------------------------------
*Page 11*
11 Hakuna maji kabisa kuzimu.
Nilitambua kuwa mahali ilipo kuzimu ni katikati
ndani ya duni. Hapo ndipo
mahali ilipo, ndani katikati ya dunia.
Nilitambua hivyo nilipokuwa kama maili 3700
ndani chini ya dunia.Tunafahamu kwamba kipenyo cha dunia ni
maili 8000. Na nusu ya kipenyo hicho ni kama
Maili 4000. Nilikuwa kama
maili 3700. Katika waefeso 4:9
<http://www.biblegateway.com/passage/? search=Ephesians%204:9;&version=31 ;>
inasema kwamba Yesu alishuka mpaka chini
pande za dunia/nchi.
Hesabu 16:32 inasema,
*Na nchi ikafunua kinywa chake na
kuwameza,na watu wa nyumba zaona wote walioshikamana na*
*Kora, na vyombo vyao vyote.*
Hapo ndipo Kuzimu ilipo sasa. Baadae Kuzimu
na mauti vitatupwa katika moto
wa Jehanamu na kutupwa katika
giza kuu. Hiyo ni baada ya hukumu, Lakini kwa sasa iko duniani.
*(Pepo)*
Nilikuwa pembezoni mwa shimo la kuzimu na
nikaona mapepo yote haya
yamejipanga katika kuta, yana ukubwa
tofauti tofauti na maumbo ya kila namna, mabaya, viumbe vibaya kiasi
unachoweza kufikiri. Walikuwa
wamejikunja, wameharibika, wakubwa na
wadogo. Kulikuwa na ng"e wakubwa,
wakubwa hivi.
*(uefu futi5)* Panya,
nyoka na minyoo, kwa sababu biblia
inaongelea kuhusu minyoo yenye
inayoambaa (
<http://www.biblegateway.com/passage/? search=Isaiah%2014:11&version=50 >Isaya
14:11
<http://www.biblegateway.com/passage/? search=Isaiah%2014:11&version=50 >)
<http://www.biblegateway.com/passage/? search=Isaiah%2014:11&version=50 >.
Kuna kila aina
ya viumbe wabaya kila eneo na inaonekana
kana kwamba imefungwa kwa
minyororo kwenye kuta.Nikashangaa
*"Kwa nini vitu hivi vimefungwa kwenye kuta"*. Sikuelewa, lakini kulikuwa
na andiko katika
<http://www.biblegateway.com/passage/? search=Jude%201:6;&version=50 ;>Yuda
1:6 <http://www.biblegateway.com/passage/? search=Jude%201:6;&version=50 ;>linasema,
*"Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe,
lakini wakayaacha makao yao
yaliyowahusu, amewaweka*
*katika vifungo vya milele chini ya giza kwa
hukumu ya siku ile kuu;"* Na hivyo ninahisi hiki ndicho nilikiona, sijui,
lakini hicho ndicho
kilichonitokea. Nilifurahi kwa sababu sikutaka
wanisogelee. Walionyesha kunichukia sana!
Hiko kilikuwa kitu kingine
ambacho sikukielewa, hawakuwa tu ni viumbe, walikuwa na chuki kubwa kwa
wanadamu. Hivyo nilifurahia kuona
wamefungwa kwenye kuta.
Nilianza kupaa shimo hili kwenye tanuru hili, na
kuachana na miali. Mara
kukawa na giza, lakini niliweza kuona mapepo yote haya pembeni ya tanuru na
walikuwa na nguvu kubwa sana.
Nikafikiri,*"Nani anayeweza kupigana *
*nao viumbe hawa. Hakuna anayeweza
kupigana nao viumbe hawa." *Lakini
bado,Hofu ile ilikuwa ni kubwa sana, sikuweza kabisa kusimama juu ya hofu hii.
*(Hakuna Matumaini)*
Kitu kibaya Kuzimu, kitu kibaya, kitu kibaya
kuliko mateso yote, niliweza
kutambua, kwamba kuna maisha
yanaendelea hapa duniani. Na ya kuwa watu hapa juu, watu wengi, hawana hata
habari kuwa ulimwengu huu uko
hapa chini na ni halisi! Hawajui kabisa kuwa ni
ulimwengu mwingine na
halisi huko hapa chini na kuna mabilioni
ya watu wanaumia na kuomba nafasi nyingine ya pili, kama wangekuwa na
nafasi ya kutoka tu mahali pale. Lakini
hawawezi kupata nafasi nyingine tena, na
wanakuwa vichaa kabisa kuona kuwa
hawawezi kuwa na fursa ya kuwa
na Yesu, kwamba wameishia mahali pale maisha yao yote. Hiki ndicho kitu
kibaya kuliko vyote, kwamba
hakukuwa na matumaini ya kutoka nje.
Nilifahamu hivyo. Nilitambua umilele.
Niliweza kuelewa umilele. Hapa
duniani, hatuwezi kuwazia, Hatuwezi kuujua. lakini pale niliuelewa. Nilijua
nitakuwa huko milele na milele, wala
sikuwa na matumaini ya kutoka nje. Niliwaza
kuhusu mke wangu. Sikuweza
kwenda kwa mke wangu! Nimekuwa
nikimwambia kama tukitenganishwa na kitu chochote kwa namna yeyote labda
tetemeko au kitu cha kutisha,
------------------------------
*Page 12*
12
nilisema *"Nitarudi*. *Nitakutafuta. Nitakurudia kama tumeachanishwa." *Lakini
hapa sikuweza kumrudia. Sikuweza
kumuona tena. Hakuwa hata na wazo lolote ni
wapi nilikuwa na sikuweza kamwe
kuongea naye tena milele. Hilo
wazo tu lilinisumbua sana! Kutokuwa na uwezo wa kuongea naye, kuwa naye, na
kwa yeye kutojua ambapo mimi
nipo, na sikuwa na matumaini kwa milele
kutoka nje! Unakuwa unaelewa, kuwa
huwezi kutoka hapo, milele!
Angalia duniani kuna matumaini siku zote. Hata watu katika kambi za mateso
huwa na matumaini ya kutoka nje,
au kufa angalau, ili waondokane na taabu.
Lakini hatujawahi kabisa kukosa
matumaini kama ilivyo kuzimu.
Katika Isaya 38:18 inasema, *"Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia
kweli yako."*
Hakuna matumaini, na kweli ni Yesu
*(Yesu akatokea)*
Wakati huu, nilikwenda juu ya tanuru hili, na
nikiwa na hofu kubwa, sina matumaini nimepotea, na nikiwa
naogopa mapepo haya. Kwa ghafla, kwa
ghafla tu, Yesu akajitokeza! *"Usifiwe
wewe Bwana"*, Yesu alijitokeza.
Mwanga huu mkali ulimulika mahali pale. Mimi
niliona tu umbo lake, umbo la mwanadamu. Sikuweza kuona uso
wake, mwanga ulikuwa mkali sana. Niliangalia
katika mwanga huu na kuona
umbo lake tu. Na mimi nikapiga
magoti yangu nikaanguka. Sikuweza kufanya
jambo lolote tofauti na kuabudu. Nilijisikia furaha. Sekunde moja
iliyopita nilikuwa nimepotea milele, na sasa
ghafla natoka nje ya eneo
hili, kwa sababu nilikuwa tayari nimemjua
Yesu. Watu wale hawawezi kutoka nje, lakini
mimi naweza kwa sababu nilikuwa tayari nimeokolewa. Nilijua na
kuelewa kwamba kulikuwa hakuna njia a
kutoka nje ya eneo hili, ni kwa Yesu
pekee. Yeye ni njia pekee ya
kukufanya usiende mahali hapa.
Ufunuo 1:6 inasema Yohana, alipokwenda mbinguni, alimuona Yesu, na sura
yake ilikuwa kama jua liking'aa kwa
nguvu zake. Naye alipomuona kwake,
akaanguka mbele ya miguu yake kama mtu
aliyekufa. Hivyo ndivyo nami
nilifanya. Nilianguka mbele ya miguu yake kama mtu aliyekufa. Sasa unaweza
kufikiria nilikuwa na maswali
milioni ya kumuuliza, lakini wakati uko pale, kile
unachoweza kufanya ni
kumwabudu na kumtukuza jina lake
Takatifu, na kumshukuru kwa kile alichotuokoa.
Nilipotulia sasa, angalau kiasi ambacho
naweza kuanza kutengeneza mawazo,
Niliwaza kumwaambia Bwana, Hata
sikumbuki kama nilimuuliza kwa sauti kubwa,
niliwaza tu na akanijibu. Mimi nikasema, *"Bwana kwa nini*
*umenileta mahali hapa? Kwa nini umenileta
mahali hapa?" *Akaniambia *"Kwa
sababu watu hawaamini kwamba*
*eneo hili ni halisi*." Alisema *"Hata baadhi ya
watu wangu mwenyewe hawaamini eneo hili ni halisi."*
Nilishitushwa kwa usemi huo. Nilidhani kila
Mkristo anaamini Kuzimu. Lakini
si kila mtu anaamini katika uhalisi
wa moto wa Kuzimu. Nilisema Bwana "*kwa
nini umenichukua mimi*?" Lakini hakujibu swali hilo.
Mimi sijui ni kwa nini yeye alinichukua mimi
kwenda huko. Uwezekano wa mimi
kwenda mahali hapo ulikuwa ni
mdogo. Mke wangu na mimi huwa tunachukia
sinema za maovu. Tunachukia lolote baya. Sipendelei hata maisha
ya majira ya kiangazi, sana napendelea kiasi
kidogo cha joto. Ni machafu.
Hakuna mpangilio. Ni kero muda wote
na machafuko na machukizo. Na mimi
upendelea kila kitu chenye utaratibu na ubora. Hakunijibu swali hilo.
Akaniambia, *"Nenda ukawaambie kwamba
ninachukia mahali hapa, kwamba si
mapenzi yangu kwa yeyote *
*mmoja wa viumbe wangu kwenda mahali
hapa, hata mmoja! Sikuumba hili kwa ajili ya mtu. Hii ilifanyika kwa*
*ajili ya shetani na malaika zake. Unatakiwa
kwenda na kuwaambia! Nimekupa
kinywa, wewe nenda na*
*uwaambie. "*
Nikajifikiria, *"Bwana, hawatakwenda kuniamini*. *Watanifikiria mimi ni
kichaa au nilikuwa na ndoto mbaya." *
*Namaanisha je wewe usinge fikiria hivi*?
Kama Nilipofikiria hivi, Bwana
akanijibu akasema, *"Siyo kazi yako*
------------------------------ *Page 13*
13
*kuwashawishi. Ni kazi ya Roho Mtakatifu!
Wewe nenda na uwaambie!" *Na
niliitika ndani, *"Ndiyo Bwana!" Ni*
*sahihi kabisa, nitakwenda na kuwaambia." *Hutakiwi kuwa na wasiwasi na
hofu juu ya mtu anafikiria nini juu
yako, wewe unachotakiwa tu ni kwenda na
kufanya hivyo na kumuachia Mungu
afanye yaliyobakia. Amina? Nami
nikasema," *Bwana, kwa nini wananichukia sana? "" Kwa nini viumbe hawa
wananichukia? *"Akasema," *Kwa*
*sababu umefanywa kwa mfano wangu na
wananichukia mimi. "*Unajua shetani
hawezi kufanya kitu chochote
dhidi ya Mungu. Hawezi kumdhuru Mungu, kwa kusema, lakini anaweza kuumiza
viumbe vyake. Ndiyo maana
shetani anachukia watu, na anawadanganya
na kuwapeleka kuzimu. Naye anaweka
magonjwa juu yao, kitu
chochote anaweza kufanya ili mradi auumize viumbe wa Mungu.
*(Amani ya Mungu)*
Na kisha Mungu akanijaza Mawazo yake.
Aliniruhusu niguse kiasi cha moyo
wake, ni kiasi gani anampenda
mwanadamu. Ajabu, sikuweza hata kulichukulia hili. Ilikuwa ni zaidi hakuna
mfano wake. Upendo alionao kwa
mtu, huwezi ukauchukulia katika mwili huu.
Unajua ni kiasi gani tunawapenda
wake zetu na watoto wetu? Naam
upendo tulionao hatuwezi hata kuulinganisha na upendo wa Mungu kwetu sisi.
Upendo wake ni mkubwa zaidi
kuliko upendo wetu na uwezo wetu wa
kupenda. Ni sawa tu kama inavyosemwa
katika *Waefeso 3:19*, *"... ili kujua*
*upendo wa Kristo ambao hupita maarifa ..." *Inakwenda mbali kupita
maarifa, huwezi hata ukapata ufahamu wake.
Sikuamini kuona ni kiasi gani alimpenda
mwanadamu, kwamba anakufa kwa ajili
ya mtu mmoja tu ili asiende
mahali hapo. Na anakuwa na uchungu mwingi kuona mmoja wa viumbe vyake
anakwenda mahali hapo.
Inamuumiza Bwana, Analia kuona mtu mmoja
anakwenda. Na nilijihisi vibaya
kwa Bwana.
Nilihisi moyo wake, basi akaniacha niguse kidogo moyo wake. Alijisikia
huzuni kwa viumbe wake kwenda mahali
pale. Nikawaza *"Imenipasa kutoka nje na
kushuhudia na kuchukua kila pumzi
ya mwisho kuwaambia dunia habari*
*za Yesu, Jinsi alivyo mzuri." *Naama ka kuwa, tuna injili. Ni habari
njema. Ni habari njema, na dunia haijui.
Imewapasa kuambiwa! Unajua, inabidi tushiriki
maarifa haya. Watu wanakosa
elimu katika eneo hili. Mungu
anataka sisi tushiriki pamoja nao jinsi yeye alivyo mzuri, na jinsi Yeye
anachukia mahali hapo.
Akaniambia pia, *"Waambie ninakuja hivi
karibuni, karibu sana." *Akasema
tena, *"Waambie ninakuja hivi*
*karibuni, karibuni sana." *Sasa nafkiri, kwa nini sikumwambia, "*Ni nini
umaaanisha Bwana?'hivi karibuni' ikoje*
*kwako?*" Hivyo ndivyo jinsi tunafikiri. Lakini
sikuweza kuuliza vitu hivyo
wakati huo. Unataka tu uendelee
kumwabudu sana. Amani ya Mungu inayokuja juu yako kuwa karibu naye
haielezeki. Nimekuwa katika huduma
za upako, lakini hakuna cha kulinganisha na
upendo na amani ya Mungu
unayojisikia kuwa karibu naye.
Na kisha nikatazama juu na nikaona mapepo hayo juu ya ukuta, walionekana
wakiwa na uso wa ukali, walikuwa
wanaonekana kama mchwa kwenye ukuta!
Walionekana kama mchwa! Bado walikuwa
ni wakubwa, lakini kwa
uwezo wa Mungu uliokaribu nawe, nguvu zote za uumbaji wa Mungu, walikuwa
wanaonekana kama mchwa
kwenye ukuta. Sikuweza kwenda juu yake.
Nikafikiri, *"Bwana ni kama mchwa
tu hawa!" *Naye akasema, *"Wewe*
*unachotakiwa tu ni kuwafunga na kuwatoa nje kwa jina langu." *Nikafikiri *"Kijana,
nguvu alizotoa kwa kanisa."*
Hivi vitu ambayo vilikuwa na ukali, tusingeweza
kushindana navyo bila Yesu,
hakuna. Wanahasira, lakini
unapokuwa pamoja naye, ni bure tu ! Ujasiri ukaja ndani yangu, nilipoona
viumbe hawa nilihisi kama niseme,
*"Nyie viumbe mliokuwa mnanitesa, mkataka
kunigawana? Haya njooni! Haya
njooni sasa!" *Labda inawezekana
nafsi yangu ilijiinua au kitu kingine, unajua, Niliwaza, *"Yesu wafate."*
*(Kuondoka Kuzimu)*
Tulipoondoka, tukapanda juu ya uso wa dunia.
Tulikwenda juu, kwa sababu
tulikuwa bado katika shimo. Punde
sikuweza kuiona tena, lakini ilikuwa ni kama upepo wa kisulisuli, kimbunga
kikubwa nasi tuko ndani yake. Ilibidi
------------------------------
*Page 14*
14
kuendelea kwenda juu, ili tutoke nje yake ilivyoonekana. Tulipofika juu
yake, nikaangalia chini duniani na
tulikuwa juu namna hii. Mviringo wa dunia
ulionekana kama hapo. Nifuraha
kuangalia tena katika nchi! Najua
Mungu aliruhusu hilo kwa ajili yangu. Tungeweza kuondoka kwenye handaki kwa
namna yoyote ambayo
Angetaka. Alijua ndani ya moyo wangu,
kwamba nilipokuwa mtoto siku zote
nilitamani kuona dunia inaonekana
vipi kutokea angani. Labda ni kwasababu niliangalia sana, Safari ya nyota
au kitu, unajua? Nilijiwadhia itakuwa
vizuri kweli kuona dunia, na kuona ikielea
angani bila kushikiliwa na
chochote. Kama Biblia inavyosema. Inasema
katika Ayubu 26: 7, *Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo
na kitu, Yeye lipo duniani juu
ya chochote.*
Kama ukiangalia, unafikiri, *"Ni nini kinashikilia
hii dunia juu? Nini
kinafanya izunguke kwa ukamilifu?" *Mungu anadhibiti hilo. Uwezo wa Mungu ulionifunika,
ulikuwa ni wa kutisha. Ana
uwezo sana. Kila kitu kimoja kimoja
viko chini ya udhibiti wake. Si tu nywele juu ya
kichwa chako zishukazo
mpaka chini kwamba hawezi kuzijua kwa idadi. Sio tu ndege aliyeanguka sakafuni
kwamba hawezi kujua. Nilikuwa
nimejazwa na mawazo haya. Mungu ana
nguvu sana. Ilinishangaza sana. Kuna
maandiko katika Isaya 40:22 yanayosema
Bwana anaketi katika muhimili wa nchi/dunia. Pale nilikuwa juu ya mhimili wa
dunia. Hata nikawaza pia, *"Bwana,
kwa nini kabla ya Christopher *
*Columbus wasingesoma maandiko na kujua
kuwa nchi/dunia ilikuwa ni
mviringo." *Unajua? Watu walishangaa, walidhani ilikuwa ni tambarare?
Hata hivyo, tuliporudi chini tulipita katikati ya
ngao; Nilijua tulikuwa
tukipita katikati ya ngao za joto lililokuwa
lililozunguka duniani. Nilijua tu hivyo. Hata
niliwaza mawazo ya kijinga, hapa niko na Mungu, na "*sijui *
*atakwendaje kupita katikati ya ngao ile ya
moto?" *Unajua jinsi ambavyo
angani wanavyotakiwa kupenya ngao
hiyo kwa pembe/makadirio sahihi. Tulikwenda
kwa njia hiyo na hakuna tatizo lolote gani lillilotokea. Hakuna cha
kushangaa! Nina hakika Bwana alitazama kwa
macho yake na kusema ninaweza tu
kupita, Kuna maandiko Zaburi
47: 9 inasema kwamba,
*... Kwa ngao za dunia ni zake Mungu ...* Mungu yuko katika udhibiti wa kila kitu, kila
kitu. Sikutaka aondoke.
Nilitaka kuwa katika uwepo wake. Tulikuwa
tunashuka kutokea juu kwa kasi California.
Tulikuwa tunashuka kwa haraka,
haraka sana, tukaingia mpaka nyumbani kwetu. Na niliangalia nikaweza
kuona kutokea kwenye paa la nyumba
yetu. Na niliweza kujiona
mwenyewe nimelala juu ya sakafu. Hili kweli
lilinishangaza sana, kwa sababu
niliona mwili wangu umelala hapo, nikawaza, *"Huyo hawezi kuwa mimi, mimi niko
hapa, huyu ni mimi*!" Unajua,
wewe hujawahi kuona wawili ambao
ni wewe mwenyewe. Hapa nilikuwa nimelala
pale nikawaza, *"Huyo si mimi
halisi*." Na kwamba andiko Paulo analolisemea, kwamba tuko ndani ya hema (2
Wakorintho 5:1), likanijia kwa
nguvu. Nikawaza *"hiyo ni hema, si*
*kitu. Huyo ni wa muda. Huyu ni mimi halisi."
*Hiyo ndiyo umilele
inavyokuwa. Kwamba haya ndiyo maisha tunayojisumbua nayo, nikakumbuka pia sisi ni
mvuke, maisha haya ni kama
mvuke kama katika Yakobo 4:14
inazungumzia juu ya ufupi wa maisha haya. Ni
muda mfupi. Miaka mia moja
kama ukiwa hai, si kitu! inapotea kama mvuke. Na nikawaza, *"Imetupasa kuishi
kwa ajili ya Mungu." *Tunachofanya
sasa, hapa, kinaandaa umilele.
Imetupasa kushuhudia. Imetupasa kutoka nje
na kuokoa waliopotea. Hatuwezi
kuwa tunajisumbua na vitu hivi vidogo kila siku vimetufunga na tunahangaika
navyo. Tunahitaji kweli kutoka
nje na kuhubiri injili na habari
njema, kwa sababu hii ni zaidi ya haraka sana.
Nikaona mwili wangu umelala hapo na nilifikiri
ilikuwa tu kama vile umetoka nje ya gari yako na ukangalia
nyuma tena kwenye gari yako. Huyo si wewe,
ni gari yako. Ni vile
imekuzunguka tu. Hivyo ndivyo jinsi
ilionekana kwangu. mwili huo umenizunguka tu
hapa duniani, lakini huyu ndiye mimi halisi. Na nikafikiri,
------------------------------
*Page 15*
15
*"Bwana usiondoke, usiondoke". *Nataka
kuendelea kuwa na wewe kwa muda. Lakini aliondoka. Nikaurudia mwili
wangu, na kitu kikanivuta kwenye mwili wangu,
kama vile nimerudishwa kwenye
pua yangu au kinywa changu.
Wakati huo, alipoondoka, hofu yote, mateso,
na adhabu zote zilinirudia kwenye mawazo yangu! Kwa sababu
inasemwa katika Biblia (1 Yohana 4:18),
*"Upendo wa kweli hufukuza mbali
hofu." *Hivyo nilikuwa karibu na
upendo kamili muda wote huo, sasa
akaniacha, na alipoondoka, kwa ghafla hofu yote na machungu ya kuzimu
yaliingia mawazoni mwangu. Sikuweza
kuvumilia, sikuweza kuvumilia! Nikapiga
mayowe. Nilikuwa katika
maumivu/uchungu makali/mkali. Sikuweza
kuishi nayo. Nilijua kuwa mwili huu haukuwa na uwezo wa
kujisimamia kwa aina hiyo ya hofu. Huwezi
ukajizuia juu ya shinikizo hiyo.
Mwili wako hauna nguvu za kutosha
kujizuia. Hivyo wakati huo sasa niliomba na
niliweza wa kuomba, *"Ondoa katika akili yangu!"*
Kwa asili, ni lazima upitie kila aina ya ushauri
nasaha ili kutoka nje ya
aina hii ya kiwewe, lakini Mungu aliondoa
hili nje, papo hapo aliondoa kiwewe, majeraha.
Aliniachia kumbukumbu, lakini aliniondolea kiwewe na hofu.
Nilimshukuru.
Hata hivyo, baada ya hayo, mambo mengi
yaliyotokea, Ningependa tungekuwa na
muda wa kugusia yote ambayo
Mungu alithibitisha yangetokea kwangu. Kama kuna mtu hapa usiku wa leo, ambaye
hamjui Bwana; unatakiwa ujiulize
swali. Unatakiwa kusema, *"Je,*
*nawaamini watu hawa, kile walichokiona ni
halisi, watu wote hawa na mimi
mwenyewe?" *Lakini cha muhimu zaidi, nini Neno la Mungu linasema kuhusu
Kuzimu. Je, unataka kuchukua
nafasi hiyo na kusema, *"Hapana mimi *
*siamini hii kama ni kweli,*. "Basi tupa Neno la
Mungu lote, na sisi sote
tunaojaribu kukuambia. Je, uko tayari kuchukua nafasi hiyo milele yako yote? hiyo
naona ni ujinga kwangu. Huwezi
ukamruhusu shetani akudanganye.
kile kiumbe kikubwa pale mwishoni kikicheka. *
(inavyoonekana katika video) *hivyo
ndivyo jinsi shetani atakuwa ukifika kuzimu. Atakucheka, kwa sababu
ulikuwa na nafasi ya kupokea Bwana
na umeikosa. Lakini utakapokuwa
pale, hakuna kurudi nyuma. hakuna kabisa
kurudi nyuma. Utakuwa huko pale
umepotea milele. Unaweza kuwa unajisemea wewe mwenyewe.
*"Mimi mzuri. Mimi ni mtu mzuri
sana. Sistahili mahali pale." *Na
pengine ni mzuri, ukilinganishwa na watu
wengi. Lakini sivyo ambavyo
unahitaji kujilinganisha mwenyewe. Tunahitaji kujilinganisha wenyewe na kiwango
cha Mungu. Kiwango cha chake
kiko juu sana kuliko chetu.
Anasema katika Neno kwamba kama ukisema
uongo mara moja, mara moja tu
katika maisha yako yote, inakufanya mwongo. Kama ukiiba kitu kimoja
tu katika maisha yako, kwa mfano
kibanio cha karatasi, dakika
kadhaa za bosi wako, au kitu chochote, mara
moja tu. Inakufanya uwe mwizi.
Kama ukiwa na hasira bila sababu, kama haukumsamehe mtu aliyekufanyia kitu
kibaya juu yako, kama ukimtamani
mwanamke, chochote ya mambo
hayo mojawapo, kama wewe ulifanya hayo
mara moja tu, Hii inakufanya uwe
mwenye dhambi, na hivyo hauwezi kuingia mbinguni. Hivyo unaweza kuona kila
mmoja wetu amepungukiwa. Sote
tumepungukiwa na hatuwezi
kufika pale kwa matendo yetu wenyewe. Tito
3:5 inasema,
*Wala si kwa matendo ya haki ambayo tumefanya, bali kwa rehema yake
alituokoa ...*
Amina, inategemea na jinsi unavyolinganisha.
Ni kama mwanamke ambaye ameona
kundi la kondoo katika
mlima, na wote walikuwa weupe sana na wazuri upande wa mlima. Akasema, *"Angalia
hao kondoo weupe,*
*angalia jinsi walivyowazuri, weup*e." Kisha
alikwenda kitandani na ghafla
usiku barafu ikaanguka. Alitazama
asubuhi yake na kuona kondoo wote wakiwa katika hali ya kufa, wachafu na
wakijivu kulinganisha na barafu
------------------------------
*Page 16*
16
nyeupe. Hivyo tunapaswa kujilinganisha sisi wenyewe na Mungu. Viwango vyake
viko juu zaidi ya vyetu. Hivyo
tunamuhitaji Mkombozi. Hatuwezi kufika pale
sisi wenyewe. Mungu alifanya
hii kuwa zawadi ya bure. Alisema
katika *Yohana 14:6, "mimi ni njia, kweli na uzima. hakuna awezaye kuja kwa
baba , isipokuwa kupitia mimi."*
Yeye ni njia pekee ya kutoka hapo.
Kwa hivyo kama kuna yeyote Yule asiyemjua
Bwana, yeyote Yule mahali hapa
ambaye hakuwahi kumsihi Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yake.
Haukuwahi kufikia maamuzi haya ambapo
inakubidi upaze sauti yako
kwa mdomo wako na kumsihi aje maishani
mwako, Unaweza kusimama? Kama kuna
yeyote mahali hapa unaweza ukasimama, Kwa ajili ya Yesu? Usimruhusu
shetani, kile kiumbe kikucheke.
Simama hivi sasa, ukiwa bado
unanafasi, kwa sababu haujui ni muda gani
tulionao. Haujui labda kesho
unaweza kuaga dunia, na kuishia mahali pale.
Ngoja nikueleze, mahali pale, moto tu
wenyewe ni ngumu kuweza kuvumilia.
wale watu tuliowaona wakiruka
kutokea katika minara wa new York.
Wanashikana mikono yao na kuruka. Inatisha kiasi gani. Unajua kama
umewahi kuwa juu na ukaangalia chini, kuruka
ni kitu kisichofikirika.
Lakini kule ni lazima ukabiliane na moto.
Na hiyi ni kwa muda wa sekunde
tano,unakuwa umeungua tayari, na moto wa pale ni kama digrii elfu mbili.
Wanasayansi wanasema katikati ya dunia ni
kama digrii kumi nna mbili elfu.
Kwa hiyo inakupaswa kuvimilia
moto ule kwa umilele. Kama uko tayari kupitia
hayo, huo utakuwa ni ujinga sana. Sasa ni wakati muafaka….
*(mtangazaji anaongea)*
Biblilia iko wazi sana, isi wote ni wenye
dhambi,na yeyote atakayeliita
jina la Bwana ataokolewa. Yesus anasema
kama ukinikiri mimi mbele za watu , naye mbele zao atakiri jina lako mbele
ya baba yake na malaika watakatifu.
na kama ukinikataa mimi mbele ya watu,
nitakukana mbele ya baba yangu.
Nataka nikuambia jambo la kufanya
kama haujawahi mbele za watu kumkiri Yesu Kristo kuwa ni Bwana na mwokozi
wa maisha yako,au kama hauna
uhakika kuwa mbinguni ni mahali ppako pa
milele, kumbuka Yesu alisulubiwa
uchi msalabani, sokoni,alisulubiwa
pale kwa ajili yako, Alivumilia aibu yako. Kama ukiomba ombi hili kutokea moyoni,
Mungu ataokoa nafsi yako, na atakupa
nafasi kwa wakati ujao
kulithibitisha hili mbele za watu. Omba nasi,
hasa wale walio kwenye
kongamano hili na wanajua imewapasa hivi. *"Mungu naamini katika wewe. Wewe ni
muumbaji wangu. mimi ni mwenye dhambi.
Nimetenda dhambi katika*
*maeneo mengi, kwa kukusudia, na
kwakutokusudia. Nimepungukiwa na utukufu
wako.Nimekosa chapa yako * *Ninanuka uovu. Yesu naamini katika wewe.
Wewe ni mtoto pekee wa Mungu.
wewe ni kondoo wa Mungu,*
*uichukuae dhambi ya ulimwengu, uliyechukua
dhambi zangu. Naamini ulukufa
msalabani.Ukamwaga damu* *yako isiyo na hatia kwa ajili ya nafsi yangu.
Naamini ulizikwa na siku ya
tatu ulifufuka. Uko hai millele na*
*milele. Nitakuita wewe Bwana. Nakuita wewe
mwokozi wangu. Nakupa wewe
maisha yangu. Nitakupenda,* *nitakutumikia siku zote za maisha yangu.
Nitakuwa wako, chema, kibaya,
uovu, mipango, ndoto zangu nakupa*
*kila kitu. Mapenzi yako yafanyike kwangu.
Naamini nimeokolewa. Si kwa
matendo mema, lakini kwa imani,* *kwa kukuamini. Kwa jina la Yesu ninaomba.
Amen."*
*>>>>> MUITO MKUU KABISA<<<<<*
Jibu hilo ni sahihi kabisa. Biblia inasema
mbingu inazizima kwa furaha kwa
mwenye dhambi mmoja anayetubu. Na sisi tunajua mfano wa yale yanayoendelea
mbinguni wakati mbingu
inaposhuhudia nini umefanya leo. Nataka
niwatangazie baadhi yenu, kisha nitahairisha
mazungumzo haya. Nataka kutoa
wito wa mabadiliko kwa wale baadhi yetu walioshuhudia haya. Tuna neema
ya kipekee kusikia yale ambayo
kaka yetu Bill aliyapitia. Nakwenda
------------------------------
*Page 17*
17 kutoa changamoto kwako na Ninakuonya,
usikubali hili isipokuwa uwe tayari
kwa ajili ya maisha ya Roho
maishani mwako. Sijaribu kukutania, nasema
tu usifanye hili kuwa ni ukiri
wako labda uwe umeamua kweli kweli. hivi ndivyo ilivyo. Kuna sehemu mbili. Moja,
sitaendelea tena kuogopa uso
wa mwanadamu. Kizuizi kimojawapo
kikubwa kwetu sisi ni kutofanya kama vile
unajua kuwa kuna Mbingu na kuna
Kuzimu. Sitaendelea kuogopa uso wa mwanadamu. Mbili, Nitaongea na kila
mmoja ninayemjua, Kuhusu Yesu,
mbinguni na kuzimu, kwa maisha
yangu yote. Hiyo ni dhamira/ahadi kubwa. Kila
mtu ninayemjua mimi ambaye
anahubiri/anawafikia watu kwa ajili ya Kristo anakuwa amefanya maamuzi haya.
Kwa nini sasa ufanye uhusiano na
mtu yeyote tu, kama si huu wa
kushiriki pamoja nao habari njema yenye
utukufu iokoayo roho zao na moto wa
Kuzimu. Ni kosa katika Roho kumjua mtu, kuzungumza nao, na kufurahi
pamoja nao, kufurahia uwepo wao, na
kamwe huwaambii kuhusu hili,
ya kuwa bila Kristo, watakwenda kuzimu. Kila
uhusiano unapaswa kuwa ni
mlango wa kuwasiliana kuhusu kweli ambayo umeshuhudia leo. Hiyo inaleta mantiki.
Kama wewe hauko tayari
kufanya hivyo, nitakuelewa. Lakini
kama uko tayari kufanya maazimio hayo
mawili, kama unakubaliana, sema haya
kwa Mungu, *"Mungu nakumini* *Wewe. Naamini katika Yesu Mwana wako, na
Roho Mtakatifu wako wa thamani.
Napokea changamoto ya*
*muda. Natangaza mwenyewe, huu ni ukiri
wangu. sitaendelea kuhofu uso wa
mwanadamu. Sitatumikishwa na* *maoni ya mtu. Utu wangu si kitu. Nachukia
hofu ya mtu. Nitamueleza kila
mtu kwa muda wa maisha yangu*
*yote yaliyobakia kuhusu Wewe Bwana Yesu.
Kuhusu Mbinguni na sehemu
inayoitwa Kuzimu. Nachukua* *hatua. sitaendelea kuwa wa tofauti, mtaabikaji
wa maisha yangu mwenyewe,
nisiyejali. Nakubali neno lako.*
*sitaogopa, nitalisema. Huu ni ukiri wangu kwa
Mwenyezi Mungu. *" Inua
jeshi lako Mungu, mji huu wote, taifa, na dunia, watu ambao wamebainisha majira
vyema kwa wakati huu wanaoishi.
Watu ambao wamekuja kuelewa
umilele ni kipindi tu kifupi kijacho, kuona kwa
uwazi katika utukufu wa
Mbinguni na ubaya wa Kuzimu, na wameamuru vipaumbele vyao viwe ni kumtii
Mungu. Sasa, tunaomba neema.
Wameweza kufanya uamuzi huu wa
kijasiri Mungu. Bila neema yako, hayatatokea
haya. Tunaamini neema yako
inatosha kutufanya tuishi katika neno la Mungu kama linavyoagiza. Neema, Neema,
Neema iwe juu ya watu wako hapa,
katika jina Yesu.
Purchase his complete testimony "*23 Minutes
in Hell*" at
<http://www.amazon.com/>Amazon.com <http://www.amazon.com/> *www.DivineRevelations.info/SWAHILI <http://www.divinerevelations.info/SWAHILI >* *
UNABII WA KWELI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni