Wafilipi 2:10-11
  •  LIJUE KANISA ALILOLIJENGA YESU KRISTO WA NAZARETI ALIVYOKUWEPO HAPA ULIMWENGUNI 

    Welcome to Prophet Hebron blog

    KITABU: LIJUE KANISA ALILOLIJENGA YESU KRISTO WA NAZARETI ALIVYOKUWEPO HAPA ULIMWENGUNI


    

    TOLEO LA SABA

    ISBN 978 – 9987- 9553-6-7

    UTANGULIZI

    Ndugu nakusalimu kwa jina la YESU KRISTO, ambaye ndiye BWANA na mwokozi wa mataifa yote, pia ndiye mfalme wa wafalme na bwana wa mabwana na hapana mfalme mwengine zaidi yake. mimi jina langu naitwa Hebron Wilson Kisamo, YESU amenichagua nimtumikie yeye kwa jinsi anavyotaka yeye ili kuukomboa ulimwengu huu ambao umepotea na shetani ameumiliki kwa asilimia 98% sawa sawa na YESU alivyoniambia mwenyewe. Amenituma ulimwenguni kote ikiwa ina maana nchi zote, mabara yote. Ujumbe huu aliniagiza rasmi na kunipa mamlaka yake tarehe 14.6.2010. Na akanipa jina la kanisa lake niliite YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRY. Akaniambia mwanangu nitautumia huu mwili wako kuukomboa ulimwengu wote, utachukiwa sana, utafanyiwa na kuitwa majina mabaya lakini usiogope tena ufurahi zaidi, kwani mimi YESU walinifanyia mabaya zaidi na ya uongo yakitokea kwa baba yao wa uongo ambaye ni lusifa, nilifurahi daima. Hakuna jambo lolote litakalofanikiwajuu yako au silaha yoyote juu yako nipo na wewe milele. Nitakutumia kwa namna ya tofauti na kwa kiwango kikubwa sana ambacho hakijaonekana tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu. Adui yako ni adui yangu, akasema YESU kwa sauti ya uchungu sana, watumishi wamenisaliti maagizo niliyowapa hawayafanyi na wamegeuza neno langu kuwa maandiko badala ya neno, maandiko yanatoka kwa shetani maana lusifa anaijua bibilia yote na maandiko hayana uthibitisho wa nguvu zake YESU. Neno linatoka kwa YESU na linaudhihirisho wa nguvu za MUNGU. Na pia wana wa adamu wanateseka wanalia na kuomba hawapati majibu, na zaidi wanazidi kupotoshwa na viongozi wa kanisa, maagizo niliyoyaacha nilivyokuwa ulimwenguni kabla ya kurudi kwa BABA yangu ili kuniandalia maandalizi ya ujio wangu ili nipate kuwaponya wengi waende mbinguni, imekuwa kinyume idadi kubwa ni ya watu wa shetani. Waliokuwa watumishi wangu wamenisaliti 98% sipo nao. Wameamua kwenda kuzimu, na shetani anawatumia na jinsi anavyowatumia, ni kubadili au kwenda kinyume na agizo la MUNGU, mfano watumishi kwa sasa wamefanya kanisa ni mahali pa biashara, kunyanganya watu vitu vyao na wakijua wananitolea mimi, na kufanya mimi YESU ndiye mnyanganyi, kwa midomo yao hunitaja kama wananipenda ila mioyoni mwao hawapo na mimi, wamekuwa watumishi wa pesa na siyo mimi, wamekuwa wakitenda miujiza lakini siyo yangu ni miujiza ya shetani, na hao ni kati ya wale ambao siku ya mwisho nitawakataa na kuwaambia sikujui. Kanisa limeniacha kunitegemea mimi, imebaki 2% tu ulimwengu mwote. Sasa mimi YESU ninalikomboa kanisa mwenyewe na ndipo unabii na utukufu wa kanisa la mwisho utakuwa mkubwa kuliko wa kanisa la kwanza unatimia sasa.

    SHUKURANI

    Namshukuru mke wangu sana kwa kunitia moyo na kuniombea, nawashukuru watumishi wote wanaoniombea na kutumiwa na MUNGU kutumika pamoja na YESU aliyeniita, mkono wa MUNGU uwe juu yao siku zote za maisha yao.

    Asante.

    MTUME NA NABII- HEBRON WILSON KISAMO

    KIONGOZI NA MWANZILISHI WA HUDUMA

    KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRY.

    P.O.BOX 13657

    ARUSHA, TANZANIA

    EAST AFRICA

    EMAIL:        maombi@prophethebron.org

    WEBSITEwww.prophethebron.org

    BLOG:        prophethebron.blogspot.com

    NAMBA ZA SIMU: 


    +255 764 042 149

    +255 759 610 820

    +255 718 916 864

    +255 718 154 433




    YALIYOMO.

    1.     JUA KANISA ALILOJENGA YESU KRISTO WA NAZARETI ALIPOKUWAMO ULIMWENGUNI

    2.     KANISA ALILOLIJENGA YESU WANAZARETI

    3.     UTALITAMBUAJE  KANISA LIMEJENGWA NA YESU WA NAZARETI

    4.     KANISA AMBALO HAJALIJENGA YESU

    5.     NUKUU YA YESU KRISTO WA NAZARETI

    6.     SALA YA TOBA

    7.     KUMBUKA




    1.  JUA KANISA ALILOJENGA YESU KRISTO WA 

        NAZARETI ALIPOKUWAMO ULIMWENGUNI

    Ndugu msomaji wa kitabu hiki cha Nabii Hebron, nakusalimu katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti ambaye ndiye BWANA na mwokozi wa mataifa yote na ndiye mwana wa pekee wa MUNGU aliye hai, aliyetumwa kuja hapa ulimwenguni kutukomboa na kulijenga kanisalake ambalo milango ya kuzimu haitaliweza.

    BABA katika jina la YESU KRISTO aliye hai, naungana na serikali yako ya Mbinguni inayofanya kazi pamoja na mimi ambayo umenikabidhi kwao, nawafungua fahamu zao wanadamu hawa wote na masikio yao na macho yao yaliyopofushwa ili wazubae mpaka ule mwisho shetani awafanye mateka wake, kuanzia sasa kila anayesoma hatakuwa mateka wa shetani, isipokuwa tu wapo wale walioandikiwa jehanamu hiyo haitabadilika lazima NENO la MUNGU aliye hai litimie  hilo halipingiki.

    Ndugu msomaji na muumini wa YESU KRISTO aliye hai na pia muumini wa yesu kristo wa uongo leo utafunguka. Inawezekana haujielewi unaburuzwa tuu na wewe unampenda YESU KRISTO wa Nazareti, siku ya leo utaujua ukweli kwa 100% na utapona. Fungua katika kitabu chako kitakatifu katika injili ya Mathayo kitabu cha ( 16: 13 -19.) Basi YESU akaenda pande za kaisaria –Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema; watu hunena u Yohana mbatizaji, wengine Eliya,wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Akawaambia ninyi mwaninena mimi kuwa ni nani? Simon Petro akajibu akasema, wewe ndiwe KRISTO mwana wa MUNGU aliye hai. YESU akajibu akamwambia, heri wewe Simon Bari-Yona, kwa kuwa mwili na damu havikufunuliwa hili; bali BABA yangu aliye Mbinguni. Nakuambia wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu wala malango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni, na lolote utakalolifunga  Duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, na lolote utakalolifungua Duniani  litakuwa limefunguliwa Mbinguni.


    Ndugu msomaji kupitia kitabu cha MUNGU ambacho ndicho kiongozi cha YESU KRISTO wa Nazareti, unaona hapa hata zamani zile wengi hawakumjua YESU kwa ukamili wengine walifikiri ndiye Eliya, wengine Yohana mbatizaji na wengine Yeremia. Ila mmoja wa wanafunzi wake Simon yeye YESU akamuuliza je, wewe wasema mimi ni nani? Petro akasema wewe ndiwe mwana wa MUNGU YESU KRISTO aliye hai. YESU akamwambia heri wewe uliye funuliwa siri hii, nami nakuambia wewe ndiwe mwamba na ndani yako nitalijenga kanisa langu ambalo milango ya kuzimu haitaliweza na nitakupa funguo zenye mamlaka yangu.

        Ndugu msomaji mpaka sasa umejua na kutambua ni kanisa lipi   

        alilolijenga YESU ndani ya Petro. YESU alijenga kanisa lake ndani

        ya Petro na sio jengo wala dhehebu. Siku hizi imekuwa kama  enzi  

        zile tuu, alivyokuwepo hapa ulimwenguni watu wanabahatisha au   

        kubuni, kubuni kwenyewe watu wanaangalia dhehebu na jengo

        wakifikiri kuwa hivyo ndivyo YESU alivyovijenga na ndivyo          

        atakavyokuja kuvichukua. Ndugu msomaji hapo umepotea kabisa  

        ila leo utaelewa haya yaliyofichika na utafunguka  sawasawa na   

       YESU alipomwambia Petro, heri yako wewe uliyefuniwa haya.

    Ndugu msomaji, natumaini unazidi kunielewa na wala sio mimi  Hebron ninaye kuelewesha haya ni MUNGU aliye ndani yangu ndiye anayekufunulia haya yote ili upone na umjue yeye maana wengi wapowapo tuu wakidhani wanamjua YESU wa kweli kama Petro ila wanabahatisha,  huu siyo wakati wa kubahatisha tena, maana katika ulimwengu huu asilimia kubwa zaidi umepotea imebaki asilimia 2 % tu kwa ulimwengu wote, ndio wanaomjua YESU wa Nazareti, ila sasa mtamjua mengi zaidi na ndivyo alivyoniambia na akisema ndivyo ilivyo yeye ndiye mwenye mamlaka kuliko vitu vyote na kipitia mamlaka yake atafanya yeye ajuavyo kulijenga kanisa lake na mtu amjue kama Petro alivyomjua yeye.

    Ndugu msomaji, nataka utambue sheria zote na mipango yote iliyoandikwa katiaka kitabu cha BIBLIA , hayo yote yameamriwa na kanisa la mbinguni yafuatwe na ndiyo maana wakatumwa manabii kuja hapa ulimwenguni ili kutujulisha uelekeo wa kufuata anavyotaka MUNGU aliye hai, alimtuma Yohana mbatizaji, Eliya,Yeremia, Musa,Isaya na wengine wengi ili kulijenga kanisa na kutufundisha, na ajabu hayo walioambiwa na kanisa la Mbinguni yote yapo katika BIBLIA,MUNGU anataka kanisa alilolijenga mtoto wake ambalo asili yake lipo Mbinguni, yafuatwe yaliyoandikwa katika kitabu chake Kitakatifu na ndiyo maana kwa hasira MUNGU akasema katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana 22: (18-19), Inasema hivi, namshuhudia  kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, mtu akiyaongeza MUNGU atamuongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, MUNGU atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu,ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki. MUNGU alivyoyasema haya inamaana hayo yaliyoongezwa hayataki na siyo yake na hakuna atakayeweza kumsadia MUNGU kazi, yeye amekwisha sema hapana ni hapana, hana majadiliano mlio haribu au kwenda kinyume  sawa sawa na NENO la MUNGU katika kitabu cha Ufunuo 22: (18-19) yatatimia na kwa wengine tayari yametimia. MUNGU siyo mtu hata aseme uongo.

    Nafikiri wengi sasa mnajiuliza sasa je! Ni kanisa  lipi YESU alilolijenga na nilipi ambalo hajalijenga yeye nakama hajalijenga yeye ni lipi? Sasa utalijua vizuri 100% na nitatumia mifano iliyoandikwa katika BIBLIA ambapo kila mtu ndio anajua mambo ya YESU wa Nazareti na kimepigwa muhuri Mbinguni ikimaanisha ni sahihi.

     

     

    2.  KANISA ALILOLIJENGA YESU WA NAZARETI

    Kanisa alilolijenga YESU KRISTO wa Nazareti ndani  ya Petro (Mwamba) ndilo kanisa lililopo mbinguni lenye mamlaka na lisiloshindwa na milango ya kuzimu na linaushirika 100% na kanisa la mbinguni,nafikiri wengi wenu mmesikia mbinguni Malaika , Makerubi, Maserafi , Wazee 24 na waliopo paradiso wote wanamsifu MUNGU na kumwimbia na kumwabudu muda wote,Ewe mwanadamu zidi kuelewa hilo ndilo kanisa la mbinguni na ndio maana wale watakaoshinda, imeandikwa hapa duniani mtapelekwa alipo MUNGU nao wataendelea kumsifu MUNGU aliye hai milele na milele, na kanisa hili nililiona mbinguni na jinsi wanavyofanya kwa MUNGU aliye hai na kuna Petro na wenzake nimewaona wanayofuraha ya ajabu mbinguni ila wanahuzunika jinsi kanisa lilivyogeuka au kutekwa na shetani, maana kanisa alilolijenga YESU KRISTO wa Nazareti 98%, Pia kumbuka yeye mwenyewe alivyokuwepo hapa ulimwenguni alikwisha tabiri na kusema watatokea makristo wengi wa uongo nao watawateka hata wale walio wateule wakitumia jina lake na ndiyo maana YESU alisema msiziamini kila roho bali zichunguzeni,je zinatoka kwangu ( soma Mathayo 24:4-5). Kanisa aliko lijenga YESU KRISTO wa Nazareti lilipewa amri kumi za MUNGU. Soma katika kitabu cha kutoka 20 chote utayaona na aliyepanga amri hizo ni MUNGU mwenyewe ambaye na mbinguni analo kanisa lake akimaanisha na hili lililojengwa juu ya Petro, liyafuate hayo yote ila siku hizi imekuwa kinyume, makanisa yanatumia jina la YESU na kumwabudu MUNGU huyu huyu aliyekataa, mfano wa amri mojawapo, msiabudu sanamu au kitu chochote alichokiumba yeye; nikuulize swali ndugu msomaji, je unaamini huyu MUSA aliyeandika amri hizi alitoka kwa MUNGU na MUNGU ndiye aliyemtuma na kumpa hizo amri10 kwa ajili yetu na kwa ulimwengu wote na kwa watu wote? Jibu ni ndiyo . Na kama ni ndiyo je kwa nini unaabudu sanamu au kuvunja amri zake? Ina maana humtaki huyu MUNGU aliyehai na umezipuuzia amri zake, na hana dhamani kwako, basi na yeye amekuacha hayupo na wewe maana hayo siyo yake.

    Kanisa alilolijenga YESU kwanza linafuata taratibu zote alizoziacha zifuatwe hapa ulimwenguni, ndizo alizoambiwa na BABA yake MUNGU wa Ibrahimu na Isaka , mfano katika kanisa la Mbinguni

    baraka hutolewa burebure na lililopo duniani ambako ndiko alikolijenga ndani ya Petro linayafanya hayo, Ubatizo wa maji mengi ndivyo ilivyoamriwa na MUNGU  na akipanga MUNGU mwanadamu ni nani mbele za MUNGU ategue anayoyataka MUNGU? Kanisa alilolijenga YESU hulijenga ndani ya mtumishi anayesimama katika kanisa jengo yeye ndani yake huwekwa mamlaka ya MUNGU na YESU mwenyewe hukaa ndani yakekama ilivyokuwa kwa Petro nyakati zile.


    3.  UTALITAMBUAJE  KANISA LIMEJENGWA NA  YESU  WA NAZARETI

    Ndani ya huyo mtumishi huyafanya mapenzi ya MUNGU tuu na siyo ya shetani maana yeye ameolewa na bwana mmoja, sisi sote ni bibi harusi wa YESU KRISTO wa Nazareti ila wengine ni bibi harusi wa yesu wa uongo. Nyumba ya Ibada siyo soko au mahali pa michango tuu ya pesa, kujenga Bar, Guest house na Bank. Hayo YESU alipokuwa hapa ulimwenguni aliyakataa na sasa yamerudishwa. Soma Marko(11:15-18). Fuatilia maisha ya Petro katika kitabu cha nyaraka za MUNGU Petro ambaye ndani yake lilijengwa kanisa hakufanya hayo, na ni mwanafunzi wa YESU alifundishwa pia na mwalimu wake yaani  YESU, sasa nikuulize swali kama huyu mwanafunzi ambaye  ndiye YESU alilijenga kanisa ndani yake na kumwita jiwe,aliyafuata aliyoagizwa wala hakwenda kinyume, je nyie mnokwenda kinyume , je nyie ni wanafunzi wa YESU wa kweli au mmekuwa waasi wa YESU na kama mmemwasi YESU na yeye anakuacha na kukuhukumu. Nitatoa mfano katika jeshi lolote huwa lina sheria zake na mwanajeshi anavyoasi hukamatwa na kuhukumiwa, hivyo ndivyo ilivyo na kwa watumishi wanaokwenda kinyume na YESU, pia watahukumiwa, na nitatoa mfano mwingine katika jeshi, wale wako katika jeshi sio wote ni wanajeshi kamili walioapa kikamilifu, wengine ni wanamgambo, wengine ni kikundi cha ugaidi tuu na wengine hawana wito ila kwa sababu ya kupata mshahara mwisho wa mwezi, huamua tuu kujiunga ila ndani yao hamna uchungu wa kuipenda hiyo jeshi, wao wapo kimaslahi tuu. Kwa nje ni wanajeshi ila ndani ya mioyo yao sio wanajeshi ni waharibifu tuu na wakipewa pesa ili waliasi jeshi hilo wao huchukua pesa na kuasi na kuliyumbisha jeshi na wale walio wanajeshi waaminifu, wao hutii sheria zote hata wakihongwa mamilioni wao wanao msimamo wala hawasikilizi mashauri yoyote yale tofauti na yale ya jemadari mkuu wao. Ila wale waliojilazimisha au kujiita wanajeshi au kujifanya wanajeshi hao ndio huwa  waasi  wa jeshi hilo na pia kuna wengine utakuta ni mwaminifu alipoanza, ila hili kundi la wasio waaminifu linamnajisi na kuvunja amri za jeshi na sababu kubwa ni tama ya pesa na maisha ya hapa duniani. Nitaendelea tena kutoa mfano wa pili na nitamalizia na mfano wa tatu ndio pointi yenyewe ili uzidi kuelewa vizuri. Mbinguni hapo awali lusifa ambaye baba yake ndiye joka kuu alikuwa malaika mkuu mwanzoni yeye aliyasikiliza na kuyatii yale yote ya jemedari mkuu yani MUNGU, ila baadaye akamuasi MUNGU na kutaka kumpindua na mimi wakati MUNGU akinifundisha haya nikamuuliza MUNGU wangu ni vipi huyu shetani alikukosea? MUNGU akaniambia siku moja nilimjaribu nikamwambia embu kaa hapo kwenye kiti changu nikasimama, kisha nikamwambia amka nipishe nikae, shetani alikataa ndipo pakatokea vita mbinguni jeshi lile la malaika watakatifu wa MUNGU wakampiga na kumtupa ulimwenguni humu na robo ya malaika waliokuwa sio waaminifu kwa jemedari mkuu  yani MUNGU. Hivyo hivyo na sasa watumishi wengi sana wamekuwa waasi wa YESU, hawasemi kweli ni wachawi kiwango cha kutisha ni waovu,wanauza madawa ya kulevya,walevi, wanazaa na waumini, hawabatizi ubatizo wa kweli huo ni uasi na watumishi wanaofanya hayo tayari ni waasi.

    Fomula hiyohiyo aliyotumiwa shetani na malaika zake ndivyo  hivyo na kwao, mimi siongezi lolote nasema kama YESU alivyoniambia na siogopi lolote na wala hakuna atakayenizuia kusema kweli yake mpaka atakaporudi na milele, na ameniambia  “Hebron usiogope” mwanadamu yeye ni nani hata ashindane na mimi? Hamna pa kukimbilia kila mahali yeye anafuatia na zaidi akaniambia Hebron sio wewe uliyejiita uje unitumikie ni mimi MUNGU wako niliyekuumba nimekupenda ulivyo na nikusudi langu wewe uzaliwe hapa ulimwenguni, ingekuwa umejiita mwenyewe, hao waasi wangesha kuuwa, ila ni mimi na nimekushika mkono naishi ndani yako na ili mtu au adui akuweze wewe ni mpaka apigane na mimi MUNGU aniweze ndio atakuweza wewe, akaniambia na haitakaa iwezekane mimi ni MUNGU nisiyeshindwa na sita shindwa milele, anayepigana na wewe anapigana na mimi. Niliogopa sanakwa sauti ya ukali aliyozungumza nayo,Hebron waokoe wanangu, wamefanywa kuwa punda, sikuwaumba wateseke wamebebeshwa mizigo. Itoe yote wawe huru, walioniasi wanawafanya punda kuwabebesha madeni yao; Ndio upunda huo. Wakati imeandikwa nyumba ya baba yangu ni mahali pa kutua mizigo yao ila wanapokuja kanisani ni kubebeshwa majukumu ya kuahidi pesa, amesema yeye sio shirika au taasisi ya kuwawekea mizigo, na mizigo hiyo haitoki kwake. Kanisa lililojengwa na YESU lina upendo halina ubaguzi, halina vikundi vya partners, halichangishi michango wala harambee, maana kama ni yeye kalijenga mambo yote hufanya yeye mwenyewe maana linawasiliana na Mbinguni na kanisa la mbinguni huachilia baraka ndani ya kanisa hilona mambo huendelea vizuri. Ila kanisa ambalo hajalijenga YESU linaacha kumuuliza yeye na kuwatuma waumini na kuwafanya punda kama ilivyo wengi katika ulimwengu huu, wamefanywa punda na matokeo yake ni ukristo wa uchovu tuu, hamna baraka za Mbinguni ni baraka za kanisa ambalo hajalijenga YESU na wewe unapeleka huko ambako sio YESU amelijenga kanisa hilo, na kama sio yeye aliyelijenga unafikiri ni nani kalijenga? Jibu ni la shetani japo jina lake  linatajwa. Alisha sema watatokea manabii wa uongo, hawa huyapinga yale ambayo MUNGU aliyelijenga kanisa hilo ndani ya Petro lenye nguvu na matokeo yake mnapigwa na shetani kamaulivyoteseka na upo kanisani! Nikuulize swali je kama wewe upo kwenye kanisa alilolijenga YESU shetani atakutesa? Jibu ni hapana.Funguka ufahamu wako usiwe punda tena, MUNGU  amekasirika na yeye anawatoa mizigo maana hamkuja hapa duniani na mizigo na yeye sio MUNGU wa kuwabebesha mizigo, tena imeandikwa, njooni kwangu enyi nyote wenye kulemewa na mizigo naye atawatua mizigo. Hilo ndilo alilolijenga YESU ila kanisa ambalo hajalijenga yeye mnabebeshwa mizigo mnapokuwa makanisani, mwisho wa ibada au kati ya ibada wanajiandaa kukusanya madeni au kuwaambia kila mtaa mtoe kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya jambo fulani, jamani huo sio mzigo? Jibu ni mzigo unawekwa juu yako kama punda. Kwani hizo sadaka ulizotoa zinafanya nini?

    Ndugu msomaji  huyo siye MUNGU anayefanya hayo, wamrudie MUNGU wa kweli naye atafanya. Alikuja YESU akateseka ili muwe na uzima na amani na furaha na huru katika kumuabudu yeye na mizigo aibebe yeye ila sasa kanisa limekuwa kinyume ambalo ndilo hajalijenga YESU linawakaba koo waumini na kuwawekea madeni na kuwalazimisha kuahidi utatoa ngapi wewe, fulani haya andika hapa na kupiga saini; jamani huu ni wizi , kanisa imekuwa kama upo mahakamani unasema kitu na kusaini ili usipotekeleza ufuatwe! Na kuna wakati YESU alisema ya kaisari mpe kaisari na ya MUNGU mpe MUNGU, embu ona leo hii mambo ya kaisari yanaingizwa kanisani, je hii ni sawa? Au huu ni uungwana? Jibu sio sawa na sio uungwana kumfanyia MUNGU mambo ya kaisari na wanayoyafanya ya kaisari katika kanisa, kanisa hilo linaongozwa na kaisari na wala siyo yeye MUNGU aliye hai, jambo la kwanza hawana MUNGU wa kweli aliyemwaminifu ndio maana unasainishwa ujifunge huo mzigo kama punda, MUNGU anachukizwa sana, haswa hizo harambee na kuambia, harambee zote zilizowahi kufanyika katika makanisa yote ulimwenguni hiyo ripoti haipo mbinguni ipo kuzimu, huo ndio ukweli.

    Endelea kufuatilia mafundisho ya Nabii Hebron nawe utajua ukweli pia pata matoleo ya vitabu nilivyoandika utajifunza mengi kuhusu YESU na utapona na utaenda mbinguni ukiyatii hayo maana pia siyo yangu mimi ni ya MUNGU aliyenituma kwa ulimwengu wote, watu wamjue yeye tuu ndiye mtawala wa kila kitu kilichopo ulimwenguni mwote na ataukomboa na kazi ndio nimeianza na haitasimama mpaka nimalize , anaifanya peke yake MUNGU na kuyatimiza makusudi yake.


    4.  KANISA AMBALO HAJALIJENGA YESU

    Ndugu msomaji    natumaini unazidi kuelewa na kufunguka kuhusu kanisa alilolijenga YESU na kanisa ambalo hajalijenga YESU . Nitaeleza kwa kifupi tu ili watu mpone na inawezekana na wengine ni watumishi hawajielewi wapo wapo tuu au wameshapotea ila wapo waasi wa YESU ambao wengine walijiingiza katika kazi ya MUNGU kwa kutumia uchawi na kutumia jina la YESU kuwatapeli watoto wa MUNGU wakijijua kabisa wanafanya nini, hao yale mapigo yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Injili yani BIBLIA yanawahusu na hakuna pa kukimbilia, MUNGU hakimbiwi, kumbuka Yona alifika wapi? Na wengineo waliopita na waliopo,hata kama mnaulinzi wa kipepo au kibinadamu MUNGU anawafikia tuu, huwa anawashangaasana wanadamu . Njia za MUNGU sio za wanadamu njia zake wala mipango yake haielezeki anaijua yeye mwenyewe.

    Ø Kanisa ambalo halibatizi ubatizo aliouacha yeye, kanisa hilo hajalijenga yeye na yeye sio mmiliki wa kanisa hilo, hata tafuta katika kitabu cha BIBLIA hauta uona ubatizo mwingine zaidi ya wa maji yanayotembea na siyo ya kisima cha kujengwa, tayari kama maji hayatembei hicho siyo kijito cha utakaso, kwa MUNGU hakuna kubadilisha kama alivyopanga, kama wanadamu wanaweza wabadili basi badala ya usiku uwe mchana na mchana uwe usiku au wabadili siku zote pawe ni usiku tuu au siku zote pawe ni mchana tuu.

    Ø Maombezi ya kutoa pesa kwa mtumishi ndio umwone akuhudumie tayari ndani yake hamna kanisa la YESU KRISTO wa kweli, kanisani huduma ni bure ila hospitali ndiyo pesa unalipa, nikuulize swali, je kanisa imekuwa ni hospitali? Jibu ni hapana. Wanaofanya hivyo hao ni waasi wa YESU wa kweli wanaongozwa na yesu wa kuzimu ambaye anashirikiana na kuzimu.

    Ø Makanisa yanayoruhusu na kufungisha ndoa za jinsia moja, mfano mwanaume amuoe mwanaume mwenzake, au mwanamke amwoe mwanamke mwenzake, jamani huu ni uchafu, ni kubadili mapenzi ya MUNGU na makusudi ya MUNGU na yeye MUNGU pia ameshaonya ila yaliendelea . Hao wanaofanya  hayo ni waasi , hawana MUNGU tena.

    Ø Kuabudu sanamu hao wameasi na wanaoshiriki wameendelea kuasi na kupotea, waulize hao waowaongoza mbona imeandikwa hivi katika kitabu cha kutoka 20:(4-5),soma sasa mbona imeandikwa hivi ndugu msomaji , hawana jibu; na usikubali majibu ya tofauti na kwenye BIBLIA ndiyo katiba ya MUNGU kwa kanisa alilolijenga YESU.

    Ø Ukiona ndoa zinafungwa kwa agano la shida na raha ujue siyo kanisa alilolijenga YESU, MUNGU hajawafungia wanadamu shida ni raha tuu, kumbuka Rebeka aliolewa na Isaka alitamkiwa mema tuu naikawani mema tuu siyo shida ( Mwanzo 24:55-59) Uisome utayaona haya.

    Ø Kuandika majina sadaka na nambaza simu na kupewa risiti,hilo kanisa siyo YESU wa Nazareti amelijenga. Kanisa alilolijenga yeye imeandikwa utoapo sadaka yako, kushoto wala kulia isijue, sasa unaona tayari hapo ni kinyume na alivyoamuru YESU wa Nazareti.

    Ø Kukopa pesa benki kwa ajili ya ujenzi wa kanisa na kulipa riba, nikuulize swali MUNGU hana pesa mpaka akope benki kwa wanadamu? YESU mwenyewe alishakataa ya kaisari mpe ya kaisari ya MUNGU mpe MUNGU. Mahali hapo ni sifuri, mmepoteza muelekeo wa MUNGU mmefuata muelekeo wa dunia  hii au ya kaisari na kila unayeupata ujumbe huu unajua kabisa haya ninayo yasema ni ya kweli unajikausha tuu, watoto wa MUNGU sasa hivi mnajua ukweli tena wanawashangaa tuu wacheni uovu huu. Hizo sizo kazi zake 100% na hukumu ipo juu yako. Unawafanya watoto wa MUNGU kuwabebesha mizigo, MUNGU amesema kuanzia sasa mtoto wake siyo punda tena wa kuwabebesha yale nisiyoyataka mimi MUNGU ole wenu. (Yeremia 29:9) kwa maana kwa jina langu hutabiri maneno ya uongo kwenu mimi sikuwatuma , asema BWANA . Je niwaulize ninyi watumishi BWANA aliwatuma mkakope benki? Mbona mnasema uongo kwa kulitumia jina lake. Zaidi soma kitabu chote cha nabii Yeremia 23: yote utaona na utajifunza MUNGU alivyosema.

    Ø Huduma za uimbaji na nyimbo za injili wale wote mnaovaa mavazi yasiyo ya heshima, nyimbo hizo haijalishi linatajwa jina lake hausiki, jambo lingine staili za kucheza wakati wa kuimba mfano kukatika kiuno kwa namna ile mbaya isiyo ya heshima kama mzinzi, hiyo ni ya kuzimu MUNGU hachezewi hivyo, hiyo ni tabia mbaya hata kibinadamu ukiwa mbele ya baba yako mzazi huwezi kumkatikia kiuno ukiimba kwa staili kama ya uzinzi, je kama kimwili tuu unaogopa na kuona aibu je MUNGU si zaidi?

    Ø Watumishi wote ambao majina yao yapo kwenye mtandao wa freemason na wanahubiri na kufanya miujiza watumishi hao wote ulimwengu mzima hao ni waasi na ni adui wa YESU wa Nazareti na pia MUNGU aliyewaumba, hao hawajajengwa na YESU KRISTO wa Nazareti , wamejengwa na yesu wa kuzimu na kazi yao ni kuwaboa na kuwatesa watoto  wa MUNGU na kuwaibia mafanikio yenu na maisha yenu kuyapeleka kuzimu.  Hao sio watumishi wake kabisa wanaitwa waasi kama vile shetani ila hutumia jina la YESU kama kivuli cha kujifichia sasa muwatambue na muwakatae mpone.

    Ø Ndugu msomaji, unazidi kufunguka, ukikuta upako au nguvu za MUNGU zinauzwa, ujue huyo ni tapeli . Hivi hata kibinadamu je kuna mwanadamu anaeweza kununua nguvu za MUNGU? Jibu hakuna. Ila za shetani zinanunulika kama vile unavyoenda kwa mganga wa kienyeji ambaye yeye hupewa nguvu hizo na shetani ambaye ndiye mungu wao.Uzidi kuelewa  kama nguvu za MUNGU zingekuwa zinanunulika watu wangekuwa wananunua uhai kwa MUNGU na wasinge kufa, ila haiwezekani na haitakaa itokee, yeye mwenyewe amekwisha sema mmepewa bure toa bure,alijua kwamba upako wake haununuliki. Unakuta mtumishi aliye asi kwa MUNGU  anachukuwa uchawi anawauzia, mfano stika eti weka kwenye gari au geti lako, inamaana MUNGU anakaa kwenye stika au kanga au kitambaa? Au kiganja cha mkono wa mtumishi? Nitakueleza kidogo maana ya vitu hivi baadhi, hiyo stika yenye picha ya mtumishi huyo kazi yake ni kukunyang’anya baraka zako ziende kwake na utajiri wako wote, tupa na uchome moto! Ikibidi muulize hii imeandikwa wapi kwenye BIBLIA jibu hana ameyatoa kuzimu. Na mimi nakuambia tupa usiogope MUNGU aliyeniita anakupenda na atakufungua siku ya leo.

      

     

    5.    NUKUU YA YESU KRISTO WA NAZARETI

    Tanzania tunayo neema kubwa isiyoelezeka hata kibinadamu, katika nchi hii MUNGU alimtumia mtumishi wake  MOSES KULOLA kueneza injili ya wokovu wa kweli na mpaka sasa anaendelea kusema kweli, ndani yake MUNGU alilijenga kanisa na akalizaa sasa TANZANIA wokovu umekuwa siyo kitu kigeni kama miaka hiyo ya 50 alivyokuwa akihubiri, Mtumishi huyu nilimuona Mbinguni na makao yake ni mazuri ajabu, aliifanya kazi bila kuasi mpaka sasa na hata asi milele, hayo ameniambia YESU  wa Nazareti aliye hai. MUNGU amembariki yeye na uzao wake na ukoo wake na sasa amemrudishia nguvu upya na kumwinua japo wapo waliotaka kumuua tena ni hao hao aliowazaa baadhi yao wameasi kwa MUNGU ila Neema ya MUNGU ipo juu yake, MUNGU amempenda sana. Msikilizenisana anachosema na wale wote hata aliowazaa na kwa sasa wamemsaliti YESU. MUNGU ameshamwambia kila kitu, msimwone ananyamaza ndani yake YESU wa Nazareti amekaa anatumia kinywa chake na hayo anayoyasema ndio kweli. Mzee huyu hajui hata uchawi, hataki pesa ya mtu alifanya kama alivyoagizwa mpaka sasa ila hata wale aliowazaa asilimia 90 wameasi na yeye anajua, ila sasa anarudi jukwaani kwa nguvu hayo kaniambia MUNGU maana wengine watumishi wanasubiri afe, hivi mtu akisema kweli ya MUNGU wanadamu waovu wanamchukia mtu huyo? Mmepotea mnamchukia MUNGU! Shauri yenu, mimi sipo. Wangeiga kama alivyo fanya oooh ! ingekuwa mbali sana na watanzania wasingeteseka ila  walimwachia mwenyewe wakakimbilia pesa, uchawi, ufreemason, ila sasa wote wenye nia mbaya  na nchi hii mtaaibika, nchi hii ndiyo Edeni na ndio Taifa tajiri kuliko yote na mtayaona . YESU ndiye anayeilinda nchi na kuinua amesema na ameniambia Hebron utayaona , waambie watoto wangu ukweli wanijue na wasijichanganye, endelea kuiombea nchi na viongozi nipo ndani yako. kwa watu weupe ilipoanzia ila sasa hakuna kitu wa kwanza amekuwa wa mwisho na wa mwisho amekuwa wa kwanza, kupitia Tanzania injili yangu itajulikana nao mataifa ni mimi MUNGU nitawaleta kwa wakati wake.

    6:   SALA YA TOBA

     Kwa wewe ambaye haujaokoka soma sala hii:-

    BWANA YESU, nipo mbele zako mbele ya agano la Damu ya YESU, naomba unisamehe dhambi zangu zote, uliandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele, namkataa shetani na kazi zake zote, kuanzia leo mimi ni mali yako YESU, nishike mkono uniongoze milele, Amen. !!


    7: KUMBUKA

    Ndugu msomaji unayempenda YESU KRISTO wa Nazareti, Hakika umelijua na kujifunza kuhusu kanisa alilolijenga YESU KRISTO wa Nazareti alivyokuwa hapa ulimwenguni na akaweka mamlaka yake na funguo za kufungua na kufunga kila kitu hapa duniani na mbinguni. Hilo ndilo alilolijenga ila yakatokea mengi ulimwenguni hapa ambayo hajayajenga yeye na hayana hizo funguo zake bali yana funguo zenye kutu zisizoweza kufungua watoto wa MUNGU wala shida zao na kubakia tuu kuteseka kama punda aliyebebeshwa mizigo na hana wakumtoa mzigo huo, ila sasa mizigo yote ameniagiza niwatoe, nyie sio punda, watu wote wa ulimwengu mzima na hakuna shetani atakayenisogelea wala mtu yeyote, MUNGU ameniambia wapigane na yeye kwanza wakimshinda ndio wataniweza mimi. Na MUNGU akaniambia hamna wa kumpiga wala kumweza yeye milele.Na ndiye aliyenishika mkono, na wewe usiogope, simama imara mwangalie YESU aliye hai na utarithi uzima wa milele.

    Ila na wewe ndugu msomaji,hakikisha umejengwa katika kanisa alilolijenga YESU KRISTO wa Nazareti ili usishindwe na shetani.

    

    Prophet Hebron at 5:25 AM

    Share

     

    Home

    View web version

    About Me

    Prophet HebronView my complete profile

    Powered by Blogger.

    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate