www.DivineRevelations.info/2v Imefasiriwa na Peter Kahale Katika safari yake ya pili, Angelica
alionyeshwa hukumu dhidi ya Wakristo
wanaomuibia Mungu katika zaka
na sadaka, hukumu dhidi ya watawa
wanaofanya ibada ya sanamu na watoto
walioasi, kitabu cha uzima cha Mwanakondoo, na mengine zaidi. "Waambie watu wangu kwamba kuja
kwangu ku karibu, Nitakuja kwa watu
wangu watakatifu, waambie watu wangu
kwamba ni watakatifu tu ndio
watakaoniona mimi." Januari 4, 2010, 05:50 usiku, Empalme,
Ecuador. Bwana alimchukua Angelica
kwa mara ya 2.
Nakala hii imechukuliwa kutoka katika
video ya ushuhuda ya kihispania. Angelica: Saa 6:00 usiku wa manane, baadhi ya ndugu kutoka kanisani
walifika katika nyumba yangu, basi
vyombo vya habari viliwasili, na kila
kitu kilichukuliwa katika kumbukumbu.
Nilikuwa juu ya kitanda, ghafla, nikaona
malaika wawili. Kama vile ilivyokuwa mwanzo, walinichukua
mikono yangu na kusema, "Inuka, kwa sababu Mfalme wa wafalme
na Bwana wa mabwana
anakusubiri." Nilipoinuka, niliona mwili wangu umelala hapo, na watu wengine waliokuwa katika chumba
hicho. Nilianza kutembea. Nilinyoosha mikono yangu kwa malaika
na tulianza kuelekea juu. Tulikuwa tunakwenda haraka sana, na
katika sekunde chache tulifika mbele ya Bwana. Nikasikia
Malaika wakiabudu, "Haleluya ... Mtakatifu, Mtakatifu."
Nilikuwa na furaha. Katika Ufalme wa Mungu kulikuwa na
bustani nzuri sana. Niliona Bwana
akinikaribia. Akasema, "Binti, nimekuwa nikisubiri, kwa sababu
nina mambo mengi ya kukuambia", "Bwana, mimi hapa, nataka kukaa na Page 2 2 wewe. Sitaki kurudi Duniani, tafadhali
napenda kukaa na wewe. "Bwana
akajibu, "Mtoto wangu, una mambo mengi ya kufanya. Una kazi, imekupasa
ufanye kazi yangu. Nitakuonyesha kitu
kwa ajili ya maisha yako, kitu kwa ajili ya watu wangu, na kitu maalum
kwa ajili ya watu, kwa sababu nataka
uokoe binadamu na sitaki mtu yeyote apotee. " Kisha, niliona malaika wawili, Mikaeli na
Gabrieli wamebeba vitabu vikubwa; vitabu hivi
vilikuwa vizuri sana na vinang `aa.Nilipokuwa
nikiangalia vitabu hivyo, niliuliza, "Ni nini hii?" na Yesu akasema, "Je, unataka kujua ni nini kilicho katika vitabu
hivi?" Nikajibu, "Ndiyo Bwana." Akasema, "Mikaeli, fungua." Malaika Mikaeli alipoanza kufungua kitabu,
niliweza kuona maandishi ya dhahabu,
kama namba, lakini sikuweza kuelewa. Niliwaza, "hiki ni nini?", Na
Malaika Mikaeli akajibu, "Maandishi yote haya na namba unazoona zimeandikwa hapa ni wale watu
duniani ambao wamemkubali Bwana
wetu kama Mwokozi wao wa pekee, kwa mafunuo yale ambayo
alikufunulia ulipokuwa pamoja naye . "Nilipatwa na msisimko na nikamuuliza, "Ni watu wangapi wamo humo?" Alinipa
jumla ya idadi ya roho katika maelfu. Moyo ulivunjika na nikaanza kulia,
nikisema, "Bwana hizo ni roho/nafsi
nyingi ambazo ni waongofu", Akaitikia, "Unaweza kuona, malaika huyu, Malaika Gabrieli ana jumla ya
idadi ya watu wale ambao walikuwa wamejitenga mbali na njia
zangu na kuwa sasa wamekuja
kwangu, wamekuja kwangu mwanangu. "Nilitazama katika idadi ile na niliona ni kiasi kikubwa. Nikasema,
"Bwana hii ina maana taji yangu imejaa lulu na kwamba sasa
utaniacha hapa katika Ufalme wako?"
Bwana alijibu, "Hapana mwanangu , muda wako wa kuja
hapa bado, imekupasa urudi Duniani.
Je, ungependa kuona taji yako?" Nilijibu kwa msisimko, "Ndiyo Bwana,
ningependa kuona taji yangu," Alisema, "Malaika Gabrieli,
mletee taji yake." Niliona Gabrieli amebeba tray kubwa sana,
yenye taji nzuri, lakini yenye lulu chache juu yake. Nilimuuliza,
"Bwana, taji hii ni ya nani? Akanijibu," Hiyo ni taji yako mwanangu.
"Nikamuuliza," Lakini Bwana, kwa nini taji yangu haijajaa lulu,
kama nafsi/roho nyingi zimekuja kwako Bwana? "Naye
akanijibu, "Binti, bado njia ndefu inakusubiri,ni roho/nafsi 3,500
tu zimekuja mbele yangu, lakini
imekupasa kwenda na kuhubiri neno langu kwa sababu kuna roho
nyingi bado ambazo zinatakiwa kuja
kwangu." Lakini Bwana, kwa nini nisibaki hapa tu? Yeye aliniambia, "Binti, kwa sababu taji ya uzima
inapaswa kujaa lulu. Nikasema, "Sawa Bwana, Nitatekeleza kazi yako." Kisha
akasema, "Nina jambo la kukuonyesha Mwanangu." Bwana alinichukua, na kwa haraka
tulishuka kutoka mbinguni na kuingia
ndani ya tundu/tanuru la kuzimu, kama ilivyokuwa mara ya kwanza wakati
nafunuliwa kuhusu kuzimu. Nilisema,
"Oh! Bwana, nini kinachotokea?" Yesu alisema, "Ninajambo la kukuonyesha kuzimu," "Lakini Bwana Sitaki kuwa hapa. Bwana, kumbuka uzoefu/ufunuo wetu
wa kwanza, tayari ulinionyesha mambo
mengi", Alisema, "Ndiyo mwanangu, lakini sasa mambo
mbalimbali tofauti, nitakuonyesha. " Tulikwenda chini kati ya miali ya moto
zaidi, na nikaanza kulia. Haikuwa rahisi
kuwa pale. Nilisema, "Bwana, Page 3 3 nataka kutoka nje ya hapa, tafadhali
nisaidie, nisaidie." Nilisikia mamilioni ya
watu, baadhi ya watu walikuwa wakisema, "Oh Bwana, nihurumie, nisaidie tafadhali, Bwana, nipe nafasi nyingine." Miongoni mwa wale watu, nilisikia mtu
mmoja akisema, "Ninaomba msamaha wako sasa Bwana, kwa
sababu nimekuibia, nisamehe kwa
kuiba, Nilikuibia Bwana na sitaki kufanya hivyo
tena." Mimi niliuliza, "Bwana, ni nani na kwa nini yeye anasema
alikuibia?" "Mwanangu nitakuonyesha yeye ni nani." Tuliingia kwenye selo yake na nikaona mtu aliyeharibiwa. Miali ya moto ikafunguka
na nikamuona alikuwa akiungua. Watu wote walio kuzimu wana nembo/
kibao juu ya vifua vyao, na 666 kwenye paji za nyuso zao. Mtu huyu
aliunyosha mkono wake na kusema, "Bwana nisamehe." Mimi nilimuuliza, "Mbona uko hapa,na kwa nini unamuomba msamaha Bwana, kwa
nini? Unasema umemuibia Mungu, lakini hakuna mtu anaweza kumuibia
Mungu? Hii haiwezekani, kwa nini
useme umemuibia Yeye? "Yeye akanijibu, "Mimi nitakuambia historia yangu ... Nilikuwa kiongozi wa Kikristo,
kwa miaka 20 nilimjua Kristo, lakini katika kipindi cha miaka 20
Nilisema: fedha zote kutoka katika
mafungu ya kumi na sadaka zangu zilikuwa zinakwenda kuwanufaisha
wachungaji, lakini hivi sasa najuta kwa
sababu nimejua kwamba hazikuwa kwa ajili yao, zilikuwa ni kwa
ajili ya Bwana, na ndio maana nasema
nimemuibia Mungu ... Wakati huu kuna watu wengi sana duniani
wanaomuibia Bwana kama mimi. Wakati
utakaporudi duniani, waambie wale watu wote ambao hawataki kutoa
zaka zao na sadaka, waimuibie Bwana,
vinginevyo, wao nao wataishia Kuzimu, na hakuna mwizi atakayeingia
katika Ufalme wa Mbinguni. Nilijua Neno
takatifu, sasa ninajutia na kutambua kuwa nilimuibia Bwana
(Malaki 3: 8).. Waambie watu wakati
wanapomtolea Mungu, basi wamtolee Bwana kwa upendo wa kweli
". (2 Kor 9: 7) ". Mtu huyu aliendelea kusihi , "Bwana nisamehe", na Bwana akamjibu, Umechelewa sana, hakuna tena nafasi kwa ajili yako" Nilimuuliza mtu huyu, "Lakini kwa nini
wewe ulimuibia Mungu, kwa nini? Wewe
ulijua vizuri sana kuwa hatuwezi kumuibia Mungu zaka na
sadaka." Yeye akajibu, "Ndiyo, mimi nilijua vizuri sana, lakini kamwe sikufuata, sikufuata kwa sababu
nilikuwa mtu wa kiburi sana." Kamwe usimuibie Bwana, toa zaka na
sadaka kwa Mungu kwa sababu kile
tunachotoa kwa Bwana Duniani si kwa ajili ya watu. Tunapotoa kwa Mungu
kwa moyo wetu wote, ni kwa ajili ya
Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana. Biblia inasema kwamba Bwana
anatujaribu, imeandikwa vyema katika Malaki 3:8-10 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi
mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema,
Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi
mmelaaniwa kwa laana; maana
mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo
chakula katika nyumba yangu,
mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama
sitawafungulia madirisha ya mbinguni,
na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Kama unataka Mungu abariki maisha yako na
familia kwa ukuu sana, Basi usimuibie Mungu. Ni wakati wa
kumbariki Mungu, ili abariki maisha yetu. Bwana akasema, "Nitakuonyesha kitu tofauti." Baada ya kuondoka mahali hapo, Bwana alinikumbusha kitu ambacho alinionyesha kabla ya uzoefu
wangu wa pili, karibia Novemba. Wakati
huo, nilionyeshwa Selo kule Page 4 4 kuzimu, na Neno maalum. Neno 'ARVIERD' alionyeshwa
Angelica. Utafiti unaonyesha kuwa ni
Kiitalia cha kale, au Kilatini. Katika utafiti tuligundua ukurasa wa 400 wa
maandiko ya kale kuhusu neno hili,
linalozungumzia Kuzimu halisi. Sikujua maana ya hilo neno, lakini
nilielewa kwamba lilimaanisha kitu fulani
kuhusu Dini . Yesu alinichukua na kunirudisha
sehemu ile ile, ili kuona selo hizo tena. Tulipoingia,
niliona maelfu ya watu. Kulikuwa na wanawake wawili
wamevaa nguo nyeusi. Nilimuuliza Yesu "Ni nani
hao?" Nilisikitika kuona mtawa, na katika
mikono yake walikuwepo nyoka wakubwa, ambao
walitengeneza kitu kama msalaba na Rozari. Nikasema, "ni nini hii, kwa nini wako
hapa?" Mmoja wao alizungumza kwa
sauti ya huzuni akisema, " Nilikuwa mtawa Duniani, lakini sasa niko
mahali hapa." Niliona jinsi alivyoanza kuomba na nyoka alifinya mikono yake. Katika mikono yake
kulikuwa na maelfu ya minyoo. Bwana
akasema, "Angalia na sikiliza maneno haya." Alianza kulia, "Oh Bwana! Siwezi kuvumiliana na hili tena,
nataka kutoka nje ya eneo hili, sitaki kuwa hapa, tafadhali Bwana
Niaidie, nisaidie!" Kisha nikaona mwanamke mwingine, na
sehemu ya maisha yao nilionyeshwa katika aina ya fulani ya
televisheni/screen. Niliona watawa jinsi ambavyo huwa kihualisia, na
maisha yao ya siri. Niliona jinsi watawa hawa walivyo na mahusiano ya kingono
na mapadri, na jinsi ambavyo baadhi ya watawa hawa walikuwa pia
wasagaji. Niliona mengi zaidi, na sasa walikuwa wakijutia na kutubu. Lakini
kwa bahati mbaya, kulikuwa hakuna tena nafasi nyingine kwa wao kutubu;
walikuwa wamechelewa mno. Wale watawa wakasema, "Nenda na ukawaambie wale wote Duniani, wasije mahali hapa, tafadhali nenda na
uwaambie wasije hapa." Page 5 5 Wakati mwingine watawa/masista na
mapadri husema kwamba watamuomba Mungu ili
aziondoe roho zilizo Purgatory. Lakini mimi nawaambia kweli, Uniamini au usiniamini. Hakuna mahali
panapojulikana kama Purgatory. Purgatory ilitungwa tu na wanadamu,
ilitungwa na mapapa. Biblia inasema wazi wazi kwamba kuna
Mbinguni na kuna Kuzimu halisi. Yesu alinichukua mpaka
maeneo yote hayo mawili, lakini kamwe sikuwahi
kupelekwa purgatory. Yeye kwa uwazi aliniambia, "Purgatory haipo, nenda na uwaambie watu wafanye maamuzi
yao wakati bado wako Duniani, kwa sababu wakati wakiwa
na uzima, kuna nafasi ya kutubu." Watu wengi wanasema, "hebu tuombe,
ili ndugu zetu waondoke purgatory." acha hiyo! Kwa
sababu kama wao walikufa bila Kristo kule Kuzimu KAMWE
hawatoki. Ni bahati mbaya lakini ni kweli, kuwa wako
Kuzimu. Lakini kama walikufa pamoja na Kristo
katika mioyo yao, basi wako uweponi mwa Baba yetu wa
Mbinguni. Moyo wangu uumaa kujua kwamba nafsi/roho
nyingi sana zinadanganywa na shetani katika
kuamini purgatory. Rafiki yangu ni wakati wa wewe kujua
ukweli, purgatory haipo, yaani ni haipo. Inakupasa
kufanya uamuzi sasa, ni wapi na na nani ambaye ungependa
kuishi milele? Unaweza kufanya uamuzi wako mwenyewe, kama
ni Ufalme wa Mbinguni na Yesu Kristo au Kuzimu na
shetani. Bwana aliniagiza niseme moja kwa moja bila
kupoza ninapowaambia hili, iwe unaamini au
hauamini.Ninatii amri ya Bwana kwa sababu siku moja wewe na mimi tutasimama mbele ya Mungu, na kushuhudia yote mema na
mabaya tuliyofanya hapa Duniani. Kama hautatubu dhambi yako
na kuabudu kwako sanamu, utaishia kuzimu. Rejea kwa Kristo;
Atakupa uzima wa milele. Sitaki kuwatisheni, lakini ni ukweli. Neno
la Bwana li wazi sana na linasema kwamba hakuna mwizi
atakayeingia mbinguni. Bwana alinionyeshea kwamba ndani ya kila
picha / sanamu kuna pepo. Ndiyo maana watu huja kwa bikira wa
Guadalupe(Virgin of Guadalupe ) , Bikira wa Sinema, Sanamu ya Bikira Maria na
bikira wengine wengi 1 2 3 4. Hata sanamu ya 'Mtoto Yesu'. Tafadhali
niamini mimi, hizi sanamu zote zina pepo nyuma yake. Watu wengi
wanadai kuwa walikwenda kwa Bikira wa Guadalupe au Mtoto Yesu na
kupokea uponyaji. Lakini miongoni mwa kila moja ya picha/
sanamu hizi kuna pepo. Shetani
anasikiliza na kwa nguvu zake za uongo, Page 6 6 wakati mwingine anafanya ionekane
kama muujiza umetokea, ili uendelee
kuamini na uendelee kumuabudu yeye. Nisikilizeni, shetani anaenda
kukulipa wewe vibaya na atakupa mauti
ya milele. Hivyo acha kuabudu picha umtafute Kristo, kwa sababu
atakupa maisha ya milele na uzima kwa
wingi (Yohana 10:10). Bwana alinionyesha watawa hao, nao
walikuwa wakilia, "Nataka kutoka hapa, najutia kuabudu sanamu, na kufanya dhambi duniani, sasa siwezi
kuondoka mahali hapa." Nilimuuliza mmoja wao, "Lakini wewe uliijua kweli? Ulijua Neno la Mungu takatifu?"
Yeye alinijibu, "Ndiyo, nilijua Neno Takatifu, lakini kamwe sikutubu, kamwe sikumtafuta Kristo. Kuna watawa
wengi walioamua kuwa hivyo kwa
sababu nyingi. Mimi nilikuwa muongofu/hivi kwa sababu ya uchungu
nilioupitia katika mauhusiano wa
kimapenzi. Kuna watawa wengi kwa sababu ya kukatishwa tamaa katika
mapenzi. Katika kesi nyingi, wachumba
wao waliwaacha katika harusi madhabahuni, au marafiki zao wa kiume
waliwasaliti, watawa wengi kwa bahati
mbaya wapo katika kiapo kwa sababu maisha yao yamejaa
matatizo na wito huu wanautumia kama
sababu tu. Ukweli halisi ni kwamba wao wanamtumikia shetani. " Neno takatifu la Bwana linasema katika 1 wakorintho 6:9-10 " Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi
ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi
ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala
watukanaji, wala wanyang'anyi.watakaorithi ufalme wa
mbinguni. Neno lake takatifu liko wazi, Ufunuo 21:8 " Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji,
na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo
mauti ya pili. Page 7 7 Watu wote kule kuzimu hawana namna
ya kutoka, kwao wamechelewa sana.
Lakini Ninyi ambao mko hai katika dunia, bado mnaweza
kupatanishwa na Mungu. Usikose nafasi
hii, labda wewe hivi sasa unaangalia hii, na inaweza kuwa nafasi yako ya mwisho
ambayo Mungu anakupa ili utubu. Epuka
kuzimu, kwa sababu Kristo ananyoosha mkono wake wa rehema
kwako. Tulipokuwa tunaondoka katika selo
nilianza kulia kwa sauti na nilikuwa
nikisema, "Bwana nitoe nje ya hapa, Bwana, mimi sitaki kuwa hapa." Alinitoa
nje na kusema, "Nataka kuonyesha zaidi ..." Tulipokuwa tukitembea, nikasikia mayowe ya
msichana mdogo, "Nisaidie! Nisaidie!" "Wewe ni nani? Kwa nini uko hapa?" Nilimuuliza. Msichana alijibu, "mimi ni kijana, nilikuwa nina miaka 15 tu wakati nilipokufa, na kuja mahali hapa." "Lakini kwa nini uko hapa? Nini kilichokuleta wewe
hapa?" Nilimuuliza. Akasema, "Mimi nilifikiri nilikuwa na maisha mbele yangu, kwa sababu
nilikuwa mdogo sana. Watu siku zote waliongea
nami kuhusu Kristo na wokovu, lakini nilisema
kwamba Wakristo wa hizo injili walikuwa vichaa/
wehu, wakati wote nililikataa Neno Takatifu.
Sikutaka kumkubali Bwana. Kila wakati
walipozungumza na mimi, niliwacheka na kuwadhihaki.
Sasa naona kwamba nilifanya makosa makubwa ya
maisha yangu. Niangalie wakati huu
niko mahali hapa ninaungua katika moto. Nilikufa katika ajali ya gari
na sasa ninajutia sana. Nimekuwa
nikitafuta njia ya ktoka hapa mara nyingi, na mara ninapoiona njia hiyo
siwezi kutoka, kwani mapepo
yanayonitesa yanasema, 'huwezi kuondoka mahali hapa, wewe ni hapa milele. 'Sitaki kuwa hapa, oh tafadhali
nisaidie, nisaidie! "Mimi nikasema, "Siwezi kufanya kitu chochote
kwa ajili yako, Ninatamani
ningewasaidia watu wote hawa." Bwana akasema, "Hakuna nafasi kwa wale ambao wako hapa, lakini kwa
wale tu walio Duniani." Msichana huyo akasema, "Oh tafadhali nenda kawaambie watu, na hata familia
yangu wasije mahali hapa. Nenda kaseme na vijana ambao bado
wana nafasi ya kumtafuta Kristo,
waambie wageuke wawe mbali na dhambi. Nilipokuwa duniani, niliishi
maisha ya ovyo, maisha yaliyojaa
dhambi, nilikuwa na kiburi sana, nilifurahia kwenda kwenye pati/starehe
za kila namna, kamwe sikuwatii wazazi
wangu, nilikuwa muasi siku zote.Sasa ninajuta sana, na ninawataka
wanisamehe. , ninataka kutoka hapa,
mwambie kila mtu juu ya uso wa nchi asije hapa, asije, tafadhali.
Waambie wawatii wazazi wao,
wamkubali Kristo, kwa sababu kweli
anaokoa, yeye kweli anaokoa, shetani
alinidanganya, sasa najua siwezi milele
kutoka mahali hapa,ni jinsi gani ninajutia. " Alilia na kunyoosha mikono yake,
nilitaka kumsaidia lakini wakati ninampa
mkono wangu aushike, yeye alianza kulia na tena katika moto. Nililia,
"Bwana, ni namna gani inavyotisha
kuwepo mahali hapa" Akanijibu, "Ndiyo Binti, kumbuka hili, nenda
Duniani na utii amri yangu, ili
wanadamu waamini kwamba Kuzimu
ni halisi na ni milele, kwa sababu bado
kuna wengi ambao hawaamini katika
Kuzimu , kuna wengi ambao wanasanifu na kuleta mzaha
wakisema kwamba kuzimu ni ya
kufikirika. " Page 8 8 Siku chache kabla ya uzoefu wangu wa
kwanza katika kuzimu Bwana alinipa maono na kusema, "Angalia, mtu huyu amekwenda kuzimu." Nazungumzia mtu maarufu anayejulikana kama MJ (Michael Jackson), yeye pia
alijulikana sana kwa glove yake nyeupe. Alikuwa kuzimu kwa
sababu ile niliyoieleza katika video yangu ya awali. Nilipokuwa
nikirekodi video hiyo, Bwana aliniambia, "Sema kuhusu yeye." Ndiyo maana ninawaambia kuhusu yeye kuwa yuko katika miali ya
Kuzimu. Wakati nakaribia sehemu hiyo ya moto,
niliona pepo wengi wakiwa katika mduara, na ndani ya
mduara huo kulikuwa na mtu aliyekuwa akiteswa. Alinyoosha mikono
yake na kulia kwa sauti, "Msaada! Msaada!" Niliweza kuelewa lugha aliyokuwa akizungumza. Nilitaka kumsaidia sana, niliweza kuona
jinsi mapepo yalivyokuwa yakimnyanyua na
kumlazimisha acheze na kuimba kama
alivyokuwa akifanya Duniani. Mapepo yalimdhihaki na kumtupa ndani ya moto.
yalimchukua tena na kumchapa mijeledi.
Alilia kwa maumivu ya kutisha. Oh, ni jinsi gani alivyokuwa
akiteswa. Ilivunja moyo wangu kuona hili na
nikasema, "Bwana, tafadhali fanya kitu,
oh! Bwana msaidie." Niliponyoosha mkono wangu kumsaidia,
mikono yangu ghafla ikawaka moto, na
kujaa na minyoo. Nikasema, "Bwana Tazama! Nini kinatokea?" Kisha
mapepo yalianza kucheka na
kunidhihaki, "Wewe unakwenda kukaa mahali hapa." Kisha niligundua siwezi kuona au kuhisi
kama Bwana yu karibu na mimi,
ilionekana nilikuwa peke yangu. Nililia, "Bwana, umeondoka, kwa nini
bado ningali hapa?" Mapepo yalisema, "Tunakwenda kukuadhibu, utakaa hapa." Kisha nikasikia sauti ya kuogopesha, ilikuwa ya kutisha, "Ha ha ha, wewe unakwenda kukaa hapa. Hatimaye nimekukamata, mahali
muafaka ninapokuhitaji. Ninakutaka wewe hapa kwa sababu wewe umeiba roho nyingi kwangu na
nitakuangamiza, hapa ndio kwako.
"Alitoa amri kwa mapepo, "Mchukueni, na mpelekeni mahali panapomstahili." Nikajibu, "Hapana, hapana, mimi sitakaa
hapa kwa sababu Bwana yu pamoja
nami. Yeye alisema hawezi kuniacha hapa." Kisha nikasikia sauti ya
Shetani "Wewe utakaa hapa, utakaa hapa kwa sababu Bwana hayuko na wewe. Angalia kote, hayuko
na wewe." Nilitazama, lakini sikuweza kumwona Bwana. Nilijisikia Mpweke, na nilianza kuwa na mashaka.
Nilianza kulia na kupiga kelele, "Bwana,
kwa nini umeniacha? Kwa nini Bwana, kwa nini?" Mara Bwana akasema, "Binti, mimi niko hapa." Nilisikia sauti yake katika masikio yangu. Nilimuangalia moja kwa moja shetani, Nikamjibu,
"Bwana yuko hapa pamoja nami." Lakini
yeye alijibu, "Hakuna hayupo, wewe angalia." Sikuweza kumuona Yesu, lakini niliweza kusikia sauti yake.
Nilianza kuwa na mashaka tena kwa sababu mapepo yalikuwa
yananisogelea. Nilihisi kamba
imefungwa kiunoni mwangu ambayo
ilinivuta kuelekea kwenye ile sauti ya uovu.
Ilisema, "Wewe ni mpumbavu, ndivyo ulivyo, mpumbavu sana. Nitakuharibu kwa sababu umesababisha
roho nyingi sisije kuzimu, roho nyingi
zinatoka nje ya kuzimu kwa Page 9 9 sababu wewe unahubiri. Usifanye hivyo
tena, funga mdomo wako, yaani funga
mdomo wako, nitakuangamiza, nitakuua. " Niliendelea kulia alipokuwa akinishitaki.
Ghafla nikamjibu, "Hapana shetani,
huwezi kuniharibu mimi, kwa sababu Bwana amesema yuko pamoja
na mimi. Siwezi kumwona, lakini najua
kwa hakika Yeye yuko hapa." Shetani anaendelea kunicheka. Nilikuwa navutwa kuelekea mahali
fulani, karibu na ile sauti mbaya.
Nikasema kwa sauti, "Damu ya Yesu ina nguvu na mimi nimefunikwa na damu
yake, imeniunika hata sasa na shetani
atakimbia mbali kwa sababu damu ya Yesu iko juu yangu. Mkubwa
zaidi ni Yeye aliyepamoja nami zaidi
yako. Mkubwa zaidi ni Yeye aliye pamoja nami. "Niliendelea kurudia
maneno haya. Kisha niliona kitu
kimeniachia; kama kitu kimenivuka, ilikuwa ni ile kamba iliyofungwa kiunoni
mwangu. Hatimaye, nilitoka Kuzimu, na
kurejeshwa katika uwepo wa Mungu.
Bwana akasema, "Nataka nikupe ujumbe huu mara utakaporejea Duniani, nenda na uwaambie watu wangu
wanitafute katika Roho na Kweli
(Yohana 4:24). Nenda uwaambie watu wangu waishi
katika utakatifu. Nenda na
uwaambie watu wangu huu ni wakati, ni wakati
wa kutafakari Neno Takatifu. Si tu nawataka watu wangu wasome,
lakini pia wameze Neno langu
Takatifu. kwa sababu Binti, hiki ndicho
kinachotokea Duniani, Duniani kila
siku uasi wa dini(apostasy)
unaongezeka, bado kuna wengi wa
watoto wangu, wengi wa watu wangu wateule
wanadanganyika. Binti, waambie
watu wangu wameze/kulishika neno langu
Takatifu ili wasidanganyike na
wautafute uwepo wangu katika roho na kweli. " Mimi nikasema, "Oh! Ndiyo Bwana.
Nitatii. Lakini Bwana, nahitaji msaada
wako, tafadhali nisaidie Bwana." Alijibu, "Binti, wakati utakaporejea, Usiwe na hofu kwa sababu
nitasimama na wewe. Nitasema kupitia mdomo wako kile nimesema kwa
watu wangu. Nimeona wengi
wakiinuka kinyume dhidi yako, lakini kumbuka nitakuwa pamoja nawe
daima kama nilivyoahidi, na mimi ni
shahidi wako mwaminifu. " Kisha nikaona malaika karibu yangu.
Nilimtambua Malaika Mikaeli, kwa
sababu nilikutana naye kabla. Bwana akasema, "Sikiliza, malaika Mikaeli atakwenda kukuonyesha
kitu". Malaika Gabrieli pia alikuwa pembeni mwangu. Kisha malaika Mikaeli
akachukua mkono wangu, na Bwana
akamwagiza, "Mchukue na umuonyeshe kile imekupasa
kumuonyesha." Tulipokuwa tunatembea, tulianza
kupanda juu ya ngazi nzuri sana.
Ilionekana kama chumba cha mpira. Na katika sehemu ya juu ya chumba
kulikuwa na madhabahu ilyokuwa na
mimbari nzuri sana ya dhahabu. Tulipofika katika mimbari, nikaona
kitabu kikubwa na nikamuuliza Mikaeli,
"kitabu hiki, ni nini?" Wakati Mikaeli alipokuwa upande wa
kulia wa mimbari, aliweka mkono wake
juu ya kitabu na kusema kwa sauti yake, "Angelica, kitabu hiki unachokiona hapa ni Kitabu cha
Uzima". Nilikifungua na nikaangalia ukurasa kwa ukurasa .Nikasema, "Je,
kitabu hiki kina maana gani, Ni mambo
gani yaliyoandikwa ndani yake?" Mikaeli akasema, "Fungua, ndani ya kitabu hiki yameandikwa
majina yote ya wale ambao Duniani wametubu na wakageuza maisha
yao kumuelekea Baba yetu wa
Mbinguni." Page 10 10 Nilipokuwa nikiangalia ndani ya kitabu,
Nilimuuliza Mikaeli, "Je, jina langu limeandikwa hapa?" "Ndiyo, angalia hapo juu na utaliona." Niliangalia, lakini sikuweza kuliona. Nikawa na wasiwasi kidogo, Nikauliza, "jina langu
haliko hapa, silioni, liko wapi?" Yeye alinijibu, "Angalia, jina lako ni hili." Nilifurahi kuona jina langu, lakini
sikuweza kulielewa ni kwa sababu lilikuwa limeandikwa katika
lugha nyingine. Niligundua kuwa majina mengi yalikuwa
yanang `aa, hivyo nikamuuliza," Kwa nini majina yale
yanang'aa na Kuwaka? "Yeye alijibu, "Majina haya unayoweza kuona yaking` aa katika
kitabu cha uzima, ni watu wale
waliopo Duniani, kwa wakati huu hivi sasa
wanatubu dhambi zao na kutafuta
uwepo wa Mungu. Tazama, majina haya mengine ambayo ni vigumu
kuonekana na baadhi yao yanafutwa
kama ilivyo tayari kwa wengine wengi, ni watu wale duniani ambao
wamegeuka mbali na njia za Mungu.
Inakupasa ufanye jambo, fanya jambo! " Kwa mara nyingine tena, akaweka
mkono wake juu ya kitabu cha uzima na
kuniambia, "Enenda ukawambie wanadamu kuwa kama majina yao
hayakuandikwa katika kitabu hiki,
hawawezi kuingia katika Ufalme wa Baba yangu wa Mbinguni, hawawezi
kuingia katika Ufalme wa Mbinguni .
"Mimi nikajibu, "Sawa, nami nitafanya hivyo." Imeandikwa katika
Ufunuo 20:15 "kama jina la mtu yeyote halikuonekana katika kitabu cha uzima, alitupwa katika ziwa la moto." Tulitoka nje na kurudi kwa Yesu,
alisema, "Ni wakati wa wewe kurudi Duniani." Je, unafikiri jina lako limeandikwa katika
kitabu cha uzima? Kama hudhanii hivyo,
nenda na umtafute Mungu. Kama umemgeuka Mungu,
patana naye, kwa sababu yeye yuko
tayari kukusamehe, bila kujali umefanya nini. Kumbuka, alikuja kuokoa
wenye dhambi; Yeye alikuja kusamehe
dhambi za wanadamu wote duniani. Wewe fungua moyo wako na
umsihi akusamehe. Yeye yuko tayari
kutusafisha na udhalimu wote, kama inavyosemwa katika 1 Yohana 1: 9 'Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni
mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha
na udhalimu wote'" Nilipokua nikirudi Duniani, niliona mwili
wangu umelala pale. Ilikuwa ni asubuhi na mapema, karibu
saa 01:00 asubuhi. Katika nyumba yangu, niliweza kuona familia
yangu na baadhi ya washirika wa kanisa. Bwana akasema,
"Binti, ingia kwenye mwili wako, ingia kwenye mwili wako,
fanya hivyo sasa", "Sawa Bwana," nilijibu. "Kumbuka hili, utakuwa na mafunuo
mengi yanayotoka kwangu, na hivi karibuni utakuwa na
ufunuo wa tatu kuhusu nini kinatokea ndani ya watu wangu.
Kumbuka tu mimi nipo pamoja nawe." Ghafla niliona mwanga na Malaika walianza kuimba. Baada ya masaa mengi,
hatimaye niliweza kufungua macho yangu. Ilinichukua muda wa siku
nyingi kupona kabisa. Mimi nataka ujue kwamba kila kitu
ulichosikia kwenye video hii sio hadithi
ya kufikirika, Bwana aliniruhusu nipate uzoefu huu. Nataka ujue kama
unahitaji Mungu akusamehe, basi fumba
macho yako na weka mkono wako wa kulia juu ya moyo wako na
uombe, sema kwake, Page 11 11 "Bwana Yesu, Ninatubu dhambi zangu
zote, Ninatubu kwa sababu mimi
nimefanya dhambi kinyume chako, Nakusihi wewe Bwana unisamehe
dhambi zangu na unisafishe kwa damu yako ya thamani, Nakusihi
uandike jina langu katika kitabu cha uzima. Nipige muhuri kwa Roho
wako Mtakatifu wako, Ingia na ukae katika maisha yangu na
unitakase na uovu wote. Nakataa tamaa za mwili wangu. Nakana maisha
yangu ya zamani, na yote yale ambayo hayakupendezi wewe,
Natangaza leo, kwamba minyororo yote iliyonifunga kwamba
ifunguke, Niko huru, kwa sababu umeniweka Huru. Kwa jina la
Yesu, Amen "" Amani ya Mungu iwe ndani ya mioyo
yetu, na ukumbuke kwamba ni Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu
pekee ndiye ambaye anatushudia hatia ya dhambi zetu.
Mungu awabariki. Angelica Zambrano Mora ---------------------------------------------- Kama unataka kuwa sehemu ya huduma
hii unaweza wasiliana nasi kwa barua
pepe zifuatazo : esdios@hotmail.com palabraderevelaciondivina@hotmail.com (Kama inawezekana, tumia Kihispania) ** Toleo hili ni Minimally Abridged,
Polished na Illustrated. Video ya awali katika lugha ya
Kihispania . Ndugu aliyefasiri ufunuo wa 2 kuhusu
mbinguni na kuzimu wa Angelica
Zambarano ni Peter Kahale ni kijana aliyeokoka na anampenda Yesu na
mwenye shauku ya kuhubiri injili ya
Yesu Kristo. Simu ya Mkononi: +255-755-255043,
+255-653-610460. Barua Pepe: kahalepeter@gmail.com

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni