Wafilipi 2:10-11
  • TIME IS FAST RUNNING OUT ( MUDA KWA HARAKA SANA UNAKWISHA )


    MUDA KWA HARAKA SANA  
    UNAKWISHA!   
    USHUHUDA WA VICTORIA NEHALE â€" NCHINI NAMIBIA

    UTANGULIZI
    Nimezaliwa  na  kuishi  Namibia maisha  yangu  yote.  Niliokoka  tarehe  06/02/2005.  Bwana  Yesu
    amenifunulia mambo mengi ya ulimwengu wa roho pamoja na kunipeleka mara kadhaa kuzimu.
    Bwana   aliniambia  niwaelezee   watu   niliyoyaona;  na   akanionya   nisiongeze  wala   kupunguza
    chochote kwa  yale aliyonionyesha au  kuniambia. Kufikia  kuandika kitabu hiki,  mwisho wa 2006,
    nilikuwa nimetembelewa    na Bwana  Yesu mara  33. Kwa  kila utembezi  huo  Bwana alinisisitizia:
    MUDA UMEISHA.
    SAFARI YA KWANZA KWENDA KUZIMU
    Mwisho  wa  juma  la  23/07/2005, nilichukua  teksi  kutoka  mji  wa  Ondangwa  (Nchini  Namibia)
    ninakoishi na kufanya kazi, kuelekea kijijini kwetu kuwaona wazazi wangu. Nilipokwa njiani nilihisi
    kuwa kitu cha ajabu kilikuwa kinaenda kutokea jioni hiyo. Nilifika nyumbani mwendo wa saa kumi
    na  mbili  jioni  na ndio  wakati  watu  walikuwa  wakiandaa  chakula  cha  jioni. Nilikuwa  jikoni  na
    ndugu zangu nimelala juu  ya shuka kukuu  chini, na  wapwa zangu walikuwa wakiimba nyimbo  za
    kanisani.
    Ghafla nikahisi nguvu kuu za  Mungu juu yangu zilizoufanya mwili wangu  kuzimia. Nilimwona mtu
    mwenye kanzu  nyeupe na kamba  yenye rangi sawa,  akinisogelea nilipokuwa  nimelala. Kulikuwa
    na  mwanga wa  ajabu  unamzunguka  kana kwamba  unatoka  kwake.  Alikuwa amevaa  viatu  vya
    hudhurungi.  Alifanana na  watu wa  mashariki  ya kati  hata ngozi  ikawa  inampenda. Mwili  wake
    ulikuwa umejaa utukufu  nilishindwa kumwangalia kwenye  macho. Alipoongea sauti yake  ilikuwa
    ya  upole, huruma,  upendo,  na yenye  mamlaka. Mawimbi  ya  upendo yalikuwa  yakinijia kutoka
    kwake.
    Akainyosha mikono yake kuelekea  kwangu na kuniinua. Ghafla nikajikuta nipo  katika mwili mzuri
    uliobadilishwa.  Nilionekana  kama  vile  nilivyo  kuwa  kijana  wa  miaka   kumi  na  nane.  nilikuwa
    nimevalia kanzu nyeupe iliyofungwa kamba nyeupe. Ijapokuwa kanzu yangu ilikuwa nyeupe lakini
    malighafi  yake  ilikuwa  tofauti  na  kanzu  yake.  Vazi  lake  lilikuwa  la  kitani  safi na  mwanga  na
    mng’ao wake ni vigumu kuelezea.
    Alisema  kwa  upendo  na sauti  ya  upole,  â€™â€™Victoria  fuatana    nami,  nitakuonyesha  mambo ya
    kuogopesha na kukupeleka sehemu ambayo hujawahi kuona maisha yako yote”.
    Akanishika  mkono  wa  kuume  na  tukaanza  kuenda. Nilihisi  kama  vile  tunatembea  hewani  na
    tunapanda   wakati   wote.   Baada   ya   muda   njiani   nikawa    nimechoka   sana.   Nikamwambia
    nisingeweza kuendelea  na safari na nikaomba kurudi nyumbani.
    Aliniangalia kwa  upole na kusema  â€œHaujachoka uko  safi, ukichoka nitakubeba.  Lakini sasa uko
    safi. Amani na iwe nawe, tuondoke”.
    Sehemu tuliyofika  ilikuwa kame  na mbaya  kuliko jangwa  lolote baya  lililojulikana na binadamu,
    bila  dalili yoyote  ya  uhai au  maisha.  Hapakuwa na  mti  wowote, nyasi  au  kiumbe chenye  uhai
    hakikuonekana. Ilikuwa ni sehemu mbaya sana.
    Tulikuja  kwenye  lango  na  yule  mtu  akanigeukia  akisema,  â€œVictoria  tutapitia langoni  na  vitu
    utakavyofundishwa vitakuogopesha na kukufadhaisha. Lakini uwe  na uhakika kokote nitakako
    kupeleka utalindwa vizuri. Fungua macho yako uangalie kila kitu nitakacho kuonyesha”.
    Nilitishika na kuanza kulia. Nilipinga na kutaka anirudishe.
    Nikamwambia kuwa sikutaka  kuingia mahali pale kwakuwa nilikuwa  naona yanayotendeka ndani
    akaniambia,  â€Amani  na  iwe nawe;  niko  pamoja  nawe  ni  lazima  tuingie  ndani,  kwa  maana
    MUDA UMEISHA”.
    Kuzimu kulivyo
    Tukapita  lango lile  mpaka  ndani na  kwa  niliyoyaona nashindwa  kusimulia  mahali pale  palivyo.
    Nina  uhakika   hakuna  mahali  pengine   duniani  pa  kutisha   kama  pale.  Mahali   pale  palikuwa
    pakubwa sana na  nilihisi kuwa palikuwa panaongezeka   wakati wote. Giza la mahali  pale lilikuwa
    kubwa  sana   na  moto  uliokuwa   unawaka  haupimiki.   Moto  wenyewe  au   miali  yake  ilikuwa
    Page 2 of 8

    haionekani  ila ukali  wake  ulikuwa juu  sana.  Nzi wa  kila  namna na  rangi  walikuwa  kila mahali.
    Palikuwepo pia na  minyoo wafupi, wanene na weusi wakijaribu  kupanda juu ya kila kitu.  Minyoo
    wakanza kupanda  juu yetu huku  inzi wakiruka kila  mahali. Harufu ya  mahali pale ilikuwa  mbaya
    mno, ilikuwa kama  nyama iliyooza  ila ni zaidi ya mara mia ya harufu yoyote ile  niliyo wahikuihisi.
    Kulikuwa kumejaa sautu za vilio na kusaga meno, pia nilisikia vicheko viovu vya pepo wabaya.
    Cha kuhuzunisha  ni  kuwa mahali  pale palikuwa  pamejaa watu  wasiohesabika.   Watu  walikuwa
    kwa namna  ya mifupa.  Nilijua mifupa hiyo  ilikuwa ni watu  kwani niliweza  kwa uhakika kuwajua
    ndugu zangu kutoka kijijini kwetu. Mifupa hiyo ya rangi ya kijivu ilikuwa imekauka sana. Walikuwa
    na meno makali  kama  ya wanyama,  midomo mikubwa na ndimi ndefu na  nyekundu. Mikono na
    miguu ilikuwa na vidole virefu vyenye kucha za kutisha. Wengine walikuwa na mikia na pembe.
    Pepo   wachafu   walikuwa   wakichangamana   na  watu.   Mapepo   hao   walikuwa   kama   kenge
    wakitembea  kwa   miguu  minne.  Waliifurahia   hali  ile  na   wakawa  wakiwatesa  na   kuwakejeli
    wanadamu,  huku wao  wakirukaruka na  kushangilia wakati  wote.  Wanadamu kwa  upande wao
    walionekana  wa kusikitisha  na  kuvunjika  moyo, walionekana  kukata  tamaa  na bila  matumaini
    yoyote. Kelele za wanadamu zilikuwa  kwasababu ya maumivu. Walikuwa wakilia, kupaza sauti na
    kusaga  meno. Hali  yao  haikuwa  ya  kusikitisha tu,  bali  pia  ya uchungu  na  masitikiko.Watu  wa
    mahali pale walikuwa wengi lakini niliona wazi kuwa wengi walikuwa wanawake.
    Makundi ya watu kuzimu
    Waligawanywa kwa  makundi tofauti lakini  haikuwezekana kuwahesabu kwa  makundi yao kwani
    walikuwa  wengi   sana.   Niliyekuwa  naye   akanipeleka  kwa   kikundi  kimoja   cha  mashariki   na
    kuniambia, “Hili ni kundi la walioshindwa KUSAMEHE. Niliwaeleza mara nyingi na kwa njia tofauti
    jinsi ya  kuwasamehe wenzao  lakini wao  wakakataa. Niliwasamehe  dhambi zao  zote lakini  wao
    wakakataa   kuwasamehe  wengine.   Muda   wao   duniani  ulipoisha   wakajipata   mahali   hapa.
    Watakuwa  mahali  milele  yote,  wanavuna  matunda  ya  matendo  yao  milele  na   milele.  Ila  ni
    uchungu kwangu kuwaona hapa katika hali hii â€" kwa kuwa nawapenda”.
    Nikaongozwa  kwa  kundi  la  pili  na  nikaambiwa  na  yule   mwenye  kunipeleka,  kuwa  walikuwa
    wenye MADENI na makundi yao yalikuwa matatu:
    1.
    Wa kwanza  ni wale  waliodaiwa na  wenzao na  walikuwa na uwezo  wa kulipa  lakini wakawa
    wakihairisha  siku baada  ya  siku.  Wangeahidi kulipa  wakati  ujao,  mwezi ujao,  mwaka  ujao
    mpaka muda  wao duniani  ukaisha na  wakajipata mahali hapa.  Watakaa mahali  hapa milele
    na milele wanavuna matunda ya kazi yao.
    2.
    Wa  pili  ni   wale  waliodaiwa  madeni   waliyoweza  kulipa  na  walikuwa   tayari  kulipa  lakini
    waliogopa madhara  yake. Waliona  kuwa wakiongea  ukweli watakataliwa,  watapelekwa jela
    au  walichokifanya   kingejulikana  dunia  yote   na  wangedhalilishwa.  Yule  mtu   akaniambia,
    “Hakuna  hata  mmoja  aliyeniuliza  njia  ya  kulipa.  Wangefanya   hivyo  ningewaonyesha  njia
    rahisi. Walitumia hekima na sababu zao ambazo hazikuwasaidia hata kidogo”.
    3.
    Waliokuwa   na   madeni   wasiyoweza   kulipa   ila   hawakuniambia   kwamba   wana   madeni
    wasiyoweza  kulipa.   Wangefanya  hivyo  ningewalipia  madeni   yao.  Pia  walijaribu   kutumia
    hekima  na  sababu zao,  ambazo  hazikuwasaidia  hata  kidogo.  Sasa wamejikuta  sehemu  hii
    wasiyoweza kutoka.  Wanakula matunda ya  matendo yao.  Moyo waniuma kwa  ajili ya  hawa
    wote kwasababu nawapenda sana.
    Katika kundi la kwanza  niliwaona ndugu zangu wawili wa kike  wa karibu, vilevile na ndugu yangu
    mmoja  wa  miaka   kumi  na  miwili.  Nilijua   miaka  yake  kwani  huo   ndio  uliokuwa  umri  wake
    alipofariki.  Katika kundi  la pili  niliwaona  baadhi ya  ndugu zangu  na  hata mchungaji  niliyekuwa
    namfahamu vizuri.  Jakes mpenzi  wangu aliyejinyonga  baada ya  mimi kuokoka   alikuwa  kwenye
    kundi la pili. Niliwaona baadhi ya majirani  zangu katika makundi yote.
    Niliwajua   watu   tuliokuwa   tukifahaminiana   na   wao   pia   wakanijua.   Watu   wa  ukoo   wetu
    waliponiona  walianza  kunitukana  kwa  lugha  chafu.  Mmoja   wao  akaniambia  kuwa  sikustahili
    Page 3 of 8

    kumfuata   yule    niliye   kuwa    naye.   Wakanikumbusha    hali   niliyokuwa    kabla   ya    wokovu.
    Waliyoyasema yalikuwa kweli kwani ni mambo niliyoyafanya. Jakes mpenzi wangu akasema kuwa
    nilikuwa  wake   na  nilistahili  kuwa   alipokuwa  maana  dhambi  zetu   zilikuwa  sawa.  Mwanzoni
    Mchungaji   alifurahia    kuniona    nikienda   alikokuwa,    lakini   alipoona    niliyeandamana   naye
    akaungana na  wenzie  kunitukana. Aliyekuwa  nami  akaniambia niyapuuzie  maneno hayo  kwani
    hawakujua walichokuwa wakifanya.
    Nikaogopa  na kushikwa  na  huzuni sana,  nilikuwa  nikitetemeka nikashindwa  kusimama.  Nikalia
    bila kujizuia  ndipo  niliyekuwa naye  akanikumbatia na  kusema, “Amani  na  iwe nawe  Victoria”.
    Palepale nguvu  zikanirudia na nikapata faraja  na amani kuwa  naye. Wakati wa  kuondoka ukawa
    umefika  naye  akasema,  â€œVictoria  nimekuonyesha  haya  ili  uchague  ni  kundi  lipi  ungependa
    kuwa, kwa  kuwa uamuzi ni  wako. Lazima  uwaambie watu kila  kitu ulichoona bila  kupunguza
    au kuongeza kitu chochote.”
    Kurudi kutoka kuzimu
    Nakumbuka tulipotoka  mahali pale pa  mateso tukiwa  pamoja, ila sijui  nilipomuacha kwasababu
    niliposhtuka na kufungua macho nilijikuta mwilini kama kawaida. Nilikuwa nimelazwa hospitali  ya
    Oshakati.  Kulikuwa  na  mpira  wa  kuingizia maji  mwilini,  mamangu  na  ndugu  zangu  walikuwa
    chumbani  humo.  Machozi  yalikuwa  hayajamkauka  mamangu.  Nilipomuuliza  Nesi  kilichokuwa
    kikiendelea akaniambia, “Umerudishwa, pengine una makosa na unahitaji kutubu.”
    Japo   Nesi   aliongea  kwa   furaha   bado   niliona   anaogopa  kunisogelea.   Nikamuulizia   daktari
    aliyekuwa akinishughulikia.
    Daktari  alipofka   hakuweza  kuelezea   ugonjwa  niliokuwa   nao.  Alidhania   kuwa  malaria  lakini
    matokeo hayakuonyesha hivyo. Joto  la mwili na shinikizo la damu vyote vilikuwa  chini sana lakini
    hakujua  sababu yake.  Hakujua  la  kufanya kwani  hangeweza  kunilaza  Hospitalini kwani  sikuwa
    mgonjwa.  Maji waliyoniingizia  kwa  mpira  yalikuwa hayaingii  vizuri  lakini  mara tu  nilipofungua
    macho yakaanza kuingia bila tatizo. Daktari akaagizia niongezewe maji mengine.
    Niliendelea  kuhofu   na  kulia   kwa  ajili   ya  mahali   pale  pa  mateso.   Matukio  ya   mahali  pale
    yaliendelea  kupita machoni  kwangu saa  zote. Sikuweza  kulala  mwili mzima  ulikuwa unaumwa,
    viungo  vyote  vilikuwa  kama vimetenganishwa  na  kuunganishwa  tena.  Tumbo  lilinisumbua  na
    kichwa kikaniuma juma zima.
    Niliamua
    kutomwelezea
    mtu
    yeyote
    niliyoyaona.
    Ni
    nani
    atakayeniamini?
    Watu
    wangenichukuliaje?  Nikajiwazia. Baada  ya  siku  tatu nikamwambia  mama  mmoja  aniombee na
    nikaishia kumwelezea  yote yaliyotokea.  Nikajihuzunikia sana kwa  kuisimulia hadithi  hiyo maana
    sasa haingeweza  kufichika. Mwishowe nilielewa  kuwa Mungu ni  Mungu. Akitaka kitu  kisimuliwe
    sina uwezo wa kukizuia eti kwasababu ya ya mawazo na hofu yangu.
    Maelezo juu ya safari
    Agosti  19, niliamka  nikihisi  nguvu za  Mungu.  Nilikuwa dhaifu  nikitetemeka  na nikajisikia  kama
    nguvu  za   umeme  zinapita  mwilini.   Jioni  nikaona  miale   ya  mwanga  mkuu   na  katikati  yake
    nikamwona mtu yule  aliyenipeleka sehemu ya mateso. Wakati huu  akaketi kwenye kiti karibu na
    kitanda changu.  Kiti  chenyewe hakikuwepo  lakini alipotaka  kukaa kilionekana.  Kilikuwa kiti  cha
    mapambo mazuri huku kikiwa kimeundwa na dhahabu tupu.
    Baada  ya  kunisalimia  akaniambia  kuwa  anaelewa  kuwa  nina  maswali  mengi  na   ndio  maana
    alikuwa  amejitokeza   ili  ajieleze   yeye  na   mambo  mengine   yaliyokuwa  yametokea.   Akaanza
    kusema,
    “
    tulikokwenda ni  kuzimu”. Nikaona mahali alipogongwa misumari.
    Mimi  ni  Yesu,  mwokozi  wako,  kama  una  mashaka yoyote  angalia  mikono  yangu.  Mahali
    Rafiki ningependa nikwambie  kuwa kuzimu sio  mawazo ya mtu bali  ni mahali pabaya pa  mateso
    kulikotengenezewa shetani  na mapepo  yake. Wanadamu  wanastahili kwenda mbinguni  pamoja
    Page 4 of 8

    na  Yesu  lakini lazima  tumchague  yeye  kabla  hatujachelewa.  Leo ukisikia  sauti  yake  usiufanye
    moyo  wako   kuwa  mgumu.  Mkubali  Yesu   kama  mwokozi  wako,   na  kama  umempokea  basi
    mwishie yeye.
    Sikujua  sababu  ya  kuambiwa   nichague  kati  ya  makundi  mawili   huko  kuzimu  na  ilhali  mimi
    nimeokoka.   Nimemwamini    yeye   na   bado    ananiambia   nichague   kwenda    kuzimu   au   la.
    Sikumuelewa.  Nikamwomba Mungu  anifunulie  maana  ya usemi  huu  na kile  angetaka  nifanye.
    Akaniambia kuwa  nilikuwa mtu  wa HASIRA  na pia SIKUWASAMEHE  dadangu na  binamu
    yangu mmoja.  Nikaomba msamaha  kwa dhambi  hiyo  halafu  nikamwomba dada  msamaha kwa
    kuweka hasira na chuki dhidi yake. Ikabakia kwenda kumwomba binamu msamaha.
    Bwana akanikumbusha kuwa  niliwahi kupata ajira ya  ualimu nikitumia cheti bandia  cha diploma.
    Akasema   kuwa  kitendo   hicho  ni  DENI   pamoja  na  WIZI.   Nilitaka   kutenda  lililo   haki   na
    nikamwomba  anipe njia  nzuri  ya  kufuata kwani  hilo  lilitosha  kunipeleka gerezani.  Akaniambia
    nikatubu kwenye idara  ya elimu. Nilikuwa tayari  kwa lolote, hata  kwenda gerezani ikiwa haiwezi
    kuepukika. Mungu akatenda maajabu na wakuu wakaniambia nichague  kama nataka kulipa au la.
    Hawakutaka kunipeleka  mahakamani kwasababu  kukiri  kwangu kuliwashangaza.  Hakika Mungu
    ni wa ajabu na analiheshimu neno lake.
    Ukiwa  na  jambo   kama  hili  nakusihi  kufanya   kilicho  cha  haki   bila  kujali  matokeo.  Unaweza
    ukafungwa  jela hapa  dunuiani lakini  hiyo  ni ya  muda.  Hakuna uchungu  au fedheha  inayoweza
    kufananishwa  na kutengwa  na  Mungu  milele  na milele.  Kuzimu  sio  mahali  pazuri; ni  afadhali
    umwache Mungu akuhukumu sasa kabla  haujachelewa. Tusiogope hukumu ya Mungu katika siku
    hizi za neema,  NI VYEMA TUMWACHE YEYE  ADHIHIRISHE CHOCHOTE KILICHO KIBAYA  MAISHANI
    MWETU  KAMA BADO  TUNA  WAKATI  WA KUJIREKEBISHA  kwani  hakuna  msamaha  upande ule
    mwingine wa kaburi.
    SAFARI YA PILI KUZIMU
    Tarehe 18/10/2005,  niliamka saa kumi  na moja  unusu alfajiri, sikuweza  kwenda kazini. Nilikuwa
    najisikia dhaifu  sana na nikawa  nimenyong’onyea; nisingeweza  kujisogeza au  kugeuka kitandani
    pangu,  uwepo  wa  Mungu ulikuwa  mkubwa  chumbani.  Nilikuwa  nikitetemeka  na  kuhisi  kama
    nguvu  za   umeme   zinapita  mwilini   mwangu.  Bwana   akaja   kunichukua  kabla   ya  saa   mbili.
    Alinisalimu na  kuniambia kuwa inatupasa  kwenda tena kwani  MUDA UMEISHA.  Nikasimama na
    tukaanza  kutembea. Jinsi  tulivyokuwa  tukitembea siku  hii  ilikuwa tofauti  na  siku zingine.  Japo
    miguu yetu ilikuwa ikitembea, ilikuwa ni kama tunaogelea zaidi kuliko kutembea.
    Tukiwa  safarani,  Yesu  akaniambia,  â€œDhambi  zote ni  mbaya  na  hakuna  dhambi  kubwa  wala
    ndogo.   Dhambi   zote   huleta   mauti,   haijalishi   ukubwa    wala   udogo”.   Akaniambia   kuwa
    tunaelekea tena kuzimu na  kisha akaniuliza kama nilikuwa na hofu.  Nikamwambia kuwa nilikuwa
    naogopa.   Akasema,  â€œRoho   ya   hofu   haitoki  kwa   Baba   yangu,   inatoka  kwa   shetani.   Hofu
    itakusababisha ufanye vitu vitakavyo kupeleka kuzimu.  Bila  imani ni vigumu kumpendeza Mungu
    na hofu ni kinyume  cha imani. Nidhahiri hofu haimpendezi Mungu  kwasababu huharibu imani ya
    mtu ya mtu ”.
    Kwa muda wote tukiwa njiani tulikuwa tukitembea upande upande lakini  baada ya kufika lango la
    kuzimu   akanishika  mkono   wangu  kwa   muda   wote  tuliokuwa   kuzimu.   Nilikuwa  na   furaha
    kwasababu  alinishika mkono  na  kwa  kunishika  aliondoa hofu  yote  ndani  yangu. Sehemu  hiyo
    ilikuwa bado  inafanana na ya  kwanza; hapakuwa  na tofauti na  sehemu ya  kwanza. Kulikuwa na
    vijidudu virukavyo, minyoo, joto lililokithiri,  harufu mbaya, mifupa, kelele. Kila kitu kilikuwa kama
    nilivyoona mara ya kwanza.
    Mtumishi aishia motoni
    Tuliingia  lango kama  lilelile  tena  akanipeleka  kwenye moja  ya  makundi  ya watu.  Kulikuwa  na
    watu wengi  niliokuwa  nawafahamu walipokuwa  hai duniani.  Watu walikuwa  katika  hali mbaya
    sana; walionekana  wamefedheheka na uchungu mzito  lakini kibaya zaidi  walionyesha sura zisizo
    na matumaini.
    Page 5 of 8

    Bwana  akamwashiria  mwanamke mmoja  mwenye  umri  wa  kati.  Nilimjua  kabla ya  kifo  chake
    kilichotokea  kwa ajali  ya gari  mwanzoni  mwa 2005.  Nilishtushwa  kumuona kuzimu  kwani sote
    tulimjua kama  mcha Mungu. Bwana akaniambia  kuwa mwanamke  alimpenda Mungu na Mungu
    pia alimpenda mwanamke  huyo. Alinitumikia alipokuwa duniani,  Aliwaongoza wengi kwa  Bwana
    na  alimjua  Bwana   vizuri.  Alikuwa  mwema  kwa  maskini   na  wahitaji;  alitoa  kwa  ajili   yao  na
    aliwasaidia katika njia mbali mbali. Alikuwa mtumishi mzuri wa Bwana katika njia nyingi.
    Maneno   haya  ya   Bwana  yalinishtua   sana  na   zaidi   nilipomuuliza  kwanini   akamwacha  mtu
    aliyemtumikia vizuri aishie kuzimu. Bwana akajibu  kuwa ijapokuwa alijua sana maandiko alikubali
    uongo wa shetani  kuwa kuna dhambi ndogo na  kubwa. Alifikiri dhambi ndogo haitamwangamiza
    kuzimu   maana   yeye   ni   mkristo.   Bwana   akaendelea   kusema,   â€œNilienda   mara   nyingi   na
    kumwambia aache alichokuwa akikifanya  lakini mara nyingi aliendelea kufikiria  kuwa dhambi
    hiyo  ni ndogo  sana  na  mwisho akachukulia  kuwa  maonyo niliyompa  yalitokana  na  dhamiri
    dhaifu aliyokuwa nayo. Kuna wakati aliacha dhambi hiyo lakini baada  ya muda akairudia huku
    akajishawishi kuwa maonyo  hayo ni sauti  ya kwake mwenyewe  maana dhambi hiyo ni  ndogo
    na haiwezi kumhuzunisha Roho Mtakatifu”.
    Nikamuuliza tena Bwana anieleze  dhambi aliyoifanya mwanamke huyo, naye akanijibu kwamba,
    “
    Mwanamke huyu  alikuwa  na rafiki  yake  Nesi katika  hospitali ya  Oshakati.  Wakati wowote
    alipokuwa  mgonjwa   hakuwa   akilipia  kadi   ya  hospitali   kama   inavyotakiwa  bali   alikuwa
    anampigia  rafiki  yake  simu  na  wanafanya  mpango  wa  yeye  kupata  dawa  kutoka  kwenye
    zahanati. Rafiki yake alikubali kumfanyia hivi wakati wote”.
    Hukumu yake ni kuwa:
    ï‚·
    ï‚·
    ï‚·
    alikubali uongo wa shetani juu ya dhambi ndogo na kubwa na hivyo kuikataa kweli yangu.
    alimsababisha mwenzie kutenda dhambi ya kuiba kwa niaba yake.
    lililo baya zaidi, alimhuzunisha Roho Mtakatifu. Hii ndio lilimpeleka kuzimu.
    “
    Haijalishi kama  utaleta mamilioni  ya nafsi  kwa wokovu bado  unaweza kuishia  kwenda kuzimu
    kwa kumhuzunisha Roho Mtakatifu. Ni lazima uangalie wokovu wa wenzio lakini uwe mwangalifu
    usisahau  roho  yako.  Uwe  makini na  kila  jambo  unaloambiwa  na  Roho  Mtakatifu”.  Baada  ya
    Bwana kuyasema hayo akaniambia turudi.
    Unayachukuliaje maneno haya?
    Wakristo wengi waliosikia simulizi hii hupata maswali mengi. Wanajiuliza,
    “Je kuhesabiwa haki, huruma na neema za Mungu hazina nafasi yoyote?”.
    “Na je unaweza kuupoteza wokovu baada ya kuupokea?”.
    “Mbona neno hili lina ukali sana? Mungu anaweza kuwa katili hivyo?”.
    Kama   nilivyosema  mbeleni   mimi  sifundishi   theolojia.   Ninasema  tu   mambo   ambayo  Bwna
    alinionyesha  na kunifundisha.  Nakuomba  uangalie Biblia  yako  vizuri kwa  majibu. Hebu  angalia
    vifungu vifuatavyo halafu ujiamulie.
    Bali  nautesa mwili  wangu na  kuutumikisha;  isiwe, nikiisha  kuwahubiri  wengine, mwenyewe
    niwe mtu wa kukataliwa.  (1Wakorintho 9:27)
    Tuseme  nini  basi? Tudumu  katika  dhambi  ili neema  izidi  kuwa  nyingi?  Hasha!  Sisi tulioifia
    dhambi tutaishije tena katika dhambi? ( Warumi 6:1-2)
    Basi dhambi isitawale ndani ya mioyo yenu ipatikanayona mauti, hata mkazitii tamaa zake â€"
    (
    Warumi 6:12)
    Maana, kama  tukifanya  dhambi kusudi  baada ya  kuupokea  ujuzi wa  ile  kweli, haibaki  tena
    dhabihu kwa ajili ya  dhambi. Bali kuna kuitazamia hukumu kwenye  kutisha, na ukali wa moto
    ulio tayari kuwala wao wapingao.    (Waebrania 10:26, 27)
    Je  naweza  kuishia  kwenda  kuzimu  baada  ya  kumtumikia   Bwana  na  kuwaongoza  wengi  kwa
    Kristo? Jiamulie mwenyewe.
    Page 6 of 8

    Kutotii
    Jumatatu  tarehe  06/03/2006, niliamka  saa  kumi  na  moja na  nusu  alfajiri.  Nilipoanza  kuomba
    nikaona  kuna  nguvu  za Mungu  za  ajabu  juu  yangu.  Mwili  wangu  ulikuwa  dhaifu na  nilikuwa
    natetemeka. Nguvu kama za umeme zilikuwa zinapita mwilini mwangu.
    Mchana  nilipokuwa   nimelala  nikaona   mwanga  mkubwa   wa  ajabu   ukikijaza  chumba  chote.
    Nikaona  vitu  vidogo  vyeupe   vyenye  umbo  la  mviringo  vikiniangukia   kama  mvua  na  kuingia
    mwilini. Kisha nikaona wingu la kitu kama  ukungu likishuka, kukijaza chumba chote na pia kuanza
    kuingia  mwilini  mwangu.  Nikamwona  Yesu  akinijia  akiwa  katikati  ya wingu  lile  la  ukungu  na
    akaketia kiti chake kandokando ya kitanda changu. Sijui kiti hicho  hutoka wapi ila huwa kinatokea
    akiwa tayari kukaa. Kiti chenyewe kimeundwa na dhahabu tupu, kuna nyota ya shaba kwenye kila
    mguu wa kiti hicho. Mahali pa kujiegemezea pamewekwa pia nyota kubwa  ya shaba na kila mguu
    wa kiti hicho kuna magurudumu ya mviringo.
    Yesu   akaninyoshea   mkono   kunisalimia.   Akaniambia   niinuke   kwa  kuwa   MUDA   UMEISHA.
    Akanivuta kwa mkono  na nikakaa juu  ya kitanda. Akaniambia, “Victoria  tuombe”. Akaomba kwa
    lugha  ambayo  sikuelewa.  Nilichoelewa pekee  ni  neno  â€˜Amina’.  Akaniuliza  nilichokuwa  naona.
    Watu  walikuwa wakiingia  kazini.  Nikaona vile  vitu  vidogo vya  mviringo  vikiwaangukia kundi  la
    wale  waliotangulia  kufika  mahali  pao  pa  kazi.  Waliofika  baadaye  walipata  mvua  ya  vitu  vile
    imekatika. Jambo hili pia nikaliona  kanisani, waliotangulia waliangukiwa na vitu hivi vyeupe lakini
    waliofika baadaye hawakuvipata.
    Yesu  akaniuliza  kama  naelewa  maana  ya  maono  hayo  nami  nikamjibu  kuwa,  â€œSielewi”.   Basi
    akanieleza,
    “
    Maono hayo  yana maana  kuwa kila  mahali unapostahili kufika  kwa wakati  fulani, na  unaujua
    wakati huo,  kuna Malaika wanawagawanya baraka,  kwa muda ule.  Anayewahi anapata baraka
    zile anayechelewa  anazikosa â€" kwa  kuwa Malaika hugawa  baraka kwa  muda tu. Vitoria  nataka
    nikuonye  kwa  kuwa  unachelewa kwenda  kazini  na  unachelewa  zaidi  kwenda  kanisani.  Elewa
    kuwa  siku  ulizochelewa   bila  sababu  umekosa  baraka  zako   za  siku  hizo  milele.  Baraka   hizo
    haziwezi  kukurudia.  Victoria  ni  lazima  uache jambo  hilo  na  usirudie  pengine  uwe  na  sababu
    nzuri”.
    Aliponiambia hivyo  nilitamani kumkimbia  au   kumpa sababu  nzuri kwa  kosa hili.  Nikamwambia
    nilikuwa  na  tatizo  la  kulala  sana  lakini  akaniangalia   moja  kwa  moja  usoni  na  kusema  kuwa
    nilikuwa  na tatizo  la  kurudi  tena kitandani  baada  ya kuamka,  nilikuwa  naangukia  majaribu ya
    kutaka kulala dakika zingine chache.
    Yerusalem Mpya
    Baadaye   akaniambia,   â€œAmka  twende   MUDA   UMEISHA   na   kuna  vitu   lazima   kuvifanya”.
    Akanipeleka mahali  sijawahi  kufika, barabara  yenyewe  ilikuwa mpya  kwangu. Tukafika  kwenye
    bustani yenye maua  mazuri na miti  mizuri ya kijani kibichi;  hakuna kitu duniani cha  kulinganisha
    na uzuri huu. Tukakalia kiti cha dhahabu kilichokuwa kwenye bustani hiyo nzuri.
    Tulipokuwa tumekaa,  Yesu aliniashiria mbele  kwa kidole chake  na kusema, “Victoria  angalia, je
    wauona  mji ule?”.  Nilipoangalia  nikaona mji  mkubwa  uliokuwa na  mwanga  mkubwa. Mji  huo
    ulikuwa  mzuri  kupita  maelezo.  Lango  lake  lilikuwa  la  dhahabu  huku  liking’aa  ajabu,  na  mtu
    mwenye  umri mkubwa  alikuwa  amekaa pale.  Mtu  huyo alikuwa  na  ndevu na  nywele  nyeupe.
    Nilikuwa  nimemwona  hapo mbeleni  na  nilipomuuliza  Bwana,  akaniambia  kuwa ni  Abrahamu,
    baba wa Imani.
    Niliona  barabara nyingi  ndani  ya  mji ule  zilizojengwa  kwa  dhahabu. Kulikuwa  na  majumba  ya
    ghorofa yalokuwa yaking’aa kama dhahabu. Mng’ao wa jiji lile kwa kweli hauelezeki.
    Yesu akanigeukia na kuniuliza, “Unafikiria nini juu ya mji ule?”
    Nilijibu kuwa ni mji  mzuri na nataka niende  huko. Yesu akasema, “Nitakupeleka huko ukiendelea
    kuwa  mtiifu,  maana  ndiko   iliko  nyumba  yako.  Ishi  kwa   uaminifu  ukishindwa,  nyumba  yako
    Page 7 of 8
    itakaliwa na kunguru na bundi. Itakuwa  uwanja wa pepo wabaya. Hata hivyo usihofu, kwasababu
    niko  pamoja  nawe, wewe  kuwa  mtiifu  tu.  Asiyetii  nyumba  yake itakuwa  makazi  ya  bundi  na
    uwanja wa mapepo wabaya”.
    Yesu Kristo  kweli  yupo na  anatupenda kwa  upendo usioelezeka.  Hitaji kubwa  la moyo  wake ni
    wanadamu tuchaguwe uzima ili tukae nae milele.
    Moyo wake  unaugua kwa  ajili ya  watu wanao kufa  na kuishia  kuzimu kwasababu  ya kuuacha
    wokovu aliowapa na kuchagua mauti.
    Haijalishi umeokoka au haujaokoka neno moja tu ukumbuke ni  kuwa: MUDA KWA HARAKA
    SANA UNAKWISHA.

    Page 8 of 8

    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate