Nafasi ya Pili
Ufufuo wa Theo Nez
www.DivineRevelations.info/Swahili
Theo Nez alikulia katika taifa wa Wanavajo karibu na pembe 4 za USA.
Bado anaishi katika eneo hilo. Mwaka 1995 alinunua kitabu cha Mary
Baxter âUfunuo wa kuhusu Kuzimuâ akifikiri ataishi tena miaka 30 ijayo
hivyo angeweza kuwa na muda mzuri kurekebisha na Mungu. Akakiweka
kandolakini, miezi sita baadae alipokuwa akifanya Meth nyumbani kwake
alikufa kwa sababu ya kutumia nyingi (over dose). Yesu Kristo mwenyewe akamchukua Theo
kwa mkono wake na akampeleka katika shimo lake la Kuzimu. Kwa masaa mawili alimsihi Yesu
asimpeleke paleâ¦.. Lakini Yesu hakuweza kubadili kitu. Mpaka pale aliposikia mke wake,
muamini, akimuombeaâ¦.Yesu akamueleza kuwa atakwenda kujibu maombi yake kwa sababu
alisimama katika neon na hakurudi nyuma⦠Yesu akampeleka Mbinguni na kwa masaa mawili
alimuonyesha mambo yajayo na akamuamuru awaambie wengine kwamba tunaishi katika
nyakati za mwisho naya kwamba Bwana amekaribia kurudi. Ujumbe wake ni kuwa hatuwezi
kuwatumikia mabwana wawili.
Hello Kaka na dada zangu wapendwa. Jina langu ni Theo nez na ninnaishi Farmington New
Mexico. Leo ningependa kushiriki nanyi ushuhuda wangu, Jinsi Mungu alivyofanya kitu cha
ajabu sana, Kwangu mimi na kwa familia yangu. Alileta Wokovu wake katika nyumba yetu.
Mwaka 1995, Nilikuwa ni mtu wa asili. Nilikunywa na kutumia madawa, sikujali kitu
chochote.Siku moja, Nilitumia zaidi kupindukia kwa haraka na moyo wangu ukasimama. Nikafa
kwa masaa. Kile nachotaka kuwaeleza, kitawafanya mfikiri mara mbili kwa habari ya maisha na
kifo. Moyo wangu uliposimama, kelele za ulimwengu zikatoweka kabisa na giza kuu likaja
kwangu. Nikaona mapepo matatu yakitoka kwenye moyo wangu, yakienda nje ya dirisha huku
yakicheka. Nilipotoka kwenye Mwili wangu, Niligeuka nyuma nikamuona Yesu alikuwa
amesimama nyuma yangu. Nywele zake zilikuwa ni dhahabu yenye weupe; Alikuwa amevalia
vazi jeupe lenye mshipi wa dhahabu. Viatu vyake vilikuwa ni sandosi za dhahabu, na alisogea na
akaongea kwa sauti ya upole.Viatu sandosi za dhahabu. Viatu vyake vilikuwa ni sandosi za
dhahabu, na alisogea na akaongea kwa sauti tulivu. Kulikuwa na mwanga uliomzunguka na
Roho yangu ikawa imekwisha mtambua. Nilitembea mpaka kwake na kumuuliza; Yesu ulikuwa
wapi, nilikuwa nikikutafuta. na akaongea kwa upole na kusema; sikuwahi kukuacha, nimekuwa
pembeni yako siku zote. Nilikuwa nikisubiri wewe utubu na kufanya kusudi la Baba.
Unafahamu, nilikuwa nimeitwa kuhubiri miaka michache iliyopita. Nikasema, Nitakwenda,lakini
nilikimbia. Nikasema siwezi kufanya, Bado ni kijana sana. Mungu anapokuita na kuingilia
maisha yako huna uchaguzi mwingine lakini inakupasa useme ndiyo Bwana. Kisha
nikamwambia Yesu, nilifikiri ningeishi miaka mingine thelathini. Njoo, imekupasa kuona mengi.
Alinishika mkono wangu na tukaanza kutembea kuelekea chini kwenye njia. Ilikuwa ni giza na
Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu
Yesu mwenyewe ndiye alikuwa mwanga. Mara nikaanza kuona pepo wametuzunguka.
Walikuwa wakijaribu kunirarua, lakini nikamshikilia Yesu mkononi kama mtoto mdogo.
Alikuwa ni kinga yangu na akaanza kuongea nami. Akasema, unajua Baba anahasira nawe. Ni
kwa sababu nilikuwa na cheza na kanisa na kukimbia kama Yona. Biblia inasema Yona aliitwa
kuhubiri lakini alimkimbia Mungu. Nimefanya hivi kwa muda wa miaka mingi. Sasa imenishika
mimi pia. Nilifahamu kuwa nilikuwa nimekufa katika dhambi zangu, na nilikuwa nimekwisha
chelewa. Tulipoendelea mbele, Yesu akaongea mambo mengi na nikamuuliza maswali mengi.
Tukasima mahali fulani na yesu akaniambia, angalia mbele. Niliweza kuona aina fulani ya
mwanga kwa mbali. Yesu akaniuliza; Unafikiri hiyo ni nini? Nikasema, Bwana hiyo inaonekana
kama kuzimu, Labda ni miali ya moto wa kuzimu. Hakika, tuliposogelea karibu, tukafika juu ya
bonde. Bonde lilikuwa kama maili mbili kwa kina na maili tatu kwa upana
Chini niliweza kuona miali ya moto, kila kitu kilikuwa ni orenji nyekundu, Nikaanza
kutetemeka, Nikaanza kuogopa. Nilifahamu kuwa nitawenda kuishia mahali pale.Yesu
akaniambia niangalie chini. Sikuweza hata kuangalia chini, nilianza kulia huku nikimkimbilia
Yesu nyuma. Nikaanza kutubu, na kuliakwa Bwana ili anisamehe. Nitahubiri sasa, nipe nafasi
moja ya mwisho. Nililia kama mtoto mdogo.
Tuliendelea mpaka tukafika chini kabisa kwenye shimo la kuzimu. Nilona vitu vingi ambavyo
maneno hayawezi kusimulia. Sehemu ile ilijaa roho za watu, na mapepo yalikuwa kila eneo.
Biblia inasema Isaya 5:14 Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake
bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao,
hushuka na kuingia humo.
Kulikuwa na Roho za watu zikiwaka katika miali ya moto. Vilio na
kelele zilikuwa kila sehemu. Hakukuwa na tumaini, hakukuwa na
tumaini kwa roho zilizopotea. Kwa nini ? Kwa sababu walimkataa
Yesu. Wengine walisubiri muda mrefu. Wengi walifanya mdhaa na
wakamkimbia Mungu. Kumkimbia Mungu kutakufanya uingie
Kuzimu. Ukishaingia mule huwezi kutoka. Tafadhali, ningependa
uinue mikono yako na kumwambia Bwana; Usiruhusu hili kutokea
kwangu. Tulipoendelea kutembea, Niliona mamia ya elfu ya mashimo.
Nilikuwa nikilia na kuomboleza tulipokuja kwenye shimo moja
ambalo ni tupu. lilikuwa na moto uliokuwa ukitoka ndani yake. Yesu
akaniambia; Hili ndilo shimo ambalo shetani amekuchimbia. Kisha nikaanza kupiga mayowe,
nikilia, Bwana sitaki kwenda pale. Nililia na kutubu, NikimuombaYesu anipe nafasi moja
nyingine
tena.
Nililia
kama
Yona
alipokuwa
kwenye
tumbo
la
Kuzimu.
Katika Kitabu cha Luka 16, tunasoma kwa habari ya Lazaro na Tajiri mmoja. Tajiri alikuwa na
kila kitu. 20 Kulikuwa pia na maskini mmoja jina lake Lazaro, aliyekuwa amejaa vidonda na
alikuwa analazwa mlangoni pa nyumba ya huyo tajiri. 21 Lazaro alitamani kula makombo
yaliyoanguka kutoka meza ya tajiri; na zaidi ya hayo, mbwa walikuwa wanakuja na kulamba
vidonda vyake! 22 Ikatokea kwamba huyo maskini akafa, malaika wakamchukua, wakamweka
Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu
karibu na Abrahamu. Na yule tajiri pia akafa, akazikwa. 23 Huyo tajiri, alikuwa na mateso
makali huko kuzimu, akainua macho yake, akamwona Abrahamu kwa mbali na Lazaro karibu
naye. 24 Basi, akaita kwa sauti: Baba Abrahamu, nionee huruma; umtume Lazaro angalau
achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe ulimi wangu, maana ninateseka mno
katika moto huu. 25 Lakini Abrahamu akamjibu: Kumbuka mwanangu, kwamba ulipokea mema
yako katika maisha, naye Lazaro akapokea mabaya. Sasa lakini, yeye anatulizwa, nawe
unateswa. 26 Licha ya hayo, kati yetu na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wanaotaka kuja
kwenu kutoka huku wasiweze, wala wanaotaka kutoka kwenu kuja kwetu wasiweze. 27 Huyo
aliyekuwa tajiri akasema: Basi baba, nakuomba umtume aende nyumbani kwa baba yangu,
28
maana ninao ndugu watano, ili awaonye wasije wakaja huku kwenye mateso. 29 Lakini
Abrahamu akamwambia: Ndugu zako wanao Mose na manabii; waache wawasikilize hao.
Lakini yeye akasema: Sivyo baba Abrahamu, ila kama mtu atafufuka kutoka wafu na
30
kuwaendea, watatubu. 31 Naye Abrahamu akasema: Kama hawawasikilizi Mose na manabii,
hawatajali hata kama mtu angefufuka kutoka wafu."
Oh Watu , tafadhali mnisikilize,hii ni halisi,weka mambo yako sawa na Mungu vile uwezavyo
.Tulipotoka nje, tulisimama katika eneo lenye ukiwa. Yesu akasema;sikia. Na nikaanza kusikia
mwanamke akisali niliweza kusikia sauti yake vizuri wakati akiomba alisema; Bwana mrudishe
tena! Mpe tena nafasi nyingine. Bwana ana watoto wawili wa kiume wa kuwalea. Yeye ndiye
pekee niliyenaye. Usimchukue Bwana!
Unaamini maombi ya imani yanaweza kuamisha chochote? Biblia inasema, chochote
mnachohitaji mkiomba , amini umekwisha pokea,na hakika mtapokea. Mwanamke huyu
akaendelea kuomba. Yesu akaniuliza, Unafikiri huyo ni nani? Nikamwambia huyo ni mke
wangu. Bwana akasema, unasikia hicho,nina watoto wawili wa kuwalea. Nikaanza kumshika
Bwana kwenye mabega, siwezi kufa sasa, familia yangubado inanihitaji. Nikaanza kutoa sababu
mbalimbali, lakini hakukuwa na jibu. Nikaanza kulia tena.
Mke wangu aliendelea kuomba. Kulikuwa na kipindi cha kusubiri ambacho kilikuwa kama
masaa na mwisho Mungu Baba akajibu hili, Akaongea na sauti yake ilikuwa kama Maji mengi.
Akasema Mwanangu; nakwenda kukupa tena nafasi nyingine kwa sababu ya maombi na imani
ya mke wako,nitakuhifadhi. Nikikurudisha, nitakwenda kukutumia.
Hapo nikaanza kusema kwa viapo,Bwana nitahubiri. Nitafanya chochote, Nitawaeleza watu
kuhusu sehemu hii, Nikasema Bwana ,Nitakusaidia kuokoa roho .
Kisha tukatembea kuelekea kwenye chumba chenye kioo kikubwa kama Televisheni.
Nilionyeshwa wakati wangu uliopita,wa sasa na utakaokuja. Nikaweza kuona ,maisha yangu
kuanzia mtoto mpaka nilipokuwa mkubwa. Yesu alinipa ufunuo, maono. Alinionyesha mambo
mengi sana ambayo ni lazima yatokee. Akasema, kweli tunaishi katika nyakati za mwisho.
Nenda na uwaeleze watu. waambie watembee katika njia sahihi na watubu. Waeleze waache
kucheza na mimi na waanze kushika amri zangu.
Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu
Akanionyesha jinsi watu wanavyojificha nyuma ya Biblia, wanayaficha matendo yao,na
wanaishi katika dhambi. Mungu anasikia na kuona kila kitu. Akasema watu hawa
wanamuheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nae. Oh jinsi wanavyopenda
kufundisha amri kwa watu, lakini wanaziacha amri za Mungu.
Akasema , usogope,Mimi ni alpha na omega, wa kwanza na wa mwisho, Unachokisikia ni haki.
Akasema; yeye aliye na sikio, na sikie kile Roho anasema kwa kanisa. Akanipa mistari mitatu,Ta
hadhari. Wa kwanza ni Kumbukumbu la torati 6:15. (15 kwani Bwana, Mungu wako, aliye
katikati yako ni Mungu mwenye wivu;) isije ikawaka juu yako hasira ya Bwana, Mungu wako,
akakuangamiza kutoka juu ya uso wa nchi.
Mstari wa pili katika Luka 16:13. Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili;
kwa maana atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au ataambatana na mmoja na
kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
Msitari wa tatu katika kitabu cha Ufunuo 3:3 Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi
ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua
saa nitakayokuja kwako.
Kaka na dada, Hatujui ni siku gani tutaonndoka katika ulimwengu huu, hatujui kesho imebeba
nini ,kwa hivyo ninaomba kwamba uweke mambo yako sawa na Mungu wakati bado unaweza.
Baada ya hili Yesu akanichukua mpaka mbinguni
na tukatembea katika malango haya ya dhahabu
katika mtaa wa dhahabu. Nikaona watu wengi wa
kila taifa na walikuwa wamesimama mbele ya kiti
kile cha enzi, wamevalia mavazi meupe, Baadhi
yao ni watu niliowafahamu, wachungaji na
manabii wa kwenye biblia. kila kitu kilikuwa ni
kizuri,kila
mtu
alikuwa
ni
mwenye
furaha;ungeweza kuona upendo wao kwenye sura
zao. Nilianza kuhisi furaha na amani.Nilipokuwa
nikitembeatembea, sikutaka tena kurudi. Yesu
akanifunulia saa kubwa. Mkono wa saa ulikuwa
umekaribia kufikia kamili kwenye 12,wakati
unakimbia
haraka,wakati
wa
kwenda
sasa.
Nikasema Bwana, sitapenda kwenda, nataka
nibaki.
Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu
Lakini ilinipasa kurudi. Tulipokuwa tukirudi niliona dunia kama kampira kadogo kama ule wa
golf. Alinileta tena kwenye chumba changumwili wangu ulipokuwa umelala. Alisogelea mahali
ambapo moyo wangu ulikuwepo. Nyama iliyozungukza moyo wanguilifunguka. Yesu
akachukua moyo wangu wa kale nje, na akautupa katika ziwa la moto, Kisha akanipa moyo
mpya, na mwanga ukaja juu yake. Nilisimama pale nikiagalia na kutafakari,wow; hata ngozi na
mifupa inasikia Yesu.
Baadae nilitafuta katika biblia yangu na nikakuta Ezekieil sura 36 :26-27, Nililia kama mtoto
mdogo kwa sababu ilikuwa imeandikwa, Pale Biblia inasema hivi: 26 Nami nitawapa ninyi
moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya
mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. 27 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na
kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.
Baada ya Yesu kurejesha roho yangu kwenye mwili wangu, lakini moyo wangu mpya haukuwa
unafanya kazi bado.Nilimuona mke wangu ameshika mikono yangu anaomba. Muda nikaona
chumba changu kimezungukwa na maelfu ya malaika, walikuwa wakisifu na kuimba kwa
nyimbo nzuri ambazo sikuwahi kuzisikia. Muziki tu wenyewe ulikuwa ni waajabu sana,Malaika
mmoja akatokeza kwa nje na akatamka, akisema; Damu ya Yesu inakuja. Na malaika wote
wakaanza kusifu na kuabudu. Kisha Damu ya Yesu ikaja tulipo,na kunisafisha mimi kuanzia
kichwani mpaka kwenye vidole vyangu vya miguu ikasafisha dhambi zangu zote. Pombe na
madawa vikatoka nje ya mwili. Nikahisi kama maji ya moto. Nilipojiangalia, ule weusi wote wa
mwili wangu ukaondoka. Nilikuwa mweupe na msafi.
Baadae malaika Yule Yule akatoka nje tena na akasema; Roho Mtakatifu anakuja.Malaika
wakaanza kuimba na kuabudu tena. Holy spirit akaja kwetu tulipo na kutujaza. Roho yangu
ikaanza kuruka tena juu na chini. Kisha nikampata Roho Mtakatifu. Roho ya Bwana ilikuwa na
moto kama umeme; ilikuwa kama moto unaowaka kwenye mifupa yangu.
Malaika walikuwa bado wakiimba na kusifu Yesu aliposema; Mwanangu, nenda kawaambie
watu nilicho kushuhudia wewe. Akaugusa moyo wangu mpya kwa vidole vyake na ukaanza
kufanya kazi. Ndipo kidogo kidogo macho yangu yakaanza kufunguka. Nikagundua mwili
wangu umekuwa wa baridi, ilikuwa ni vigumu kidogo kuongea. Nikamuuliza mke wangu
kilichotokea. Akaniangalia na kuniambia; Uko sawa? Kisha akaanza kulia.
Kulikuwa bado kuna maumivu kwenye kifua changu chote, nikaona kama ninaopresheni.
Nilikuwa mdhaifu na kiu; Kitu cha kwanza kuuliza ilikuwa ni maji. Kisha fahamu zangu
Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu
zikaanza kunirudia na nikakumbuka kilichonitokea. Kisha nikaanguka kwa Magoti na kuomba
kwa muda wa masaa matatu mpaka jua likachomoka.
Kutoka siku hiyo maisha yangu yamekuwa tofauti. Nilikuwa muasi, Lakini Mungu akanishusha
kwa magoti , nikaanza kulia kama mtoto mdogo, nikiomba rehema. Nilikuwa nikifikiri, nikienda
kuzimu, haitajalisha. Lakini sikuwa najua ni kiasi gani kuzimu ni chungu mpaka pale Bwana
aliponifunulia. Sasa namshukuru Bwana kila siku kwa maisha ambayo amenirejeshea, familia, na
huduma aliyonipa.
Kaka na dada ,Ninaomba kwamba msichezee kanisa na kuwa na mabwana wawili, Kwa sababu
huwezi ukacheza na Mungu. Ni kitu cha kutisha kama nini kuangukia katika mikono ya Mungu
aliyehai. Hivyo usidanganyike,Mungu hadhiakiwi. Biblia inasema;Apandacho mtu, ndicho
atakachovuna, Yeye apandaye uovu, atavuna huo. Ndiyo Mungu ni Mungu wa upendo; amejaa
huruma na rehema. ni Mungu wa nafasi ya pili, lakini ni Mungu wa hukumu .Biblia inasema
Yeye ni moto ulao.hivyo imetupasa tujiandae, kwa sababu hujui ni lini utakwenda kufa, Bilblia
inasema katika waebrania 9:27, kama inavyoamriwa kwa wanadamu kufa mara moja, lakini
baada ya hili ni Hukumu.
Siku inakuja ambayo sote tutasimama mbele zake Mungu, na vitabu vyetu vitafunguliwa. Utakw
enda kuwa pale. Kila Mtu ambaye anasikiliza ushuhuda huu atakwenda kuwa pale. Hiyo itakuwa
ni mwito ambao huwezi kukosa. Hii inaweza kuwa ni mwito wako wa mwisho, usiasi mbele zak
e Mungu. Tafakari kwa makini kuhusu hili, Itaenda kuwa peponi au kuzimu. Unaweza usipate na
fasi nyingine kama mimi; Ni kwa neema ya Mungu tu.
Niko hapa leo ilikushiriki nanyi ushuhuda huu, ningependa unyanyue mikono yako na uongee na
Bwana, Mshukuru Yeye kwa kuwatahadharisha, Mshukuru Yeye kwa maisha haya ya thamani.
Kama ungependa kuokoka, unahitaji sala hii, Ngoja niombe sala hii pamoja nawe hivi sasa.
Bwana Yesu ,nisamehe. Ninakupokea wewe kama Bwana Mwokozi wangu. Njoo moyoni mwan
gu na maishani mwangu. Nipe Uzima wa milele, ili niweze kuishi nawe milele. Nipe maisha ya a
mani na furaha. Aksante Bwana. Katika Jina la Yesu, Amen.
Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu
Kama ukipenda kuniandikia anuani yangu ni:
Last living days Ministries
P.O. Box 3701
Farmington, NM 87499
USA
Unachokisikia kwenye ushuhuda huu ni simulizi ya kweli. Mimi ni
Mtu wa India Mnavajo.Ninaishi Four Corners. Nina rasimisha kan
da hii kwa Wamarekani wenyeji wote Marekani nzima.
Ninatoa Ruhusa kunakili ushuhuda huu.
Ndugu aliyefasiri ufunuo huu ni Peter Kahale ni kijana aliyeokoka na anampenda Yesu na
mwenye shauku ya kuhubiri injili ya Yesu Kristo.
Simu ya Mkononi: +255-769-610460, +255-653-610460.
Barua Pepe: kahalepeter@gmail.com
Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni