Katika safari yake ya pili, Angelica
alionyeshwa hukumu dhidi ya Wakristo
wanaomuibia Mungu katika zaka
na sadaka, hukumu dhidi ya watawa
wanaofanya ibada ya sanamu na watoto walioasi, kitabu cha uzima cha
Mwanakondoo, na mengine zaidi. *"Waambie
watu wangu kwamba kuja kwangu ku
karibu, Nitakuja kwa watu*
*wangu watakatifu, waambie watu wangu
kwamba ni watakatifu tu ndio watakaoniona mimi."*
*Januari 4, 2010, 05:50 usiku, Empalme,
Ecuador. Bwana alimchukua Angelica
kwa mara ya 2.*
*Nakala hii imechukuliwa kutoka katika video
ya ushuhuda ya kihispania.* *Angelica: *Saa 6:00 usiku wa manane, baadhi
ya ndugu kutoka kanisani
walifika katika nyumba yangu, basi vyombo
vya habari viliwasili, na kila
kitu kilichukuliwa katika kumbukumbu.
Nilikuwa juu ya kitanda, ghafla, nikaona malaika wawili. Kama vile
ilivyokuwa mwanzo, walinichukua mikono
yangu na kusema, *"Inuka, kwa *
*sababu Mfalme wa wafalme*
*na Bwana wa mabwana *
*anakusubiri." *Nilipoinuka, niliona mwili wangu umelala hapo, na
watu wengine waliokuwa katika chumba hicho.
Nilianza kutembea.
Nilinyoosha mikono yangu kwa malaika na
tulianza kuelekea juu.
Tulikuwa tunakwenda haraka sana, na katika sekunde chache
tulifika mbele ya Bwana. Nikasikia Malaika
wakiabudu,
"Haleluya ... Mtakatifu, Mtakatifu." Nilikuwa na
furaha.
Katika Ufalme wa Mungu kulikuwa na bustani nzuri sana. Niliona Bwana
akinikaribia. Akasema, *"Binti,*
*nimekuwa nikisubiri, kwa sababu nina mambo
mengi ya kukuambia", *"Bwana,
mimi hapa, nataka kukaa na
------------------------------ *Page 2*
2
wewe. Sitaki kurudi Duniani, tafadhali napenda
kukaa na wewe. "Bwana
akajibu, "Mtoto wangu, una mambo
mengi ya kufanya. Una kazi, imekupasa ufanye kazi yangu. Nitakuonyesha kitu
kwa ajili ya maisha yako, kitu
kwa ajili ya watu wangu, na kitu maalum kwa
ajili ya watu, kwa sababu
nataka uokoe binadamu na sitaki mtu
yeyote apotee. " Kisha, niliona malaika wawili, Mikaeli na
Gabrieli
wamebeba vitabu vikubwa; vitabu hivi vilikuwa
vizuri
sana na vinang `aa.Nilipokuwa nikiangalia
vitabu hivyo, niliuliza, "Ni nini hii?" na Yesu akasema, *"Je,
unataka*
*kujua ni nini kilicho katika vitabu hivi?"
*Nikajibu,
"*Ndiyo Bwana*." Akasema, *"Mikaeli, fungua."
*Malaika Mikaeli alipoanza kufungua kitabu, niliweza
kuona maandishi ya dhahabu,
kama namba, lakini sikuweza
kuelewa. Niliwaza, *"hiki ni nini?", *Na Malaika
Mikaeli akajibu, *"Maandishi
yote haya na namba unazoona * *zimeandikwa hapa ni wale watu duniani
ambao wamemkubali Bwana wetu kama
Mwokozi wao wa pekee, *
*kwa mafunuo yale ambayo alikufunulia
ulipokuwa pamoja naye . *"Nilipatwa
na msisimko na nikamuuliza, *"Ni watu wangapi wamo humo?" *Alinipa jumla
ya idadi ya roho katika maelfu.
Moyo ulivunjika na nikaanza kulia, nikisema,
"Bwana hizo ni roho/nafsi
nyingi ambazo ni waongofu",
Akaitikia, *"Unaweza kuona, malaika huyu, Malaika Gabrieli ana jumla ya
idadi ya watu wale ambao*
*walikuwa wamejitenga mbali na njia zangu na
kuwa sasa wamekuja kwangu,
wamekuja kwangu*
*mwanangu. *"Nilitazama katika idadi ile na niliona ni kiasi kikubwa.
Nikasema, *"Bwana hii ina maana taji*
*yangu imejaa lulu na kwamba sasa utaniacha
hapa katika Ufalme wako?" *Bwana
alijibu, *"Hapana*
*mwanangu , muda wako wa kuja hapa bado, imekupasa urudi Duniani. Je,
ungependa kuona taji yako?"*
Nilijibu kwa msisimko, "Ndiyo Bwana,
ningependa kuona taji
yangu," Alisema, "Malaika Gabrieli, mletee taji
yake." Niliona Gabrieli amebeba tray kubwa sana, yenye taji
nzuri, lakini yenye
lulu chache juu yake. Nilimuuliza, "Bwana, taji
hii ni ya nani?
Akanijibu," Hiyo ni taji yako mwanangu.
"Nikamuuliza,*" Lakini* *Bwana, kwa nini taji yangu haijajaa lulu, kama
nafsi/roho nyingi*
*zimekuja kwako Bwana? *"Naye akanijibu,
*"Binti, bado njia*
*ndefu inakusubiri,ni roho/nafsi 3,500 tu
zimekuja mbele yangu, lakini imekupasa kwenda na kuhubiri*
*neno langu kwa sababu kuna roho nyingi
bado ambazo zinatakiwa kuja
kwangu." *Lakini Bwana, kwa nini
nisibaki hapa tu? Yeye aliniambia, *"Binti, kwa
sababu taji ya uzima inapaswa kujaa lulu. *Nikasema, "Sawa
Bwana, *Nitatekeleza kazi yako*." Kisha
akasema, *"Nina jambo la
kukuonyesha Mwanangu."*
Bwana alinichukua, na kwa haraka tulishuka
kutoka mbinguni na kuingia ndani ya tundu/tanuru la kuzimu,
kama ilivyokuwa mara ya kwanza wakati
nafunuliwa kuhusu kuzimu. Nilisema, *"Oh!
Bwana, nini*
*kinachotokea?" Yesu alisema, "Ninajambo la
kukuonyesha kuzimu," "Lakini Bwana Sitaki kuwa hapa.*
*Bwana, kumbuka uzoefu/ufunuo wetu wa
kwanza, tayari ulinionyesha mambo
mengi", *Alisema, *"Ndiyo *
*mwanangu, lakini sasa mambo mbalimbali
tofauti, nitakuonyesha. "* Tulikwenda chini kati ya miali ya moto zaidi, na
nikaanza kulia. Haikuwa
rahisi kuwa pale. Nilisema, *"Bwana,*
------------------------------
*Page 3*
3 *nataka kutoka nje ya hapa, tafadhali nisaidie,
nisaidie." Nilisikia
mamilioni ya watu, baadhi ya watu*
*walikuwa wakisema, "Oh Bwana, nihurumie,
nisaidie tafadhali, Bwana,*
*nipe nafasi nyingine."* Miongoni mwa wale watu, nilisikia mtu mmoja
akisema, *"Ninaomba*
*msamaha wako sasa Bwana, kwa sababu
nimekuibia, nisamehe kwa kuiba,*
*Nilikuibia Bwana na sitaki kufanya hivyo tena."
*Mimi niliuliza, *"Bwana, * *ni nani na kwa nini yeye anasema alikuibia?"
*"Mwanangu
*nitakuonyesha yeye ni nani*.*" *Tuliingia
kwenye selo yake na nikaona mtu
aliyeharibiwa. Miali ya moto ikafunguka na
nikamuona alikuwa akiungua. Watu wote walio kuzimu wana nembo/kibao
juu ya vifua vyao, na 666
kwenye paji za nyuso zao. Mtu huyu
aliunyosha mkono wake na kusema,
*"Bwana nisamehe*." Mimi nilimuuliza, "*Mbona
uko hapa,na kwa nini* *unamuomba msamaha Bwana, kwa nini?
Unasema umemuibia Mungu*,
*lakini hakuna mtu anaweza kumuibia Mungu?
Hii haiwezekani, kwa nini useme
umemuibia Yeye? *"Yeye
akanijibu, *"Mimi nitakuambia historia yangu ... Nilikuwa kiongozi wa
Kikristo, kwa miaka 20 nilimjua Kristo,*
*lakini katika kipindi cha miaka 20 Nilisema:
fedha zote kutoka katika
mafungu ya kumi na sadaka zangu *
*zilikuwa zinakwenda kuwanufaisha wachungaji, lakini hivi sasa najuta kwa
sababu nimejua kwamba*
*hazikuwa kwa ajili yao, zilikuwa ni kwa ajili ya
Bwana, na ndio maana
nasema nimemuibia Mungu ... Wakati*
*huu kuna watu wengi sana duniani wanaomuibia Bwana kama mimi. Wakati
utakaporudi duniani, waambie*
*wale watu wote ambao hawataki kutoa zaka
zao na sadaka, waimuibie Bwana,
vinginevyo, wao nao wataishia*
*Kuzimu, na hakuna mwizi atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni. Nilijua
Neno takatifu, sasa ninajutia na*
*kutambua kuwa nilimuibia Bwana (Malaki 3: 8)
.. Waambie watu wakati
wanapomtolea Mungu, basi*
*wamtolee Bwana kwa upendo wa kweli ". (2 Kor 9: 7) ". *Mtu huyu aliendelea
kusihi , *"Bwana nisamehe", *na
Bwana akamjibu, *Umechelewa sana, hakuna
tena nafasi kwa ajili yako"*
Nilimuuliza mtu huyu, *"Lakini kwa nini wewe
ulimuibia Mungu, kwa nini*? Wewe ulijua vizuri sana kuwa
hatuwezi kumuibia Mungu zaka na sadaka."
Yeye akajibu, *"Ndiyo, mimi
nilijua vizuri sana, lakini kamwe*
*sikufuata, sikufuata kwa sababu nilikuwa mtu
wa kiburi sana."* Kamwe usimuibie Bwana, toa zaka na sadaka
kwa Mungu kwa sababu kile
tunachotoa kwa Bwana Duniani si
kwa ajili ya watu. Tunapotoa kwa Mungu kwa
moyo wetu wote, ni kwa ajili ya
Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.
Biblia inasema kwamba Bwana anatujaribu,
imeandikwa vyema katika Malaki
3:8-10
<http://www.biblegateway.com/passage/? search=Malachi+3%
3A8-10&version=NIV&interface=print >*Je!
Mwanadamu *
*atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi.
Lakini ninyi mwasema,
Tumekuibia kwa namna gani?*
*Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia
mimi, naam, taifa hili lote.*
*Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula
katika nyumba yangu,
mkanijaribu kwa njia hiyo, asema *
*Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na
kuwamwagieni baraka, hata*
*isiwepo nafasi ya kutosha, au la. *Kama
unataka Mungu abariki maisha yako
na familia kwa ukuu sana, Basi
usimuibie Mungu. Ni wakati wa kumbariki Mungu, ili abariki maisha yetu.
Bwana akasema, *"Nitakuonyesha kitu tofauti."
*Baada ya kuondoka mahali
hapo, Bwana alinikumbusha kitu
ambacho alinionyesha kabla ya uzoefu wangu
wa pili, karibia Novemba. Wakati huo, nilionyeshwa Selo kule
------------------------------
*Page 4*
4
kuzimu, na Neno maalum.
*Neno 'ARVIERD' alionyeshwa Angelica. Utafiti unaonyesha kuwa ni Kiitalia
cha kale, au Kilatini. Katika *
*utafiti tuligundua ukurasa wa 400 wa
maandiko ya kale kuhusu neno hili,
linalozungumzia Kuzimu halisi.*
Sikujua maana ya hilo neno, lakini nilielewa kwamba lilimaanisha kitu
fulani kuhusu *Dini*
.
Yesu alinichukua na kunirudisha sehemu ile ile,
ili
kuona selo hizo tena. Tulipoingia, niliona maelfu ya
watu. Kulikuwa na wanawake wawili wamevaa
nguo nyeusi. Nilimuuliza Yesu "*Ni nani hao?"*
Nilisikitika kuona mtawa, na katika mikono
yake
walikuwepo nyoka wakubwa, ambao walitengeneza
kitu kama msalaba na Rozari.
Nikasema, *"ni nini hii, kwa nini wako hapa?"
*Mmoja wao alizungumza kwa
sauti ya huzuni akisema, "
*Nilikuwa mtawa Duniani, lakini sasa niko mahali hapa." *Niliona jinsi
alivyoanza kuomba na nyoka alifinya
mikono yake. Katika mikono yake kulikuwa na
maelfu ya minyoo. Bwana
akasema, *"Angalia na sikiliza*
*maneno haya." *Alianza kulia, *"Oh Bwana! Siwezi kuvumiliana na hili tena,
nataka kutoka nje ya eneo hili,*
*sitaki kuwa hapa, tafadhali Bwana Niaidie,
nisaidie!"*
Kisha nikaona mwanamke mwingine, na
sehemu ya maisha yao nilionyeshwa katika aina ya fulani ya
televisheni/screen. Niliona watawa
jinsi ambavyo huwa kihualisia, na maisha yao
ya siri. Niliona jinsi watawa
hawa walivyo na mahusiano ya kingono na
mapadri, na jinsi ambavyo baadhi ya watawa hawa walikuwa pia
wasagaji. Niliona mengi zaidi, na sasa
walikuwa wakijutia na kutubu. Lakini kwa
bahati mbaya, kulikuwa hakuna
tena nafasi nyingine kwa wao kutubu;
walikuwa wamechelewa mno. Wale watawa wakasema, *"Nenda na ukawaambie
wale wote Duniani, wasije*
*mahali hapa, tafadhali nenda na uwaambie
wasije hapa."*
------------------------------
*Page 5* 5
Wakati mwingine watawa/masista na mapadri
husema
kwamba watamuomba Mungu ili aziondoe roho
zilizo
*Purgatory*. Lakini mimi nawaambia kweli, Uniamini au
usiniamini. Hakuna mahali panapojulikana
kama Purgatory.
Purgatory ilitungwa tu na wanadamu, ilitungwa
na mapapa.
Biblia inasema wazi wazi kwamba kuna Mbinguni na kuna
Kuzimu halisi. Yesu alinichukua mpaka
maeneo yote hayo
mawili, lakini kamwe sikuwahi kupelekwa
purgatory. Yeye
kwa uwazi aliniambia, *"Purgatory haipo, nenda na*
*uwaambie watu wafanye maamuzi yao wakati
bado wako*
*Duniani, kwa sababu wakati wakiwa na uzima,
kuna nafasi*
*ya kutubu."* Watu wengi wanasema, *"hebu tuombe, ili
ndugu zetu *
*waondoke purgatory." *acha hiyo! Kwa
sababu kama wao
walikufa bila Kristo kule Kuzimu KAMWE
hawatoki. Ni bahati mbaya lakini ni kweli, kuwa wako
Kuzimu.
Lakini kama walikufa pamoja na Kristo katika
mioyo yao,
basi wako uweponi mwa Baba yetu wa
Mbinguni. Moyo wangu uumaa kujua kwamba nafsi/roho nyingi
sana
zinadanganywa na shetani katika kuamini
purgatory.
Rafiki yangu ni wakati wa wewe kujua ukweli,
purgatory haipo, yaani ni haipo. Inakupasa kufanya
uamuzi sasa, ni
wapi na na nani ambaye ungependa kuishi
milele? Unaweza
kufanya uamuzi wako mwenyewe, kama ni
Ufalme wa Mbinguni na Yesu Kristo au Kuzimu na
shetani. Bwana
aliniagiza niseme moja kwa moja bila kupoza
ninapowaambia hili, iwe unaamini au
hauamini.Ninatii amri
ya Bwana kwa sababu siku moja wewe na
mimi tutasimama mbele
ya Mungu, na kushuhudia yote mema na
mabaya tuliyofanya hapa
Duniani. Kama hautatubu dhambi yako na
kuabudu kwako sanamu, utaishia kuzimu. Rejea kwa Kristo; Atakupa
uzima wa milele.
Sitaki kuwatisheni, lakini ni ukweli. Neno la
Bwana li wazi sana na
linasema kwamba hakuna mwizi atakayeingia
mbinguni. Bwana alinionyeshea kwamba ndani ya kila picha /
sanamu kuna pepo. Ndiyo
maana watu huja kwa bikira wa Guadalupe(
<http://en.wikipedia.org/wiki/Our_Lady_of_ Guadalupe >Virgin of Guadalupe
<http://en.wikipedia.org/wiki/Our_Lady_of_ Guadalupe >
<http://en.wikipedia.org/wiki/Our_Lady_of_ Guadalupe >)
, Bikira
wa Sinema, Sanamu ya Bikira Maria na bikira
wengine wengi 1 2 3 4.
Hata sanamu ya *'Mtoto Yesu'*. Tafadhali
niamini mimi, hizi sanamu zote zina pepo nyuma yake. Watu wengi wanadai
kuwa walikwenda kwa
Bikira wa Guadalupe au Mtoto Yesu na
kupokea uponyaji. Lakini
miongoni mwa kila moja ya picha/sanamu hizi
kuna pepo. Shetani anasikiliza na kwa nguvu zake za uongo,
------------------------------
*Page 6*
6
wakati mwingine anafanya ionekane kama
muujiza umetokea, ili uendelee kuamini na uendelee kumuabudu
yeye. Nisikilizeni, shetani anaenda kukulipa
wewe vibaya na atakupa mauti
ya milele. Hivyo acha kuabudu
picha umtafute Kristo, kwa sababu atakupa
maisha ya milele na uzima kwa wingi (Yohana 10:10).
Bwana alinionyesha watawa hao, nao walikuwa
wakilia, *"Nataka kutoka hapa,
najutia kuabudu sanamu, na *
*kufanya dhambi duniani, sasa siwezi
kuondoka mahali hapa." *Nilimuuliza mmoja wao, "Lakini wewe uliijua
kweli? Ulijua Neno la Mungu takatifu?" Yeye
alinijibu, *"Ndiyo, nilijua
Neno Takatifu, lakini kamwe sikutubu,*
*kamwe sikumtafuta Kristo. Kuna watawa
wengi walioamua kuwa hivyo kwa sababu nyingi. Mimi nilikuwa*
*muongofu/hivi kwa sababu ya uchungu
nilioupitia katika mauhusiano wa
kimapenzi. Kuna watawa wengi kwa*
*sababu ya kukatishwa tamaa katika mapenzi.
Katika kesi nyingi, wachumba wao waliwaacha katika harusi*
*madhabahuni, au marafiki zao wa kiume
waliwasaliti, watawa wengi kwa
bahati mbaya wapo katika kiapo*
*kwa sababu maisha yao yamejaa matatizo na
wito huu wanautumia kama sababu tu. Ukweli halisi ni kwamba*
*wao wanamtumikia shetani. "*
Neno takatifu la Bwana linasema katika 1
wakorintho 6:9-10
<http://www.biblegateway.com/passage/? search=1+Corinthians+6%
3A9-10&version=AMP >*"
Au*
*hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi
ufalme wa Mungu? *
*Msidanganyike; waasherati hawataurithi
ufalme wa Mungu, wala * *waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji,
wala walawiti, wala*
*wevi, wala watamanio, wala walevi, wala
watukanaji, wala*
*wanyang'anyi.watakaorithi ufalme wa
mbinguni.* Neno lake takatifu liko wazi, Ufunuo 21:8
<http://bible.cc/revelation/21-8.htm >" *Bali waoga, na*
*wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na
wazinzi, na wachawi, na*
*hao waabuduo sanamu, na waongo wote,
sehemu yao ni katika lile *
*ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.*
------------------------------
*Page 7*
7
Watu wote kule kuzimu hawana namna ya
kutoka, kwao wamechelewa sana. Lakini Ninyi ambao mko hai
katika dunia, bado mnaweza kupatanishwa na
Mungu. Usikose nafasi hii, labda
wewe hivi sasa unaangalia hii,
na inaweza kuwa nafasi yako ya mwisho
ambayo Mungu anakupa ili utubu. Epuka kuzimu, kwa sababu Kristo
ananyoosha mkono wake wa rehema kwako.
Tulipokuwa tunaondoka katika selo nilianza
kulia kwa sauti na nilikuwa
nikisema, *"Bwana nitoe nje ya hapa,*
*Bwana, mimi sitaki kuwa hapa*." Alinitoa nje na kusema, *"Nataka kuonyesha
zaidi ..." *Tulipokuwa
tukitembea, nikasikia mayowe ya msichana
mdogo, "*Nisaidie! Nisaidie*!" "*Wewe
ni nani? Kwa nini uko*
*hapa?" *Nilimuuliza. Msichana alijibu, *"mimi ni*
*kijana, nilikuwa nina miaka 15 tu wakati*
*nilipokufa, na kuja mahali hapa." *"*Lakini kwa
nini*
*uko hapa? Nini kilichokuleta wewe hapa?"*
Nilimuuliza. Akasema, *"Mimi nilifikiri nilikuwa* *na maisha mbele yangu, kwa sababu
nilikuwa*
*mdogo sana. Watu siku zote waliongea nami*
*kuhusu Kristo na wokovu, lakini nilisema
kwamba*
*Wakristo wa hizo injili walikuwa vichaa/wehu,* *wakati wote nililikataa Neno Takatifu. Sikutaka
*
*kumkubali Bwana. Kila wakati
walipozungumza*
*na mimi, niliwacheka na kuwadhihaki. Sasa
naona* *kwamba nilifanya makosa makubwa ya
maisha yangu. Niangalie wakati huu niko
mahali hapa ninaungua*
*katika moto. Nilikufa katika ajali ya gari na
sasa ninajutia sana.
Nimekuwa nikitafuta njia ya ktoka hapa mara* *nyingi, na mara ninapoiona njia hiyo siwezi
kutoka, kwani mapepo
yanayonitesa yanasema, 'huwezi*
*kuondoka mahali hapa, wewe ni hapa milele.
'Sitaki kuwa hapa, oh tafadhali
nisaidie, nisaidie! *"Mimi nikasema, *"Siwezi kufanya kitu chochote kwa
ajili yako, Ninatamani
ningewasaidia watu wote hawa."*
Bwana akasema, *"Hakuna nafasi kwa wale
ambao wako hapa, lakini kwa wale tu
walio Duniani."* Msichana huyo akasema, *"Oh tafadhali nenda
kawaambie watu, na hata familia
yangu wasije mahali hapa. *
*Nenda kaseme na vijana ambao bado wana
nafasi ya kumtafuta Kristo, waambie
wageuke wawe mbali na * *dhambi. Nilipokuwa duniani, niliishi maisha ya
ovyo, maisha yaliyojaa
dhambi, nilikuwa na kiburi sana, *
*nilifurahia kwenda kwenye pati/starehe za kila
namna, kamwe sikuwatii
wazazi wangu, nilikuwa muasi siku* *zote.Sasa ninajuta sana, na ninawataka
wanisamehe. , ninataka kutoka hapa,
mwambie kila mtu juu ya uso wa*
*nchi asije hapa, asije, tafadhali. Waambie
wawatii wazazi wao, wamkubali
Kristo, kwa sababu kweli anaokoa, * *yeye kweli anaokoa, shetani alinidanganya,
sasa najua siwezi milele kutoka
mahali hapa,ni jinsi gani*
*ninajutia. "*
Alilia na kunyoosha mikono yake, nilitaka
kumsaidia lakini wakati ninampa mkono wangu aushike, yeye
alianza kulia na tena katika moto. Nililia,
"Bwana, ni namna gani
inavyotisha kuwepo mahali hapa" Akanijibu,
*"Ndiyo Binti, kumbuka hili, nenda Duniani na
utii amri yangu, ili wanadamu waamini kwamba Kuzimu ni*
*halisi na ni milele, kwa sababu bado kuna
wengi ambao hawaamini katika
Kuzimu , kuna wengi ambao*
*wanasanifu na kuleta mzaha wakisema
kwamba kuzimu ni ya kufikirika. "* ------------------------------
*Page 8*
8
Siku chache kabla ya uzoefu wangu wa
kwanza katika kuzimu
Bwana alinipa maono na kusema, *"Angalia, mtu huyu*
*amekwenda kuzimu." *Nazungumzia mtu
maarufu anayejulikana
kama MJ (Michael Jackson), yeye pia
alijulikana sana kwa glove
yake nyeupe. Alikuwa kuzimu kwa sababu ile niliyoieleza katika
video yangu ya awali. Nilipokuwa nikirekodi
video hiyo, Bwana
aliniambia, *"Sema kuhusu yeye." *Ndiyo
maana ninawaambia
kuhusu yeye kuwa yuko katika miali ya Kuzimu.
Wakati nakaribia sehemu hiyo ya moto, niliona
pepo wengi
wakiwa katika mduara, na ndani ya mduara
huo kulikuwa na mtu
aliyekuwa akiteswa. Alinyoosha mikono yake na kulia kwa sauti,
*"Msaada! Msaada!" *Niliweza kuelewa lugha
aliyokuwa
akizungumza.
Nilitaka kumsaidia sana, niliweza kuona jinsi
mapepo yalivyokuwa yakimnyanyua na kumlazimisha
acheze na kuimba kama alivyokuwa
akifanya Duniani. Mapepo
yalimdhihaki na kumtupa ndani ya moto.
yalimchukua tena na kumchapa
mijeledi. Alilia kwa maumivu ya kutisha. Oh, ni jinsi gani alivyokuwa akiteswa.
Ilivunja moyo wangu kuona hili na nikasema,
"*Bwana, tafadhali fanya kitu,
oh! Bwana msaidie*."
Niliponyoosha mkono wangu kumsaidia,
mikono yangu ghafla ikawaka moto, na kujaa na minyoo. Nikasema,
*"Bwana Tazama! Nini kinatokea*?" Kisha
mapepo yalianza kucheka na
kunidhihaki, *"Wewe unakwenda kukaa*
*mahali hapa."*
Kisha niligundua siwezi kuona au kuhisi kama Bwana yu karibu na mimi,
ilionekana nilikuwa peke yangu.
Nililia, *"Bwana, umeondoka, kwa nini bado
ningali hapa?" *Mapepo yalisema,
*"Tunakwenda
kukuadhibu, * *utakaa hapa." *Kisha nikasikia sauti ya
kuogopesha, ilikuwa ya kutisha, *"Ha
ha ha, wewe unakwenda kukaa*
*hapa. Hatimaye nimekukamata, mahali
muafaka ninapokuhitaji*. *Ninakutaka
wewe hapa kwa sababu wewe* *umeiba roho nyingi kwangu na
nitakuangamiza, hapa ndio kwako. "*Alitoa
amri kwa mapepo, *"Mchukueni, na *
*mpelekeni mahali panapomstahili."*
Nikajibu, *"Hapana, hapana, mimi sitakaa hapa
kwa sababu Bwana yu pamoja nami. Yeye alisema hawezi *
*kuniacha hapa." *Kisha nikasikia sauti ya
Shetani *"Wewe utakaa hapa,
utakaa hapa kwa sababu Bwana*
*hayuko na wewe. Angalia kote, hayuko na
wewe." *Nilitazama, lakini sikuweza kumwona Bwana. Nilijisikia
Mpweke, na nilianza kuwa na mashaka.
Nilianza kulia na kupiga kelele, *"Bwana,
kwa nini umeniacha? Kwa *
*nini Bwana, kwa nini?"*
Mara Bwana akasema, *"Binti, mimi niko hapa." *Nilisikia sauti yake katika
masikio yangu. Nilimuangalia
moja kwa moja shetani, Nikamjibu, *"Bwana
yuko hapa pamoja nami." *Lakini
yeye alijibu, *"Hakuna hayupo,*
*wewe angalia." *Sikuweza kumuona Yesu, lakini niliweza kusikia sauti yake.
Nilianza kuwa na mashaka tena
kwa sababu mapepo yalikuwa yananisogelea.
Nilihisi kamba imefungwa kiunoni
mwangu ambayo ilinivuta
kuelekea kwenye ile sauti ya uovu. Ilisema, *"Wewe ni mpumbavu, ndivyo
ulivyo, mpumbavu sana. *
*Nitakuharibu kwa sababu umesababisha roho
nyingi sisije kuzimu, roho
nyingi zinatoka nje ya kuzimu kwa *
------------------------------ *Page 9*
9
*sababu wewe*
*unahubiri. Usifanye hivyo tena, funga mdomo
wako, yaani funga mdomo wako,*
*nitakuangamiza, nitakuua. "* Niliendelea kulia alipokuwa akinishitaki. Ghafla
nikamjibu, "*Hapana
shetani, huwezi kuniharibu mimi, kwa *
*sababu Bwana amesema yuko pamoja na
mimi. Siwezi kumwona, lakini najua kwa
hakika Yeye yuko hapa*." Shetani anaendelea kunicheka.
Nilikuwa navutwa kuelekea mahali fulani,
karibu na ile sauti mbaya.
Nikasema kwa sauti, "*Damu ya Yesu ina*
*nguvu na mimi nimefunikwa na damu yake,
imeniunika hata sasa na shetani atakimbia mbali kwa sababu *
*damu ya Yesu iko juu yangu. Mkubwa zaidi ni
Yeye aliyepamoja nami zaidi
yako*. *Mkubwa zaidi ni Yeye aliye*
*pamoja nami. *"Niliendelea kurudia maneno
haya. Kisha niliona kitu kimeniachia; kama kitu kimenivuka,
ilikuwa ni ile kamba iliyofungwa kiunoni
mwangu.
Hatimaye, nilitoka Kuzimu, na kurejeshwa
katika uwepo wa Mungu. Bwana
akasema, *"Nataka nikupe ujumbe huu mara utakaporejea Duniani, nenda *
*na uwaambie watu wangu wanitafute katika
Roho na Kweli (Yohana 4:24).*
*Nenda uwaambie watu wangu waishi katika
utakatifu. Nenda na uwaambie*
*watu wangu huu ni wakati, ni wakati wa kutafakari Neno Takatifu. Si tu*
*nawataka watu wangu wasome, lakini pia
wameze Neno langu Takatifu. *
*kwa sababu Binti, hiki ndicho kinachotokea
Duniani, Duniani kila siku*
*uasi wa dini(apostasy) unaongezeka, bado kuna wengi wa watoto wangu, *
*wengi wa watu wangu wateule
wanadanganyika. Binti, waambie watu*
*wangu wameze/kulishika neno langu Takatifu
ili wasidanganyike na wautafute
uwepo wangu katika roho* *na kweli. "*
Mimi nikasema, *"Oh! Ndiyo Bwana. Nitatii.
Lakini Bwana, nahitaji msaada
wako, tafadhali nisaidie Bwana."*
Alijibu, *"Binti, wakati utakaporejea, Usiwe na
hofu kwa sababu nitasimama na wewe*. *Nitasema kupitia*
*mdomo wako kile nimesema kwa watu wangu.
Nimeona wengi wakiinuka kinyume
dhidi yako, lakini*
*kumbuka nitakuwa pamoja nawe daima kama
nilivyoahidi, na mimi ni shahidi wako mwaminifu. "*
Kisha nikaona malaika karibu yangu.
Nilimtambua Malaika Mikaeli, kwa sababu
nilikutana naye kabla.
Bwana akasema, *"Sikiliza, malaika Mikaeli
atakwenda kukuonyesha kitu". *Malaika Gabrieli pia alikuwa
pembeni mwangu. Kisha malaika Mikaeli
akachukua mkono wangu, na Bwana
akamwagiza, *"Mchukue na*
*umuonyeshe kile imekupasa kumuonyesha."*
Tulipokuwa tunatembea, tulianza kupanda juu ya ngazi nzuri sana. Ilionekana
kama chumba cha mpira. Na
katika sehemu ya juu ya chumba kulikuwa na
madhabahu ilyokuwa na mimbari
nzuri sana ya dhahabu.
Tulipofika katika mimbari, nikaona kitabu kikubwa na nikamuuliza Mikaeli, *"kitabu
hiki, ni nini?"*
Wakati Mikaeli alipokuwa upande wa kulia wa
mimbari, aliweka mkono wake juu
ya kitabu na kusema kwa
sauti yake, *"Angelica, kitabu hiki unachokiona hapa ni Kitabu cha Uzima". *Nilikifungua
na nikaangalia
ukurasa kwa ukurasa .Nikasema, *"Je, kitabu
hiki kina maana gani, Ni mambo
gani yaliyoandikwa ndani*
*yake?" *Mikaeli akasema, *"Fungua, ndani ya kitabu hiki yameandikwa majina
yote ya wale ambao Duniani*
*wametubu na wakageuza maisha yao
kumuelekea Baba yetu wa Mbinguni."*
------------------------------
*Page 10* 10
Nilipokuwa nikiangalia ndani ya kitabu,
Nilimuuliza Mikaeli,
*"Je, jina langu limeandikwa hapa?" "Ndiyo,
angalia hapo juu*
*na utaliona." *Niliangalia, lakini sikuweza kuliona. Nikawa na
wasiwasi kidogo, Nikauliza, "jina langu haliko
hapa, silioni,
liko wapi?" Yeye alinijibu, "*Angalia, jina lako ni
hili*."
Nilifurahi kuona jina langu, lakini sikuweza kulielewa ni kwa
sababu lilikuwa limeandikwa katika lugha
nyingine.
Niligundua kuwa majina mengi yalikuwa
yanang `aa, hivyo
nikamuuliza," *Kwa nini majina yale yanang'aa na Kuwaka?*
"Yeye alijibu, *"Majina haya unayoweza kuona
yaking` aa katika kitabu cha
uzima, ni watu wale waliopo*
*Duniani, kwa wakati huu hivi sasa wanatubu
dhambi zao na kutafuta uwepo wa Mungu. Tazama, majina *
*haya mengine ambayo ni vigumu kuonekana
na baadhi yao yanafutwa kama
ilivyo tayari kwa wengine*
*wengi, ni watu wale duniani ambao
wamegeuka mbali na njia za Mungu. Inakupasa ufanye jambo, fanya*
*jambo! "*
Kwa mara nyingine tena, akaweka mkono
wake juu ya kitabu cha uzima na
kuniambia, *"Enenda ukawambie*
*wanadamu kuwa kama majina yao hayakuandikwa katika kitabu hiki, hawawezi
kuingia katika Ufalme wa*
*Baba yangu wa Mbinguni, hawawezi kuingia
katika Ufalme wa Mbinguni . "*Mimi
nikajibu, "Sawa, nami
nitafanya hivyo." Imeandikwa katika Ufunuo 20:15 *"kama jina la mtu yeyote
halikuonekana katika kitabu cha *
*uzima, alitupwa katika ziwa la moto." *Tulitoka
nje na kurudi kwa Yesu,
alisema, *"Ni wakati wa wewe kurudi*
*Duniani."* Je, unafikiri jina lako limeandikwa katika kitabu
cha uzima? Kama hudhanii
hivyo, nenda na umtafute
Mungu. Kama umemgeuka Mungu, patana
naye, kwa sababu yeye yuko tayari
kukusamehe, bila kujali umefanya nini. Kumbuka, alikuja kuokoa
wenye dhambi; Yeye alikuja kusamehe
dhambi za wanadamu wote
duniani. Wewe fungua moyo wako na umsihi
akusamehe. Yeye yuko tayari
kutusafisha na udhalimu wote, kama inavyosemwa katika 1 Yohana 1: 9
'Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni
mwaminifu na wa haki hata
atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na
udhalimu wote'"
Nilipokua nikirudi Duniani, niliona mwili wangu umelala pale.
Ilikuwa ni asubuhi na mapema, karibu saa
01:00 asubuhi. Katika
nyumba yangu, niliweza kuona familia yangu
na baadhi ya
washirika wa kanisa. Bwana akasema, "Binti, ingia kwenye
mwili wako, ingia kwenye mwili wako, fanya
hivyo sasa",
"Sawa Bwana," nilijibu.
*"Kumbuka hili, utakuwa na mafunuo mengi
yanayotoka * *kwangu, na hivi karibuni utakuwa na ufunuo
wa tatu kuhusu*
*nini kinatokea ndani ya watu wangu. Kumbuka
tu mimi nipo*
*pamoja nawe." *Ghafla niliona mwanga na
Malaika walianza kuimba. Baada ya masaa mengi, hatimaye
niliweza kufungua
macho yangu. Ilinichukua muda wa siku nyingi
kupona kabisa.
Mimi nataka ujue kwamba kila kitu ulichosikia
kwenye video hii sio hadithi ya kufikirika, Bwana aliniruhusu
nipate uzoefu huu. Nataka ujue kama unahitaji
Mungu akusamehe, basi fumba
macho yako na weka mkono
wako wa kulia juu ya moyo wako na uombe,
sema kwake, ------------------------------
*Page 11*
11
*"Bwana Yesu, Ninatubu dhambi zangu zote,
Ninatubu kwa sababu mimi
nimefanya dhambi kinyume chako,* *Nakusihi wewe Bwana unisamehe dhambi
zangu na unisafishe kwa *
*damu yako ya thamani, Nakusihi uandike jina
langu katika kitabu *
*cha uzima. Nipige muhuri kwa Roho wako
Mtakatifu wako, Ingia* *na ukae katika maisha yangu na unitakase na
uovu wote. Nakataa *
*tamaa za mwili wangu. Nakana maisha yangu
ya zamani, na yote*
*yale ambayo hayakupendezi wewe,
Natangaza leo, kwamba* *minyororo yote iliyonifunga kwamba ifunguke,
Niko huru, kwa *
*sababu umeniweka Huru. Kwa jina la Yesu,
Amen ""*
Amani ya Mungu iwe ndani ya mioyo yetu, na
ukumbuke kwamba ni Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu pekee
ndiye ambaye
anatushudia hatia ya dhambi zetu. Mungu
awabariki.
*Angelica Zambrano Mora*
*----------------------------------------------* Kama unataka kuwa sehemu ya huduma hii
unaweza wasiliana nasi kwa barua
pepe zifuatazo : esdios@hotmail.com
palabraderevelaciondivina@hotmail.com *(Kama inawezekana, tumia Kihispania)*
*** Toleo hili ni Minimally Abridged, Polished na
Illustrated.*
*Video ya awali katika lugha ya Kihispania*
*.*
*Ndugu aliyefasiri ufunuo wa 2 kuhusu mbinguni na kuzimu wa Angelica
Zambarano ni Peter Kahale ni kijana*
*aliyeokoka na anampenda Yesu na mwenye
shauku ya kuhubiri injili ya Yesu
Kristo.*
UNABII WA KWELI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni