<http://www.divinerevelations.info/SWAHILI >* Bwana akasema, "*Ninatuma ujumbe huu kwa
watu wangu katika dunia,kwa sababu
mimi niko hai katika *
*ulimwengu wa roho.*"
Ufunuo 4:1
*Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile
ya kwanza*
*niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena
nami, ikisema, Panda hata
huku, nami*
*nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo. *
Ufunuo 5:11-12
*Kisha nikatazama, nikasikia sauti ya malaika
wengi sana, idadi
isiyohesabika, maelfu na*
*maelfu. Walikuwa wamekaa kuzunguka kiti cha enzi, wale viumbe hai wanne na
wale wazee;*
*wakasema kwa sauti kuu: "Mwanakondoo
aliyechinjwa anastahili kupokea
uwezo, utajiri, *
*hekima, nguvu, utukufu na sifa."* Tafadhali, kanisa sikilizeni nini kilichotokea
katika maisha yangu. Katika
ndoto, Bwana alianza
kushughulika nami. Nakumbuka katika ndoto
hiyo, Nilitembea nje ya nyumba
yangu. Nilitembea katika mitaa kwa jirani zangu na mara nilihisi kwamba
mtu akiniinua mikono yangu
juu angani nami nilikuwa
nikitembea mbio juu ya mawingu na
nikimtukuza Mungu. Mwangaza mkubwa
alikuja juu yangu na sauti ilisema nje ya mwangaza huo, *"Ricardo,
Ricardo, acha kazi yako kwa sababu
nataka kufanya kitu*
*kwa maisha yako na kwa kanisa langu juu ya
dunia." *Baada ya kusikia
maneno haya, mimi nilitetemeka na nikaamka kutoka katika ndoto
yangu. Nikainuka na mimi
nikaanza kulia kwa Mungu na
kuuliza, "ni kitu gani, hiki Bwana?"
Sauti hiyo ilikuja kwangu kwa nguvu sana.
Ilitokea kwangu kwa siku nyingi. Kisha nikaendelea kulala
tena na nikaota ndoto hiyohiyo moja na Bwana
alirudia mara kwa mara ujumbe
huo kwangu. Baada ya
mara kwa mara kurudia, niliamka na kupiga
mayowe kwa sababu sauti ya Mungu iliongezeka kwa kiasi
kila wakati. Niliamka nikiwa natetemeka, nilipiga
kelele na wazazi wangu
waliniuliza, *"Je, kuna tatizo*
*gani?" *Niliwaambia kuhusu ndoto na mama
yangu aliniombea na aliniambia, "*Kama Bwana*
*anazungumza na wewe, basi Yeye atakupa
ufahamu. "*Tuliendelea kuomba usiku
kutwa mpaka wakati
wa mimi kwenda kazini asubuhi. Mama yangu
aliniambia nijiandae kwenda kazini. Tulimuomba Bwana
------------------------------
*Page 2*
2
ishara ili tujue kama yeye ndiye alizungumza
na mimi. Nilioga, nikajiandaa, na nikaenda kazini.
Nilikuwa nafanya kazi katika "maabara ya
Chile".
Mimi kwa kweli napenda kazi yangu. Nilikuwa
nikipitiwa katika kituo cha
basi na kwenda kazini. Mara niliposhuka, mtu mmoja aliniambia kwa
haraka, *"Unafanya nini hapa?
Hautakiwi kuwa mahali*
*hapa tena. "*Katika matukio kadhaa, wengine
waliniambia kitu hiko. Jambo
la kushangaza ni kwamba wao hawakuwa wamezaliwa mara ya pili. Hii ni
ishara ambayo Mungu alinipa.
Baada ya ishara hii,
niliamua kwenda kwa bosi wangu ili niache
kazi. Nikamwambia*, "Mimi
menipasa kuondoka katika* *kampuni kwa sababu Mungu ameniagiza
kujiondoa." *Bwana anapotupa amri, ni
LAZIMA kutii. Bosi
wangu alikuwa na wasiwasi kwa ajili yangu na
aliuliza, *"Je,utakwenda
kufanya nini? Wapi utapata kazi* *nyingine nzuri kama hii? "*Nilimwambia
imenipasa kumtii Mungu. Basi,
walinifanyia mahafali makubwa
ya kuniaga ya watu elfu mbili kwa ajili yangu.
Baada ya hapo, nilikusanya
vitu vyangu vyote na kurudi nyumbani. Nilifika nikiwa nalia, mama yangu
alikuwa tayari ananisubiri kwa
mbele ya nyumba.
Nilimwambia kuwa niliamua kuacha kazi yangu
kwa sababu Bwana alithibitisha
ndoto zangu kupitia watu hao. Yeye akajibu, *"Kama Bwana
amekuambia, basi namuomba afanye
katika maisha yako vile*
*apendavyo."*
Tuliingia ndani na tukaongea mpaka usiku.
Basi, niliimuambia ninahitaji kwenda
kitandani kwa sababu Mungu atazungumza na
mimi usiku wa leo katika ndoto.
Nilidhani angeongea nami katika ndoto, lakini
haikutokea kama nilivyowaza.
Lakini alisema nami kwa njia ya tofauti. Nilipokwenda katika chumba cha
kulala na
nilipotoa nguo zangu, chumba kikaanza
kutikisika. Na nilianza kupiga
kelele, *"Ni*
*tetemeko linaikumba Santiago, Chile." *Nilijaribu kuondoka katika chumba
changu,
lakini mtu asiyeonekana alinizuia kupita
mlangoni. Nilikuwa na uwezo wa
kumuona mama yangu na familia yangu katika
chumba hicho na nilipiga kelele kwa msaada lakini hakuna mtu aliyeweza
kunisikia. Sasa najua, kiumbe huyu
asiyeonekana alikuwa ni malaika wa Bwana.
Nilirudi nyuma na kujilaza juu ya
kitanda changu na nikalmlilia Mungu, nikaomba
aniambie nini kinaendelea. Sauti ikasema nami. Roho mtakatifu akaanza
kusema nami katika sauti nzuri
sana, akisema, "*Ricardo, Kwa kuwa umeacha
kazi kwa sasa, nitahitaji wewe
uende kanisani na uwe*
*unaomba kwa muda wa saa saba kila siku kwa maisha yako, na kwa kanisa
langu duniani." *Baada ya
Bwana kuacha kuongea nami, chumba
kikaacha kutikisika. Nikaainua mkono
wangu na kuona ya kuwa
ninaweza kuondoka chumbani tena. Kishanikamkimbilia mama yangu na
kumueleza *"
Nimesikia sauti*
*ya Roho mtakatifu" *na nikatoka nikaanza
kuongea kwa sauti nje ya nyumba.
Watu hawaamini kuwa Mungu bado anaongea na watu hata leo lakini
nakueleza ni kweli, Anaongea na
watu! Kama Bwana
aliweza kuongea na Abrahamu, anaweza
kuongea nasi pia na kanisa lake leo.
Nikaenda kanisani na kuongea na Askofu na tukakubaliana
kufungua kanisa kila siku asubuhi saa 2
ili niweze kutii agizo la
Mungu alilonipa. Kila asubuhi nilikwenda
kanisani na nikaomba saa moja,
mawili na kwa mara ya tatu sikuwa na chochote cha kuombea na nikawa
nikimuuliza Mungu, " *Bwana ni
kitu gani kingine*
*niombee?Nimebakiwa na masaa manne
yaliyobakia!"*
Kisha, nikasikia tetemeko linatokea nyuma ya mlango wa kanisa. Nikahisi
kanisa linayumba kushoto
na kuliakama mtu aliyelewa. Lilipokuwa
likiyumba, nikasikia sauti ikiongea
nami lakini wakati huu
haikuwa sauti kama ile ya kwanzaniliyokuwa kwenye maono. Suti ile ya kwanza
ilikuwa ya mamlaka,
lakini wakati huu aliongea nami kwa sauti ya
huzuni. Akasema, "*Ricardo,
Ricardo omba kwa ajili ya*
*kanisa langu! Kanisa langu si kama lilivyokuwa kabisa, Kanisa langu
duniani limebadilika. Kanisa*
------------------------------
*Page 3*
3
*langu limepoteza imani yake. Kanisa langu haliamini kuhusu mimi na wala
kuamini kama mimi ni *
*hai hata leo . Liambie kanisa langu kwamba
nipo ni hai!! Omba kwa ajili ya
kanisa, kwa sababu*
*kanisa langu haliombi wala kufunga tena!" *Mtikisiko uliacha baada ya yeye
kumaliza.Nikaanza tena
kuomba na kutembea juu na chini kwa muda
wa masaa manne yaliyobakia
nikiwasihi watu wa Mungu
wawe na uhamsho. Siku ya Alhamisi ya wiki ya pili ya maombi,
niliamka na maumivu makubwa
katika mifupa yangu na
viungo vyangu na sikutaka kuinuka. Mama
yangu alikuwa akiniamsha kwenda
kanisani kuomba, lakini nililalamika kuwa mwili wangu na mifupa yangu
ilikuwa ina maumivu. Basi
akanishauri kuwa niombee
pale nyumbani. Hata hivyo nilimkumbusha
kuwa Mungu ameniambia niombee
kanisani. Hivyo akanisaidia kunivalisha na kunipeleka kanisani.
Asubuhi ile kulikuwa na
watu wengi waliokuwa
wakiomba pale kanisani, nami nikawaomba
waniombee kwa ajili ya mwili wangu
kwa sababu ya maumivu katika mwili wangu. Niliwaeleza kuwa
nilikuwa mdhaifu sana kuweza
kufanya maombi.
Hivyo walinipaka mafuta na kuniombea mwili
wangu na nikapata nguvu za ajabu
kutoka kwa Mungu!!Haleluya! Nikaanza kuomba
nikitembea mbele na kurudi nyuma, nikiomba
rehema za Mungu
kwa taifa la Chile na kwa familia na watu
walioathiriwa na madawa na kwa
kanisa. Nilimaliza maombi na kisha nikarudi tena
baadae kwa ajili ya ibada ya
usiku. Baada ya Baraka za
askofu,niliinua mikono yangu na nikahisi mtu
fulani alipita na kuugusa
mgongo wangu. Lilipotokea jambo hili nilipoteza nguvu zangu zote na
nikaanguka sakafuni.Askofu
aliniuridha nini kilikuwa ni tatizo
na mimi, na nikajibu hata sifahamu,
nikamueleza kuwa sina nguvu na siwezi
kuzumgumza vizuri. Kisha kanisa likanizunguka na kuanza kuniombea
kwa lugha huku wengine wakiomba
kwa sauti. Baadhi ya
watu walianza kuona malaika akija na kuniuliza
niuache mwili wangu. Askofu
akakemmea, *"Hautauacha mwili wako!" *Aliposema hivyo,
Malaika waliacha kuniita ili
niuache mwili wangu.
Unaona, Mtu yeyote mwenye mamlaka katika
Yesu ataheshimiwa na malaika wa
Bwana. Askofu akaniomba pia, *"Kwa muda gani
malaika anahitaji akuchukue kutoka
katika mwili wako?" *
Nikamuuliza malaika, *"unanichukua kwa saa
moja?mawili?Matatu?"*Malaika
akajibu*, " hapana,* *utaondoka kwa muda wa masaa 8 kwenda
kumuona Yesu katika mbingu ya tatu
kwa sababu anataka*
*kuongea nawe."*Kisha malaika akanieleza,
*"Mimi siye ambaye nitakuongoza
wewe kwenda mbinguni,* *kwa sababu mimi ni malaika wako ambaye
nimekulinda wewe kila siku tokea
kuzaliwa katika dunia hii.*
*Malaika wawili watakuja kutokea mbinguni ili
kukuchukua wewe mpaka mbingu
ya tatu usiku wa* *manane." *Nikamueleza hili askofu na na
akaazimia kunichukua mimi kwa gari
ya ndugu mmoja katika
kristo kwa nyumba ya mchungaji katika
ghorofa ya pili. Nilipofika tu
chumbani, tuliweza kusikia mbwa wakibweka na watu wakilia.
Baada ya maono yangu nilielezwa kuwa
wanaume wawili waliovalia mavazi
mazuri meupe
yanayong'aa walionekana mtaani na wakaja
hadi ghorofa ya kwanza ya nyumba na wakapanda hadi
ghorofa ya pili nilipokuwepo. Malaika hawa ni
wazuri. walikuwa na nywele
nyeupe zinazong'aa, nyeupe
zaidi ya barafu/theluji, na macho yao
yalipendeza kama lulu.Ngozi yao ilikuwa nyororo kama ya mtoto
lakini bado walikuwa wakionekana kuwa na
misuli kama wanyayuaji wa vitu
vizito(bodybuilders).
Malaika hawa walikuwa na nguvu!! Kisha
nikamueleza Askofu, malaika hawa wako mahali hapa
walotumwa kunichukua twende
mbinguni.Malaika mmoja akaanza kunisihi
niuache
mwili wangu.
Lilipokuwa likitokea hili, mifupa yangu ilianza kuniuma tena. kwa hiyo
ndugu wangu katika Kristo
pembeni mwangu walianza kunichua na
kunieleza kuwa walihisi baridi
ikiongezeka katika mwili
wangu.Kwa hiyo walichukua hita ili kuupa joto mwili wangu, nilianza kuogopa
na kuanza kwenda huku
------------------------------
*Page 4*
4
na huku. Nilianza kuhisi kifo kinanichukua na nikasema kwa sauti wa ndugu
zangu hawa katika Kristo, "
Msinizike, nitarudi tena!"
Niliuacha mwili wangu na nikarukia kitandani.
Niliwaona ndugu hawa
wakiushikamwili wangu na kusema, "Ameondoka, *"Ameuacha mwili
wake!" *Lakini nilikuwa pembeni yao
nikiwaeleza *"niko*
*hapa!*" Lakini hawakuweza kuniona kwa
sababu ulikuwa ni mwili usioharibika
wa kiroho. Ndugu hawa walianza kuufunika mwili wangu katika
blanketi.
Malaika mmoja aliniambia, *"Ni wakati wa
kuondoka sasa kwa kuwa Bwana
anakusubiri!" *Kila
mmoja aliushika mkono wangu na kuninyanyua kwenda mbinguni na tulipita
katika anga kwa mwendo
wa mwanga. Nitakueleza wewe hivi, hata kama
hauamini mojawapo ya mambo
haya, Yesu Kristo yupo
na anaishi milele!! Baadae ,Bwana aliponieleza niurudie mwili
wangu , nikimueleza,, *" Ni nani
katika dunia ataniamini,*
*niache tu niishi na wewe!! hakuna atakaye
amini huu ufunuo, hakuna
atakayeamini kwa sababu hawana* *imani! Tatikzo la kukosekana kwa imani ni
kubwa sana, ni nani ataamini huu
ufunuo?" *Bwana akajibu,
*" Kuna mtu fulani ataamini maono haya, ni
wale walio wa kanisa langu la
kweli wataamini."* Nilipokuwa nimeuachaa mwili wangu usiku ule
nilikuwa nikipaa kwa spidi ya
ajabu nikiwa naenda
kwa Bwana. Niliweza kuangalia chini na kuona
sayari dunia. Kisha nikapita
karibu kabisa na mwezi, Mwezi huu mzuri uliiangaza anga usiku katika
dunia. Kisha, niliweza kuona
jua na ukubwa wake kwa
macho yangu; Niliweza kuona miali ya moto
ilivyokuwa ikilipuka na kutoa
joto mpaka kwenye dunia. Kisha tuliendelea na kuona nyota nyingi
tulizozipita. Mungu aliruhusu mimi
nione jua, mwezi na nyota
kwa kusudi: Kusudi hilo ni kuuambia nyinyi
nyote kwamba Mungu wetu ni
muumbaji mkuu wa Ulimwengu!!! Si mdogo kwa namna yeyote ile!
Tuliendelea kusafiri kwa mwendo huu mkali
hadi tulipofika mahali ambapo
hakukuwa na nyota tena.
hakukuwa na uumbaji wowote, ilikuwa ni Giza
tu.Niliweza kuangalia chini na kuona nyote zote zikiwa
chini. Nilianza kuogopa na nikawauliza malaika,
*"Mnanipeleka wapi?
Nirudisheni kwenye kitanda*
*changu duniani*" walinishika na kunibana zaidi
na kuniwekea miguu yao kwa miguu yangu na kunishika.
Nilianza kulegea kwa sababu ya hofu
niliyokuwanayo. Malaika wakaniambia "
Nyamaza Kimya!
Tunakupeleka kwenye mbingu ya tatu ambapo
Yesu anakusubiri ili aongee nawe!" Malaika walisimama
na wakati huu niliangalia pande zote na
sikuona chochote cha uumbaji,
sifahamu nilikuwa wapi, nafikiri
ilikuwa ni mbingu ya pili.
Kisha nikiwa katika hali ya kujiachia malaika wakiwa wamenishika na mara
nikajisikia na kusikia kelele
za kutisha juu yangu. Malaika wakanibana na
kusema, *" Ricardo, usiogope,
Yesu yuko pamoja nasi!"*
walipokuwa wakiongea,walisema*, " Inua kichwa chako na uangalie juu yako!"
*Nilishangazwa
sana na
kile nilichokiona kwa sababu kulikuwa na
viumbe vilivyokuwa katika mwendo
juu yetu. Malaika mmoja akasema, *" Angalia, tutakuonyesha wewe kile
ambacho unakiona juu yetu! *Malaika
mmoja akanyoosha
mkono wake akapunga huku na huku ili kutoa
mwanga uangaze sehemu yote ile
ya anga ili kuona kitu kilichokuwepo mahali pale. Anga lilipokuwa na
muangaza hakukuwa na kitu
chochote ila mapepo na
mashetani yalikuwa yamezunguka anga lote
lile. BWANA AWAKEMEE WOTE KWA JINA
LA YESU!!Biblia ni kweli!! Kila kitu kinachoendelea
katika ulimwengu huu ndo
kile ambacho unakiona
katika Ufunuo. Yesu anakuja hivi karibuni!!
Nawezaje kukushawishi, ni hivi
*KARIBUNI!!*Nikamuuliza malaika, "*Mahali hapa ni wapi?*Mmoja
akajibu, *" Hapa ni mahali pa
ulimwengu wa Giza ambapo*
*Shetani na malaika zake ( mapepo) wanaishi,"
*Akaanza kusema, *" Ndio
maana kuna uharibifu mwingi* *duniani! Mapepo haya yanakuja duniani
kutokea mahali hapa na kusababisha
uharibifu na uovu wa kila*
------------------------------
*Page 5*
5 *aina na uovu katika makabila ya wanadamu!"
Dunia imejaa mapepo!" *Kuna
mapepo milioni na
milioni , idadi haihesabiki.
Kisha malaika, alianza kunipeleka
niangalie kwa ukaribu na kunionyesha sura za viumbe hivi na nyingi ya hivi
viumbe vimekwisha onekana kwenye
Runinga. Viumbe hivi ni VIBAYA!!
Niliona viumbe vilivyofanana na viumb
vya kwenye michezo ya runinga ya
Thundercats na Power Rangers na katuni ya caricatures ambavyo ni halisi kabisa
kwa maisha ya duniani. Wabunifu wote
wa muvi na michezo hii wameweka
mkataba na shetani kutoa vitu hivi
kwenye runinga na sinema!! Michoro yote ile
inatokea katika ulimwengu war oho ambao niliuona. Unafikiri kwa nini watoto
wa siku hizi wamekuwa
wakaidi?? ni kwa sababu
mapepo haya yanawanigia watoto hawa
wanapokuwa wakiangalia maonyesho haya
ambayo yanawaoyesha wao (mapepo). Ndiyo maana
imetupasa kuwafundisha watoto
kuchagua nini cha
kuangalia kwenye TV. Malaika aliniambia hiki ni
halisi na kweli. Mapepo
haya yote yapo na watu wanafanya makubaliano na shetani ili kuleta
mapepo haya duniani. Haya
mapepo yanaanza kunitukana
mimi, na kanisa, na Baba, na Bwana Yesu na
Dunia kwa sababu hawamuheshimu
Mungu au uumbaji wake wowote.
Kisha nikaona kiumbe halisi kabisa kiitwacho
Hugo, huyu ni katuni maarufu
sana nchini Chile. Ilikuwa
inaogopesha kuangalia. Alikuja karibu yangu
na kunieleza, "Tutaenda duniani na kuwaua watoto wote!"
Kwa nini unafikiri watoto wanaua watoto
wenzao? Ni kwa sababu baadhi yao
husema kuna kitu kilikuja
kutoka katika runinga na kuniambia nifanye
hivi au vile. Mapepo haya hupanda chuki duniani, Bwana
akomboe na kusafisha Chile!! Mmoja wa
malaika akaniambia *"Endelea
kuangalia!" *Na mapepo
yakasema, *"Tumejaribu kuharibu kanisa,
lakini hatuwezi kwa sababu tunapomuuua mmoja, basi*
*wanainuka maelfu kuchukua nafasi ya kifo
chake!" *Tokea kuanza kwa kanisa,
Shetani amejaribu
kuliharibu, kanisa ambalo huubiri injili ya kweli
na kufanya kazi ya Mungu, lakini hawezi kwa sababu
Yesu anatulinda! Utukufu kwa Mungu! Kisha
mapepo yakasema, *"Ngoja tufanya
jambo jipya, ngoja*
*tuingie makanisani, kwa sababu pale kuna
wengi ambao ni wetu! Tutaenda kuwatumia watu hawa*
*kusambaza umbea na kuleta migawanyiko
katikati ya ndugu ndani ya kanisa." *Shetani
anazunguka kila
mahali akitafuta kuharibu wale wanaopenda
haki ya Mungu. Kama andiko linavyosema:
1Petro 5:8 *Muwe macho; kesheni! Maana adui
yenu, Ibilisi, huzungukazunguka
kama simba *
*angurumaye akitafuta mawindo. *
Sikutaka kuendelea kuona tena, lakini malaika akaniambia niendelee
kuangalia matukio yanayotokea.
Niliona mapepo yakiruka kila kona pindi nyota
moja ing'aayo ilipokuwa
inakuja. nyota hii ilipokuwa
inatokeza na kusogea, ilikuwa inaleta sifa nyingi na ibada kwa Bwana. Hii
haikuwa nyota kama nyota,
kumbe ilikuwa ni mamilioni ya malaikawakiwa
juu ya farasi weupe wakimtukuza
Mungu wa Majeshi!!
Walikuwa wakiimba *"Mtakatifu,Mtakatifu, Mtakatifu, ni yeye aishie enzi na
enzi! Bwana ndiye Alpha na*
*Omega, Mwanzo na Mwisho na kila chenye
pumzi na kimsifu Bwana!" *Kisha
nikaaona vita kubwa na
------------------------------ *Page 6*
6
sikuona mapepo tena. *"Usiogope kabisa kwa
sababu kuna malaika wengi zaidi
upande wetu zaidi ya*
*upande wa adui!"* Malaika walifa ya njia mpaka mbingu ya tatu.
Walijigawa katika makundi
mawili, moja kulia na jingine
kushoto.Ilikuwa ni njia iliyowazi mpaka mbingu
ya Tatu! Njia hii ilinyooka
mpaka mbinguni na uliweza kuona Mji mtakatifu wa Mungu.
*(Kuna picha ya satellite duniani ambayo
imechukua picha kutokea katika mji
huu. Mji huu*
*Mtakatifu upo! Hii imetokea kwenye radio na
TV.)* Nilweza kuona njia ya utukufu na malaika wa
ajabu. Waliisafisha
njia yote kuwafukuza mapepo na hawakuacha
kumsifu Mungu na kubariki Jina
lake! Malaika
wakaniweka mbele yao na kuniambia, " *Imekupasa kusubiri hapa*!"
Kwa mbali, niliangalia na kutokea katika mji
huu niliona mtu fulani akiwa
na mazazi mazuri meupe
amepanda farasi mweupe. Mtu huyu alipokuwa
akizidi kunisogelea, malaika waliendelea kusifu jina la
Mungu na kumtukuza. Mtu huyu alikuja mpaka
umbali wa mita 4 tokea nilipo.
Kiumbe huyu alikuwa
mzuri, alikuwa ni mzuri zaidi ya wale malaika
wengine. Nilitegemea angeongea nami, lakini
alichokifanya ilikuwa ni kuniangalia na kusema
kwa sauti, *"Mimi ni malaika
mkuu Mikaeli ambaye*
*ninajukumu la kukulinda wewe pamoja na
kanisa la Duniani!" *Nilimuona malaika mkuu Mikaeli uso
kwa uso na alikuwa ni kiumbe cha thamani
sana! Aligeukia upande wake na
kuonyesha njia ya mimi
kuingia mji Mtakatifu. Alisema, *"Ingia! Bwana
Yesu anakusubiri!" *Nilikuwa nikitembea katika njia ile
nikifuata mji ule na nilipokuwa nikitembea,
Malaika walikuwa wakiimba na
kumsifu Bwana. Nililia na
kulia nilipokuwa nikiuangalia mji ule.
Mji ulikuwa umeumbwa kwa dhahabu halisi angavu na mlango wa kuingilia
ulikuwa umeundwa kwa
lulu. Sakafu ilikuwa ni ya muonekano wa kioo
angavu(crystal). Sijawahi
kuona kitu kama hiki duniani
na hakuna mwanadamu awezaye kukiunda. Msanifu wa majengo ya mbinguni ni
Bwana wetu na Mungu
wa Ulimwengu wote.Nilikuwa nje ya mji na
milango yote ilikuwa imefunguliwa.
Na milango hiyo ikiwa
bado hii wazi, niliweza kuona ndani na katika kuta kulikuwa na madini ya
Rubi na safira na lulu
ambayo yaling'aa. Na ndani ya mji ule kulikuwa
na sauti milioni na milioni
ya sauti zikimsifu Mungu!
Nilitetemeka kutokea nje ya mji niliposikia hivi. nilisikia sauti moja
ambayo ilitikisa mbingu na nyuma
ya sauti hii ilikuwa ni mamilioni na mamilioni ya
sifa kwa Mungu yakisifu *"Mtakatifu,
*
*MtakatifuMtakatifu ndiye mwanakondoo wa Mungu na Baba ambaye utukufu una
yeye na heshima*
*milele na milele AMEN!" *Sauti kubwa
ikasikika ikisema "IWENI WATAKATIFU
KWA SABABU
MIMI NI MTAKATIFU! NI WATAKATIFU TU NDIO WATAKAOINGIA KATIKA MJI HUU!
KWA
SABABU PASIPO UTAKATIFU HAKUNA
ATAKAYEMWONA BWANA." Bila utakatifu
hakuna
atakayemuona Bwana. Sauti ikasikika ikisema, *"Ingia" *na nikaingia
ndani ya mji ule. Na
nikaona Kiti cha ajabu cha enzi
kimezungukwa na moto. Na moto unatoka
katika kiti kile cha enzi, Nikatulia
kimya na nikamuona Yesu , Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana!
Nilijihisi mdhaifu mbele zake na
nikaanguka chini
nikaishiwa na nguvu.Mkono wake ukatoka
kwenye miali ile ya moto na
kunishika na akasema, *"Simama kwa miguu yako!" *Nilipata nguvu na
nikasimama. Nilianza kugusa
miguu yake na mikono
yake na mwili. Nilipoona uso wake, muonekano
wake ni tofauti sana na
wachoraji wa dunia wanavyochora katika michoro yao! Watu
wengi wanaunda miungu ya mbaona
wengine taswira
mbalimbali! Lakini nataka nikuambie hivi ndugu
yangu, Yesu Yule hafanani na
taswira hizo. Ni Mungu mwenye misuli na nguvu! Si Mungu wa
ukawaida, Ni Mungu mwenye nguvu zote!!
Anasema, "Mimi *si*
*Mungu niliyeumba na mbao, au chaki,Ni
Mungu ninayeishi!" *Anaendelea, *"Liambie
kanisa langu * *duniani mimi ni halisi!! Ni kweli ninaishi na nipo!
Waambie watu wangu
kuwa Mbinguni ni Halisi*
*na ninawasubiri!" *Aliniambia,"*Njoo, tembea
pamoja nami na nitakuonyesha
jambo moja kubwa.* ------------------------------
*Page 7*
7
Tuliangalia chini na niliweza kuona dunia na
vitu vyote vilivyofanywa
kwenye dunia. Yesu akasema, *"Ninaweza kuona kila kitu ambacho kanisa
langu linafanya!" *Anajua kila
kitu tunachokifanya na
mimi niliweza kuona wengi wenu kutokea
mbinguni. Yesu akaniambia, "Angalia
katika kanisa langu!" Niliweza kuona ndugu kwa ndugu, na
makanisa kwa makanisa. Yesu akaniambia,
"*Kanisa
langu*
*limepoteza imani yake,hawataki kuniamini,
uovu umeongezeka duniani na watu hawataki kuamini *
*kuwa nipo. Waambie watu wangu ninakwenda
kufanya kitu kikubwa duniani!
Kanisa langu linarudi*
*nyuma badala ya kukua." *Bwana alianza
kulia kwa ajili ya kanisa lake na akasema, *" Hili kanisa si*
*kanisa langu*! Nikamuambia Bwana, *"Bwana
usiseme hivyo! Wewe unajua kuwa
tu kanisa lako."*
Bwana Yesu akajibu, *"Hapana kanisa langu
linatembea kwa nguvu za miujiza,ishara na maajabu!*
*Kanisa langu limepungua! Hatahivyo,
waambie, nitakuja kuwafufua tena!"*
Aliniambia niendelee kutembea pamoja nae na
tulikwenda mahali fulani penye
mlango na mlango ulikuwa umetengenezwa kwa dhahabu
halisi.Nilianza kukimbia huku na huku
kwenye mtaa uliofanywa
kwa dhahabu na nikawa ninachukua vumbi la
dhahabu na kujipaka kwenye mwili
wangu. Na Yesu aliniambia nirudi na akaniambia kuna mitaa ya
dhahabu mbinguni. *" Hii yote
ni urithi kwa watu*
*wangu," *Bwana akasema. *" Lakini kwenye
kanisa langu kuna wezi wengi
ambao wananiibia fungu la* *kumi na sadaka! Waambie watu wangu
hakuna mwizi atakayeingia kwenye ufalme
wa Mungu!"*
Inabidi turekebishe maisha yetu kwa ajili ya
Bwana.Kisha tuliona meza ndefu
sana kwa ajili ya watu mamilioni ikiwa na chakula cha kutosha na
vinywaji. Kulikuwa na mataji
mengi na glasi kwa ajili ya
watu kunywea. Bwana akasema, *"Yote haya
yameandaliwa kwa ajili ya watu
wangu!" *Meza hii iliandaliwa kwa ajili ya harusi ya Mwana
kondoo.
Kuna dada mmoja katika Kristo ambaye pia
alipelekwa mbinguni na kasha
aliona malaika wakienda na
kurudi wakiwa wanatayarisha chakula cha Harusi hii! Nikamuambia Bwana, *"
Kwa nini dada huyu*
*aliona malaika wakitayarisha vitu hivi, lakini
mimi sioni matayarisho
yoyote yanayofanyika? *Bwana
akajibu, *"Ni kwa sababu matayarisho yote yamekamilika!" *Kuna mataji kwa
wote wanaofanya kazi na
ni watii kwa Bwana. Kisha nikamuuliza, "
*Bwana utakuja lini basi,kama
maandalizi yote*
*yamekamilika?Itachukua muda gani mpaka utakaporudi? Nionyeshe muda, Ni
muda gani umebaki*
*katika saa ya mbinguni?" *Watu wengine
wamekuwa na maono ya muda,
wakionyesha kuwa itakuwa ni
usiku muda ambao Bwana Yesu atarudi. Niliuliza, " *Ni lini saa itagota
katika mshale wa saa sita*
*usiku?Je ni dakika moja imebakia? dakika
tano?" *Bwana Yesu akausoma uso
wangu kwa muda
kidogo, kasha akajibu, "*Ricardo,mbinguni hakuna muda tena!" *Kisha
nikaitikia, *"Vizuri bwana ,*
*kama hakuna muda tena, kwa nini bado
haujarudi?" *Yesu akanyanyua mkono
wake na kuchukua
kidole gumba chake na vidole vyake vingine na kunionyesha alama
inayoonyesha kitu fulani kidogo
sana na akasema*,"Muda wote uliobakia ni
Neema ya Mungu kwa wale waliorudi
nyuma warejee tena*
*na kutubu na kuifanya kazi ya kwanza." *Na Bwana wa Majeshi hajarudi kwa
sababu ametupa sisi sote
muda kidogo sana wa kutubu na Muda huo
unaitwa, " Muda wa neema/rehema ya
Baba" Yesu anarudi
muda wowote, ni lazima tuanze kumtafuta kwa moyo wetu wote na tufunge na
kuomba na tuzifanye kazi
za kwanza. Nimemaliza kila kitu. Yesu alirudia,
*" Tuko kwenye muda wa
Neema ya Mungu!"*
Kisha malaika alitokea upande wetu wa kuume akisema kwa sauti, *"Muda
umewadia!! muda*
*umekwisha. Maandalizi yote yamekamilika!
Yesu anampokea bibi harusi wake(
kanisa)!" *Bwana Yesu
anarudi na kila ishara iliyoko kwenye maandiko inatimia! Sinema zinaonyesha
kitu fulani cha kutisha
kinakuja. Wanasayansi wanatambua kitu
fulani kikubwa kitatokea, hawajui ni
kitu gani
hicho!Hatahivyo, Sisi kanisa tunatambua kwamba Yesu anarudi hivi karibuni!
Malaika walipomaliza
kusema, kasha mamilioni ya malaika walianza
kuruka na kushangilia kwamba
bibi harusi(kanisa)
linarudi mbinguni. Nikaendelea kumuuliza, *" Kitu gani kinaendelea?" *Lakini
hakuna aliyeonekana
------------------------------
*Page 8*
8
kujali, wote walikuwa wakishangilia kwa habari njema. Nilijumuika na
malaika na kuanza kulisifu jina
la Yesu pia! Wakati huo nilipoinua mikono
yangu nilihisi mtu fulani
ameninyanyua kuondoka mbinguni
na kunirudisha chini kwa spidi ya ajabu. Hivi sasa, malaika wanashangilia kwamba
Bwana Harusi anarudi. Nilirudi
duniani na niliachwa pale
madhabahuni kanisani ambapo nitakuwa
ninaomba kila siku. *Muda ni mfupi
sana!! *Kama hutaki kuniamini mimi, basi usiamini. Lakini anakuja
na itakuwa ni ujio wa milele.
Watu wa Mungu
hawaamini katika unyakuo. Tafadhali amka,
Kwa jina la Mungu amka katika
ukweli!! *(Ricardo analia)*
.
Bwana Yesu alikuwa karibu yangu, na
aliniambia, "*Ricardo, hivi ndivyo
ambavyo unyakuo utakuwa*
*kama utatokea hivi sasa!" *niliweza kuona dunia yote na Roho mtakatifu
mzuri ambaye anatupa amani
na furaha ya kuishi katika dunia.Kisha nikaona
kama mvuke ukiingia kanisani
na ukanizunguka na
nikamuuliza Bwana*, "Hii ni nini?" *Akasema, *"Hiki ndicho nakiita
Unyakuo."*Kisha nikaona watu
wakivunja milango ya kanisa, wakitaka kuja
ndani, na kupayuka, "*Watoto
wangu wako wapi? Wote *
*wametwaliwa!" *Watoto wote katika ulimwengu wametwaliwa kwa sababu Mungu
hata waacha nyuma.
Mtu wa kwanza kuingia katika kanisa alikuwa
ni Mwalimu wa kwaya, akapayuka, *"
Kanisa liko wapi!*
*nimeachwa nyuma! Nimebaki! Nimebakia!" *Baada ya mwalimu wa kwaya, niliona
wachungaji
wengine, waumini wa wakiume na wa kike,na
waangalizi wa kanisa wote
wanalia, *"Nimeachwa*
*nyuma!" *Wazazi wengi na wanandoa wengi waliwatafuta wale wawapendao na
watu wale walioko
kanisani wakawajibu, *"Muwapendao hawako
mahali hapa! Bwana amewachukua," *Watu
hawa
walianza kulia, *"Yaani kumbe ni kweli, Yesu amekja na kuchukua bibi
harusi!"*.
Watu walikuwa wakilia na kuomboleza
wakitamani kama tu wangemuamini Yesu
Kristo. Kila mtu
asiyemuamini Yesu kama Masihi amepotea! Nikaona watu wengi na wachungaji
wakilia na watu
walianza kuwadai wachungaji, *"Kwa nini
wewe hukuhubiri ukweli, kwa nini
hukufundisha utakatifu*
*na kunionya mimi kuhusu yote haya? Ni kwa sababu yako nimeachwa nyuma! "*Wengi
wataachwa
nyuma kwa sababu hawaishi maisha
matakatifu. Tunahitaji kuhubiri utakatifu
wa kweli na kuwafundisha
watu toba ya kweli! Niliona jinsi watu walivyopiga wachungaji na
kuwakatakata na kuondoa nywele
zao. Wachungaji walilia na kuomba watu
wasiwadhuru. Watu hawakuacha kwa
sababu walikuwa sasa
na mapepo. Kuna makanisa kabisa ambayo yataachwa
nyuma. Nilimuona kaka mmoja alikuwa
anajaribu
kuyakwarua macho yake mwenyewe kwa
sababu ya huzuni kuu. Na watu walipigiza
vichwa vyao sakafuni na kwenye kuta kwa sababu
hawakutambua kuwa Yesu alikuwa ndiye
jibu pekee. Kwa sababu
watu walitaka kuendelea katika dhambi na
uovu na kuishi maisha vile
walivyotaka. Watu walijikata wenyewe na kupigiza vichwa vyao mpaka
kiasi cha kuona fuvu zao zikiweka ufa
na walianguka chini.
Damu ilitiririka bure ndani ya kanisa kwa watu
ambao walikuwa wakijijeruhi
wenyewe. Kisha nikaona kijana akipiga kelele kwa Mungu, *"Tafadhali
Bwana, nichukue!" *Alikuwa
amechelewa mno. Yesu
alikuwa tayari amekwishakuja na kulipokea
kanisa lake. Hapo nilianguka
chini kwa sababu niliona mambo mengi zaidi ya kutisha.
Yesu akaniambia, *"Katika dhiki kuu, kutakuwa
na matatizo makubwa haijawahi
kutokea kabla."*
Kisha nikauliza*, "Kwa nini watu wanaruka
nyuma baada ya kuumizana vibaya wao wenyewe?" *Bwana
Yesu akajibu, *"Kwa sababu kwa wakati huu,
watu watatamani kifo, lakini
hawatakipata. Kifo*
*kitakuwa kimetoweka katika uso wa dunia*.
Nilimwuliza Bwana, "Kwa nini wachungaji wote hawa na
watu wameachwa nyuma?" Na Bwana
akasema, "Kwa sababu ninajua mioyo yao.
"Mungu anatujua sisi
.. Anajua yote ya mioyo yetu. Nilianguka chini,
karibu kuzimia. Yesu alisema, *"nimetaka kukuonyesha *
------------------------------
*Page 9*
9
*hili ili kwamba uonye kanisa langu na kuwapa
matumaini. Waambie kwamba kama watu watatubu*
*sasa, mimi nitawasamehe wakati bado kuna
muda. Nitafanya jambo kubwa
katika dunia. "*
Tafadhali,fungua macho yako. Kanisa la kiinjili
nchini Chile linaongezeka. *"Waambie watu wangu*
*kama wataomba msamaha, nitawasamehe."
*kisha nikaona maono mengine na
nikaona moto umefunika
mbingu nzima. Yesu akasema, *"Je, umeweza
kuona? Huo moto uliona juu ya nchi/dunia, ni moto juu*
*ya nchi ya Chile. Kwa sababu Chile itakuwa
kwa ajili ya Kristo! Mungu
ataibadili Chile! *" kisha
nikaona moto unataka kuja juu ya Chile na
Yesu akasema," *Macho ya Baba yangu yako juu ya Chile.*
"Mara moto utakapokaa juu ya Chile, nchi
nyingine zitaona na kujua kuwa
Mungu yuko mahali hapo.
Kanisa lote duniani litafurahi kwa sababu
Uwepo wa Mungu unatembea Chile. Bwana alinichukua
katika maono mpaka mahali paitwapo "Paseo
Humada
"
Akanionyesha watu waliokuwa vilema na walio
na matatizo. Kisha nikaona waamini wa kweli
wakiomba juu ya viwete wasio na miguu na
wakitiisha viungo kukua. Viungo
vilitii na kukua mbele ya
macho yao. Watu wasio na mikono waliiota
mikono kwa upya mara moja. Wakati huu, Bwana
ataonesha miujiza ya uumbaji. Katika
makanisa watu ataponywa. Katika siku
hii, wafu watafufuliwa na
Mungu akutumia wewe ndani ya Chile kufanya
miujiza hiyo kama mitume wa zamani walivyofanya
katika Biblia.
Huo ni ufunuo mzima ambao Mungu alinipa
(Ricardo Cid). Yeye anakuja hivi
karibuni. Maranatha! Amina!
*Ndugu aliyefasiri ufunuo wa Ricardo Cid wa Masaa 8 Mbinguni ni Peter
Kahale ni kijana aliyeokoka na*
*anampenda Yesu na mwenye shauku ya
kuhubiri injili ya Yesu Kristo.
UNABII WA KWELI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni