Wafilipi 2:10-11
  • YESU KRISTO WA UONGO NI NANI NA UTAMJUAJE?


    KITABU: MJUE YESU KRISTO WA UONGO (Mathayo Mtakatifu 24:4-5)



    TOLEO LA SITA

     ISBN 978 – 9987- 9553-7- 4

    UTANGULIZI

    Ndugu nakusalimu kwa jina la YESU KRISTO, ambaye ndiye BWANA na mwokozi wa mataifa yote, pia ndiye mfalme wa wafalme na bwana wa mabwana na hapana mfalme mwengine zaidi yake. mimi jina langu naitwa Hebron Wilson Kisamo, YESU amenichagua nimtumikie yeye kwa jinsi anavyotaka yeye ili kukomboa ulimwengu huu ambao umepotea na shetani ameumiliki kwa asilimia 98% sawa sawa na YESU alivyoniambia mwenyewe. Amenituma ulimwenguni kote ikiwa ina maana nchi zote, mabara yote. Ujumbe huu aliniagiza rasmi na kunipa mamlaka yake tarehe 14.6.2010. Na akanipa jina la kanisa lake niliite YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRY. Akaniambia mwanangu nitautumia huu mwili wako kuukomboa ulimwengu wote, utachukiwa sana, utafanyiwa na kuitwa majina mabaya lakini usiogope tena ufurahi zaidi, kwani mimi YESU walinifanyia mabaya zaidi na ya uongo yakitokea kwa baba yao wa uongo ambaye ni lusifa, nilifurahi daima. Hakuna jambo lolote litakalofanikiwajuu yako au silaha yoyote juu yako nipo na wewe milele. Nitakutumia kwa namna ya tofauti na kwa kiwango kikubwa sana ambacho hakijaonekana tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu. Adui yako ni adui yangu, akasema YESU kwa sauti ya uchungu sana, watumishi wamenisaliti maagizo niliyowapa hawayafanyi na wamegeuza neno langu kuwa maandiko badala ya neno, maandiko yanatoka kwa shetani maana lusifa anaijua bibilia yote na maandiko hayana uthibitisho wa nguvu zake YESU. Neno linatoka kwa YESU na linaudhihirisho wa nguvu za MUNGU. Na pia wana wa adamu wanateseka wanalia na kuomba hawapati majibu, na zaidi wanazidi kupotoshwa na viongozi wa kanisa, maagizo niliyoyaacha nilivyokuwa ulimwenguni kabla ya kurudi kwa BABA yangu ili kuniandalia maandalizi ya ujio wangu ili nipate kuwaponya wengi waende mbinguni, imekuwa kinyume idadi kubwa ni ya watu wa shetani. Waliokuwa watumishi wangu wamenisaliti 98% sipo nao. Wameamua kwenda kuzimu, na shetani anawatumia na jinsi anavyowatumia, ni kubadili au kwenda kinyume na agizo la MUNGU, mfano watumishi kwa sasa wamefanya kanisa ni mahali pa biashara, kunyanganya watu vitu vyao na wakijua wananitolea mimi, na kufanya mimi YESU ndiye mnyanganyi, kwa midomo yao hunitaja kama wananipenda ila mioyoni mwao hawapo na mimi, wamekuwa watumishi wa pesa na siyo mimi, wamekuwa wakitenda miujiza lakini siyo yangu ni miujiza ya shetani, na hao ni kati ya wale ambao siku ya mwisho nitawakataa na kuwaambia sikujui. Kanisa limeniacha kunitegemea mimi, imebaki 2% tu ulimwengu mwote. Sasa mimi YESU ninalikomboa kanisa mwenyewe na ndipo unabii na utukufu wa kanisa la mwisho utakuwa mkubwa kuliko wa kanisa la kwanza unatimia sasa.

    SHUKURANI

    Namshukuru mke wangu sana kwa kunitia moyo na kuniombea, nawashukuru watumishi wote wanaoniombea na kutumiwa na MUNGU kutumika pamoja na YESU aliyeniita, mkono wa MUNGU uwe juu yao siku zote za maisha yao.

    Asante.

    MTUME NA NABII- HEBRON WILSON KISAMO

    KIONGOZI NA MWANZILISHI WA HUDUMA

    KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRY.

    P.O.BOX 13657

    ARUSHA, TANZANIA

    EAST AFRICA

    EMAILmaombi@prophethebron.org

    WEBSITEwww.prophethebron.org

    BLOG:      prophethebron.blogspot.com

    NAMBA ZA SIMU: 

    +255 764 042 149

    +255 759 610 820

    +255 718 916 864

    +255 718 154 433

     

     

     

    YALIYOMO.

     

     

    1.     MJUE YESU KRISTO WA UONGO

    2.     KAZI ZA YESU KRISTO WA UONGO

    3.     UTAMTAMBUAJE YESU KRISTO WA 

     

    UONGO

    4.     SALA YA TOBA

        5.  NUKUU YA YESU KRISTO WA NAZARETI



    1.   MJUE YESU KRISTO WA UONGO.

    Ndugu msomaji na mwanadamu yeyote wa taifa lolote kwa rangi yoyote na jinsia yoyote na kwa umri wowote na hata viumbe vyote, milima, wanyama wa nchi kavu na majini, mwezi, nyota, na kwa ujumla vitu vyote pamoja na ulimwengu wote na sayari zote. Hivi vyote ni mali ya MUNGU aliye hai ambaye ndiye BABA yake YESU KRISTO wa Nazareti / au kwa jina lingine YESU wa Galilaya na mwana pekee wa MUNGU;  nakusalimu kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti, au watu wengine wanamwita Nabii Issa ili uelewa vizuri.

    Ndugu msomaji, siku ya leo imempendeza MUNGU kuwafungua ufahamu na kumjua YESU KRISTO wa Nazareti, aliye YESU wa kweli, na pia kumjua Yesu Kristo wa uongo, ili msipotezwe tena na mpone. Soma katika kitabu cha injili ya Mathayo 24:23-25; NENO la MUNGU linasema, wakati huo mtu akiwaambia tazama KRISTO yuko hapa au yuko kule msisadiki, kwa maana watatokea Makristo wa uongo na Manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza kamayamkini hata walio wateule. Tazama nimekwisha waonya mbele.

    Ndugu msomaji, nafikiri watu wengine mnasikia nasema kuwa yesu kristo wa uongo, unanishangaa; sawa, na ninaposema kuwa YESU wa kweli unanishangaa, usiogope, leo utafunguka 100%. Kwanza kabisa nitakueleza maana ya YESU, au YESU ni nini? YESU maana yake ni MUNGU pamoja na sisi, tunajua kuwa miungu mingi hapa ulimwenguni zaidi ya huyu MUNGU aliyeuumba ulimwengu huu. Mfano, shetani ni aina ya mungu pia. Hebu jiulize, sasa katika injili ya Mathayo 24:24 (a)Kwa maana watatokea Makristo wa uongo, sasa nikuulize wewe ndugu msomaji, tazama hata Biblia imeandika. Na zaidi, soma katika kitabu hiki cha injili ya Mathayo 24:4-5,11. YESU huyu wa Galilaya na Nazareti, nanukuu kamaBiblia inavyosema, YESU akajibu akawaambia, angalieni, mtu asiwadanganye. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema mimi ni Kristo; nao watawadanganya wengi, mstari (11) na manabii wengi wa uongo watatokea na kudanganya wengi.

    Ndugu msomaji, YESU alikwishasema angalieni mtu asiwadanganye ila kwa sasa yametimia 98% na ulimwengu unaongozwa na huyu yesu  kristo wa uongo, na ambaye YESU huyu wa Nazareti aliyajua hayo yatatokea, na watatumia jina lake kwa ajili ya kuwapoteza hata wewe mteule ili uangamie, ila sasa haya yamefichuliwa na MUNGU, na nitakufundisha vizuri ili roho yako ipone. Kwanza kabisa nitakueleza ufunuo huu wa kumjua na asili yake yesu kristo wa uongo ambao pia YESU wa Nazareti ambaye ndiye YESU wa kweli na mwana wa MUNGU wa pekee, alishatabiri au kuyasema ni ya  kweli 100%, ila wanadamu walipigwa upofu na kushindwa kutofautisha YESU wa ukweli ni yupi na wa uongo ni yupi na yukoje. Nitakueleza kwa ufupi tu, ila masomo mengine utayapata katika vitabu nilivyoandika, na CD, DVD na Tape.

    Joka kuu ambaye ndiye baba yake shetani alivyofukuzwa mbinguni, alipofika kuzimu, joka huyu alitengeneza serikali yake kwa kuiga mfano wa picha ya Mbinguni, nitaeleza kwa kifupi, ila endelea kufuatilia masomo na vipindi vya Nabii Hebron. Nitaendelea kuelezea kwa jinsi ambavyo ninavyoelezwa niwafundishe, msidanganyike kama mnavyodanganyika 98% ulimwengu mzima, wala mimi sipunguzi neno, wala kuongeza lolote, nampenda YESU wa Nazareti. Huyu joka kuu ndiye aliyemzaa yesu kristo wa uongo, na huyu yesu kristo wa uongo ni aina ya malaika wa shetani (na ndiye yesu kristo wa uongo).

    Ndugu msomaji, jiulize kwa nini YESU alisema makristo wa uongo watawadanganya wengi, YESU wa Nazareti, anayo maana kwamba, kristo huyo wa uongo, baba yake ni baba wa uongo. Baba wa uongo ni shetani. Natumaini unazidi kufunguka ufahamu wako (soma Mathayo 24:5). Yesu huyu wa uongo makao yake yalikuwepo kuzimu, ila kwa sasa hayapo tena, mimi Hebron kwa kuongozwa na YESU KRISTO wa Nazareti alinifunulia siri hii, na kuniamuru nimkamate na kubomoa serikali yake yote. Nilimaliza kazi hiyo tarehe 2 Machi 2013 majira ya saa kumi na mbili jioni kwa masaa ya Afrika Mashariki (Tanzania).

    Huyu yesu wa uongo alikuwa ndiye mwanakondoo wa joka kuu kwa ajili ya kuuangamiza ulimwengu wote. Yesu huyu wa kuzimu alijitengenezea majina ya watakatifu wa mbinguni, akawaita wengine hivyo hivyo, akiwamo Yuda Iskarioti. Huyo hata mbinguni hayupo. Wakawa wanalo kanisa kubwa sana ambalo yesu wa uwongo ndiye analiongoza, na lilikuwa na nguvu sana, na nguvu hizo zilikuwa wanapewa  watumishi waliopo ulimwenguni humu ambao wamemsaliti YESU au kwenda kinyume na MUNGU wa Ibrahimu alivyopanga. Na siri hiyo wale watumishi waasisi wa baadhi ya dini ulimwenguni hapa wanajua kabisa ila sasa mwisho umeshafika, mtayaona. Kazi ya huyu yesu wa kuzimu ni kubadilisha mpango wa MUNGU aliye hai na kuweka mpango wake wa mungu mfu ili wanadamu ile siku ya mwisho waende kwa mungu mfu, na hata kwa sasa 98% ya vifo vya Wakristo wanaokufa, hawaendi kwa YESU wa Nazareti, wanaenda kwa yesu wa kuzimu. Yesu huyu wa kuzimu anacho mpaka kitabu cha uzima wake wa kuzimu, kamailivyo, tunavyojua mbinguni YESU KRISTO wa Nazareti anacho kitabu cha uzima wa milele. Huu ni ujanja wa shetani sababu binadamu wanampenda YESU wakisikia jina lake, ila hawamjui ni wa Galilaya au ni wa kuzimu. Leo utafunguka, ila wengi watumishi mnaoupata ujumbe huu mnajijua nyie mnawaangamiza watoto wa MUNGU; nawatangazia baba yenu wa uongo hayupo tena na gadhabu ya YESU KRISTO wa Nazareti ipo kazini. Ndugu msomaji, hivi haushangai imeandikwa siku ya mwisho wengine watajitetea, BWANA, kwa jina lako niliponya, kwa jina lako nilitoa mapepo, na BWANA atasema sikujui, mahali pako ni kwenye lile ziwa la moto. Funguka ufahamu, kwa nini mtu atumie jina la YESU kuponya halafu akataliwe siku ya mwisho? Ina maana hakuongozwa na YESU wa Nazareti au wa Galilaya. Aliongozwa na YESU wa uongo na huyo huitwa nabii wa uongo maana baba yake ni yesu wa uongo. Huyu yesu wa uongo amejenga makanisa mengi ulimwenguni 98% ni makanisa yake, na humo jina la YESU linatajwa kawaida, na Biblia husomwa. Kwa kubadilisha yale ya MUNGU wa kweli yasifuatwe ili kukupata wewekama wengine 98% walivyopatwa. Hebu jichunguze.

    Nitaelezea kwa kifupi mifano ya Manabii wa MUNGU waliopita ambao wapo mbinguni kwa sasa.  Mfano Musa alipokwenda mlimani kuongea na MUNGU, na mara nyingine alipelekwa mbinguni hali akiwa hapa ulimwenguni. Aliamriwa ayafanye yale ambayo ameyaona mbinguni kwa YESU wa Nazareti. Mfano mwingine Yohana mbatizaji aliagizwa aje ulimwenguni abatize watu kwa maji mengi, haya ndiyo ya YESU wa kweli wa Nazareti. Huyu yesu wa kuzimu au wa uongo ndiye muasisi wa ubatizo wa kikombe na wote mliobatizwa ubatizo wa kikombe hamjabatizwa na YESU wa Nazareti, haijalishi limetajwa jina lake, jina hilo ni la kristo wa uongo, na wewe unakuwa mkristo wa uongo! Hata wanaobatiza ubatizo huo wanaongozwa na yesu wa kuzimu.Kama mlikuwa hamjui mfunguke; angalieni kukimbia kwenu na kufanya hiyo kazi isiwe ni bure. Na mwisho ni kilio ukifikiri unamtumikia YESU wa Nazareti kumbe ni yesu wa kuzimu. Ukiangalia kwenye mtandao wa freemason, tafuta majina ya watumishi, jina utakaloliona, ujue mtumishi huyo anaongozwa na yesu wa uongo au wa kuzimu. Usitishwe na jina analolitaja, hao ni wauaji wa watoto wa MUNGU. Zile sala za toba wanazoongoza watu, majina yao huandikwa kwenye kitabu cha uzima wa yesu wa uongo kuzimu. Huyu yesu wa kuzimu hukaa ndani ya dini na watumishi wa makanisa na hutaja jina la YESU ila ndani yao ni roho ya uharibifu juu ya maisha yako, na hata kama ni mtumishi unaependa kurejea kwa YESU wa Nazareti, tubu ili upone, kinyume chake utaangamia japo YESU wa Nazareti ameniambia kuna baadhi yao hata toba yao haitasikilizwa, hukumu ipo juu yao tayari. Ndugu msomaji, natumaini unazidi kufunguka ufahamu wako, na kuanzia leo amua moyoni mwako, na usikae katika madhabahu za yesu wa kuzimu (uongo).













    KAZI  ZA YESU WA UONGO

    Ni kuhakikisha waumini ambao wanayakiri au kuyatenda yale ambayo MUNGU amesema yafuatwe hayafuatwi.

    Mfano:

    1. Imeandikwa, utoapo sadaka, hata kulia na kushoto isijue. Ina maana asijue mtu. Yesu wa kuzimu alichokifanya kwa kanisa lake unaambiwa andika jina lako, kiasi, namba za simu, na kupewa risiti ya malipo ya sadaka yako. Hivyo ujue sadaka yako imeenda kuzimu na zaidi hata usipoandika jina kwenye sadaka hiyo, na unaitoa katika madhabahu hiyo, bado haipokelewi na YESU wa Nazareti, sadaka bado zinaenda huko.

    2.     Haijalishi umeinenea nini, ujue hayo yote yanaenda kwa yesu wa     

         uongo hata ukimtaja YESU wa Nazareti unajisumbua.

         YESU wa Nazareti hawezi kuja kwenye ngome ya yesu wa uongo wala kukaa hapo, wala hatakaa aje milele. Matokeo yake hauoni baraka, unazidi kufilisika, unabakia kusoma imeandikwa katika Malaki 3:10,11. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye wala hataharibu mazao ya ardhi yenu, wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi. Ndugu msomaji, badala ya wewe kubarikiwa kama NENO la YESU wa Nazareti, imekuwa ni kinyume, unashangaa unatoa sana, sio ajabu hata viti vya madhabahuni umemtolea wewe lakini unapokea baraka za yesu wa kuzimu (kufilisika, hauna mwelekeo, na unapoona hayo tambua kuwa hata safari yako kwenda mbinguni siyo. Unaelekea kwa yesu wa kuzimu maana hayo ndiyo yake.

    3. Kila mtu anajua amri kumi za MUNGU, na mojawapo   inasema  usiabudu sanamu, miungu au kitu chochote zaidi ya MUNGU, au hata alichokiumba kwa mfano wake. Lakini siku hizi makanisa baadhi ulimwenguni huku, yanaabudu watoto wa MUNGU, sanamu. Na watu wengi mmeshindwa kuelewa je, si YESU, mbona anatajwa kanisani kwetu? Ni sawa kabisa, YESU wa kweli na wa Nazareti ni mtoto wa MUNGU aliyeandika amri hizo na yeye hashiriki uongo wa kuabudu sanamu au kuvunja amri za BABA yake, mahali hapo ujue ni kanisa la yesu wa uongo, YESU wa Nazareti alisema watatumia jina lake kuwapoteza wengi, kama ilivyo sasa wengi wamepotea kwa kudanganywa na jina la YESU wa uongo. Na hao wote watapelekwa kwa baba yao wa uongo, na hapo watu watalia na kusaga meno! Usishiriki ibada hizo, ni bora ukae nyumbani ili usiangamie, huku ukiendelea kumuomba YESU wa Nazareti akuongoze katika madhabahu ya YESU wa Nazareti. Pia uwe makini unaweza kukuta jina la kanisa limeandikwa maneno mazuri mfano: Kanisa la Yesu wa Galilaya, Nazareti, Kanisa la Mungu au la Ufufuo, au jina lolote, ila ukiingia ukikuta watu wapo kinyume na Biblia au ni michango tu, ujue hapo wanaongozwa yesu wa uongo, na wewe unazidi kupigiliwa misumari, hauendi popote.

    4. Imeandikwa nyumba ya baba yake YESU wa Nazareti ni nyumba ya ibada na sala tu! Kila mtu anajua hivyo, enzi zile YESU wa Nazareti alipokuwa hapa ulimwenguni aliingia hekaluni akakuta wanafanya biashara, YESU huyo wa kweli wa Nazareti aliingia akatimua kila biashara bila kuogopa (Marko 11:15-18) usome. Sasa mambo haya yaliingizwa na yesu wa uongo katika kanisa, ila YESU wa Nazareti aliyakataa, hebu ona leo hii yalivyo makanisani. Je nikuulize swali, hapo YESU wa ukweli wa Nazareti yupo? Jibu ni yesu wa kuzimu ndio madhabahu yake, Mfano kanisa hilowanaomtaja yesu wao wanafanya biashara (wana benki). Wakati  YESU wa kweli mwana wa MUNGU alishakataa, na kama amekataa na hilo kanisa linafanya hayo, ndugu msomaji, funguka ujue hapo ni yesu wa uongo na wanatumia jina lake, usishiriki tena, utalaaniwa na MUNGU. Haya ni ya yesu huyu ambaye ndiye kristo wa uongo, maana kazi ya YESU wa Nazareti ni kuhubiri injili ya kweli na ni bure tuu.!

    5. Imeandikwa nimekupa bure huduma nawe utoe bure. Huyo ni YESU wa Nazareti asema hivyo. Utashangaa katika kanisa jina la YESU linatajwa, na unaambiwa toa pesa ndio ufunguliwe. Jamani fungukeni, huyo ni  yesu wa kuzimu (uongo). Na kawaida, fomula ya shetani hatoi kitu bure, lazima utoe kwanza, kwa mfano, unapo /  ulipoenda kwa mganga ambaye pia na huyu ni mtumishi wa shetani 100%, huduma lazima atakuambia toa kitu mfano Pesa, kuku, mbuzi na zaidi hata kuzini na wewe. Ukiyakuta haya, nakuambia kama nilivyoambiwa na YESU wa Nazareti hapo ni yesu wa uongo ndiye anayesimamia, na hamfunguliwi, na hata ukifunguliwa ni kwa muda tu, na hali yako mbaya hurudia mara mia mpaka unajuta ni kwa nini uliokoka badala ya kwenda kuokoka uwe hai, unakuwa umejipeleka kufa, na ndio unakuwa hauna mbele wala nyuma, na mambo hayaendi.

     6. Ukikuta kiongozi wa kanisa ni mzinzi, mlevi au mchawi, wazee wa kanisa wako hivyo, ndugu msomaji, ujue hapo wanaongozwa na yesu wa uongo au yesu wa kuzimu. Haijalishi wananena kwa lugha, hizo lugha sizo za kutoka kwa YESU wa Nazareti. Hata huyo yesu wa kuzimu anakopi lugha hizo, ila zake hazina udhihirisho, na anaponena watu hawaelewi, mnaunganishwa mfe kiroho, na ukifa kiroho, mbinguni kwa YESU wa Nazareti hauendi. Ukikuta mtumishi wa kanisa anazini na hata zaidi kuzaa nje ya ndoa, na hata hatengwi kanisani anaendelea kuhubiri, ndugu msomaji funguka, huyo hana YESU wa Nazareti, huyo ni mtumishi anayeongozwa na YESU wa uongo. YESU wa kweli hakai ndani ya mtumishi mzinzi, madhara yake wote mnarithishwa roho ya uzinzi na laana kwa kanisa hilo lote. Hiyo ni namna ya yesu wa uongo anavyofanya ili mlaaniwe na muangamie, haijalishi ni kanisa la kiroho, hilo ni kanisa la yesu wa kuzimu.

    7. Habari nyingine. Ukikuta mahali wanachoma udi halafu wanataja jina la YESU, ndugu msomaji funguka, hapo ni mahali pa yesu wa uongo. Kazi ya udi ule moshi na harufu yake ni chakula cha majini (mapepo). Na udi unapochomwa, yale maroho ya yesu wa kuzimu huja kuongoza ibada hiyo, na yesu wa uongo utasikia anatajwa tu. Wengi mmekuwa mkiona sehemu mbalimbali kwenye maduka, hoteli, magari na nyumba yoyote wanayoabudia, ukiona hayo funguka, hapo hizo kazi zao zinaongozwa na majini au shetani, sasa funguka, huo ni usanii kwa kupitia YESU wa uongo. Udi ni chakula cha majini, hata wengi wenu mnajua, je YESU wa Nazareti anashirikiana na majini? Jibu hapana.

    8. Wanaojiita wakristo na wanatumia udi kwenye maisha yao, hao wote hawana YESU wa ukweli, wanaongozwa na yesu wa kuzimu. Hata ibada wanazokwenda ni kujiunganisha zaidi na huyo yesu wa kuzimu, ukiwa mlevi, umezika Biblia kanisani au mahali popote, huyo sio wa YESU wa ukweli, ni wa yesu wa kuzimu  na akikuongoza na wewe anakupeleka huko.

    9. Tunajua ya kwamba nyumba ya ibada ni nyumba ya sala tu, haitakiwi kufanyika kitu mfano kumzika mtu kanisani, haijalishi anayo heshima gani. Kumbuka YESU wa Nazareti ndiye mwenye heshima kuliko mtumishi yeyote ulimwenguni hapa, ila yeye alipokufa alizikwa mbali na kanisa, mpango wa yesu wa kuzimu ni kuzika madhabahuni ili kuharibu nyumba ya ibada, na nyumba hiyo huwa ni eneo la mizimu, maana huyo mtu hatafufuka, na jengo hilo hizo ibada mnazoenda kushiriki ni mpango wa yesu wa kuzimu. Mnapoenda kushirikiana na mizimu, na nyie mnaunganishwa bila kujua, haijalishi amezikwa kwa jina la YESU. Huo sio mpango wa YESU wa Nazareti. Kimwili tu, mwanadamu hapendi kwenda kaburini, maana mtu akishakufa basi, na kaburini ni mahali pa mfu, na kama kwenye kanisa mfu amezikwa hapo, tujue mahali hapo ni madhabahu mfu na wote mnaosali hapo mmekufa. Huu ndio ukweli, fungukeni mpone, haya ninayokuambia, usiniangalie mimi kama Hebron, haya siyaongezi wala sipunguzi hata moja, nakufikishia kama vile Yohana mbatizaji alivyotumwa kubatiza kwa maji mengi bila kubadilisha, na mimi haya ndiyo niliyoambiwa niyahubiri ulimwengu mzima siku zote, naatakayejaribu kunizuia hataweza, MUNGU atamuua. Na atakayepanga jambo baya juu yangu, kabla hajafanya, atafanyiwa yeye; asema bwana. Kama unabisha wewe jaribu. Jambo lingine inawezekana wewe ni muumini na unayaona matendo machafu kanisani, na ukimweleza mtumishi anayakataa, japo anajua ni kweli, mahali hapo ujue anaonozwa na yesu wa uongo! Maana kama ndani yake angekuwa ana YESU wa kweli, angekusikiliza, ila hawezi kukusikiliza sababu hampo njia moja na yeye. Yeye yupo katika njia ya yesu wa uongo. Mahali hapo sio salama. Mwenye kusikia na kuelewa na aelewe.

    10. Ndugu msomaji, nikuulize swali, Je, unajua ule mwisho wa ulimwengu huu atakuja YESU wa Nazareti kuwachukua wale walio wake, sasa ndugu msomajikama wewe upo chini ya yesu wa uongo, unategemea akuchukueje? YESU wa kweli atakuchukua uende kwake? Jibu ni hapana. Laiti tungeona jinsi watu maelfu kila siku wanakufa na kwenda kwa yesu wa kuzimu, yaani kuna siku moja katika nchi hii yaTanzania siku nzima wote wanakwenda kuzimu, wote waliokata roho kwa kufa, inatisha na kuna siku moja katika vifo vya waliokata roho ni watu 21 tu walienda paradiso. Wengi wameenda kuzimu, muwe makini msitishwe tena na miujiza ya kipepo, huo ni ujanja wa shetani kuwateka, ila wajanja wamefunguka. Zaidi hata katika ulimwengu huu kama YESU mweyewe alikataa asiitwe mwema (mtakatifu), akasema hakuna aliye mwema, ni MUNGU tu, leo hii unasikia mtu au watu wanajiita mama mtakatifu, dada mtakatifu, baba mtakatifu, je, hii ni sawa? Jibu siyo sawa. Na yesu wa kuzimu, wale anaowaongoza, huitwa hayo majina aliyoyakataa YESU wa Nazareti, kataa,! mmeambiwa ni udaganyifu, hata kibinadamu tunajua yupo ROHO MTAKATIFU anayetoka kwa MUGU MTAKATIFU. Ila yesu wa kuzimu hutoa roho chafu na huendeleza machafukama ilivyo sasa.

    11. Yesu wa kuzimu katika kanisa anazo sadaka nyingi sana, sadaka ya YESU wa Nazareti ni fungu la kumi tu na shukurani unayopenda kumpa kwa moyo mweupe. Hizo nyingine zote zimebuniwa na yesu wa uongo ili kukuibia wewe. Yesu wa uongo hukusanya madeni na kuwadai waumini ili kulipia madeni na kujengea mahekalu ya yesu wa uongo, na hao wanaosimama kuchangisha au kudai, hao ni manabii wa uongo. YESU wa Nazareti sio masikini wala yeye hafanyi makusanyo kuijenga nyumba yake ya sala. Kama ni yake, hufungua milango ya kuifanya peke yake kwa njia anayoitaka yeye. Alisema msisumbukie mtakula nini, mtavaa nini. Hayo YESU wa Nazareti aliyasema. Je, yeye anasema uongo? Ndugu msomaji angalia panavyonuka, kanisa lilivyotekwa na YESU wa uongo 98%. Na kama kanisa linanuka, ina maana na waumini nao wananuka dhambi na laana au baraka za yesu wa uongo, au kristo wa uongo.

    12. Yesu wa uongo huchagua partner watu wenye pesa ili awanyang’anyemali zao na watu wakijua unawafanya partners na YESU wa kweli kumbe ni yesu wa kuzimu huyo. Siku zote partners kanisani hachaguliwi masikini, lazima awe na pesa, je hao wasio na pesa ni takataka? Jibu ni yesu wa kuzimu, ndiye mwenye ubaguzi; ila YESU wa Nazareti watu wote huwa partners wake wote iwe wana pesa au hawana, anawapenda wote. Jambo lingine ndugu msomaji,  ukiona waumini wanamuogopa au kuingiwa na hofu kila wanapomuona badala ya kumfurahia mchungaji wao, ujue huyo aliyepo ndani yake ni yesu wa kuzimu, ndiye anatisha.







    13. Yesu kristo wa uongo hutibu kwa kutumia madawa ya kienyeji mfano   mizizi ya miti  huchemsha na kuwapa watu wanywe na kutoza fedha fulani ndipo upate tiba hiyo, wakati YESU KRISTO wa Nazareti alisema umepewa bure toa bure, ila YESU mwana wa MUNGU  alishasema watakuja kwa jina langu kuwadanganya hata wateule kama ilivyo sasa. Yameshatokea, baadhi ya watumishi walijiita wachungaji  walichemsha madawa na kutumia jina la YESU na wengi walikunywa, na wote waliokunywa dawa hizo walipigwa chapa 666 ya shetani na walinyang’anywa vitu vyao, mfano nyota na kupelekwa kuzimu na nafsi zao kukamatwa na shetani.

         Ndugu msomaji hiyo ilikuwa ni mbinu ya shetani ili kuwavuna au kuwateka wana wa MUNGU, ile pesa  unayotoa ni utajiri wako kwa hiari yako mwenyewe umempa shetani na ile dawa uliyokunywa ni mauti. Hivyo ili upone tafuta mahali kuna mtumishi wa kweli akufungue kinyume na hapo utaangamia tuu.

    14. Yesu kristo huyo wa uongo huongoza kanisa lake kimwili na siyo kiroho, mfano ili kujua jambo fulani katika maombi hutumia vitu vya kimwili, mfano moshi ukienda juu ndipo wamejibiwa, huo ni uongo, YESU wa Nazareti alisema imetupasa kumuomba MUNGU katika roho na kweli. Kuomba katika roho huoni chochote au kutumia kitu kilichofanywa au kuumbwa na MUNGU, zaidi hata YESU ambaye ndiye kweli na uzima ambaye inatupasa yeye na kufuata njia zake, yeye aliomba katika roho na kweli, na alijibiwa na BABA yake. Njia  ya maombi ya YESU wa Nazareti yakupasa kuomba kama YESU wa Nazareti  tuu kinyume na hapo  huo ni mchomeko na MUNGU ameniambia mtayaona haya na mtajua ukweli muda siyo mrefu ajuavyo yeye atafanya na yeye siyo mtu hata aseme uongo na vitu vyote vitapita ila neno lake litabakia palepale.

    15.               Yesu kristo huyo wa uongo nguvu zake huweka kwenye stika, vitambaa na kuwauzia waumini, ndugu msomaji funguka ufahamu wako na upone. Hizo stika au vitambaa mnavyouziwa kwenye makanisa na hao watumishi, hao ni watumishi wa yesu wa uongo, hizo ni hirizi  siri iliyofichika hapo unapoinunua  na kuiweka kwenye vitu vyako, ule utajiri wako na uthamani wako wa nyota anazichukua yeye na waliotumia stika hizo utaona maendeleo yako ya kiroho na kimwili hudumaa, ndani ya stika hizo huwa zina majini ambayo ndio roho mchafu wa yesu wa uongo hukaa hapo na kuharibu maisha yako. Mfano unakuta stika imeandikwa kwa jina la yesu ninakuona (I SEE YOU) ina maana hivi, yeye ndiye  anayekuona huyo mtumishi na mapepo yake. Badala ya YESU wa Nazareti kukuona.

    Ninakuuliza swali,  je wewe unataka mtumishi akuone au YESU wa Nazareti akuone? Jibu ni YESU wa Nazareti akuone. Funguka ufahamu usidanganyike tena, tupa  stika hizo; choma. YESU wa kweli hakai kwenye stika au vitambaa. Nikuulize swali je, YESU anakaa au nguvu zake zinakaa kwenye stika? Jibu ni hapana, ila nguvu ya yesu wa uongo ni sawa tu na mganga wa kienyeji, nguvu zake hukaa kwenye vitu na humpa mtu, hutembea navyo na huvitegemea kama ndiye mungu wao, na hii itakusababisha hata na wewe mwanadamu unakuwa umeshirikishwa uchawi bila kujua wala kupenda na pia kuabudu sanamu bila kupenda au kujua na kujikuta umeingia kwenye laana  ya kuachwa na MUNGU. Hebu waulize, imeandikwa wapi tutegemee nguvu za YESU  wa kweli zinakaa kwenye stika ? Jibu hawana. Majibu ya Biblia  au kwa lugha nyingine katiba ya uzima wa milele, na madhara yake ni kuangamia, usitishwe na miujiza wanayoifanya, alikwisha sema YESU wa Nazareti watatokea makristo wa uongo, na ndio hao 98% ulimwenguni ni makristo wa uongo tu; Ili uwajue wewe chunguza wanayoyafanya je ni ya YESU wa Nazareti au  wa Galilaya? Utayakuta mengi zaidi ni ya kristo wa uongo na ndivyo ilivyo 98% ya wakristo wote ulimwenguni wanaongozwa na YESU wa uongo na hao wote ni shetani amewavuna ila YESU wa Nazareti alichoniambia atawatoa huko na wale watakao msikiliza watapona na wale watakao kataa kumsikiliza wataangamia ( Imeandikwa katika kitabu cha ufunuo wa Yohana 22: 18-20 ) Namshuhudia kila mtu akiyaongeza, MUNGU atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki, MUNGU atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki. Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, naam; naja upesi. Amen na uje Bwana YESU.

    Ndugu msomaji hayo yote kinyume na YESU wa Nazareti alivyopanga au neno la MUNGU aliye hai, Hao tayari hilo neno la MUNGU  katika kitabu cha ufunuo wa Yohana 22: 18-19 linawahusu na wewe uliyeshiriki hivyo ili upone achana na hayo, mfuate YESU KRISTO aliye njia ya kweli na uzima utapona.



    16.               Yesu kristo wa uongo huruhusu kufungisha ndoa za jinsia moja mfano, mwanaume kwa mwanaume au mwanamke kwa mwanamke. Huo sio mpango wa MUNGU aliye hai ni mpango wa mungu mfu ambaye ndie shetani au baba yake yesu wa uongo, katika kanisa hilo au mtumishi anayefungisha ndoa hizo, ndugu msomaji tambua kabisa mnaangamizwa hata ibada mnazoshiriki  na sadaka zenu na nyie majina yenu au hao yapo katika kitabu cha uzima wa shetani ambao yesu wa uongo ndiye mkulima wa shamba hilo na hao wakristo ndio mavuno ya shetani( soma mambo ya walawi 18: 20-22)

    Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye, nawe usitoe kizazi chako chochote na kuwaapisha Moleki, wala usilinajisi jina la MUNGU wako, mimi ndimi BWANA. Usilale na mwanaume mfano wa kulala na mwanamke, ni machukizo.

    Ndugu msomaji, hebu zidi kufunguka na kuelewa vizuri na ujue mambo yalivyoharibika, MUNGU amekataa mtu asilale na mwenzake mwenye jinsia moja, leo hii eti mnafungisha hizo ndoa. Tena wanatumia jina la YESU, Jamani, hao hawajatoka kwa MUNGU kabisa ni wanaongozwa na yesu wa uongo ndio maana wanasema na kufanya ya uongo na machukizo na kunajisi nchi na watu wake.

    17.               Kazi ya kanisa la YESU wa Nazareti ni kuupinga uovu na kusimamia yale yote anayotaka MUNGU aliye hai yatendeke peke yake. Imeandikwa usizini hiyo ni amri ya MUNGU aliyeitoa kwa watu wote wa ulimwengu huu na kila mtu anajua kuzini ni dhambi kabisa, cha ajabu hawa makristo wa uongo wanawaambia watoto wa MUNGU aliowaumba yeye peke yake watumie kondomu kujikinga na magonjwa na kupata mimba. Hii siyo sawa huyo ni yesu wa uongo ndie ndiye anayevunja amri ya MUNGU ya kuzini. Badala ya kuwaombea watoto wa MUNGU waache uzinzi wao wanawatengenezea njia ya kuepuka pigo la MUNGU wasipatwe na magonjwa na wazidi kuendelea na uzinzi na haijalishi hata hizo kondomu wanatumia na bado ukimwi wanapata, njia salama ni kuacha uzinzi tuu. Kuvaa kondomu ni mpango wa yesu kristo wa uongo katika makanisa na hukaa ndaniyao, msishangae wanapo yataja hayo hata makanisani au kuhamasisha semina watu wavae kondomu.


    18.               Yesu kristo wa uongo huongoza kanisa lake kwa sheria wanazopanga wao na siyo alizopanga MUNGU na hujipangia majira ya miaka yake katika imani hiyo japo jina la YESU hutajwa, mahali hapo sawa sawa na kitabu kinavyoelezea yaani Biblia ujue ni pa yesu wa uongo. Kwa nini mahali hapo au anayefuata hayo yanayofanywa au kupitishwa hapo huitwa yesu wa uongo? Ni kwa sababu hayo yanafanywa au kupitishwa hapo siyo ya YESU wa Nazareti au YESU wa ukweli. Na ikibidi waulize haya maswali hakika watakuzungusha tu hawana jibu la Biblia na kama hawana jibu la kwenye Biblia hayo majibu yametoka wapi? Jibu ni kuzimu. Na kama ni kuzimu na watu hao wanaongozwa na YESU wa uongo ili kuwaangamiza. Mwanadamu ufunguke ufahamu wako. YESU wa Nazareti amechukia sana pia na BABA yake yaani MUNGU na kwa ujumla serikali yote ya Mbinguni.

    Ujumbe huu ni kwa ajili ya ulimwengu wote.


    SALA YA TOBA.

     Kwa wewe ambaye haujaokoka soma sala hii:-

    BWANA YESU, nipo mbele zako mbele ya agano la Damu ya YESU, naomba unisamehe dhambi zangu zote, uliandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele, namkataa shetani na kazi zake zote, kuanzia leo mimi ni mali yako YESU, nishike mkono uniongoze milele, Amen. !!


    KUMBUKA :

    Maneno haya alivyonieleza mimi pia niliogopa sana, maana pia nilikuwa sijajua haya, akaniambia mwanangu HEBRON niandalie kanisa wakati wangu wa kurudi umekaribia ili nije kuwachukua wale walio wangu mimi YESU wa Nazareti, na uukomboe ulimwengu wote mimi nitakuwezesha na ndiye ninaekufundisha haya yote na ndie ninaye yasema haya yote kupitia kinywa chako, nimekushika mkono mimi YESU wa Nazareti usiogope atakayejaribu  tu kusema neno baya juu yako upanga wangu upo juu yake, atakayejaribu kukuangamiza ataangamia yeye mwenyewe, songa mbele. Waeleze watoto wangu kweli na uwafungue kutoka mateso ya shetani, uwaponye na uwapende watu wote wa ulimwengu  huu na uwaeleze habari hii njema kutoka kwangu mimi YESU wa Nazareti,  wanirudie mimi wasiangamie, maana 98% ya watu wote ulimwenguni tayari wameangamia, huo ndio ukweli na mimi siongezi lolote wala kuponguza. Nimeichagua Tanzania ndiyo Edeni na ndilo Taifa tajiri kuliko yote ulimwenguni. Anitengeneza nchi hii peke yake na mtayaona haya yote niwaambiayo.


    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate