Wafilipi 2:10-11
 • UNABII WA KURUDIWA UCHAGUZI WA URAIS KENYA 2017 ULISHATABIRIWA MWAKA 2013

  BWANA YESU ASIFIWE!

  Hatimae unabii aliyotabiri Nabii Hebron umetimia na kuelezwa na BWANA YESU mwaka 2013 kuhusu uchaguzi uliyopita. YESU alimwambia uchaguzi utarudiwa tu na leo umetimia kupitia supreme court ya Kenya, umefuta uchaguzi wa Kenya wa 2017 na kuamuru urudiwe upya.

  Maneno haya YESU alimwambia na akamwambia itatimia na yule aliyempanga awe kiongozi wa nchi hiyo itatimia. MUNGU ndiye amesimamia haki; hivyo Utukufu arudishiwe MUNGU na siyo wanadamu. Zaidi utasoma blog ya unabii huo katika blog ya Nabii Hebron 17th February 2013.

  MANENO YA MUNGU WA KWELI HAYAENDAGI BURE, LAZIMA NENO LAKE LITIMIE, NA LIMETIMIA.

  UBARIKIWE!  Nakusalimu kwa jina la YESU KRISTO wa Nazarethi, aliye hai, Mfalme wa Wafalme.

  Huu ni unabii ambao tayari ndivyo ilivyo na itakavyokuwa, ndiye Rais atakayeshinda uchaguzi wa rais. Japo kabla ya kumtaja, kwanza kabisa iliandaliwa mipango ya kuhakikisha hataishi, ila MUNGU ndiye anayemlinda na hakuna la adui litakalofanikiwa juu yake, ila asijishughulishe na mambo ya kishirikina atamuudhi YESU na kuachwa, hivyo kusababishwa uchaguzi kurudiwa upya.

  Atakayekuwa rais ni mgombea ambaye ni waziri mkuu katika nchi hiyo, na huyu kupitia yeye nchi itainuliwa sana na maisha ya wananchi hao yatakuwa mazuri."
  Nawasalimu katika jina la YESU KRISTO wa Nazareth aliye hai, BWANA wa Mabwana, MUNGU wa miungu, ambaye ndiye MUNGU wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.

  Ndugu Wakenya, MUNGU anawapenda sana. Niliyajua haya nilipowekewa mzigo moyoni mwangu kuombea nchi ya Kenya, hasa ni katika uchaguzi mkuu 2013. Wananchi wa Kenya, kwa rangi zote, makabila yote, na watu kwa jinsia zote; nyie wote ni yeye kawaumba na nyie ni mali ya MUNGU, na MUNGU anawawazia mema na siyo mabaya, ila shetani anaiwazia mabaya nchi yenu. Ila, mkitii haya niliyoelezwa na MUNGU, shetani atashindwa kuleta machafuko katika uchaguzi wa mwaka 2013.

  MUNGU ameniambia watu wote na vyama vyote anawapenda sana, japo nitaendelea kuiombea tu ili kusudi la MUNGU lisimame. Watoto wa MUNGU, kuhusu suala la uchaguzi haswa la Urais, muombeni MUNGU awape kiongozi ambaye MUNGU ndiye atakayewapa awaongoze. Yeye anamjua yupi atawaongoza vema, na atakuwa mwema na mwenye hekima, YESU akaniambia, watu wanaomba tu kama wanavyotamania, ila siyo MUNGU anavyotaka na madhara ya kuomba unachotaka, utapewa ila usimlaumu MUNGU. Ila mkimuomba wape kiongozi wa kuongoza mzuri hakika atawapatia, hivyo baadhi wanaomba kwa kumpenda wanayemtaka, ila hawajui ndani ya moyo atafanyaje. Muache ukabila, kabila zote ni za MUNGU, nay eye ndiye muasisi wa lugha zote, wekeni ukabila mbali muwe na umoja, upendo na mshikamano. Nyakati hizi ingieni kwa maombi, mwachieni MUNGU awape rais yeye, hii ni siri ya MUNGU, japo ninajua kila kitu na matokeo ya uchaguzi wa nchi hii ila sijaruhusiwa kutamka.

  Ujumbe:
  Muombeni yeye awachagulie kiongozi mwema, maana wengine ndani yao hawaiwazii mema nchi, ila yote MUNGU ameyaona, na ameniambia kanisa lijipange upya kwa kumuomba MUNGU awape kiongozi kutoka kwake na si vinginevyo, na yeye atafanya. MUNGU ibariki Kenya, wafungue fahamu zao wale wasiojielewa kuhusu uchaguzi 2013.

  Hakuna maoni:

  Visits

  Translate