*Page 10*
10
*Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu*
Akanipeleka mpaka kwenye kiwanda kikubwa
na ghala kubwa na kisha akanileta
kwenye nyumba yake binafsi.
Pale alikaa kuniambia: "Mimi ni Malkia wa
pwani (queen of the coast) na ningependa sana kufanya kazi na wewe.
Nina kuhahidi nitakupa utajiri na vyote
vinavyokwenda pamoja nayo, ulinzi
na vyote vinavyokwenda na hayo,
uzima na 'malaika' atakayekuongoza wewe. "
Akabonyeza kidude na mwili wa binadamu mbichi ukaja (katika vipande) ndani
ya trei(sahani) na tukala pamoja.
Akaamuru boa (nyoka) aje na akaniambia
nimmeze.sikuweza. Alisisitiza lakini
sikuweza, ninawezaje kumeza
nyoka aliyehai tena aina ya boa. Akutumia nguvu yake na nikammeza. Haya
yalikuwa ni maagano matatu: *mwili*
*wa binadamu na damu*, *boa(nyoka) *na
*malaika mapepo *walikuwa pale siku
zote ili kuhakikisha hakuna siri
iliyowekwa wazi. Lakini 'pepo' alipewa uwezo wa kuniadhibu
kama nikienda tofauti na pia
kiniletea chakula kutoka baharini
wakati wowote nikiwa hapa duniani. Niliahidi
kumtii siku zote daima. Na
baada ya ahadi hii alinipeleka na sehemu nyingine ya bahari, Hii sasa ilikuwa ni
kisiwa. Kulikuwa na miti na
kila mmojawapo ya miti ulikuwa na
kazi yake tofauti:
- Mti wa sumu,
- Mti wa mauaji, - Mti wa kutaja/kuonyesha, na
- Mti kwa ajili ya tiba.
Alinipa nguvu ya kujibadili katika kila aina ya
mnyama wa baharini kama
kiboko, boa constrictor(Nyoka) na
mamba na kisha akatoweka kabisa. Nilikaa katika bahari kwa wiki nzima kwa
njia (kama ya mamba) aliyetajwa
hapo juu nikarudi tena duniani.
*Maabara za ulimwengu wa chini*
Nilikaa Lagos kwa wiki moja nikarudi baharini,
wakati huu nilikaa kwa miezi miwili. Nilikwenda katika maabara
za kisayansi kuona nini kilichokuwa kinatokea.
Nikaona madakitari wa akili
na wanasayansi wanafanya kazi kwa
umakini sana. Kazi ya wanasayansi hawa ni
kubuni mambo mazuri kama magari ya kifahari, nk, silaha mpya na
kujua siri za dunia hii. Na kama ingewezekana
kujua nguzo ya dunia
wanayoitaka, lakini Namshukuru Mungu,
MUNGU TU ANAYEJUA.
Niliingia katika chumba cha kubuni na huko nikaona sampuli nyingi za nguo,
manukato na aina mbalimbali za
bidhaa za urembo. Mambo haya yote
kulingana na Shetani ni kwa ajili ya
kuvuruga mitazamo ya wanaume kutoka
kwa Mwenyezi Mungu. Niliona pia miundo/ ubunifu tofauti ya umeme, kompyuta
na kengele. Pia kulikuwa na
TV ambapo walijua wale waliozaliwa tena
kuwa Wakristo katika ulimwengu.
Pale unaweza kuona na
kutofautisha wale ambao ni waendaji wa kanisani tu na wale ambao ni
Wakristo halisi.
Nikatoka katika maabara na kuingia katika
'chumba cha giza' na 'chumba cha
kukaushia. Chumba cha giza ni
mahali ambapo wanaua mwanachama yeyote anayeasi.Wanamuua kwanza kwa
kuchukua damu ya mtu huyo na
kisha wanampeleka mtu huyo kwenye chumba
chenye mashine ambapo itamsaga na
kuwa unga kisha
wanachukua unga na kuupeleka katika chumba cha kupakia ambapo wataufunga na
kuupeleka kwa waganga wa
kienyeji kwa ajili ya hirizi zao. Kulikuwa na
mambo mengi ambayo ni vigumu
kueleza kwa maandishi. Pamoja
na nguvu yote hii ndani yangu, nilikuwa bado sijahitimu kukutana na
Lucifer/shetani lakini tu nilikuwa na sifa ya
kuwa wakala wake. Yote sawa,ila niliridhika
kwamba mimi sasa nilikuwa na
nguvu na ninaweza kukabili,
changamoto na kuharibu vitu kadiri nipendavyo. Je, kunaweza kuwa na nguvu
nyingine yoyote ile popote pale
basi niliiweka katika mawazo yangu.
------------------------------
*Page 11*
11 *Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
aliojaliwa na Mungu*
*Sura3: Utawala wa uovu*
*« Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu;
mimi nalikuja ili wawe na
uzima, kisha wawe nao tele.» Yohana * *10:10*
Nilipokuwa nikirudi Lagos, niliendelea na
biashara yangu na baada ya wiki
mbili nikarudi tena baharini. Malkia
wa Pwani alinipa kile alichokiita "kazi yake ya
kwanza". Nilitakiwa niende kijijini kwangu na kumuua mjomba
wangu, mzee mmoja mganga maarufu
aliyehusika kwa kifo cha wazazi wangu
kulingana na taarifa yake huyo
Malkia.
Nilimtii na nikaenda lakini kwa sababu sikuwahi kuua hapo mwanzo, sikuwa na
ujasiri wa kumuua, badala yake
nilimuharibia dawa zake na kumuacha akiwa
hana nguvu. Kwa sababu ya hili
nililofanya alipoteza wateja wake
wote mpaka leo hii. Nikarudi kutoa ripoti ya zoezi hilo lakini alikuwa
hasira nami. Alisema matokeo ya kutokutii
maelekezo yake ilikuwa ni kifo, lakini kwa
sababu ya upendo wake kwangu
atanituma tena nirudi kijijini na kuua
wazee wawili ambao alisema waliunga mkono suala la mauaji ya wazazi wangu.
Kama hii ndio ilikuwa ni adhabu
kwa kutotii maelekezo yake au sio, mimi sijui.
Hata hivyo, nilitii na nikarudi kijijini na 'niliweza'
kuua watu hawa na
kupeleka damu yao kwake. Kutokana na kitendo hiki kilichotokea katika mazingira ya
kutatanisha ya kufa, wazee
katika kijiji wakaenda kuuliza kwa
mganga mwingine mwenye nguvu ambae kwa
kawaida huwa anatuma radi kuchunguza
muuaji ni nani. Kwa bahatimbaya kwa sabab ya watu hawa,
nilikutana na mganga kiroho ambapo
alikuwa akijaribu kuongea
namapepo na nikamuonya asiseme chochote
kama alipenda maisha yake. Alitoka
nje na akawaambia wazee waende nyumbani na kuomba msamaha kwa
mmoja kati ya watoto wao waliemuuzi
na hakutaja jina langu.
Radi aliyoituma ikarudi na ikapiga katikati yao
na kuua baadhi na kuacha
wengi wamejeruhiwa. Baada ya tendo hili la kwanza, nguvu ndani yangu ilianza
kujidhihirisha yenyewe.
Nilimuumbua msichana yeyote aliyekataa
kufanya urafiki nami nk.
*Mkutano wangu na Shetani*
Nikarudi Lagos. Siku moja, msichana mmoja aliyeitwa NINA alikuja kwangu.
NINA ambae wazazi wake
wanatokea Jimbo la Anambra alikuwa mzuri na
mrembo sana lakini anaishi sana
katika bahari, yaani ulimwengu
wa chini ya bahari. Alikuwa ni wakala mkereketwa wa Malkia wa Pwani(Queen
of the Coast) na alikuwa muovu
sana. Yeye aliwachukia Wakristo sana na
alikwenda mwendo mrefu kupambana na
Ukristo. Mimi nilikutana naye
kwa mara ya kwanza wakati wa ziara yangu ya baharini ya kwanza. NINA
alikuja kwa ajili ya kazi ya Malkia wa
Pwani.
Tuliondoka mara moja na nilipofika pale chini
niligundua kuwa tutafanya
kikao na Lucifer/Shetani. Shetani, katika mkutano huu, alitupa maelekezo
yafuatayo: Kupambana na waamini na
sio wasioamini, kwa sababu
wasioamini hao tayari ni wake. Baada ya
kusema hayo, mmoja wetu akauliza
swali: "Kwa nini?" Akasema sababu ni kwamba Mungu alimfukuza nje ya 'mahali"
pale (alikataa kuita neno'
Mbinguni 'na katika muda wote katika
mikutano yetu tuliyofanya pamoja naye
hakuwahi kutaja neno 'Mbinguni'.
Badala yake alitumia neno 'mahali pale') kwa sababu ya kiburi, na kwa hiyo *yeye
hataki Mkristo yeyote afike
huko (Mbinguni).*
Pia alituambia kwamba hatupaswi kupambana
na wanafiki. "Wao ni kama mimi,"
alisema. Aliendelea na hotuba yake na akasema: "Tunapaswa tu kupambana
na Wakristo halisi" Kwamba wakati
wake umekaribia, kwa hiyo
tunapaswa kupambana kama vile haijawahi
kutokea na kuhakikisha kwamba
hakuna anayeingia mahali pale:" Sasa mmoja wetu akasema tumesikia
kwamba Mungu alimtuma mtu kuwaokoa watu
warudi kwa Mungu" Shetani
kisha akauliza: "nani huyo?" mjumbe mmoja
akajibu "Yesu" na kwa mshangao
mkubwa, Lucifer akaanguka katika kiti chake. Akapiga kelele kwa mtu huyo
na akamuonya kamwe asilitaje
jina hilo kwenye mikutano yetu
------------------------------
*Page 12*
12 *Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
aliojaliwa na Mungu*
kama anapenda maisha yake. Ni kweli
kwamba kwa jina la Yesu kila goti
litapigwa (Flp. 2: 10), ikiwa ni pamoja
na Shetani. Baada ya tukio hilo akatupa sisi moyo na
alituambia kwamba tusiwajali "hawa
wakristo", kwamba yeye Lucifer
atakuja hivi karibuni kutawala dunia na
atatupa,sisi mawakala wake, mahali
bora ili tusihadhirike/tusitaabike sawa na wengine duniani na yeye atatufanya
sisi watawala. *Aliendelea
kusema kwa kuwa mwanadamu*
*anapenda mambo ya kushangaza na ya
ajabu, ataendelea kutengeneza mambo
hayo na kuhakikisha* *kwamba mwanadamu hana muda kwa ajili ya
Mungu wake na kwamba atatumia
yafuatayo kuharibu*
*kanisa:*
1.fedha,
2.mali, 3.Wanawake.
Mwishoni mwa hotuba hii akafunga Mkutano.
Mkutano huo ndio uliokuwa wa
kwanza kwangu mimi kukutana
na Shetani. Mingine kadhaa ilifuata baada ya
mkutano huu. Tulipokuwa tukiondoka, Malkia wa Pwani, ambae
sasa alionekana katika maumbo mbalimbali,
alinialika mimi na nyumbani
mwake. Aliingiza majivu ya binadamu
pamoja na vitu vingine ndani ya mifupa yangu
ya miguu yote, jiwe (si jiwe la kawaida) katika kidole changu na
kitu kingine ndani ya mfupa wa mkono wangu
wa kulia.
Kila moja ya vitu hivi ilikuwa na kazi yake. Jiwe
katika kidole changu
ilikuwa ni kwa ajili ya kujua mawazo ya mtu yeyote dhidi yangu. Moja katika mkono
wangu wa kulia ilikuwa
kuniwezesha mimi kuharibu na yale yalio
katika miguu ni kwa ajili ya kufanya miguu
yangu kuwa migumu zaidi na
kuifanya kuwa hatari zaidi na pia kuniwezesha mimi kubadilika na kuwa
mwanamke, mnyama, ndege, paka, nk
Alinichukua mpaka kwenye moja
ya maabara na akanipa darubini, TV na video.
Hivi havikuwa vitu vya kawaida
lakini vilikuwa vinatumika katika kuchunguza Wakristo waliozaliwa mara ya pili
na waendaji tu wa kanisani
ndani ya kanisa.
Mwishowe alinipa wasichana kumi na sita wa
kufanya nao kazi. NINA alikuwa
ni mmoja wao. Nilikuja tena Lagos nikiwa na zawadi hizo nilizozitaja hapo
juu.
*Kugeuzwa kuwa wakala wa shetani*
Sikuwa na hisia za kibinadamu wala huruma
katika moyo wangu tena.
Nilikwenda katika utekelezaji mara moja na niliharibu majengo matano kwa mpigo. Zote
zilizama ndani ya ardhi na
wenyeji wao. Hii ilitokea Lagos mwaka
Agosti 1982. Mkandarasi aliwajibika kwa
kutoweka msingi mzuri na alilipa
haswa kwa hili. Uharibifu mwingi unaotokea hivi leo katika dunia si kwamba
wote umesababishwa na mwanadamu.
Wajibu wa shetani ni kuiba,
kuua na kuharibu. Nasema tena, "Shetani hana
zawadi ya bure".
Nilikwenda kusababisha ajali katika barabara n.k. Kisa ninachopenda
kusimulia ni kuhusu kijana mmoja
aliyekuwa ndio ameokoka tu ambae alikwenda
akishuhudia wokovu wake na
ukombozi alioupata. Alikuwa
anasababisha madhara mengi katika ulimwengu wa roho kwa ajili ya kufanya
hivi, hivyo nilipanga kufanya ajali
kwa ajili yake. Siku moja alikuwa kwenye basi
zuri sana akienda Lagos.
Alikuwa ameitwa ili aje kutoa ushuhuda
wake. Basi lilipokuwa katika mwendo wa kasi, mimi nikalizungusha tairi nje
ya barabara hivyo likaenda na
kugonga kwenye mti. Abiria wote walikufa
isipokuwa huyu kijana.
Kupona kwake ilikuwa ni kimuujiza kwa
sababu alitoka nje ya gari kupitia buti ya basi na kupiga kelele: "niko
salama! niko salama! "Tulijaribu kumzuia
asishuhudie lakini tulishindwa.
Kwa njia ya TV, tunaweza kujua mtu
aliyetubu, mpya na tunamfuatilia kwa
ukaribu kuona kama tunaweza kumfanya akarudi nyuma. Kama baada ya
miezi sita hatuwezi kufanikiwa,
tunakwenda katika biashara yake na
------------------------------
*Page 13*
13 *Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
aliojaliwa na Mungu*
kuifanya iwe mufilisi. Kama yeye ni mtumishi
wa umma tutamnyanyasa kupitia
kwa bosi, na kama inawezekana
tunafanya bosi kusitisha mkataba au uteuzi wake. Kama baada ya haya yote
hawezi kurudi nyuma basi tunaachana
nae. Lakini kama atarudi nyuma anauawa
kuhakikisha kwamba hapati nafasi ya
pili kutubu.
Niliharibu maisha kwa kiasi kwamba Lucifer akafurahishwa na kunifanya niwe
mwenyekiti wa wachawi.
Mwezi mmoja baada ya Uenyekiti wangu,
mkutano uliitishwa. Tulihudhuria
mkutano huo kama ndege, paka na
nyoka. Viumbe hawa hutumiwa kwa ajili ya sababu zifuatazo:
1. Kuwa ndege kunafanya wachawi wawe
hatari zaidi.
2. Kuwa paka kunafanya wachawi wawe na
uwezo wa kuwa katika roho na
binadamu. 3. Kuwa panya kunawawezesha wachawi
kuingia katika nyumba kwa urahisi,
kisha wakati wa usiku wanakuwa
kivuli, na kisha binadamu na kunyonya damu
za watu.
Katika mkutano huo tulikuwa na agenda moja tu: *"Wakristo" *Tukapanga
kuitisha mkutano wa Afrika wa
wachawi mjini Benin mwaka 1983.
Tulichapisha katika magazeti yote ya kila
siku na vyombo vyote vya habari
vya umma. Nguvu zote za giza walijipanga na walikuwa na uhakika sana kwamba
hakuna kitu chochote
kitakachoingilia kwa kupinga mkutano huu.
Kwa kweli kila kitu kilipangwa
vizuri na kulikuwa hakuna mwanya.
Ghafla, Wakristo Nigeria wakaingia kwenye maombi na sifa kwa Mungu wao na
mipango yetu yote ilizimwa. Si
tu kwamba mipango yetu ilizimwa peke yake
lakini pia kulikuwa na mtafaruku
haswaa katika ufalme wa giza.
Matokeo yake, mkutano wa wachawi 'na mapepo haukuweza kufanyika Nigeria.
Wakristo wanapaswa kutambua
kwamba wakati wao wanaingia ndani katika
sifa halisi kwa Mwenyezi Mungu,
kunakuwa na shida na mvurugano
kote ndani ya bahari na angani,na mawakala wa shetani wanakuwa hawana
nafasi ya kupumzika/kutulia. Maombi
ni kama kutupa bomu la kushitukiza katikati
yetu na kila mtu anatoroka
kuokoa maisha yake.
Kama Wakristo wakitambua na kutumia nguvu na mamlaka ya Mungu aliyowapa,
wataweza kudhibiti mambo
ya taifa lao! Wakristo tu ndio wanaonaweza
kuokoa taifa letu.
Baada ya mkutano huu kushindikana, ambao
baadae ulifanyika nchini Afrika Kusini, niliitwa tena baharini.
Nilipofika, niliambiwa kutokea wakati huo
nilitakiwa kufanya bahari kama
nyumbani kwangu na kutembelea
dunia kwa shughuli ngumu tu. Nilipewa kazi
mpya: kubuni hirizi za waganga, nikiwa mhusika mkuu wa chumba
na mtumaji wa zawadi, yaani ufunguzi wa
makanisa (nyumba za maombezi),
ufunguzi wa nyumba za kujifungua,
kufungua maduka na kufanya yafanikiwe,
kuwapa 'watoto na fedha. Haya yataelezwa moja baada ya jingine:
*1. Ufunguzi wa "Makanisa ya nguo nyeupe":*
Wakati mtu anakuja kwetu kwa msaada wa
kujenga nyumba ya maombi na
kumsaidia kufanya uponyaji nk,
basi atapewa baadhi ya sheria: a) Atakubali kuchangia kwetu nafsi moja au
mbili kila mwaka.
b) Katika ngazi fulani ya ofisi katika kanisa mtu
atakuwa anaunganishwa na
jamii yetu.
c) Hakuna mwanachama angeruhusiwa kuja katika nyumba ya maombi na viatu
mguuni.
Akisha kubali matakwa hayo,*atapewa kitu
changarawe nyeupe, mifupa ya
binadamu, damu na hirizi, vyote*
*katika chungu*. Atapewa maelekezo ya *kuzika chungu hiki na vitu vyake
vyote mbele ya kanisa na atazika*
*msalaba juu yake*. *Baada ya maziko
msalaba tu ndio unapaswa kuonekana.
*Atashauriwa
*kujenga Bwawa* *au kuweka basini ambapo roho chafu
zinaendelea kuweka maji maalum. Maji
haya ndiyo unasikia huyaita*
*"maji matakatifu."*
Watu wengi wakisumbuliwa na roho mbaya
wanakwenda kwa hawa "manabii" kwa ajili ya kuwafukuza. Ukweli
ni kwamba, wao huongeza mapepo zaidi kwao.
*Shetani hawezi kumuondoa nje
shetani. *(Luka 11:17-19) Kile
------------------------------
*Page 14* 14
*Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
aliojaliwa na Mungu*
nabii atakifanya ni, atamuombea mshirika na
kisha atampa mshirika kitambaa
chekundu ili kuweka katika nyumba yake, na kisha atamshauri awe
anaomba akiwa na mishumaa na uvumba.
Kwa kitendo hiki mtu anatualika
sisi kwenye nyumba yake. Wakati mwingine
mshirika anashauriwa kuleta mbuzi
n.k, kwa ajili ya sadaka. Sadaka hizi ni kwa ajili yetu kuja na kusaidia kumtibu
mtu huyu. Nabii hana uwezo
wa kutibu au kuponya
*2. Ufunguzi wa Maternities (sehemu za
kujifungulia):*
Kama mwanamke anakuja kwetu kwa ajili ya kupata msaada wa kufungua kituo
cha uzazi na kukifanya
kifanikiwe, atapewa sheria zifuatazo:
"Mwezi utachaguliwa ambao watoto wote
wanaozaliwa katika mwezi huo kwenye
kituo hicho watakufa, na miezi mingine watoto wataishi."
Kama atakubali basi atapewa, dawa ambayo
itawavutia watu kuingia katika
kituo hicho cha uzazi. Kuna
maternities kama hizi Onitsha, Lagos, nk viatu
haviruhusiwi katika vituo hivyo.
*3. Ufunguzi wa Maduka ya dhana:*
Mtu anapotufuata sisi kwa ajili ya msaada
katika suala hili, anapewa pete
na mashariti kwamba hakuna
mwanamke atakayeruhusiwa kugusa pete yake. Ni lazima pia akubali kuwa
mwanachama wetu. Kama atakubali
kupokea kutimiza masharti hayo, duka lake
litakuwa linajaa vifaa vya ubora
na vya kisasa.
*4. Kutoa Watoto* Kama mwanamke tasa atakwenda kwa
mganga, baada ya kuweka malalamiko yake,
ataulizwa kuleta yafuatayo:
jogoo mweupe, mbuzi, chaki ya asili na baby
care. Ataambiwa arudi na
atakapokuwa ameondoka,mganga atakuja kwetu kuleta vitu hivi. Kisha
tutachanganya vitu fulani ambavyo ni
vigumu kuelezea kwa maandishi, na
tutaweka majivu ya mwanadamu. Atatumia
dawa hii kumpikia chakula mwanamke
nk. Atapata mimba na kuzaa, lakini siyo binadamu wa kawaida. Kama
mtoto ni wa kike ataweza
kuishi na hata kuolewa lakini
atakuwa bado tasa maisha yake yote. Kama
mtoto ni wa kiume ataishi lakini
atakufa kifo cha ghafla. Huwa awaishi kuzika wazazi wao.
Napenda kukueleza hapa kwamba utasa mara
nyingi unasababishwa na mapepo.
Unaweza kuona mwanamke
tasa hapa duniani, lakini anaweza kuwa na
watoto wengi tu baharini. Kwa hiyo nashauri watoto wa Mungu
kumsubiri Mungu pekee kwa sababu Mungu tu
ndio huwapa watu watoto halisi.
*5. Kutoa fedha:*
Kama mtu anakuja kwetu kwa ajili ya kupata
fedha, atapewa masharti yafuatayo kuyatimiza: Ataambiwa kutoa
sehemu ya mwili wake au kama ana familia
ataambiwa kuleta mtoto wake wa
kiume. Kama yuko mwenyewe
basi ataombwa kumtoa kafara kaka yake au
mdogo wake. Yeyote atakayeamua kumleta ni lazima atoke
katika tumbo moja. Kitu muhimu
cha kutaja: siku ya kufanya
mauaji ya mhusika, mtu ambaye amempeleka
atapewa mkuki,au mshale. Uhusiano
wake utawekwa katika file kwenye kioo. Mara baada ya mtu yule
anayetakiwa kumtoa kupita, ataambiwa
apige ile sehemu ya faili iliyo
kwenye kioo,basi akifanya tu hivi yule mtu
anakufa pale mahali alipo.
Kuna njia nyingine lakini jambo moja Shetani hufanya ni kwamba:
anahakikisha kwamba katika njia hio
tofauti, mtoaji anakuwa mwajibikaji kwa ajili ya
kifo cha mwathirika, kwa
kufanya mtoaji ampige mlengwa,
kumbuka *Shetani hana zawadi ya bure!* ------------------------------
*Page 15*
15
*Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
aliojaliwa na Mungu*
*Sura 4: Jinsi shetani anavyopigana na Wakristo*
*«Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya
damu na nyama; bali ni juu ya
falme na mamlaka, juu ya wakuu *
*wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya
katika ulimwengu wa roho. »* *Waefeso. 6: 10-12 *
*Kupigana na Wakristo*
Baada ya amri ya Lucifer kupambana na
Wakristo, sisi tuliketi na kuchora
ramani ya kupambana nao kama
ifuatavyo: 1. Kusababisha magonjwa.
2. Kusababisha utasa.
3. Kusababisha usingizi katika kanisa.
4. Kusababisha machafuko katika kanisa.
5. Kusababisha uvuguvugu katika kanisa.
6. Kuwafanya wawe wajinga wa neno la Mungu.
7. kwa mitindo na uigaji.
8. Kupambana nao kimwili.
Miongoni mwa hayo juu napenda kuwaeleza
mawili:
*1. Kupambana kimwili:* Kwa TV niliyopewa, niliwaona Wakristo
waliozaliwa mara ya pili. Hatupigani
na wanafiki kwa sababu wao ni
mali yetu tayari. Tuliweza kuwatuma
wasichana wetu kwanza katika makanisa
makubwa. Ndani ya kanisa walikuwa wanatafuna jojo au kumfanya mtoto
alie au kufanya chochote ambacho
kilivuruga watu kusikiliza neno
la Mungu. Wanaweza kuamua kuja kiroho na
kusababisha watu kulala wakati
mahubiri yanaendelea. Wakikuona uko makini kwa sababu ya mahubiri,
wanaweza kukusubiri nje ya kanisa na
unapokuwa ukitoka kuja nje ya
kanisa, mmoja wao anakusalimu na hata
kukupa zawadi ( na mara nyingi ni
zawadi ya kitu kile upendacho ) na wataonekana ni marafiki sana. Atafanya
kila kitu na kabla haujajua
kinatokea unakuwa umesahau kila kitu
ulichojifunza kanisani . Lakini kwa Mkristo
halisi,mmoja ya wasichana hawa
,baada ya ibada, ataruka nje kukusalimu na atapenda kujua nyumba yako
kwa kisingizio kwamba yeye ni
mgeni katika mji na hawajui
Wakristo wengi wanaomzunguka. Ukimpeleka
nyumbani kwako, kwa haraka
atanunua ndizi na Mkristo atachukulia hii kama ishara ya upendo.
Ataendeleza ziara zake mpaka
hatimaye anaweka mbali mwanga wa
Kristo ndani yako na kisha anaacha kuja.
Shughuli kuu katika makanisa
yaliyo hai na shirika zilizo hai ni : kuwasumbua Wakristo wasisome na kujifunza
neno la Mungu, na hivyo kuwafanya
wajinga wa mamlaka na
ahadi za Mungu. Katika mikutano ya injili
wasichana hawa wanatumwa
kusababisha kutoelewana na ugomvi. *Jinsi wakirsto wanavyojulikana?*
Wakristo waliozaliwa mara ya pili hawajulikani
kwa Biblia wanayobeba kila
siku au ibada nyingi
wanazohudhuria. Wanajulikana katika
ulimwengu wa roho kwa mwanga ambao huendelea kuangaza wakati wote
kama mshumaa mkali sana katika moyo au
mduara wa mwanga unaozunguka kichwa
au ukuta wa moto
unaowazunguka. Mkristo anapokuwa
akitembea, tunaona malaika wakitembea pamoja naye mmoja mkono wa
kuume, mmoja kushoto, na mmoja nyuma. Hii
inafanya kuwa vigumu kwa sisi
kuja karibu yake.
Njia pekee ya sisi kufanikiwa ni kwa kumfanya
Mkristo atende dhambi, na hivyo anatoa mwanya wasisi kuja na
kuingia ndani. Mkristo akiwa anaendesha gari
na tunapotaka kumdhuru,
tunaona kwamba siku zote hayuko peke
------------------------------
*Page 16* 16
*Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
aliojaliwa na Mungu*
yake katika gari. Siku zote kuna malaika
pembeni mwake. *Oh kama Mkristo
akijua tu yote ambayo Mungu* *anafanya kwa ajili yake, hawezi kutenda
dhambi au kuishi ovyo ovyo !*
*2. The Making of Backslidden Christians*
Kama mwenyekiti aliyeteuliwa na Lucifer,
niliwatuma wasichana hawa
makanisani na sharika zinazoishi/hai . Wasichana hawa wanakuwa wamevalia vizuri
na baada ya mahubiri wanakuja
kwenye madhabahu kama
wameitwa, na watajifanya kuwa wamempokea
Kristo na wataombewa. Mwishoni mwa
ushirika au ibada watazungukazunguka nje na kumsubiri
mhubiri ambaye kiukweli atakuwa na
furaha sana na waongofu hawa
wapya.
Waongofu hawa wapya wanaweza hata
kumfuata mhubiri nyumbani kwake. Kama mhubiri hana roho ya
kupambanua watamvutia aingie katika dhambi
ya uzinzi au uasherati . Hii
inafanyika wakati pale mhubiri
anapokuwa amemtamani. Atahakikisha
amendelea katika dhambi hii mpaka pale atakapoona amemzimisha Roho
wa Mungu ndani yake na kisha anaondoka,
huku *mkakati wake umetimia.*
Mahali hapa ningependa kutoa ushuhuda wa
Mhubiri. Katika ulimwengu wa
roho/kipepo yeye anajulikana kama mtu wa Mungu(man of God). Anapokwenda
kwenye magoti yake kunakuwa na
mvurugano kati yetu. Kwa hiyo
tunatuma wasichana hawa kwake. Mtu huyu
anaweza hata kuwalisha lakini
atakataa kunaswa na mitego yao. Walijaribu kila walivyoweza lakini kamwe
hawakuwahifanikiwa. Matokeo
yake, wasichana hawa waliuawa
kwa kushindwa kwao.
Mimi nilijigeuza na kuwa mwanamke kisha
nikamwendea, kwa maneno na vitendo nilijaribu kumshawishi, lakini
alikuwa mgumu. Hii ilikuwa ni kazi kubwa mno
kwangu, hivyo nilidhamiria
kumuua kabisa kimwili. Siku moja,
Mhubiri huyu alikwenda soko la barabara ya
Oduekpe. Nilimwangalia na alipoinama chini kununua baadhi ya
bidhaa nilijizungusha kwenye tairi za trailer
iliyokuwa imebeba mafuta ya
mafuta kuelekea sokoni alipokuwa
mhubiri. Trailer/gari likapiga nguzo kubwa sana
ya NEPA na ikangukia katikati ya soko, na kuacha watu wengi
wamekufa, lakini Mhubiri alitoka mzima. Jinsi
gani alipona ulikuwa ni
muujiza. Siku nyingine, nilimuona
akisafiri kwenda Nkpor kwa miguu.
Nililizungusha gari la jeshi lililokuwa limebeba viazi vikuu vya kumuua.
Lori lilikwenda moja kwa moja ndani ya
barabara mpya ya makaburini, na
kuwaua watu wengi mno, lakini
muhubiri huyu bado alikuwa mzima. Baada ya
jaribio hili la pili tulikata tamaa.Yeye bado yuko hai hata leo hivi!
Kwa sababu ya mkristo mmoja, shetani
anaweza kuamua kuharibu roho nyingi,
akifikiri anaweza kumuua, lakini
siku zote anashindwa. Matukio haya
yameyotokea kwa Wakristo wengi bila ya wao kujua, lakini Mungu wao
huwaokoa mikononi mwa adui zao siku zote.
Shida ni kwamba, Shetani hachoki.
Mawazo yake yako palepale:
"Ninaweza kufanikiwa." Lakini kamwe
hafanyikiwi. kama tu Mkristo atatembea na *Upendo wa Mungu na *
*kubakia ndani yake na ajichanganyi na
mambo mengine ya maisha haya,
shetani hawezi kumpata,*
*vyovyote vile shetani anaweza kujaribu.
Wasioamini tu ndio wako chini yake.*
*Ukandamizaji wa Wakristo*
Hii hutokea hasahasa katika ndoto. Mkristo
anaweza kuona katika ndoto yake
yafuatayo:
1. Mtu mfu anamtembelea 2. Kinyago kinamfuata.
3. Marafiki wanaogelea katika mto
4. Marafiki wanaleta chakula na wanamsihi ale.
5. Msichana wa kike anafanya ngono au
msichana aliyeolewa anafanya mapenzi
na mwanaume. Hii, kama si haitashughulikiwa, wakati mwingine
husababisha utasa.
Au mwanamke mjamzito anajiona anajamiiana
na mtu. Hii, kama
haikushughulikiwa, inaweza kusababisha
kuharibika kwa mimba. ------------------------------
*Page 17*
17
*Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
aliojaliwa na Mungu*
Kama Mkristo akikutana na hayo huu katika ndoto yake, hatakiwi kuweka kando
mambo haya kwa kupuuzia
bali akitoka kwenye ndoto tu inampasa
ajichunguze mwenyewe na atubu dhambi
yeyote ile inayojulikana na
kufunga pepo wote na kumsihi Mungu arejeshe kila kitu alichokutana nacho
ndotoni. Hii ni muhimu sana. Mtu
ni lazima pia kutafuta msaada na ushauri kwa
mkristo aliyejazwa na Roho
Mtakatifu, wakongwe katika imani.
*Shetani na mkakati wa kuvuna roho* Yesu Kristo alipokuwa akiondoka duniani,
aliwapa wanafunzi wake amri:
"Akawaambia enendeni ulimwenguni
kote mkafanye wanafunzi kwa kila taifa"
Wakati Wakristo bado wanasubiri
mazingira mazuri na wakati mzuri kwa ajili ya kutii amri hii, Tofauti ni kwamba,
*mawakala wa shetani wako
na bidii kubwa zaidi katika kuvuna*
*roho za Wakristo !*
Moja ya maeneo ya shetani katika kuvuna
roho ni shule za sekondari, hasa za wasichana. Baadhi ya wasichana
wetu wanatumwa katika shule kama
wanafunzi. Tunawapa kila chupi ya kisasa
na nzuri na zenye gharama kubwa.
Hii ndio kipaumbele cha kwanza, kwa sababu
katika hosteli za wasichana wao hupendelea kutumia chupi tu .
Mawakala wetu kamwe hawakosi kitu
chochote, vipodozi, nguo , chupi ,
vitabu, fedha na mahitaji. Sabuni
maalumu za kuoga atapewa ili kutoa kwa
mwanafunzi yeyote ambaye atahitaji sabuni kutoka kwake. Msichana
anayetaka kuwa kama yeye atavutiwa na
kufanya urafiki nae. Hatua kwa hatua
wakala wetu atatutambulisha
kwake. Nasi tutamtembelea kimwili na kuanza
kumpa zawadi na kumtimizia mahitaji yake. Kwa hili, atajiunga
nasi kwa hiari . Yeye naye atawavuta wengine
na itaendelea hivyo. Hii
inachukuliwa kama mkakati wenye
dhamira ya kufanikiwa.
Jambo moja la kuzingatia: shetani hamlazimishi mtu yeyote. Anachokifanya ni
kuwavutia watu na kuwafanya
waje kwake kwa hiari. Ndiyo maana Biblia
inasema: "mpingeni shetani naye
atawakimbia" (James 4:7). Eneo
jingine la kuvuna roho la shetani ni kutoa lifti. Tunawapeleka wasichana
wetu kusimama barabarani, na kwa
kawaida huwa ni warembo sana na wamevaa
mavazi ya kuvutia. Unaweza pia
kuwapata kwenye hoteli na kupitia
maeneo haya tunawapata wanaume na wanawake. *Watu wengi tunaowaona
wanatangazwa katika magazeti*
*kama wamepotea, ni baada ya kutoa lifti kwa
wasichana, wasiowajua.*
Unapaswa kuwa makini ni nani ambaye
unampa lifti. ------------------------------
*Page 18*
18
*Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
aliojaliwa na Mungu*
*Sura 5: Nilipokutana na Yesu* Katika mwezi Februari 1985, tulikuwa na
mkutano wetu wa kawaida katika
bahari, baada ya hapo niliamua
kusafiri kwenda Port Harcourt katika jimbo la
Rivers, kutembelea mke wa
marehemu mjomba wangu. Nilikutana na mtu mmoja aitwaye Anthony. Yeye ana
karakana pale kwenye makutano ya
Nwaja, sambamba na barabara ya
Trans-Amadi, Port Harcourt, Rivers State.
Alimtuma mtu huyu kwa ajili yangu
na kwa sababu katika jamii yetu tuna sheria kwamba hatupaswi kukataa muito,
niliamua kujibu muito wake.
Nilikwenda kwake mchana siku ya
Alhamisi ya wiki hiyo. Alianza kwa kusema
Mungu amempa ujumbe kwa ajili
yangu. Akatoa Biblia yake na kuanza kuhubiri. Kulikuwa na Wakristo
wengine watatu wameketi (mwanaume na
wanawake wawili). Aliendelea
na mahubiri yake kwa muda mrefu na sikuwa
na uhakika kama nilisikia yote
aliyosema. Alinisihi nipige magoti kwa ajili ya maombi. Nilimtii na taratibu nikapiga
magoti.
*Mara ghafla akaanza maombi yake.
Naliangushwa chini na roho wa Mungu na
nikaanguka*
*nikajinyoosha*. Nilijitahidi kuinuka na nikasimama kama chuma.
Nikavunjavunja viti vya chuma ndani ya
karakana. Niliangalia nje na kuona
wanachama watatu wa jamii yetu ya siri,
mwanaume na wasichana wawili.
*Walikuja katika umbo la binadamu na kusogea mpaka mlangoni lakini kwa
sababu ya nguvu ya Mungu*
*hawakuweza kuingia.*
Nina hakika kengele ndani ya bahari
iliwataarifu shida ilipokuwa na kwa TV
walijua wapi ambapo tatizo lilikuwa na walituma waokoaji wasio na nguvu. Hii
mara zote hufanyika wakati
mwanachama yeyote ameingia katika
matatizo. Wakati wale wakristo wawili
wakinivuta chini kwenye magoti yangu,
wasichana wawili waliendelea kuomba na kufunga mapepo, lakini hawakuwa
wanalenga hasa nini wanachofunga.
Wakaniuliza kama
ninamuamini Yesu Kristo, sikusema chochote.
Wakaniuliza niite jina la Yesu,
nami nilikataa. Wakaniuliza jina langu niliwaambia. Wakajitahidi kwa masaa na
wakaniachia niende. Hakuna
roho iliyoondolewa ndani mwangu,
hivyo nilitoka hivyohivyo sawa na nilivyoingia.
*Maatukio ya Kanisani*
Siku iliyofuata ilikuwa ni Ijumaa, nilialikwa na Anthony huyo huyo
kuhudhuria usiku wa mkesha wao katika
kanisa la Assemblies of God, Silver Valley,
Port Harcourt. Nilikubali
mwaliko huu kwa sababu kuhudhuria ibada
ya makanisa na kusababisha usingizi na machafuko ilikuwa ni sehemu ya kazi
yetu. Ibada ilianza na pambio.
Tuliimba mpaka mmoja wa wajumbe
wenzangu akaanzisha kiitikio maarufu cha
bendi moja ya kikristo,
kinachozomea uwezo na mamlaka ya nguvu zingine isipokuwa nguvu za Yesu.
Kisha nikaanza kucheka. Nilicheka kwa
sababu katika roho niliwaona maisha
yao karibu robo tatu ya watu
waliokuwa wanaimba kiitikio kile walikuwa
wanaishi katika dhambi. Nilijua kuwa *kwa sababu ya dhambi*
*katika maisha yao, ni wazi kuwa
wangeharibiwa vibaya na nguvu hizi. Ni
muhimu kwa wakristo kutii neno*
*la Mungu na si kuruhusu dhambi kubaki katika
maisha yao. *Katika ibada hiyo tulikuwa wanne kutoka
baharini na tulikuwa tukiimba na kupiga makofi
pamoja nao. Tena nataka
kusisitiza hapa kwamba wakati ibada
inaanza, waumini ni vyema na wanashauriwa
kwanza kukiri dhambi zao na kutubu, kisha kwenda katika kipindi
cha sifa halisi kwa Mungu. Hii itafanya wakala
wa Shetani awe na wasiwasi
sana na ataondoka ili kuyaokoa
maisha yake.
Katika ibada hii tulikuwa tunaujasiri sana hata tukaingia katika utendaji.
Wengi walianza kulala, pambio zilikuwa
zikiimbwa kwa udhaifu na mambo yakaenda
zig-zag. Ndugu Anthony alikuwa
tayari amewaambia kuhusu mimi
kwa hiyo saa 02:00 waliniita nitoke mbele na waanze kuniombea. Mara
nilipotoka mbele walianza kuita damu ya
Yesu. Nikawasimamisha na kusema: "Si
kuomba kwa damu ya Yesu ndio ufumbuzi.
Mimi ni mwanachama
mkubwa sana katika jamii za watu wa chini ya bahari. Kama mnakubali kwamba
mnaweza kunikomboa, basi
nipige magoti. "Maneno haya niliyasema
sikuwa nimeyapanga. *Damu ya Yesu
inaogopesha mapepo na *
------------------------------ *Page 19*
19
*Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
aliojaliwa na Mungu*
*kumlinda muamini, lakini haifungi mapepo.
Kufunga mapepo na kuyatoa inafanyika tu pale Mkristo*
*anapotumia mamlaka yake na kutoa amri.*
Walikubaliana na mimi nikapiga magoti. Katika
hatua hiyo dada mmoja
aliiongozwa na Roho wa Mungu na
kuongea kwa sauti akasema: "Kama hauko vizuri, usijaribu kusogea karibu!"
Nina uhakika wengi hawakuwa
wameelewa nini maana yake. *Ni hatari kwa
Mkristo anayeishi katika dhambi
kutoa pepo. *Wengi waliondoka
na wachache wakatoka kuja kuomba kwa ajili yangu. Walipoanza kusema "Katika
jina la Yesu," Nikasikia
(mpasuko mkubwa) big bang kubwa ndani
yangu na nikaanguka juu ya sakafu.
Mara pepo wanaokuruka ndani
yangu wakanza kufanya kazi. Nikaanza kukimbia kwa kifua changu. Mtu yeyote
mwenye hili pepo la kuruka ni
muovu na hatari sana. Ndugu/Waamini
hawakuona nini kinatokea kiroho.
Nilikuwa nakimbia mbio kwa sababu
ya nguvu kubwa iliyokuwepo katika chumba. Nguvu mbili za upinzani zikaanza kufanya kazi
pia na anga likabadilika.
Ghafla nikasimama na nikawa na vurugu
sana nk. Pepo, likatoka ndani yangu na
kumkamata mvulana aliyekuwa kati yao
na likaanza kupambana nao, likijaribu kuniokoa mimi. Ndugu hawakupoteza
muda nae badala yake
wakamkamata yeye pamoja na wengine
waliokuwa wanaogopa na kumfungia katika
vestry ya kanisa. Hii iliendelea
mpaka 7:00 Nilikuwa nimechoka sana kimwili na nikawa nimetulia, hivyo ndugu
wakakusanyika karibu yangu
tena na kuanza kuniambia: Wataje
ni akina nani hao nk Nilikaa kimya tu. Baada ya
kusubiri kwa muda mrefu na
kuona sikuwa nimesema kitu, walidanganyika na kuamini kwamba nilikuwa
nimekombolewa. Wakaomba na
tukatawanyika. Nilikuwa kimwili
dhaifu kiasi kwamba ilikuwa ni vigumu
kutembea kwenda hata nje ya kanisa.
Lakini kitu fulani kilitokea, mara baada ya kwenda nje ya kanisa na kuvuka
barabara, nikawa na nguvu nyingi za
kimwili. Labda inawezekana baadhi ya mapepo
yaliyotoka yakarudi tena ndani
yangu. Nilikasirika sana na
kuamua kulipiza kisasi juu ya kanisa. "Hawa watu wamenidhalilisha"
Nikajisemea mwenyewe, na kwa jinsi
walivyonifanyia nitarejea Lagos na kupata
nguvu zaidi pamoja na wengine
waovu kama mimi, na kisha narudi
Port Harcourt kulipiza kisasi kwa kanisa zima la Assembly of God, Silver
Valley.
*Safari yangu ya Lagos*
Nilipofika kwenye nyumba ya mke wa mjomba
wangu, Niliwaambia nitaondoka
kurudi Lagos mara moja. Nilikataa wasinisihi kubaki na nikachukua teksi
mpaka kituo cha magari cha
Mile 3. Ambapo nilichukua teksi
ya kwenda Onitsha. Nia yangu ilikuwa
kusimama Onitsha, kumuona rafiki na
kisha kuendelea mpaka Lagos. Pale Mile 3 tukaondoka na tulipokuwa tumefika njia
panda ya kwenda Omagwe,
katika makutano ya uwanja wa ndege
wa Kimataifa, nikasikia sauti ikiniita kwa jina
langu la asili "NKEM."
Nikageuka nyuma kuona kama kuna sura yeyote ninayoijua kwenye teksi, lakini
hakukuwa na mmojawapo anayenijua.
Huyu anaweza kuwa nani? Ni
marehemu mama yangu tu ndiyo alikuwa
akiniita kwa jina hilo, wengine wote
pamoja na ulimwengu wa kipepo walinijua mimi kama Emmanuel.
Nilipokuwa bado nashangaa, sauti ikasikika
tena : *" NKEM , unakwenda
kunisaliti kwa mara nyingine tena *
*?" *Sikuweza kuitambua sauti lakini sauti
iliendelea kuniuliza : *" Je, unakwenda kunisaliti kwa mara nyingine*
*tena*" Ghafla nikawa na homa kali. Joto
lililotoka mwilini mwangu lilikuwa
liko juu mno kiasi kwamba abiria
wengine walilisikia. Mmoja wao akaniuliza:
"Mheshimiwa, ulikuwa vizuri kabla ya kusafiri?"Niliwaambia
nilikuwa vizuri na sikuwa naumwa hata na
kichwa kabla ya kuondoka Port
Harcourt.
Tulipofika Umuakpa Owerri, nilianguka ndani
ya teksi. Kilichofuata ni kwamba watu wawili, warefu na
wakubwa, walikuja kunichukua mmoja upande
wa kushoto na mwingine upande wa
kuume, na hawakuzungumza
neno lolote kwangu. Waliniongoza kwenye
barabara mbaya sana yenye chupa na vipande vya chuma vilivyokuwa
vinanikatakata nikaanza kulia, lakini hawa watu
hawakusema neno lolote.
Tuliendelea mbele na kufika kwenye
barabara ya kasi. Ilikuwa hapa mmoja
akaniambia *"Wewe unatafutwa sana"*na tukaendelea. Tuliendelea mpaka
------------------------------
UNABII WA KWELI
Home
UNABII WA KWELI
KUKOMBOLEWA KUTOKA KWENYE NGUVU ZA GIZA na Emmanuel ENI SEHEMU YA PILI (PART 2)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni