Welcome to Prophet Hebron blog
Home New: Makala muhimu... Kanisa lilivyotekwa, joka kuu sasa lafungwa miaka 1000 Prophet Hebron - Live on Radio Prophet Hebron videos ▼
Tuesday, November 5, 2013
KITABU: UBARIKIO WA KWELI KWA ULIMWENGU WOTE
TOLEO LA 12
NOVEMBER 2013
ISBN – 978-9987 - 9717- 2- 5
UTANGULIZI
Ndugu nakusalimu kwa jina la YESU KRISTO, ambaye ndiye BWANA na mwokozi wa mataifa yote, pia ndiye mfalme wa wafalme na bwana wa mabwana na hapana mfalme mwengine zaidi yake. mimi jina langu naitwa Hebron Wilson Kisamo, YESU amenichagua nimtumikie yeye kwa jinsi anavyotaka yeye ili kukomboa ulimwengu huu ambao umepotea na shetani ameumiliki kwa asilimia 98% sawa sawa na YESU alivyoniambia mwenyewe. Amenituma ulimwenguni kote ikiwa ina maana nchi zote, mabara yote. Ujumbe huu aliniagiza rasmi na kunipa mamlaka yake tarehe 14.6.2010. Na akanipa jina la kanisa lake niliite YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRY. Akaniambia mwanangu nitautumia huu mwili wako kuukomboa ulimwengu wote, utachukiwa sana, utafanyiwa na kuitwa majina mabaya lakini usiogope tena ufurahi zaidi, kwani mimi YESU walinifanyia mabaya zaidi na ya uongo yakitokea kwa baba yao wa uongo ambaye ni lusifa, nilifurahi daima. Hakuna jambo lolote litakalofanikiwajuu yako au silaha yoyote juu yako nipo na wewe milele. Nitakutumia kwa namna ya tofauti na kwa kiwango kikubwa sana ambacho hakijaonekana tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu. Adui yako ni adui yangu, akasema YESU kwa sauti ya uchungu sana, watumishi wamenisaliti maagizo niliyowapa hawayafanyi na wamegeuza neno langu kuwa maandiko badala ya neno, maandiko yanatoka kwa shetani maana lusifa anaijua bibilia yote na maandiko hayana uthibitisho wa nguvu zake YESU. Neno linatoka kwa YESU na linaudhihirisho wa nguvu za MUNGU. Na pia wana wa adamu wanateseka wanalia na kuomba hawapati majibu, na zaidi wanazidi kupotoshwa na viongozi wa kanisa, maagizo niliyoyaacha nilivyokuwa ulimwenguni kabla ya kurudi kwa BABA yangu ili kuniandalia maandalizi ya ujio wangu ili nipate kuwaponya wengi waende mbinguni, imekuwa kinyume idadi kubwa ni ya watu wa shetani. Waliokuwa watumishi wangu wamenisaliti 98% sipo nao. Wameamua kwenda kuzimu, na shetani anawatumia na jinsi anavyowatumia, ni kubadili au kwenda kinyume na agizo la MUNGU, mfano watumishi kwa sasa wamefanya kanisa ni mahali pa biashara, kunyanganya watu vitu vyao na wakijua wananitolea mimi, na kufanya mimi YESU ndiye mnyanganyi, kwa midomo yao hunitaja kama wananipenda ila mioyoni mwao hawapo na mimi, wamekuwa watumishi wa pesa na siyo mimi, wamekuwa wakitenda miujiza lakini siyo yangu ni miujiza ya shetani, na hao ni kati ya wale ambao siku ya mwisho nitawakataa na kuwaambia sikujui. Kanisa limeniacha kunitegemea mimi, imebaki 2% tu ulimwengu mwote. Sasa mimi YESU ninalikomboa kanisa mwenyewe na ndipo unabii na utukufu wa kanisa la mwisho utakuwa mkubwa kuliko wa kanisa la kwanza unatimia sasa.
SHUKURANI
Namshukuru mke wangu sana kwa kunitia moyo na kuniombea, nawashukuru watumishi wote wanaoniombea na kutumiwa na MUNGU kutumika pamoja na YESU aliyeniita, mkono wa MUNGU uwe juu yao siku zote za maisha yao.
Asante.
MTUME NA NABII- HEBRON WILSON KISAMO
KIONGOZI NA MWANZILISHI WA HUDUMA
KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRY.
P.O.BOX 13657
ARUSHA, TANZANIA
EAST AFRICA
EMAIL:maombi@prophethebron.org
WEBSITE: www.prophethebron.org
BLOG: prophethebronblogspot.com
NAMBA ZA SIMU:
+255 764 042 149
+255 759 610 820
+255 718 916 864
+255 718 154 433
YALIYOMO
1. UBARIKIO NI NINI
2. UBARIKIO WA KWELI
3. UBARIKIO WA UONGO
4. FAIDA ZA UBARIKIO WA MAPNGO WA MUNG ALIYEHAI
5. HASARA ZA KUBARIKIWA KINYUME NA MPANGO WA MUNGU ALIYE HAI
6. JINSI MUNGU ANAVYOTAKA TENDO LA UBARIKIO LIFUATWE
7. UBATIZO WA WATOTO WADOGO MWISHO
8. SALA YA TOBA
9. KUMBUKA
1. UBARIKO NI NINI
Ubarikio ni kiapo kizuri kutoka kwa MUNGU aliye hai ikuwa ina maana baraka kutoka kwake au kuthibitishwa na MUNGU yale mema na mazuri yawe juu yako au maana nyingine ubarikio ni kukabidhiwa kwa MUNGU katika madhabahu ili uwe wake na yeye akumiliki na ili sababu ya huyo aliyewekewa wakfu, makusudi ya MUNGU yatimie kwake kwa sababu ile mwanadamu aliyezaliwa hapa ulimwenguni huwa amepangiwa na MUNGU makusudi yake ayafanye katika ulimwengu huu na siyo makusudi ya shetani mtu aje ayatende hapa ulimwenguni.
Na maana nyingine ya ubarikio au kubarikiwa ni kupitishwa na MUNGU ya kuwa unafaa au linafaa:
mfano soma (Mwanzo 1:27-31)MUNGU akamuumba mtu kwa mafano wake, kwa mafano wa MUNGU alimuumba mwanamume na mwanamke aliwaumba. MUNGU akawabariki, MUNGU akawaambia zaeni mkaongezeke makijaze nchi na kuitiisha, mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
MUNGU akasema na tazama nimewapa kila mche utoao mbegu ulio juu ya uso wa nchi yote pia na kila mti ambao matunda yake yanambegu , utakuwa ndio chakula chenu, na chakula cha kula wanyama wa nchi wenye uhai, majani yote ya miche ndicho chakula chenu ikawa hivyo.
MUNGU akaona kila kitu alichofanya na tazama ni chema sana ikawa jioni, na asubuhi, siku ya sita.
Ndugu msomaji natumaini unaelewa sasa maana ya ubarikio au kubarikiwa; Ni kudhibitishwa na MUNGU unafaa na baraka zake ziwe juu yako au kama vile mimea yote na wanyama wote alivyovibariki ili vifae kwa chakula cha wanadamu. Na ndiyo maana sisi wanadamu tunakula na tumekuwa na afya na tunaishi, sababu kubwa ni vyakula tunavyokula amevibariki au kuvitakasa vifae kwa ajili yetu kinyume na asingevibariki visingefaa kwa chakula cha wanadamu.
2. UBARIKIO WA KWELI
Ubarikio wa kweli kwa wanadamu wote wa ulimwengu huu ni ubarikio ambao alibarikiwa YESU wa Nazareti alipokuwa mtoto mdogo na ni ubarikio ambao hata ukisoma katika kitabu cha Biblia kupitia Nabii Isaya utaona YESU huyo alivyobarikiwa na hapa tunasoma katika kitabu cha Luka 2:25 Na tazama pale Yerusalemu palikuwa na mtu jina lake Simeoni naye alikuwa ni mtu mwenye haki, mcha MUNGU akitarajia faraja ya Israeli na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona BWANA. basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho na wale wazazi walipomleta YESU ndani ili wamfanyie kama ilivyodesturi na sheria, yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru MUNGU akisema, sasa BWANA wamruhusu mtumishi wako kwa amani kama ulivyosema kwa kuwa macho yangu yameuona utukufu wa wokovu wako, uliouweka tayari mahoni pa watu wote.
Nuru na kuwa mwangaza wa Mataifa, na kuwa utukufu wa watu wote wa Israeli.
Na babaye na mamaye walikuwa wakistaajabia hayo yaliyonenwa juu yake. Simeoni akambariki, akamwambia mama yake, tazama huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli na kuwa ishara itakayonenewa.
Utaendelea kusoma (Luka 2:35-52).
Ndugu masomaji natumaini unazidi kuelewa sasa kuhusu ubarikio wa kweli ni upi ambao ndio MUNGU aliye viumba viumbe vyote anaoutaka na aliyo uanzisha yeye. Ni Ubarikio kwa watu au wanadamu wabarikiwe wakiwa watoto wadogo tu kama ilivyokuwa kwa YESU wa Nazareti ambaye ndiye tunaye muamini na sisi tunafuata njia yake maana yeye alikuja ili atuonyeshe njia na kutuonyesha hata katika njia ya ubarikio wake na zaidi utaona MUNGU akimwandaa mtumishi wake Simeoni kwa ajili ya kumbariki YESU na alimwambia hautakufa mpaka umwone YESU na alionywa na yeye akasubiri mpaka alipokuja YESU ndipo akambariki na akamtambua kupitia yeye.
(Soma Luka 2:33) hata wazazi wake walishangaa maneno hayo na kweli ikatimia, akawa kweli ni nuru ya Mataifa kama ilivyo leo na kupitia yale yaliyonenwa kuhusu kufuatia kuanguka kwake na kuinuka kwa watu wataona ishara na ndiyo maana alivyokufa zitaonekana ishara.
Hii ilitokea kwa YESU sababu MUNGU alimbariki na akatamkiwa maneno ambayo kupitia roho mtakatifu ambaye anao ushirika na MUNGU akayataja na yakawa. Huu ndio ubarikio ambao MUNGU alioupanga kwa ajili ya watu wote ili makusudi yake yatimie kwa wanadamu.
Na hii ilifanyika kwa sababu hapo awali MUNGU alimbariki Adam na Hawa ila baada ya anguko la Adam na Hawa hizo baraka zikaondoka ikabakiwa ni laana (Mwanzo 1:26) hivyo YESU akaja tena kuanzisha
upya au kuturejeshea ubarikio kwa jinsi ambayo alivyotaka yeye na ndio maana akaitwa njia ya uzima na ukweli (Yohana 14:6) Ubarikio wa kweli ni lazima mtoto akiwa mdogo hajui dhambi au hajui lolote akiwa bado ni Malaika wa MUNGU ndiye abarikiwe ( Ubarikio) Ninamaanisha mtoto mdogo hajui hata jina lake, hajui jambo lolote, kuhusu ulimwengu huu, hajui shule ni nini? Hajui hata uzinzi ni nini, huyo ndiye mtoto na wakiwa umri huo ndio wanabarikiwa, siyo wakishajua uzinzi,ulevi, na mambo ya dunia hii ndio wabarikiwe hiyo ni makosa na ni kumdharau MUNGU, hata wakibarikiwa na umri huo MUNGU habariki maana siyo mpango wake hapo katikati adui ameshawahi amewaingizia mambo yake ya uovu.
3. UBARIKIO WA UWONGO
Ubarikio huu ambao hata mimi nilishabarikiwaga nikiwaga darasa la saba ninajua kila kitu kiovu, hata kunywa pombe nilishalewaga, huu ni ubarikio feki, usiotoka kwa MUNGU na hata katika Bilblia tafuta katika kitabu cha Mwanzo mpaka mwisho haupo na kama haupo katika kitabu kitakatifu , huo umetoka kwa mungu asiyejulikana, yaani Ibilisi na ndio mpango huu adui kautuma ili kuliteka kanisa na wanadamu wote ili mtoto anapozaliwa asipokee zile baraka ambazo anatakiwa atamkiwe na mtumishi kupitia Roho Mtakatifu, ili badilishwa ikawa kinyume na Neno lisemavyo sasa ole wao wabarikio watu wazima soma (Ufunuo 22:18-20):
Nitatoa tofauti kati ya mtoto na mtu mzima.
MTOTO MDOGO
MTU MZIMA
Ø Mtoto mdogo hajijui
Ø Hajui kusoma wala kuandika
Ø Hajui kutukana
Ø Hazini
Ø Haibi wala kudokoa sukari
Ø Hasemi uongo
Ø Hajui hata kusoma biblia wala kusali
Ø Ana umri wa miaka 0 – 5
Ø Mtu mzima anajijua
Ø Anajua kisoma na kuandika
Ø Anajua kutukana
Ø Anazini
Ø Anaiba na anadokoa sukari
Ø Anasema uongo
Ø Anajua kusoma biblia na kusali
Ø Umri wa miaka 5 – 17, 18 anapevuka.
Natumaini mpaka sasa unazidi kuelewa kuhusu mtoto mdogo ni yupi na mtu mzima ni yupi. Sasa nikuulize swali ndugu msomaji je hauoni tulidanganyika au mnaendelea kudanyanyika na kumzoea MUNGU ili kusudi lake kuhusu watoto wanapozaliwa alikamilishe limepuuziwa na badala ya akiwa mtoto mdogo abarikiwe, kanisa linamwagia maji na kupiga namba 666, na wakati wa mtu akijielewa ndio abatizwe na aanze kufundishwa Neno la MUNGU ili awe mwanafunzi mzuri wa YESU, ndiyo anarudishwa eti abarikiwe.
Nataka muelewe MUNGU akipanga kitu chake na wanadamu waka kaidi na yeye huwaacha na akiwaacha mnalaaniwa na wote ambao mnabarikiwa mkijijua hambarikiwi na MUNGU mnalaaniwa, maana katika biblia hakuna mahali ambapo imeandikwa mtu mzima awekwe wakfu, yeye alishaeleza katika Neno lake, na akasema pia yeye asiye ya shika maneno yangu na kuyatenda atafananishwa na mpumbavu mbele za MUNGU. (Soma Mathayo 7:24-27) sasa huu ndio ukweli je! Neno la MUNGU tafuta wapi limeandika watu wazima wabarikiwe? Jibu hakuna.
Hiyo ni picha halisi kabisa jinsi ulimwengu huu kupitia watumishi hawafuati Neno la MUNGU lisemavyo, hawafuati neno la MUNGU linavyosema, wamebakia kufuatisha mapokeo ya wanadamu ambao tayari biblia inasema ni wapumbavu na hapa hakuna ujanja wa kujitetea. Tayari ni wapumbavu. Na kama ni wapumbavu basi huo siyo ubarikio ni laana mbele za MUNGU.
Maana hao watu wazima wanatendewa jambo la uongo tofauti na YESU wa Nazareti. Na zaidi tazama katika biblia YESU aliitwa mbarikiwa alipopelekwa madhabahuni.
Na hao wanaobarikiwa yawapasa waitwe wabarikiwa na siyo KIPA IMARA au neno lingine lolote hiyo ni kufuru (Maana kipa ni mchezaji anayekaa golini kuzuia magoli yasiingie ndiye akiwa golini anasimama Imara, ili azuie magoli.
Kinyume cha kuwa ni wabarikiwa utashangaa watu hawa siku hiyo ni sherehe na disco na pombe ndivyo vinavyofanywa sherehe, sasa embu funguka ufahamu wako hata hizo pombe, disco ni mpango wa MUNGU?, jibu siyo mpango wa MUNGU ila ni mpango wa shetani, na katika sherehe hizo, siku hizi mapepo ya disco, ulevi na mizimu huja kusherekea na kufurahi maana ule mpango wa MUNGU alioupanga kwa mtoto huyo haujatimia ni mpango wa shetani ndio umetimia na baada ya ubarikio hiyo laana utaona mtoto atakavyokuwa muovu, mtenda dhambi maarufu.
Na katika watu waovu zaidi katika dunia hii kwa upande wa wakristo chunguza utaona wale wote waliobarikiwa wakiwa watu wazima ndiyo wamekuwa watu wa ajabu zaidi na walio barikiwa wakiwa hawana akili hawajui , wanakuwaga tofauti na zile baraka zimetimia ndani ya maisha yao maana kabla ya kujua lolote walipelekwa kwa bwana na yeye akawashikilia mikononi mwake na hata shetani hawawezi maana hana uhalali nao.
Ila mfunguke kuhusu ufunuo huu ambao ninawaeleza watu wote ili mpone na zaidi ujue kanisa linavyofanya kinyume na Biblia na kama ni kinyume hilo silo kanisa lake maana MUNGU huliangalia neno lake ili litimie. Sasa angalia lipo wapi Neno lake kwenu nyie ambao mmekuwa watu wazima mnabarikiwa? Jibu hakuna Neno lake aliloamuru hivyo ndivyo ni laana mnawekwa wakfu na shetani na kuwa Imara katika kutenda dhambi.
Maana MUNGU aliye hai hajakupitisha ukiwa mtoto mdogo. Ila wameacha Neno la MUNGU na kulitii wakaligeuza na kumfanya MUNGU hana akili na yote aliyoyapanga ni upuuzi kwao.
Wafanyao hivyo wao wamekwisha angamia.
4. FAIDA ZA UBARIKIO WA MPANGO WA MUNGU ALIYE HAI.
Kwanza kabisa unakuwa umempendeza MUNGU kwa kulishika Neno lake na kulitii na pia una kuwa haufananishwi na mtu mpumbavu mbele za MUNGU sababu umelitii Neno lake na yeye huja kukubariki maana umekuwa umelishika neno lake.
Pia umekuwa umeanza kubarikiwa na MUNGU tokea ukiwa mtoto mdogo kama YESU wa Nazareti alivyobarikiwa akiwa mtoto mdogo na wewe unaunganishwa na baraka za MUNGU kama ilivyo ahadi yake kuwabariki watoto wadogo (wakfu) na mtoto anakuwa mikononi mwa MUNGU aliye hai, na MUNGU anaanza kumtengeneza kiroho na kimwili.
Na mtoto atakuwa mwema na tabia njema na ndani yake anayo hofu ya MUNGU. Pia unakuwa umeshiriki ubarikio alioutaka MUNGU. Kama alivyoagiza hata kupitia manabii wake waliotangulia na wewe kuwa ( yaani mtoto mdogo kushiriki kama YESU alivyoshiriki na akapewa baraka.
Na zaidi mtoto anakuwa na malaika wa ulinzi ambao wataendelea kumlinda siku zote na kuhakikisha kuwa yale yaliyowekwa na MUNGU ndani ya mtoto huyo yametimia katika ulimwengu huu na mwisho wake urudi mbinguni alipotokea, mfano alivyo YESU alitokea mbinguni na alipo barikiwa alikaa na malaika wake na wao hata Herode alivyotaka kumuua aliwaambia wazazi wake,waondoke hapo alipokuwa, hii ni sababu alikuwa anao malaika ambao wanahakikisha lile kusudi la MUNGU litatimia tu, Na mwisho mtoto atafanikiwa maisha yake maana tayari alikuwa na kibali alichopewa na MUNGU hapa duniani.
5. HASARA ZA KUBARIKIWA KINYUME NA MPANGO WA MUNGU AU
NENO LAKE
a. Hasara moja wapo wewe unakuwa umeshiriki jambo ambalo halipo hata mbinguni ndipo yeye MUNGU katika makao yake na hata katika kitabu cha mwongozo wa kwenda mbinguni (Biblia).
Jambo lingine unakuwa umeshiriki kuvunja amri ya MUNGU.
( Kumbukumbu la torati 5:8 -9) 6:14-16.)
Na pia unabeba au kulaaniwa na MUNGU maana umetenda kinyume, tazama hata Adam na Hawa walipoenda tofauti na walivyoagizwa na MUNGU katika bustani ya Edeni walilaaniwa, hivyo fomula ni hiyo hiyo tu ila zamani ilikuwa ni kimwili na ila sasa unalaaniwa katika roho na matokeo yake na mapigo yanatokea katika mwili. Na pia unakuwa umetumia jina lake na kufanya kinyume na yeye alivyotaka na ulifanya kinyume na yeye tayari umeabudu miungu mingine.
Ina maana umeyakataa yaliyo yake ukayakubali yasiyo yake.
b. Mtoto anekuwa katika msingi usio wa MUNGU kweli, haijalishi jina la YESU limetumika. Mtoto huyo ataishi kwa kushikiliwa na shetani na ndiyo maana utakuta mtoto hadi kufikia mtu mzima unajuta hata kwa nini umemzaa, anavuta bangi au jeuri anakuwa mwizi, mtukutu ni mtu wa ajabu hana sifa za kuwa mkristo kutokana na matendo anayoyafanya.
Hii yote ni sababu ya kubariki kinyume na MUNGU alivyopanga.
YESU alipelekwa kwenda kubarikiwa akiwa mtoto, sasa siku hizi mtoto anabatizwa kwanza halafu akiwa mtu mzima ndio anabarikiwa! Je huu ndio mpango wa MUNGU?
Jibu ni hapana mtoto angewekwa wakfu kama YESU, haya yote mabaya wasingempata, angeanza na baraka, ndio msingi wake MUNGU. Hivyo ndivyo sababu mojawapo na shetani anawashitaki kwa MUNGU. “si unaona hawa watu uliowaumba kwa mfano wako hawafuati amri zako” na MUNGU ni wa haki husema ni kweli maana ni kweli, japo yeye mwenyewe shetani anakutengenezea kosa ili uangamie na hapo hapo anakushitaki tena, ona jinsi shetani alivyomnafki na alivyo mbaya sana, lakini watu hawaelewi na kama ni vibaya ndiyo maana watumishi wanabarikia kinyume na MUNGUalivyopanga yeye.
c. Hasara nyingine hauendi mbinguni unakuwa umeshiriki kiapo cha baraka ambacho siyo kiapo alichokitaka yeye MUNGU ili ubarikiwe. Na MUNGU hakubali kiapo cha baraka ambacho hakijatokea kwake ! Ni kuulize swali je, wewe utakubali kusaini mkataba ambao haukuhusu? Jibu ni hapana, hutasaini . Hivyo ndivyo ilivyo kwa MUNGU pia.
d. Hasara nyingine ni ule wakati wa wewe kubarikiwa ndio unapelekwa kubatizwa hapa hapo uelewe hivi bila MUNGU kukubarikia hata huo ubatizo ni feki, ubarikio kwa watoto wadogo kwanza ndiyo unavyofungulia baraka ya ubatizo, au haujui kuwa ubatizo ni baraka na njia ya kufungulia baraka hizo ni pale mtoto anapowekwa wakfu, sasa ni ajabu hayo ambayo anatakiwa ayapate mtoto mdogo kutoka kwa MUNGU inapuuziwa. Je nikuulize swali kama huyo mtoto haja pokea kibali cha baraka na yale anayotaka MUNGU yatendeke je yatatokea? Jinbu hakuna lolote ni (zero job). Hasara unayoipata hapa majira yako ya baraka na ubatizo wa MUNGU kwako yanakuwa yamepitwana wakati, na MUNGU huenda na wakati, ndiyo maana kuna majira ya Masika na kiangazi, majira ya kupanda na kuvuna, sasa wewe majira ya kuvuna wewe ndio unapanda na mvua imeshakatika. Je huoni hata kibinadamu watu watakuona mpumbavu? Funguka, huu ni mfano nimekupa ili uelewe upone. Maana sababu kubwa MUNGU anayotaka ni kazi aliyonituma niwaeleze ukweli, mumjue MUNGU wa kweli na mumrejee yeye.
e. Wewe unakuwa ni mtu wa dini tu na sheria na jina lako pia linakuwepo katika dini au dhehebu ulilobarikiwa ukiwa mtu mzima na jina lako halipo mbinguni hata hao wanaobarikia watu wazima na hao hawapo katika kitabu cha uzima wa milele. Na zaidi watabakia kusema mafundisho ya ubarikio ni kumlea mtoto katika njia ufaayo, haiwezekani sababu huyu mtoto anayefundishwa mafundisho hayo, hana baraka za MUNGU na roho Mtakatifu hajamtamkia baraka na kama hujatamkiwa hutaweza lolote lile hivyo ni akili za wanadamu na saikolojia Kuangamiza roho za wanadamu. Msingi wa mtoto kufanikiwa ni pale anapowekwa wakfu tu, kinyume na hapo ni uongo mtupu na mnaofanya hivyo oneni aibu kwa kumdharau MUNGU.
f. Hautaki wokovu unakuwa mgumu maana nafsi yako imeshikiliwa na mapokeo ambayo yametokea kuzimu ya kumpinga MUNGU. Na kama hayajatoka kwa MUNGU hayo ni ya mpinga kristo. Haiwezekani eti wewe ni mkristo halafu unapinga wokovu (Warumi 10:9-11) ina maana ndani yako ipo roho ya mapokeo ya dini na mapokeo ya mafundisho ya wanadamu na hawajui yametokea wapi, ni ya shetani na ile roho haimtaki YESU aingie ndani yako. Huu ni upofu ambao shetani ametumia njia mojawapo kuliteka kanisa na wewe unakataa wokovu . Ila pia ujue makanisa mengine asili yake ni kuzimu hata kama wanalittaja jina la YESU kazi yao ni kumpinga MUNGU tu na kuvunja amri zake na kuwafundisha mafundisho potufu ili wayashike na wao wawe potefu warudi kwa shetani, bila waumini kujijua. Mfano halisi kanisa linaabudu sanamu, hilo linampinga MUNGU asilimia mia moja (100%) na asili yake ni kuzimu ili kuwapeleka wanadamu shimoni kupitia ubarikio feki.Aliniambia YESU, mtu anapokula kiapo na dini yaani yeye ni wa dini tu na siyo wa MUNGU na ndiyo maana hawanitaki mimi YESU kabisa. Kumtaka YESU kikweli ni kupitia ndani ya moyo wako, kiimani, kimatendo na siyo kwa mdomo tu, watu wengi zaidi wananitaja mdomoni tu lakini ndani ya mioyo yao hawanitaki na mimi YESU siwataki watu wa jinsi hiyo. Na ili mtu anikubali ni mpaka hiyo roho ya dini itoke ndani yake na ayakatae mafundisho yake na anifuate mimi katika kweli, maana ndani yake roho ya kuasi ina mshikilia ndani yake ndio maana ana niasi na mimi na BABA yangu yaani MUNGU. Na roho ya kuasi ikiwa ndani yake haijalishi ni kwa mtumishi au muumini, atashiriki pombe tu tena hata atazibariki kwa sababu hana aibu wala uoga mbele za MUNGU wake, atafanya uchawi, kuoa wake zaidi ya mmoja bila hofu ya kuogopa kumkosea MUNGU, na kuvunja amri zake na hata katika sherehe za ubarikio, ubatizo na harusi watashiriki vitu vya shetani, Mfano: Pombe, disco na mila.
Sasa nakuuliza swali je, YESU anayashiriki hayo? au Roho Mtakatifu ameruhusu disco kwenye sherehe za ubarikio? Hii ni sababu YESU hashiriki kubarikiwa watu wazima bali ni roho ya kuasi ya mpinga Kristo, hivyo usishangae ukiyaona hayo yanafanyika ni sababu siyo YESU amebariki ila ni shetani amelaani.
6. JINSI MUNGU ANAVYOTAKA TENDO LA UBARIKIO LIFUATWE
a. Mtoto mdogo anapozaliwa apelekwe madhabahuni awekwe wakfu tena iwe ni madhabahu ya kweli iliyo hai ambayo YESU anakaa hapo.
b. Mtoto anawekwa wakfu kabla hajajua lolote kama ilivyofanyika kwa YESU, hata asijue neno lolote la uovu na kutoka katika kinywa chake, hata asijue uzinzi ni nini wala kuufanya.
c. Usitoe pesa Kwa ajili ya huduma ya kuweka mtoto wakfu.
d. Mtoto awekwe wakfu kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, asitajiwe jina la mtumishi kumwekea wakfu
e. Usimpeleke mtoto kuwekwa wakfu kwa nabii wa uongo au mtumishi ambaye ni freemason na mlevi au hajaokoka wala kubatizwa na maji mengi huyo siyo mtumishi wa YESU wa kweli na siyo mwanafunzi wake, angekuwa ni mwanafunzi wake angetenda yale aliyoyafundisha YESU wa Nazaeti, YESU anasema hao ni wezi wamekuja kuharibu kazi yake na siyo wake.
7. UBATIZO WA WATOTO WADOGO – MWISHO
MARKO 11:27-33
Ujumbe huu mimi Hebron na kufikishia wewe kama alivyonielezea na mimi nina tii. Ujumbe huu ni kwa watu wote walioumbwa na MUNGU anayejulikana ambaye nimezisoma habari zake katika kitabu kitakatifu yani Biblia, MUNGU ambaye yeye ndiye anayeijua misingi ya dunia hii na yeye ndiye aliyeiweka, yeye aliyeumba mtu pamoja na wewe iwe unampenda au humpendi ila atabakia kuwa MUNGU tu na kama humpendi ina maana ndani yako wewe unampenda shetani.
Ujumbe huu ameniambia tarehe 25.09.2013, muda wa saa nane mchana majira ya saa za Africa Mashariki, Arusha Tanzania, mahali nilipokuwepo.
Ameniambia Hataki kusikia tena watoto wadogo wanabatizwa ubatizo wa Mungu asiyejulikana, ikiwa ina maana kwa ubatizo ambao hajaugiza BABA yake, pia ubatizo ambao hata yeye hakubatizwa na maji ya kikombe, Alibatizwa ubatizo wa maji mengi ambao ndio ulioagizwa na MUNGU anayejulikana.
Wanaobatiza hivyo hao siyo wa MUNGU anayejulikana ni wa Mungu asiyejulikana yaani ( Baali) na mlio batizwa ubatizo huo umeshakabidhiwa kwa shetani kwa kupigwa chapa ya namba 666.
Soma Makala yangu Hebron katika blog yangu ya tarehe 26.09.2013. Utaelewa vizuri jinsi YESU alivyonieleza na utapona ukipenda maana siyo watu wote watakaopona ila ni wale watakaolifanyia kazi na kutokushiriki hata ibada hizi na nyumba zao za sala, hii ni picha halisi wanamwabudu Mungu asiyejulikana, na wewe ukishiriki unakuwa hivyo hivyo, ila upone Toka utengwe nao utapona.
Wewe chunguza utaujua ukweli (pia soma kitabu changu cha Nabii Hebron utaelewa zaidi. (UBATIZO WA KWELI KWA ULIMWENGU WOTE).
MATHAYO 18: 6-7, Na yeyote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo waaminio afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake na atupwe baharini (hao wanaowabatiza watu ubatizo tofauti Mathayo 18: 6 -7 inawahusu.
ONYO: Onyo hili nalifikisha Kama alivyonielekeza YESU wa Nazareti ambaye pia ndie Baba yangu, watakao sikia wasikie watakao puuza au kutokusikia wasisikie asema BWANA WA MAJESHI.
Wote mnao batizwa ubatizo wa maji ya kikombe na watoto wadogo, hamtauona ufalme wake ambaye yeye YESU ndiye njia ya uzima na ukweli, msikilize yeye tu ndio salama, usishiriki mafundisho ya uongo, sasa hivi watumishi 98% katika ulimwengu wote siyo watumishi wake, wengi ni wachawi, freemason, watumishi wakujiita, na pesa tu, na wengine ni wafanya mazingaubwe wa shetani.
Hii ni kwa mitume, manabii, wachungaji, wainjilisti, walimu. Wanaojiita kwa jina lake.Hakuna cha kujitetea tena, soma Biblia kuhusu ubatizo na vitabu vyangu na pia endelea kusoma blog yangu Hebron ataujua ukweli zaidi hautakuwa kipofu, utauona mwanga na giza litaondoka.
UBATIZO KWA WATOTO WADOGO – STOPUBATIZO WA KIKOMBE – STOP
SALA YA TOBA.
Kwa wewe ambaye haujaokoka soma sala hii:-
BWANA YESU, nipo mbele zako mbele ya agano la Damu ya YESU, naomba unisamehe dhambi zangu zote, uliandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele, namkataa shetani na kazi zake zote, kuanzia leo mimi ni mali yako YESU, nishike mkono uniongoze milele, Amen. !!
KUMBUKA :
Ujumbe huu ni kwa ajili ya watu wote wa Mataifa yote MUNGU anataka taratibu alizopanga yeye ili kuwabariki watoto wadogo zifuatwe kinyume na hivyo mtaangamia na kuteketezwa na shetani, amesema mrudieni yeye ili awe Baba yenu badala ya wanadamu kuwa baba yao ni shetani kwa kufuata ubarikio wa shetani (Kubarikia watu wazima).
Akaniambia Hebron Mimi ndiye niliyepanga watoto wadogo wabarikiwe kwa nia njema sana, ila wanadamu wamenikataa, akaniambia wanadamu wanafikiri kunitaja kwa midomo wananipenda halafu hawayatendi yale yangu mimi nitawapenda. Siwapendi watu wasiolishika Neno langu, Neno ndiye mimi MUNGU. Walitende Neno langu kama lilivyo na kuwa watakatifu hapa na mimi nitampenda mtu huyo.
Akaniambia injili yangu imebadilishwa hata wewe Hebron ni shahidi maana nimekufundisha jinsi inavyotakiwa injili yangu; ni kasema, ni kweli BABA, “Endelea kuwaeleza ukweli wanijue mimi MUNGU wao, uwaponye na kuwafungua katika vifungo vyote. Na hakuna kitakalosimama mbele yako milele nipo pamoja na wewe, Nimekushika mkono.
About Me
Prophet HebronView my complete profile
Powered by Blogger.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni