Nawasalimu kwa jina la YESU WA NAZARETI aliye hai na ndiye
aliye mwana wa pekee wa MUNGU sasa na milele, wala hatakuwepo mwingine zaidi
yake. YESU huyu yeye ndiye agano la MUNGU kati yake na wanadamu ili kwa kupitia
yeye watu wafike mbinguni na wamuone MUNGU na zaidi hata biblia inamtaja kuwa
yeye ndiye njia ya uzima na kweli. Sasa niwaulize swali watu waote wa mataifa,
je ipo njia nyingine tena ya kweli ya kutupeleka mbinguni ambayo MUNGU ameleta
tuifuate? Jibu, haipo. Ni YESU WA NAZARETI peke yake au kwa jina lingine
anaitwa Nabii Issa.
Nitaelezea kwa ufupi kuhusu mkristo anayejiita yeye ni
mkristo lakini hajabatizwa kwa maji mengi yanayotembea. Nilipokuwa nafundishwa
na YESU mimi Hebron, sikuyajua haya na mengi sana ila ilibidi anifundishe yeye
mwenyewe kwanza kabla ya kunituma kuifanya kazi yake sababu sikusomea katika
chuo chochote hapa duniani ila mwalimu wangu ni yeye YESU WA NAZARETI. Alinifundisha
kama alivyowafundisha wale wanafunzi wake wa kwanza. Akaniambia watu wanapigwa
upofu na shetani ili wasije mbinguni wala wasinione nao wengi wao wananipenda
ila hawapo katika njia ya kweli, wapo katika njia ya mwovu ambayo ni ya
shetani. Wametekwa na mafundisho ya uongo nao wamekuwa watoto wa baba wa uongo
ambaye ndiye Ibilisi. Sasa nakutuma Henron uwaeleze mataifa yote ukweli na
watakao yatii maneno niliyokutuma watapona ila watakao yakataa damu yao
haitamlilia MUNGU katika mikono yake. Katika biblia hakuna ubatizo wa maji ya
kikombe, wala maji ya kisima, wala mtu kubatizwa kwa jina la mchungaji yeyote
yule. Batizo za jinsi hii zote ni batizo za agano la kuwa wewe ni mfuasi wa
shetani, ila wewe haujui ni siri iliyofichika. Amenituma YESU, sasa muelewe na
mwatumie na wengine ujumbe huu na zaidi soma kitabu cha UBATIZO WA KWELI KWA
ULIMWENGU WOTE cha Nabii Hebron utaelewa zaidi.
Ili uwe mkristo ni lazima uokoke na ubatizwe kwa ubatizo wa
maji mengi tena ukiwa mtu mzima, unazo akili. Nataka muelewe hata siku zote mtu
unapoingia mkataba wowote hapa ulimwenguni ni lazima uusome, uuelewe, ndipo
uukubali, usaini. Sasa nikuulize swali ulipokuwa mtoto mdogo ulielewa kuwa
unabatizwa? Na ulikuwa unayo akili? Na je neno ubatizo ni kumwagiwa maji
kichwani tu? Jibu, siyo. Kubatizwa ni kuzamishwa. Sasa uone tu hapa tayari
haujabatizwa ila umemwagiwa maji, hivyo basi siyo mkristo kabisa ni mkristo
jina na mbinguni hauendi. MUNGU alileta ubatizo wa maji mengi na YESU pia na
yeye alibatizwa ili kuonyesha njia. Sasa nawauliza ulimwengu, je hamuoni
mmedanganywa na kupotezwa ingali mnampenda YESU lakini hamuelezwi ukweli ili
mumfuate? Sasa uamue leo, ubatizwe ubatizo wa maji mengi uweke agano na YESU
kuwa sasa wewe ni mkristo na ni mfuasi wake, umetimiza ahadi zako kwa kubatizwa
kwa maji mengi.
Natumaini mnaelewa japo hata mimi iliniuma sana sababu
nilidanganywa, nikaishi miaka mingi nikifikiri mimi ni mkristo salama kumbe
nilikuwa ni mkristo mauti, ila neema yake ilinitoa nikawa mkristo hai na sasa
nipo na YESU wa kweli kama mfuasi wake na mtumishi wake. Nawaeleza mumrejee
MUNGU, mambo yameharibika kanisa limerudia yale ya Mafarisayo ya kulibadilisha
neno la MUNGU na ndio sababu watu wamepotezwa. Neno linapobadilishwa tu uelewe
ndio njia ya mbinguni imebadilishwa na kufuatwa njia ya jehanamu. Hivyo ikatae
njia ya jehanamu sasa umeelewa YESU akija sasa sijui utakuwa katika eneo gani,
wakati ndio sasa, hata hao wanaowabatiza watu kwa ubatizo ambao haupo katika
biblia, hao pia siyo wakristo, huo ndio ukweli hata ukirudi katika neno la
MUNGU, imeandikwa usiongeze neno wala kulipunguza (Ufunuo 22:18-19). MUNGU
amekataa, sasa nyie wanadamu au makanisa je hamuoni mtahukumiwa kwa ajili ya
hiki? Hata hiyo kazi na injili za jinsi hii nawatangazia mnapoteza muda wenu
bali mnamfurahisha shetani kwa kutengeneza njia za kuwaangamiza watoto wa MUNGU
waende jehanamu. Na ndiyo sababu nawaeleza kwa ujasiri kabisa hata ukisoma
katika biblia utaona haupo na kama haupo basi umetokea wapi? Umeongezwa kwa kutoka
kwa shetani. Shetani alitumia njia hii ili kuweka agano na wanadamu ili wawe watu
wake kwa njia ya kuwabatiza watu kwa njia ya ubatizo wa kikombe, maji ya
kisima, kuwabatiza watu kwa jina la mchungaji. Nawaeleza siri hii mfunguke ili
mpone. YESU akija anaagalia agano lake. Sasa jiangalie wewe liko wapi agano
lako la ubatizo aliobatizwa YESU? Jibu unalo peke yako.
Nawasihi mbatizwe upya na mkatengwe nao wala sehemu kama
hizo penye agano la batizo za jinsi hiyo hapo hata siku moja hataonekana YESU
WA NAZARETI hata kama jina lake linatajwa sababu hakuna agano lake la ubatizo
wa maji mengi yanayotembea. Na kama umeshajua ukweli unasubiri nini? Je YESU
akilinyakua kanisa lake sasa na wewe hauoni hautanyakuliwa sababu hauna agano
la YESU WA NAZARETI bali unalo agano la shetani? Mrejee sasa utubu na yeye
atakusamehe, na usishiriki katika maeneo ya jinsi hiyo sababu hakuna agano
lake. Hata sadaka zako uelewe ulizipeleka kwa shetani na kila unapoenda hata
katika makanisa ya jinsi hiyo uelewe unaenda kujihudhurisha mbele za shetani na
siyo mbele za MUNGU.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe, niandike jina langu katika
kitabu chako cha uzima wa milele. Uniongoze nikabatizwe ubatizo kama uliobatizwa
wewe pasipo kubadilishwa ili niingie agano na wewe, niwe mkristo wa kweli na
siyo mkristo wa uongo tena. Amen.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni