Welcome to Prophet Hebron blog
NINI MAANA YA KUBATIZWA KWENYE DRUM AU TANK?
Ubatizo huu hauna tofauti sana na ubatizo wa kisima kama nilivyoelezea. Yale madhara yote yaliyopo katika ubatizo wa kisima na hapa yapo vile vile. Soma katika blog yangu nimeelezea maana ya kubatizwa katika kisima, huu ni ubatizo wa shetani pia ila umefanyika katika drum au tank na mtu ajione yeye anabatizwa katika maji mengi lakini ni kinyume pia. Hapa tofauti yake ule wa kisima unakuwa umejiingiza katika jeneza kuzimu ila huu wa drum au tank unakuwa umebatizwa na ukapatanishwa na gereza alilofungiwa joka kuu ambaye ndiye baba yake shetani, hivyo unakuwa umefungiwa katika kiwango cha juu zaidi katika ufalme wa shetani na usitoke utakuwa unaanguka tu katika huo mdwara maisha yako yote na siku ya mwisho utabakia na joka kuu kama mtoto wake na yeye baba yako hivyo uelewe jinsi mambo yalivyo haribika kupitia manabii wa uongo na mapokeo ya shetani. Wewe tafuta katika biblia hajabatizwa mtu kwenye drum au tank ni mtoni tu, neno limebadilishwa tayari na kama limebadilishwa basi haupo na MUNGU sasa rejea.
2010 aliponiita YESU aliniambia Hebron nataka nikueleze na nikufundishe, mimi nimekuchagua na nilijua ikifika wakati nitakutumia na sasa peleka injili yangu kwa mataifa yote. Nimesalitiwa na baadhi niliyowaita wanitumikie sasa wanaleta injili za kishetani na watu hawajui ila sasa watajua ukweli na watapona na hata sasa mnapona na kutoka kwenye mikono ya shetani. Hicho ni kiapo cha ubatizo kati yako wewe na lile joka lililotupwa mbinguni liwe baba yako, sasa kataa maana neema ipo sasa sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote ikiwemo kubatizwa katika drum naomba unitoe kwa joka kuu. Uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele, shetani sikutaki tena, mpinga kristo sikutaki tena katika jina la YESU. Amen.
Mrejeeni YESU na kubatizwa ili awe BABA yako na akunyakue uende mbinguni siku moja.
NABII HEBRON.
About Me
Prophet HebronView my complete profile
Powered by Blogger.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni