Imefasiriwa na Alpha Wilson Magubila kwa Neema
aliojaliwa na Mungu
Kwa kipindi cha masaa 23,
binti mdogo wa ki-Ecuado
aitwaye Angelica alioneshwa
falme za Mbinguni na Kuzimu, na kurudi
kwa Kristo mara ya pili.
Alishuhudia Yesu akilia kwa
huzuni
aonapo umati wa roho
zilizopotea milele, ulimwengu uliomkataa yeye, kanisa lisilo
tayari kabisa
kwa ujio wake, watu
wameacha kushuhudia kwa
walipotea mbali na kweli, na
anasa za dunia zimeteka hata watoto kwa
shetani. Alishuhudia watu
maarufu wakiteswa katika
moto, waimbaji,
wanamuziki na hata Papa.
Angelica alioneshwa jinsi ufalme wa Mbinguni
ulivyoandaliwa kwa
uzuri na utayari, utukufu
usioweza kufikirika, ambapo
hakuna uovu. Japokuwa Yesu
anakuja kwa ajili ya watakatifu tu; wengi wa
wana wa Mungu hawatakuwa
tayari kwa siku ile, na
wataachwa
nyuma katika ulimwengu
utakaogawanyika vipande vipande.
www.DivineUfunuo.info/23
(Mahojiano
kwa video, mwanzoni ni kwa
lugha ya Kihispania, huko El
Empalme, Ecuador. Sept. 29, 2009).
Maxima (Mama yake Binti):
Jina langu ni Maxima
Zambrano Mora, tunasali
kanisa la "Casa de Oracion"
huku El Empalme. Tulikuwa katika kufunga kwa
siku 15, na kulia kwa Mungu.
Binti yangu Angelica aliungana
nasi
pia. Katika kipindi hicho cha
siku 15 cha kufunga, niliweza kupata maono zaidi ya asili,
ambayo
sijawahi kuona kabla. Tulikuwa
tunaomba na kufunga katika
kipindi maalumu cha kumtafuta
Bwana, tuliendelea kuomba na kulia pale nyumbani, tukisubiri
Mungu aseme nasi.
Bwana alitutia matumaini
makubwa sana. Kwaajili ya
majaribu yetu tulikaribia
kukata tamaa, lakini Bwana alikuwa pamoja
nasi kutusaidia. Alitupa neno
la Yeremia 33:3 "Niite, nami
nitakuitikia, ame nitakuonesha
mambo makubwa, magumu
usiyoyajua." Binti yangu alitia msisitizo sana katika neno hili
kwa Bwana, japokuwa sikujua
kwa wakati huo. Angelica (Binti Mhusika):
Jina langu ni Angelica
Elizabeth Zambrano Mora.
Nina umri wa miaka 18, na
ninasoma chuo cha
"Colegio José MarÃa Velazco Ibarra",
hapa El Cantón, El Empalme,
Ecuador. Kwanza nilimpokea
Kristo nilipokuwa na umri wa
miaka
12, lakini nalijiambia mwenyewe, "Hakuna hata
mmoja wa rakifi zangu
aliyeokoka na nikajisikia
aibu miongoni mwao", kwa
hiyo nirudi nyuma mbali na
Mungu na kuishi maisha mabaya. Lakini
Mungu alinivuta nitoke huko.
Siku ya sherehe ya kutimiza
miaka 15, nirejea tena
kupatana na Bwana, lakini nia
haikutulia sawa sawa. Biblia inasema (Yakobo
1:8), "Mtu wa nia mbili husita-
sita katika nia zake zote" na
mimi
nilikuwa sawa na mtu huyu.
Baba yangu aliwahi kusema "Hutakiwi kuwa hivyo, siyo
vizuri, ni
vibaya mwanangu" lakini
nalimjibu, "Hivi ndivyo nilivyo,
nataka kuwa hivyo, hakuna
mtu wa kuniambia namna nitakiwavyo
kuwa, wala chakufanya, wala
namna ya kuvaa, au
mwenendo."
Naye alijibu, "Mungu
atakushughulikia na atakubadilisha wewe."
Siku ya sherehe ya kutimiza
miaka 17, nilimkaribia Bwana.
Tarehe 28 mwezi Aprili
nilimwendea
Bwana na kumwambia, "Bwana, nijisikia vibaya sana,
najua kuwa mimi ni mwenye
dhambi" na
nilimweleza jinsi ninavyojisikia.
"Bwana, nisamehe mimi.
Natamani uandike jina langu katika
kitabu cha Uzima na unipokee
niwe mwanao." Nilitubu na
kutoa maisha yangu kwa
Bwana rasmi.
Nikasema "Bwana, naomba unibadilishe, ufanye tofauti
ndani mwangu." Nililia kwa
moyo wangu
wote, huku nikimwomba
Bwana anibadilishe mimi.
Lakini kwa kadri ya muda ulivyozidi kupita,
sikuona madiliko yoyote.
Badiliko pekee nikuwa nilianza
kuhudhuria kanisani, kusoma
biblia na
kuomba. Hayo tu ndiyo mabadiliko katika maisha
yangu.
Ilipofika mwezi Agosti,
nilikaribishwa katika mfungo
wa siku 15. Niliamua kushiriki,
lakini kabla ya kuanza nilisema: "Bwana,
naomba unishughulikie hapa."
Katika kipindi chote cha
mfungo,
Bwana alikuwa anasema na
karibu kila mtu, kasoro mimi tu! Ilikuwa kama vile Bwana
hajaniona,
na hilo liliniumiza sana.
Nikaomba, "Bwana,
hutanishughulikia mimi?"
Nikaomba na kulia peke yangu na kusema tena,
"Bwana, je unanipenda? Je
upo hapa? Upo nami hapa?
Kwanini husemi
nami kama unavyosema na kila
mmoja hapa? Unasema mambo mengi kwa wenzangu,
hata maneno
ya unabii, lakini siyo kwangu"
Nilimwomba ishara ya kuwa yu
nami, na Bwana akanipa neno
la Yeremia 33:3, "Niite, nami
nitakuitikia, nami nitakuonesha
mambo makubwa, magumu
usiyoyajua." Nikasema,
"Bwana, je umesema nami?"
Kwasababu nilisikia sauti yake na kupata
maono ya maneno
yaliyoandikwa katika Yeremia
33:3.
Nikasema "Bwana, hiyo ni
kwaajili yangu?" Nilitunza na kukaa nalo kimya mwenyewe
wakati kila
mmoja akishuhudia
waliyopewa na Bwana na
kuoneshwa. Lakini mimi
nilitunza siri yangu na mara kwa mara nilijikumbusha na
kutafakari maneno: " Niite"
maana yake nimwombe, lakini
nini maana
ya: "mambo makubwa,
magumu" niliwaza, "Huenda ikamaanisha Mbinguni na
Kuzimu." Kwa hiyo nalimwambia "Bwana,
naomba unioneshe Mbinguni
tu, lakini siyo kuzimu,
kwasababu nimesikia kuzimu
ni sehemu ya kutisha na
mbaya sana." Lakini baadaye nikaomba kwa moyo wangu
wote, "Bwana kama ni
mapenzi yako kunionesha, na
iwe hivyo, lakini nibadilishe
kwanza. Naomba ufanye
tofauti ndani mwangu, nataka kuwa tofauti."
Tulipomaliza kufunga, kulikuwa
na majaribu na vipindi vigumu
na mara nyingine nalijisikia
kuishiwa nguvu, siwezi tena
kuendelea na Bwana. Lakini alinipa nguvu. Nilianza kusikia
sauti yake na kumjua vema
zaidi. Tukawa marakifi wazuri.
Bwana ni rafiki yetu mwema,
na Roho Mtakatifu pia. Niliwahi
mwambia, "Bwana, wewe ni rafiki yangu bora. Nataka
kukujua vema," na
nilishirikiana naye katika
mawazo yangu yote.
Nilimwomba kipindi chote cha
mwezi Agosti hadi Novemba, na mtumishi wa Bwana akaja
nyumbani kwetu na kusema,
"Bwana akubariki." Nikajibu,
"Ameni." Kisha akasema,
"Nimekuja kukuletea ujumbe
toka kwa Mungu…...Jiandae, kwasababu Bwana
atakuonesha mambo
makubwa, magumu
usiyoyajua. Atakuonesha
wewe Mbinguni na kuzimu
kama ulivyokuwa unamwomba neno la Yeremia 33:3."
Nikamwuliza, "Ndiyo, lakini
umepataje kujua?
Sijamweleza yeyote."
Akanijibu, "Mungu
unayemtumikia na kumsifu, ndiye nimsifuye, alinieleza kila
kitu."
Mara tukaanza kuomba.
Baadhi akina dada toka
kanisani kwetu na wana familia
wangu wakaungana nasi kuomba. Lakini mara
tulipoanza kuomba, nilianza
kuona Mbingu zikifunguka.
Mara nikasema "naona mbingu
zikifunguka, na malaika wawili
wanashuka kuja tulipo" Mtumishi wa Mungu akasema
"waulize kwanini wamekuja
hapa"
Walikuwa warefu na wazuri
wakupendeza; wana mbawa
nzuri. Walikuwa wakubwa na wenye kung'aa, na
walionekana wakiangaaza,
mng'ao kama wa dhahabu.
Walivaa sandozi za vito vya
thamani na walivaa mavazi
matakatifu. "Kwanini mko hapa?" Wakatabasamu na
kusema, "Tupo hapa
kwasababu tuna kazi
yakufanya….. tupo hapa
kwasababu unatakiwa
utembelee Mbinguni na kuzimu na hatutaondoka mpaka yote
yatakapo pita." Nikawajibu
"safi sana, lakini mimi
natamani kutembelea Mbinguni
tu, siyo kuzimu"
Wakatabasamu na kuendelea kuwepo na hawakusema lolote
zaidi. Baada ya kumaliza
maombi, niliendelea kuwaona
wakiwepo.
Pia nilianza kumwona Roho
Mtakatifu; ni rafiki yangu bora; ni Mtakatifu, amejaa pote na
yuko kila mahali wakati wote.
Ninamwona, anaangaza na
kung'aa sana, naona tabasamu
lake na mtazamo wake wa
upendo! Ni vigumu sana kumwelezea, kwa sababu ni
mzuri zaidi ya malaika. Malaika
wana uzuri wao lakini Roho
Mtakatifu ni zaidi sana kwa
yote. Naweza kuisikia sauti
yake, sauti ilijaa upendo na matulizo makuu. Siwezi
kuelezea kabisa sauti yake;
kama radi si radi wakati huo
huo yakuvutia. Yeye husema
"Niko pamoja nawe" Kwa hiyo
nalijitahidi kuendelea kutembea na Mungu, japo
majaribu yalizidi kutuzingira.
Tulikuwa tunapita kipindi
kigumu sana, lakini chenye
ushindi waajabu. Mie husema
"Bwana, mapenzi yako yatimizwe." Niliendelea
kuwaona malaika wale hata
nikiwa shule na pia darasani.
Nilikuwa mwenye furaha ajabu
kwa sababu niliwaona vema.
Mtumishi wa Bwana, aliyetutembelea, aliniambia
nijiandae, kwa sababu
nitakwenda kuona Mbingu na
kuzimu. Lakini pia aliniambia
kitu kigumu. Alisema
"Nitakufa." Haikuwa rahisi niliposikia neno hili. "Nitakufa namna gani? mie
mdogo sana", Nilimuuliza.
Akanijibu, "Usihofu juu ya
lolote, Kila kitu Mungu
afanyacho hakina makosa wala
mawaa, na atakurejesha duniani, ili utoe ushuhuda juu
ya Mbinguni na Kuzimu,
kwakuwa hilo ndilo Bwana
anataka sote tujue" Nikasema
"Amen, lakini nitagongwa na
gari au nitakufaje?" Mawazo yalinisonga sana, lakini Bwana
akaniambia nisihofu, kila kitu
kiko katika uwezo wake.
Nikasema, "Ahsante Bwana"
Ilipofika tarehe 6 Novemba,
baada ya kurejea nyumbani toka shule, malaika wale
walikuwa nami, hata
nilipokuwa namsifu Bwana.
Wao walikuwa hawaongei
nami; bali walidumu kusema,
"Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Hallelujah," huku
wakimpa utukufu, heshima na
sifa Baba wa Mbinguni. Roho
Mtakatifu pia alikuwa na
malaika wale huku akifurahi.
Watu wengi husema injili/ wokovu ni wa kuchosha/
kukera, lakini huo ni uongo
mkubwa toka kwa mwovu ili
kuwafanya watu wasitafute
uwepo wa Mungu. Nami pia
niliamini hivyo hapo kwanza, lakini baada ya kukutana na
Bwana na Roho Mtakatifu,
najua injili haikeri wala
kuchosha, niburudisho la ajabu
hapa duniani!
Ninaweza kumwona; kucheza na kuongea naye Roho
Mtakatifu. Lakini malaika
walikuwa hawaongei nami, ila
walikuwa wakimsifu Bwana.
Nikimwambia Roho twende
nami nakufanya hili na lile huja na kuwa nami. Ninaweza
kujihisi na kumwona vema.
Japokuwa wengi hawamwoni,
yeye yupo! Mahusiano haya
yamendelea, hata hakuna
sababu ya kuyasimamisha, hasa baada ya kuonja radha
yake na faida za Roho
Mtakatifu…… hakuna njia ya
kujitenga naye jinsi alivyo
mwema na wafaida, hasa
nikikumbuka alikonitoa, jinsi nilivyokuwa, ninamshukuru
sana kwa rehema zake na
upendo wake kwa wanadamu
na kwangu mimi!
Tarehe 7, Novemba,
nilipokuwa narudi nyumbani, nikasikia sauti ikisema
"Jiandae, kwakuwa leo
utakufa," Nilijua kuwa ni Roho
Mtakatifu kwa vile nilimwona
vema. Niliipuuza sauti yake na
kusema "Bwana, Sitaki kufa leo!" Lakini alirudia, "Jiandae,
kwakuwa leo utakufa!" Mara hii
sauti ilikuwa ya juu zaidi na
mkazo mkubwa. Nikajibu,
"Bwana, najua ni wewe
unayesema nami; nimeuliza ili kupata uhakika tu, mapenzi
yako yatendeke. Nitafanya kila
utakalo niambia, najiachia
kwako Bwana, japo naogopa,
najua upo nami, nawe ni wa
kweli." Niliomba, "Bwana, Yule mtumishi wako uliyemtumia
kunipa ujumbe mara ya
kwanza, mlete muda huu,
nimkute nyumbani, na umpe
tena neno hili aseme nami
kuwa leo ndiyo siku yangu ya kufa." Sasa mara zote Bwana
hujua ya nyuma, yaliyopo na
yajayo. Alijua kuwa
nitamwomba neno hili. Kwa
hiyo nilipofika nyumbani
nikamkuta mtumishi wa Bwana ameishafika!.
Maxima (Mama ya Binti):
Binti yangu alipofika nyumbani,
tulikuwa jikoni. Mara Angelica
alipomwona mtumishi wa
Bwana, akasema, "Bwana akubariki." Mtumishi wa Mungu
akajibu, "Bwana akubariki
nawe. Je uko tayari? Kwa
kuwa leo ndiyo siku Bwana
atakayo kuchukua, saa kumi
jioni." Angelica alisimama na kushikwa na mshangao
kwamba Bwana amejibu ombi
lake na kufanya vilevile
alivyomwomba njiani.
Angelica:
Niliposikia hayo maneno ya mtumishi, nikasema, "Ameni...
lakini sitaki kufa, sitakufa!
Hapana, Bwana, naogopa,
naogopa sana, ninahofu
kubwa!" Mtumishi wa Bwana
akasema, "Tuombe ili hofu ikutoke sasa kwa jina la
Bwana." Nikasema, "Ameni" na
tukaomba. Ghafla nikajisia
hofu yote imenitoka na furaha
isiyoelezeka ikajaa ndani
mwangu, nakuanza kuwaza kuwa kifo ni kitu chema kuliko
vyote nikitamanicho kinifike!
Nikanza kutabasamu na
kicheka wakati huo kila mmoja aliyepo akinitazama.
Wakaniona jinsi nilivyobadilika
toka unyonge na kuwa
mwenye furaha.
Nilikuwa natabasamu,
narukaruka na kuimba. Picha wakimwombea:
Maxima:
Binti yangu ghafla akawa
mwenye furaha ndani ya moyo
na kuanza kula. Alionja karibia
kila kitu kilichokuwepo, huku akisema,
"Kama sitarudi, sawa
nimeshakula na kushiba."
Angelica:
Kila mmoja akaanza kucheka
na kuuliza, "kwanini uko hivyo badala ya kuwa na huzuni,
unafuraha
na mwenye raha?" nikawajibu,
"Ndiyo ninafuraha: ninakwenda
kumwona Bwana, nitakuwa
naye, lakini sijui kama nitarudi. Kwa
hiyo nataka kugawa vitu
vyangu vyote." Wote
wakastaajabu na
kuniuliza, "Unataka kugawa
vitu vyako vyote?" macho ya mama yangu yalinitazama kwa
mshangao zaidi!
Maxima:
Binti yangu akaanza kugawa
vitu vyake. Aligawa vyote,
vyote! Ma-dada wa kanisani walikuwepo,
nao pia aliwapa baadhi ya vitu
kwa kila mmoja. Nilipomuuliza
nia yake, alisema, "Kama
nikirudi,
watanirejeshea vyote, lakini nisiporudi, watabaki navyo."
Angelica:
Niliwaza huzuni aliyokuwa
nayo mama yangu niliposema
maneno hayo. Lakini nilijisikia
furaha tupu, kwa hiyo nikaendelea
kugawa vitu: nguo, kitanda,
simu ya mkononi, kila kitu,
lakini kwa
sharti: kama nikirudi, kila kitu
kitarejeshwa kwangu. Wote wakaanza kucheka.
Maxima:
Binti yangu alikuwa na
msimamo na nia ya dhati,
lakini kama mama nilishikwa
na huzuni sana. Haikuwa jambo rahisi.
Niliwaza, "Bwana muda huo
ukiwadia, itakuwajekuwaje?"
Sikuweza
kuelewa. Na walipoanza
kuomba, nilikuwa napanga vitu ndani ya nyumba. Walisema,
"Dada njoo
tuombe." Lakini niliwajibu,
"Nyie endeleeni, nitajiunga
nanyi muda si mrefu. Ngoja
nimalizie kazi hii."
Angelica:
Wote walikuwa wananiangalia
mimi tulipokuwa tunaomba.
Niliomba, "Bwana, nataka
kufanya mapenzi yako. Wewe si
mwanadamu hata useme
uwongo au ujute, najua wewe
ni mkweli. Kama
nitakuaibisha, basi vema
unichukue moja kwa moja; lakini kama nitayafanya
mapenzi, basi
unirejeshe tena, lakini nisaidie
kusema ukweli, niandae mimi,
nisaidie kuhubiri na
kuwaambia watu kutubu." Hiyo ndiyo ilikuwa
sala yangu fupi sana.
Nilimwambia mtumishi wa
Bwana,
"Usimwambie mama yangu
maneno niliyomwomba Bwana." Naye akajibu,
"sitamwambia sasa,
lakini mara Bwana
atakapokutwa, nitamwambia."
Tuliendelea kuomba na
kuungana katika duara. Maxima:
Ilipofika saa 9:30 jioni, Bwana
akamwambia mtumishi wake
ampake mafuta binti yangu.
Kwa hiyo
baadhi yetu tulikwenda chumbani na kumpaka mafuta.
Alitupa dakika mbili tumpake
mwili mzima,
toka kichwani hadi chini, kila
mahali, mwili mzima. Akawa
mwili wote amepakwa mafuta. KIFO CHAKE
Angelica:
Mama yangu na dada mmoja,
Fátima Navarrete, walinipaka
mafuta. Kadri walivyokuwa
wananipaka, nilijisikia kama kuna kitu kinanifunika, kama
kioo kilinizunguka mimi. Ni
vigumu
kuelezea, nilijisikia kama
nimezingirwa na ngao fulani,
na nashindwa kuelezea nilivyokuwa
najisikia. Baada ya hapo kila
walipojaribu kunigusa
walishindwa!
Maxima:
Kadri tulivyokuwa tukimwombea Angelica,
nilijaribu kuweka mkono juu
yake, nilishindwa!
Alikuwa amezingirwa na kitu.
Ilikuwa ajabu, hakuna
aliyeweza kumgusa tena! Uzio huo ulianzia
kichwani hadi miguuni, karibia
sentimenta 30 (Inchi 12). Hilo
lilinitisha zaidi mimi.
Nimewawekea
mikono wengi kabla, katika huduma ya Bwana, lakini
jambo kama hili halijawahi
kutokea!
Nikasema, "Oh, kuna jambo
lazima linatendeka," na
nikaanza kuomba na kumshukuru Bwana.
Ghafla, nikasikia furaha kubwa
sana. Huzuni iliyokuwa moyoni
ikanitoka, maumivu yakakoma
na
sasa nikasikia raha na furaha ajabu! Tuliendelea kuomba na
ilipofika saa 10.00 jioni, binti
yangu
akaanguka sakafuni.
Angelica:
Wakati wa maombi, nilisikia kuishiwa pumzi; nikashindwa
kupumua. Nikasikia maumivu
tumboni
na moyoni. Nilijisiki damu
ikisimama, na ghafla maumivu
makali mwili mzima. Nililoweza kusema, "Bwana, nipe nguvu,
nipe mimi nguvu!" kwasababu
nilijisikia kushindwa kuendelea
zaidi.
Sikuwa na nguvu kabisa, zote
zilinitoka! Na nilipoangalia juu mbinguni, katika roho, si kwa
macho
ya mwilini, niliona mbingu
zikifunguka. Niliwaona
malaika, siyo wawili au kumi,
bali kwa mamilioni wakiwa pamoja
wamekusanyika. Katikati yao
niliona mwanga, mara 10,000
zaidi ya
jua. Na nikasema, "Bwana ni
wewe unayekuja!" Maxima:
Alipoanguka chini, tulijaribu
kumsimamisha, lakini
hakuweza kusimama
mwenyewe. Muda huu
tuliweza kumgusa. Alikuwa akisema, "Omba. Sina nguvu,
mama, sina nguvu na ninasikia
maumivu." Mwanzo alisikia
maumivu tumboni, na baadaye
moyoni. Tuliendelea kuomba
na kumsihi Bwana. Bwana
alichukua maisha yake!
Picha Mwili wake:
Sijawahi katika maisha yangu
kumwona mtu akifa.
Nilishuhudia binti yangu, akigugumia maumivu! Haikuwa
rahisi hata kidogo! Sikuweza
kuelewa maneno yake ya
mwisho, na mwisho alitulia.
Niliweka mikono yangu usoni
pake, na kioo mdomoni kuona kama alikuwa anapumua.
Hakuwa na pumzi tena, alitulia
kimya kabisa. Nilimshika,
alikuwa angali na joto kama
kawaida. Nilichukua shuka na
kumfunika na kwa muda mfupi akaanza kupoa na kuwa wa
baridi sana. Nywele zake
zikalala, kama za maiti na
akabadilika ubaridi wa barafu.
Angelica:
Yesu alikuwa anashuka chini, na nikajisikia mwili ukifa. Kadri
Yesu na malaika walivyozidi
kukaribia, nikajisikia kuondoka,
na sikuwa mimi tena. Sikuwa
hai tena, nilikuwa nakufa na
kugugumia maumivu! Wakati mwili wangu ulipoanguka chini,
walikuwa tayari wamefika.
Nyumba yetu ilijaa malaika, na
katikati yao niliona mwanga
mkali kuliko wa jua! Ilikuwa
vigumu; nilisikia maumivu makali wakati roho yangu
ilipotenganishwa na mwili.
Nilikuwa nalia na kupiga
kelele, kadri nilivyoona mwili
wangu sakafuni. Nilimuuliza,
"Bwana, nini kinachotokea? Nini kinachotokea?" Nilijaribu
kuugusa mwili wangu na
kuurudia tena, lakini
nilipojaribu, ilikuwa kama
kushika hewa: sikuweza
kuugusa, mkono wangu ulipitiliza. Hakuna kati ya
waliokuwa wananiombea
aliyenisikia! Na nikapiga
kelele, "Bwana, nisaidie mimi!"
Maxima:
Mume wangu alifika tulipokuwa tunaomba, na alimkuta pale.
Bwana alinipa nguvu kwa
kuwa sikujua la kufanya.
Ilikuwa kama vile yuko
mahututi (kwenye coma), lakini
nilijua yuko salama, kwasababu ilikuwa ni kazi ya
Bwana. Kwahiyo nikasema
"Bwana, mapenzi yako
yafanyike."
BWANA YESU KRISTO
Angelica: Wakati huo nasikia sauti ya
Bwana, sauti nzuri kama radi
lakini ya UPENDO, "Usiogope,
Binti, kwa kuwa mimi ni
Yehova, Mungu wako, na
nimekuja hapa kukuonesha niliyokuahidi wewe. Inuka, kwa
kuwa mimi ni Yehova,
ninayekushika mkono wako wa
kuume na kukuambia,
usiogope, nitakusaidia wewe."
Ghafla, nikasimama. Nilikuwa nimepiga magoti chini,
ninauangalia mwili wangu,
nikitaka kuurejea bila
mafanikio. Niliposikia sauti
yake, woga ukanitoka, na
sikuwa na hofu tena. Nilipoanza kutembea, malaika
wakaanza kufungua njia.
Kulikuwa na mwanga mkali
ung'aao, na nilipouangalia
nilisikia amani ya ajabu. Kadri
nilivyoangalia, nilimwona mwanaume mzuri, mrefu,
aliyevaa vizuri na kuvutia sana
kumwangalia, mwenye siha
njema. Mwanga ulitoka kwake.
Kulikuwa na mwanga mkali
kiasi cha kushindwa kumwangalia uso wake! Lakini
niliweza kuona nywele zake za
dhahabu ing'aayo na vazi
jeupe na mshipi kifuani pake.
Ukisomeka, "MFALME WA
WAFALME NA BWANA WA MABWANA."
Nilimwangalia miguuni pake,
alikuwa amevaa sandozi zenye
mng'ao wa dhahabu, dhahabu
safi. Alikuwa mzuri sana!
Akaninyooshea mkono wake. Nilipomshika mkono wake,
haikuwa kama nilipojaribu
kuugusa mwili wangu, mkono
haukupitiliza. Nikauliza, "Nini
kinachotokea?" naye akasema,
"Nitakuonesha wewe kuzimu ili ukirudi uwaambie wanadamu
kuwa kuzimu ni halisi; kuwa ni
kweli ipo. Na pia utukufu
wangu nitakuonesha wewe, ili
uwaambie watu wangu
wajiaandae, kwa kuwa utukufu wangu ni halisi na mimi pia."
Akasema, "Binti, usiogope"
akarudia kusema tena na mimi
nikasema, "Bwana, nataka tu
kwenda Mbinguni, lakini siyo
kuzimu, kwasababu nimesikia kunatisha!" Akasema, "Binti,
nitakuwa nawe. Sitakuacha
huko na nitakuonesha huko
mahali kwasababu wengi
wanajua kuzimu ipo lakini
hawaiogopi. Wanaamini ni mchezo, na
kuzimu ni mzaha, na wengi
hawajui lolote juu yake. Ndiyo
maana
nitakuonesha wewe huko kwa
sababu wanaopotea ni wengi kuliko wanaoingia katika
utukufu
wangu." Aliposema hayo,
niliona machozi yakitiririka
kwenye vazi lake.
Nikamwuuliza, "Bwana, kwanini unalia?" Akanijibu,
"Binti, kwasababu wengi
wanaangamia, na
nitakuonesha hii, ili
uende na uwaambie ukweli na
wewe usirudie hapo." KUZIMU
Ghafla, alivyokuwa anaongea,
kila kitu kikaanza kutembea.
Ardhi ilitikisika na kupasuka,
na
nikaona shimo jeusi tii chini. Shimo:
Tulikuwa tumesimama kama
kwenye mwamba na malaika
wakituzunguka. Nikasema,
"Bwana,
sitaki kwenda mahali huko!" akasema, "Binti, usiogope niko
pamoja nawe." Kwa sekunde
chache
tukashuka kwenye shimo jeusi.
Nilijaribu kuangalia lakini
kulikuwa na kiza kikuu. Niliona duara
kubwa, na kusikia mamilioni ya
sauti.
Nilipata moto. Nikajisikia ngozi
yangu kuungua. Nikamuuliza,
"Bwana, hiki ni nini? sitaki kwenda mahali huko!" Bwana
akasema hilo ni lango tu la
kwenda kuzimu. Kulikuwa kuna
harufu
mbaya, yakutisha,
isiyovumilika, na nikamsihi Yesu asinipeleke mimi. Naye
akajibu, "Binti, ni
muhimu ufike na kujua sehemu
hii." Nikalia, "Lakini kwanini,
Bwana, kwanini?" naye
akasema, "Ili ukawaambie ukweli
wanadamu; wanadamu
wanaangamia, wanapotea na
wachache sana
wanaoingia ufalme
wangu." (Mat.7:14) Akishasema hivi, hulia sana.
Maneno yake yalinitia nguvu
na kunihimiza, kwa hiyo
nikaendelea kutembea.
Ziwa la Moto:
Tulifika mwisho wa tanuru/ lango, nilipoangalia chini
niliona umati umefunikwa na
miali ya moto. Bwana akasema
"Binti, nakupa hii." Ilikuwa ni
faili kubwa lenye karatasi
ambazo hazijaandikwa chochote. "Binti, chukua na
kalamu hii ili uweze kuandika
yote nitakayokuonesha,
utakayoyaona na kusikia.
Utaandika kila kitu ukionacho
na utaishi nayo." Nikasema, "Bwana, nitafanya, lakini
nimeshaanza kuona mengi
mno, Bwana. Ninaona roho
zikiteswa, na kuzamishwa
kwenye moto."
Maxima: Muda uliendelea kupita, na
binti yangu alikuwa bado
kalala pale. "Bwana, nini
kinachotokea?" Machozi
yalikuwa yakimtoka kwenye
macho, lakini kila nilipomfuta, yalitoka tena. Nikaweka kioo
mdomoni pake kuona kama
anapumua, hakukuwa na
pumzi. Tuliangalia mapigo ya
damu, wapi, hakuna kitu!.
Tuliweka mikono tumboni pake, wapi! Hakuna kitu.
Mtumishi wa Bwana akasema,
"mahali alipo sasa, siyo mahali
pa kutabasamu bali mahali pa
mateso."
Angelica: Nikamwambia Yesu,
Nitashuhudia kuwa kuzimu ni
halisi, kwamba ipo, lakini nitoe
hapa sasa!" na akanijibu,
"Binti, hatuja ingia bado mahali
penyewe, na sijakuonesha chochote, tayari unataka
nikutoe huku?" nikasema
"Bwana, tafadhari nitoe mahali
hapa," tukaendelea kushuka
kwenye korongo/shimo
lakutisha! Nikaanza kulia na kupiga yowee, "Bwana,
hapana, hapana, hapana,
hapana……… Sitaki kwenda!"
naye hujibu, "Unatakiwa kuona
haya."
Niliona mapepo yakutisha, ya kila aina, makubwa na
madogo. Yalikuwa yanakimbia
sana, na yameshika vitu
mkononi. "Bwana, kwanini
yanakimbia hivyo na
yameshika nini?" akanijibu, "Binti, wanakimbia hivyo
kwasababu wajua muda wao
karibu kwisha, kwasababu
muda wa kuwaharibu/
kuwapoteza wanadamu,
hususani watu wangu. Na walivyoshika mkononi ni
mishale ya kuwaharibu
wanadamu, kwasababu kila
pepo amepewa jina na kwa
kadri ya jina lake, ana mishale
ya kumharibu mtu na kumleta huku kuzimu; malengo yao ni
kumharibu mtu na kumleta
kuzimu." Na niliendelea kuona
mapepo yakikimbia na kutoka
kuelekea duniani na Bwana
akaniambia; "Wanakwenda duniani ili kuleta na kuwatupa
wanadamu huku." Alipokuwa
akisema hivyo, Bwana hulia,
hulia sana. Kila alipolia nami
nililia pia.
Maxima: Binti yangu alikuwa amekufa
kwa masaa 23, lakini sikutoa
taarifa kwenye mamlaka
yoyote. Niliomba, "Bwana,
nitasubiri kwa masaa 24.
Kama binti yangu hatarudi ndani ya saa 24, nitampigia
simu Daktari." Lakini, Bwana
alimrejesha kabla ya saa 24
hazijatimia.
Angelica:
Bwana akaniambia, "je uko tayari kuona
nitakachokuonesha wewe?"
Nikasema, "Ndiyo Bwana,".
Alinipeleka kwenye sero moja,
ambapo nilimwona kijana
akiwa matesoni katikati ya miali ya moto. Nikajulishwa
namba sero yake, japokuwa
sikuweza kujua ile namba,
ilionekana kama imeandikwa
kinyume hivi. Palikuwa na
nembo kubwa mle ndani, na kijana alikuwa na namba 666
kwenye kipaji cha uso. Pia
alikuwa na aina ya kipande
cha chuma imebandikwa
kwenye ngozi yake. Funza
walikuwa wanamtafuna, haikuweza kuharibu kipande
kile; wala moto haukuweza
kukiunguza. Akapiga kelele,
"Bwana, nirehemu mimi. Nitoe
mahali hapa. Nisamehe mimi
Bwana!" lakini Yesu alimjibu, "umechelewa, umechelewa
sana: nilikupa fursa lakini
hutaka kutubu." Nikamuuliza
Yesu, "Bwana, kwanini huyu
yuko hapa?" mara
nikajulishwa. Akiwa duniani, kijana huyu
alijua neno la Mungu, lakini
ghafla akajitenga na Bwana na
kuchagua
pombe, madawa ya kulevya na
kupita katika njia zisizofaa. Hakutaka kufuata njia ya
Bwana. Yesu
alimwonya mara nyingi juu la
litakalompata. Yesu akasema,
"Binti, yuko hapa kwasababu
kila anayeyakataa maneno yangu,
anaye amhukumuye: lile neno
nilisema naye litamhukumu
siku
ya mwisho," (Yohana 12:48) na
Yesu akalia tena. Bwana akilia, nitofauti nasi
tuliavyo na zaidi yetu. Yeye
hulia na maumivu makali
moyoni na
uchungu usioelezeka. Bwana
akasema, "Sikutengeneza kuzimu kwaajili ya wanadamu,"
Nikamuuliza, "Sasa Bwana
kwanini wanadamu wapo
huku," Akanijibu, "Binti,
niliumba kwajili
ya shetani na malaika zake, ambayo ni mapepo;(Mat.
25:41) lakini, kwasababu ya
dhambi na
kukosekana kwa toba,
wanadamu huishia hapa, na
wengi wangamiao kuliko wanaofika katika
utukufu wangu!" Akaendelea
kulia na huniumiza sana
nimwonapo akilia. "Binti,
nalitoa maisha
kwaajili ya wanadamu, ili wasiangamie, ili wasiishie
hapa [Kuzimu]. Nalitoa maisha
yangu kwa
upendo na huruma, ili
wanadamu waendee toba na
kuingia katika ufalme wa Mbinguni." Yesu
kwa huzuni huugua kiasi cha
kushindwa kustahimili
maumivu, kadri aonavyo watu
pale kuzimu.
Kwa kuwa na Yesu, kulinifanya nijisikie salama. Niliwaza,
"kama nikimwacha Bwana
aende,
ninge-nasa kuzimu pale"
Nikamuuliza, "Yesu, je nina
ndugu yangu mahali hapa?" Akanitazama
kwa jinsi nilivyokuwa nalia na
akasema, "Binti, niko nawe,"
Kwasababu nilikuwa mwenye
hofu
sana. Akanipeleke kwenye sero nyingine. Sikuwahi
kuwaza kumwona ndugu yangu
kwenye sero
ile. Nilimwona mwanamke
akiteswa, alikuwa na funza
wakimla uso wake, na mapepo yakimchoma
mikuki mwilini. Naye hupiga
kelele, "Hapana, Bwana,
nihurumie, nisamehe mimi,
tafadhari, nitoe
mahali hapa kwa dakika moja!" (Luka 16:24)
Kuzimu, watu huteswa na
kumbukumbu za waliyoyafanya
duniani. Mapepo hudhihaki
watu na
kuwaambia, "abudu na kusifu kwasababu huu ndiyo ufalme
wenu!" na watu hupiga kelele
11
wakikumbuka kuwa walimjua
Mungu, kwasababu walijua
neno. Walimjua Bwana waliteswa mara
dufu ya wengine.
Bwana akasema, "Hakuna tena
nafasi kwa walioko pale
[kuzimu]; kungali na nafasi
kwa walio hai." Nikamuuliza, "Bwana,
kwanini bibi yangu mkubwa
yupo pale? Sijui kama alikujua
wewe.
Kwanini yupo kuzimu Bwana?"
akanijibu, "Binti, yupo hapa kwasababu alishindwa
kusamehe….. binti, yeyote
asiyesamehe, sitamsamehe
huyu."
Nikamuuliza, "Bwana, lakini
wewe husamehe, na una rehema." Naye akanijibu,
"Ndiyo, binti,
lakini nilazima kusamehe,
kwasababu hawajawasamehe
wengi, na ndiyo maana wengi
wapo hapa, wameshindwa
kusamehe…… nenda
kawaambia wanadamu ni
muda wa kusamehe, hasa
hasa watu wangu, kwakuwa
wengi miongoni mwa watu wangu hawajasamehe.
Waambie
waache malaaumu, mafundo,
chuki mioyoni mwao, kwa
kuwa ni muda wa kusamehe!
Kama kifo kikimsitukiza mtu
aliyeshindwa kusamehe, huyo
mtu atakwenda kuzimu,
kwakuwa hakuna
awezaye kununua maisha."
Tulipoondoka hapo, bibi yangu mkubwa alifunikwa na moto na
akapiga makelele, "Aaaah," na
akaanza kutukana jina la
Mungu, na kumlaani Bwana;
kila mtu
kuzimu humtukana Mungu. Tulipoondoka eneo lile,
nikaona kuwa kuzimu imejaa
roho ziteswazo. Watu wengi
huinua mikono
nje, wakimwomba Yesu
msaada wa kuwatoa nje. Lakini Bwana hakuwa na lolote
la kufanya kwao,
nao huanza kumtukana Mungu.
Mara Yesu hulia sana na
kusema, "Inaniumiza sana
kuwasikia, inaniumiza mimi sana
wanavyofanya, kwasababu
siwezi kufanya lolote kwaajili
yao. Ninacho
kueleza ni hiki; nina nafasi kwa
hao walioko duniani, ambao hawaajafa, walio hai, wanao
muda
wa kutubu!"
Bwana akaniambia kuna watu
wengi maaruku huku kuzimu,
na pia wengi waliomjua Bwana.
Akasema, "Nitakuonesha
upande mwingine wa tanuru."
Tukaenda mahali penye
mwanamke
aliyezingirwa na miali ya moto. Alikuwa katika maumivu
makubwa na kupiga makelele,
akiomba
huruma kwa Bwana. Yesu
akanyoosha mkono kwake na
akaniambia, "Binti, Yule mwanamke
umwonaye pale, amezingirwa
na miali ya moto ni Selena."
Kadri tulivyokuwa
tunamkaribia,
akapiga kelele, "Bwana, nihurumie mimi, nisamehe
mimi Bwana, nitoe mahali
hapa!" lakini
Bwana akamtazama na
kusema, "Umechelewa,
umechelewa sana, huwezi kutubu sasa."
Selena
Aliponiona mimi akasema,
"Tafadhari, nakuomba wewe,
waambie watu hivi, tafadhari
sema na usinyamaze; nenda waambie
wasije mahali hapa; nenda
waambie wasisikilize nyimbo
zangu, wala
wasiimbe hizo nyimbo."(1
Yohana 2:15) Nikamuuliza, "kwanini unataka mimi
niwaambie hivyo?"
naye akanijibu, "Kwasababu
kila wakati watu wanaposikiliza
nyimbo zangu, nateswa zaidi
na zaidi, na mtu anayeimba na
kusikiliza nyimbo zangu,
anaelekea mahali hapa.
Tafadhari, nenda
uwaambie wasije huku; nenda
waambie kuzimu ni halisi, ipo kweli!". Akapiga kelele na
mapepo
humchoma mikuki na Selena
kulia, "Nisaidie mimi,
nihurumie mimi Bwana!" lakini
kwa huzuni Bwana alimwambia,
"umechelewa sana."
Nikaangalia pande zote za
eneo lile, lilikuwa limejaa
waimbaji na wasanii waliokufa.
Walikuwa wakiimba na kuimba, bila
kusimama. Bwana
akanifafanulia, "Binti, mtu
aliyepo hapa, lazima
aendelee kufanya kile
alichokuwa anafanya duniani, kama hajatubu."
Kadri nilivyokuwa naangalia
eneo lile, niliona mapepo
mengi yakinyunyiza vitu kama
mvua.
Nilidhani ni mvua inanyesha. Lakini niliona watu kwenye
miali ya moto wakikimbia mbali
na ile
mvua na kupiga yowee,
"Hapana, nisaidie, Bwana!.....
Hapana, haiwezekani kuwa hivyo," na
mapepo yalikuwa yanacheka
na kuwaambia watu, "Sifu na
kuabudu kwasababu hapa ni
ufalme
wenu milele na milele!" Niliona miali ya moto ikiongezeka na
funza za watu zikiongezeka
zaidi!
Hayakuwa maji yale bali
kiberiti cha kuongeza miali ya
moto na kuongea maumivu ya kila mtu.
Nikamuuliza Yesu, "Ni nini
kinachotokea?..... Bwana, ni
nini hiki?" Bwana akanijibu,
"Huu ni
ujira wa yeyote asiyetubu." (Zaburi 11:6).
Bwana akanipeleka mahali
alipo mtu aliyejulikana sana.
Kabla ya maono haya, nilishi
maisha kama
msichana wa kikristo wa nia mbili. Nilidhani kila mtu
anayekufa anakwenda
Mbinguni; wale
walifanyiwa ibada za mazishi
watakwenda mbinguni, kumbe
sikuwa sahihi, nilikosa. Alipofariki
Papa John Paul II, marafiki
zangu na ndugu walisema
amekwenda mbinguni. Taarifa
zote kwenye
LUNINGA [TV], na vyombo mbalimbali vya habari vilisema,
"Papa John Paul II amefariki,
apumzike kwa amani.
Anafurahia sasa kuwa na
Bwana na malaika Mbinguni"
na mimi niliamini yote kuwa ndivyo. Lakini
kumbe nilikuwa najidanganya
mwenyewe, kwasababu
nimemwona
kuzimu, akiteswa kwa miali ya
moto. Nilimtazama uso wake, alikuwa mwenyewe Papa John
Paul
II! Bwana akaniambia,
"Angalia, Binti, Yule
mwanaume umwonaye pale, ni
Papa John Paul II. Yuko hapa; akiteswa
kwasababu hakutubu."
Papa John Paul II
Lakini nikamuuliza, "Bwana,
kwanini yuko hapa? Alikuwa
akihubiri kanisani." Yesu akanijibu,
"Binti, hakuna mwasherati,
wala muabudu sanamu,
hakuna mchoyo na hakuna
mwongo
atakayerithi ufalme wangu." (Eph 5:5) Nikamjibu,
"Ndiyo, najua ni kweli, lakini
nataka kujua
kwanini yuko hapa, kwasababu
alikuwa akiwahubiria umati wa
watu!" Na Yesu akanijibu, "Ndiyo,
Binti, alisema mengi, lakini
hakusema kweli kama ilivyo.
Hakusema kweli na kweli
aliijua na
japokuwa aliijua kweli, alipenda fedha zaidi ya
kuhubiri habari za wokovu.
Hakutoa uhalisia;
hakusema kuzimu ni halisi na
mbinguni kupo; Binti, sasa
yuko mahali hapa." Nilipomwangalia mtu huyu,
alikuwa na joka kubwa lenye
sindano nyingi mwilini mwake,
limemzingira shingoni, naye
hujaribu kumtoa. Nalimwomba
Yesu, "Bwana, msaidie!" Mwanaume hupiga kelele,
"Nisaidie mimi, Bwana
nihurumie; nitoe mahali hapa;
nisamehe mimi! Ninatubu
Bwana; Nataka nirudi duniani,
nataka nirudi duniani nikatubu." Bwana alimtazama
na kumwambia, "Ulijua vizuri
yote haya. Ulijua vema kuwa
kuzimu ni halisi, ipo……..
umechelewa; hakuna tena
nafasi kwaajili yako." Bwana akasema, "Tazama
Binti, nitakonesha maisha ya
mtu huyu." Yesu akanionesha
kioo kikubwa kama LUNINGA
[TV]; nikaona alivyotoa misa
mara nyingi kwa umati wa watu. Na watu wale
walivyokuwa waabudu
sanamu. Yesu akasema,
"Tazama, Binti, wapo waabudu
sanamu wengi hapa [Kuzimu].
Ibada ya sanamu haiwezi kuokoa Binti. Ni mimi pekee
niwezaye kuokoa, na nje
yangu hakuna mwingine
aokoaye. Nawapenda wenye
dhambi, lakini nachukia
dhambi Binti. Nenda na uwaambie wanadamu kuwa
nawapenda na ninataka waje
kwangu."
Kadri Bwana alivyokuwa
akisema, nilianza kuona mtu
huyu akipokea makusanyo makubwa ya sarafu na fedha;
vyote alivihifadhi. Alikuwa na
fedha nyingi sana. Naliona
sura yake imeketi katika
mamlaka yake, lakini pia
naliweza kuona zaidi. Japo ni kweli watu hawa hawaoi,
ninakuhakikishia wewe,
sizushi, Bwana alinionesha
mimi, wanalala na masista; na
wanawake wengi!
Bwana akanionesha watu hawa wanaishi kwa uasherati,
na neno linasema hakuna
mwasherati atakayerithi ufalme
wake. Kadri nilivyokuwa
naona, Bwana akaniambia,
"Tazama, Binti, yote ninayokuonesha, ndiyo
yanayoendelea, ndivyo
alivyoishi [Papa] na ndivyo
yanayotokea katikati ya watu
wengi, katikati ya mapadre na
mapapa waliopo." Kisha Bwana akasema, "Binti, nenda
na uwaambie wanadamu ni
muda wa kugeukia."
Bwana akanionesha sehemu
watu wengi wanavyoelekea
kuzimu. Nikamuuliza, "Bwana, namna gani wanakuja huku?"
akanijibu, "Nitakuonesha."
Akanionesha lango lenye watu
wengi wakipita. Watu hawa
walikuwa wamefungwa toka
mikononi hadi miguuni. Walivaa mavazi meusi na
kubeba mizigo mgongoni
mwao. Yesu akasema, "Binti,
hao watu uwaonao hawanijui
mimi bado. Mizigo waliyobeba
ni dhambi, lakini nenda waambie walete mizigo
kwangu, nami nitawapumzisha;
kwa kuwa mie ndiye mwenye
kusamehe dhambi zao zote….
Binti, nenda na uwaambie
waje kwangu, kwani nawasubiri na mikono yangu
iko wazi kuwapokea, na
uwaambie hapo wanaelekea
mahali hapa [kuzimu]."
Kadri nilivyokuwa nawatazama
watu wakitembea, nikamwambia, "Bwana, Yule
mtu pale ni binamu yangu; na
Yule kijana pia, Bwana, na
Yule binti pale anayelekea
kuzimu; oh familia yangu
inakuja huku kuzimu!" Bwana akajibu, "Binti, wanakuja huku,
lakini nenda uwaeleze
wanakoelekea, nenda waeleze
kuwa wanakwenda kuzimu.
Nenda waeleze kuwa
nimekuchagua wewe uwe mlinzi wangu……
nimekuchagua wewe kama
mlinzi, hii inamaanisha kuwa
unatakiwa uwaambie ukweli.
Unatakiwa uende uwaeleze
yote niliyokuonesha wewe. Kama hutawaambia na jambo
likampata mtu huyu, damu
yake itakuwa juu yako, lakini
ukiende na kufanya
nilivyokueleza, hapo mtu huyu
nitamdai mwenyewe. Kama mtu hatatubu, hapo wajibu
ulionao utaondolewa, kwa
kuwa atadaiwa mwenyewe na
damu yake haitakuwa juu
yako. (Ezekia 3:18)"
Yesu akaniambia wengi wa watu maarufu wanaelekea
huku [kuzimu], maarufu na
watu muhimu. Kwa mfano,
Michael Jackson. Huyu alikuwa
maarufu duaniani kote lakini
alikuwa mjumbe wa shetani. Japokuwa wengi
wanaweza wasione na
kuelewa hivyo, lakini huo ndiyo
ukweli. Huyu
alikuwa na mkataba na
shetani: alikubaliana na shetani ili awe na heshima na
sifa ilikuwa vutia
wapenzi wengi.
Michael_Jackson
Hizo hatua na mitindo
aliyokuwa anafanya, ndivyo nilivyoona mimi mapepo
yakicheza na
kutembea yanapotesa watu
kuzimu. Yalikuwa yanateleza
kwa kurudi nyuma na siyo
mbele, huku yakipiga kelele; yakifurahia
mateso wanayopata watu.
Ngoja nikuambia wewe kuwa
Michael
Jackson yuko kuzimu. Bwana
alinionesha baada ya kufa Michael. Alinionesha Michael
Jackson
akiteswa kwenye miali ya
moto. Nikalia kwa Yesu,
"Kwanini?" haikuwa rahisi
kuona mtu huyu alivyokuwa anateswa na
alivyokuwa analia na kupiga
mayowe. Yeyote anayesikiliza
nyimbo za
Michael Jackson au kuziimba
au ni mpenzi/shabiki wa Michael Jackson, ninakuonya
kuwa shetani
anakutega katika mtego wake
ili mwisho uishie kuzimu. Mara
hii, jitoe na kumkana shetani
kwa jina Yesu! Yesu anataka
kukuweka huru wewe, ili
usipotee milele. Bwana
akaniambia, "Binti,
kuna watu wanijuao pia
wanakuja huku." Nikamuuliza, "Bwana, inakuwa je mtu
akujue harafu
aje huku?" akanijibu, "Mtu Yule
aliyeacha njia zangu na mtu
Yule anayeishi aina mbili za
maisha [wokovu na dhambi]." Akaanza kunionesha watu
wanaoelekea kuzimu.
Walikuwa
wamefungwa kamba toka
mikononi hadi miguuni. Kila
mmoja alivaa vazi jeupe, lakini limetobokatoboka, lina-
mabakamabaka na
limekunjamana. Yesu
akaniambia, "Binti, angalia
watu
walioniacha mimi. Binti, nataka kukueleza, siji duniani kwaajili
ya watu hawa. Nakuja kwaajili
ya watakatifu, waliotayari,
wasiolaumiwa, wasio na
makunyanzi na wasio na
mawaa…… nenda uwaambie warejee kwenye
njia zao za zamani," (Efeso
5:26-27) Nilianza kuwaona
wengi
miongoni mwa wajomba zangu
na watu wengine wengi waliorudi nyuma na kuziacha
njia za
Bwana. "Nenda kawaambie
ninawasubiri, walete mizigo
yao nami nitawapumzisha."
YESU alikuwa analia baada ya
kusema hayo, "Binti, wanakuja
huku [kuzimu]. Nenda
kawaambie
wajomba zako; nenda
kawambie ndugu zako kuwa wakuja huku! Binti, wengi
hawatakuamini,
lakini mimi ni shahidi wako
mwaminifu, ni shahidi wako
mwaminifu. Sitakuacha wewe.
Hata kama hawataamini, Binti,
nenda na uwaambie ukweli
huu, kwa kuwa nipo nawe. Pia
Binti
nitakuonesha jinsi watu
wanavyofika huku." Tulikwenda kwenye lango,
ambapo tuliona umati wa watu
wakiangukia ndani ya shimo
kubwa.
Siyo elfu moja wala elfu mbili,
bali wingi wake kama mchanga wa bahari, hawana idadi!
Walikuwa wananguka kwa kila
sekunde, mfano wa mkono
uliojaa mchanga umwakikapo
chini.
Zile roho zilikuwa zinaanguka kwa kasi. YESU alikuwa akilia,
na kusema, "Binti hivi ndivyo
wanadamu wanavyopotea; hivi
ndiyo mwanadamu
apoteavyo!!!..... Binti,
inaniumiza sana mimi nionavyo wanadamu
wanavyoangamia."
YESU akasema, "maapepo pia
hufanya mikutano huku." Na
nikasema, "mapepo yanafanya
mikutano?" Yesu akasema, "Ndiyo, Binti, wanakutana
kupanga, kupanga
watavyowafanya
wanadamu. Wanakutana kila
siku kwa siri." Na kwa hilo,
Yesu akanipeleka kwenye sero,
ambapo niliona meza ya mbao
na viti vikizunguka meza. Na
palikuwa na mapepo, aina zote
za
mapepo. Yesu akaelezea, "Binti, wanapanga kwenda
kuharibu nyumba/familia za
wachungaji,
wamisionari, wainjilisti na wote
wanijuao mimi. Binti wanataka
kuwaharibu; wanamishale mingi."
Mapepo hucheka na kudhihaki,
na kusema, "acha tuwaharibu
wanadamu na kuwaleta huku."
Yesu
akasema, "Nenda na uwaambie nipo pamoja nao
watu wangu. Waambie
wasiache milango wazi,
wasimpe nafasi shetani, kwa
kuwa shetani anazunguka-
zunguka kama simba angurumaye,
akimtafuta wa kummeza. (1
Petro 5:8)" Lakini neno
linasema, "anatembea kama",
kwasababu
simba halisi, ni Simba wa Yuda, Yesu Kristo wa Nazareti
(Ufunuo 5:5)! Yesu akasema,
"Binti,
wanataka kuharibu/
kuangamiza familia za
wachungaji." Nikamuuliza, "Kwanini wanataka
kuharibu familia za
wachungaji?" na Yesu akajibu,
"Kwasababu wanawajibu wa
maelfu ya watu
ambao ni kondoo wa kundi; kondoo wa kundi Bwana
aliowakabidhi wao. Wanataka
watu hao
warudie dunia tena; waangalie
nyuma na kuishia kuzimu….
Nenda kawaambie wachungaji kusema iliyo kweli tupu.
Waeleze wahubiri kweli tupu
na kusema kila kitu
ninachowaambia na
wasinyamaze nayo haya
ninayowaambia!" Tulipokuwa tunaondoka hapo,
akaniambia, "Nataka
nikuoneshe kitu kingine….
Wapo pia watoto
huku." Na nikamjibu, "watoto
huku Bwana? Kwanini wawepo watoto huku? Neno lako
lasema,
'Waacheni watoto wadogo
waje kwangu, na msiwazuie:
kwa maana Ufalme wa
Mbinguni ni wao." (Mathayo 19:14) Yesu akajibu,
"Binti, ni kweli, ufalme wa
mbinguni ni wao, lakini mtoto
lazima
aje kwangu, kwa kuwa kila
ajaye kwangu sitamtupa kamwe." (Yohana 6:37)
Ghafla, Bwana
akanionesha mvulana wa
miaka nane akiteswa kwenye
moto. Mvulana akalia, "Bwana
nihurumie mimi, nitoe mahali hapa, sitaki
kuwepo hapa!" aliendelea
kupiga kulia na kelele. Nikaona
mapepo
yamemzunguka mtoto huyu,
yaliyofanana na cartoon. Kulikuwa na aina za Dragon,
BoyZ, Ben 10,
Pokémon, Doral, na nyingine
nyingi. "Bwana, kwanini mtoto
huyu yuko huku?" Yesu
akanionesha picha ya mkanda wa maisha
mtoto huyu. Nilimwona
anavyotumia muda karibia
wote kwenye
LUNINGA [TV] akiangalia
cartoon. Cartoon ya Ben 10: Pokemon:
Yesu akasema, "Binti, hayo
maigizo ya cartoon, sinema
zake, michezo mbalimbali ya
kuigiza
inayooneshwa kila siku kwenye LUNINGA [TV] ni vyombo vya
shetani atumiavyo kuwaharibu
wanadamu….. tazama, binti
ilivyotokea kwa mtoto huyu."
Nilimwona jinsi mtoto huyu
alivyokuwa mkaidi na asiye mtii kwa wazazi wake. Wazazi
wake aliposema naye alikimbia
na
kutupatupa vitu ovyo na kuto-
watii. Baada ya hapo
akagongwa na gari na ukawa mwisho wa
maisha yake. Yesu akasema,
"Tangu hapo yupo mahali
hapa."
Nilimtazama mtoto Yule
akiteswa. Yesu akasema, "Binti, nenda na uwaambie
wazazi
wawaelekeze watoto wao
kama ilivyo katika neno
langu."(Mithali 22:6) Neno la
Mungu ni halisi, linatuambia tumwonye mtoto
kwa fimbo, lakini si kila wakati,
pale tu mtoto anapoonyesha
ukaidi
kwa wazazi. (Mithali 22:15)
Bwana akaniambia kitu cha kuhuzunisha sana na kuumiza
mno. Akasema, "Binti, wapo
watoto
wengi sana huku kwasababu
ya cartoon, kwasababu ya
ukaidi." Nikamuuliza, "Bwana, kwanini
lawama ziwe hizi cartoon?"
Naye akanieleza, "Kwasababu
ni mapepo yanayobeba ukaidi,
kiburi,
ukali na chuki kwa watoto, ili wasifanye vitu vizuri; na
mapepo mengine huwaingia
watoto ili
wasifanye mambo mazuri, bali
wafanye mabaya: vile
waonavyo kwenye LUNINGA [TV] watoto
hutaka kufanya vivyo hivyo."
Kuzimu ipo, kuzimu ni halisi,
na watoto lazima waamue
watakwenda na nani.
Nikasema, "Bwana, niambia, kwanini kuna watoto huku?" na
Yesu akanijibu,
"Mara watoto wapatapo kujua
kuna mbinguni na kuzimu,
hapo wanayonafasi ya
kuchagua." UFALME WA MBINGUNI
Kuna mengi ya kusema juu ya
kuzimu, lakini kwasasa
niwashirikishe niliyoyaona
Mbinguni. Yesu
akasema, "Binti, sasa nitakuonesha nilichowaandalia
watakatifu wangu." Tuliondoka
kule
kuzimu kupitia lango lake.
Tulipokuwa tukisafiri kutoka
nje ya kuzimu, ghafla tukatokea mahali
penye mwanga. Sikuona giza
tena, mateso wala miale ya
moto. Akasema, "Binti,
nitakuonesha
utukufu wangu," na tukaanza kupanda juu kwenda Ufalme
wa Mbinguni! Mara tukafika
kwenye
mlango wenye maandishi
makubwa yaliyoandikwa kwa
dhahabu, yalisema: "Karibu kwenye Ufalme wa Mbinguni."
LANGO LA MBINGUNI
Yesu akasema, "Binti, ingia,
kwa kuwa mimi ni Mlango na
kila aingiaye kupitia kwangu,
ataingia na kupata marisho."(Yohana 10:9)
Baada ya Bwana kusema
maneno hayo, mlango
ukafunguka na tukaingia.
Niliwaona malaika
wakimpa utukufu, heshima na sifa Baba Yetu wa Mbinguni!
(Ufunuo 7:11-12) Kadri
tulivyozidi
kutembea, tulikaribia meza
niliyoweza kuona mwanzo
wake laini siyo mwisho. (Ufunuo 19:9)
Niliona enzi kubwa, na enzi
ndogo zimezungukwa na
maelfu ya viti. Katikati ya viti
niliona mavazi
na mataji. Bwana akaniambia, "Binti, taji unayoiona pale ni
taji ya Uzima."(Ufunuo2:10)
Yesu akasema, "Tazama, Binti,
hii ndiyo niliyowaandalia watu
wangu." Niliona ile meza
imefunikwa na vitambaa vyenye upindo wa dhahabu.
Kulikuwa na sahani, glasi za
dhahabu,
matunda; kila kitu
kimeandaliwa. Ilikuwa nzuri
ajabu. Kulikuwa na chombo kikubwa katikati ya
meza, kilichokuwa na mvinyo
tayari kwa mulo. Na Yesu
akasema, "Binti, kila kitu kipo
tayari kwa
ujio wa kanisa langu." MEZA YA KARAMU YA
MBINGUNI
Tulikwenda mahali pengine,
niliwaona watu wengi wakiwa
bustanini. Kulikuwa na watu
wanaofahamika sana kwenye Biblia, lakini hawakuwa wazee,
bali vijana. Palikuwa na kijana
akiwa
na kitambaa mkononi,
akicheza na
kuzungukazunguka na kumsifu Bwana. Yesu akasema, "Binti,
Yule kijana pale ni mtumishi
wangu Daudi." Alikuwa akimpa
utukufu Baba yetu. Ghafla,
kijana
mwingine akapita na Yesu akaniambia, "Binti, huyu ni
Joshua; Yule Musa; na Yule
pale ni
Ibrahimu." Yesu huwaita kwa
majina yao. Wote walikuwa na
mwonekano mmoja! Ajabu sana
Mbinguni! Yesu akasema,
"Mwanamke Yule ni mtumishi
wangu, Maria Magdalena; na
Yule
mtumishi wangu Sara." Lakini pia akaniambia, "Binti,
huyu ni Maria. Maria,
aliyemzaa Yesu Kristo,
ambaye ni mimi.
Binti, nikwambie, yeye hana
habari ya yanayotokea duniani. Nataka kukwambia, nenda
kawaambie wanadamu,
waambie waabudu sanamu
kuwa kuzimu ni halisi, na
waabuduo
sanamu hawata urithi Ufalme wangu, lakini waambie kama
wakitubu, wataweza kuingia
makao
ya mbinguni. Nenda waambie
nawapenda na pia waambie
Maria hajui chochote [kinachotendeka duniani] na
pekee wanayeweza kuheshimu
ni mimi, kwasababu si maria
wala
mtakatifu Gregory wala
mtakatifu yeyote awezaye kuokoa. Mimi ndiye niokoaye
na nje yanguhakuna
yeyote, hakuna yeyote, hakuna
yeyote – aokoaye!" Alirudia
mara tatu-kuwa hakuna
yeyote awezaye kuokoa; isipokuwa yeye.
Wanadamu wamedanganywa
na kuamini kuwa kwa kupitia
wadhaniwao ni watakatifu,
sivyo
ilivyo, bali ni mapepo, yafanyayo kazi kupitia sanamu
zilizofanywa kwa mikono ya
watu. Lakini
ngoja nikueleze kwamba
Bwana anataka kukupa kilicho
bora. Anataka wewe uingie katika Ufalme
wa Mbinguni; tubu na kuacha
aliojaliwa na Mungu
Kwa kipindi cha masaa 23,
binti mdogo wa ki-Ecuado
aitwaye Angelica alioneshwa
falme za Mbinguni na Kuzimu, na kurudi
kwa Kristo mara ya pili.
Alishuhudia Yesu akilia kwa
huzuni
aonapo umati wa roho
zilizopotea milele, ulimwengu uliomkataa yeye, kanisa lisilo
tayari kabisa
kwa ujio wake, watu
wameacha kushuhudia kwa
walipotea mbali na kweli, na
anasa za dunia zimeteka hata watoto kwa
shetani. Alishuhudia watu
maarufu wakiteswa katika
moto, waimbaji,
wanamuziki na hata Papa.
Angelica alioneshwa jinsi ufalme wa Mbinguni
ulivyoandaliwa kwa
uzuri na utayari, utukufu
usioweza kufikirika, ambapo
hakuna uovu. Japokuwa Yesu
anakuja kwa ajili ya watakatifu tu; wengi wa
wana wa Mungu hawatakuwa
tayari kwa siku ile, na
wataachwa
nyuma katika ulimwengu
utakaogawanyika vipande vipande.
www.DivineUfunuo.info/23
(Mahojiano
kwa video, mwanzoni ni kwa
lugha ya Kihispania, huko El
Empalme, Ecuador. Sept. 29, 2009).
Maxima (Mama yake Binti):
Jina langu ni Maxima
Zambrano Mora, tunasali
kanisa la "Casa de Oracion"
huku El Empalme. Tulikuwa katika kufunga kwa
siku 15, na kulia kwa Mungu.
Binti yangu Angelica aliungana
nasi
pia. Katika kipindi hicho cha
siku 15 cha kufunga, niliweza kupata maono zaidi ya asili,
ambayo
sijawahi kuona kabla. Tulikuwa
tunaomba na kufunga katika
kipindi maalumu cha kumtafuta
Bwana, tuliendelea kuomba na kulia pale nyumbani, tukisubiri
Mungu aseme nasi.
Bwana alitutia matumaini
makubwa sana. Kwaajili ya
majaribu yetu tulikaribia
kukata tamaa, lakini Bwana alikuwa pamoja
nasi kutusaidia. Alitupa neno
la Yeremia 33:3 "Niite, nami
nitakuitikia, ame nitakuonesha
mambo makubwa, magumu
usiyoyajua." Binti yangu alitia msisitizo sana katika neno hili
kwa Bwana, japokuwa sikujua
kwa wakati huo. Angelica (Binti Mhusika):
Jina langu ni Angelica
Elizabeth Zambrano Mora.
Nina umri wa miaka 18, na
ninasoma chuo cha
"Colegio José MarÃa Velazco Ibarra",
hapa El Cantón, El Empalme,
Ecuador. Kwanza nilimpokea
Kristo nilipokuwa na umri wa
miaka
12, lakini nalijiambia mwenyewe, "Hakuna hata
mmoja wa rakifi zangu
aliyeokoka na nikajisikia
aibu miongoni mwao", kwa
hiyo nirudi nyuma mbali na
Mungu na kuishi maisha mabaya. Lakini
Mungu alinivuta nitoke huko.
Siku ya sherehe ya kutimiza
miaka 15, nirejea tena
kupatana na Bwana, lakini nia
haikutulia sawa sawa. Biblia inasema (Yakobo
1:8), "Mtu wa nia mbili husita-
sita katika nia zake zote" na
mimi
nilikuwa sawa na mtu huyu.
Baba yangu aliwahi kusema "Hutakiwi kuwa hivyo, siyo
vizuri, ni
vibaya mwanangu" lakini
nalimjibu, "Hivi ndivyo nilivyo,
nataka kuwa hivyo, hakuna
mtu wa kuniambia namna nitakiwavyo
kuwa, wala chakufanya, wala
namna ya kuvaa, au
mwenendo."
Naye alijibu, "Mungu
atakushughulikia na atakubadilisha wewe."
Siku ya sherehe ya kutimiza
miaka 17, nilimkaribia Bwana.
Tarehe 28 mwezi Aprili
nilimwendea
Bwana na kumwambia, "Bwana, nijisikia vibaya sana,
najua kuwa mimi ni mwenye
dhambi" na
nilimweleza jinsi ninavyojisikia.
"Bwana, nisamehe mimi.
Natamani uandike jina langu katika
kitabu cha Uzima na unipokee
niwe mwanao." Nilitubu na
kutoa maisha yangu kwa
Bwana rasmi.
Nikasema "Bwana, naomba unibadilishe, ufanye tofauti
ndani mwangu." Nililia kwa
moyo wangu
wote, huku nikimwomba
Bwana anibadilishe mimi.
Lakini kwa kadri ya muda ulivyozidi kupita,
sikuona madiliko yoyote.
Badiliko pekee nikuwa nilianza
kuhudhuria kanisani, kusoma
biblia na
kuomba. Hayo tu ndiyo mabadiliko katika maisha
yangu.
Ilipofika mwezi Agosti,
nilikaribishwa katika mfungo
wa siku 15. Niliamua kushiriki,
lakini kabla ya kuanza nilisema: "Bwana,
naomba unishughulikie hapa."
Katika kipindi chote cha
mfungo,
Bwana alikuwa anasema na
karibu kila mtu, kasoro mimi tu! Ilikuwa kama vile Bwana
hajaniona,
na hilo liliniumiza sana.
Nikaomba, "Bwana,
hutanishughulikia mimi?"
Nikaomba na kulia peke yangu na kusema tena,
"Bwana, je unanipenda? Je
upo hapa? Upo nami hapa?
Kwanini husemi
nami kama unavyosema na kila
mmoja hapa? Unasema mambo mengi kwa wenzangu,
hata maneno
ya unabii, lakini siyo kwangu"
Nilimwomba ishara ya kuwa yu
nami, na Bwana akanipa neno
la Yeremia 33:3, "Niite, nami
nitakuitikia, nami nitakuonesha
mambo makubwa, magumu
usiyoyajua." Nikasema,
"Bwana, je umesema nami?"
Kwasababu nilisikia sauti yake na kupata
maono ya maneno
yaliyoandikwa katika Yeremia
33:3.
Nikasema "Bwana, hiyo ni
kwaajili yangu?" Nilitunza na kukaa nalo kimya mwenyewe
wakati kila
mmoja akishuhudia
waliyopewa na Bwana na
kuoneshwa. Lakini mimi
nilitunza siri yangu na mara kwa mara nilijikumbusha na
kutafakari maneno: " Niite"
maana yake nimwombe, lakini
nini maana
ya: "mambo makubwa,
magumu" niliwaza, "Huenda ikamaanisha Mbinguni na
Kuzimu." Kwa hiyo nalimwambia "Bwana,
naomba unioneshe Mbinguni
tu, lakini siyo kuzimu,
kwasababu nimesikia kuzimu
ni sehemu ya kutisha na
mbaya sana." Lakini baadaye nikaomba kwa moyo wangu
wote, "Bwana kama ni
mapenzi yako kunionesha, na
iwe hivyo, lakini nibadilishe
kwanza. Naomba ufanye
tofauti ndani mwangu, nataka kuwa tofauti."
Tulipomaliza kufunga, kulikuwa
na majaribu na vipindi vigumu
na mara nyingine nalijisikia
kuishiwa nguvu, siwezi tena
kuendelea na Bwana. Lakini alinipa nguvu. Nilianza kusikia
sauti yake na kumjua vema
zaidi. Tukawa marakifi wazuri.
Bwana ni rafiki yetu mwema,
na Roho Mtakatifu pia. Niliwahi
mwambia, "Bwana, wewe ni rafiki yangu bora. Nataka
kukujua vema," na
nilishirikiana naye katika
mawazo yangu yote.
Nilimwomba kipindi chote cha
mwezi Agosti hadi Novemba, na mtumishi wa Bwana akaja
nyumbani kwetu na kusema,
"Bwana akubariki." Nikajibu,
"Ameni." Kisha akasema,
"Nimekuja kukuletea ujumbe
toka kwa Mungu…...Jiandae, kwasababu Bwana
atakuonesha mambo
makubwa, magumu
usiyoyajua. Atakuonesha
wewe Mbinguni na kuzimu
kama ulivyokuwa unamwomba neno la Yeremia 33:3."
Nikamwuliza, "Ndiyo, lakini
umepataje kujua?
Sijamweleza yeyote."
Akanijibu, "Mungu
unayemtumikia na kumsifu, ndiye nimsifuye, alinieleza kila
kitu."
Mara tukaanza kuomba.
Baadhi akina dada toka
kanisani kwetu na wana familia
wangu wakaungana nasi kuomba. Lakini mara
tulipoanza kuomba, nilianza
kuona Mbingu zikifunguka.
Mara nikasema "naona mbingu
zikifunguka, na malaika wawili
wanashuka kuja tulipo" Mtumishi wa Mungu akasema
"waulize kwanini wamekuja
hapa"
Walikuwa warefu na wazuri
wakupendeza; wana mbawa
nzuri. Walikuwa wakubwa na wenye kung'aa, na
walionekana wakiangaaza,
mng'ao kama wa dhahabu.
Walivaa sandozi za vito vya
thamani na walivaa mavazi
matakatifu. "Kwanini mko hapa?" Wakatabasamu na
kusema, "Tupo hapa
kwasababu tuna kazi
yakufanya….. tupo hapa
kwasababu unatakiwa
utembelee Mbinguni na kuzimu na hatutaondoka mpaka yote
yatakapo pita." Nikawajibu
"safi sana, lakini mimi
natamani kutembelea Mbinguni
tu, siyo kuzimu"
Wakatabasamu na kuendelea kuwepo na hawakusema lolote
zaidi. Baada ya kumaliza
maombi, niliendelea kuwaona
wakiwepo.
Pia nilianza kumwona Roho
Mtakatifu; ni rafiki yangu bora; ni Mtakatifu, amejaa pote na
yuko kila mahali wakati wote.
Ninamwona, anaangaza na
kung'aa sana, naona tabasamu
lake na mtazamo wake wa
upendo! Ni vigumu sana kumwelezea, kwa sababu ni
mzuri zaidi ya malaika. Malaika
wana uzuri wao lakini Roho
Mtakatifu ni zaidi sana kwa
yote. Naweza kuisikia sauti
yake, sauti ilijaa upendo na matulizo makuu. Siwezi
kuelezea kabisa sauti yake;
kama radi si radi wakati huo
huo yakuvutia. Yeye husema
"Niko pamoja nawe" Kwa hiyo
nalijitahidi kuendelea kutembea na Mungu, japo
majaribu yalizidi kutuzingira.
Tulikuwa tunapita kipindi
kigumu sana, lakini chenye
ushindi waajabu. Mie husema
"Bwana, mapenzi yako yatimizwe." Niliendelea
kuwaona malaika wale hata
nikiwa shule na pia darasani.
Nilikuwa mwenye furaha ajabu
kwa sababu niliwaona vema.
Mtumishi wa Bwana, aliyetutembelea, aliniambia
nijiandae, kwa sababu
nitakwenda kuona Mbingu na
kuzimu. Lakini pia aliniambia
kitu kigumu. Alisema
"Nitakufa." Haikuwa rahisi niliposikia neno hili. "Nitakufa namna gani? mie
mdogo sana", Nilimuuliza.
Akanijibu, "Usihofu juu ya
lolote, Kila kitu Mungu
afanyacho hakina makosa wala
mawaa, na atakurejesha duniani, ili utoe ushuhuda juu
ya Mbinguni na Kuzimu,
kwakuwa hilo ndilo Bwana
anataka sote tujue" Nikasema
"Amen, lakini nitagongwa na
gari au nitakufaje?" Mawazo yalinisonga sana, lakini Bwana
akaniambia nisihofu, kila kitu
kiko katika uwezo wake.
Nikasema, "Ahsante Bwana"
Ilipofika tarehe 6 Novemba,
baada ya kurejea nyumbani toka shule, malaika wale
walikuwa nami, hata
nilipokuwa namsifu Bwana.
Wao walikuwa hawaongei
nami; bali walidumu kusema,
"Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Hallelujah," huku
wakimpa utukufu, heshima na
sifa Baba wa Mbinguni. Roho
Mtakatifu pia alikuwa na
malaika wale huku akifurahi.
Watu wengi husema injili/ wokovu ni wa kuchosha/
kukera, lakini huo ni uongo
mkubwa toka kwa mwovu ili
kuwafanya watu wasitafute
uwepo wa Mungu. Nami pia
niliamini hivyo hapo kwanza, lakini baada ya kukutana na
Bwana na Roho Mtakatifu,
najua injili haikeri wala
kuchosha, niburudisho la ajabu
hapa duniani!
Ninaweza kumwona; kucheza na kuongea naye Roho
Mtakatifu. Lakini malaika
walikuwa hawaongei nami, ila
walikuwa wakimsifu Bwana.
Nikimwambia Roho twende
nami nakufanya hili na lile huja na kuwa nami. Ninaweza
kujihisi na kumwona vema.
Japokuwa wengi hawamwoni,
yeye yupo! Mahusiano haya
yamendelea, hata hakuna
sababu ya kuyasimamisha, hasa baada ya kuonja radha
yake na faida za Roho
Mtakatifu…… hakuna njia ya
kujitenga naye jinsi alivyo
mwema na wafaida, hasa
nikikumbuka alikonitoa, jinsi nilivyokuwa, ninamshukuru
sana kwa rehema zake na
upendo wake kwa wanadamu
na kwangu mimi!
Tarehe 7, Novemba,
nilipokuwa narudi nyumbani, nikasikia sauti ikisema
"Jiandae, kwakuwa leo
utakufa," Nilijua kuwa ni Roho
Mtakatifu kwa vile nilimwona
vema. Niliipuuza sauti yake na
kusema "Bwana, Sitaki kufa leo!" Lakini alirudia, "Jiandae,
kwakuwa leo utakufa!" Mara hii
sauti ilikuwa ya juu zaidi na
mkazo mkubwa. Nikajibu,
"Bwana, najua ni wewe
unayesema nami; nimeuliza ili kupata uhakika tu, mapenzi
yako yatendeke. Nitafanya kila
utakalo niambia, najiachia
kwako Bwana, japo naogopa,
najua upo nami, nawe ni wa
kweli." Niliomba, "Bwana, Yule mtumishi wako uliyemtumia
kunipa ujumbe mara ya
kwanza, mlete muda huu,
nimkute nyumbani, na umpe
tena neno hili aseme nami
kuwa leo ndiyo siku yangu ya kufa." Sasa mara zote Bwana
hujua ya nyuma, yaliyopo na
yajayo. Alijua kuwa
nitamwomba neno hili. Kwa
hiyo nilipofika nyumbani
nikamkuta mtumishi wa Bwana ameishafika!.
Maxima (Mama ya Binti):
Binti yangu alipofika nyumbani,
tulikuwa jikoni. Mara Angelica
alipomwona mtumishi wa
Bwana, akasema, "Bwana akubariki." Mtumishi wa Mungu
akajibu, "Bwana akubariki
nawe. Je uko tayari? Kwa
kuwa leo ndiyo siku Bwana
atakayo kuchukua, saa kumi
jioni." Angelica alisimama na kushikwa na mshangao
kwamba Bwana amejibu ombi
lake na kufanya vilevile
alivyomwomba njiani.
Angelica:
Niliposikia hayo maneno ya mtumishi, nikasema, "Ameni...
lakini sitaki kufa, sitakufa!
Hapana, Bwana, naogopa,
naogopa sana, ninahofu
kubwa!" Mtumishi wa Bwana
akasema, "Tuombe ili hofu ikutoke sasa kwa jina la
Bwana." Nikasema, "Ameni" na
tukaomba. Ghafla nikajisia
hofu yote imenitoka na furaha
isiyoelezeka ikajaa ndani
mwangu, nakuanza kuwaza kuwa kifo ni kitu chema kuliko
vyote nikitamanicho kinifike!
Nikanza kutabasamu na
kicheka wakati huo kila mmoja aliyepo akinitazama.
Wakaniona jinsi nilivyobadilika
toka unyonge na kuwa
mwenye furaha.
Nilikuwa natabasamu,
narukaruka na kuimba. Picha wakimwombea:
Maxima:
Binti yangu ghafla akawa
mwenye furaha ndani ya moyo
na kuanza kula. Alionja karibia
kila kitu kilichokuwepo, huku akisema,
"Kama sitarudi, sawa
nimeshakula na kushiba."
Angelica:
Kila mmoja akaanza kucheka
na kuuliza, "kwanini uko hivyo badala ya kuwa na huzuni,
unafuraha
na mwenye raha?" nikawajibu,
"Ndiyo ninafuraha: ninakwenda
kumwona Bwana, nitakuwa
naye, lakini sijui kama nitarudi. Kwa
hiyo nataka kugawa vitu
vyangu vyote." Wote
wakastaajabu na
kuniuliza, "Unataka kugawa
vitu vyako vyote?" macho ya mama yangu yalinitazama kwa
mshangao zaidi!
Maxima:
Binti yangu akaanza kugawa
vitu vyake. Aligawa vyote,
vyote! Ma-dada wa kanisani walikuwepo,
nao pia aliwapa baadhi ya vitu
kwa kila mmoja. Nilipomuuliza
nia yake, alisema, "Kama
nikirudi,
watanirejeshea vyote, lakini nisiporudi, watabaki navyo."
Angelica:
Niliwaza huzuni aliyokuwa
nayo mama yangu niliposema
maneno hayo. Lakini nilijisikia
furaha tupu, kwa hiyo nikaendelea
kugawa vitu: nguo, kitanda,
simu ya mkononi, kila kitu,
lakini kwa
sharti: kama nikirudi, kila kitu
kitarejeshwa kwangu. Wote wakaanza kucheka.
Maxima:
Binti yangu alikuwa na
msimamo na nia ya dhati,
lakini kama mama nilishikwa
na huzuni sana. Haikuwa jambo rahisi.
Niliwaza, "Bwana muda huo
ukiwadia, itakuwajekuwaje?"
Sikuweza
kuelewa. Na walipoanza
kuomba, nilikuwa napanga vitu ndani ya nyumba. Walisema,
"Dada njoo
tuombe." Lakini niliwajibu,
"Nyie endeleeni, nitajiunga
nanyi muda si mrefu. Ngoja
nimalizie kazi hii."
Angelica:
Wote walikuwa wananiangalia
mimi tulipokuwa tunaomba.
Niliomba, "Bwana, nataka
kufanya mapenzi yako. Wewe si
mwanadamu hata useme
uwongo au ujute, najua wewe
ni mkweli. Kama
nitakuaibisha, basi vema
unichukue moja kwa moja; lakini kama nitayafanya
mapenzi, basi
unirejeshe tena, lakini nisaidie
kusema ukweli, niandae mimi,
nisaidie kuhubiri na
kuwaambia watu kutubu." Hiyo ndiyo ilikuwa
sala yangu fupi sana.
Nilimwambia mtumishi wa
Bwana,
"Usimwambie mama yangu
maneno niliyomwomba Bwana." Naye akajibu,
"sitamwambia sasa,
lakini mara Bwana
atakapokutwa, nitamwambia."
Tuliendelea kuomba na
kuungana katika duara. Maxima:
Ilipofika saa 9:30 jioni, Bwana
akamwambia mtumishi wake
ampake mafuta binti yangu.
Kwa hiyo
baadhi yetu tulikwenda chumbani na kumpaka mafuta.
Alitupa dakika mbili tumpake
mwili mzima,
toka kichwani hadi chini, kila
mahali, mwili mzima. Akawa
mwili wote amepakwa mafuta. KIFO CHAKE
Angelica:
Mama yangu na dada mmoja,
Fátima Navarrete, walinipaka
mafuta. Kadri walivyokuwa
wananipaka, nilijisikia kama kuna kitu kinanifunika, kama
kioo kilinizunguka mimi. Ni
vigumu
kuelezea, nilijisikia kama
nimezingirwa na ngao fulani,
na nashindwa kuelezea nilivyokuwa
najisikia. Baada ya hapo kila
walipojaribu kunigusa
walishindwa!
Maxima:
Kadri tulivyokuwa tukimwombea Angelica,
nilijaribu kuweka mkono juu
yake, nilishindwa!
Alikuwa amezingirwa na kitu.
Ilikuwa ajabu, hakuna
aliyeweza kumgusa tena! Uzio huo ulianzia
kichwani hadi miguuni, karibia
sentimenta 30 (Inchi 12). Hilo
lilinitisha zaidi mimi.
Nimewawekea
mikono wengi kabla, katika huduma ya Bwana, lakini
jambo kama hili halijawahi
kutokea!
Nikasema, "Oh, kuna jambo
lazima linatendeka," na
nikaanza kuomba na kumshukuru Bwana.
Ghafla, nikasikia furaha kubwa
sana. Huzuni iliyokuwa moyoni
ikanitoka, maumivu yakakoma
na
sasa nikasikia raha na furaha ajabu! Tuliendelea kuomba na
ilipofika saa 10.00 jioni, binti
yangu
akaanguka sakafuni.
Angelica:
Wakati wa maombi, nilisikia kuishiwa pumzi; nikashindwa
kupumua. Nikasikia maumivu
tumboni
na moyoni. Nilijisiki damu
ikisimama, na ghafla maumivu
makali mwili mzima. Nililoweza kusema, "Bwana, nipe nguvu,
nipe mimi nguvu!" kwasababu
nilijisikia kushindwa kuendelea
zaidi.
Sikuwa na nguvu kabisa, zote
zilinitoka! Na nilipoangalia juu mbinguni, katika roho, si kwa
macho
ya mwilini, niliona mbingu
zikifunguka. Niliwaona
malaika, siyo wawili au kumi,
bali kwa mamilioni wakiwa pamoja
wamekusanyika. Katikati yao
niliona mwanga, mara 10,000
zaidi ya
jua. Na nikasema, "Bwana ni
wewe unayekuja!" Maxima:
Alipoanguka chini, tulijaribu
kumsimamisha, lakini
hakuweza kusimama
mwenyewe. Muda huu
tuliweza kumgusa. Alikuwa akisema, "Omba. Sina nguvu,
mama, sina nguvu na ninasikia
maumivu." Mwanzo alisikia
maumivu tumboni, na baadaye
moyoni. Tuliendelea kuomba
na kumsihi Bwana. Bwana
alichukua maisha yake!
Picha Mwili wake:
Sijawahi katika maisha yangu
kumwona mtu akifa.
Nilishuhudia binti yangu, akigugumia maumivu! Haikuwa
rahisi hata kidogo! Sikuweza
kuelewa maneno yake ya
mwisho, na mwisho alitulia.
Niliweka mikono yangu usoni
pake, na kioo mdomoni kuona kama alikuwa anapumua.
Hakuwa na pumzi tena, alitulia
kimya kabisa. Nilimshika,
alikuwa angali na joto kama
kawaida. Nilichukua shuka na
kumfunika na kwa muda mfupi akaanza kupoa na kuwa wa
baridi sana. Nywele zake
zikalala, kama za maiti na
akabadilika ubaridi wa barafu.
Angelica:
Yesu alikuwa anashuka chini, na nikajisikia mwili ukifa. Kadri
Yesu na malaika walivyozidi
kukaribia, nikajisikia kuondoka,
na sikuwa mimi tena. Sikuwa
hai tena, nilikuwa nakufa na
kugugumia maumivu! Wakati mwili wangu ulipoanguka chini,
walikuwa tayari wamefika.
Nyumba yetu ilijaa malaika, na
katikati yao niliona mwanga
mkali kuliko wa jua! Ilikuwa
vigumu; nilisikia maumivu makali wakati roho yangu
ilipotenganishwa na mwili.
Nilikuwa nalia na kupiga
kelele, kadri nilivyoona mwili
wangu sakafuni. Nilimuuliza,
"Bwana, nini kinachotokea? Nini kinachotokea?" Nilijaribu
kuugusa mwili wangu na
kuurudia tena, lakini
nilipojaribu, ilikuwa kama
kushika hewa: sikuweza
kuugusa, mkono wangu ulipitiliza. Hakuna kati ya
waliokuwa wananiombea
aliyenisikia! Na nikapiga
kelele, "Bwana, nisaidie mimi!"
Maxima:
Mume wangu alifika tulipokuwa tunaomba, na alimkuta pale.
Bwana alinipa nguvu kwa
kuwa sikujua la kufanya.
Ilikuwa kama vile yuko
mahututi (kwenye coma), lakini
nilijua yuko salama, kwasababu ilikuwa ni kazi ya
Bwana. Kwahiyo nikasema
"Bwana, mapenzi yako
yafanyike."
BWANA YESU KRISTO
Angelica: Wakati huo nasikia sauti ya
Bwana, sauti nzuri kama radi
lakini ya UPENDO, "Usiogope,
Binti, kwa kuwa mimi ni
Yehova, Mungu wako, na
nimekuja hapa kukuonesha niliyokuahidi wewe. Inuka, kwa
kuwa mimi ni Yehova,
ninayekushika mkono wako wa
kuume na kukuambia,
usiogope, nitakusaidia wewe."
Ghafla, nikasimama. Nilikuwa nimepiga magoti chini,
ninauangalia mwili wangu,
nikitaka kuurejea bila
mafanikio. Niliposikia sauti
yake, woga ukanitoka, na
sikuwa na hofu tena. Nilipoanza kutembea, malaika
wakaanza kufungua njia.
Kulikuwa na mwanga mkali
ung'aao, na nilipouangalia
nilisikia amani ya ajabu. Kadri
nilivyoangalia, nilimwona mwanaume mzuri, mrefu,
aliyevaa vizuri na kuvutia sana
kumwangalia, mwenye siha
njema. Mwanga ulitoka kwake.
Kulikuwa na mwanga mkali
kiasi cha kushindwa kumwangalia uso wake! Lakini
niliweza kuona nywele zake za
dhahabu ing'aayo na vazi
jeupe na mshipi kifuani pake.
Ukisomeka, "MFALME WA
WAFALME NA BWANA WA MABWANA."
Nilimwangalia miguuni pake,
alikuwa amevaa sandozi zenye
mng'ao wa dhahabu, dhahabu
safi. Alikuwa mzuri sana!
Akaninyooshea mkono wake. Nilipomshika mkono wake,
haikuwa kama nilipojaribu
kuugusa mwili wangu, mkono
haukupitiliza. Nikauliza, "Nini
kinachotokea?" naye akasema,
"Nitakuonesha wewe kuzimu ili ukirudi uwaambie wanadamu
kuwa kuzimu ni halisi; kuwa ni
kweli ipo. Na pia utukufu
wangu nitakuonesha wewe, ili
uwaambie watu wangu
wajiaandae, kwa kuwa utukufu wangu ni halisi na mimi pia."
Akasema, "Binti, usiogope"
akarudia kusema tena na mimi
nikasema, "Bwana, nataka tu
kwenda Mbinguni, lakini siyo
kuzimu, kwasababu nimesikia kunatisha!" Akasema, "Binti,
nitakuwa nawe. Sitakuacha
huko na nitakuonesha huko
mahali kwasababu wengi
wanajua kuzimu ipo lakini
hawaiogopi. Wanaamini ni mchezo, na
kuzimu ni mzaha, na wengi
hawajui lolote juu yake. Ndiyo
maana
nitakuonesha wewe huko kwa
sababu wanaopotea ni wengi kuliko wanaoingia katika
utukufu
wangu." Aliposema hayo,
niliona machozi yakitiririka
kwenye vazi lake.
Nikamwuuliza, "Bwana, kwanini unalia?" Akanijibu,
"Binti, kwasababu wengi
wanaangamia, na
nitakuonesha hii, ili
uende na uwaambie ukweli na
wewe usirudie hapo." KUZIMU
Ghafla, alivyokuwa anaongea,
kila kitu kikaanza kutembea.
Ardhi ilitikisika na kupasuka,
na
nikaona shimo jeusi tii chini. Shimo:
Tulikuwa tumesimama kama
kwenye mwamba na malaika
wakituzunguka. Nikasema,
"Bwana,
sitaki kwenda mahali huko!" akasema, "Binti, usiogope niko
pamoja nawe." Kwa sekunde
chache
tukashuka kwenye shimo jeusi.
Nilijaribu kuangalia lakini
kulikuwa na kiza kikuu. Niliona duara
kubwa, na kusikia mamilioni ya
sauti.
Nilipata moto. Nikajisikia ngozi
yangu kuungua. Nikamuuliza,
"Bwana, hiki ni nini? sitaki kwenda mahali huko!" Bwana
akasema hilo ni lango tu la
kwenda kuzimu. Kulikuwa kuna
harufu
mbaya, yakutisha,
isiyovumilika, na nikamsihi Yesu asinipeleke mimi. Naye
akajibu, "Binti, ni
muhimu ufike na kujua sehemu
hii." Nikalia, "Lakini kwanini,
Bwana, kwanini?" naye
akasema, "Ili ukawaambie ukweli
wanadamu; wanadamu
wanaangamia, wanapotea na
wachache sana
wanaoingia ufalme
wangu." (Mat.7:14) Akishasema hivi, hulia sana.
Maneno yake yalinitia nguvu
na kunihimiza, kwa hiyo
nikaendelea kutembea.
Ziwa la Moto:
Tulifika mwisho wa tanuru/ lango, nilipoangalia chini
niliona umati umefunikwa na
miali ya moto. Bwana akasema
"Binti, nakupa hii." Ilikuwa ni
faili kubwa lenye karatasi
ambazo hazijaandikwa chochote. "Binti, chukua na
kalamu hii ili uweze kuandika
yote nitakayokuonesha,
utakayoyaona na kusikia.
Utaandika kila kitu ukionacho
na utaishi nayo." Nikasema, "Bwana, nitafanya, lakini
nimeshaanza kuona mengi
mno, Bwana. Ninaona roho
zikiteswa, na kuzamishwa
kwenye moto."
Maxima: Muda uliendelea kupita, na
binti yangu alikuwa bado
kalala pale. "Bwana, nini
kinachotokea?" Machozi
yalikuwa yakimtoka kwenye
macho, lakini kila nilipomfuta, yalitoka tena. Nikaweka kioo
mdomoni pake kuona kama
anapumua, hakukuwa na
pumzi. Tuliangalia mapigo ya
damu, wapi, hakuna kitu!.
Tuliweka mikono tumboni pake, wapi! Hakuna kitu.
Mtumishi wa Bwana akasema,
"mahali alipo sasa, siyo mahali
pa kutabasamu bali mahali pa
mateso."
Angelica: Nikamwambia Yesu,
Nitashuhudia kuwa kuzimu ni
halisi, kwamba ipo, lakini nitoe
hapa sasa!" na akanijibu,
"Binti, hatuja ingia bado mahali
penyewe, na sijakuonesha chochote, tayari unataka
nikutoe huku?" nikasema
"Bwana, tafadhari nitoe mahali
hapa," tukaendelea kushuka
kwenye korongo/shimo
lakutisha! Nikaanza kulia na kupiga yowee, "Bwana,
hapana, hapana, hapana,
hapana……… Sitaki kwenda!"
naye hujibu, "Unatakiwa kuona
haya."
Niliona mapepo yakutisha, ya kila aina, makubwa na
madogo. Yalikuwa yanakimbia
sana, na yameshika vitu
mkononi. "Bwana, kwanini
yanakimbia hivyo na
yameshika nini?" akanijibu, "Binti, wanakimbia hivyo
kwasababu wajua muda wao
karibu kwisha, kwasababu
muda wa kuwaharibu/
kuwapoteza wanadamu,
hususani watu wangu. Na walivyoshika mkononi ni
mishale ya kuwaharibu
wanadamu, kwasababu kila
pepo amepewa jina na kwa
kadri ya jina lake, ana mishale
ya kumharibu mtu na kumleta huku kuzimu; malengo yao ni
kumharibu mtu na kumleta
kuzimu." Na niliendelea kuona
mapepo yakikimbia na kutoka
kuelekea duniani na Bwana
akaniambia; "Wanakwenda duniani ili kuleta na kuwatupa
wanadamu huku." Alipokuwa
akisema hivyo, Bwana hulia,
hulia sana. Kila alipolia nami
nililia pia.
Maxima: Binti yangu alikuwa amekufa
kwa masaa 23, lakini sikutoa
taarifa kwenye mamlaka
yoyote. Niliomba, "Bwana,
nitasubiri kwa masaa 24.
Kama binti yangu hatarudi ndani ya saa 24, nitampigia
simu Daktari." Lakini, Bwana
alimrejesha kabla ya saa 24
hazijatimia.
Angelica:
Bwana akaniambia, "je uko tayari kuona
nitakachokuonesha wewe?"
Nikasema, "Ndiyo Bwana,".
Alinipeleka kwenye sero moja,
ambapo nilimwona kijana
akiwa matesoni katikati ya miali ya moto. Nikajulishwa
namba sero yake, japokuwa
sikuweza kujua ile namba,
ilionekana kama imeandikwa
kinyume hivi. Palikuwa na
nembo kubwa mle ndani, na kijana alikuwa na namba 666
kwenye kipaji cha uso. Pia
alikuwa na aina ya kipande
cha chuma imebandikwa
kwenye ngozi yake. Funza
walikuwa wanamtafuna, haikuweza kuharibu kipande
kile; wala moto haukuweza
kukiunguza. Akapiga kelele,
"Bwana, nirehemu mimi. Nitoe
mahali hapa. Nisamehe mimi
Bwana!" lakini Yesu alimjibu, "umechelewa, umechelewa
sana: nilikupa fursa lakini
hutaka kutubu." Nikamuuliza
Yesu, "Bwana, kwanini huyu
yuko hapa?" mara
nikajulishwa. Akiwa duniani, kijana huyu
alijua neno la Mungu, lakini
ghafla akajitenga na Bwana na
kuchagua
pombe, madawa ya kulevya na
kupita katika njia zisizofaa. Hakutaka kufuata njia ya
Bwana. Yesu
alimwonya mara nyingi juu la
litakalompata. Yesu akasema,
"Binti, yuko hapa kwasababu
kila anayeyakataa maneno yangu,
anaye amhukumuye: lile neno
nilisema naye litamhukumu
siku
ya mwisho," (Yohana 12:48) na
Yesu akalia tena. Bwana akilia, nitofauti nasi
tuliavyo na zaidi yetu. Yeye
hulia na maumivu makali
moyoni na
uchungu usioelezeka. Bwana
akasema, "Sikutengeneza kuzimu kwaajili ya wanadamu,"
Nikamuuliza, "Sasa Bwana
kwanini wanadamu wapo
huku," Akanijibu, "Binti,
niliumba kwajili
ya shetani na malaika zake, ambayo ni mapepo;(Mat.
25:41) lakini, kwasababu ya
dhambi na
kukosekana kwa toba,
wanadamu huishia hapa, na
wengi wangamiao kuliko wanaofika katika
utukufu wangu!" Akaendelea
kulia na huniumiza sana
nimwonapo akilia. "Binti,
nalitoa maisha
kwaajili ya wanadamu, ili wasiangamie, ili wasiishie
hapa [Kuzimu]. Nalitoa maisha
yangu kwa
upendo na huruma, ili
wanadamu waendee toba na
kuingia katika ufalme wa Mbinguni." Yesu
kwa huzuni huugua kiasi cha
kushindwa kustahimili
maumivu, kadri aonavyo watu
pale kuzimu.
Kwa kuwa na Yesu, kulinifanya nijisikie salama. Niliwaza,
"kama nikimwacha Bwana
aende,
ninge-nasa kuzimu pale"
Nikamuuliza, "Yesu, je nina
ndugu yangu mahali hapa?" Akanitazama
kwa jinsi nilivyokuwa nalia na
akasema, "Binti, niko nawe,"
Kwasababu nilikuwa mwenye
hofu
sana. Akanipeleke kwenye sero nyingine. Sikuwahi
kuwaza kumwona ndugu yangu
kwenye sero
ile. Nilimwona mwanamke
akiteswa, alikuwa na funza
wakimla uso wake, na mapepo yakimchoma
mikuki mwilini. Naye hupiga
kelele, "Hapana, Bwana,
nihurumie, nisamehe mimi,
tafadhari, nitoe
mahali hapa kwa dakika moja!" (Luka 16:24)
Kuzimu, watu huteswa na
kumbukumbu za waliyoyafanya
duniani. Mapepo hudhihaki
watu na
kuwaambia, "abudu na kusifu kwasababu huu ndiyo ufalme
wenu!" na watu hupiga kelele
11
wakikumbuka kuwa walimjua
Mungu, kwasababu walijua
neno. Walimjua Bwana waliteswa mara
dufu ya wengine.
Bwana akasema, "Hakuna tena
nafasi kwa walioko pale
[kuzimu]; kungali na nafasi
kwa walio hai." Nikamuuliza, "Bwana,
kwanini bibi yangu mkubwa
yupo pale? Sijui kama alikujua
wewe.
Kwanini yupo kuzimu Bwana?"
akanijibu, "Binti, yupo hapa kwasababu alishindwa
kusamehe….. binti, yeyote
asiyesamehe, sitamsamehe
huyu."
Nikamuuliza, "Bwana, lakini
wewe husamehe, na una rehema." Naye akanijibu,
"Ndiyo, binti,
lakini nilazima kusamehe,
kwasababu hawajawasamehe
wengi, na ndiyo maana wengi
wapo hapa, wameshindwa
kusamehe…… nenda
kawaambia wanadamu ni
muda wa kusamehe, hasa
hasa watu wangu, kwakuwa
wengi miongoni mwa watu wangu hawajasamehe.
Waambie
waache malaaumu, mafundo,
chuki mioyoni mwao, kwa
kuwa ni muda wa kusamehe!
Kama kifo kikimsitukiza mtu
aliyeshindwa kusamehe, huyo
mtu atakwenda kuzimu,
kwakuwa hakuna
awezaye kununua maisha."
Tulipoondoka hapo, bibi yangu mkubwa alifunikwa na moto na
akapiga makelele, "Aaaah," na
akaanza kutukana jina la
Mungu, na kumlaani Bwana;
kila mtu
kuzimu humtukana Mungu. Tulipoondoka eneo lile,
nikaona kuwa kuzimu imejaa
roho ziteswazo. Watu wengi
huinua mikono
nje, wakimwomba Yesu
msaada wa kuwatoa nje. Lakini Bwana hakuwa na lolote
la kufanya kwao,
nao huanza kumtukana Mungu.
Mara Yesu hulia sana na
kusema, "Inaniumiza sana
kuwasikia, inaniumiza mimi sana
wanavyofanya, kwasababu
siwezi kufanya lolote kwaajili
yao. Ninacho
kueleza ni hiki; nina nafasi kwa
hao walioko duniani, ambao hawaajafa, walio hai, wanao
muda
wa kutubu!"
Bwana akaniambia kuna watu
wengi maaruku huku kuzimu,
na pia wengi waliomjua Bwana.
Akasema, "Nitakuonesha
upande mwingine wa tanuru."
Tukaenda mahali penye
mwanamke
aliyezingirwa na miali ya moto. Alikuwa katika maumivu
makubwa na kupiga makelele,
akiomba
huruma kwa Bwana. Yesu
akanyoosha mkono kwake na
akaniambia, "Binti, Yule mwanamke
umwonaye pale, amezingirwa
na miali ya moto ni Selena."
Kadri tulivyokuwa
tunamkaribia,
akapiga kelele, "Bwana, nihurumie mimi, nisamehe
mimi Bwana, nitoe mahali
hapa!" lakini
Bwana akamtazama na
kusema, "Umechelewa,
umechelewa sana, huwezi kutubu sasa."
Selena
Aliponiona mimi akasema,
"Tafadhari, nakuomba wewe,
waambie watu hivi, tafadhari
sema na usinyamaze; nenda waambie
wasije mahali hapa; nenda
waambie wasisikilize nyimbo
zangu, wala
wasiimbe hizo nyimbo."(1
Yohana 2:15) Nikamuuliza, "kwanini unataka mimi
niwaambie hivyo?"
naye akanijibu, "Kwasababu
kila wakati watu wanaposikiliza
nyimbo zangu, nateswa zaidi
na zaidi, na mtu anayeimba na
kusikiliza nyimbo zangu,
anaelekea mahali hapa.
Tafadhari, nenda
uwaambie wasije huku; nenda
waambie kuzimu ni halisi, ipo kweli!". Akapiga kelele na
mapepo
humchoma mikuki na Selena
kulia, "Nisaidie mimi,
nihurumie mimi Bwana!" lakini
kwa huzuni Bwana alimwambia,
"umechelewa sana."
Nikaangalia pande zote za
eneo lile, lilikuwa limejaa
waimbaji na wasanii waliokufa.
Walikuwa wakiimba na kuimba, bila
kusimama. Bwana
akanifafanulia, "Binti, mtu
aliyepo hapa, lazima
aendelee kufanya kile
alichokuwa anafanya duniani, kama hajatubu."
Kadri nilivyokuwa naangalia
eneo lile, niliona mapepo
mengi yakinyunyiza vitu kama
mvua.
Nilidhani ni mvua inanyesha. Lakini niliona watu kwenye
miali ya moto wakikimbia mbali
na ile
mvua na kupiga yowee,
"Hapana, nisaidie, Bwana!.....
Hapana, haiwezekani kuwa hivyo," na
mapepo yalikuwa yanacheka
na kuwaambia watu, "Sifu na
kuabudu kwasababu hapa ni
ufalme
wenu milele na milele!" Niliona miali ya moto ikiongezeka na
funza za watu zikiongezeka
zaidi!
Hayakuwa maji yale bali
kiberiti cha kuongeza miali ya
moto na kuongea maumivu ya kila mtu.
Nikamuuliza Yesu, "Ni nini
kinachotokea?..... Bwana, ni
nini hiki?" Bwana akanijibu,
"Huu ni
ujira wa yeyote asiyetubu." (Zaburi 11:6).
Bwana akanipeleka mahali
alipo mtu aliyejulikana sana.
Kabla ya maono haya, nilishi
maisha kama
msichana wa kikristo wa nia mbili. Nilidhani kila mtu
anayekufa anakwenda
Mbinguni; wale
walifanyiwa ibada za mazishi
watakwenda mbinguni, kumbe
sikuwa sahihi, nilikosa. Alipofariki
Papa John Paul II, marafiki
zangu na ndugu walisema
amekwenda mbinguni. Taarifa
zote kwenye
LUNINGA [TV], na vyombo mbalimbali vya habari vilisema,
"Papa John Paul II amefariki,
apumzike kwa amani.
Anafurahia sasa kuwa na
Bwana na malaika Mbinguni"
na mimi niliamini yote kuwa ndivyo. Lakini
kumbe nilikuwa najidanganya
mwenyewe, kwasababu
nimemwona
kuzimu, akiteswa kwa miali ya
moto. Nilimtazama uso wake, alikuwa mwenyewe Papa John
Paul
II! Bwana akaniambia,
"Angalia, Binti, Yule
mwanaume umwonaye pale, ni
Papa John Paul II. Yuko hapa; akiteswa
kwasababu hakutubu."
Papa John Paul II
Lakini nikamuuliza, "Bwana,
kwanini yuko hapa? Alikuwa
akihubiri kanisani." Yesu akanijibu,
"Binti, hakuna mwasherati,
wala muabudu sanamu,
hakuna mchoyo na hakuna
mwongo
atakayerithi ufalme wangu." (Eph 5:5) Nikamjibu,
"Ndiyo, najua ni kweli, lakini
nataka kujua
kwanini yuko hapa, kwasababu
alikuwa akiwahubiria umati wa
watu!" Na Yesu akanijibu, "Ndiyo,
Binti, alisema mengi, lakini
hakusema kweli kama ilivyo.
Hakusema kweli na kweli
aliijua na
japokuwa aliijua kweli, alipenda fedha zaidi ya
kuhubiri habari za wokovu.
Hakutoa uhalisia;
hakusema kuzimu ni halisi na
mbinguni kupo; Binti, sasa
yuko mahali hapa." Nilipomwangalia mtu huyu,
alikuwa na joka kubwa lenye
sindano nyingi mwilini mwake,
limemzingira shingoni, naye
hujaribu kumtoa. Nalimwomba
Yesu, "Bwana, msaidie!" Mwanaume hupiga kelele,
"Nisaidie mimi, Bwana
nihurumie; nitoe mahali hapa;
nisamehe mimi! Ninatubu
Bwana; Nataka nirudi duniani,
nataka nirudi duniani nikatubu." Bwana alimtazama
na kumwambia, "Ulijua vizuri
yote haya. Ulijua vema kuwa
kuzimu ni halisi, ipo……..
umechelewa; hakuna tena
nafasi kwaajili yako." Bwana akasema, "Tazama
Binti, nitakonesha maisha ya
mtu huyu." Yesu akanionesha
kioo kikubwa kama LUNINGA
[TV]; nikaona alivyotoa misa
mara nyingi kwa umati wa watu. Na watu wale
walivyokuwa waabudu
sanamu. Yesu akasema,
"Tazama, Binti, wapo waabudu
sanamu wengi hapa [Kuzimu].
Ibada ya sanamu haiwezi kuokoa Binti. Ni mimi pekee
niwezaye kuokoa, na nje
yangu hakuna mwingine
aokoaye. Nawapenda wenye
dhambi, lakini nachukia
dhambi Binti. Nenda na uwaambie wanadamu kuwa
nawapenda na ninataka waje
kwangu."
Kadri Bwana alivyokuwa
akisema, nilianza kuona mtu
huyu akipokea makusanyo makubwa ya sarafu na fedha;
vyote alivihifadhi. Alikuwa na
fedha nyingi sana. Naliona
sura yake imeketi katika
mamlaka yake, lakini pia
naliweza kuona zaidi. Japo ni kweli watu hawa hawaoi,
ninakuhakikishia wewe,
sizushi, Bwana alinionesha
mimi, wanalala na masista; na
wanawake wengi!
Bwana akanionesha watu hawa wanaishi kwa uasherati,
na neno linasema hakuna
mwasherati atakayerithi ufalme
wake. Kadri nilivyokuwa
naona, Bwana akaniambia,
"Tazama, Binti, yote ninayokuonesha, ndiyo
yanayoendelea, ndivyo
alivyoishi [Papa] na ndivyo
yanayotokea katikati ya watu
wengi, katikati ya mapadre na
mapapa waliopo." Kisha Bwana akasema, "Binti, nenda
na uwaambie wanadamu ni
muda wa kugeukia."
Bwana akanionesha sehemu
watu wengi wanavyoelekea
kuzimu. Nikamuuliza, "Bwana, namna gani wanakuja huku?"
akanijibu, "Nitakuonesha."
Akanionesha lango lenye watu
wengi wakipita. Watu hawa
walikuwa wamefungwa toka
mikononi hadi miguuni. Walivaa mavazi meusi na
kubeba mizigo mgongoni
mwao. Yesu akasema, "Binti,
hao watu uwaonao hawanijui
mimi bado. Mizigo waliyobeba
ni dhambi, lakini nenda waambie walete mizigo
kwangu, nami nitawapumzisha;
kwa kuwa mie ndiye mwenye
kusamehe dhambi zao zote….
Binti, nenda na uwaambie
waje kwangu, kwani nawasubiri na mikono yangu
iko wazi kuwapokea, na
uwaambie hapo wanaelekea
mahali hapa [kuzimu]."
Kadri nilivyokuwa nawatazama
watu wakitembea, nikamwambia, "Bwana, Yule
mtu pale ni binamu yangu; na
Yule kijana pia, Bwana, na
Yule binti pale anayelekea
kuzimu; oh familia yangu
inakuja huku kuzimu!" Bwana akajibu, "Binti, wanakuja huku,
lakini nenda uwaeleze
wanakoelekea, nenda waeleze
kuwa wanakwenda kuzimu.
Nenda waeleze kuwa
nimekuchagua wewe uwe mlinzi wangu……
nimekuchagua wewe kama
mlinzi, hii inamaanisha kuwa
unatakiwa uwaambie ukweli.
Unatakiwa uende uwaeleze
yote niliyokuonesha wewe. Kama hutawaambia na jambo
likampata mtu huyu, damu
yake itakuwa juu yako, lakini
ukiende na kufanya
nilivyokueleza, hapo mtu huyu
nitamdai mwenyewe. Kama mtu hatatubu, hapo wajibu
ulionao utaondolewa, kwa
kuwa atadaiwa mwenyewe na
damu yake haitakuwa juu
yako. (Ezekia 3:18)"
Yesu akaniambia wengi wa watu maarufu wanaelekea
huku [kuzimu], maarufu na
watu muhimu. Kwa mfano,
Michael Jackson. Huyu alikuwa
maarufu duaniani kote lakini
alikuwa mjumbe wa shetani. Japokuwa wengi
wanaweza wasione na
kuelewa hivyo, lakini huo ndiyo
ukweli. Huyu
alikuwa na mkataba na
shetani: alikubaliana na shetani ili awe na heshima na
sifa ilikuwa vutia
wapenzi wengi.
Michael_Jackson
Hizo hatua na mitindo
aliyokuwa anafanya, ndivyo nilivyoona mimi mapepo
yakicheza na
kutembea yanapotesa watu
kuzimu. Yalikuwa yanateleza
kwa kurudi nyuma na siyo
mbele, huku yakipiga kelele; yakifurahia
mateso wanayopata watu.
Ngoja nikuambia wewe kuwa
Michael
Jackson yuko kuzimu. Bwana
alinionesha baada ya kufa Michael. Alinionesha Michael
Jackson
akiteswa kwenye miali ya
moto. Nikalia kwa Yesu,
"Kwanini?" haikuwa rahisi
kuona mtu huyu alivyokuwa anateswa na
alivyokuwa analia na kupiga
mayowe. Yeyote anayesikiliza
nyimbo za
Michael Jackson au kuziimba
au ni mpenzi/shabiki wa Michael Jackson, ninakuonya
kuwa shetani
anakutega katika mtego wake
ili mwisho uishie kuzimu. Mara
hii, jitoe na kumkana shetani
kwa jina Yesu! Yesu anataka
kukuweka huru wewe, ili
usipotee milele. Bwana
akaniambia, "Binti,
kuna watu wanijuao pia
wanakuja huku." Nikamuuliza, "Bwana, inakuwa je mtu
akujue harafu
aje huku?" akanijibu, "Mtu Yule
aliyeacha njia zangu na mtu
Yule anayeishi aina mbili za
maisha [wokovu na dhambi]." Akaanza kunionesha watu
wanaoelekea kuzimu.
Walikuwa
wamefungwa kamba toka
mikononi hadi miguuni. Kila
mmoja alivaa vazi jeupe, lakini limetobokatoboka, lina-
mabakamabaka na
limekunjamana. Yesu
akaniambia, "Binti, angalia
watu
walioniacha mimi. Binti, nataka kukueleza, siji duniani kwaajili
ya watu hawa. Nakuja kwaajili
ya watakatifu, waliotayari,
wasiolaumiwa, wasio na
makunyanzi na wasio na
mawaa…… nenda uwaambie warejee kwenye
njia zao za zamani," (Efeso
5:26-27) Nilianza kuwaona
wengi
miongoni mwa wajomba zangu
na watu wengine wengi waliorudi nyuma na kuziacha
njia za
Bwana. "Nenda kawaambie
ninawasubiri, walete mizigo
yao nami nitawapumzisha."
YESU alikuwa analia baada ya
kusema hayo, "Binti, wanakuja
huku [kuzimu]. Nenda
kawaambie
wajomba zako; nenda
kawambie ndugu zako kuwa wakuja huku! Binti, wengi
hawatakuamini,
lakini mimi ni shahidi wako
mwaminifu, ni shahidi wako
mwaminifu. Sitakuacha wewe.
Hata kama hawataamini, Binti,
nenda na uwaambie ukweli
huu, kwa kuwa nipo nawe. Pia
Binti
nitakuonesha jinsi watu
wanavyofika huku." Tulikwenda kwenye lango,
ambapo tuliona umati wa watu
wakiangukia ndani ya shimo
kubwa.
Siyo elfu moja wala elfu mbili,
bali wingi wake kama mchanga wa bahari, hawana idadi!
Walikuwa wananguka kwa kila
sekunde, mfano wa mkono
uliojaa mchanga umwakikapo
chini.
Zile roho zilikuwa zinaanguka kwa kasi. YESU alikuwa akilia,
na kusema, "Binti hivi ndivyo
wanadamu wanavyopotea; hivi
ndiyo mwanadamu
apoteavyo!!!..... Binti,
inaniumiza sana mimi nionavyo wanadamu
wanavyoangamia."
YESU akasema, "maapepo pia
hufanya mikutano huku." Na
nikasema, "mapepo yanafanya
mikutano?" Yesu akasema, "Ndiyo, Binti, wanakutana
kupanga, kupanga
watavyowafanya
wanadamu. Wanakutana kila
siku kwa siri." Na kwa hilo,
Yesu akanipeleka kwenye sero,
ambapo niliona meza ya mbao
na viti vikizunguka meza. Na
palikuwa na mapepo, aina zote
za
mapepo. Yesu akaelezea, "Binti, wanapanga kwenda
kuharibu nyumba/familia za
wachungaji,
wamisionari, wainjilisti na wote
wanijuao mimi. Binti wanataka
kuwaharibu; wanamishale mingi."
Mapepo hucheka na kudhihaki,
na kusema, "acha tuwaharibu
wanadamu na kuwaleta huku."
Yesu
akasema, "Nenda na uwaambie nipo pamoja nao
watu wangu. Waambie
wasiache milango wazi,
wasimpe nafasi shetani, kwa
kuwa shetani anazunguka-
zunguka kama simba angurumaye,
akimtafuta wa kummeza. (1
Petro 5:8)" Lakini neno
linasema, "anatembea kama",
kwasababu
simba halisi, ni Simba wa Yuda, Yesu Kristo wa Nazareti
(Ufunuo 5:5)! Yesu akasema,
"Binti,
wanataka kuharibu/
kuangamiza familia za
wachungaji." Nikamuuliza, "Kwanini wanataka
kuharibu familia za
wachungaji?" na Yesu akajibu,
"Kwasababu wanawajibu wa
maelfu ya watu
ambao ni kondoo wa kundi; kondoo wa kundi Bwana
aliowakabidhi wao. Wanataka
watu hao
warudie dunia tena; waangalie
nyuma na kuishia kuzimu….
Nenda kawaambie wachungaji kusema iliyo kweli tupu.
Waeleze wahubiri kweli tupu
na kusema kila kitu
ninachowaambia na
wasinyamaze nayo haya
ninayowaambia!" Tulipokuwa tunaondoka hapo,
akaniambia, "Nataka
nikuoneshe kitu kingine….
Wapo pia watoto
huku." Na nikamjibu, "watoto
huku Bwana? Kwanini wawepo watoto huku? Neno lako
lasema,
'Waacheni watoto wadogo
waje kwangu, na msiwazuie:
kwa maana Ufalme wa
Mbinguni ni wao." (Mathayo 19:14) Yesu akajibu,
"Binti, ni kweli, ufalme wa
mbinguni ni wao, lakini mtoto
lazima
aje kwangu, kwa kuwa kila
ajaye kwangu sitamtupa kamwe." (Yohana 6:37)
Ghafla, Bwana
akanionesha mvulana wa
miaka nane akiteswa kwenye
moto. Mvulana akalia, "Bwana
nihurumie mimi, nitoe mahali hapa, sitaki
kuwepo hapa!" aliendelea
kupiga kulia na kelele. Nikaona
mapepo
yamemzunguka mtoto huyu,
yaliyofanana na cartoon. Kulikuwa na aina za Dragon,
BoyZ, Ben 10,
Pokémon, Doral, na nyingine
nyingi. "Bwana, kwanini mtoto
huyu yuko huku?" Yesu
akanionesha picha ya mkanda wa maisha
mtoto huyu. Nilimwona
anavyotumia muda karibia
wote kwenye
LUNINGA [TV] akiangalia
cartoon. Cartoon ya Ben 10: Pokemon:
Yesu akasema, "Binti, hayo
maigizo ya cartoon, sinema
zake, michezo mbalimbali ya
kuigiza
inayooneshwa kila siku kwenye LUNINGA [TV] ni vyombo vya
shetani atumiavyo kuwaharibu
wanadamu….. tazama, binti
ilivyotokea kwa mtoto huyu."
Nilimwona jinsi mtoto huyu
alivyokuwa mkaidi na asiye mtii kwa wazazi wake. Wazazi
wake aliposema naye alikimbia
na
kutupatupa vitu ovyo na kuto-
watii. Baada ya hapo
akagongwa na gari na ukawa mwisho wa
maisha yake. Yesu akasema,
"Tangu hapo yupo mahali
hapa."
Nilimtazama mtoto Yule
akiteswa. Yesu akasema, "Binti, nenda na uwaambie
wazazi
wawaelekeze watoto wao
kama ilivyo katika neno
langu."(Mithali 22:6) Neno la
Mungu ni halisi, linatuambia tumwonye mtoto
kwa fimbo, lakini si kila wakati,
pale tu mtoto anapoonyesha
ukaidi
kwa wazazi. (Mithali 22:15)
Bwana akaniambia kitu cha kuhuzunisha sana na kuumiza
mno. Akasema, "Binti, wapo
watoto
wengi sana huku kwasababu
ya cartoon, kwasababu ya
ukaidi." Nikamuuliza, "Bwana, kwanini
lawama ziwe hizi cartoon?"
Naye akanieleza, "Kwasababu
ni mapepo yanayobeba ukaidi,
kiburi,
ukali na chuki kwa watoto, ili wasifanye vitu vizuri; na
mapepo mengine huwaingia
watoto ili
wasifanye mambo mazuri, bali
wafanye mabaya: vile
waonavyo kwenye LUNINGA [TV] watoto
hutaka kufanya vivyo hivyo."
Kuzimu ipo, kuzimu ni halisi,
na watoto lazima waamue
watakwenda na nani.
Nikasema, "Bwana, niambia, kwanini kuna watoto huku?" na
Yesu akanijibu,
"Mara watoto wapatapo kujua
kuna mbinguni na kuzimu,
hapo wanayonafasi ya
kuchagua." UFALME WA MBINGUNI
Kuna mengi ya kusema juu ya
kuzimu, lakini kwasasa
niwashirikishe niliyoyaona
Mbinguni. Yesu
akasema, "Binti, sasa nitakuonesha nilichowaandalia
watakatifu wangu." Tuliondoka
kule
kuzimu kupitia lango lake.
Tulipokuwa tukisafiri kutoka
nje ya kuzimu, ghafla tukatokea mahali
penye mwanga. Sikuona giza
tena, mateso wala miale ya
moto. Akasema, "Binti,
nitakuonesha
utukufu wangu," na tukaanza kupanda juu kwenda Ufalme
wa Mbinguni! Mara tukafika
kwenye
mlango wenye maandishi
makubwa yaliyoandikwa kwa
dhahabu, yalisema: "Karibu kwenye Ufalme wa Mbinguni."
LANGO LA MBINGUNI
Yesu akasema, "Binti, ingia,
kwa kuwa mimi ni Mlango na
kila aingiaye kupitia kwangu,
ataingia na kupata marisho."(Yohana 10:9)
Baada ya Bwana kusema
maneno hayo, mlango
ukafunguka na tukaingia.
Niliwaona malaika
wakimpa utukufu, heshima na sifa Baba Yetu wa Mbinguni!
(Ufunuo 7:11-12) Kadri
tulivyozidi
kutembea, tulikaribia meza
niliyoweza kuona mwanzo
wake laini siyo mwisho. (Ufunuo 19:9)
Niliona enzi kubwa, na enzi
ndogo zimezungukwa na
maelfu ya viti. Katikati ya viti
niliona mavazi
na mataji. Bwana akaniambia, "Binti, taji unayoiona pale ni
taji ya Uzima."(Ufunuo2:10)
Yesu akasema, "Tazama, Binti,
hii ndiyo niliyowaandalia watu
wangu." Niliona ile meza
imefunikwa na vitambaa vyenye upindo wa dhahabu.
Kulikuwa na sahani, glasi za
dhahabu,
matunda; kila kitu
kimeandaliwa. Ilikuwa nzuri
ajabu. Kulikuwa na chombo kikubwa katikati ya
meza, kilichokuwa na mvinyo
tayari kwa mulo. Na Yesu
akasema, "Binti, kila kitu kipo
tayari kwa
ujio wa kanisa langu." MEZA YA KARAMU YA
MBINGUNI
Tulikwenda mahali pengine,
niliwaona watu wengi wakiwa
bustanini. Kulikuwa na watu
wanaofahamika sana kwenye Biblia, lakini hawakuwa wazee,
bali vijana. Palikuwa na kijana
akiwa
na kitambaa mkononi,
akicheza na
kuzungukazunguka na kumsifu Bwana. Yesu akasema, "Binti,
Yule kijana pale ni mtumishi
wangu Daudi." Alikuwa akimpa
utukufu Baba yetu. Ghafla,
kijana
mwingine akapita na Yesu akaniambia, "Binti, huyu ni
Joshua; Yule Musa; na Yule
pale ni
Ibrahimu." Yesu huwaita kwa
majina yao. Wote walikuwa na
mwonekano mmoja! Ajabu sana
Mbinguni! Yesu akasema,
"Mwanamke Yule ni mtumishi
wangu, Maria Magdalena; na
Yule
mtumishi wangu Sara." Lakini pia akaniambia, "Binti,
huyu ni Maria. Maria,
aliyemzaa Yesu Kristo,
ambaye ni mimi.
Binti, nikwambie, yeye hana
habari ya yanayotokea duniani. Nataka kukwambia, nenda
kawaambie wanadamu,
waambie waabudu sanamu
kuwa kuzimu ni halisi, na
waabuduo
sanamu hawata urithi Ufalme wangu, lakini waambie kama
wakitubu, wataweza kuingia
makao
ya mbinguni. Nenda waambie
nawapenda na pia waambie
Maria hajui chochote [kinachotendeka duniani] na
pekee wanayeweza kuheshimu
ni mimi, kwasababu si maria
wala
mtakatifu Gregory wala
mtakatifu yeyote awezaye kuokoa. Mimi ndiye niokoaye
na nje yanguhakuna
yeyote, hakuna yeyote, hakuna
yeyote – aokoaye!" Alirudia
mara tatu-kuwa hakuna
yeyote awezaye kuokoa; isipokuwa yeye.
Wanadamu wamedanganywa
na kuamini kuwa kwa kupitia
wadhaniwao ni watakatifu,
sivyo
ilivyo, bali ni mapepo, yafanyayo kazi kupitia sanamu
zilizofanywa kwa mikono ya
watu. Lakini
ngoja nikueleze kwamba
Bwana anataka kukupa kilicho
bora. Anataka wewe uingie katika Ufalme
wa Mbinguni; tubu na kuacha
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni