nje. Ni Lazima tuwe
    na moyo safi, moyo safi ambao umejazwa na uwepo wake. Moyo
    uliojazwa upendo wake. Moyo uliojazwa
    Mungu. Ufu 3: 15-16 Nayajua matendo yako, ya
    kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa
    heri kama ungekuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa sababu una
    uvuguvugu, wala hu baridi wala moto,
    nitakutapika utoke katika kinywa changu…
    .19 Wote niwapendao mimi nawakemea,
    na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. UFALME WA MBINGUNI Kisha malaika akaniuliza "Je, uko tayari?
    Bwana ametutuma kwa kusudi hili". Mimi nikajibu" Ndiyo,
    niko tayari" kwa kuwa Bwana alikuwa ameniondolea
    mbali hofu zangu zote. Tukio hilo lilikuwa ni tofauti na matukio
    mengine mawili yaliyotangulia. Wakati huu sikwenda
    mbinguni kwa namna ile kama mwanzo. Wakati huu ghafla
    naliingia katika Ufalme wa mbinguni. Nilipotazama nilitambua
    nilikuwa nimevaa vazi zuri jeupe. Tukaanza kutembea na malaika
    walikuwa wakimuabudu Bwana na kusema "Angalia kote kwani
    tuna mambo mengi ya kukuonyesha". Nami nikaanza kuona
    sehemu zile nilikuwa nikiziona katika
    uzoefu wangu wa kwanza kama vile maua na bustani nzuri. WATOTO MBINGUNI Tulipopita bustanini tukafikia mahali
    fulani ambapo palijazwa watoto wengi.
    Watoto hawa walikuwa na umri wa miaka kati ya 2-3. Walicheza,
    walifanya michezo na kuimba. Malaika
    walisema." Angalia, walio kama hawa Ufalme wa Mbinguni ni wao.
    Kumbuka, ni kwa wale tu ambao
    wanafungua mioyo yao. Wengi wa
    watoto hawa waliuawa. Wengi walitolewa
    kwenye mimba zao. Mama zao
    walikatisha maisha yao."Watoto walimuabudu Bwana na kucheza
    kwenye kile kilichoonekana kwangu
    kuwa ni bembea. Nilipowasogelea walisogea karibu sana kwangu. Malaika
    Mkuu Michael akaniambia "Leo Bwana
    anakupa upendo mkubwa kwa watoto". Hapo awali niluwapenda
    watoto lakini wakati mwingine nilichukia
    tabia zao, kulia, kunung'unika au kuzungumza sana. Niliwapenda wakae
    tu kimya. Michael akasema " Mungu
    anakupa upendo mpya kwa ajili ya Page 3 watoto. Utakaporudi duniani, utakuwa
    kama asali kwao. Watakutafuta na
    utakuwa baraka kwao. Unajua kwa nini Mungu ameweka upendo huu katika
    moyo wako kwa ajili ya watoto ? Mungu
    anataka wewe uvune roho zao. Kuna watoto wengi katika
    Jahannamu. Lazima huzungumze na
    wazazi wao ili wajue. " Watoto wengi katika kizazi hiki ni waasi.
    Hawawatii wazazi wao. Siku hizi, watoto
    hudanganywa na Shetani kwa njia ya televisheni. Vipindi vingi
    wanavyojenga havijengi kwa njia
    yeyote. Wazazi hawatambui hilo, lakini kuna watoto wengi wanaangalia picha
    za ngono. Katuni zinazokuja kwa njia ya
    TV hazitoi elimu, zimejaa uovu. Watoto husukumwa na
    maonyesho hayo na wao huwa waasi.
    Wanaendelea daima kutowatii wazazi
    wao. Kwa sababu hii watoto hawa huishia
    Kuzimu. (Angalia Angelica ushuhuda wa
    2 kwa maelezo zaidi). Waefeso 6:1 "Watoto, watiini wazazi
    wenu katika Bwana, kwa maana kufanya
    hivyo ni vizuri. "Waheshimu baba yako na mama yako," hii ndio amri
    ya kwanza yenye ahadi, 3 "upate baraka
    na uishi siku nyingi duniani." Mbinguni, watoto walikuwa wakiomba,
    wakicheka na kumuabudu Bwana.
    Nilikuwa na furaha kubwa kuona furaha yao. Malaika aliniambia kuwa
    wengi wao walikuwa wametolewa, ni
    kweli iliumiza moyo wangu sana. Na unajua nini maana ya huzuni?
    Wanawake wengi wamekuwa wakitoa
    mimba. Vijana na wazee, walioolewa na ambao bado. Wanawake hawa
    hawakuwa wanataka watoto hawa.
    Wakati mwingine baba zao waliwasindikiza pamoja nao kliniki.
    Watoto wale wanakwenda mbele ya
    Mungu. Lakini wanaume na wanawake wa duniani wanahesabiwa
    kuwa wauaji. Neno la Mungu linasema
    kwamba hakuna muuaji yeyote yule atakayeingia katika ufalme wa
    mbinguni (Gal 5:19-21, Rev 21,8). Kama
    umefanya hivi Tubu hivi leo. Kama hutaki kutubu na kuomba Mungu
    kwa ajili ya msamaha hiki ndicho
    kitafanyika siku yako ya hukumu. Watoto wako watakuja kama ushahidi
    juu yenu na kusema "Wewe ulikuwa
    mama yangu, ulikuwa baba yangu, na alichukua uhai wangu".
    wanakupendeni, wamewasamehe, lakini
    kama hutaki kutubu dhambi hii,
    utakwenda kuzimu milele. Ndani ya makanisa
    dhambi hii imekuwa ikifanyika. KUINGIA KUZIMU Kisha tukarudi mahali pale Yesu
    alikuwa, nilikuwa ni mwenye furaha. Nilipomkaribia Bwana alinichukua
    mkononi. Mara alipogusa mkono wangu nilijisikia kama mtoto mchanga
    aliyeguswa na Baba mwenye upendo. Yesu aliponishika mkono
    wangu tulianza kushuka kuelekea mahali pa giza sana. Niliweza kuona
    kulikuwa na miali mikubwa ya moto. Yesu aliniambia "Tunakwenda kwenye moyo wa kuzimu". "Moyo wa kuzimu? Kuzimu ina moyo?
    "Mimi nilimuuliza. Alijibu "Ndiyo binti yangu, Kuzimu ina moyo,
    mimi nitakuonyesha nini kilichopo ndani yake. Kuna
    wachungaji wengi, wainjilisti,
    manabii na mitume katika sehemu hii. Watu
    hawa mara ya kwanza walinitumikia lakini sasa wako katika
    eneo hili ". Nilianza kulia na kusema "Hapana zaidi Bwana, sitaki
    kuona hili tena". Nilihisi nilishuhudia vya kutosha. Lakini
    tuliendelea kushuka kupitia njia iliyokuwa kama giza mpaka kwente
    nguzo zilizokuwa kama mlango. Mlango ukafunguka nasi tuliingia. Page 4 MCHUNGAJI ALIYEASI Tulipoingia nikasikia sauti ya mtu
    imesikika akilia "Baba Baba, nitoe
    mahali hapa. Siwezi kuvumilia tena ". Nilimuuliza Bwana "Ni nani huyo? Ni
    lazima atakuwa anakufahamu alipokuwa
    duniani kwa sababu umesema utanionyesha watu ambao waliwahi
    kukutumikia wewe. Sielewi kwa nini
    amesema wewe kama `Baba`, wakati yeye yuko Kuzimu? "Bwana akasema" Alikuwa Mchungaji "Mtu huyu akasimama pale akijifanya ameshika Biblia. Yule mtu katika kuzimu
    aliendelea kuhubiri `Tubu,tubuni ndugu,
    Kanisa la Kristo, ni lazima mtubu. Niliuliza "Kwa nini anahubiri mahali hapa
    BWANA". BWANA akaniambia "Kile watu walifanya duniani huendelea kukifanya katika eneo hili" (Gal 6:7-8). Nami nikaanza kulia na
    nikauliza "Kama alikuwa mchungaji kwa nini yuko mahali hapa?"
    Yesu alisema "Binti, ni kutokana na hivi". Nilionyeshwa maisha yake akiwa
    duniani kwenye screen iliyojitokeza
    mbele yangu. "Duniani alikuwa mwenye upendeleo kwa watu.
    Alionyesha upendeleo kwa watu wa
    madaraja mbalimbali katika mahali pangu patakatifu. Kuonyesha
    upendeleo ni dhambi. Alihubiri mara
    nyingi kutoka kwenye mimbari huku akionyesha upendeleo. Alionyesha
    upendeleo kwa watu wenye mali,
    kwa watu ambao walikuwa daraja la juu. Wale watu walikuwa na fedha,
    lakini hawakuwa na hofu ya neno
    langu. Alionyesha upendeleo kwa watu wale ambao hawakuwa na hofu
    ya Mungu; katika nyoyo zao. "Nikalia kwa Bwana" Bwana sikujua kuonyesha upendeleo ni dhambi.
    "Alisema" Ndiyo binti, watu wengi walitaka kunitumikia na kuwa na sehemu ya kanisa lake hilo, lakini
    hakuwaruhusu kushiriki. Mchungaji
    huyu kamwe hakutubu ili atoke kwenye upendeleo. Kwa sababu ya
    dhambi hii, watu wengi hawakuja
    kwake. Hii ni sababu yeye yuko
    katika eneo hili. Hata kuzimu anahubiri neno
    langu kwa upendeleo "(Gal 6,7-8). Yakobo2:8 8 Kama kweli mnatimiza ile
    sheria ya kifalme iliyomo katika
    Maandiko, "Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe," mnafanya
    vema. 9 Lakini kama mnafanya ubaguzi,
    mna tenda dhambi na sheria inawahukumu kuwa ninyi ni wakosaji. 10
    Kwa maana mtu ye yote anayetimiza
    sheria yote isipokuwa akashindwa kutimiza sehemu moja tu,
    amekuwa na hatia ya kuvunja sheria
    yote. (tafadhali soma yakobo sura yote ya 2 ambayo inahusika na dhambi
    ya upendeleo- kuonyesha upendeleo au
    ubaguzi ). Kule Kuzimu, mtu huyu aliifuata nafsi na
    kusema "Chukua hii, Nashiriki Biblia
    yangu pamoja na wewe, hubiri" . Alimwangalia Yesu na alisema, "Baba ,
    siwezi kuvumilia kuwa mahali hapa tena.
    Sitaki kutenda dhambi tena. Nipe nafasi nyingine tena "Bwana
    alijibu" ! hakuna fursa nyingine zaidi kwa ajili yako. Umechelewa sana. " Bwana aliposema hayo, mchungaji
    akaanza kulaani na kukufuru. Nikasema
    " Bwana, sitaki kuona mambo haya tena , tunaweza kuondoka?" Akanijibu
    "Hapana". Kuna waumini kila mahali
    ambao wanafanya upendeleo. Ingawa inaonekana haina maana sana,
    ni dhambi kubwa. Bwana aliniambia
    kuwaambia watu "Usipendelee watu ni dhambi" MZIGO WA BWANA Katika uzoefu Sijawahi kuona uso wa
    Bwana. Napenda daima kuangalia
    mavazi yake au mikono yake, lakini kamwe siwezikuona uso wake. Kila
    wakati nikijaribu kuuona uso wake
    najihisi kama nitakuwa kipofu. Mara nyingi naona machozi yakitoka chini ya
    nguo zake. Viatu vyake ni dhahabu.
    Wakati ule machozi yakifika katika viatu vyake, hubadilika na kuwa
    kama changarawe zenye thamani. Mara
    nyingi Yesu akianza kulia. Anasema "Binti, moyo wangu una maumivu". Moyo wake unaumia akituona yeye katika dhambi. Nasema sisi, kwa sababu mimi pia najiweka.
    Mungu hataki kutuona tunafanya
    dhambi. Kusudi la Mungu ni kutufanya Page 5 tutembee katika roho na siyo kutimiza
    tamaa za mwili (Gal 5,16-18). Anatamani
    sisi tufanye mambo makubwa kwa ajili ya ufalme wake. MIZIKI YA KIDUNIA NDANI YA
    KANISA Bwana akasema, "Nitakuonyesha dhambi nyingine inayofanyika juu ya
    madhabahu ya makanisa. Ni kuhusu muziki." Bwana alinionyeshea watu wakicheza na kusikiliza miziki ya rock,
    miziki ya rap na nyimbo za reggae katika makanisa. Hii haimpendezi
    Bwana. Neno la Mungu linasema
    anatutaka sisi tumwabudu katika Roho
    na Kweli. Hasemi anatafuta ambao wana
    rap katika roho na kweli. Tulienda sehemu nyingine Kuzimu na
    nikaona mkristo kijana ambaye alikuwa
    akiimba muziki wa kikristo wa rap au muziki wa staili ya reggae.
    Nikamuuliza Bwana 'Kwa nini yuko
    mahali hapa? Bwana kwa kweli nahitaji kujua kwa nini yuko mahali hapa? Kwa
    nini anaimba?". Wakati huu nilikuwa
    nakumbuka jinsi wanamuziki wengi walivyokuzimu Selena, Michael Jackson, na wanamuziki wengine wengi wanaungua katika moto wa Kuzimu. Nikamuuliza Bwana je, alikuwa
    akiimba katika kanisa?". Alijibu "Ndiyo binti aliimba katika kanisa ." Bwana hakusema kitu kingine chochote baada ya taarifa hiyo. Nilianza kuongea na kijana huyu.
    Alisema "kina langu ni marko.Niko
    mahali hapa kwa sababu sikumuabudu Bwana. bali niliimba miziki ya aina ya
    rap. Nilikuwa nikiimba miziki hii katika
    kanisa lakini sikupenda kuomba, sikuwa na maisha ya
    maombi.Sikupendelea kutafuta uwepo
    wa Mungu badala yake. Lengo langu katika kuimba nyimbo hizi ilikuwa ni
    kuwavutia vijana kanisani. Nilitaka
    makundi ya kihuni yaje kanisani, sikuweza kutambua ni Mungu pekee
    ndiye ambaye angeweza kuwavuta . Ni
    Yeye peke yake ambaye anashughulika na nyoyo zao. " Nilimuuliza "Ni kwa muda gani
    umekuwepo mahali hapa? je kuna
    sababu nyingine yoyote ya wewe
    kuwepo hapa? ".Alisema, " miaka 4. Ndiyo
    nilikuwa na kiburi sana, Niko pia hapa
    kwa sababu hiyo. Hapa mapepo unitesa na daima hunicheka wanasema '
    miziki ya kiduni ni chombo tunachotumia
    kuleta vijana mahali hapa.' Marko alikuwa amefungwa kabisa
    wakati anasema nami . Mikono yake na
    mwili yake vilikuwa vimefungwa na nyoka. Alikuwa akilia na kuniuliza mimi "Je,
    unaweza kunisaidia?" Nikamjibu "Hapana Marko, naweza
    kama ningeweza lakini siwezi". Alinijibu "Najua kamwe siwezi kutoka
    nje ya hapa. Niangalie, niko nateseka. Wakati nilipokufa nilianguka
    katika tanuru. Baada ya kufika chini ya tanuru mwili wangu ulilipuka kwa
    kuwa nimefika kuzimu. Minyoo huwa inatoka nje ya mwili wangu na
    nimebakia katika adhabu hizi hata sasa. Nimekuwa na umbo baya na moto wa
    kuzimu unaendelea kunichoma. Siwezi kuvumilia tena. Mapepo
    yanasema huu ni ufalme wangu na
    kwamba Shetani ni mungu wangu ". Nilisema "Naelewa, lakini Marko duniani
    ulikuwa na nafasi ya kutubu." Akasema kwa sauti "Wambie vijana
    wamuabudu Yesu. Wambie kanisa lote Waabudu. Mungu anatafuta waabudio
    halisi! "Baada ya Marko kuongea moto
    ulikuja kati yetu. Niliposogea tu mbali akawa amezungukwa na miali ya
    moto. Wakati tunazungumza moto
    ulikuwa umefika tu kwenye kiuno chake, baada ya kauli yake ya mwisho
    mateso yaliendelea kama hapo awali. Page 6 Bwana akaniambia "Binti, watu wengi wanafikiri kwamba kwa baadhi ya
    miziki na vipindi fulani wanaweza kuwavutia watu wa mataifa na
    kuwafikia watu walioathirika na
    madawa ya kulevya. Hapana! si
    watu wanaoweza kumgeuza mtu aache
    dhambi, ni Roho Mtakatifu ambaye
    anahusika nao na kumshawishi mtu kwa dhambi zake. Ni mimi ambaye
    nagusa mioyo. Ni mimi ambaye
    nashughulika na moyo ya mtu, mimi pekee ndiye mwenye uwezo wa
    kuokoa. Watu wanadhania wao ndio
    waokoao. " Hivi ndivyo Bwana aliniambia. Nililia. Hii
    ilikuwa ni ngumu kwangu, bado ni
    ngumu tu. Nadhani kama wewe ni msikilizaji wa aina hii ya muziki lazima
    UACHE. Hii ni kati ya wewe na Mungu
    hata hivyo. Mimi nimefanya kutimiza mapenzi ya Mungu
    kukueleza, Siwajibiki tena kwa sababu
    nimekuambia kile Mungu alisema. Kama unataka kukubaliana na
    hili, kubali. Kama unataka kukataa,
    kataa, nimetimiza wajibu wangu. Hili ndilo jambo analolihitaji kwangu.
    Kama nisipomtii, Kuzimu inanisubiri
    (Ezekiel 3,16-21). Sitaki kwenda mahali pale na kuishia katika mateso,
    tayari nimetembelea huko mara 3,
    mahali pale ni halisi kuliko maisha haya ya Duniani. Tulipoondoka kwenye
    shimo la Mark alianza kutukana/
    kukufuru. Bwana aliniambia 'Ukiondoka katika eneo hili
    kawaambie kanisa langu waniabudu
    mimi katika Roho na Kweli ". Yohana 4:23 23 Lakini wakati unakuja,
    tena umekwisha timia, ambapo wale
    wanaoabudu inavyostahili watamwabudu Baba katika roho na
    kweli. Watu wanaoabudu kwa njia hii
    ndio anaowataka Baba. 24 Mungu ni roho na wote wanaomwabudu
    imewapasa kumwabudu katika roho na
    kweli." (Pia angalia Col 3,16-17, na Eph 5, 17-21) MKE WA MCHUNGAJI Tulipokuwa tukienda kwenye eneo
    jingine tofauti nikamuona mwanamke
    Kuzimu. Alikuwa akilia" Siwezi kuvumilia tena. Siwezi kuvumilia tena!
    Bwana, nisaidie." Huyu mwanamke
    aliwahi kumtumikia Mungu kwa miaka mingi wakati alipokuwa duniani.
    Baada ya maisha haya hauwezi kupata
    thawabu ni kwa miaka mingapi ulimjua Bwana (Ezekieli 18:21-32 ).
    Tunarithi wokovu(salvation) tu kwa njia
    ya kumtumikia Mungu kwa mioyo yetu yote na maisha yaliyo katika
    mapenzi yake ( Mathayo 7: 21-23 ). Huyu
    mwanamke alijua neno la Mungu. Hata kuhubiri neno la Mungu
    alilihubiri, lakini alikuwa kuzimu kwa ajili
    ya dhambi ya uzinzi ((Admin Note: 'Once Saved Always Saved' is a
    false doctrine, a Christian can indeed be
    disqualified – Gal 5, 19-21, Eph 5, 3-5). Hii ilinifanya niwe na huzuni
    sana na ilinisumbua. Kuzimu, aliteswa
    na majoka katika namna ile ile makahaba walivyokuwa wakiteswa.
    Alikuwa akiyaambia mapepo " Mimi ni
    mke wa mchungaji, msiniguse. msinifanyie hivi". Mapepo yaliendelea
    kumtesa hata hivyo. Bwana
    alinithibitisha kile mwanamke huyu aliniambia kuhusu uzinzi. Alisema, " Yeye yuko mahali hapa kwa kufanya
    uasherati na uzinzi. Duniani yeye alikuwa mke wa mchungaji ambae
    pia alihubiri neno la Mungu. Alikuwa
    na watoto pia, lakini hii haikumfanya aache usaliti kwa
    mume wake ". Unajua nini? Dhambi hii inafanyika
    katika makanisa mengi. Hata Watumishi
    wengi wa neno la Mungu wamefanya dhambi hii. Hii ni lazima
    kuachwa. Hii imeendelea kwa muda
    mrefu sasa. Mpingeni shetani naye atawakimbia. Weka imani yako kwa
    Yesu. Ilikuwa ni ngumu kwa mimi kuona
    hili. Ni huzuni kujua mara nyingi hili linafanyika. Wagalatia 5:19 19 Basi matendo ya
    mwili ni dhahiri nayo ni haya: uasherati,
    uchafu, ufisadi, 20 kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira,
    fitina, mafarakano, uzushi, 21 husuda,
    ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya,
    kama nilivyokwisha waonya kabla,
    kwamba watu watendao mambo kama haya, hawataurithi Ufalme wa Mungu. Page 7 MWINJILISTI KIJANA KATIKA
    MIALE YA MOTO Kisha nikasikia kijana analia "Nisaidie
    Bwana, Nisaidie" kijana ambaye alikuwa
    analia alikuwa mwinjilisti duniani. Yeye alifanya uasherati mara
    kwa mara. Neno la Mungu
    linatahadharisha "Kama hawawezi
    kujidhibiti wenyewe wanapaswa kuoa. Ni afadhali
    zaidi kuoa kuliko kuwaka kwa tamaa
    "(1Cor7). Ni afadhali kuoa na kuepuka dhambi, kwa maana kama
    ukiishi katika dhambi na ukafa
    utakwenda motoni/kuzimu. Mtu huyu alikuwa mhubiri wa neno la Mungu. Hii
    inatufundisha kwamba tunapaswa
    kuomba bila kukoma na siku zote tuwe macho kwa ajili ya mitego ya adui,
    ambaye anatafuta jinsi gani anaweza
    kuwashambulia watumishi wa neno la Mungu. Kuna mamilioni ya
    mapepo ambayo yako tayari kwa
    kuwajaribu wahubiri. Ni muhimu sana kwa kanisa kufanya maombi kwa ajili ya
    wachungaji wake, nyumbani na duniani
    kote. Wanahitaji ulinzi kwa mashambulizi ya kila wakati.
    Niliposogea mbali kidogo miali ya moto
    ilimvaa na kuanza kumuunguza. Moyo wangu uliumia sana kwa ajili ya kijana
    huyo. Hata sasa bado ninasikia huzuni
    kwa ajili yake. Nashiriki hili ili na wewe utambue ni lazima kutii neno la
    Mungu. 1 John 2:3 3 Na tunaweza kuwa na
    hakika kwamba tunamjua Kristo ikiwa
    tunatii amri zake. 4 Mtu ye yote akisema, "Ninamjua' 5 Lakini mtu ye
    yote anayetii neno lake, huyo ndiye
    ambaye upendo wa Mungu umekamilika ndani yake kwa kweli. Hivi
    ndivyo tunavy ojua kuwa tumo ndani ya
    Kristo. MCHUNGAJI ALIYETESEKA
    KUZIMU Katika sehemu iliyofuata nilimuona
    Mchungaji akiwa katika mateso. Alikuwa
    ameshikilia mikono yake kwa namna ambayo alionekana kama
    anakunywa pombe, alikuwa kama mlevi.
    Niliwaza, mchungaji mlevi Kuzimu? Alikuwa ni mnafiki katika kanisa. Alikuwa
    mchungaji aliyechunga kusanyiko
    kubwa lenye washirika wengi. Yeye pia alikuwa mwongo na mzinifu.
    Pembeni na mchungaji alikuwepo pepo
    ambaye ilionekana kama ni mwanamke na aliendelea kuwa mlevi na
    mzinzi na pepo ambaye aliyemtesa. Mtu
    huyu alisema "nilikuwa mchungaji, nilihubiri neno la Mungu
    lakini sikuwa naishi neno la Mungu.
    Nalipenda kulewa na pia kumsaliti mke wangu. Kamwe sikutubu dhambi
    hizi. "Mtu huyu alijua kwamba neno la
    Mungu linasema wazinzi hawataurithi ufalme wa mbinguni, wala
    walevi (Gal 5:19-21 & Rev 21,8). Watu wengi duniani wanahubiri neno la
    Mungu lakini wanaendelea kuishi katika
    dhambi. Watu inawapasa kuachana na dhambi na kuanza
    kumtafuta Mungu. Mchungaji huyu
    aliniambia "Ni lazima uwaonye watu
    wasije mahali hapa. Tafadhali, ni lazima
    uwaonye kanisa waepuke moto wa
    Kuzimu." Bwana kisha akanionyesha katika screen kubwa sehemu ya maisha
    yake. Duniani alihubiri wakati mke wake
    alikuwa pamoja naye akimsaidia huduma yake. Alikuwa tajiri
    na mwenye mafanikio, lakini sasa
    kuzimu, alikuwa hana nafasi ya wokovu. Hakuwa na mwanamke
    aliyempenda duniani. Kwa milele yote
    alichonacho ni adhabu ya milele ... adhabu, adhabu, adhabu, hiki ndicho
    alichonacho! Ilinikatisha tamaa
    nilipoona jinsi mchungaji anaweza
    kuishia katika Kuzimu na nikamuambia Bwana
    mimi sitaki kuona mambo haya tena, pia
    hata kuhubiri. Bwana akaniambia "Binti yangu, ni lazima kutimiza mapenzi yangu. Ni Lazima
    kutii, nitakuonyesha ni kwa nini ". WITO UKIKATALIWA, HATMA
    YAKO INABADILIKA Tulipoingia selo nyingine kulikuwa na
    mwanamke na BWANA aliniambia
    mambo mengi kuhusu yeye. Aliitwa katika wito wa kumtumikia Mungu kwa
    huduma akiwa na umri wa miaka 15.
    Wakati huo alimwambia Mungu "siko tayari kwa ajili ya huduma", "mimi
    bado ni mdogo. Niruhusu nimalize shule
    vyema". Baada ya hilo tena BWANA akamwita tena. Alisema pia
    "Nimeolewa sasa, ni lazima nizingatie
    kutunza watoto wangu. Huu si wakati . " Baada ya watoto wale kukua
    na kuanza kuwa na familia zao wenyewe
    mwanamke alizingatia Page 8 kuwalea wajukuu wake. BWANA
    aliniambia" Niliendelea kumuita katika maisha yake yote, lakini yeye alinipuuza, na kukataa wito wake ." Bwana akaniuliza " Je, wewe utakataa mwito wangu ? " Mimi nilisema " Hapana BWANA. Lakini Bwana hii si
    rahisi kwangu". Bwana akaniambia "Ni mimi nizungumzae kupitia wewe. Mimi ni Njia, Kweli, na Uzima.
    Mimi nitakusaidia na kukuongoza
    wewe." Nilikuwa ninalia na nikaweka ahadi " Sawa BWANA, Mtu
    yeyote akiinuka dhidi yangu na ainuke.
    Umenihahidi utakuwa pamoja nami hivyo nitaendelea haitojalisha
    chochote. " Siendi kuishia hapa." Hivi
    ndivyo nilimuambia Mchungaji wangu hivi karibuni, Nataka kuendelea
    kwa sababu ni lazima nitimize wito wa
    Mungu juu ya maisha yangu. Huyu mwanamke hatimaye alikuwa
    mzee na akafariki na akaenda kuzimu
    kwa ajili ya kutotii. Karibu roho 5000 za watu wamepotea kuzimu
    kwa sababu yake. Mapepo kule kuzimu walikuwa wakimwambia " Angalia uone, roho nyingi za watu wako
    hapa kwa sababu yako" Alimwangalia
    Yesu na kulia " Bwana nisamehe kwa kutotii wito
    wangu.Nisamehe kwa kutokuitikia."
    Watu wangapi leo ulimwenguni wako
    katika hali hii. BWANA anapokuita na
    kukuchagua, ni lazima utii. Bwana
    aliniita mimi nikiwa na miaka 17.
    Nilikuwa sijui chochote kwa habari ya Biblia.
    Kutokea hapo Roho mtakatifu amekuwa
    akinifundisha. Kuzimu, Huyu mwanamke aliendelea kumsihi BWANA
    kwa msamaha kwa kukataa wito.
    BWANA akasema " Huna fursa nyingine zaidi ya msamaha". Bwana kwa machozi akaniambia "Usinikatae" Nimekuita na kukuchagua wewe. Wewe ni Mlinzi wangu ili
    ulipeleke Neno langu ulimwenguni
    kote." (Ndugu Msomaji) Mungu amekuchagua
    wewe ili uisikie ujumbe huu. Wengi
    hawata usikia. lakini Mungu amekuchagua wewe uusikia. Yule
    mwanamke kuzimu alimwambia BWANA
    mimi ni mdogo,nasoma, shughuli nyingi, wakati bado. Angalia kile
    kilichotokea kwenye maisha yake.
    Ametubu lakini hivi sasa amechelewa. Sasa ninakuuliza wewe, Kitu gani
    ungefanya? Je, utatii kile Bwana
    anakuita ukifanye? Umechaguliwa na BWANA ili uwafikie waliopotea.Ni lazima
    kutimiza kusudi la Mungu Kwa sababu
    ametuchagua sisi ili tukae katika kusudi lake timilifu. Kama
    tutafanya hivi basi tutakuwa katika
    uwepo wake milele yote. Usiendelee kukataa zaidi, pokea.Roho Mtakatifu
    atakuongoza, na sio mwanadamu.
    Mungu mwenyewe atakuongoza. Mwanamke huyu aliendelea kuteswa na
    mapepo kuzimu. Yalimueleza "Mungu
    alisema na wewe na akakuita. Haukumtii BWANA na sasa uko mahali
    hapa milele". Nililia nilipokuwa namuacha yule
    mwanamke na nikamsihi BWANA anisamehe kwa kutaka kuacha
    kuhubiri neno lake. Unafahamu ni kwa nini nilitaka kuacha
    kuhubiri? ni kwa sababu baadhi ya watu walianza
    kunishtaki wakisema mimi ni nabii wa uongo. Baada ya kujionea
    mwenyewe uzoefu huu sijali tena mashtaka yao juu yangu.
    Wanaweza kusema chochote wanachoweza kusema lakini
    nitaendelea kuhubiri neno lake. Bwana aaliniambia "Usiwaogope wanadamu, niogope mimi. Usijali kuhusu maoni
    yao, niangalie mimi." Sasa ni kwa nini tuogope maoni ya watu.
    Wao hawawezi kukuhakikishia uzima wa milele, bali ni
    Yesu pekee awezaye.Hata kama watu wataendelea
    kukupinga, usiruhusu hilo liwe ni
    kikwazo na kukufanya uache. Mashitaka yao nay awe sababu ya
    kukuinua na kukufanya imara. Mungu
    atatumia hili kukusaidia kuvumilia na kusonga mbele. Majaribu tuliyonayo ni
    magumu lakini Yesu yupo pamoja nasi. Page 9 Luka 12 4 Nawaambieni ninyi rafiki zangu: msiwaogope wale wanaoua
    mwili, wasiweze kufanya kitu kingine zaidi. 5 Nitawaonyesheni yule ambaye ni lazima kumwogopa: mwogopeni yule
    ambaye baada ya kuua ana uwezo wa kumtupa mtu katika moto wa
    Jehanamu. Naam, ninawaambieni,
    mwogopeni huyo.- Yesu. KUJIUA Bwana alisema "innaniuma sana kuwa Upendo wa wengi katika dunia
    umepoa. Majaribu mengi sana yanakuja kwenye dunia.
    Nitakuonyesha mmojawao ambaye
    mwanzo alinipenda na kunitumikia." Tulipokaribia sehemu nyingine mtu moja
    akapaza sauti "Bwana wangu Mungu
    wangu nilikuwa nikikupenda sana. Nilikuwa nikitaka kufanya
    makusudi yako kila wakati, lakini
    nilikuwa na nia mbili. Sikuwa na
    msimamo madhubuti katika safari yangu nawe
    Nilipokuwa nikihubiri uliniongoza.
    Wakati huo nilikuwa nimtiii kwako. Lakini mara nilikuwa nikikuacha na
    kurudi kwenye mambo yangu ya kale.
    Nikirudi kwako, unanirejesha Mimi tu hawakuweza kusimama maisha
    yangu. Hiyo ndiyo maana Mimi alijiua.
    Sikuweza kujisimamia maisha yangu. Ndiyo maana nilijiua." Mtu huyu kuzimu ni muuaji.Kuwa muuaji
    sit u kukpiga mtu na risasi au kutoa
    mimba. Mauaji pia ni pamoja na kuchukua uhai wako. Kama ukijiua
    unakwenda Kuzimu. Imeandikwa:
    Hakuna muuaji atakayeurithi Ufalme wa Mbinguni' (Gal 5,19-21, Ufu 21,8).
    Hakuwepo katika uwepo wa Mungu kwa
    sababu alijiua.Unajua nini, kama wewe ni mmojawapo wa wale watu
    wanaochoka kumtumikia Mungu,na
    huwezi kuendelea, umechanganyikiwa, Umechoka kumtumikia Mungu, labda
    inawezekana Dunia inakuvuta.
    Nakueleza kataa matamanio ya mwili, Kataa!! Tembea katika Roho.Mungu
    atakusaidia ukae katika kusudi lake. Hili
    sio jukumu la wachungaji au mtu yeyote mbali na wewe mwenyewe.
    Unatakiwa kuitika muongozo wa Roho
    Mtakatifu. Wagalatia5:16 Basi, nasema hivi: mwenendo wenu na uongozwe na Roho,
    nanyi hamtafuata tena tamaa za kidunia. 17 Maana, tamaa za kidunia hupingana na matakwa ya Roho; na
    matakwa ya Roho hupingana na tamaa za kidunia. Mambo hayo mawili
    hayaafikiani; kwa sababu hiyo hamwezi
    kufanya yale mnayotaka ninyi wenyewe. HATARI YA KUPIGANA,
    MGAWANYIKO NA NA UGOMVI
    USIO WA KIMUNGU Baada ya kuondoka katika eneo lile -
    watu wawili walikuwa wakipigana
    Kuzimu. Mapigano kuzimu Hii ilikuwa ni ufunuo wangu wa mara ya 3
    wa kuzimu na sikuwahi kuona hili. Kuna
    makanisa mengi ambayo yamejazwa na wanafiki. Wanaume
    ambao ni wazuri makanisani lakini
    kiukweli hupigania maslahi. Wanapigania fedha, hupigania waumini
    makanisani, nao huendelea kupigania.
    Wanafiki! Nafsi ni mali ya Kristo. Fedha si kwa ajili ya watu, ni kwa
    ajili ya kufanya kazi ya Ufalme wa
    Mungu. Watu hawa wawili walipigana kwa hasira na wanaume
    wengi zaidi walikuja na kujiunga katika
    mapigano. Mapepo yaliendelea kuwapa mateso wakati wao
    wakiendelea kupigana. Moto
    ukawachoma na walikuwa katika
    adhabu kubwa, walipiga kelele na mayowe kwa
    uchungu. Nilimuuliza Bwana "Kwa nini
    wanapigana?" Bwana hakunijibu.
    Nikawageukia watu wale na kuwaambia "Acheni! Mbona mnapigana? Mko katika
    mateso na mnaendelea kupigana.
    Niambie kwa nini mko mahali hapa, nataka kujua. "Mtu mmoja alinitazama
    na kusema" Tunapigana kwa sababu
    hatuwezi kutoka mahali hapa. Tunafanya vile vile tulivyokuwa
    tukifanya duniani. Duniani tulipigania
    maslahi/faida,Tulipigania washirika na kuwasogeza kwenye mikusanyiko yetu,
    tulipigana ili kupata zaidi kwa ajili yetu
    wenyewe. Sasa nimetubu na ninaomba msamaha kwa Mungu. Lakini
    najua Neno la Mungu kabisa kuwa
    stoweza kusamehewa." "Watu hawa walipigana muda wote. Bwana
    aliniambia "Kuna watu wengi duniani ambao mwanzoni walikuwa watumishi waaminifu, lakini sasa
    wanaelekea mahali hapa. Waambie
    wasije mahali hapa. " Page 10 Huu ni wajibu wangu. Nimekuwa
    nikiwaonya wachungaji pia. Nimekwenda kwenye maeneo ambapo
    lengo la huduma limekuwa kutengeneza faida. Kuna
    wachungaji ambao wanapigana kwa ajili ya fedha na
    kuwachukua wajumbe wa makanisa. Hii ni sababu ileile ya watu
    wale waliokuwa wakipigana kule kuzimu. Pia nimekuwa
    katika maeneo ambapo wachungaji wanampenda Mungu kwa
    mioyo yao yote.Wako tayari kutoa uhai wao kwa ajili ya Injili
    na wanapenda kufanya kazi kwa ajili ya Ufalme wa Mungu.
    Lakini pia kuna wachungaji ambao ni wanafiki, lakini
    wote hawa pia. Hii ni bure na hivyo ndivyo ilivyo kwa baadhi
    ya wainjilisti. Inatisha kwamba baadhi
    ya viongozi wanapigana ili kuchukua washirika kwenye makanisa
    yao wenyewe. Wanataka kujaza
    makanisa yao kwa urahisi. Nafsi/Roho si zetu, ni zake Yesu Kristo. Hizi ni roho/
    nafsi zilizo kuzimu kwa sababu hizi.
    Hakuna unyenyekevu katika mashindano. Mungu hapendelei sisi tugawanyike.
    Anapenda tuendelee kuungana kama
    ilivyo hivi sasa. Angalia jinsi wachungaji ambavyo wamekuwa
    wakikusanyika hivi leo, Huyu ni
    mchungaji na huyo na huyo.
    Tunakutana kwa kusudi moja tu. Mungu anatutaka
    sisi tushikamane. Anataka kutuona
    tukisaidiana. Haijalishi unatokea wapi. Unaweza kuwa umetokea
    Ufaransa au New York au Italy,
    haijalishi. Bado unaye Roho Mtakatifu
    Yule Yule. Mungu anatutaka tuwe wamoja.
    Sisi ni mwili mmoja na yeye ni Kichwa. Imetupasa kuungana pamoja kwa ajili
    ya kazi ya Mungu, na pia ni lazima
    tupendane sisi kwa sisi, tusiwe kama wale watu wanaoishia kuzimu. Angalia
    jinsi walivyomalizikia Kuzimu,
    wanapigana na kutongea maneno machafu wao kwa wao. Ilinifanya
    nijisikie vibaya. Baada ya uzoefu huu
    nililia sana. Nililia kwa sababu inaniuma kuona jinsi wanaume na
    wanawake wengi wanapigania vitu vya
    ulimwenguni. Hawapigani kwa mambo yaliyo muhimu, mambo ya
    rohoni. Usipiganie vitu vya mwilini bali
    pigana na shetani mwenyewe ili tusikose Baraka zetu. Baraka za Mungu
    ndizo njema kuzipigania, lakini kupigana
    na kusababisha mgawanyiko ndani ya kanisa si jambo la Mungu. Inaniuma kuona adhabu ya milele ya
    watu wanaosababisha migawanyiko.
    Nilipokuwa nikiwaona watu hawa wakipigana Kuzimu, Mmojawao
    aliniambia "utakarorejea duniani
    waambie watu wasipigane au kusabisha migawanyo". Labda kwa siri unapigana
    na kusababisha migawanyo. Labda
    katika jamii unapingana na watu. Mungu akuaiishi ila anakusahihisha.
    Anataka uwe na moyo wa unyenyekevu
    na roho iliyopondeka.Tubu na usirudie kosa. Mungu anatamani
    kutuona tumeingia katika uwepo wake,
    lakini imetupasa kutembea katika utakatifu. Ni lazima tuwe watatakatifu
    kwa sababu yeye ni mtakatifu. Waebrania 12:14 Tafuteni kwa bidii
    kuwa na amani na watu wote, na huo
    utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
    15 mkiangalia sana mtu asiipungukie
    neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na
    kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa
    unajisi kwa hilo. MATEKA Kuna mambo mbalimbali ambayo
    hufanyika kuzimu. Sikutaka kuona kitu
    kingine chochote baada ya kuona watu wale waliokuwa wakipigana. Lakini
    kabla ya kuondoka Mungu alinionyeshea
    roho za watu walio kuzimu ambao bado wako hai duniani. Watu
    hawa wamefungwa na kuonekana kuwa
    katika magereza/selo. Huu ufunuo wa Mungu alionipa ni sawa na
    kile nilichosikia watumishi wengine wa
    Mungu wakisema katika Page 11 shuhuda zao. Kuzimu nikamuona
    msichana Ninayemjua hapa duniani.
    Nikamuona msichana huyu katika moja ya selo hizo. Mimi bado sijamweleza.
    Bwana akaniambia si wakati wake wa
    yeye kumwambia kwa sababu hataweza kulipokea jambo hili. Nisubiri
    wakati wa bwana kumwambia. Bwana
    atakaponieleza basi itakuwa wakati muafaka wa yeye kusikia.Yeye ni
    rafiki yangu. Mimi nisingeweza kujua
    kama isingekuwa huu ufunuo. Ufunuo wa Bwana kwangu ni kwamba
    yeye alikuwa katika selo kwa sababu
    alikuwa mtumwa wa dhambi (Rum 6,16). Nilisema "Bwana Sielewi.
    Nilinaona nafsi/roho zikianguka katika
    tanuru na kutua ndani ya kuzimu lakini zingine ziliishia mahali hapa." Niliona pia
    Wakristo wenye nia mbili wakiishia
    mahali hapa. Niliangalia na kuona watu wengi wamefungwa na
    dhambi. Bwana aliniambia "msichana unayemuona anaishi katika uasherati. Yeye pia ana chuki/
    uchungu katika moyo wake, si amani
    yangu. Nenda kuzungumze nao ". Bwana alisema "wao" kwa sababu
    kulikuwa na msichana mwingine mahali
    pale ambaye nilikuwa namjua. Wasichana wawili walikuwa katika
    sehemu ile ya utumwa. Wasichana hao
    wamefungwa na dhambi (Yohana 8,31-36, Rom 6,15-21). Bwana
    akaniambia "Nenda ukawaambie kwamba nataka kuwaweka mateka
    huru na kuwakomboa. Nataka kuwakomboa
    kutoka katika magereza waliyomo
    na kufanya mambo makubwa katika maisha yao ". Mimi nilijibu "Ndiyo Bwana nitawaambia". Tulipoendelea kutembea niliona roho
    nyingi kwenye utumwa. Kwa bahati
    mbaya, wote walikuwa wamemjua Mungu kwa wakati fulani. Tulitembea
    hadi kwa mwanamke mwingine
    niliyemjua, ambaye alikuwa katika hali hiyohiyo kama rafiki yangu. Alisema kwa
    kilio "Bwana Siwezi kubaki hapa tena."
    Bwana akamwambia "Hii ni dhamiri yake, yeye anaishi katika
    uasi/kutokutii, katika dhambi." Alinifunulia mambo zaidi kuhusu mwanamake huyu akasema "Nenda kawaambie wanawake hawa yale
    umeona." Tayari nimesema na mmoja lakini bado mwingine ( Tukirejea
    nyuma), bado wakati muafaka. Baada ya
    kusema nao inakuwa ni wajibu wao kupokea hilo au la. Mungu anataka
    kuwaweka huru mateka na kuwafungua
    wale waliofungwa. Anataka kukutoa wewe nje ya utumwa na uteka
    na kuwapa uhuru. Chuki husababisha
    utumwa. Chuki, uchungu na hisia hizi zote husababisha kufika mahali
    hapo. Lazima kumwomba Mungu
    kutafuta moyo wako, ni nini katika moyo wako? Kukiri kwamba kuna umuulize
    Bwana auchunguze moyo wako. Mungu
    atavunja minyororo hiyo na kukutoa katika gereza hilo. Ukikiri na
    kutubu Bwana atakuweka huru, lakini
    kwanza lazima kukiri dhambi na kutubu. 15 Basi, tuseme nini? Je, tutende dhambi ati kwa sababu hatuko chini ya
    Sheria bali chini ya neema? Hata kidogo! 16 Mnajua kwamba mkijitolea ninyi wenyewe kama watumwa na kumtii
    fulani, mnakuwa kweli watumwa wake mtu huyo--au watumwa
    wa dhambi, na matokeo yake ni kifo, au
    wa utii, na matokeo yake ni kukubaliwa kuwa waadilifu KUZIMU & ZIWA LA MOTO Kisha Bwana alianza kunipeleka juu na
    kunitoa nje ya Kuzimu. Ilikuwa kama
    tunapanda ngazi ndani ya handaki lenye giza. Tulipofika juu
    nilitazama chini na kuona kuzimu katika
    muonekano tofauti. Kuzimu ni mahali pakubwa sana. Katika
    muonekano wangu niliona kuzimu kama
    sehemu iliyo katikati yenye kina na nikaona pia ziwa la moto
    vimetenganishwa. Ziwa la moto lilikuwa
    chini ya kuzimu.Hivi ndivyo ambavyo naweza jaribu kuelezea kile
    nilichokiona. Niliona mkusanyiko
    mkubwa wa moto na salfa. juu ya
    mkusanyiko huu niliona umbo la mdoli,au mwili.
    Mkusanyiko huu ni ziwa la moto, Baada
    ya Bwana kunionyeshea Ziwa la Moto tuliondoka. Ufu 20, 15 Na mtu
    yeyote ambaye hakuonekana
    ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika ziwa la moto. Page 12 TAFUTA & MTUMIKIE BWANA
    MUNGU Kwa wale ambao wanasikiliza au
    kusoma ushuhuda huu napenda kusema hili nanyi. Mungu amekupa
    ujumbe huu kwa sababu Yeye ni halisi! Hatumtumikii mungu wa mbao.
    Hatumtumikii mungu mfu. Tunamtumikia Mungu aliye hai.
    Aliniambia "Mimi kamwe sibadiliki! Ninaendelea kuwa Mungu
    aliye hai! Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Ni Mungu wa jana, leo na hata milele. Sijawahi kubadilika na kamwe
    sitabadilika. "Usisahau kuwa tunamtumikia Mungu mkubwa. Tafuta
    uwepo wake katika Roho na Kweli. Usiwe mnafiki, mtumikie Yeye
    katika Roho na Kweli. Mungu ambariki
    kila mmoja na kila mmoja wenu. Muda unatuacha.Mungu anahitaji
    kanisa lake tutembee katika
    Utakatifu.Kila muda unaapokwenda tusiukumiwe na dhambi.Sasa ni
    muda muafaka.Mpokee Yeu kama
    BWANA na Mwokozi na umtumikie yeye kwa moyo wote. Ndugu aliyefasiri ufunuo wa 3 wa
    mbinguni na kuzimu wa Angelica
    Zambarano ni Peter Kahale ni kijana aliyeokoka na anampenda Yesu na
    mwenye shauku ya kuhubiri injili ya
    Yesu Kristo. Simu ya Mkononi:
    +255-769-610460,
    +255-653-610460. Barua Pepe:
    kahalepeter@gmail.com

    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate