*Page 21*
21
*Alikataa. Badala yake hasira iliota mizizi. Hakutaka kuileta kwangu.
Hasira *
*iliongezeka kila siku na alisema moyoni
mwake, "Nipo hapa namtumikia Mungu
kwa*
*moyo wote, na mume wangu anatembea na mwanamke mwingine! 'je hiyo ni sawa'*
*aliniuliza.*
*"Hapana sio sawa. Lakini alikuja na kuomba
msamaha na kusema kwamba*
*asingerudia tena.*
*"Nilimwambia, 'Binti, jikague mwenyewe, uone kama sio wewe mwenyewe*
*uliyesababisha haya"*
*"Sio mimi Bwana," alisema, mimi ni mtakatifu,
yeye ndiye mkosaji.'
Hakutaka*
*kunisikiliza.* *"Muda ulizidi kwenda. Hakuweza kuniomba au
kusoma Biblia. Alikuwa na
hasira si*
*kwa muwe wake tu, bali na kwa wale
waliomzunguka. Alinukuu Maandiko,
lakini* *hakuweza kumsamehe.*
*"Hakutaka kunisikiliza. Moyo wake ullizidi
kuwa na uchungu, na dhambi
kubwa*
*ilimwigia. Uuaji uliingia katika moyo wake
mahali ambapo zamani palikuwa na*
*upendo. Na siku moja, katika hasira yake
alimuua mume wake na yule mpenzi
wa*
*mume wake. Shetani alimwingia kabisa
akajiua."* Niliitazama roho ile iliyokuwa imepotea na
kumwacha Kristo na kuhukumiwa
moto na
mateso milele. Nilisikiliza alivyomjibu Yesu.
"*Sasa nitasamehe Bwana,"
alisema. "Nitoe* *huku. Sasa nitakutii. Ona Bwana, sasa
nahubiri Neno lako. Baada ya saa
moja mapepo*
*yatakuja na kunitesa zaidi. Yatanitesa kwa
masaa mengi. Kwa sababu
nilikuwa nahubiri* *Neno lako mateso yangu ni makubwa zaidi.
Tafadhali, Bwana, nakuomba
unitoe."*
Nililia pamoja na yule mwanamke aliyekuwa
katika shimo na kumwomba Bwana
aniepushe na machungu yote ya moyo. "*Usiruhusu chuki iingie katika moyo
wangu,*
*Bwana Yesu*." Nilisema
"*Haya, tuendelee mbele." *Yesu alisema.
Katika shimo lingine kulikuwa na mwili wa
mwanaume, akilia*, "Bwana," alilia, "nisaidie*
*kuelewa kwanini nipo hapa."*
Yesu alimwambia. "*Amani, tulia. Utaelewa
kwa nini upo hapa*."
"*Nitoe, nami nitakuwa mtu mzuri." *Yule mtu
aliomba. Yesu alimjibu, "*Hata kuzimu bado
unadanyanya."*
------------------------------
*Page 22*
22
Ndipo Yesu aliponigeukia na kusema, "*Mtu huyu alikuwa na miaka 23
alipokuja hapa.*
*Hakutaka kusikiliza injili yangu. Alisikia Neno
langu mara nyingi na mara
nyingi*
*alikuwa katika nyumba yangu. Nilimvuta kwa Roho wangu aingie katika
wokovu,*
*lakini aliipenda dunia na tama zake. Alipenda
kunywa na hakutaka kusikia
wito*
*wangu. Alilelewa kikanisa lakini hakutaka kujitoa kwangu. Siku moja
aliniambia,*
*"siku moja nitatoa maisha yangu kwako,
Yesu." Siku hiyo haikufika. Usiku
mmoja,*
*baada ya sherehe, alipata ajali mbaya ya gari akafa. Shetani alimdanganya
mpaka*
*mwisho.*
*"Aliuawa pale pale. Alipuuza wito wangu.
Watu wengine vile vile walikufa
kwenye* *ajali ile. Kazi ya Shetani ni kuua, kuiba na
kuharibu. Laiti kama kijana
huyu*
*angelinisikiliza! Sio mapenzi ya Baba kwamba
mtu yeyote apotee. Shetani
alikuwa* *anaitaka roho ya mtu huyu, na aliiharibu
kupitia kutokujijali, dhambi na
vinywaji*
*vikali. Nyumba zinaharibiwa kila mwaka kwa
sababu ya pombe."*
Laiti watu wangetambua kwamba tamaa za dunia ni zakitambo tu! Ukija kwa Yesu
atakuokoa na vinywaji vikali. Mwite Yesu,
atakusikia na kukusaidia. Atakuwa
rafiki yako.
Kumbuka kwamba anakupenda, na kwamba
anao uwezo wa kusamehe dhambi zako. Wakristo wenye ndoa, Yesu anawaonya
kwamba msizini. Ukimtamani mtu wa jinsia
tofauti na yako, hata kama hujakutana naye
kimwili, ni uzinzi moyoni mwako.
Vijana, kaa mbali na madawa ya kulevya na
ngono. Ukitenda dhambi Mungu atakusamehe. Mwite sasa wakati nafasi ipo.
Watafute Wakristo wakubwa,
waulize kama
mnaweza kujadiliana juu ya matatizo yako.
Utashukuru kwamba ulipata muda
sasa katika ulimwengu huu kabla hujachelewa.
Shetani anakuja kama malaika wa nuru
kuudanganya ulimwengu. Ndio maana
dhambi za
ulimwengu huu zilionekana kuvutia kwa kijana
huyu, ingawaje alilijua Neno Takatifu la
Mungu. Sherehe moja zaidi, aliwaza, Yesu
ataelewa bwana. Lakini kifo hakina
huruma.
Alingojea mno.
Niliitazama roho ya mtu yule, nilikumbushwa juu wa watoto wangu*. "Oh
Mungu, ebu*
*waokoe." *Najua kwamba wengi mnaosoma
haya mna watoto wenu, labda watoto,
ambao
hamtaki waende kuzimu. Waambie habari za Yesu wakati muda upo bado. Waambie
watubu dhambi zao na Mungu atawasamehe
na kuwatakasa.
Vilio vya yule mtu vilinisumbua moyoni
mwangu siku nyingi. Sitasahau kamwe
vilio vyake vya majuto. Nakumbuka nyama yamwili wake
ikining'nia na kuungua katika moto.
Sitasahau uozo,harufu ya mauti, mashimo
mahali ambapo palikuwa na macho,
roho
chafu ya kijivu na mafunza yaliyokuwa yanapita kwenye mifupa. Mikono ya
skeletoni ya
yule mtu aliinyosha kwa Yesu akimsihi huku
tukielekea kwenye shimo lingine.
------------------------------
*Page 23* 23
*"Bwana Mpendwa*,' niliomba, *"nipe nguvu za
kuendelea."*
Nilisikia sauti ya mwanamke ikilia kwa
kutapatapa. Vilio vya wafu vilikuwa
kila mahali. Kisha tulifika kwenye shimo alimokuwemo yule
mwanamke. Alikuwa anaomba kwa
roho
yake yote Yesu amtoe kule. "*Bwana*,"
alisema, "*Sijakaa huku vya kutosha?
Mateso yangu* *ni zaidi ya ninavyoweza kuvumilia.
Nakuomba, Bwana, nitoe.*" Kilio cha
kwikwi kilitikisa
mwili wake, na kulikuwa na maumivu hata
katika sauti yake. Nilijua kwamba
alikuwa anateseka kweli kweli.
Nilisema, "*Yesu, huwezi kufanya lolote?"*
Yesu alizungumza na yule mwanamke*.
"Ulipokuwa duniani*," alisema, *"nilikuita
na*
*kukuita uje kwangu. Nilikuhimiza urekebishe moyo wako, uwasamehe wengine,*
*utende yaliyo sawa, kaa mbali na dhambi.
Hata usiku wa manane
nilikutembelea na*
*kukuvuta kwangu kwa Roho wangu. Kwa
midomo yako ulisema unanipenda, lakini* *moyo wako ulikuwa mbali nami. Hukujua
kwamba hakuna kitu ambacho
kimefichika*
*kwa Mungu? Uliwadanganya wengine, lakini
usingeweza kunidanganya mimi.
Bado* *niliwapeleka wengine wakwambie utubu, lakini
hukusikia. Hukutaka kusikia,*
*hukutaka kuona, na katika hasira
uliwafukuza. Nilikuweka mahali ambapo
ungeweza*
*kusikia Neno langu, lakini hukutaka kutoa roho yako kwangu.*
*"Hukusikitika, wala hukuona aibu kwa yale
uliyokuwa unayafanya. Uliufanya
moyo*
*wako kuwa mgumu na ulinipa kisogo. Sasa
umepotea milele. Ulipaswa kunisikiliza."*
Kwa kusikia haya, alimtaza Yesu na kuanza
kumlaani Mungu. Nilihisi uwepo wa
roho
chafu na nilijua kwamba ndizo zilizokuwa
zinalaani na kuapa. Inasikitisha kweli kupotea
milele kuzimu. Mpinge Sheatani wakati
unaweza, na atakukimbia.
Yesu alisema, "*Dunia na vyote vilivyomo
vitapita, lakini maneno yangu
hayatapita*." ------------------------------
*Page 24*
24
*Sura ya 5*
*Pango la Hofu*
Nilijaribu kukumbuka mahubiri niliyowahi kusikia kuhusu kuzimu. Lakini
sikuwahi kusikia
mambo ya kutisha kama ambayo Bwana
alikuwa ananionyesha hapa. Kuzimu
kulikuwa
kubaya mno kuliko mtu yeyote anavyoweza kudhani au kuwaza. Iliniumiza sana
kujua
kwamba roho zilizokuwa zinateseka kuzimu
zitakuwa kule milele. Hakuna namna
ya
kutoka. Nimedhamiria kwamba nitafanya kila
linalowezekana lililo katika uwezo wangu
kuziponya
roho na mateso haya. Ni lazima nimhubirie kila
ninayekutana naye, maana
kuzimu ni mahali pa kutisha, na hii ni taarifa ya kweli.
Unaelewa ninachosema? Kama
wenye
dhambi hawatatubu na kuiamini injili, kwa
vyovyote vile wataishia kuzimu.
Mwamini Bwana Yesu Kristo, na mwite akuokoe na dhambi. Soma sura ya 3 na ya
14 ya
Injili ya Yohana. Halafu tafadhali soma kitabu
hiki toka mwanzo hadi mwisho
ili uelewe
zaidi habari za kuzimu na maisha ya baadaye. Unapoendelea kusoma mwombe Yesu
aingie katika moyo wako na asafishe dhambi
zako usije ukachelewa.
Yesu alitembea kuelekea kuzimu. Njia ilikuwa
umeungua, kavu,
imepasukapasuka na yenye ukiwa. Niliona mistari ya mishimo mpaka
mwisho wa upeo wa macho.
Nilichoka
sana. Moyo wangu, na roho yangu ilivunjika
kutokana na yale niliyoyaona na
kuyasikia, na hata hivyo nilijua kwamba mengi yalikuwa
yananisubiri mbele.
"*Yesu, nipe nguvu za kuendelea*," nililia.
Yesu alitangulia, nami nilimfuata nyuma kwa
karibu. Nilijaa huzuni kwa
ajili ya mambo ambayo nilikuwa nimeyaona. Nilikuwa najiuliza
kimoyomoyo kama walimwengu
watanisadiki. Nilitazama kulia kwangu na
kushoto kwangu na nyuma
yangu-kulikuwa na
mashimo ya moto kwa kadri ya upeo wa macho yangu. Nilizungukwa na moto, na
roho
zinazoungua. Nililia kwa uchungu mwingi.
Utisho na ukweli wa mambo ambayo
nilikuwa
nayaona yalikuwa makubwa mno kwangu kuyabeba.
"*O dunia tubu*," nililia. Kwikwi za kilio zilitikisa
mwili wangu
nilipoendelea kutembea na
Yesu. Nilikuwa najiuliza kitu gani kitafuata.
Nilikuwa natakakari kwamba sijjui familia
yangu na ndugu zangu walikuwa wanafanya
nini. Lo, nilikuwa nawapenda
kwelikweli!
Nilikumbuka jinsi nilivyokuwa nafanya dhambi
kabla sijarejea kwa Bwana Yesu, na
nilimshukuru Mungu kwamba nilirejea wakati
muda ulikuwepo bado.
Yesu alisema, *"Sasa tunataka kuingia katika
pango ambalo litatupeleka
ndani ya* *tumbo la kuzimu. Umbo la kuzimu ni kama
mwanadamu aliyelala katikati ya
dunia.*
------------------------------
*Page 25*
25 *Mwili umelala chali, mikono na miguu
imenyooka. Jinsi nilivyo na mwili wa*
*waumini, ndivyo kuzimu kulivyo na mwili wa
dhambi na mauti. Kama vile
mwili wa*
*Kristo unavyojengeka kila siku, ndivyo hivyo hivyo mwili wa kuzimu
unavyojengeka*
*kila siku*."
Tulipokuwa tunakwenda kwenye pango, tulipita
kwenye mashimo ya moto na
vilio vya waliohukumiwa vilikuwa vinasikika. Wengi
walimwita Yesu tulipokuwa
tunapita. Wengine
walijaribu kupanda kutoka kwenye mashimo
ya moto ili kumfikia, lakini
hawakuweza. Mmechelewa, mmechelewa, roho yangu ililia.
Uso wa Yesu ulijaa masikitiko tulipokuwa
tunatembea. Nilipoyatazama mashimo
ya moto
nilikumbuka jinsi tulivyokuwa tunapika kutumia
mkaa nyuma ya nyumba yetu na jinsi
makaa yalivyokuwa yanawaka kwa masaa
mengi kwa rangi nyekundu. Ndivyo
nilivyoona
kuzimu.
Nilishukuru tulipoingia kwenye pango. Niliwaza, pangoni hamuwezi kuwa
pabaya kuliko
mashimo ya moto. Kumbe!
Mara tulipoingia ndani nilianza kuona manyoka
makubwa, panya wakubwa, na
roho wachafu wengi, wote wakikimbia kutoka
kwenye uwepo wa Mungu. Nyoka
walitupigia
mirusi na panya walipiga kelele. Kulikuwa na
kelele nyingi mbaya. Nyoka
wakali na vivuli vyeusi vilituzunguka. Yesu alikuwa ndio
mwanga pekee ulioonekana katika
pango. Nilikaa
karibu sana na Yesu.
Mapepo yalikuwa pande zote za pango, na
yalikuwa yanakwenda mahali fulani juu na nje
ya pango. Baadaye nilitambua kwamba
mapepo haya yalikuwa yanakwenda duniani
kufuata maagizo ya Shetani.
Akihisi hofu yangu ya mahali hapa penye giza,
unyevunyevu na uchafu, Yesu alisema,
"*Tutafika mwisho wa pango hivi karibuni.
Lazima nikuonyeshe mambo haya.
Njoo,*
*nifuate*."
Majoka makubwa yalitambaa kupitia tulipokuwapo. Majoka mengine yalikuwa na
ukubwa
wa futi nne, na urefu wa futi ishirini na tano.
Kulikuwa na hewa chafu,
nzito, na pepo
wachafu walikuwa kila mahali. Yesu alisema, "*Tutafika sasa hivi kwenye
tumbo la kuzimu. Sehemu hii ya
kuzimu*
*ina kimo cha maili kumi na saba na maili tatu
kuzunguka, kama duara*."
Yesu alinipa vipimo kamili.
Nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu
kuandika na kusimulia yote
niliyoyaona na kusikia.
Nitafanya kwa utukufu wa Baba, utukufu wa
Mwana na utukufu wa Roho Mtakatifu.
Mapenzi ya Mungu yafanyike.
------------------------------
*Page 26*
26
Nilijua kwamba Yesu alikuwa ananionyesha mambo yote haya ili niwaonye
wanaume na
wanawake wa dunia kuiepuka kuzimu kwa
gharama yoyote ile. Mpendwa, kama
unasoma
haya na bado humfahamu Yesu, acha kila kitu, tubu dhambi zako, na mwalike
awe
Mkombozi wako.
*Sura ya 6*
*Matendo Katika Kuzimu*
Mbele yetu niliona mwanga hafifu.Yesu na mimi tulitoka kwenye pango la
kutisha na
tulisimama kukabiliana na tumbo la kuzimu.
Niliona, kwa kadri ya upeo wa
macho,
shughuli nyingi zikifanyika katikati mwa kuzimu.
Tulisimama, na Yesu alisema. "*Ninakwenda
kukupitisha kwenye tumbo la
kuzimu, na*
*nitakufunulia mambo mengi. Njoo, nifuate*."
Sisi wawili tulitembea kuelekea mbele.
Yesu alisema, "*Mbele yetu kuna mambo
mengi ya kuogofya. Sio hisia za mtu
fulani,*
*ni mambo ya kweli. Hakikisha unawajulisha
wasomaji wako kwamba nguvu za* *mapepo ni halisi. Waambie kwamba Shetani ni
halisi, na nguvu za giza ni
halisi.*
*Waambie wasikate tamaa, maana ikiwa watu
wangu walioitwa kwa Jina langu *
*watajinyenyekeza na kuomba na kuacha njia zao mbaya, nitawasilikiliza
kutoka*
*mbinguni na kuiponya nchi yao na miili yao.
Jinsi vile ambavyo mbinguni ni
halisi ,*
*ndivyo kuzimu kulivyo halisi *" Mungu anataka ujue habari za kuzimu, na
anataka akuokoe usiende kuzimu.
Mungu
anataka ujue kwamba kuna njia ya kutokea,
na njia hiyo ni Yesu Kristo,
Mwokozi wa roho yako. Kumbuka, ni wale tu ambao majina yao
yameandikwa kwenye Kitabu cha
Uzima
cha Mwana Kondoo ndio watakaookoka.
Tulifika kwenye shughuli ya kwanza katika
tumbo la kuzimu. Ilikuwa kulia kwa pale
tulipoingilia na juu ya kilima kidogo kwenye
kona ya giza ya kuzimu.
Nilikumbuka maneno ya Bwana aliponiambia,
"*Mara nyingine nitakuwa kama*
*nimekuacha, lakini sitakuacha. Kumbuka kwamba nina mamlaka yote mbinguni
na*
*duniani. Wakati mwingine mapepo na roho
zilizopotea hazitatuona au kujua*
*kwamba tupo hapa. Usiogope.
Unachokwenda kuona ni halisi. Mambo haya* *yanatokea sasa hivi na yataendelea kutokea
mpaka kifo na kuzimu
vitakapotupwa*
*katika ziwa la moto.*"
------------------------------
*Page 27* 27
Msomaji, hakikisha kwamba jina lako
limeandikwa kwenye Kitabu cha Uzima cha
Mwana
Kondoo.
Mbele yetu nilisikia sauti na vilio vya roho ikiwa kwenye mateso. Tulipanda
kilima na
kuangalia. Mwangaza ulikuwepo kwa hiyo
niliweza kuona waziwazi, vilio
ambavyo huwezi
kudhania kuwa vinaweza kuwepo viliijaza anga. Vilikuwa vilio vya mwanaume.
"*Nisikilize*," Yesu alisema. "*Unachokwenda
kusikia ni kweli. Jihadharini
enyi wahubiri*
*wa injili, maana haya ni maneno ya uaminifu
na kweli. Amkeni wainjilisti, wahubiri,*
*na waalimu wa neno langu, nyie wote ambao
mmeitwa kuhubiri injili ya Bwana
Yesu*
*Kristo. Kama unafanya dhambi tubu, la sivyo
utaangamia vile vile*." Tulitembea hadi futi kumi na tano kutoka
shughuli hii. Niliviona viumbe
vidogo vimevaa
nguo nyeusi vikitembea kuzunguka kitu kama
sanduku. Baada ya kuchunguza
zaidi niliona kwamba sanduku lile lilikuwa jeneza na
viumbe vilivyokuwa
vinazunguka vilikuwa
mapepo. Lilikuwa jeneza la kweli, na kulikuwa
na mapepo kumi na mawili
yakitembea kulizunguka. Walikuwa wanalizunguka jeneza
wakiimba na kucheka. Kila mmoja
alikuwa
na mkuki mkali mkononi mwake, ambao
alikuwa akichoma kwenye jeneza kupitia
vitundu vidogo.
Kulikuwa na hali ya hofu kuu hewani, na
nilitetemeka nilipoona yaliyokuwa
mbele yangu.
Yesu aliyatambua mawazo yangu, kwa maana
alisema, "*Mtoto, kuna roho nyingi zikiwa*
*kwenye mateso hapa, na kuna aina nyingi za
mateso kwa ajili ya roho hizi.
Kuna*
*adhabu kubwa zaidi kwa wale ambao
walikuwa wahubiri wa injili halafu wakaanguka*
*katika dhambi, au ambao hawakuitikia wito wa
Mungu katika maisha yao*."
Nilisikia kilio kilichoujaza moyo wangu na hali
ya kukata tamaa. "Hakuna
tumaini, hakuna tumaini!" aliita. Kilio hiki cha kukata tamaa
kilitoka kwenye jeneza.
Ulikuwa mlio mfululizo
wa kukata tamaa.
"Mungu, inasikitisha kweli!" Nilisema.
"*Njoo*." Yesu alisema, "*Twende karibu zaidi*." Baada ya kusema hayo
alisogea karibu
na jeneza na kutazama ndani. Nami nilifuata,
nikatazama ndani. Ilionekana
kwamba wale
pepo wachafu walikuwa hawatuoni. Ukungu mchafu wa kikahawia uliijaza jeneza.
Ilikuwa roho ya mtu. Mapepo
walichoma
mikuki yao ndani ya jeneza huku nikiangalia.
Sitasahau kamwe kuteseka kwa roho hii.
Nilimlilia Yesu, "*Mtoe Bwana, mtoe*." Mateso ya
roho yake yalikuwa ya kusikitisha. Laiti kama
angelitoka. Nilimvuta mkono
Yesu na
kumwomba amtoe mtu yule kwenye jeneza.
------------------------------ *Page 28*
28
Yesu alisema, "*Mwanangu, amani, tulia*."
Yesu aliposema hivyo, yule mtu alituona.
Alisema, "*Bwana, Bwana, nitoe.
Nihurumie*." Nilitazama ndani ya jeneza na kuona roho.
Ndani ya roho kulikuwa na moyo wa
mwanadamu, na damu ilibubujika kutoka
kwenye moyo huo. Kule kuchomwa mikuki
kulikuwa kunaichoma roho yake.
"*Sasa nitakutumikia Bwana*." Alisihi, "*Nakuomba nitoe*." Nilijua kwamba
mtu huyu alisikia
uchungu wa kila mkuki uliomchoma.
"*Anateswa usiku na mchana*." Bwana
alisema, "*Aliwekwa hapa na Shetani, na*
*Shetani ndiye anayemtesa*." Yule bwana alilia,"Bwana, sasa nitahubiri injili
ya kweli. Nitahubiri juu
ya dhambi na
kuzimu. Lakini nakuomba nitoe hapa."
Yesu alisema, "*Mtu huyu alikuwa mhubiri wa
Neno la Mungu. Kuna wakati* *alinitumikia kwa moyo wake wote na
kuwaongoza wengi kwenye toba. Baadhi ya*
*watu waliookolewa wananitumikia hadi leo, na
miaka mingi imepita. Tamaa ya
mwili*
*na udanganyifu wa mali ulimpotosha. Alimruhusu Shetani amtawale. Alikuwa
na*
*kanisa kubwa, gari zuri na kipato kizuri.
Alianza kuiba sadaka.
Alizungumza zaidi*
*nusu uongo na nusu kweli. Hakutaka nimsahihishe. Nilimpelekea wajumbe
wangu*
*kumwambia atubu na kuhubiri kweli, lakini
alipenda zaidi anasa za dunia
hii kuliko*
*maisha ya Mungu. Alijua kutokufundisha au kuhubiri ukweli wowote isipokuwa
ule*
*uliuofunuliwa katika Biblia. Lakini kabla hajafa
alisema kwamba ubatizo wa
Roho*
*Mtakatifu ulikuwa ni uongo na wale waliosema kuwa wanaye Roho Mtakatifu*
*walikuwa wanafiki. Alihubiri kwamba unaweza
kuwa mlevi na ukaenda
mbinguni,*
*hata bila kutubu.*
*"Alisema kwamba Mungu asingempeleka mtu yeyote kuzimu – kwamba Mungu *
*alikuwa mwema sana asingefanya hivyo.
Alisababisha watu wengi kukosa neema*
*ya Bwana. Hata alisema hanihitaji, kwa
sababu alikuwa kama Mungu.
Alikwenda* *hadi kiasi cha kuendesha semina kufundisha
mafundisho haya ya uongo.*
*Alilikanyaga Neno langu takatifu chini ya
miguu yake. Hata hivyo,
niliendelea*
*kumpenda.* *"Mwanangu, heri kutokunijua kabisa kuliko
kunijua halafu ukageuka na
kuacha*
*kunitumikia*," Bwana alisema
"*Heri kama angelikusikiliza, Bwana*!" Nililia.
"*Heri kama angeijali roho yake na roho za *
*watu wengine."*
------------------------------
*Page 29*
29
*"Hakunisikiliza. Nilipokuwa namwita hakusikia. Alipenda maisha ya raha.
Nilimwita*
*na kumwambia atubu, lakini hakutaka
kunirudia. Siku moja aliuawa na akaja
hapa*
*moja kwa moja. Sasa Shetani anamtesa kwa sababu aliwahi kuhubiri Neno
langu na*
*kuwaokoa watu wengi kwa ajili ya ufalme
wangu. Haya ndio mateso yake*."
Niliangalia mapepo yalivyozidi kuzunguka
jeneza. Moyo wa mtu yule ulidunda na damu ya
kweli ilichirika. Sitasahau kamwe kilio chake
cha maumivu na huzuni.
Yesu alimtazama yule mtu kwenye jeneza
kwa huruma kubwa na kusema, "*Damu
ya* *roho nyingi zilizopotea iko kwenye mikono ya
mtu huyu. Wengi wao wamo
katika*
*mateso hivi sasa*." Kwa mioyo ya huzuni
mimi na Yesu tulisogea mbele.
Tulipokuwa tunaondoka, niliona kundi lingine la mapepo likienda kwenye
jeneza. Yalikuwa
na urefu wa kama futi tatu, yamevaa nguo
nyeusi, na vitambaa vyeusi kuziba
nyuso zao.
Walikuwa wanabadilishana zamu kuitesa roho hii.Tunakataa kutubu na
kujishusha,
utadhani sisi tu ndio tuko sawa wakati wote.
Lakini sikiliza, roho, kuzimu
ni halisi.
Tafadhali sana usiende mahali kule. Ndipo Yesu aliponionyesha saa kubwa,
imeujaza ulimwengu wote. Niliisikia
ikienda tik tak
tik tak. Mshale wa saa ulikuwa unakaribia
majira ya saa sita, na mshale wa
dakika ulikwenda mbio na kusimama dakika tatu kabla
ya saa sita. Taratibu mshale
wa dakika
ulisogelea saa sita kamili. Ulipokuwa unasogea
mbele mlio wa saa
uliongezeka mpaka ukaonekana kama unaijaza dunia nzima.
Mungu alizungumza kama tarumbeta, na sauti
yake kama ya maji mengi. "*Sililiza
*
*ambayo Roho ayaambia makanisa," alisema.
"Iweni tayari, maana kwa wakati* *msiodhania, nitakuja tena. Nasikia saa ikilia.
Ni saa sita. Bwana harusi
amekuja kwa*
*ajili ya bibi harusi wake*"
Je uko tayari kwa ajili ya kuja kwa Krsito,
rafiki yangu? Au uko sawa na wale wanaosema,
"*Sio leo, Bwana*?" Je unaweza kumwita ili
uokolewe? Je unaweza kumpa roho
yako leo?
Kumbuka, Yesu anaweza kukuokoa kutoka
maovu yote kama utamwita leo, na kutubu.
Omba kwa ajili ya familia yako na wapendwa
wako ili wamwendee Yesu wasije
wakachelewa.
Sikiliza Yesu anavyosema, "*Nitakulinda na
mabaya. Nitakuchunga katika njia zako*
*zote. Nitakuokoa. Nitawakoa unaowapenda.
Niite leo upate kuishi*."
Kwa machozi mengi ninaomba kwamba nyie
wote mnao soma kitabu hiki mtajua
kweli bila kuchelewa. Kuzimu ni milele. Ninajitahidi
kwa kadri ya uwezo wangu
kuyaeleza yote
niliyoyaona na kusikia. Najua mambo haya ni
kweli. Unapoendelea kusoma
sehemu inayobaki ya kitabu hiki, ninaomba kwamba
utatubu na kumchukua Yesu kuwa
Mwokozi
wako binafsi.
------------------------------
*Page 30* 30
Nilisikia Bwana akisema, "*Ni wakati wa
kuondoka. Tutarudi tena kesho*."
*Sura ya 7*
*Tumbo la Kuzimu*
Usiku uliofuata Yesu na mimi tulikwenda kuzimu tena. Kwanza tuliingia
kwenye sehemu
kubwa ya wazi. Kwa kadri ya upeo wa macho
yangu, vitendo viovu vilikuwa
vikiendelea.
Vingi ya vitendo hivi vilikuwa vinafanyika maeneo yaliyotuzunguka. Kama
futi kumi hivi
kutoka mahali tulipokuwa tumesimama , niliona
kitu cha pekee, cha pekee kwa
sababu
viumbe viovu na pepo wachafu waliingia na kutoka kwa haraka mahali pale.
Ilikuwa kama sinema ya kutisha. Kwa kadri ya
upeo wa macho yangu, roho
zilikuwa katika
mateso, na ibilisi na malaika zake walikuwa
kazini. Ile hali ya giza giza ilijaa kelele za
uchungu na kukata tamaa.
Yesu alisema, "*Mtoto, Shetani ni mdanganyaji
duniani na mtesi wa roho
kuzimu.*
*Nguvu za kipepo unazoziona hapa mara ingine huenda duniani kuumiza, *
*kusababisha mateso na kudanganya.
Nakwenda kukuonyesha mambo ambayo *
*hayajawahi kuonekana kwa undani namna hii.
Baadhi ya mambo utakayoyaona*
*yatakuwa yanatokea hivi sasa, na baadhi ya mambo yatatokea baadaye*."
Nilitazama mbele tena. Ardhi ilikuwa ya rangi
ya kijivu, bila maisha , wala
kitu chochote
cha kijani. Kila kitu kilikuwa kimekufa au katika
hali ya kufa. Sehemu nyingine zilikuwa
baridi na nyevu nyevu, na nyingine zilikuwa
moto na kavu. Na wakati wote
kulikuwa na
harufu nzito, mbaya, ya nyama inayochomwa
na kuoza, ikichanganyikana na harufu ya
mavi, na takataka zilizooza.
"*Shetani anatumia mitego mingi
kuwadanganya watu wa Mungu," *Yesu
alisema*.
* *"Katika safari zetu za kuzimu nitakuonyesha
UNABII WA KWELI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni