Wafilipi 2:10-11
  • DAMU YA YESU NI NINI?


    JE DAMU YA YESU INATENGENEZWA NA POMBE?

    JE DAMU YA YESU INATENGENEZWA NA CHEMICALS?

    KWA NINI DIVAI INAITWA DAMU YA YESU?

    SASA KWA NINI BAADHI YA MAKANISA YANAVITUMIA NAKUVIITA NDIYO DAMU YA YESU? Wamepotea!

    BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE, katika somo hili nitaelezea ukweli na watu waujue kweli kuhusu damu ya YESU ni nini sababu ulimwengu umepotoshwa na shetani kwa kiasi kikubwa hata imefikia kuita kilevi ndiyo damu ya YESU na hata watu kanisani wanashiriki pombe wakielezwa ndiyo damu ya YESU matokeo yake ni pombe wanakunywa na wala hakuna kutakaswa zaidi yake unakuwa mjinga zaidi. Soma Mithali 20:1, Isaya 28:2, 1 Korintho 6:9-10 inaelezea walevi hawataurithi uflame wa MUNGU. Shetani aliona watu hawapendi pombe wanamkimbilia YESU sasa atawapataje njia aliyoifanya ni kuwashirikisha divai (pombe) ili siku ile ya mwisho awashtakie kupitia (1 Korintho 6:9-10).

    Katika neno la MUNGU anasema Ole wake ampaye mtu kileo, sasa cha ajabu kanisa eti linampa mtu kilevi, je ni YESU kweli yupo hapo kumpinga BABA yake? Jibu siyo. Na wengine wanasema YESU alitengeneza divai pombe. Nataka uelewe YESU hakutengeneza pombe, divai ni lazima ichache na ilale kama vile mtu anayetengeneza pombe za kienyeji na za viwandani. YESU alikuta wameishiwa, yeye akasema jazeni maji yale mabalasi na kisha akaamuru yawe divai muda huo huo na hata watu walipoionja wakasema mbona hii ni nzuri kuliko iliyoisha yaani haina uchachu. Ile YESU aliyoitengeneza ilikuwa kama juice fresh. Hivyo muelewe ni dhambi kumsingizia BWANA WETU YESU kuwa alitengeneza pombe.

    Jambo lingine nataka uelewe  ujue divai ni haramu, unapotumia akili zinavurugika, hata YESU aliposulubiwa pale msalabani askari alichukua divai (pombe) akachanganya na manemane akataka kumlambisha YESU lakini YESU alikataa sababu alitaka asiwe mjinga awe na akili timamu wakati akipambana na shetani muda ule, na pili shetani alitaka YESU anywe ili YESU awe anamkosea MUNGU lakini alishinda. Sasa YESU mwenyewe alikataa sasa iweje leo ndiyo iwe damu yake? Tunajua damu ya YESU ni takatifu, sasa hivi vileo ndio utakatifu? Huu ni uchafu, watu wanakunywa wengine wakijua na wengine hawajui, utubu leo na usinywe tena katika jina la YESU wa kweli.

    Na cha ajabu hata wale wanafunzi wa YESU baada ya YESU kupaa walilazimishwa wanywe divai lakini walikataa sababu divai hiyo ilikuwa ni kileo. YESU alipokuwa na wanafunzi wake yeye alichukua juice ya zabibu fresh. Sasa leo watu wanatengeneza wine halafu wanadangaya watu ndiyo damu ya YESU.

    A.    JE DAMU YA YESU INATENGENEZWA NA POMBE?

    Damu ya YESU haina kilevi chochote na kama hivyo damu ingekuwa na kilevi basi ingekuwa ni MUNGU amewafanya watoto wake wawe wajinga na awazuie wasiende mbinguni. Umekunywa kitu chenye kilevi ukaelezwa ndiyo damu ya YESU, nakueleza umepotezwa na unapokea afya ya kwenda kuzimu pasipo wewe kujua wala kupenda. Nataka uelewe zaidi sasa hivi shetani anayajaza mafundisho potofu na watu wanayapokea sehemu kubwa hawataki kuacha pombe sababu kubwa inaitwa ni damu ya YESU.

    Jamani watu mwogopeni MUNGU, YESU, ROHO MTAKATIFU, mnawakana peupe na kuyapokea ya shetani na mpinga kristo, angalia safari yako isiishie jehanamu, rejea sasa. Na isitoshe, yapo makanisa hata ya kipentekoste baadhi wanashiriki wine baada ya ibada, hapo hakuna MUNGU ni bar ya shetani na roho wa shetani, unazubaishwa kiroho na kimwili ili YESU akija asiwanyakue kwenda mbinguni, na nyie mkifikiria ni wateule tayari kumbe ni wakataliwa mbele za MUNGU.

    Damu ya YESU haimfanyi mtu apoteze fahamu zake, ajikojolee, atukane, agombane, mgomvi na ufisadi. Mmfunguke fahamu na kuyapima maneno haya. Divai ukipima kwenye vipimo utaona kiasi fulani cha Alcohol, sasa unakunywa alcohol, hivyo hiyo siyo damu ya YESU bali hiyo ni pombe na kilevi.

    B.    JE DAMU YA YESU INATENGENEZWA NA CHEMICALS?

    Ninaposema haikutosha kanisa likazidi kupotoshwa na shetani, wanadamu wakatengeneza juice za chemicals zenye rangi ya nyeusi na zambarau, wakaweka na sukari zikauzwa madukani. Hata mimi Hebron pasipokujua kabla sijafundishwa na YESU nilikuta katika sehemu mbali mbali nilizokuwa nikiabudu na niliuita damu ya YESU na kuona ni kitu kitakatifu kumbe ni chemicals, kazi ya mikono ya wanadamu na zingine zikachanganywa na chumvi. Hizo pia sizo damu ya YESU kabisa, kama kutumia wewe tumia tu kwa afya yako. Shetani ananyanyua mashtaka anawashtaki, yaani yeye mwenyewe anawatengenezea mapokeo na kisha unayapokea anakushtaki kwa MUNGU na zaidi unapotea. Hivi hata kibinadamu je kuna kiwanda kinachoweza kutengeneza damu ya mtu? Jibu, hakipo sasa iweje hiyo?

    Ndiyo sababu mapepo yanaishi ndani ya watu wanaukunywa hiyo divai, kama ingekuwa kweli ni damu ya YESU kwa wingi watu walivyoitumia hakuna mtu aliyekunywa angeteswa na mapepo au mateso, ikupe picha halisi. Ukiangalia ukiomba ukitamka kwa kinywa chako nakumwagia damu ya YESU katika ulimwengu wa roho mapepo, shetani wanaogopa, wanakimbia ila utashangaa mtu ana pepo anapewa hiyo anakunywa na hayatoki, hii ni picha halisi siyo damu ya YESU ya kweli ni ya uongo na madhara yake, unapoitumia unazidi kupokea uzima wa kuzimu kutoka kwa yesu wa uongo ambaye ndiye mpinga kristo. Inachanganyikana na damu yako katika mwili na ulimwengu wa roho na hata ukasema shindwa kwa damu ya YESU inakuwa ni kazi bure sababu kimwili unayo damu yako imechanganyikana na damu feki ya yesu wa uongo na katika ulimwengu wa roho pia, damu ya YESU wa kweli haina mlango wa kukufikia sababu tayari unakuwa ulikubali mwenyewe kimwili kwa kujua au kutokujua na hivyo hata ile damu ya YESU ya kweli haiwezi kukufunika sababu mlango tayari umeshapokea hiyo ya uongo hivyo uikatae, utubu, uanze upya  ili damu ya YESU ifanye kazi katika ulimwengu wa roho na mwili.

    Mpango huu uliletwa kama mapokeo ili kuhakikisha kanisa linatekwa na kanisa kwa njia hiyo ndivyo watu wanajifungia mateso kwa kujua au kutokujua. Na pia ni hatari sana kwa sababu baadhi ya watumishi ni wachawi na hutumia njia hiyo kuinenea mambo ya kukufunga usifunguke uujue ukweli na uzidi kutii hata ujinga wa uongo au kukupumbaza. Na ndiyo sababu utaona mahali pengi wanasema damu ya YESU, namwaga damu ya YESU lakini hakuna mabadiliko ni sababu ni feki. Inawapumbaza watu ili kupona usishiriki, mtegemee YESU nyakati hizi ni mabaya sana. YESU anajiandaa kuja kulinyakua kanisa, sasa angalia damu yake iliyomwagika pale msalabani isizuiliwe kunena msamaha juu yako na neema juu yako sababu utakuwa unashawishiwa  na pombe (divai). YESU alikataa pale msalabani sababu alijua ni chukizo na ni dhambi angepata dhambi kama angeinywa shetani akapate mlango wa kumshtaki ila alishinda. Na wewe ushinde sasa. Tubu BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu uniokoe. Uliandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Natapika damu feki iliyoitwa divai (pombe) na hizo za chemicals katika mwili na katika roho, Amen.

    Ubarikiwe. Zaidi fuatilia katika YouTube za prophet Hebron Wilson na blog, karibu sana pia katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE.

    NABII HEBRON.


    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate