Wafilipi 2:10-11
  • MAANA YA BENDERA ZA NCHI KUWEKWA KANISANI AU KWENYE MADHABAHU

    Ujumbe huu umetolewa  24th September 2014 na Prophet Hebron
    BWANA YESU ASIFIWE, YESU WA NAZARETI anawapenda watoto wa MUNGU na anataka msipotezwe tena bali mpone roho zenu. Amenituma niwaonyeshe njia ya kweli sababu shetani akiwatumia watumishi wake anawatumia kuwapoteza watu ili wasimuone MUNGU na ile siku ya mwisho wakajumuike na yeye katika motoila wewe utakayeelewa haya ninayokueleza na kubadilika utapona roho yako. Kwanza kabisa nataka uelewe kuwa katika kanisa ni mahali pa sala peke yake na hakiruhusiwi kitu chochote kuwekwa hii ni sababu MUNGU hachanganywi na chochote na pia imeandikwa ya MUNGU mpe MUNGU na ya Kaisari mpe Kaisari.

    Leo ninawafunulia siri za hizi bendera zinazowekwa katika makanisa na watu wengi wakiziona wanafikiri wana nia njema na nchi hiyo, jibu siyo. Ukiona katika kanisa lolote linaweka bendera ya nchi yake na mengine utashangaa wanaweka bendera zaidi ya nchi nne au zaidi. Sasa nataka uelewe, jambo la kwanza ujue unapoyaona hayo uelewe mtumishi au kuhani wa madhabahu hiyo yeye siyo mtumishi aliyetoka kwa MUNGU bali ametoka kwa shetani haijalishi analitaja jina la YESU. Hao ndio wale wakristo wa uongo. Hizi bendera ni maagizo rasmi ambayo mtumishi aliyepewa nguvu na shetani na hupewa maagizo ya kuteka hizo nchi ili watu wasimjue MUNGU wa kweli na pia kuharibu uchumi wa hizo nchi na endapo mtumishi atakuwa amepanda cheo zaidi katika ufalme wa shetani ndivyo atakavyopewa nchi nyingi zaidi azishughulikie na kuziteka katika ulimwengu wa roho, siyo kwamba anajipangia tu aweke bendera, hapana! Ni amri anayopewa na shetani na wengine utakuta wana makanisa katika mikoa mbali mbali, hivyo badala ya kuweka ya nchi peke yake wanatengeneza zao binafsi zenye nembo zao ili kuwateka watu wa mikoa hiyo na kuharibu uchumi wa mikoa hiyo na kuwafunga watu wasiende mbinguni japo kibinadamu watu hawajielewi. Hii ni siri ninayowafunulia watu wa MUNGU mpone roho zenu katika nchi zote na mataifa yote.

    Hivyo basi sasa uelewe nini maana ya bendera kuwekwa kanisani au bendera za nchi mbali mbali, hayo ni maagano ya shetani anayoyaingiza na mtumishi ateke hizo nchi zisiende kumjua MUNGU. Hivyo uelewe sasa ukitaka kupona roho yako huo ndio ukweli halisi, madhabahu ya jinsi hiyo ni za maagano ya shetani na kama ni za maagano ya shetani basi hata wewe muumini ujijue kuwa umeingizwa katika agano la kuwa mwana wa shetani pasipo wewe kujua, funguka ufahamu, masikio na macho ya rohoni upone roho yako. Bendera ni kwa ajili ya serikali za nchi peke yake. Utasema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, uniandike jina langu katika kitabu cha ufalme wako. Leo hii nitoe katika kanisa lenye agano la bendera za nchi, niweke katika agano la damu yako na uzima wako. Uniongoze nisitekwe tena na shetani na watumishi wake kuanzia sasa najitoa sadaka kwako YESU WA NAZARETI. Amen.



    Hakuna maoni:

    Visits

    Translate