BWANA YESU ASIFIWE!
Karibu katika somo ambalo na kwenda kukufundisha mimi Nabii
Hebron kama MUNGU alivyonifundisha ili uelewe siri hii iliyofichika kuhusu
kitabu cha ufunuo. Ukisoma katika kitabu cha Ufunuo 13:1-3 biblia inaelezea
kuhusu makufuru makufuru na ukiendelea kusoma Ufunuo 13:1-7, 16…inaelezea
vizuri zaidi.
MAKUFURU
Ni maneno mabaya yanayotolewa na huyu mnyama mwenye pembe
kumi ambaye alipewa uwezo na joka kuu ili kutawala ulimwengu na kuwafanya
wanadamu waweze kumtukana MUNGU pasipo wao kujua au kupenda japo wapo ambao wanajua
kabisa wanamtukana MUNGU na wao wanapewa nguvu na huyu mnyama. Nitaelezea kwa
ufupi; zaidi fuatilia YouTube ya Nabii Hebron na vitabu na kanisani yapo
mafundisho yatakusaidia kuponywa nafsi yako.
Makufuru
yapo ya aina mengi; nitaelezea 3…
1. MAKUFURU
YA KICHAWI
Makufuru haya ni maneno ambayo wachawi au washirikina
huyasema wakati wakiwa katika kazi zao au matambiko vile vitu wanayoyafanya
ndiyo makufuru na vitu vinatokea hao hupewa nguvu na huyo mnyama mwenye pembe
kumi na kwa jinsi nyingine kila mchawi ni mwana chama wa namba 666, hata anayeendaga
huko na yeye huwekewa namba 666 na huyo mnyama sababu ni roho zake ndizo
zitendazo kazi sababu unamsujudia na yeye anakuwa ndiye mungu wako pasipo wewe
kupenda wala kujua.
Watu wengi mmesikia kuwa watu wana wanga usiku, wengine
wanapaa kwenye ungo, kulala makaburini, kuzini na waganga wa kienyeji,
kuogeshwa na waganga wa kienyeji na mambo mengine yote unayofanyiwa nao pamoja
na malipo; hayo malipo unakuwa umempa sadaka huyo mnyama na pia unakuwa na wewe
unaunganishwa katika kumtukana MUNGU kwa sababu hayo unayoyashiriki siyo yake,
hayapo katika biblia na ukisoma katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana 22:18-20
MUNGU alikataa yasifuatwe tofauti na alivyoandika katika kitabu chake, ila yeye
alijua habari ya huyu mnyama mwenye pembe 10 na vichwa vyake ataleta maneno
mabaya (makufuru) ili atukanwe MUNGU kwa matendo unayoyafanya au kuvunja amri
zake.
2. MAKUFURU
YA MITAMBIKO
Mitambiko yote ni ibada za shetani na yanapofanyika anatukuzwa huyu mnyama kwa sababu unakuwa
umemfuata huyu mizimu wakati huo na
kisha unaenda kanisani, hapo wewe unakuwa ni mnafiki mbele za MUNGU bali Bwana
wako anakuwa huyu mnyama katika
ulimwengu wa roho pasipo wewe kujua wala kupenda na unakuwa unayo namba 666. Hivyo
ni vizuri uombewe, utubu na uache hiyo namba 666 ikutoke kwa jina la YESU WA
KWELI kwa sababu yupo yesu wa uongo pia; yeye yupo chini ya huyu mnyama
aliyepewa amri ya kuwateka wanadamu ambaye ndiye mpinga kristo na kusababisha
katika ulimwengu huu kumetokea ukristo wenye mbili ambao ni ukristo wa kweli na
ukristo wa uongo.
3. MAKUFURU
YA UKRISTO WA UONGO YAKOJE?
Kila kiumbe kinajua kuwa YESU
yeye ndiye njia ya uzima na kweli na yeye ndiye Nabii ambaye ameteuliwa na
MUNGU aliyeumba vitu vyote ya kuwa ndiye atakayekuja katika unyakuo na katika
kutoa hukumu ya kiama au kwa lugha nyingine anaitwa Nabii Issa. Hapa ndipo
lilipoanza chimbuko la kuongezeka ukristo wa pili ambaye ndiye wa uongo upo
tofauti na lilivyo neno la MUNGU likachanganywa na uongo, ikawa injili ya namna
nyingine soma Wagalatia 1: 6-9 na injili hiyo ya tofauti inawafanya watu
wanaoipokea walaaniwe. Makufuru haya ndiyo maneno ya kumtukana MUNGU pale
yanapochanganywa na neno la kweli au kutumia biblia ikisomwa kanisani halafu
mmeamua kuchangisha pesa katika nyumba ya sala au ili uombewe unadaiwa pesa
kwanza umpe pastor ndiyo maneno ya kumtukana MUNGU sababu yapo kinyume na yeye,
siyo yake. Utajiuliza sasa mbona hayapo katika biblia sasa yanatokea wapi na ni
wapo shina lake au mafunuo hayo yanatokea wapi na yapo kinyume na neno la
MUNGU.
Ukisoma katika kitabu cha Ufunuo
wa Yohana 22:18-20 inaonya usiongeze neno lolote; MUNGU akijua huyu mnyama
ataleta injili yake ya tofauti ataichanganya neno lake; hapa mwenye akili na
aelewe. Siyo kila mtumishi anayesoma biblia kanisani anatumiwa na MUNGU, wengi
zaidi wameongozwa na huyu mnyama na tayari wanazo namba 666 na wewe muumini
unapoabudu hapo namba hiyo inakugonga katika ulimwengu wa roho pasipo wewe
kujua wala kupenda kwa sababu ya matendo haya:
1. Ubatizo
wa kikombe, ubatizo wa kisima, kubatizwa kwa jina la mchungaji. Ubatizo wa
kisima; unaweza kisima kukaa karibu na madhabahu ndani au likawa nje ya kanisa.
Hili ni kufuru la huyo mnyama na hapo umepokea ubatizo wa makufuru haujatokea
kwa MUNGU. Je umetokea wapi? Haijulikani. Hivyo yule mnyama ndivyo anavyomuaga
hizo za batizo tofauti na biblia na watumishi baadhi wakatawaliwa na namba 666.
2. Kuomba michango
ya TV, radio, imeadikwa usifikirie nini nitatenda; unapoona hivyo uelewe ni ile
roho ya mnyama hayo ni maneno mabaya ya kuharibu ahadi za MUNGU
3. Kuandika
sadaka majina, kupewa risiti, kusomwa jina umetoa vizuri; unapewa cheti cha
hongera unakuwa mtoaji bora. Ni makufuru ya huyo mnyama na ndiye anayewapa
nguvu na hii inawafanya ulimwengu kutekwa na shetani 98% kwa sababu ya makufuru
ya huyu mnyama.
4. Huduma zenye
kuongozwa na huyu mnyama, kuhani anakuwa ni mzinzi kisiri au hata kiwazi wazi bila hofu; pasipo
kuangushwa na shetani katika dhambi ya uzinzi, anakuwa ni mlevi, anajisifia
sana, anatenda miujiza ya kipepo, anaweka bendera au kujenga minara yake; ile
minara ni vichwa vya huyu mnyama vinampa mawasiliano ya nini cha kufanya,
wengine wapo katika chama cha freemason hata sasa majina yao yapo waziwazi. Habari
zaidi ni pesa na mengineyo ambayo hayampendezi MUNGU hufanyika hapo. Zaidi hupenda
kufanya maagano ya makafara ya uzinzi, kuosha waumini miguu badala ya watumishi
wa MUNGU.
NOTE:
Yapo mengi ila zaidi endelea
kusoma blog hii na kutumia wengine wapate kusoma ili wasiongozwe tena na makufuru
ya huyu mnyama.
Mrejee YESU wa kweli; sema
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, hata pale nilipokutukana wewe
MUNGU wangu kupitia kuyatenda mambo yasiyokupendeza wewe au kupokea mafundisho
kinyume na sheria zako. Ninamkataa huyu mnyama mwenye vichwa 10 na mambo yake
yote ya uongo yanayompinga kristo. Futa jina langu kwenye kitabu cha hukumu
andika jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Nakupenda BWANA
YESU, niongoze mahali ambapo hakuna makufuru, mahali ambapo wewe MUNGU wa kweli
upo. Amen.
MUNGU AKUBARIKI.
NABII HEBRON.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni