Wafilipi 2:10-11
  • KUKOMBOLEWA KUTOKA KWENYE NGUVU ZA GIZA na Emmanuel ENI SEHEMU YA KWANZA (PART 1)

    Sura 1: Nilipotorokea kwenye "Maisha
    mapya"*
    *"Mfunze mtoto namna ya kuishi vizuri, naye
    hatasahau njia hiyo hata
    uzeeni." (Mithali 22: 6). *
    Hii ni simulizi ya Kazi ya Mungu- yenye nguvu, ya ajabu naya kushangaza-
    katika kutii amri ya YESU KRISTO
    akiniambia: *"Nenda na ushuhudie kile
    nilichokufanyia"*
    Mara nyingi mtu anadhani bahati mbaya ni
    kama kitendo cha kukosa na kwamba hatuwezi kufanya chochote
    kubadilisha matokeo ya maisha yetu. Kwa
    kiasi fulani hii ni kweli. Katika
    kesi ya mtoto wa Mungu, maisha yake
    yamepangwa (Mithali 16: 9). Hata kama
    mpango huo umetimia au bado inategemea na sababu mbalimbali,
    ukaribu wa mtu binafsi na Mungu, mtazamo
    wake kuhusu madhumuni ya mwisho ya
    maisha, na mazingira ya
    kijamii na kiroho anayojikuta akiwa mwenyewe
    ndani yake. Safari ya maisha yako inakuwa na
    changamoto kwa sababu baadhi za nje. Tabu
    inakuja pale unapotoa Uhuru
    wako kwa njia moja au nyingine, kwa wema
    au ubaya. Unaweza kupenda au
    ukachukia. Unaweza taka kuelewa au kutoelewa . Utayari wa kutii ni nguvu kubwa
    ya Mkristo mpya aliyezaliwa,
    wakati utayari wa kuasi ni nguvu
    kubwa ya kuharibu kwa mtenda dhambi.
    Mtoto anapoachwa peke yake katika dunia
    anatawaliwa na moja ya mamlaka hizi mbili: nzuri au mbaya, sahihi
    au isiyo sahihi , Mungu au shetani. Kila mtu
    anapimwa na nguvu hizi mbili
    za maisha, na kila mmoja ni lazima
    achague maisha yapi ni lazima aishi. Na
    naamini kwamba hivyo ndivyo Biblia inasema: "Mfunze mtoto namna
    ya kuishi vizuri, naye hatasahau njia hiyo hata
    uzeeni.". Utakubaliana nami
    kuwa mtu wa karibu sana na kipenzi
    cha moyo wa mtoto yeyote ni mama
    yake.Yatima ni mtoto mwenye bahati mbaya na wazi kuwa ameachiliwa
    katika mashambulizi ya shetani zaidi kuliko
    watoto wenye wazazi . Mama ni
    mlinzi wa mwili na roho lakini
    inakuwa ni janga mara mbili pale wazazi wote
    wawili wamepotea na zaidi sana katika mazingira ya utata.
    Hadithi yangu inaanza miaka 22 iliyopita katika
    kijiji kidogo kinachoitwa
    Amerie Iriegbu Ozu Item katika Ma
    mlaka ya Serikali za Mitaa Bende, jimbo la Imo.
    Wazazi wangu walikuwa si katika kundi la miongoni mwa tajiri
    lakini baba yangu alikuwa na neema ya kurithi
    hekta 42 za ardhi kutoka kwa
    babu yangu , baraka ambayo leo hii
    imenisababishia bahati mbaya sana ambayo
    haikuwahi kutokea katika historia ya familia. Baba yangu alichukiwa
    sana na ndugu zake wa mbali na karibu kwa
    sababu ambazo mimi sizijui, labda
    kwa sababu ya urithi
    wake
    mkubwa wa
    ardhi.
    Tulikuwa ni familia yenye furaha, wazazi
    wangu baada ya kutupata sisi
    wanne: Love , Margaret , Emmanuel na
    Chinyere . Baada ya kuwa na mabinti wawili wa kwanza , wazazi wangu
    walisubiri kwa miaka 14 kabla ya
    kunipata mimi ( mwana pekee wa kiume ) na
    baadaye dada yangu mdogo Chinyere
    . Hii ilileta furaha ya kweli
    kwa familia, lakini furaha hii ilikuwa ni ya muda mfupi tu baada ya janga
    la kwanza kutokea . Mama yangu
    mpenzi na anayejali alikufa. Ilidaiwa kuwa
    alikufa kutokana na uchawi, na
    miaka minne baadaye baba yangu
    alifariki, tena ilidaiwa kuwa naye ni kwa njia ya juju iliyofanywa dhidi
    yake. Miaka miwili baada ya kifo cha
    wazazi wote wawili, dada yangu mkubwa,Love,
    alitoweka kimaajabu na
    Margaret, binti wa pili wa wazazi wangu
    akachanganyikiwa akili. Ilikuwa ni mlolongo wa majanga katika maisha ya
    familia yenye unyenyekevu na furaha.
    Dada yangu mdogo Chinyere na mimi
    tulipelekwa kwa babu na bibi yetu. Pale
    nilimaliza elimu yangu ya msingi
    na baadaye nilijiunga na Item High School. Nilisoma mpaka darasa la III la
    shule ya sekondari na nikaacha kwa
    sababu ya ukosefu wa fedha kwa ajili ya ada
    n.k. Muda mfupi baada ya hili,
    babu na bibi pia walikufa. Baada ya
    ------------------------------ *Page 3*
    3
    *Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
    aliojaliwa na Mungu*
    sherehe zote za mazishi, ndugu yangu
    nisiyemjua alimchukua dada yangu mdogo Chinyere , na hadi leo hii sijui
    yuko wapi. Kwa sababu ya malezi mabaya,
    nililazimika kurudi kwenye nyumba
    ya baba yangu, na kuishi huko
    peke yangu katika umri wa miaka 13. Jinsi gani
    mtoto wa miaka 13 anajilisha mwenyewe katikati ya maadui wa
    baba yake na yeye mwenyewe? Jinsi gani
    nilivyokuwa Naogopa! Matuukio haya
    yalionekana kama yamenileta
    katika mwisho wa kuishi. Je kulikuwa na mtu
    aliyejali? Je kuna yeyote aliyehusika na *"Mikosi ya kijana huyo*
    *mdogo?"*
    Siku moja nilikutana na rafiki niliyemjua
    nilopokuwa shule ya msingi
    aitwaye Chinedum Onwukwe . Chinedum
    alinipenda sana na waliposikia yote yaliyonisibu alinichukua mpaka kwa
    wazazi wake ambao kwa urahisi tu
    walinipokea na kunifanya kama mwana wao
    wa pili. Maisha yakaja tena
    kawaida.Walinijali vyema. Nilikuwa na
    furaha tena: Sasa nilijua kuwa Mungu wa mama yangu aliyemuomba wakati
    aliokuwa hai alikuwa hai mahali
    fulani hivi. Amenipatia wazazi wapya, ndivyo
    nilivyojiwazia, nilifurahia
    wema huu kwa miaka miwili na kisha
    shetani akapiga tena . Chinedum na wazazi wake walikuwa wakisafiri
    kuelekea Umuahia na gari yao
    ikaingia ndani ya tipa lililobeba
    mzigo kama udongo. Chinedum na wazazi
    wake walikufa papo hapo! Baada ya
    kusikia habari hizi niliduwaa. Huzuni yangu inaweza tu kufikirika. Niliweza
    kuvumilia kipindi chote cha
    sherehe za mazishi, Nikiwatafutia
    wale wapishi kuni za kupikia na shughuli
    zingine: na mwishoni mwa hayo
    nikarudi nyumbani kwa baba yangu na nikarudia tena ajira hafifu ili niwe na uwezo
    wa kujilisha.
    Niliendelea kufanya kazi zisizo za kawaida
    katika mashamba, katika bustani,
    kuvua samaki pamoja na wazee
    mpaka siku moja, mtu mmoja katika eneo langu alinikodisha kufanya kazi
    katika shamba lake kwa 50k . Pale
    shambani alinikabili kwa mlolongo wa maswali.
    Kwanza, akaniomba nimuonyeshe
    ardhi ya baba yangu, pili,
    nimkabidhi shamba hilo, bila kujali jinsi uhusiano wetu ulivyokuwa. Katika
    kesi zote hizo mimi nilipinga na
    alikasirika. Kisha aliapa kuniua katika msitu.
    Nikawa na hofu nikakimbia na
    kupiga kelele ili nipate msaada. Kwa
    bahati mbaya, kwa sababu eneo hilo lilikuwa mbali na ni ndani ya msitu
    mnene hakuna mtu aliyesimama kwa
    msaada lakini msaada ulitoka kwa Mungu.
    Alinikimbiza na kisu chake lakini kwa kuwa
    nilikuwa mdogo nilikimbia haraka
    sana kuliko yeye nilianguka ndani ya shimo lenye kina cha mita 1.82 hivi na
    nilifunikwa na majani yaliyokua
    ndani yake. Naye akatafuta na baada
    ya muda akakata tamaa . Baadaye nilijitahidi
    kutoka nje ya shimo na kupitia
    njia nyingine nikarudi kijijini.Nilitoa taarifa ya tukio hilo kwa wazee wa eneo letu
    lakini hakuna hatua
    zilizochukuliwa - kawaida ya watoto yatima.
    Tukio hili liliunda chuki kubwa katika moyo
    wangu mdogo, hakuna mtu
    alinipenda, hakuna aliyenifikiria na kunijali.
    Nilitafakari kwenye mawazo yangu kwa nini
    mtu yeyote alitaka kuniua baada
    ya kujua kuwa mimi sikuwa na
    wazazi . Maisha yalijawa na taabu. Sasa najua
    ya kuwa Mungu katika upendo wake alimzuia shetani asinichochee
    wazo la kwenda kujiua. Nilimgeukia Mungu na
    kuwa mwanachama kamili wa
    Kanisa la Assemblies of God
    katika kijiji changu (bado nipo) lakini kwa
    bahati mbaya hakuna aliyejali ingawa hata baadhi ya wapendwa
    walijua kwa habari yangu. Ni muhimu
    kutambua kwamba nilikuwa mwanachama
    kamili wa kanisa bila kumjua
    Yesu Kristo. Sikujua nini maana ya kuzaliwa
    mara ya pili . Kama wewe uko katika Kanisa la Yesu Kristo na
    unajikuta katika hali ambayo nilijikuta,
    mkabidhi Bwana Yesu Kristo maisha
    yako. Maandiko yanasema: "
    *7*
    *Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni." *(1 Peter5 : 7 ).
    Katikati ya ugumu huu wa maisha na mateso
    ALICE alitokea! Alice alikuwa
    msichana niliyemjua wakati wa siku
    zangu za shule ya msingi. Alikuwa na miaka
    mitano zaidi yangu tulitokea kijiji kimoja. Tulikuwa darasa
    moja,tuliketi kwenye benchi moja na akawa
    rafiki yangu sana. Na 'upendo'
    huu katika hali ya utoto, tuliweka
    ahadi ya ' kufunga ndoa ' wakati tukiwa
    wakubwa. *Mzaha! *Mtoto wa miaka 11 wakati huo, bila wazazi, sina
    elimu , sina chakula , naweka ahadi ya ndoa
    kwa msichana wa miaka mitano
    zaidi yangu! Alice baadaye aliondoka
    ------------------------------
    *Page 4* 4
    *Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
    aliojaliwa na Mungu*
    na kwenda Akure kwa elimu yake ya
    sekondari na alinitumia barua za 'upendo'
    nyingi. Wakati mwingine nilipokutana na Alice ,
    nilikuwa nina miaka 15 na yeye
    alikuwa 20. Yeye alipomaliza elimu
    yake ya sekondari alifanya kazi na Benki ya
    Standard Lagos ( sasa Benki ya
    Kwanza), ambapo wazazi wake walikuwa wakiishi.
    Alice akiwa anajua historia yangu na matatizo
    yangu aliichukua hii kama
    fursa. Aliniambia nijiunge naye Lagos
    na akanipa anuani yake pamoja na N50 ( naira
    : Sarafu ya Taifa ya Nigeria)! Hiyo ilikuwa ni bahati kwa kijana
    wa miaka 15 ambaye hakuwahi kupata N2 kwa
    siku! Hii ilikuwa ni mana kutoka
    mbinguni na hii ilimaanisha
    kuwa Lagos lazima palikuwa ni mahali pa
    ajabu penye fedha nyingi na mambo mema ya maisha kwa wote
    kufurahia. Ni lazima kwenda Lagos
    kutengeneza pesa yangu mwenyewe na
    kupata
    utajiri pia . Kwenda Lagos
    kwa akili yangu ilikuwa ni njia pekee ya kutoroka. Kukimbia kutoka kwa
    maadui wa baba yangu, kukimbia
    kutoka kwa madui zangu, kutoroka kutoka
    kwenye njaa na matatizo yangu yote.
    Kukimbia! Kukimbia! Ndiyo,
    kukimbia kutoka katika yote yale ambayo ni mabaya!!!
    ------------------------------
    *Page 5*
    5
    *Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
    aliojaliwa na Mungu* *Sura 2: Mwanzo*
    *«. Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa
    mtu, Lakini mwisho wake ni
    njia za mauti. » Mithali 14:12*
    *« Bali wabaya wanafanana na bahari
    iliyochafuka; maana haiwezi kutulia, na maji yake hutoa tope na takataka.*
    *Hapana amani kwa wabaya; asema Mungu
    wangu. » Isaya 57: 20-21 *
    Na maisha ya nje ya Yesu Kristo ni sawa na
    ilivyoelezwa katika maandiko
    hapo juu. Niliondoka katika kijiji changu na N50 na anwani niliyopewa na Alice,
    kukimbilia *uhuru, haki,
    starehe *na yote yanayokwenda pamoja
    nayo: lakini kama utakavyoona hapo baadaye
    ilikuwa ni tofauti sana na kile
    nilichofikiria kwenye moyo wangu mdogo. Nilipofika Lagos , ilikuwa ni nzuri sana
    katika macho yangu na
    niliilinganisha na Mbinguni, chochote
    kile Mbinguni kulivyofanana. Niliona yale
    majengo yote marefu na mazuri na
    katika kila uso niliweza kuona furaha ( hivyo nikajiwazia). Watu walionekana
    kuwa na shughuli nyingi sana
    na kila mmoja alijali mambo/
    biashara yake. Nilipatwa na msisimko na
    nikajisemea moyoni , *"Sasa nimejua
    kuwa niko Huru!* Niliwasili Akintola Road, Victoria Island na
    nilipokelewa vizuri na Alice
    na wazazi wake. Wazazi wake walinijua
    mimi na historia yangu kwa sababu tunatoka
    katika kijiji kimoja lakini
    kamwe hawakujua uhusiano wangu na binti yao. Alice alinitambulisha tena kama
    kijana aliyemchagua amuoe.
    Wazazi walishtuka lakini baada ya
    majadiliano naye, walikubaliana juu ya hali
    yangu kwamba wangeweza
    kuniendeleza kielimu kwanza. Alice alikataa pendekezo lao na akaomba niwe
    ninaishi naye katika gorofa yake
    mwenyewe. Wazazi hawakuweza
    kukubaliana na hili lakini alisisitiza. Walikuwa
    na mabishano kuhusu hili
    kwa siku nne na kwa ushawishi usioelezeka walikubali na nikaishi na Alice.
    Alice, msichana ambaye ni mzuri sana,
    aliniambia kuwa alikuwa ni mhasibu wa
    Benki ya Standard na kwamba
    angeweza kunifanya mimi tajiri na kunipa
    vyote navyovihitaji katika maisha haya na alisema: " wewe kaa tu na
    ufurahie!" Mtazamo wangu ya kwanza kuhusu
    Lagos kumbe ulikuwa ni kweli;
    miezi michache iliyopita nilikuwa
    katika kibanda kidogo katika kijiji kidogo
    kulichozungukwa na chuki, njaa na mateso na mimi hapa, tazama
    ninaishi katika mji mkubwa, ghorofa nzuri na '
    mke ' mzuri ambaye
    aliniahidi kunipa maisha yeyote kadiri
    yanavyotoa. Alinimwagia zawadi, fedha ,
    mavazi, 'upendo' nk Mimi sikuwahi kamwe kujua kwamba dunia imejaa
    haya ' mambo mema . Shetani kweli ni
    mdanganyifu ! Maandiko dhahiri
    yanasema : " Mwizi haji isipokuwa
    kuiba, kuua na kuharibu. Mwana pekee wa
    adamu ( Yesu Kristo) anayeweza kukupa uhai na kukupa zaidi
    "(Yohana 10: 10). Ndugu msomaji, shetani
    hana zawadi ya bure ! Chochote
    anachokupa ni kwa ajili ya kuipata
    roho yako . Hali hii ya furaha ilikuwa ya muda
    mfupi, kwa sababu baada ya muda wa miezi mitatu mambo ya
    ajabu yalianza kutokea.
    *Uzoefu wa Kushangaza*
    Usiku mmoja, niliamka usiku wa manane na
    nikaona nyoka mkubwa aina ya boa -
    constrictor kando yangu. Nilitaka kupiga kelele lakini sikuweza. Usiku
    mwingine, niliamka na kuona
    mwili wa Alice kama unaoangaza
    kama mifuko ya Cellophane. Usiku mwingine,
    alitoweka na kutokea tena na
    tena. Usiku mwingine nilisikia kelele za ajabu au kucheza katika sebule n.k.
    Sikuweza kuvumilia tena matukio haya
    ya kutisha hivyo niliamua
    kumuliza, na jibu la kwanza ilikuwa ni vurugu
    na onyo kali. Alisema: "
    Usiniulize swali hili tena au nitapambana na wewe. "
    Tangu wakati huo nilijua maisha yangu
    yalikuwa hatarini. Niliona ni
    afadhali mateso kijijini kuliko kile
    nilichokuja kugundua. Nikawa ninamhofia. Siku
    mbili zikapita na akaja na tabasamu, zawadi na akanikumbatia.
    Akaniambia jinsi gani anavyonipenda na
    kunijali na akaniambia nisiwe na
    hofu na aliahidi kunieleza mambo
    ------------------------------
    *Page 6* 6
    *Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
    aliojaliwa na Mungu*
    fulani hapo baadaye. Alinichukua mpaka klabu
    na usiku ule alinikumbusha
    ahadi yake ya kunifanya mimi tajiri nk, na aliniambia: "Siku moja utajua yote
    ninayoyafahamu ! " Tukarudi
    nyumbani na maisha yakaendelea kama
    kawaida kati yetu. Ndani nilijua nilikuwa katika
    hatari , lakini nitawezaje
    kutoroka na wapi nitatorokea? Ni muhimu kukumbuka hapa kwamba wazazi wa
    Alice hawakumjua binti yao, ingawa
    ni mdogo, alijihusisha sana
    na uchawi na mizimu na alinionya sana kamwe
    nisije kuwaambia kama
    ninayapenda maisha yangu. Ndugu msomaji, unaweza kufikiria , msichana
    mwenye umri wa miaka 20 anafanya
    mambo haya yote? Dunia ya nje
    ilimwona kama msichana mzuri sana na mpole
    anayefanya kazi na Benki kubwa
    lakini alikuwa ni wakala mkubwa wa shetani. Kuna akina Alice wengi katika
    dunia ya leo kama utakavyokuta
    baadaye katika kitabu hiki.
    *Ugunduzi wa Kutisha*
    Siku moja, baada ya yeye kuondoka kwenda
    kazini, niliamua kufanya ukaguzi katika ghorofa. Pamoja na ujana
    aliokuwa nao, gorofa ilikuwa imejazwa vya
    kutosha. Alikuwa na friji nne na
    baada ya kufungua friji moja, niliona
    fuvu la binadamu, sehemu mbalimbali za mwili
    wa binadamu safi na kavu. Ndani ya dari kulikuwa na mifupa.
    Katika kona nyingine moja ya vyumba nikaona
    (kile baadaye nilijua kama
    'chamber') sufuria imejaa damu na mti
    mdogo katikati ya sufuria, kibuyu na nguo
    nyekundu pamoja nacho. Sikuweza kuendelea. Sasa nilijua kwamba
    nilikuwa ni mtu mfu na kwa kuwa sikuwa na
    mahali pa kukimbilia. niliyatoa
    maisha yangu kwa chochote
    kitakachokuja, maisha au kifo na naliendelea
    kufunga mdomo. Alice akarudi kutoka kazini na nilijua kabisa katika
    ofisi yake kuwa alijua nini nilichokifanya katika
    nyumba.
    *Kuingia katika ulimwengu wa Kichawi*
    Siku iliyofuata aliniomba nimfuate kwenye
    mkutano. Nilikuwa tayari ni mfungwa na sikuwa na uchaguzi.
    Tulikwenda kwenye jengo kubwa sana nje
    kidogo ya Lagos. Tulipowasili (jengo
    lilikuwa na ukumbi wa mkutano
    chini ya ardhi), nilielekezwa na Alice kuingia
    kinyumanyuma. Nilimtii na niliingia kwa mgongo, yeye pia alifanya
    hivyo. Ukumbi ulikuwa mkubwa wenye vijana
    na wanawake500 wameketi katika
    mduara, na aliyekuwa ameketi
    juu yao alikuwa ni mtu ambaye kichwa chake
    ndicho kiliweza kuonekana lakini hakikuwa na mwili, kama
    Kiongozi. Baadhi ya vijana hawa walikuwa
    wanafunzi, wanafunzi wa vyuo
    vikuu, wahitimu, walimu nk Alice
    akabonyeza kiswichi ukutani na kiti kikakatoka
    chini ya ardhi nami nikaketi. Yeye naye alifanya hivyo na kiti
    kingine kikatoka kwa ajili yake naye akaketi.
    Akanitambulisha katika
    mkutano ule kama mwanachama mpya na
    wao wakampongeza na kunikaribisha. Alice
    alikuzwa nafasi kwa sababu ya hili. Yote waliyoyajadili katika
    mkutano mimi sikuyaelewa. Mwishoni mwa
    kikao na tulipokuwa karibu kuondoka,
    niliambiwa nirudi peke yangu
    siku iliyofuata na Kiongozi. Hii ilikuwa ni mara
    yangu ya kwanza kukutana na dunia ya uchawi.
    Usiku huo huo, saa 2:00 (na hii ni saa ya
    kawaida ya mikutano na shughuli
    hatari za nguvu zote za giza na
    mawakala wao), Alice aliniamsha na
    akanifunulia mambo fulani. Alisema: "Mimi si binadamu wa kawaida. Mimi
    ni nusu binadamu na nusu roho lakini hasa ni
    wa rohoni. Unachokiona katika
    kona ya chumba changu ndicho
    natumia wakati wa maombi yangu ya kila
    asubuhi, ili roho zile ziniongoze kwa siku nzima. Kwa habari ya mifupa
    mimi nitakuambia baadaye. "
    Sikusema neno. Alileta baadhi ya vitabu juu ya
    siri za dunia kwa ajili
    yangu kusoma, na kwa sababu ya shauku
    ya kutaka kujua niliamua kuvisoma. Muda mfupi tu nilivipenda na akaona kuwa
    nimevipenda.Bila ya mimi kujua
    alituma jina langu katika jamii ya kichawi huko
    India. Kama nilivyokuwa
    nimekwisha elekezwa, siku iliyofuata
    nilikwenda peke yangu kwenye ile jamii na nikakutana na wengine tisa na
    baadhi ya mashahidi. Ilikuwa
    tunaingizwa rasmi. Tuliitwa pale katikati ya
    ukumbi na mambo yafuatayo
    tulifanyiwa:
    ------------------------------ *Page 7*
    7
    *Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
    aliojaliwa na Mungu*
    1. Mchanganyiko unaoonekana kama putty
    ulipitishwa juu ya miili yetu. Hii inakufanya uwe *mwanacham*
    *a kamili*.
    2. Glass yenye kimiminika kama mafuta
    tulipewa kunywa. Hii inakufanya kuwa
    *wakala.*
    3. Unga ulio kama wa risasi ulipakwa katika vichwa vyetu. Hii inakufanya
    uwe na uwezo wa
    kujifunza siri zao.
    Bila kujua, hii sherehe kumbe ilikuwa
    ikirekodiwa India na Siku ya pili
    nilipokea barua kutoka kwao. Katika barua nilielekezwa nitie doa kwa damu yangu
    mwenyewe na baada ya hilo
    niitume tena kwao kwa njia
    waliyoielekeza, si ya Posta. Nilifanya. Kutokea
    siku hii hakuna kurudi
    nyuma; kurudi nyuma ina maana ni kifo kama mmoja wao mara zote walinikumbusha
    hili na nilijua kuwa hakukuwa na
    matumaini tena kwa ajili yangu.
    *Makataba na Alice*
    Asubuhi moja mapema, aliniambia kulikuwa na
    sherehe muhimu inayotakiwa kufanywa katika nyumba. Saa 2:00
    usiku alileta mtoto anayetambaa, msichana,
    hai. Mbele ya macho yangu, Alice
    alitumia vidole vyake kunyofoa
    macho ya mtoto. Kilio cha mtoto yule kiliuvunja
    moyo wangu. Kisha akamchinja na kumkata mtoto vipande
    vipande na akaweka damu na mwili ndani ya
    tray na akaniambia nile.
    Nilikataa. Aliniangalia moja kwa moja
    kwenye macho yangu na kile kilichotoka
    kwenye macho yake hakiwezi kuelezeka kwa maandishi. Kabla
    sijatahamaki nini kinatokea nilikuwa si tu
    natafuna nyama lakini pia
    nilikuwa nakunywa damu. Wakati haya
    yanatokea, alisema: "Hii ni mkataba kati yetu
    sisi, kamwe hutokuja kusema nje chochote una chokiona mimi
    nakifanya au chochote kuhusu mimi kwa
    binadamu yeyote duniani. Siku
    ukivunja ahadi hii basi utakuwa
    umeondoka. "ikiwa inamaanisha kuwa siku
    nikivunja mkataba huu nitauawa. Baada ya tukio hili nilianza kuwa na hisia za
    ajabu ndani yangu.
    Nilibadilika na sikuweza kujizuia. Neno la onyo
    kwa akina mama. Je, unawajua wasaidizi wa
    nyumba yako? Ni vipi historia
    yake inafanana? Je, unajali kujua yote kuhusu yeye kabla ya kumkabidhi maisha
    ya watoto wako nk? Jinsi gani
    Alice alimpata mtoto anayetambaa
    na kumchinja, unaweza kujiuliza. Kwa hiyo
    wazazi, unatakiwa kujua historia
    ya wasaidizi wenu. Pale Alice alipoona kwamba amefanikiwa
    kunifanya kikamilifu kujihusisha na
    ulimwengu wa mapepo na
    nilikuwa nikiongezeka kwa kasi katika hilo,
    aliridhika na alijua mkakati
    wake umekamilika. Alinitafutia gorofa kwa ajili yangu, alinisaidia kuimalizia na baada
    ya hapo akajitenga na
    uhusiano.
    *Mkataba nchini India*
    Jumuiya ya Delhi, India ilinitumia barua ya pili
    ikinisihi niende India. Ndani ya barua pia walinielekeza nifanye
    yafuatayo: " Kula kinyesi, kula panya waliooza
    na wanaonuka, na kufanya
    ngono na mapepo katika makaburi
    wakati wa usiku"
    Baada ya kutimiza hayo hapo juu nilifungwa nisifanye ngono na mwanamke
    yeyote duniani. Nilituma majibu
    india nikiwataarifu kuwa sikuwa na visa na sijui
    jinsi ya kufika india. Kwa
    wakati huu nilikuwa nimeanza
    kufanya 'biashara'. Nilikuwa ni mfanyabiashara kiharamu mkubwa lakini kwa
    sababu ya nguvu hizi nyuma yangu
    sikuwa na shida na watu wa bandari nk
    Nilianza kuwa na fedha nyingi, chakula na vitu
    havikuwa tena adimu. Siku
    moja, nilifunga gorofa yangu na nikatoka; niliporudi, nikafungua mlango na
    tazama, mtu ameketi katika
    sebule. Niliogopa. Akasema: "Je, wewe
    ------------------------------
    *Page 8*
    8 *Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
    aliojaliwa na Mungu*
    si Emmanuel Amos?" nikamjibu ni mimi.
    Akasema: " nimetumwa kuja kukuchukua
    twende zetu India, Hivyo
    jitayarishe." Nilifunga kila mahali, nikaenda na kuketi kandokando yake
    nikisubiri amri inayofuata. Lakini kama
    umeme, alinigusa na tukatoweka kabisa.
    Sehemu iliyofuata nilijikuta niko mwenyewe
    ilikuwa ni kwenye ukumbi mkubwa
    wa mkutano Delhi, India, pamoja na umati wa watu wengine waliokuwa
    wamekaa tayari kwa ajili ya
    kutukaribisha. Walileta mafaili
    ambapo jina langu lilikuwa tayari limeandikwa
    na akaniambia niweke sahihi
    yangu pembeni.Nikafanya. Sahani iliyokuwa na nyama mbichi za watu,
    zilizokatwa vipande vipande na basini ya
    damu vililetwa. Jagi tupu za maji
    zililetwa na kila mtu akapewa yake,kasha mtu
    asiyekuwa na kichwa akawa
    akipita huku akimimina damu na nyama katika jagi zetu. Mishumaa tofauti
    tofauti iliwaka pamoja na ubani.
    Mwanaume asiyekuwa na kichwa
    akafanya manuizo na kila mtu akanywa damu
    na nyama na mkutano ukaisha.
    *Uingizwaji nchini India* Sasa kipindi cha kupimwa kikafika. Nilipelekwa
    kwenye bonde lenye mita 200
    kwa urefu. Ndani yake kulikuwa
    na mchanganyiko wa nyoka hatari na
    wanyama pori . Sikutakiwa kupiga kelele
    kwa sababu kama nikipiga kelele bai nimeshindwa mtihani na adhabu yake
    ilikuwa ni KIFO. Baada ya siku saba
    za uchungu nililetwa kwenye
    sehemu iliyoitwa ' INDIA JUNGLE'.
    Katika msitu huu niliona aina tofauti za ndege
    wa kipepo; ni ndege wa kipepo kwa sababu sura za ndege hawa
    zingine zilikuwa ni za mbwa, baadhi kama
    paka, n.k lakini wakiwa na
    mabawa.Ndani ya Msitu kulikuwa na
    pango na pango hilo lilifunguliwa tu na hawa
    ndege mapepo. Walifungua pango na nikaingia ndani. Mambo
    niliyoona ni vigumu kuelezea. Kulikuwa na
    viumbe wa kutisha, baadhi
    walionekana kama binadamu lakini wana
    mikia na bila sura za watu, nk Hii ilikuwa ni
    sehemu nyingine ya mateso. Mateso yale yanaweza kuwa kama nusu
    ya kuzimu. Nilikuwa katika hali ile kwa siku 7
    na kisha nilitolewa nje.
    Kisha nilipelekwa kwenye maktaba kubwa
    sana yenye vitabu vikubwa na vya
    kipepo kwa ajili ya kujifunzia. Baadaye nilichukua vitabu viwili: Abbysinia ,
    ambayo ina maana ya
    uharibifu, na Assina , ambayo ina maana
    kutoa uhai au kuponya. Baadaye nilipewa
    vitabu vingi zaidi. Nilipewa
    maelekezo ya kujenga chemba mara baada ya kurudi Nigeria na mambo yafuatayo ndani
    yake : " sufuria ya asili
    iliyojazwa damu ya binadamu, mti mbichi
    ndani yake, na fuvu la binadamu , manyoya ya
    tai , ngozi ya mnyama pori ,
    ngozi ya nyoka na udongo unaon'gaa kando ya sufuria. " damu ndani ya chungu
    ilitakiwa kunywa kila asubuhi na
    dua. Nilipewa maelekezo kuwa
    nisije kula chakula kilichopikwa na binadamu
    na kwamba nitalishwa
    kimiujiza. Nilirudi Nigeria kwa njia hiyo hiyo niliyoiendea, na kutekeleza yote .
    *Niliporudi nyumbani Nigeria*
    Sasa nilikuwa ni mmojawapo katika sehemu
    ya ulimwengu wa roho na ningeweza
    kusafiri popote pale sehemu
    yoyote duniani. Kwa mujibu wa vitabu nilivyoleta, ni kwamba viumbe wa
    kiroho (kipepo) wanaishi katika anga.
    Nilifikiri labda sasa wangeweza kuongeza
    nguvu yangu, hivyo niliamua
    kujaribu. Nilitoka nje ya nyumba yangu,
    nikafanya baadhi ya manuizo na kuita upepo wa kisulisuli nikatoweka.
    Nikajikuta mwenyewe katika anga na
    kuona hawa viumbe wa kipepo. Je, unataka
    nini waliniuliza; niliwaambia
    nataka nguvu.
    Nilikuja tena duniani baada ya wiki mbili baada ya kupokea nguvu kutoka
    kwao. Kama nilivyosema hapo awali,
    Sikuweza kujizuia/kujidhibiti mwenyewe.
    Pamoja na nguvu zote hizi
    nilizokuwa tayari nimezipokea, bado
    nilihitaji nguvu zaidi na zaidi ! Hivyo niliamua kwenda chini ya ardhi ili
    kuthibitisha kile kilichoandikwa katika
    vitabu nilivyopewa.
    ------------------------------
    *Page 9*
    9 *Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
    aliojaliwa na Mungu*
    Siku moja nilikwenda mahali fulani kichakani,
    nikafanya baadhi ya manuizo
    kama ilivyoelezwa kwenye vitabu
    nikaamuru ardhi kufunguka. Ardhi ikafunguka na mapepo yakaunda ngazi mara
    moja. Nikapiga hatua na kuingia
    moja kwa moja ndani ya ardhi. Kulikuwa na
    giza kuu ambalo linaweza tu
    kulinganishwa na moja ya mapigo
    ambayo yalitokea kule Misri kama iliyoandikwa katika Biblia. Niliona mambo
    mengi ambayo ni vigumu kueleza.
    Niliona watu walio katika minyororo, watu
    wanaotumika kwa ajili ya
    kutengeneza fedha - majukumu yao ilikuwa
    ni kufanya kazi mchana na usiku kukusanya fedha kwa watekaji wao.
    Nikaona baadhi ya wanachama wasomi/wenye
    akili wa jamii ambao walifika
    kutoa baadhi ya sadaka na walirudi
    duniani na baadhi ya zawadi walizopewa na
    mapepo yanayotawala sehemu zile. Niliona baadhi ya viongozi wa
    makanisa ambao walikuja kwa ajili ya kupata
    nguvu, nguvu ya kusema jambo
    lolote na linakubaliwa bila ya
    kuhoji katika kanisa. Nilikaa kwa muda wa wiki
    mbili na kurudi baada ya kupokea nguvu zaidi. Watu waliniona
    kama mdogo nisie na hatia lakini hawakujua
    nilikuwa ni hatari. Kuna watu
    wengi kama hao katikati yetu; ni wale
    tu walio katika Kristo Yesu pekee ndiyo wako
    salama katika hali halisi ya usalama.
    *Mkataba na Malkia wa Pwani(Queen of The
    Coast)*
    Jioni moja, niliamua kutembea tembea.
    Barabara ya kituo cha mabasi cha
    Ebute Metta, nilimuona msichana/binti mrembo/mzuri amesimama. Sikuzungumza
    neno lolote. Siku ya pili nilipopita
    pia nikaona bado yuko pale pale.
    Siku ya tatu nikamuona tena bado amesimama
    pale pale na nikajitambulisha
    kwake kama Emmanuel Amos. Lakini yeye alikataa kujitambulisha.
    Mimi nikamuuliza jina lake na anwani lakini
    yeye alicheka tu. Yeye
    akaniuliza yangu nami nilimuambia mtaani
    tu. Nilipokuwa nataka kuondoka, akasema
    atanitembelea siku moja. Kwenye mawazo yangu mimi nikasema,
    haiwezekani, sikumpa namba ya nyumba
    yangu basi sasa atawezaje kufika.
    Lakini ni kweli kwa maneno yake,
    nilisikia mlango wangu ukibisha baada ya wiki
    toka tumekutana pale katika kituo cha basi. Alikuwa ni yeye,
    msichana wa ajabu! Nilimkaribisha lakini katika
    mawazo yangu (Nilijiuliza
    msichana huyu mzuri atakuwa ni
    nani, je, hajui kuwa alikuwa amekanyaga
    katika uwanja hatari?) Nilimfurahisha naye akaondoka. Baada ya
    ziara
    hii ya kwanza, ziara zake zikawa mara kwa
    mara bila uhusiano wowote.
    Katika ziara zake alikuja kwa muda ule ule, na
    hakuja dakika moja kabla au iliyofuata! baadhi ya ziara zake
    nilipenda kumpeleka Lagos Barbeach, au
    katika Hoteli ya Paramount au Hoteli
    ya Ambassador nk Wakati wote
    huu, bado hakuniambia jina lake. Niliamua
    kutokuwa na wasiwasi kwani nilijua uhusiano wetu usingeendelea
    zaidi ya hapo. Nilikuwa nimepewa maelekezo
    kamwe nisiguse mwanamke.
    Ghafla ziara zake zikawa ni usiku. Katika ziara
    yake moja aliniambia: "Sasa
    ni wakati wako wewe kunitembelea mimi." Tulikaa pamoja usiku na saa 2:00
    asubuhi kesho yake tukachukuana.
    Tuliingia pamoja katika basi na
    alimwambia dereva atuache barbeach.
    Tuliposimama, nilimuuliza: "tunakwenda
    wapi?" Alisema: "Usijali, Utakwenda kufahamu nyumba yangu"
    alinipeleka kwenye kona ya barbeach,
    akatumia kitu kama mkanda na
    kuufunga ukituzunguka na mara moja nguvu
    fulani ikaja kutoka nyuma yetu na
    kutusukuma ndani ya bahari. Tukanza kupaa juu ya uso wa maji na moja
    kwa moja tukaingia ndani ya
    bahari. Ndugu msomaji, hiki kilitokea
    nikiwa katika mwili wangu! Wakati ule
    tumezama ndani chini kwenye kitako
    cha bahari kwa mshangao nikajiona tuko tunatembea kwenye barabara ya magari
    ya mwendo kasi . Tukaenda mpaka
    kwenye jiji lenye watu wengi
    na walio na shughuli sana.
    *Ulimwengu wa Roho*
    Niliona maabara nyingi, kama za maabara za sayansi, maabara za kubuni, na
    ukumbi wa michezo(theatre). Nyuma
    ya mji, niliona wasichana wazuri na vijana
    wazuri. Hakuna wazee.
    Akanitambulisha kwao na walinikaribisha.
    Akanipeleka kwenye sehemu kama "chumba cha giza", "chumba cha kukaushia",
    na "chumba cha kufungashia."
    ------------------------------

    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate