Wafilipi 2:10-11
  • HAYA NDIYO MADHARA YA KUABUDU PICHA ZA WATU WALIOACT SINEMA ZA YESU!

    Welcome to Prophet Hebron blog

     

    HAYA NDIYO MADHARA YA KUABUDU PICHA ZA WATU WALIOACT SINEMA ZA YESU!

    BWANA YESU ASIFIWE watu wote wa mataifa yote, YESU anawapenda na pia MUNGU anawapenda na ROHO MTAKATIFU anawapenda vile vile na leo amenituma niwaletee habari njema za uponyaji wa roho na mwili ili miili isike ikaangamia na roho kuhukumiwa siku ile ya hukumu. Napenda kuwashukuru watu wote ambao waliamua kufundisha kuhusu maisha ya YESU kwa njia ya sinema, walifanya vizuri wameelimisha watu wengi zaidi. Ila katika jamii na dini na imani wamefanya kosa kubwa sana na MUNGU amelichukia sana jambo hili na ninasema ukweli kutoka moyoni wangu bila unafiki kabisa sababu msema kweli ni mpenzi wa MUNGU na msema uongo ni mpenzi wa shetani.

    Ukisoma kitabu cha Kutoka 20:4-6; 4usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.5usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa  mimi BWANA, MUNGU wako, ni MUNGU mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao. MUNGU anasema usivisujudie wala kuvitumikia mimi ni MUNGU mwenye wivu wote ambao watakao vitumikia  ntawapatiliza wana maovu yao na kizazi chao. Point hapa ni utaona amri ya MUNGU amekataa kitu chochote kisisujudiwe kikafanywa.

    Sasa shetani amewateka watu fahamu zao na kuwafanya watu walaaniwe na MUNGU na kutengwa na MUNGU kwa njia hizi za picha za mafundisho ya YESU, cha ajabu ujue fahamu zimetekwa na shetani watu wameacha kumwangalia YESU mbinguni wameanza kuangalia zile picha za walioact sinema hizo na kuwafanya ndiyo YESU katika ulimwengu huu na cha ajabu hata katika fikra za wanadamu ukiwauliza mnaijua sura ya YESU watakuambia ndiyo na kumbe ni sura ya mtu ndiyo ipo kwenye fahamu, katika eneo hilo shetani amewateka wengi sana ikiwemo mimi Hebron hapo mwanzoni nilijua ndiyo hiyo hata nilipokutana na YESU 2009, Serengeti national park ilikuwa ni vigumu kumkubali YESU kwa jinsi sura yake nilivyoijua mpaka aliponielimisha kuhusu ukweli huu na sura ya picha ya YESU haupo katika ulimwengu huu kabisa, hivyo nawaeleza watu wote wa mataifa unapozipamba katika nyumba hizo picha au katika kanisa tayari unakuwa umemkosea MUNGU unampa mwanadamu nafasi ya kumwabudu ukiwa unajua au haujui na matokea yake unakuwa umevunja amri moja wapo ya MUNGU.

    Ikiwa ni kanisa linapamba hizo picha katika nyumba hiyo au picha za wanafunzi wa YESU   hata Petro tayari kanisa linakuwa limevunja amri ya kwanza na ya pili na ya tatu. Sasa kama kanisa lenyewe limeshamvunjia MUNGU amri zake je kanisa hilo litakuwa na uhusiano na MUNGU wa kweli tena? Jibu hapana litakuwa na uhusiano na miungu hata waumini ndipo wanapopelekwa katika ulimwengu wa roho. Huu ni wakati wa watu kutubu na kumrejea YESU wa kweli katika hizo picha unapoziabudu zitafanya usiende mbinguni, wengine wanazilalia, wanazitolea sadaka wakifananisha na YESU. Nawaeleza yeye ni mwana wa pekee hafananishwi na chochote kile na unapozitolea sadaka na ibada haina tofauti na picha yako, rafiki yako au mtu yeyote? Je ulimwengu huku ndiko kwenda mbinguni? Jibu ni kupelekwa jehanamu, sasa usishiriki na hizo picha ile hasira ya MUNGU isiwe juu yako, sababu nawaeleza nilivyokuwa naongea na YESU jambo hili linamuumiza sana na shetanni anafurahia sana watu wanavyoacha kuweka fahamu zao katika roho ili wamwone YESU lakini inashindikana sababu katika nafsi zao tayari wanawaweka wale walioact sinema hizo wakiwa na nia njema ya kuelimisha jamii.

    Na hata kama mtaupata ujumbe huu najua mnampenda YESU sasa mwatangazie ulimwengu waache kuwaabudu nyie sababu nyie siyo MUNGU wala YESU ili mataifa yapone na MUNGU atawabariki sana kwa sababu mtakuwa mmeshiriki kumwaibisha shetani na mafundisho yake ya uongo na watumishi wake wanaowadanganya watu kuwa ni sura ya YESU wakati ni uongo mkubwa na jamii mmeipokea na kuamini hivyo katika ulimwengu wote 95% watu wote wanajua Brian ni YESU na Robert hivyo hana watu wamepotea na huu ndio ukweli na kwa jinsi hii inaonyesha wapo chini ya miungu hawa watu wote pasipo kujua sababu ya mafundisho ya uongo.

    Hivyo basi ili upone na usimuuzi MUNGU usiabudu tena hizo picha, zitoe ndani mwako hata katika pete unaufikiri ni sura ya YESU hapana, watu wanampenda YESU na ndiyo sababu wakisikia ni picha ya YESU wanaamini ila wangefundishwa siyo hawa wameact tu hili tatizo lisingekuwepo, na mimi amenituma kwa mataifa yote nieleze ukweli ili watu wapone. Msiabudu picha za sinema, hakuna sura za YESU, wala za mitume wa YESU, wala ya malaika,wala ya Maria na wengineo. Hizo ni acting tu. Na zaidi hata Mama Maria yeye siyo MUNGU, kina Petro na wale mitume, hata malaika wote hawastaili kuabudiwa na hawaabudu mwezi, wala jua, wala nyota, wala picha ya kiumbe chochote wao wanastahili kumwabudu MUNGU pia na ndivyo wanavyofanya mbinguni niliwaona wanamsujudu MUNGU mbinguni ila cha ajabu huku ulimwenguni watu wanawasujudu hawa watu, hawa ni kama wewe tu ila tofauti ni kuwa wao tayari wameishinda ulimwengu na sasa wapo mbinguni na wewe jitahidi utafika. Acha kuwaabudu, kuwasujudia ni dhambi unakuwa unasujudia miungu na mwisho utaenda huko kwa miungu.

    NABII HEBRON.

    Prophet Hebron at 11:37 AM

    Share

     

    Home

    View web version

    About Me

    Prophet Hebron

    View my complete profile

    Powered by Blogger.

    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate