*Page 20*
20
*Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
aliojaliwa na Mungu* jengo moja kubwa na refu lililofanana na jengo
la mikutano. Tulipokanyaga
ndani ya sakafuni tu sauti kutoka
ndani ikasema: "*Muingizeni ndani"
*Waliniingiza ndani kisha wakatoweka, na
kuniacha peke yangu. Nilichokiona ndani ya ukumbi huu ni vigumu
kueleza, lakini nitajaribu
kuelezea kadiri nitakavyoweza. Ukumbi
ulipambwa vizuri sana na ulikuwa mkubwa
sana na mrefu kiasi kwamba ilikuwa
ni vigumu kuona mwisho wake. Nilitembea mpaka katikati na ndipo niliweza wa
kuona mwisho wake. Mwishoni
kulikuwa na madhabahu. Kisha
nikaona kiti cha enzi na na aliyekuwa ameketi
juu ni mwanaume mzuri sana
mwenye nguo inayong`aa kama jua. Akasema: *"Njoo!" *Lakini kwa sababu ya
mwangaza wake sikuweza kwenda. Kila
nilipojaribu kunyanyua mguu
wangu nilianguka.
Nilisimama, nikajaribu tena na nikaanguka.
Ghafla mtu huyo akatoka kwenye kiti cha enzi alipokuwa
amekaa,akahamia kwa juu kidogo nilipokuwa
nimesimama. Kisha mikono miwili
ikatoka nje ya mtu huyo,
ikanishika kichwa changu na kunitikisa na mwili
wangu wa kibinadamu ukajivua kama unavua nguo.. Na yule
mimi mwenyewe sasa akasimama. Mikono
akaikunja kama mtu anaye kunja nguo na
akaitupa kwenye kona. Mtu
yule akarudi tena kwenye kiti chake cha enzi
na akakaa na kusema tena: *" Njoo! "*
*Kutakaswa Kiroho*
Nikatembea mpaka pale naye akasogea
kutoka katika kiti cha enzi, akanyofoa
miguu yangu mmoja baada ya
mwingine na akamwaga kile kilichokuwa ndani yake, na akaiweka tena vizuri.
akafanya hivyo pia kwenye
mikono na akaiweka tena, Yaani ni hivi
sehemu zote ambazo Malkia wa Pwani
aliweka nguvu zake humo.
Nikatafakari sana kwenye fikra zangu, huyu atakuwa nani na amejuaje kuwa
maeneo haya ndiyo yalikuwa
yametunza nguvu zangu. Baada ya haya
alirudi tena kwenye kiti chake na
akaniambia niende. Nilipoanza tu
kutembea, vitu fulani vikaanza kuanguka kutoka kwenye mwili wangu , magamba
yakaanguka kutoka katika
macho yangu, nk, lakini kabla sijafikia
madhabahu tayari vikaacha.
Aliniuliza. *" UNAKWENDA WAPI ?"*
Nikajibu, nikasema, "Ninaenda Onitsha kumuona rafiki."Akasema: *"Ndiyo,
lakini mimi nitakuonyesha nini*
*ulichopanga kwenye akili yako*. " Hadi wakati
huu sikujua alikuwa ni nani,
lakini jambo moja nililokuwa na
uhakika nalo ni kwamba alikuwa mwenye nguvu zaidi kuliko nguvu zote
nilizowahi kukutana nazo. Alisema kwa
ishara na mtu ambaye aliamriwa kunionyesha
mimi nini nilichokuwa
nimedhamiria moyoni kukifanya. Mtu huyu
alinipeleka kwenye chumba na akufungua kitu kama ubao. Kwa kweli, kama
kulikuwa na njia ya kutoroka
ningeweza kutoroka, kwani mbele yangu
yaliandikwa yote niliyopanga kufanya
dhidi ya Wakristo na mpango
wangu dhidi ya kania la Assemblies of God, Silver Valley. Mtu huyu
akanileta tena madhabahuni na akaniacha.
Akatoka katika kiti cha enzi na akanishika kwa
mikono yake na akasema kuwa
anakwenda kunionyesha mimi
mambo fulani. Tulipokuwa njiani Akasema: *"Mimi sitaki wewe upotee lakini
nikuokoe na hii ni nafasi yako *
*ya mwisho. Kama hautatubu na kuja
kunitumikia, utakufa. *Nitakuonyesha
makazi ya waliookolewa na
waasi." Alivyosema hivyo, nikajua alikuwa ni *Yesu Kristo.*
*Ufunuo wa Kimbingu*
Tukaingia katika chumba fulani na akafungua
kitu kama pazia. Niliona dunia
nzima, watu na shughuli zote za
kinachoendelea. Nikaona Wakristo na wasio wakristo wote wanafanya jambo
moja au jingine. Tulikwenda
kwenye chumba cha pili . Akafungua pazia
tena na nilichokiona ilikuwa ni
kitu mbaya kuonekana. Watu
wamefungwa minyororo ! Aliwaita watu hawa " *wanafiki. *"Watu hawa
walionekana ni watu wenye huzuni
kubwa, Akasema: ". *Watabakia hivi mpaka
siku ya hukumu "*
Tulienda katika chumba cha tatu. Akafungua
pazia na nikaona watu wengi wanafuraha na wakiwa wamevaa
mavazi meupe. Wakati huu nikamuuliza : " Ni
kina nani hao " Akasema: *"Hawa
ni wale waliokombolewa *
*wanasubiri ujira wao. " *Tulikwenda katika
chumba cha nne na nilichokiona kilikuwa cha kutisha mno.
------------------------------
*Page 21*
21
*Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
aliojaliwa na Mungu* Ndugu msomaji, ni vigumu kuelezea.
Ilionekana kana kwamba mji mzima unawaka
katika moto. Kuzimu ni halisi
na niyakutisha. Kama ulikuwa umefanywa
kuamini kwamba Mbinguni na Kuzimu ni
hapa duniani na kwamba hakuna maisha mengine mara baada ya kifo
bali ni kuoza na kupotea kabisa,
ni bora ukashauriwa vizuri hapa na
sasa kwamba kuzimu halisi ni halisi na kuna ni
kweli mbingu ipo!
Usistaajabu Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani Aliwaonya watu kuhusu kuzimu.
Nasema tena , kuzimu ni halisi.
Niliiona na ni mahali pa kutisha.
Nikamwuliza : " Ni nini ?" Jibu lake lilikuwa :
*"Hii imetayarishwa kwa
ajili ya shetani na malaika wake na* *kwa walioasi" *Akataja kwa majina yao kama
ilivyoandikwa katika Ufunuo
21:8: "Bali waoga na wasioamini na
haramu, na wauaji, na wazinzi na wachawi,
waabudu sanamu na waongo wote,
sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti ambayo ni mauti ya pili
" .
Tulipoenda katika chumba tano na Alipofungua
pazia, nilichoona kinaweza tu
kuelezewa kama UTUKUFU.
Ilikuwa ni kama tunangalia kutokea kwa juu. Niliona *mji mpya*. Mji ulikuwa
ni mkubwa na mzuri! Mitaa ni ya
dhahabu. Majengo hayawezi kulinganishwa na
kitu chochote katika dunia hii.
Alisema: " *hili ni tumaini la watu*
*wa Mungu. *Je, utakuwepo mahali pale "Haraka nikajibu" Ndiyo " Baada ya
hayo tulirudi katika kiti cha enzi na
Akasema: "!*Nenda kashuhudie nini
nilichokufanyia "*
Tena, alinichukua mpaka katika chumba
kingine na alipofungua pazia nikaona mambo yote ambayo nilikuwa
naenda kukutana nayo kwenye safari yangu
ya kwenda Onitsha na Lagos na
jinsi gani hatimaye atanikomboa.
Baada ya hayo Akaniambia : *"Usiogope,
nenda, nami nitakuwa pamoja nawe." *Aliniongoza,
nje ya ukumbi
na akatoweka kabisa, na mara nikaamka
kwenye kitanda katika nyumba ya
mwanaume mwingine. Nikapiga
kelele, mtu na mke wake wakakimbia kutoka katika chumba chao. Wakachungulia
na kisha wakaingia "Kwa nini
niko hapa? " Niliuliza. Mwanaume yule ndio
alielezea jinsi nilivyoanguka
katika teksi na jinsi walivyonipeleka
kwenye kanisa la Katoliki pale Owerri. Jinsi walivyomleta Daktari, ambaye
alikuja na baada ya kunichunguza
afya yangu alisema mapigo yangu yalikuwa ya
kawaida na kwamba wanapaswa
kusubiri na kuona nini
kitatokea. Daktari akawapa uhakika kwamba nitapata nguvu tena. Ndipo
alinichukua kwenye gari lake mpaka
nyumbani kwake na alikuwa akisubiri. Pia alikiri
kwamba hakujua kwa nini
alimuamini Daktari na kwa nini
alichukua jukumu la kunichukua mpaka nyumbani kwake.
Waliniuliza jina langu na anwani ambayo
niliwapa na baada ya hapo niliamua
kukaa kimya na sikuwaambia
uzoefu wangu huo. Nilikaaa kwa utulivu na
familia hii yenye wema kwa siku mbili na kisha mtu huyu na mkewe
walinipeleka mpaka kituo cha magari cha
Owerri, ambapo nilichukua teksi na
kwenda Onitsha. Yote yale Bwana
alinionyesha kuhusu safari yangu yalitokea
moja baada ya jingine. Nilichukua teksi nyingine ya kwenda Lagos.
Jambo la kwanza asubuhi iliyofuata. Nilitii na
kuondoka Lagos kuelekea Port
Harcourt. Huwa najiuliza mara
nyingi, kwa nini Bwana aliamua kuniokoa mtu
kama mimi. Mtu muovu na muharibifu, wakala wa Shetani !
Nilipata jibu katika maneno haya matatu:
*Mungu ni upendo*. Hakika, Mungu
ni Upendo! (1 Yohana 4:8 , 4:16)
------------------------------
*Page 22* 22
*Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
aliojaliwa na Mungu*
*Sura6: Vishawishi na Ushindi*
*« Kondoo wangu huisikia sauti yangu; mimi
nawajua, nao hunifuata. Mimi nawapa uzima wa milele; nao*
*hawatapotea milele, wala hakuna mtu
atakayeweza kuwatoa mkononi mwangu.»
Yohana10: 27-28*
Baada ya kubadilika na kwenda kwa Kristo,
jambo la kwanza lililotokea ni kwamba zawadi zote kutoka baharini,
darubini, TV, mashati, picha nilizopiga nikiwa
ndani ya maabara za baharini
na picha ya Malkia wa Pwani ambazo
zilionekana katika gorofa yangu zilitoweka.
Niliporudi Port Harcourt, nilikuwa na hamu ya kushuhudia kile Bwana
alichonifanyia kwa ajili yangu lakini
sikuruhusiwa ndani ya kanisa . Mke wa
marehemu mjomba wangu, ambaye pia ni
Mkristo, alinichukua mpaka
kwa mchungaji mmoja, lakini swali alilouliza lilikuwa ni: "Je,ameleta
karatasi?" Ilikuwa ni baadaye sana
nilielewa kwamba karatasi ilikuwa ni 'barua ya
uanachama. Barua ya
uanachama inahusika vipi na ushuhuda
wangu wa nguvu ya Kristo na kile amefanya kwa ajili yangu- Mungu,
amenikomboa kutoka katika nguvu za giza
na kuniingiza katika ufalme wa Mwana wake
mpendwa, ambaye nimepata ukombozi
kupitia damu yake, yaani,
na hata msamaha wa dhambi zangu ? Nilihuzunika, baada ya kujua kwamba Shetani
haruhusu waumini wachanga
kwenda na kushuhudia, hasa wale
ambao hapo awali walikuwa washiriki wakubwa
katika shughuli zake , na
anafanya kila kitu kuzuia shuhuda hizo. Tena nikakumbuka, ni dhahiri Bwana aliniagiza
"*kwenda na kushuhudia kile
amenifanyia *" na hapa nilikutana
na kipingamizi. Labda ilikuwa bado si wakati
wake. Hivyo niliamua kuachana
na kutoa ushuhuda wangu kwa mtu yeyote. Nilisafiri na wafanyabiashara
watatu kutoka Aba kwenda Togo kwa
safari ya kibiashara. Pale
nilinunua bidhaa yenye thamani ya N160,000
(Mia moja na sitini elfu za
Naira). Kati ya pesa hizi pesa yangu binafsi ilikuwa ni shs N70,000 na nyingine yote
iliyobakia N90 ,000
nilikopa kwa wafanyabiashara wa Aba.
Miongoni mwa mambo niliyonunua ilikuwa ni
furushi la kamba, madawa
mbalimbali ( hasa antibiotics ) , sindano, vipimajoto, nk
Nilipofika mpakani mwa Nigeria, Tulishikiliwa
kwa ajili ya ushuru wa
Forodha na baadaye tulitakiwa kutoa
rushwa. Tulikataa na bidhaa zilikamatwa ikiwa
ni pamoja na zile za wenzangu. Miezi michache baadaye, Ile
mizigo ya wenzangu ilitolewa, ila yangu
haikuruhusiwa. nilirudi baadaye na
nikaambiwa kulipa N40,000, lakini
nilipoangalia mali yangu ile niligundua kwamba
bidhaa zote muhimu, kama furushi la kamba, sindano, madawa,
nk, tayari vilikuwa vimeibiwa. Nilitathmini bidhaa
iliyobaki na nikajua
kwamba kulipa N40,000 kwa ushuru
itakuwa tu ni kuongeza hasara, hivyo niliamua
kuachilia bidhaa iliyobaki. Wafanyabiashara ambao niliwakopa fedha
walianza kunifukuzia. Baadhi
waliwaita polisi, wengine walichukua
sheria mkononi mwao na wakapanga
kunifanyia kitu kwa maisha yangu.
Suluhisho pekee lilikuwa ni kufunga akaunti yangu Bank na kutumia fedha zote
nilizokuwa nazo kulipa madeni
yote. Kwa neema ya Mungu, nililipa
yote isipokuwa N1,000 ambayo ilikuwa ni kwa
ajili ya mwenye nyumba wangu
Lagos. Nilikuwa mufilisi kabisa na nilikopa hata 20k kwa ajili ya nauli ya teksi.
Nilikwenda kwa wakristo wachache niliowajua,
ili kutafuta msaada wa
kuniwezesha kuanza upya. Hakuna
aliyesema ndiyo au hapana, badala yake
walinisihi niende siku inayofuata kila mara nikachoka kwa habari ya
kutafuta msaada. Sikujua neno la Mungu
pamoja na kuchanganyikiwa katika
moyo wangu nilisoma Biblia bila
kuelewa. Wakati bado natafakari nini cha
kufanya, nilipokea simu ya haraka kutoka kijijini mwangu. Nilikimbia
nyumbani na kukuta kwamba jengo dogo
nililokuwa nimeanza kujenga lilikuwa
limevunjwa na mjomba wangu
ambaye pia alikuwa ametishia kuniua. Asili
yangu ya kale ndani yangu ilishtuliwa. Nikakumbuka wakati nikiwa
na jamii ile ya baharini (secret society), jinsi
alivyokuwa akiniogopa na
alikuja kwa magoti mbele yangu. Lakini
sasa alijua nimebadilika (jinsi alivyojua sikujua
kwani sikuwa nimesafiri kwenda nyumbani tangu nilipobadilika)
------------------------------
*Page 23*
23
*Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
aliojaliwa na Mungu* na sasa alinitishia. Nilimuita Bwana na
nikasema: "Basi, wewe umeniokoa
mimi na kuniacha nimevurugika na
kuruhusu adui zangu kufurahia juu yangu! "
Nililia kwa sauti nikadhamiria
kurudi kwenye ile jamii ya kichawi. Angalau wanaweza kuniokoa kutoka katika
kuchanganyikiwa kote huku na pia
watafundisha mjomba wangu
somo ambalo hatasahau maisha yake yote.
Ingawa nilifanya uamuzi huu,
nilikuwa na hofu mbili ndani yangu 1. Wakati nilipokuwa nabadilika, Bwana
aliniweka wazi akaniambia: " *Hii ni
nafasi yako ya *
*mwisho. *" Ukirejea tena kwenye jamii ile ina
maana ni kifo, sio tu kifo
cha kimwili lakini pia cha kiroho.
2. Kama nikibakia katika Bwana, mjomba
wangu alikuwa anatishia kuniua.
Nilichanganyikiwa na nilihitaji msaada. Nilikuwa
mjinga wa neno la Mungu na
kamwe sikujua kile ambacho Neno linasema kwa habari ya hayo juu. Ndugu
msomaji , utagundua hapa kwamba
nilikuwa na mchanganyo
huu wote kwa sababu ya ukosefu wa
mfuatiliaji nikiwa bado mchanga.
Kuwafuatilia waongofu wachanga ni muhimu sana na Wakristo wanapaswa
kuchukulia hili kwa umakini. Kama unajua
huwezi kufuatilia muumini
mchanga, tafadhali usiende kushuhudia. Yesu
Kristo alisisitiza hili mara
tatu Alipomuuliza Peter: " Simoni, mwana wa Yona, wanipenda mimi zaidi kuliko
hawa? ... Lisha kondoo wangu.
"Wengi wa waongofu wapya
wanarudi nyuma kwa sababu ya kukosa
ufuatiliaji mzuri. Kama unampenda Yesu,
jali kondoo wake! *Vita na shetani*
Katika kipindi hiki mawakala wa Malkia wa
Pwani walianza kunitafuta sana.
Niliteseka sana katika mikono yao.
Nilikuwa na ndoto mbaya. 1 Mei 1985, mwezi
mmoja baada ya kuokoka saa 02:00 usiku, wengine katika nyumba
walikuwa wamelala. Niliamshwa na mawakala
hawa. Wakaniamuru kutoka nje ya
nyumba. Nilitii, nikatoka nje
na walinifuata nyuma. Ilikuwa kama yote
yanayotokea ni ndoto, lakini hii ilikuwa katika uhalisia. Tulitembea
mpaka juu ya ardhi ya maziko kanisa la
Mtakatifu Paulo Anglican , off Aba
Road, Port Harcourt.
Tulipofika pale walisema: "Ni lazima urudi.
Kama ukikataa tutakuua au kukufanya fukara. "Baada ya maelekezo
haya waliondoka. Nikapata ufahamu wangu na
kujishangaa nimefika vipi pale
makaburini. Nikarudi kitandani na
kulala. Waliamua kuwa wananishambulia
mchana. Mara kwa mara, wakati natembea kandokando ya barabara
walijaribu kupambana na mimi. Wengine karibu
yangu waliniona napambana na
hewa au kuniona nakimbia kama
mtu anayefukuzwa.
Mimi peke yangu ndiye niliewaona. Basi, walifanya hivyo kwa mara nne na
wakaacha. Kisha kiongozi wao ,
Malkia wa Pwani, achukua jukumu. Siku ya
kwanza alikuja katika gari ambalo
aliliegesha kando ya nyumba yetu.
Alikuwa amevaa vizuri na kama kawaida yeye ni mzuri sana. Watu
walionizunguka walimchukulia kuwa ni
mpenzi wangu. Mara akaingia ndani nilijua
alikuwa ni nani. Alikuja saa
12.00 mchana wakati eneo lote lilikuwa
busy kidogo. Akakaa chini na miongoni mwa mambo mengine aliyoyasema ni:"
Unaweza kwenda kanisani
kwako, amini chochote unachotaka kuamini,
*lakini kama tu hautanitangaza*,
nami nitakupa chochote kile katika
maisha haya " Sikuwa nimejua maandiko hivyo nilimsikiliza na kumuangalia
anatembea tembea pale. Aliomba
na alijaribu kunishawishi nirudi kwake.
Sikusema ndiyo au hapana kwake.
Alisimama, akaenda ndani ya gari
yake na akaondoka. Kama mara mbili hivi mke wa mjomba wangu
alimkaribisha nyumbani kwake bila
kujua alikuwa ni nani nami
kamwe sikuwahi kumwambia mke wa mjomba
wangu alikuwa ni nani. Ziara yake ya
mwisho alibadili namna yake ya kunisihi. Wakati huu alinipa onyo kali
akisema kwamba amejaribu
sana kunibembeleza nirudi kwake na
kwamba nimekuwa mkaidi sana, na kwamba
hii ilikuwa ni ziara yake ya mwisho.
Kama bado nakataa kurudi, atakuja mwezi Agosti ama kuniua , au
kunilemaza au kunifanya maskini. Kisha
akaondoka.
Nilikuwa na hofu, hivyo siku moja nilikwenda
kanisani na kumuita ndugu
mpendwa. Nilimwambia matatizo yangu na mtazamo wangu juu ya baadhi ya
washirika wa kanisa , nk Huyu ndugu
alinipa anuani ya ofisi ya umoja
------------------------------
*Page 24*
24 *Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
aliojaliwa na Mungu*
wa maandiko (Scripture Unions ) na
akaniambia: *" Pale watanipatia msaada*"
Siku hiyo ilikuwa ni siku ya
mwisho kumuona huyu " ndugu." Sijawahi kumuona popote Port Harcourt mpaka
leo. Nilichukua anwani na siku
iliyofuata, nilichukua teksi mpaka No 108
Bonny Street, ambapo zilikuwa
ofisi hizo ni na kukutana na mchapaji
ambaye alinipa robo ya mpangilio wa shughuli za Umoja wa Maandiko (SU)
Kundi la Rumuomasi Pilgrims,
wakiwa ndio karibu na mimi. Akasema: " Njoo
siku ya Jumapili! " Nilikuwa
pale katika Fellowship Centre -
Shule ya St Michael's State , Rumuomasi - saa 8:00 mchana, bila kujua
kwamba ibada inaanza saa 9:00 mchana,
lakini nilikutana na kikundi cha maombi, hivyo
nikajiunga nao .
Baada ya ibada siku hiyo nilijua kwamba
mahali pale palikuwa sahihi kwangu.Mungu akanipa msichana ambaye
alikuwa kama mama kwangu, yeye alijitoa
kikamilifu katika kunielezea Neno
la Mungu na kunishauri pia. Ndugu
wakaonyesha utayari na kunijali. Niliona
Upendo wa kweli. Roho Mtakatifu alianza kunipa ufahamu wa Neno la
Mungu na imani yangu ilikua. Lakini Malkia wa
Pwani hakujionyesha kwa
sababu aliwekwa wazi. Zaburi 91,
Ulinzi wa Mungu, ulitimia katika maisha yangu.
*Isaya 54:17*: "*Silaha yoyote itakayofanywa juu yako *
*haitafanikiwa, na ulimi wowote utakaoinuka
juu yako katika hukumu wewe
utauhukumu. Hilo ndilo fungu la urithi *
*la watumishi wa Yehova, na uadilifu wao ni
kutoka kwangu," asema Yehova.. *"Hii pia ilitimia.
Septemba 1985, Nilipokea ujumbe kuwa jina
langu limeonekana kama msambazaji
wa Silver Brand Cement,
Lagos na kwamba nilitakiwa kufika ofisini
tarehe 27/9/85.Niliondoka Port Harcourt tarehe 26/9/85 na kufika
Lagos usiku. Asubuhi iliyofuata 27/9/85,
nilikwenda ofisini nikaambiwa na
Meneja Utumishi kuwa sehemu
yangu ilijazwa na mtu mwingine. Akanieleza
nifike siku iliyofuata tarehe 28/9/85 kumuona Mkurugenzi
Mtendaji. Nilipokuwa njiani kuelekea nyumbani
kwangu, nikipita njiani, mtu
akaja kutoka nyuma na kunikaba
na akajaribu kubana pumzi yangu na mdomo
wangu kwa pamoja. Nilijitahidi kuokoa maisha yangu, na ingawa
watu walikuwa wanapita, hakuna aliyekuja
kuniokoa, lakini Bwana aliingilia
kati. Wakati mimi bado najitahidi
kwa mikono nikasikia akilia kwa sauti na
kunisukuma mbali akisema : "Ni nani huyo aliyeko nyuma yako? "
Alirudia mara ya pili na kutoweka. Kutoka kwa
sauti nilijua alikuwa ni
mwanamke lakini kamwe sikumuona ni
nani. Nilichanganyikiwa na kupigwa na
bumbuwazi. Hapa tena mwenye nyumba wangu alikuwa na
hasira sana na akasema: " Kwa nini
umekimbia na fedha ya kodi
yangu?" Nilimsihi na nikajaribu kumuelezea
kwamba kwa sasa mimi si kazi na
nitamlipa fedha zake zote kwa haraka mara nipatapo fedha.
Kwa jinsi alivyoonyesha nilifikiri suala hili
limeisha. Siku iliyofuata
28/9/85, nilikwenda na kukutana na
Mkurugenzi mtendaji ambaye aliomba
msamaha kwa kumpa nafasi yangu mtu mwingine. Alipokuwa bado
anaongea kijana mmoja akaingia na kuniuliza:
" Je, wewe sie Emmanuel?
"Nikasema ndiyo ni mimi: "Ndiyo ,
mimi niko. " Akasema: "Ndiyo, hatimaye
tumekupata sasa! Je, umemaliza kukimbia? Tumetembelea mara kwa
mara Port Harcourt na kugundua kwamba
daima huwa unatembea na mama yako wa
kiroho. Amekuwa kikwazo
sana kwetu na sasa kwa sababu umekuja
Lagos tumekukamata! Hautarudi tena Port Harcourt. Mimi ndiye
nimechukua nafasi yako " Nikampa
changamoto na kumwambia : " Huwezi
kunifanya kitu chochote "
Mkurugenzi Mtendaji alishangazwa na kile
kilichotokea katika ofisi yake ! Nikaomba radhi mwenyewe na
nikarudi nyumbani.
Dakika chache baadaye nikasikia mlango
unabishwa na NINA akaingia.
Akaniuliza kama nilikuwa narejea Port
Harcourt. Nikajibu ndiyo. Aliniomba nirudi kwao akanieleza kuwa kazi
nilizokuwa nimefundishwa zilikuwa
hazipatikana mtu wa kuzirithi: KOTIPARI
( katika lugha ya Kiyoruba ).
Nilikuwa nimepatiwa mafunzo :
- Kuwa juu ya mawakala wa nguvu za mapepo.
- Kuwa juu ya " chumba cha bahari cha
maelekezo, " kufuatilia matukio
katika dunia, kutuma na kupokea
ishara, na kuhamasisha majeshi, nk
- Kuwa karibu na Malkia wa Pwani. Hii inahusisha si tu sherehe, sadaka ,
utekelezaji wa kazi maalum
------------------------------
*Page 25*
25
*Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu*
alizonituma, lakini pia mambo mengine
magumu kuelezea.
- Kwa msaada wa nguvu za giza , kuanzisha
jamii mpya za siri(jamii ya
kichawi) ambazo zitaonekana hazina madhara ili kuwavutia vijana na zaidi waendaji
tu wa kanisani .
Alisema, kama ataongozana naye, kilichokuwa
kinanisubiri ni mara mbili ya
baraka za kwanza. Alikiri kwamba
walihusika kwa mali yangu kukamatwa na kuibiwa, pia kwamba wao ndio
waliomchochea mjomba wangu
kuharibu jengo langu na kutishia maisha
yangu. Kwamba kama nikikataa
kumfuata, wangefanya zaidi na
kuhakikisha kwamba sitafanikiwa. Kwamba walikuwa wameamua kupambana mama
yangu wa kiroho: "Kama
tutampata yeye, tumekupata wewe" alisema.
Wakati huo, Nilianza kumhubiria.
akasimama na kusema:
"Wanakudanganya, " Akaondoka. Hii ilifanyika jioni ya tarehe 28/9/85 .
Mara dakika tano zikapita nikasikia mwingine
anabisha. Wakati huu walikuwa
watu wanne. Wakanionyesha
ishara nitoke nje na nikajiona mwenyewe
naanza kuwafuata. Tulitembea hadi katika nguzo 2 na mmoja wao
akaniuliza: "Je, unatujua sisi? " nikasema
hapana. Aliendelea kusema: "
Tumeajiriwa na mwenye nyumba wako
tukuue." Wakati anaendelea kuzungumza
mmoja wao akatoa bunduki na mmoja akatoa sime. Sikujua cha
kufanya, nilijua kuwa wataniua, lakini Mungu
katika Njia zake za ajabu
akafanya ishara ambayo ilinishangaza
mimi na wenyewe.
Mtu aliyekuwa na bunduki akanifyatulia risasi lakini hakukuwa na sauti. Mtu
mwenye kisu akakitumia nyuma ya
mgongo wangu lakini hakikuingia ila tu kililia
kama mtu anamchapa fimbo
mtu. Walikuwa na hofu kama mimi.
Roho wa Mungu alikuja juu yangu na nikaanza kuhubiri. Watatu wao
wakakimbia, lakini mtu wa nne akaanguka
na akaanza kulia na kuniomba nimuombee.
Sikuweza hata kujua nini cha kuomba
wakati huo lakini nilisema tu:
" Bwana, tafadhali msamehe, Msamehe bwana. Amina! " Aliyalitoa maisha yake
kwa Kristo, Nilimpeleka kwenye
kanisa la Pentekoste na alielezea kile
kilichotokea kwa Mchungaji.
Nilimkabidhi kwa Mchungaji na nikaondoka.
Nilipoingia tu ndani ya nyumba mwenye nyumba akaja anakimbia na akapiga
magoti akinisihi: " Tafadhali
nisamehe. Nilidhani uliamua kukimbia kwenda
Port Harcourt kwa sababu ya
fedha yangu (N1,000).
"Nilimsamehe na hatimaye tulikubaliana kwamba fedha ilipwe kwa awamu .
Usiku huo, mida ya saa 08:00 usiku Bwana
aliniamsha. Sikuweza kujua kwa
nini niliaamka nikaenda sebuleni na
nilichokiona ilikuwa ni kobe mkubwa
ananifuata. Mara nikakumbuka shule ya kujifunza Biblia tulipokuwa Port
Harcourt, juu ya nguvu katika neno. Ndipo
nikasema maneno haya: " Kobe ,
tangu nilipozaliwa , nyumba ya kobe
ni ama kichakani au baharini, lakini kwa kuja
ndani ya nyumba wakati madirisha na milango ni imefungwa
umefanya dhambi, na kwa sababu hii ni lazima
ufe. "Mara baada ya kusema
hivi akatoweka kabisa. Nilikwenda
chumbani na kulala. Mara ya pili tena, niliamka
na kusikia kelele sebuleni. Nilikwenda na tazama mbele yangu
ilikuwa ni kitu cha kutisha. Nikarudia maneno
yaleyale na mara baada ya
kusema: "Kwa kutenda dhambi hii
lazima kufa, " kikatoweka pia. *Wakati wa
safari hii ya Lagos niliona wema, ukuu wa Mungu na uaminifu*
*wake.*
Asubuhi iliyofuata tarehe 29/9/85, nilichukua
basi zuri sana mpaka Port
Harcourt. Nilipofika Ore ,basi likagonga
mti. Liliharibika kidogo lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa. Dereva akalivuta
kwenye barabara na akaendelea
kuendesha, basi likaanza kuyumba kutoka
upande mmoja wa barabara hadi
mwingine. Nikakumbuka vitisho vya
NINA, hivyo nikasimama katika basi, na kuhubiri nilihitimisha kwa kusema :
"Ni kwa sababu yangu mimi haya
yanayotokea. Lakini tangu sasa , hakutakuwa
na ajali mpaka tufike Port
Harcourt, katika jina la Yesu ! "Na mimi
nikakaa. Kwa kweli, wakati nimeketi nilishangaa, kitu gani nimekisema. Na
hivyo ndivyo ilivyokuwa. Gari
lilitembea
vizuri
mpaka
Port Harcourt.
Hakukuwa
na
ajali
zaidi
au kuharibika.
Biblia inasema sawa kuwa*;"Mtu yeyote
akishambulia, haitakuwa kwa maagizo
yangu.Yeyote atakayekushambul*
*ia ataanguka kwa sababu yako."(Isaya 54:
15). *Wao ( Malkia wa Pwani na mawakala wake ) walijaribu, lakini
kwa sababu mkutano wao haukuwa katika
Bwana bali kinyume na mtoto wake
,wote wakajikwaa na kuanguka.
"Pindi adui atakapokuja kama mafuriko ya
mto, Roho wa Mungu atainua kiwango dhidi yake" (Isaya 59: 19).
Nampa Mungu utukufu wote kwa ajili ya
kujionyesha mwenye nguvu kwa niaba
yangu.
------------------------------
*Page 26* 26
*Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
aliojaliwa na Mungu*
*Sura7: Shughuli za mawakala wa shetani*
« *Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya
damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu *
*wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya
katika ulimwengu wa roho. Kwa
sababu hiyo twaeni silaha zote za *
*Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya
uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.»*
*Waefeso. 6: 11-12*
Kitabu hiki hakitakuwa kamili kama mbinu
mbalimbali za uendeshaji wa
mamlaka hizi hazitawekwa wazi. Pia
ni muhimu kwamba aina mbalimbali ya namna na jinsi zinavyojitokeza ziwekwe
wazi.
Jambo moja li wazi nalo ni kwamba ni shetani
atakuchochea uamini kwamba
yeye ni hadithi tu za kufikirika au
mawazo ya uovu ambayo ni rahisi, au atakufanya uone zaidi sana kwa habari
ya nguvu zake na mamlaka ya
Mungu iwepo chini. Biblia inasema: " *Kwa
maana kushindana kwetu sisi si
juu ya damu na nyama; bali ni juu*
*ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo
wabaya katika ulimwengu wa roho.*
Biblia inasema kwamba silaha za Wakristo
dhidi ya shetani na mawakala wake
" *si za mwili, bali zina uwezo*
*katika Mungu hata kuangusha ngome, tukiangusha mawazo na kila kitu
kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya*
*Mungu , na tukiteka nyara kila fikira ipate
kumtii Kristo" *(*2 Wakorintho
10: 4-5). *Tena maandiko yanasema:
wazi *" Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi za
Ibilisi" (1 Yohana 3: 8). *Yesu baada
ya kuzivua enzi na mamlaka, alifanya onyesho
la waziwazi, alishinda dhidi
yao .
*"Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa
chako," (Mithali 6:2)*.
Hivyo mtoto wa Mungu ni lazima kuwa makini
kukiri neno la Mungu, ambalo
Mungu ameahidi ataharakisha
kulifanya. Kuna ukiri mara tatu umesemwa katika neno la Mungu
1. Ungamo la Uongozi wa Kristo.
2. Ungamo la imani katika Neno, katika Kristo
na katika Mungu Baba.
3. Kukiri dhambi.
Tunaposikia neno "kukiri ," sisi kwa urahisi tunafikiria kwa habari ya
dhambi. Kamusi inafafanua kukiri ni :
1. Kuanzisha kile kitu tunaamini.
2. Kushuhudia kwa kitu ambacho tunakijua.
3. Kushuhudia ukweli ambao tumeridhia .
Kwa hiyo inapaswa kusikitikiwa kuwa tunapotumia neno kukiri (confession)
kwenye fikra zetu tunafikiria
dhambi. Mwandishi yuko hapa kukutia moyo
mtoto wa Mungu kuanza leo kukiri
kile Mungu amesema. hata
wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na
Kristo; yaani, tumeokolewa kwa
neema na akatufanya tukae katika mbingu
(juu sana zaidi ya enzi na mamlaka)
katika Yesu kristo. Kwa hiyo
Wakristo wanapaswa kutambua ambapo wamekaa. Wanapaswa kujua kwamba
wanatembea katika urefu huo, juu
ya Shetani na mawakala wake. Bwana Yesu
Kristo amewapa ninyi nguvu zote na
mamlaka ili kwa hizo tupate
kuwa washirika wa uzima na utauwa (2 Petro 1 : 3).
Mungu hakuwa na kusudi la kwamba
mazingira yawatawale watoto wake, badala
yake neno la Mungu katika
kinywa cha Mkristo ni lazima kidhibiti hali/
mazingira yake. Mungu alisema katikaYer. 23:29 akisema: "Je*, si*
*neno langu kama moto? asema Bwana, na
kama nyundo ivunjayo mawe vipande
vipande?" *Wakristo,
Namaanisha waliozaliwa mara ya pili,
wanapaswa kutambua kuwa wakati jina la Yesu linatamkwa, kile
kinachotoka nje ya vinywa vyao ni moto.
Mkristo anaposimama juu ya mamlaka
aliyopewa na Kristo na anatoa
amri kwa jina la Yesu, moto hutoka katika
kinywa chake na pepo lolote kudhibiti hali husika ni lazima kutii. Yesu
yu hai leo ili kuangalia kwamba kila neno lake
linakuja kupita. Tena,
nataka kuonyesha ukweli muhimu kuwa
------------------------------
*Page 27* 27
*Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema
aliojaliwa na Mungu*
Wakristo wengi wanatazama kijuu juu , na hiki
ndicho ambacho Shetani
anatumia. Yesu, baada ya Peter kumsema kwake kwa habari ya ule mtini uliokauka baada
ya kulaaniwa na Bwana ,
alisema:
(Matthew's account) *"Amin, nawaambia
UNABII WA KWELI
Home
MAFUNDISHO YA INJILI YA KWELI
UNABII WA KWELI
KUKOMBOLEWA KUTOKA KWENYE NGUVU ZA GIZA na Emmanuel ENI SEHEMU YA TATU (PART 3)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni