Wafilipi 2:10-11
  • UBATIZO WA MAJI YA KUCHEMSHA AU YA MOTO UNAMAANISHA NINI?

    Welcome to Prophet Hebron blog

    Yesu ni bwana na mwokozi wa mataifa yote

    UBATIZO WA MAJI YA KUCHEMSHA AU YA MOTO UNAMAANISHA NINI?

    Katika ubatizo ambao nimesema ni ubatizo wa maji ya moto au ya kuchemsha, huu ni ubatizo ambao ni wa kisima ambao pia ni chukizo mbele za MUNGU kabisa na ni ubatizo ambao katika nchi za Ulaya wanautumia huwa  wanayachemsha maji yanapata moto kama vile ya kuoga kisha watu wanaingizwa katika kisima wanabatizwa kinyume na biblia na mpango wa MUNGU.

    Soma biblia yote hakuna ubatizo wa kuchemsha maji, huku ndiko kutekwa na shetani tena zaidi, sasa tendo hili linapofanyika katika kuchemsha maji kinachofanyika hapo katika ulimwengu wa roho unalaaniwa na MUNGU na shetani pia na zaidi unakuwa umepatanishwa na moto wa jehanamu ambao baadaye baada ya hukumu watachomwa na shetani, malaika zake na wanadamu waliomfuata yeye na kwenda kinyume na MUNGU, na mtu unapobatizwa na maji moto kile ni kiapo unachokuwa umekiingia cha kupatanishwa na moto wa jehanamu, nataka muelewe mkatubu mkabatizwe upya sababu haujabatizwa bali mmepotea na MUNGU anawapenda, amenituma mimi Hebron niwaeleze habari hizi njema za ukweli na zitawaweka huru na siku moja mtafurahi na YESU mbinguni.

    Shetani yeye alimkosea MUNGU peke yake lakini hakutaka amkosee mwenyewe tokea mbinguni akiwadanganya thelusi moja ya malaika mbinguni wakamtii yeye na akatupwa nao kuzimu na hata sasa 98% ya watu wote katika ulimwengu huu ameiteka ili hao watu wakiwemo na wakristo baadhi yao siku ya mwisho watahukumiwa pamoja na thelusi moja ya malaika walioasi mbinguni na wanadamu wa sasa na watumishi wa uongo.

    Tubu: BWANA YESU naomba unisamehe, uniondolee hili agano la moto wa jehanamu wa ubatizo wa maji ya kuchemsha. Uniongoze YESU. Amen.

    NABII HEBRON KISAMO.

    Prophet Hebron at 9:58 AM

    Share

     

    Home

    View web version

    About Me

    Prophet Hebron

    View my complete profile

    Powered by Blogger.

    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate