Umeandikwa na Dkt. Augostino Maquengo* *Ulipokewa na Dkt. Augostino Maquengo
mnamo tarehe 16/5/11:* www.DivineRevelations.info/SWAHILI <http://www.divinerevelations.info/SWAHILI > Bwana alinitembelea asubuhi mara tu nilipofika
ofisini. Niliuhisi uwepo
Wake kisha mkono
ukanijia juu ya mabega yangu.Nami nilihisi
moto juu yangu na nikaisikia
sauti ya Bwana ikiniongelesha akisema: " yaandike chini na
uwaambie."
Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenyezi
Mungu
kwa wachungaji, wainjilisti, makasisi na
watumishi wengine: " ghadhabu yangu itawamaliza" Nanyi hamtanyakuliwa,
kwani mmeziacha
njia zangu na kuwafanya kondoo wangu mali
yenu binafsi na chanzo cha
utajiri wenu ,Kwa hiyo
Bwana hatawanyakua wachungaji hawa,wanjilisti na watumishi wangu waliopenda
ufanisi badala
ya ujumbe wa kutubu,kubadilika, kuja kwangu
ambako kuko karibu na mada ya
kunyakuliwa.
Kanisa wanalolisema kuwa langu, limekuwa ukumbi wa kujitumbuiza likiongozwa
na
wachungaji,makasisi na mashemasi wa
kanisa. Wala na kunywa na kusherehekea
nyumbani
mwangu na mbele yangu pasina kuogopa,kutetemeka au kuniheshimu. Oh,
Utukufu
Wangu
umeondoka mahekaluni mwao na uwepo
Wangu uliondoka kitambo kutoka
makanisani mwao. Wao hawatanyakuliwa wasiponililia mimi
Mungu wao kwa uchungu katika toba.
Watumishi wangu wamepotoshwa na
ulimwengu nao sasa wanafanya mipango ya
kuingiza njia za
kiulimwengu makanisani. Wao husherehekea siku ya wapendanao kanisani na pia
husherehekea
siku ya kimataifa ya waongo kanisani ,nao
husema katika siku ya kuomboleza
,leo ni siku ya
majonzi nasi basi tuvalie mavazi meusi. Wote wamepotoshwa.
Wachungaji,wainjilisti na makasisi wametabiri
nyakati za utele,nyakati za
kukombolewa na
kufanikiwa ilhali panakuja humu ulimwenguni
misiba na mateso makubwa, na kuharibiwa kwa
ulimwengu. Watumishi wangu hawanisikii
kamwe.
Wamejipotosha na ulimwengu na hata
wameziacha njia zangu.
Wao hawanitafuti katika maombi ,kufunga na kulitafkari neno langu. Wao
hufunga na kuomba ili
kuniomba vipawa vya kuponya,miujiza na
kutabiri kwa manufaa yao wenyewe. Na
hata wao
husema: Nitatayarisha ujumbe wa kuhubiri. Nitatayarisha mkutano. Mimi nina
shughuli nyingi ya
kuwapa ushauri nasaha waumini.lazima
niwatunze waumini, nao hawana wakati
kwa ajili yangu
Mimi, ambaye ndiye mmiliki wa kondoo hawa. Hawa wachungaji hawatanyakuliwa
asema Bwana
wa majeshi. Ikiwa hamniogopi mimi, basi
zirarueni nguo zenu,nyoyo zenu na
hata akili zenu kwa
machozi na kutubu. Nataka toba la kitaifa la kanisa ,maombolezo na kilio.
Mjivishe mavazi ya
vumbi na mlie kwa toba la sivyo nyinyi
hamtakuja kwangu mbinguni.
------------------------------
*Page 2* 2
Kondoo wangu wanakula chakula kilicho
oza,kilichorogwa kutokana na jumbe za
watumishi
Wangu na hawa wachungaji.
Wanaekeza kwa ajili ya siku za usoni kwa miradi ya ujenzi kanisani nao
hawafahamu kwamba hii
miradi yote itakatizwa na maangamizo na
majangwa ya ghafla. Baada ya
kuliokoa kanisa langu
kutoka humu ulimwenguni,hii miradi yote ya ujenzi itageuzwa kuwa bure. Ni
viwekezo ambavyo
havita zaa chochote.
Badala yake yafaa muwekeze katika kuhubiri
neno la uhai lisilo bandia.
Hubirini badala yake Kufanikiwa kwa nafsi na roho kupitia kwa toba
na uzima wa milele. Bwana
asema hivi, nalipenda
sana kanisa langu,ambalo hunitafuta kila siku
na huliogopa jina langu
takatifu!! Wakati umekwisha. Wakati umefika tamati.
Saa yaja sasa hivi,
nitakapolinyakua kanisa langu.
Mara tu baada ya tukio hili, Majanga, misiba,
na mateso ya kutisha ambayo
haijawahi kuwa humu duniani itaangamiza maisha mengi.
Wakati adui yangu atachukua hatamu,
hapatkuwa na
toba tena,wala wakati wa kunitafuta ,kwani
Mimi sitayajibu maombi yoyote,
neema itakuwa imeondolewa na Roho wangu Mtakatifu
hatakuwa ulimwenguni. Adui atachukua
hatamu nanyi
mtasaga meno yenu na kupiga mayowe
mioyoni mwenu kwa mateso na kuvunjika.
Zivunjeni nyoyo zenu sasa na mzifanye zimwage damu
ya toba,zipasuenii nyoyo zenu kwa
toba katika
sekunde za mwisho za wakati uliosalia, la
sivyo ghadhabu ya kutisha iwapate.
Lakini watu hawa wana roho ya kuasi, nao wameasi na kwenda zao. Hakuna
asemaye moyoni
mwake, wacheni sasa tumuogope Bwana
Mungu wetu apeanaye mvua ya sasa na
hata ya awali
katika wakati wake.Ametuhifadhi kwa ajili ya wakati teule wa mavuno. Uovu
wenu umeyageuza
mambo haya, na dhambi zenu zimezuia
mambo mazuri kuja kwenu.
Kwani miongoni mwa watu wangu
panapatikana watu waovu, wananyemelea kama
afanyavyo
yule amtegae nyoka,wameweka mitego na
wamewanasa watu. Kama vile kizimba
kilivyojaa
ndege basi ndivyo nyumba zao zimejaa udanganyifu, kwa hivyo wao wamekuwa
wakubwa na
tajiri sana.
Wao wamekuwa wanono, wanang'ara, naam,
wamezidi matendo ya waovu, wao
hawahukumu vyema mambo ya wakiwa lakini bado
wanafanikiwa; na haki za wanyonge
hawazihukumu au
kuzitilia maanani. (Jeremiah 5:24-28)
Nyinyi hamtanyakuliwa asema Bwana,
isopkuwa mbadilishe mienendo yenu na kutubu.
Mimi sitawanyakua wale waliooana na
televisheni, sinema na burudani ambazo
zimechukua
muda wenu mwingi nanyi hamna wakati
kwangu miye Mungu na neno langu. Mimi sitawanyakua wakristu waendao kanisani
jumapili pekee ili kutuliza
ghadhabu yangu juu
ya maisha yao ,nao wanadhani kwamba Mimi
Mungu sioni wala kuyafahamu yale
wafanyao. Jumapili, wao huenda tu kanisani kujionyesha
nguo zao nzuri na kupiga gumzo
na marafiki wao.
Nyumba yangu imekua mtandao wa kijamii .
Mimi Yesu Kristo, Bwana wenu sitawanyakua
wale wanaoutumia muda wao mwingi kuitazama
televisheni au katika kuvisoma vitabu vya
riwaya na mambo mengine.Kwa
sababu wamezigeuza
riwaya hizi pamoja na mafunzo ya kisayansi
kuwa washauri wao, badala ya kuwa na Roho
Mtakatifu kama rafiki wao wa kweli tena bora.
Muumini yeyote aliyesahau kumtafuta Roho
Wangu Mtakatifu na amezifanya
televisheni na itikadi
zingine za kipepo kuwa marafiki wake wa dhati badala ya neno Langu ata
achwa nyuma
kukumbana na mpinga Kristu na alama ya
mnyama muovu.
------------------------------
*Page 3* 3
Mapepo yamefaulu kujiipenyeza ndani na
katikati ya kanisa na kanisa leo
limegeuzwa
kuwa na tabia na itikadi za kipepo, badala ya
kuwa na neno Langu na tabia zangu Mimi Bwana
Yesu.
Kanisa kama hili lita achwa nyuma.
Wale waishio maisha yao wakiitangaza miili
yao kwa kuvaa miundo ya nguo
iliyo chafu na isiyokuwa ya heshima, wakiiweka wazi na
kuionyesha matiti yao na kuifunua
miili yao;huu bila
shaka ni mfumo wa kidunia. Wakrsitu hawa
wananiambia Mimi Mungu wao, Mungu
, tayari nimekupa moyo wangu na hiyo imetosha.
Kuhusu sehemu yangu ya nje, niache
niitunze kwa
kuvaa nipendavyo.
Wacha ijulikane kweli kwamba tayari ni
mekwisha waacha muishi na kuufurahia ulimwengu.
Kwani hamfahamu kuwa Mimi ni Mungu aliye
na wivu? Mimi nina wivi kwa ajili
yenu lakini nyinyi
mnanishiriki na ulimwengu, kamwe sitokubali
hivyo. Muumini yeyote ambaye amenigeuza kitu cha
kuchezea asemaye moyoni mwake;
Mungu sio
mbaya hadi hawezi elewa kwamba tunaishi
katika karne ya ishirini na moja na
kwamba sisi huishi jinsi tuishivyo.
Wakati wa Nuhu uovu ulikuwa mchache kuliko
sasa, wakati wa luti hapakuwa na
uovu kama leo,
kwa hiyo tubuni la sivyo hamtakuwa na
udhuru. Mimi sitawachukua wale wanunuao,kuuza na
kucheza michezo siku yangu
takatifu ya kuabudu ya
jumapili au jumamosi.
Siku yoyote ile viongozi wenu wameweka kwa
ajili ya kuniabudu Mimi ni sharti iwe Yangu pekee,
Mimi ndiye Bwana.
Siku hii lazima itakaswe kwangu pekee. Watu
hawaniheshimu Mimi Bwana na
Mungu wao.
Wao huniambia na kubishana na watumishi wangu wa kweli wakisema hii ni
sheria nasi tu katika
wakati wa neema.Kwani Bwana wenu hawezi
kuheshimiwa na kuogopwa?
Kwani neema yamaanisha kumkosea heshima
Mungu wenu? Nyinyi hubishana nami hata
maombini namna vile mtabishana muunapo
ujumbe huu.
Mimi sitawachukua waongo,wenye kiburi,
waumini wabatili ambao marafiki wao
wakuu ni watu wa kawaida nao hujipotosha wenyewe na
ulimwengu. Mimi Bwana na Mungu wenu
nimewaamuru
katika neno langu jitengeni kutoka miongoni
mwao nanyi msijihusishe na
kongwa zisizo sawa. Mimi sitawachukua wale waongezao maneno
yao ndani ya ukweli , wale
wawasengenyao
watumishi wangu na wachungaji ambao
hunitumikia kwa kweli na kulibeba neno
langu. Ole wake Yule aongezae na kuondoa kutoka kwa neno
langu la unabii !
Huu ndio msimamo wangu, kubalini au kataeni
asema Bwana.
Mimi Yesu mesia, Mungu wenu na hapana
mwingine. Jitayarishe ,jitayarishe Mimi naja upesi!
UNABII WA KWELI
Home
MAFUNDISHO YA INJILI YA KWELI
UNABII WA KWELI
UJUMBE KUTOKA KWA BWANA YESU KWAAJILI YA MATAIFA YOTE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni