Wafilipi 2:10-11
  • JE, UNAMWABUDU SHETANI AU MUNGU WA KWELI? UTAJUAJE?


    KITABU: JINSI KANISA LINAVYO ABUDU SHETANI

    JINSI KANISA LINAVYO ABUDU SHETANI

    KIMEANDIKWA  NA MTUME NA NABII

    HEBRON WILSON KISAMO.


    YALIYOMO

    1.    SANAMU NI NINI KATIKA KANISA?

    2.    IBADA ZA WAFU

    3.    SADAKA ZA MAVUNO

    4.     MADHABAHU ILIYOKUFA

    5.     SADAKA NI NINI?

    6.    KWA NINI MADHABAHU ZINAKUFA

    7.    SALA YA TOBA

    CONTACTS: 

    +255 759 610 820

    +255 718 154 433

    +255 718 916 864

    +255 764 042 149

    EMAIL: publications@prophethebron.org

                 maombi@prophetehebron.org

    Website: www.prophethebron.org


    TOLEO LA TATU

    JULY 2012

    ISBN – 978-9987-9553-3-6

    UTANGULIZI

    Ndugu nakusalimu kwa jina la YESU  KRISTO, ambaye ndiye Bwana na Mwokozi  wa Mataifa yote, pia ndiye Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana na hapana Mfalme mwingine zaidi yake. Mimi jina langu naitwa Hebron Wilson Kisamo, YESU amenichagua nimtumikie yeye kwa jinsi anavyotaka yeye ili kukomboa ulimwengu huu ambao umepotea  na shetani ameumiliki kwa asilimia 98% sawa sawa na YESU alivyoniambia mwenyewe. Amenituma ulimwengu wote ikiwa inamaana nchi zote, mabara yote. Ujumbe huu aliniagiza  rasmi na kunipa  mamlaka yake  tarehe 14.06.2010. Na akanipa jina la Kanisa lake niliite  YESU NI BWANA NA MWOKOZI  WA MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRY.  Akaniambia mwanangu nitautumia huu mwili wako kuukomboa ulimwengu wote, utachukiwa sana,utafanyiwa na kuitwa majina mabaya lakini usiogope tena ufurahi zaidi, kwani mimi YESU walinifanyia mabaya  zaidi na ya uongo yakitokea kwa baba yao wa uongo ambae ni lusifa, nilifurahi daima.

    Hakuna jambo lolote litakalofanikiwa juu yako au silaha yoyote juu yako, nipo na wewe milele. Nitakutumia kwa namna ya tofauti na kwa kiwango kikubwa sana ambacho hakijaonekana tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu. Adui yako ni adui yangu, akasema YESU kwa sauti ya uchungu sana, watumishi wamenisaliti maagizo niliyowapa hawayafanyi na wamegeuza  NENO langu kuwa maandiko badala ya Neno, maandiko yanatoka kwa shetani maana lusifa anaijua Biblia yote, na maandiko hayana uthibitisho wa nguvu zake YESU. Neno  linatoka kwa YESU na lina udhihirisho wa nguvu za  MUNGU. Napia wana wa adamu wanateseka wanalia na kuomba hawapati majibu, na zaidi wanazidi kupotoshwa na viongozi wa kanisa, maagizo niliyoyaacha nilivyokuwa ulimwenguni kabla ya kurudi kwa BABA yangu ili  kuniandalia maandalizi ya ujio wangu ili nipate kuwaponya wengi waende mbinguni, imekuwa kinyume idadi kubwa ni ya watu wa shetani. Waliokuwa  watumishi wangu wamenisaliti 98% sipo nao. Wameamua kwenda kuzimu, na shetani anawatumia na jinsi anavyowatumia, ni kubadili au kwenda kinyume na agizo la MUNGU, mfano watumishi kwa sasa wamefanya kanisa ni mahali pa biashara, kunyanganya  watu  vitu vyao na wakijua wamenitolea mimi, na kunifanya mimi YESU ndiye mnyanganyi, kwa midomo yao hunitaja kama wananipenda ila mioyoni mwao hawapo na mimi, wamekuwa watumishi wa pesa na sio mimi, wamekuwa wakitenda miujiza lakini siyo yangu ni miujiza ya shetani, na hao ni kati ya wale ambao siku ya mwisho nitawakataa na kuwaambia sikujui. Kanisa  limeniacha kunitegemea mimi, imebaki 2 % tu ulimwengu mwote. Sasa  mimi YESU ninalikomboa kanisa mwenyewe na ndipo unabii na utukufu wa kanisa la mwisho utakuwa mkubwa kuliko wa kanisa la kwanza unatimia sasa.

    SHUKURANI

    Namshukuru  Mke wangu sana kwa kunitia moyo na kuniombea, nawashukuru watumishi wote wanaoniombea na kutumiwa na MUNGU kutumika pamoja na YESU aliyeniita, mkono wa MUNGU uwe juu yao siku zote za maisha yao.

    Asante.

    MTUME NA NABII – HEBRON WILSON KISAMO

    KIONGOZI NA MWANZILISHI  WA HUDUMA

    KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE

    INTERNATIONAL MINISTRY.

    P. O. BOX 13657

    ARUSHA, TANZANIA

    EAST AFRICA

    EMAIL: publications@prophethebron.org

                 maombi@prophetehebron.org

    Website: www.prophethebron.org



    1.    SANAMU NI NINI? ( Juu ya Kanisa) Torati 5: 8-9

    Sanamu ni kitu chochote kisicho na uhai.  Ni kitu kilichotengenezwa na mwanadamu na hakina uhai wala hakipumui wala kuongea.

    Asili ya kuwafanya watu waabudu sanamu ilitokea kwa Lusifa ( shetani), tokea vizazi na vizazi baada ya shetani  kuwateka wanadamu.

    Ndipo MUNGU akamtuma Musa ulimwenguni humu kuja kuwaokoa wana wa Israeli kwa Farao ili awatoe kifungoni, na alipokuwa amewatoa kifungoni , huyu huyu Musa ,alienda mlimani kuongea na MUNGU. Musa akakawia na  ndipo  MUNGU akamwambia, rudi nenda ukawaangalie watu wako  mana wana shingo ngumu  yaani hawaamini, hawaelewi, wametekwa na shetani na hata MUNGU wa kweli hawamtaki.

    Musa akakuta wametengeneza sanamu,mfano wa ndama ndio wanamuabudu, eti ndio mungu huyo !

    Ndugu msomaji na mwana wa MUNGU tena unafanana  nayeye na unapumua kama yeye, embu funguka ufahamu wako na akili yako umjue MUNGU wa kweli usiwe kama wale wana wa Israeli pale jangwani, walivyo muudhi MUNGU. ( Soma neno la MUNGU linaelezea waziwazi ya kwamba msiabudu sanamu, au kuifanya Mungu wakoutaangamizwa.Soma Kutoka 32: 35). MUNGU hakuwa mjinga kukuumba wewe kwa mfano wake, msaidizi ambaye ni amekuumba ili umwabudu yeye peke yake,wala usiabudu hata kitu alichokiumba yeye iwe nchi kavu, majini,hata angani,hata malaika wake, hata watakatifu walioko mbinguni –hao ni yeye amewaumba ni viumbe vyake vyote vinategemea msaada kutoka kwake, kwa taarifa kamili aliyoniambia YESU , mnaofanya hivyo mmepotea, nilipokuwa ulimwenguni niliwaahidi nitawatumia msaidizi ambaye ni ROHO MTAKATIFU. Ndiye yupo kwa ajili ya kukuombea wewe, sasa nikuulize swali, YESU alituachia  msaidizi na huyu msaidizi atakuongoza ili ufike mahali alipo YESU! Je YESU alisema hawa watakatifu ndio wawe wasaidizi wa kukuombea na kukuongoza? Jibu hapana; hapo tayari umeabudu sanamu na unapotea,funguka ufahamu hata kwenye kitabu cha Ufunuo  22:(19-20) Ole wake atakayeongeza maneno ya unabii wa kitabu hiki, nikuulize swali –je! Hawa watakatifu wapi kwenye Biblia tumeambiwa kuwa tuwaombe hao  watuombee? Tafuta – hakika 100% hautaona, huo ni mchomeko wa shetani ili wewe upotee uangamizwe, maana anayeabudu kitu tofauti na MUNGU wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo atahukumiwa. Soma  Kutoka 32:33 -35 na  Bwana atamfuta jina lake  katika kitabu cha uzima. Je wewe  unapenda ufutwe jina lako katika kitabu cha uzima? Jibu hapana.  Na kama unaabudu sanamu ujue kabisa wewe ni adui wa MUNGU, ni rafiki wa shetani. Yawezekana wewe haujui , unampenda MUNGU ila umeyarithi sasa yakatae ili upone, maana ni machukizo kwake.

    Ndugu msomaji, ukisoma katika kitabu cha torati 5: (8 -9 )  MUNGU amekataa usichonge au kujifanyia sanamu ya kitu chochote duniani, mbinguni, na hata kilicho chini ya bahari usikiabudu. Na  hii ni moja ya amri aliyompa Musa kwa ajili ya wanadamu wote. Ukisoma yeremia 17:5, 7 amelaaniwa  amtegemeaye mwanadamu, amebarikiwa amtegemeaye MUNGU, inamaana  kumwabudu yeye tu! Watakatifu wote hawa waliokuwa ulimwengini ni wanadamu!  Wakati YESU ananieleza ujumbe huu, pembeni yake nilimuona Ibrahimu Baba yetu na pembeni yake mama yake YESU akihuzunika sana na kuumia moyo wake akichukia yeye  kuabudiwa. YESU akaniambia nafikiri unaona hata mama yangu analia ! Ni jambo la kuhuzunisha sana jinsi mpango wa MUNGU ulivyobadilishwa na hata amri zake na kudharauliwa tena wazi wazi, acheni moto unawasubiri wafanyao hivyo, ni janja ya shetani ndani ya kanisa ili msimuone YESU, YESU sio mnafiki hashirikiani na mahali ambapo amri za MUNGU hazifuatwi haijalishi jina lake linatajwa hapo, na nikupoteza muda maombi hayo hayaendi mbinguni  ni machukizo ameniambia YESU na mimi sipunguzi neno  lolote nampenda, namuheshimu.

    Nikuulize swali – je kama umeshajua sanamu haina uhai na unaabudu – je itakujibu? Na   je majibu yatakuwa ni ya  MUNGU aliye hai au mungu mfu? Jibu mungu mfu. ( shetani ). Mpango wa MUNGU kitu chochote  kisiabudiwe na kufanywa MUNGU,ukishiriki wewe ni mungu mfu! Na huendi mbinguni .

    Chanzo cha kuabudu sanamu ndani na nje ya kanisa ni baada ya wale mitume wa YESU kuondoka wengine wakakengeuka na kumkufuru roho Mtakatifu,tafadhali wanaoacha ujumbe huu ni kwa ulimwengu wote,wanaofanya hivyo ujue   umepotea  hauna YESU na wanaofanya  ibada kama  hizo sio kwa YESU na kama sipo kwa YESU ni shetani ndie amekaa hapo, funguka.  Utaona  Musa mwenyewe alivunja ile sanamu ya ndama ,na zaidi  hata mama yake YESU na wazee 24 hawataki  waabudiwe na wanachukia sanaa, na zaidi mnaofanya hivyo hausikilizwi maana kama MUNGU  ameshakataa na hata pia katika kitabu cha mwongozo na safari ya mbinguni yaani Biblia imekataa sasa kwa nini mnajilazimisha? Soma Ufunuo 22 : 18 -20 Aliyeyaleta haya ameshamuhukumu na amemkufuru Roho Mtakatifu, Tafuta kitabu chote hautaona , mrudie YESU na umwabudu yeye tu ndiye Mfalme wa wafalme.


    2.    IBADA ZA WAFU

    Ni Ibada ambazo zina ushirikiano na mizimu. Mizimu ni roho za watu waliokufa walipokuwa hapa ulimwenguni, hawakuokoka au kuishi maisha matakatifu, sasa wakifa hawa huenda kwa baba yao kuzimu. ( ndio maana wanaitwa mizimu) ukienda mbinguni unaitwa mtakatifu na wanaokufa katika utakatifu wanaenda paradiso, na wanapumzika  wanasubiri ule mwisho, na siku hizi watu husema  ( peponi ) Sio sawa, peponi ni nyumbani kwa mapepo, nafikiri unaelewa mapepo, huu usemi siyo sahihi, nikuulize  je, unapenda kwenda kwa mapepo? Jibu ni hapana. Watu wameshikwa hata ufahamu wa kujua wanatamka nini.

    Ibada za wakfu ni mpango wa shetani ili wewe usitengeneze maisha yako au  uhusiano wako wewe na MUNGU ukijua kwamba ukifika utaombewa, ni kwamba inakula kwako. Soma Muhubiri 9: 4-5 na zaidi hata Waebrania 7:27, baada ya kukata kauli ni hukumu, hizo ibada ni ibada potofu tu, kama imeandikwa ukikata roho tu ni hukumu, hizo ibada za wakfu ni za nini tena?

    Hizo ibada kila unaposhiriki wale wafu wanakunajisi na wewe uwe kampani moja mkamwabudu shetani, funguka usishiriki. Ni ibada sawa na kuabudu sanamu, kufanya matambiko,kushiriki uchawi, Nikuulize swali – Je YESU ndiye ametufundisha haya? Jibu Hapana.

    YESU ameniambia hata kaburi lake lisiabudiwe limetengenezwa, nayeye hayupo hapo, yupo mbinguni ndipo makao yake yalipo.

    Akaniambia,hapa ulimwenguni kwenye mabara yote,baadhi ya watumishi wamejenga makaburi na kuyaita  kaburi langu, na kuyaita makaburi ya watumishi walio maliza kazi yao duniani, wale wakwanza,hawa  wa sasa hata waliokufa 99% wapo kuzimu hawajapokelewa wanasubiri hukumu huu ni ukweli ( 100%) siyo kufikiri kuwa mtumishi ndio tiketi ya kwenda mbinguni, ni utakatifu na kufuata aliyoyaagiza MUNGU, kama haukufuata, na ukaabudu vinginevyo, mfano sanamu- utaenda kwa waasisi wa sanamu ambae ni shetani maana anao uhalali na wewe unaabudu, MUNGU aliye hai hana uhalali na wewe maana haujamuabudu yeye na umemkana na yeye atakukana waziwazi, badilika mrudie YESU wa kweli.

    Usidanganyike mwana wa MUNGU ukaambiwa hapa ni nyumbani mwa mtakatifu yeyote hapa duniani, makao yao yapo mbinguni na ukikuta kuna kaburi  ukaambiwa hapa ni Golgotha lamba udongo, usikubali YESU  ameniambia waambie huo ni usanii, kwanza kiafya tu utapata minyoo, magonjwa, pili maana yake hayo makaburi unapolamba huo udongo nafsi yako unajipatanisha na mauti yaliyo juu ya hilo kaburi, tatu –unaanza kuporomoka maisha yako, ya kiroho na kimwili na mwisho wake na wewe ni kuzimu, ni kuulize swali wapi YESU aliagiza hivyo,yeye ndiye njia ya uzima na ukweli Yohana 14:6, sasa ndiyo muasisi amesema tufanye hayo? Jibu  hapana. Unakuwa umeabudu  sanamu.

    Jambo linguine hili ni sugu kiasi ambacho linafanyika kwa kumpinga YESU ndani ya kanisa. Jambo hili ni kuhusu sadaka ya mavuno, ameniambia waeleze watoto wangu hiyo sadaka siitaki na sizipokei kwa maana hata nilivyokuwa ulimwenguni mojawapo ya mambo ambayo niliyokataa ni hiyo sadaka ya mavuno kwa jinsi ilivyoletwa kwenye nyumba yangu, pia ikafanya nyumba yangu siyo ya sala tena imekuwa soko. Funguka  msomaji sadaka ya mavuno au mazao, hii ni sadaka ya fungu la kumi kutokana na kile ulichopata ndio utoe 10%. Sasa  sadaka hii wewe uza uweke kwa bahasha asijue mtu hapo ni sawa. Pili unapoleta hayo mazao kila mtu anajua umemtolea nini matokeo yake siyo siri tena, hupati thawabu ya MUNGU unapata ya wanadamu. Jambo lingine unapoleta  hivyo unamfungulia shetani nafasi ya kurudisha yale aliyoyakataa YESU yasifanyike ndani ya nyumba ya sala, mazao hayo utashangaa baada ya ibada  kanisa linakuwa soko au mnada! Sasa ndugu msomaji embu soma kitabu  cha marko 11:(15-18)  inaelezea jinsi YESU alivyowakuta wakiuza ndani ya kanisa alivyokasirika, akatibua kila kitu maana hayo hayafai sio mahali pake, siku hizi hayo mambo yamerudishwa, na shetani,nikuulize  swali je! Mnada unaruhusiwa ndani ya kanisa? Au YESU alipenda biashara ifanyike ndani ya nyumba ya sala, au kanisa kazi yake kunadi vitu? Jibu hapana.

    MADHARA YAKE KWAKO

    1.    Unakuwa unashiriki kuchafua nyumba yake.

    2.    Unakuwa haubarikiwi maana kila mtu anajua siri yako.

    3.    Baraka zako zinanadiwa watu wanapanda  bei zaidi ya 3 na hao wamekuwa wanashiriki mnagawana unabakia hamna, uanafilisika mkono wa MUNGU haupo juu ya mazao yako!

    4.    Inakuwa siyo sadaka tena maana imenajisika kwa kuonwa na watu, pia imehusika kufanya biashara ndani ya nyumba ya sala.

    NOTE: Ndugu msomaji  embu angalia jinsi kanisa lilivyotekwa na shetani mpaka mambo ya shetani yanapewa kipao mbele na ya YESU yamepuuziwa . Nakuambia 98% YESU hayupo ulimwenguni 2% amua uingie upande wa YESU wa kweli, kanisa limekuwa ni biashara kweli halipo watumishi 45% ni washirikina wa kiwango cha juu sana, sasa kweli utaponea wapi? Muangalie YESU.

    MADHABAHU ILIYOKUFA

    Madhabahu iliyokufa ni madhabahu ambayo haifuati taratibu za MUNGU na maelekezo aliyoyaacha YESU,chunguza madhabahu unayoabudu ukikuta haipo sawasawa na YESU muasisi wa kanisa alivyopanga ikawa kinyume ujue hiyo ni madhabahu mfu,

    Ø  Ukichangisha pesa – hiyo ni mfu

    Ø  Kuandika majina kwenye sadaka – mfu

    SADAKA NI NINI ?

    Sadaka ni Ibada kamili kati yako wewe na MUNGU aliyekuumba,unamtolea  MUNGU ili sadaka yako inene kama ya Abeli.na ili sadaka yako inene mbele za MUNGU,  kwanza mtu asijue umetoa kiasi gani. Ukisoma katika injili ya Mathayo 6: (2-4) inaelezea usishauriwe na mtu, hata mtumishi, utoe kiasi gani.

    Sadaka ya kweli ni fungu la kumi tu na shukurani. Sadaka za michango hizo hazimuhusu MUNGU,  sadaka za kuahidi, madeni, Imani, eti ukipata ulete na zote hata ukombozi siyo za mpango wa MUNGU, huu ni ujanja wa shetani ameliteka kanisa  na kubadili mpango wa MUNGU ili wewe usifanikiwe na ushiriki kufanya haya ambayo hajaruhusu upate dhambi.

    Ukiambiwa toa mpaka iume usifanye hivyo, haipokelewi .Toa kwa furaha,  YESU hanyan’ganyi pesa kama ilivyo makanisani siku hizi, huyo ni shetani na anayefanya hivyo ndani ya moyo wake mtumishi huyo anayo  roho ya kuasi na tamaa juu ya pesa.

    Ukifuatwa kudaiwa pesa labda mfano wa kununua kitu, mfano kinanda,gari, mabati, usitoe YESU siyo omba omba na hana shida kama ni mpango wake ataleta watu watafanya tena kwa furaha. Ukitoa haubarikiwi ni sawa na kutupa jalalani, ameniambia YESU niuambie ulimwengu wote ubadilike awarudi sasa, na utukufu wake wa mwisho ndio huu sasa umeanza ni kweli tuu mpaka aje na kuharibu uovu wote.

    Ukikuta madhabahu inachangisha au kukopa benki –hapo hayupo na sadaka zenu zinapotea, YESU  halipi riba, leo analazimishwa kulipa riba, hapo ni shetani amekunja nne anawachuna, YESU hakopi wala kulipa riba, leo hii iweje kanisa likope benki? Sio kanisa  lake, hata kama jina lake linatajwa hapo ni machukizo. ( Marko 7: 6-7)

    -          inapokopa benki – mfu

    -          inatoa huduma za kiroho kwa pesa – mfu

    -          madhabahu inayofanya kazi  za biashara – mfu

    -          kazi ya kanisa la YESU siyo kufanya biashara, huoni majibu unakaa hapo miaka nenda rudi haupo kiroho wala kimwili.

    -          Utaona ni mateso magonjwa, umasikini ufukara tuu ndio unaokujaa.

    -          Ukiona nguvu za giza zinakutesa na hazikutoki ujue hapo ni mfu.

    -          Inamatabaka, viongozi ni washirikina, hapo ni pesa tu.

    NOTE:  KWA NINI MADHABAHU ZINAKUFA?

    Sababu ni unakuta mtumishi, hana muda na YESU, ni mzinzi, au mlevi,au anatumia nguvu za giza, au anaifanya hiyo kazi kama ya mshahara, au amejiita mwenyewe, au yupo kwa kusudi la pesa tu. Japo wengi ni washirikina. Mahali hapo hautaona jibu na zaidi unapokuwa kwenye madhabahu mfu, tayari na wewe hapa duniani unakuwa mfu japo unatembea  umekuwa boksi tu.

    Hii yote ndiyo ni mojawapo ya kanisa lilivyotekwa na shetani,usikubali kuchezewa tena, wewe ni wa dhamani sawa na YESU anakupenda sana ndio maana unapata ujumbe huu.

    7. SALA YA TOBA

    Kwa wewe  ambaye  hujaokoka na unapenda kuokoka.

    UTASEMA MANENO HAYA:

    Bwana  YESU,  nipo mbele zako naomba Rehema, unisamehe makosa yangu naomba uandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima  wa milele; Bwana YESU nishike mkono, mimi ni wako kuanzia sasa .  AMEN !

    MUNGU akubariki sana akutunze,  milele na Roho mtakatifu akuongoze mahali alipo YESU wa kweli ndio akupeleke hapo ukasali hapo. AMEN.

    KUMBUKA.

    Ndugu  msomaji wa kitabu hiki, hii ni njia ambayo MUNGU anasema na wewe na kukufundisha na kukuonya kwa sababu anakupenda, hataki upotee umjue yeye 98% kanisa halina MUNGU hai linaabudu  MUNGU mfu, wewe usishiriki hayo na wewe utakuwa mfu na kama unashiriki ibada  hizo tayari wewe ni mfu na umehukumiwa, haijalishi jina la YESU linatajwa  hapo huo ni mchomeko au mtego ili unaswe hapo uangamizwe, toka huko na usirudi huko ni kwa mfu. Mwabudu MUNGU aliye hai, hakai kwenye vitu vya kutengenezwa na wanadamu, au hata kwenye vitu alivyo viumba amekataa visiabudiwe  sasa kama unaviabudu ujue umepotea wewe ni wa shetani.

    MASOMO YA ZIADA.

    2WAKORINTHO 6: 16 -18

    KUTOKA 32: 1-35

    KUMBUKUMBU LA TORATI 5:8-9

    KUMBUKUMBU LA TORATI 4:15-23

    YESU AKUPONYE, YEYE NI MWINGI WA REHEMA UKIACHA KUABUDU MASANAMU ATAKUSAMEHE NA USISHIRIKI TENA.

    YESU AKUSHIKE MKONO NA KUKUTOA KWENYE TANURU LA MOTO WA SHETANI (IBADA ZA SANAMU) MTEGEMEE YESU TU. UBARIKIWE


    © Prophet Hebron

    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate